Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Al Habib Seyyid Omar Bin Seyyid Abdallah – Mwinyi baraka.

i
Katika

ulimwengu wa Uislamu

(i)

Muharram 1429 - January 2008

Toleo la pili All rights reserved Second addition.

ii.
Yaliyomo:

No.

Ukurasa.

1. Yaliyomo……………………………………... iii.

2. Dibaji………………………………………….. vi.

3. Utangulizi……………………………………… vii.

4. Sehemu ya kwanza…………………………… viii.

5. Kuzaliwa kwangu na malezi yangu…………… 1.

6. Kuanza kusoma………..……………………… 1.

7. Kwenda Makerere…………………………….. 2.

8. Miaka ya Uganda……………………………... 3.

9. Kuanza kusomesha skuli ya Dole…………….. 3.

10. Daawa Ilallah………………………………….. 8.

11. Sehemu ya pili………………………………… 18.

12. Picha ya Al habib Seyyid Omar – Mwinyi Baraka.. 31.

13. Vitabu vilivyotoka……………………………… 32.

iii
DIBAJI:

Al-hamdul-lillah wa Swalatu was salaam alaa Khayru

Khalqillah Sayyidna Muhammad wa A-lihi wa Swahbihi waman waala

wa Baad.

Hichi ni kitabu ambacho Al-habib Sayyid Omar Bin Abdallah

mashuhuri kwa jina Mwinyi-Baraka katika wajukuu wa Sayyid Abubakkar

Bin Salim-Mola-Enaat huko Hadharamut, kwa taabu alielezea

mwenyewe akiwa amejinyoosha kwenye kitanda alipokua mgeni wa

Bw. Mohamed Khan Shemeji yake na Al-mar-hum Swaahib El- Ishara

Bw. Akram Mohd aliyefia Mwanza - Tanzania kati ya Mwaka 1988 na

89 Allahu Yarhamuhu wa Jamiil Muuminina wal Muuminaat.

Alikua akizungumza kwa shida sana pengine Dak. 10. Pengine

ndo gha-ya Dak. 15. Kwa hiyo ilikuwa tukimfwata na Tepu Recorder

mara kwa mara tukiwa na Akh. Aly Mzee Comorian toka Mkunguni

kwa Al-marhumu Mohamed Bin Mahdi na wanawe kina Akh. Islam,

Khamis na Al-marhumu Mahdy Mohamed Mahdy Allahummaghfirlahum

wa yarhamhum jamiia.

Al-hamdu-lillah tuliwahi kumaliza kunasa na kunukuru yote

kuhusu safari zake za Europe na Amerika kama itavoonekana ndani

yake.

Kwa vile lengo kubwa la safari zake tukiacha kusoma ilikua ni

Jihadi katika Dini ya Mnyezi Mungu nayo si nyingine bali ni Uislamu,

tumeonelea kukiita “Mwinyi Baraka katika Ulimwengu wa Uislamu

– I ” tukitegemea kwa imani zote kua:

(a) Kitazagaza maarifa mazuri kwa watakaokisoma

(b)

Kutakua angalau na kumbukumbu ya mmoja wa wanafalsafa

wa Kisufi mkubwa lakini hakupata umashuhuri nchini kwao

mpaka amekufa.

(c) Tutafaulu Insha-allah kumjulisha yule ambae hakumjua

mwanachuoni mkubwa huyo wa East-Africa na labda

vi.
kumuigiza au kumtakia dua, kwani ipo hasara kubwa kwa kule

kushindwa kumtumia vile ambavyo ingepasa.

Tabia yake katika kujitupa chini na kujiona kua si kitu

alifahamika vibaya kwa ambao hawakumjua, na hijabu ya wazi wazi

kwa walomjua vizuri kabisa. Dalili kubwa ilionekana mara nyingi

alipokuwepo Jijini hapa, si wengi walojua, kwa hiyo ilifikia mpaka

anaondoka si wengi walokua na habari hata ile ya kuepo Jijini hadi

kufikia mwezi mzima! mara kadhaa alipata mwaliko kwa mwanafunzi

wake mkubwa, alipokua madarakani Al-hajj Aly Hassan Mwinyi-

(Mzee Rukhsa )-Ikulu na alitutaka rukhsa aende au asiende.

Ahlil Majaalis El Ula El Qa-diriyya hawataacha kulia kwa

huzuni kila wakifikiria uamuzi aloutoa baada ya makubaliano kua

angeandika tafsiri ya kite kwa lugha ya Kiswahili ya kitabu kitukufu

Qur an baada ya kushindikana kuitoa tafsiri hiyo kwa njia ya TVZ,

lakini pia Majaalis nao hawakuwahi kwa sababu aliomba aende

Comorro akamshauri mkewe aje nae D‟Salaam nyumbani kwa Almarhumu

Bw. Moh‟d Mhdy (A.Y) kinyume ya mambo ni kwamba

kwenda kwake Comorro alikua ameshaitwa kwenda kukutana na ajali

yake badala ya kuja tena D‟Salaam kwa ajili ya kazi ya tafsiri ambayo

ilitarajiwa kuchukua miaka mitatu mizima.

Na ilifikiriwa kutoa juzuu moja moja kama alivoanza hivo Almarhumu

Sheikh Abdallah Swaleh El-Farsy (Ay).

Bumbuwazi tulolipata bila ya kumuomba aanze na utangulizi

na Surat El-Fa-tiha tu tulifunukiwa nalo baadae kabisa kua lau mtu

angejua ghaibu basi kuzidisha kheri kwetu ingetumilikisha angalau na

tafsiri ya Surat El-Fatiha ya Al-habib Sayyid Omary Abdallah Mwinyi

Baraka (Rahmatullah layhi).

Kwa sababu Al-habib alitudarisha vizuri sana kuhusu somo la

Nafsi (Tizama kitabu chetu “Maana halisi ya Imani”) hatuoni haja

yeyote ya kulaumu walokua na uwezo mkubwa na kueka kumbukumbu

ya mwanachuoni huyo kabla na labda baada ya kufa kwake.

Akielezea mwenyewe Al-habib kua kila alipokua Makka Almarahumu

Bin Bazz alikuwa akimtanguliza… “Omar Swalisha”.

Akimwambia: “Bwana Mtume SAW akisema, Ahlishsharafaa laa

Ahlisharaf watu wa Sharaf hupitana kwa Sharaf. Walaa Yaa arifa

Ahlish-sharaf wala hawawajui watu wa Sharaf Illa Dhawish Sharaf,

Illa ambao ni watu wa Sharaf”.

v.
Kwa niaba ya Majaalis natwaa fursa hii kuwashukuru mno

vijana wa Darasa la kila Jumatano Baadal-Maghrib Mtaa wa Sadani

Ilala baina kina Sharif Karama kwa juhudi yake kubwa katika

kuziandaa kwa makini na uangalifu sana jumla ya makala hizo na

kuzitoa katika Computer, kina Sharif El-Beyt Hussen, Fuad, Mohamed,

Mkhashshe, Swahibul-Ishara Swaleh Hariz, Okashi, Mustafaa, kina

Ababil Abdallah Twalib Arusha na wote wa Jalsa hiyo Mnyezi Mungu

atawajazi Fid Dunia Wal A-khirah.

AL-FAQEER.

AHMAD SHEIKH.

vi.
UTANGULIZI:

Al-hamdu-lillahi Rabbil Allamin, Was Swalaatu Was Salaam,

Ala Asharafil Anbiya Wal Mursalin Alladhi Unzila Alayhi

Lawlaa Nafarun Min Firqatin Kulli Twaa Fatin Layatafaqqahli

Fil Diin Wa‟alaa Alihit Twaahirina wa Aswaha-bihil

Akramiin.

(Amma Baad)

Wemeniamrisha nsoweza kuwavunja na wakanitaka

watu ambao naona uzito kwenda kinyume nao nieleze

yatayosahilika katika safari zangu.

Sasa naingia kufanya hayo kwa msaada wa Mnyezi

Mungu na uwezo wake Laa-hawla Walaa Quwata Illa Billahil

Aliyyil Adhim.

OMAR ABDALLAH

DAR ES SALAAM - TANZANIA

1987

vii.
S E H E M U

YA

K W A N Z A

viii.
KUZALIWA KWANGU NA MALEZI YANGU:

“Naona afadhali nielezee kwanza msingi wa malezi.

Nilizaliwa Zanzibar mwisho mwaka 1917 yaani

December kwa mujibu wa Sheikh, yeye atakuwa anamjua

Mzee wangu vizuri kwani alikua ameoa kwao, kwa Babu na

Mama wote Masharifu walozaliwa Ngazija. Babu Abu-Bakkar

Bin Salim, Mama Lydiid Jamallilleye.

Babu mkubwa Sayyid Abdul-Hassan baada ya miaka

miwili yaani 1938 Baba yangu huyo alifariki-Mungu

amrehemu. Na baada ya miaka mitano ya umri wangu mama

alifariki - Mungu amlaze mahali pema . Nikalelewa na Mume

wa Khaalal Ibin Khaalat wa Mama yangu Seyyid Abdul-

Fattaah Bin Ahmed Jamalilley akiitwa sharifu Abudu.

KUANZA KUSOMA:

Nilipelekwa chuoni kwa Al-Mar-hum Seyyid Sheikh

Bin Abdul-Rahman Babake Seyyid Hassan Sheikh nikawa

nasoma, na Sala nimesoma kwa Bibi mkubwa mwana-Ashata

kama alivokua akiitwa Aisha lakini wakimwita Mwana-

Ashata.

Nikabaki baada ya kuhitimu nasomesha watoto chuoni huko

huko na Khalafu nikawa nakwenda nasomesha watoto chuoni kwa

Sharifu Abudu, na wakati huo huo tena nikatiwa Skuli, lakini kwa

sababu ya kukawia kuingia Skuli, sikupata Mnazi mmoja.

Nikapelekwa Mwembe-ladu kutoka Kisiwandui asubuhi, ninarudi

halafu nakwenda saa nane tena mpaka mwisho nikaja zangu Mnazimmoja.

Baada ya kusoma miaka mitatu Mwembe-ladu na mwalimu

wa mwanzo wa Skuli hiyo alikuwa Juma Mohamed, wakimwita

Juma Mohamed Mushte - sijui kwanini Mwalimu Juma Allahu-

Yarham.

1.
Zilikuwa Klas mbili halafu mwisho zikawa tatu, halafu

nikaenda Gulioni. Nikaendelea na masomo Skuli na huku

nikienda chuoni na kusomesha mpaka nakumbuka mwaka

gani nilipotiwa Skuli, ilikua 1928.

Nilipokua STD. 7 Sharifu Abudu akafariki na huku

nimeshaanza kusoma soma kwa Seyyid Abal-Hassan na vile

vile Nahaw. Alivofariki nikabaki chuoni. Nimekiendesha

chuo bila shaka mwenyewe ni Seyyid Abal-Hassan ninasalisha

Msikiti wake Msikiti wa Sharifu Abudu Vikokotoni.

KWENDA MAKERERE COLLEGE:

Nikasomesha Mukhtasaraf pale baada ya Swalatil-Fajr nae

Seyyid Abal-Hassan akawa anasomesha Umdatus Saaliki baada ya

vitabu kadhaa wa kadhaa tulivokua tumeishasoma. Sera zote

takribin, Mukhtasarat kwa Seyyid Abdul-Fattah tumewahi kuvisoma

kwake. Nikaanza na Nahaw hapo, ilihudhuriwa na watu mahodari

katika masomo hayo. Kama Seyyid Mustafa, Sheikh Mohamed

Qamus baada ya Swalatil-Ishaa. Hatukumaliza kitabu mie nilikua

nimeishakwenda Secondary School na nikapata kupelekwa

Makerere nkaenda Makerere College.

Nilikua na bahati nzuri ya kufanya Mitihani, siku zote nakua

Fas aghlabu. Katika Primary yote na Secondary nilipasi vizuri. Na

nikisoma mwenyewe vibuku vibuku na hasa palikuwepo magazine

ikiitwa Islamic Review kulikua na Library ya Sunni Mkunazini

nikipenda sana kusoma. Kulikuwepo kama zile nikipata sana sana

kusoma kama habari za kina Khuwaja Kamalud-din nikiona raha

kwenda kusoma.

Makerere niliingia 1939 nikapata Diploma ya Education baada

ya miaka miwili na nikakaa mwaka wa tatu kuspeshalaiz katika

Biology.

2.
MIAKA YA UGANDA:

Miaka ya Uganda ilikuwa ya faida sana kwa kufwatana

Waislamu huko. Kutwalii nao, wakija Makerere tukitwalii na

Sheikh wao Sheikh Shuayb na mmoja Maallim Juma na wengineo,

hasa Nahaw, na Sheikh Shuayb akisoma mantik, Ambayo niliwahi

kusoma kidogo kwa Muhsin Bin Aly Barwani pamoja na mwanae

Aly muhsin halafu mimi nikaendelea kwa Sheikh Sleiman Bin

Alawy.

KUA MWALIMU SHULE YA DOLE:

Mwisho nikarudi Zanzibar nikawa Mwalimu wa Sayans na

Religion (DINI) katika shule ya Dole pamoja na Teachers Training

yake. Wakati huo ndio nikapata fursa ya kufundisha Vijana wengi

ambao sasa wameshika madaraka makubwa kama President Aly

Hassan Mwinyi Vice President Idriis Abdul-Wakyl na wengineo.

Huku ninasomesha Dole na Beit-Raas.

Skuli ile ya Dole ikawa Beit-Raas na kila nikija mjini

ninasomesha msikiti wa Sharif Abudu, na daima nasoma kwa

Sheikh Sleiman na Sheikh Muhsini. Na vitu vingi nimesoma kwa

Sheikh Sleiman, Fanni. Hata mtu akiniuliza Elimu yako ya Dini

umeipata kwa nani, ntamwambia kwa Sharif Abudu, Seyyid Abdul-

Fattan. Secondary Seyyid Abal-Hassan na Seyyid Mustafa Bin

Jafar ambaye ni Father in Law wangu (Mkwe wangu).

Na ikiwa kuna ilimu inaweza kuhisabiwa pamoja kua ya Ki-

University, basi Universtity niloipata huko huko kwetu basi ni

Sheikh Sleiman, Seyyid Abal-Hassan, Sheikh Muhsin, Seyyid

Mustafa Bin Jaafar ambae ni Father in Law wangu (Mkwe wangu)

zote zinajulikana nimezipata kwao Shikh Sleiman Alawy Babake

Sheikh Zamil alikua mwanachuoni aliyekusanya mambo mengi

taabu kuyakuta kwa mtu mmoja yeyote.

1951 nkapata Scholorship ya London kwenda kusoma Islamic

and Comperative Law. Unasoma Law ya Kiingereza, Law ya

kiafrica na bila shaka kwa wingi - Sheria ya Kiislam na katika ajabu

za kusoma mtu huyo ni kua walimu wa sheria ya Kiislamu

3.
walikuwa ni Waingereza, na wengine walikuwa ni maadui wa

Islamu. Lakini ni Law ni Fiq-hi, lakini wapo walokuwa

wakinisomesha vitabu kama Dr. Aly Hassan Abdul-Qadir Director

wa Islamic Cultural Centre alikueko siku hizo - London University

ilimkodi School of Oriental Studies ilimtaka awe akija akisomesha.

Nikasoma Fiq-hi, Usulil-Fiqhi kwake, nikasoma na kiarabu zaidi

kwa Wazungu.

Somo hilo liliniletea hasa katika kusomeshwa na mmoja

katika wakristo, walikua wakitaka kuuvunja Uislamu sana Imani.

Na kutaka kuponda kisichopondeka kwa Bw. Mtume - SAW

Anderson akiitwa. Tumepigizana kelele mara nyingi kwenye klasi.

Na nilikuwa nikisoma kinamna ya peke yangu pengine

mimi na Mwalimu tu, pengine Walimu wawili na miye mwanafunzi

mmoja pengine walimu watatu na mwanafunzi ni miye mmoja. Na

miye kila nikipata fursa nikipondana pondana. Pengine klasi inajaa

mpaka watu wanakwenda kwenye Dining Hall – mahali pa kulia

chakula – manake watu wanasoma Law walikuwa wakichukua kitu

kinaitwa LLM au LLB na ISLAMIC LAW – yaani sheria ya

Kiislamu ni moja katika subjects.

Wote wakija kwake sasa wakipanga aje awasomeshe na siye

sote tuko pamoja. Tukipigizana kelele sana kilichontokea katika

fikra za mwanzo kabisa ni khabari ya alipokuja kwenye mambo ya

ndoa katika sheria ya Kiislamu akapata fursa ya kutaja ndoa ya

Sayyidatna Zeynab Mtume SAW akasema hivo wanavosema wao:-

“Siku moja alimuoza Zeyd Bin Harith kwa sababu Zeyd Bin

Harith alikua ni mtumwa wake Mtume akamwacha huru

akamuoza Zeynab. Zeynab alikua mtoto wa Shangazi yake na

walikuwa hawataki aolewe na mtu ambae aliwahi kua mtumwa.

Lakini kwa kumstahi Mtume na kusemewa kwa Mtume

akamuoa sasa Khalafu akaja akamwacha akamuoa Mtume.

Ndoa yake yalosemwa ndani ya Qur-an.

Aya Qur an ilokusudiwa hapo ni ile ilioko katika 33:37.

“Na (wakumbushe) ulipomwambia yule ambaye Mnyezi

Mungu amemneeshesha (kwa kumuafikia Uislamu) na wewe

ukamneemesha (kwa kumpa kugusana naye ni Bw Zaid Bin Harith

ulipomwambia “shikamana na Mkeo na umche Mnyezi Mungu

(usimuache)”. Na ukaficha katika Nafsi yako aliyotaka Mnyezi

Mungu kuyatoa (nayo ni kuwa Mnyezi Mungu amekuamrisha

4.
umuoe wewe huyo mkewe atakapomuacha ili iondoke ile itikadi

iliyokua ya kuwa mtoto wa kulea ni kama mtoto wa kumzaa) na

ukawachelea watu, hali Mnyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi ya

kumchelea. Basi alipokwisha Zaid haja yake na mwanamke huyo,

tulikuoza wewe ili isiwe taabu kwa Waislamu kuwaowa wake wa

watoto wao wa kupanga wanapokuwa hawana haja nao. Na amri ya

Mnyezi Mungu ni yenye kutekelezwa”.

Qur an: 33:37

Ilikuaje wao wanasema kamuona akampenda akamwambia

mwache nimuowe miye. Na hakika ya amri ni jambo ilikua Zayd

akipata taabu sana nyumbani kwa Zeynab. Ilikua Mabibi wa

Kikureish wanadharau yule Bibi aliyeolewa na mtu ambae alikua ni

Mtumwa, nae ni mzalendo. Akimtaabisha Zeyd. Zeyd akitaabika

akija akimwambia mtume “Niachie nimuache” akamwambia “ Kaa

nae, Kaa nae”. mwisho akapewa Rukhsa, alipopewa rukhsa Zeyd

akamwacha Mtume SAW akamuoa. Sababu mbili:-

Kwanza:-

Kwa kikureishi hapana rukhsa kumuoa mtu ambae

alikua mke wa mtumwa wake, mtu ambae alikua

mtumwa wake akamwacha huru halafu akawa mkewe

akimwacha hapana rukhsa kumuoa. Azwaaj adiyaihi.

Ili kuondoshwa hayo iwe anza wewe hapana atae

thubutu mwingine kila mtu ataogopa asitukanwe

asifanzweje - wewe anza.

“Tulikuoza wewe ili isiwe taabu kwa Waislamu kuwaowa

wake wa watoto wao wa kupanga wanapokuwa hawana

haja nao. Na amri ya Mnyezi Mungu ni yenye kutekelezwa”.

“Likay laa yakuna ararajun fii azwaaj ad-i yaaihi midhaa

qadhaa minha watwaran wa kana amrullahi maf-u-la”

Ya pili:- Ilikua ni tabu kwa Zeynab kuolewa na watu wengine

baada ya kua kaolewa na mtu Ad-iyaai – alikua ni

mtumwa sasa Mtume ASW amekua kilugha ya

kisasa yeye ndo alo Run Life yake. Jambo gani zuri zaidi

angelifanya kuliko kumchukua yeye akamuoa.

5.
Sasa wamemgeuza badala ya kumsifu kua ni mtu mtukufu namna

hii na hivi Firaq akampenda. Nikasema pale pale kwenye klas na

tulikuwa watu wangapi watu wanne, mimi na huyo aliekua akieleza

na Profesa wa African Law na mmoja akifanza kazi ya

Administration katika Afrika na mmoja alikua Jaji India sasa alikua

akisomesha English Law nikawaambia jambo:-

Something for which you have aught you have to have

praised him, respected him. You have taken the very

theme blame him and to make it the cause of saying bad

things about the profet.

Jambo kama hili mtu atataka Udhuru vipi-

“Idhaa mahaasin allatii ataytuha aadat dhunubihi

Faqul-llii kayfa aatadhir”

“Ikiwa mema yangu niliyoyafanya yanahisabiwa ndo

madhambi sasa natoa udhuru vipi tena”

“Aa, yamekwisha hayo ni moja katika mambo yalotokea katika

klas. Mikutano hiyo wasokua Waislamu na vikundi vya Waislamu.

Ndo mwanzo Vijana wa Kiislamu wanaanza kukusanyika pamoja

na kukutana toka nchi za nje na mmoja mmoja wa kule na

wanafanya mikutano wanasoma, wanazungumza – palikua na

pahala panaitwa Aclistus Square, kwa Editor wa Islamic Review

kwenye Laasiri watu wanakutana wanadiscuss. Inasomwa Maqra

inatafsiriwa, inaelezwa na Al-hamdulillah ikielezwa wao hutaka na

mie nitie langu.

Ikaendelea hivo hivo mpaka nikapata safari ya Marekani na

mie ni mwanafunzi wa U.K niko England. Na kule kule England

bila shaka fursa zimetokea katika makanisa vikundi vya wakristo

nami nakwenda kutoa khutba fanni ni wengi na wanafurahi wasikie

khabari za Uislamu na hivi.

Nakumbuka Wales nilitoa khutba moja very famous - sana

ilijaa watu sana kabisa. London nilikua nipo hapo nikitoa khutba

sasa itakuja safari ya Marekani.

Nilipokua mwanafuzi London School of Oriental African

Studies Al-Madrasati Qarasaatish-Sharqiyyat katika London

University ilipatikana fursa ya kwenda States wanafunzi wanaotaka

6.
kwenda watoe kiasi kadhaa wa kadhaa na wakifika huko

watatizamwa, watakua wageni wa Jumuiya ya Kimarekani moja

wapo – wazungushwe wonyeshwe maisha ya Kimarekani yaliyo

mema kwa mujibu wa vipimo vyao na mengine kwa vipimo vya

watu wote.

Kwa umri waliokua wakiutaka mimi nilikua nimekwisha kua

mtu mzima lakini walipoona application yangu na kuniona

wakanitia kati. Ilikuwa taabu kupata kipando tena, mwisho nikapata

Greck Line ikanichukua mpaka Quebec, mji baada ya mji mpaka

Batholomeo mpaka New York. Njiani bila shaka nikaona Niagara

Falls. Shalalar Niagara – Mmiminiko wa maji katika mahali

wanapokwenda watu kutizama. Pahala pa ajabu penye Nature –

yaani umbo la ajabu.

Bin Adam hajatia mkono wake, wenyewe tu linakwenda –

lipo. Kutoka hapo ndo nkaenda Batholomeo – Batholomeo New

York nkapokelewa na wenzangu wengine mmoja mmoja. Tena

mmoja kutoka London tukakutana huko huko. Nimekwenda

tukakutanika pamoja na Waislamu wawili watatu mmoja mtu wa

Kimasr, mmoja wa Pakistan lakini sasa imekwisha kua kikatiba –

Bangladesh tena. Na Dini nyinginezo na kabila nyinginezo.

Tukachukuliwa kuzungushwa tukapitishwa States mbali mbali, na

kila pahali tunapata fursa ya kupokewa kwa heshima na

kuonyeshwa na kushughulikiwa, na wasaa wa kutoa fikra.

Na bila shaka mtu Muislam kila akipata fursa jambo la

mwanzo hutizama njia awaonyeshe watu nini Uislamu, nini faida

zake nini ukweli wake, na Al-hamdulillah sikuziwacha fursa hizo.

Hata unaona Naby Yusuf AS alipoulizwa habari za ndoto na wale

watu wawili katika gereza kabla hajawajibu kawaambia.

“Enyi Wafungwa wenzangu wawili Je! waungu wengi

wanaofarikiana ndio bora (kuabudiwa) au Mnyezi

Mungu mmoja mwenye nguvu (juu ya kila kitu)”.

Qur an: 12:39

“Inni Taraktu Millata Qawm Laa Yuuminun Billahi

Wal-yawmil Akhir”

Qur an: 12:39

7.
DAAWA ILALLAH:

Mwisho akawatajia Mnyezi Mungu khalafu ndo akawafasiria

tena. Hii ndo kazi ya Muislamu. Da-awa Ilallah siku zote kwa

nyendo zake, kwa maneno yake, kwa vitendo vyake, kwa mawaidha

yake kwa kila namna zake yeye anaupokea Uislamu. Anapita watu

kwa njia nzuri kabisa, kwa hekma na mawaidha mazuri.

“Id-u Ilaa Sabiili Rabbika Bilhikma wa Mawidhatan

Hasana……..”

“Kuja kwenye njia ya rabbu wako kwa hikma

na mawaidha mazuri”.

“…Wajaadilhum Billati Hiya Ahsan…”

“Usishindane nao illa kwa namna iliyo njema kabisa”

“…Qul Haadhihi Sabilli…”

“Sema hii njia yangu”

“…Ad-u-llahi Alla Baswiratu Anaa wa Mamit Tabaan”

“Na ita kwa Mnyezi Mungu, juu ya utambuzi kwa fikra,

kwa mipango kwa kujua ntafanya nini, na hii kazi hii mimi

anaenifwata”.

Basi ndo kazi ya Muislamu tena madamu yuko duniani hali

haonywi basi atakua kama watu wabaya anajua ataepukana nayo

kadri anavoweza. Mema anayajua atayafuata kadri anavyoweza.

Lakini Mission yake kubwa ni Da‟awa Ilallah – Propagation kwa

kiasi chake anachokijua na uwezo wake na uhodari wake na alicho

nacho basi kila State ikitokea haya.

Nakumbuka kuna State nyingine nikipata fursa mpaka

kwenye Radio nikisikilizwa mtu aseme khabari za kwao. Bila shaka

nikisema khabari za kwetu nayo ni Zanzibar na wao ni watu wa

Dini nyingine. Anataka kujua Dini gani – Uislamu, Uislamu ni nini,

unawaambia na kuwaeleza na unawafahamisha na kuwaonyesha vile

utofauti uliopo baina ya Uislamu na Ukrito.

Si kwa kuponda kiasi ya kua wajue tu nini kiliopo kilicho

kikubwa kilicho tofautisha bila shaka, kikubwa kilichotofautisha ni

8.
itikadi ya Wakristo kua Nabii Isa ana uungu. Waislamu wanakataa

yeye ni Mtume tu pamoja na wengine Illa yeye kaitwa na Mnyezi

Mungu:-

“…Abdullahi wa Rasuluhu wa Ibni Ammatihi Wakalimatuhu

Al-qa-ha Ilaa Maryam Waru-hum-minhu”.

Basi mambo kama haya inapatikana fursa. Illa nakumbuka

hivi hivi nilipofika Noxivil, ilisadifu Jumamosi wakaniambia kua

kesho Jumapili tunakwenda katika Kanisa na wao kule ni katika

wakubwa wa Kanisa, “Jee! utatufwata?” Nikawaambia

intakufwateni, nyie mtakwenda na yenu na mimi ntakwenda na

yangu.

Nilipokwenda nkasikia mkubwa wao ananadi kua tumepata

mgeni na si wa Dini yetu na tutampa yeye fursa atoe Sermon,

Aprichi – haya jazaa kheyr. Nikasimama nikatoa nikaprich kitu

kikubwa. Kulikua Nigroes wengi, ni mji wa Wanigroes walo na sura

nzuri wanaoendesha mambo yao na kila namna. Basi nikawatajia

bila shaka mwanzo wa usawa wa Kiislamu bila shaka mwanzo ule

Uislamu hauna nani weusi nani weupe kama Kanisa – Msikiti wa

weusi na weupe. Hapo ndo nkapatiwa fursa ya kuisoma kama

kungineko, kokote kuisoma aya:-

“Yaa Ayyuhanaas Innaa Khalaqna-kum Min

Dhakarin wa Untha…”

“Enyi watu hakika sisi tumekuumbeni wanaume na

wanawake (wengine wakatafsiri) kutokana na yule yule

mmoja (Naby Adam) na mwanamke yule yule mmoja

(Hawwa)”.

“…Wajaalna-kum Shuuban wa Qabaaila

Litaarafu…”

“…Tukakujaalieni “Nations” na “Tribes” na kabila

kubwa na kabila ndogo ndogo mkaongeza nchi na

kabila katika nchi mpate kujuana msaidiane (mjue

namna ya kukaa pamoja msijiweke Divisions au

Labour)”

Qur an: 49:13.

9.
“…Inna Akramakum Indallahi Atqa-kum”.

“…Mtukufu wenu kwa Mnyezi Mungu ni yule mcha

Mungu kuliko nyote. (Hali hii watu hufasiri wakaona

kama hapana namna nyingine za kutukuzana illa ni

utukufu tu)”.

Qur an: 49:13

Kuna maneno mengi ya Kiislamu “Akram” na si Akram tu

kuna “Ashraf” haikusemwa “Inna Ashrakum” bila shaka

Afdhwalakum maana yake mbali. Maana ya Qur an inakata

kuzingatiwa – Kila neno lina maana yake na pahala pake na uzito

wake.

Na katika khutba nilizokua nikitoa huko Marekani kuonyesha

Uislamu nilitumia aya hii kuonyesha kua sisi hatuna ugomvi na

wakristo kwa kusoma:-

“Qu-lu Amanna Billahi wa Maa Unzila A Layna wa

Maa-Unzila Ila Ibrahima wa Isma-iila Wais-haaq

wa Yaa-quuba Wamaa-utiya Musa wa Isa

Wamaa Utiyyiina Min Rabbihim”.

Inatwambia:-

“Semeni:- Tumemuamini Mnyezi Mungu, tulicho

teremshiwa na kilichoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na

Is- haq na Yaaqub na wajukuu. (Wamaa Uutiya Musa) – na

anayopewa Musa wa Isa – (Wamaa Uutiyyan – Nabiyyuna

Min Rabbihim) wanayopewa na Mitume kutokana na

Rabbu wao. Yote tumeyaamini kua yameletwa na Mungu:-

(Laa Nufarraqu Baina Ahadin Mini- hum). Hatufariqishi

baina yeyote katika wao, (Wa Nahnu Lahu Muslimu) na

sisi kwa Mnyezi Mungu tumeslimu”.

Qur an: 3:84.

“Fain Amanu Bimithli Maa Amantum Bihi Faqadih

Tada Wain-Tawallaw Fainna Maahum Fii Shiqa-qin

Fasayakfiikahumullah wa Huwas-Samiiun Aliim”.

Qur an: 2:137

10.
“Basi watu hao (Manasara na Mayahudi) kama mnavoamini

(nyinyi) itakua kweli wameongoka na wakikengeuka

(wakikupa mgongo, nyongo) basi wao wapo

katika upinzani tu. Basi Mnyezi Mungu atakulinda na

shari yao, nao hawatakudhuruni kitu-(Wa Huwa-

Samiiun Alym) na ndo mwenye kusikia na mwenye

kujua. (Sibghata – llahi) – hiyo radhi ya Mnyezi

Mungu kisha ipanga katika nyoyo za waja, hiyo

Sibghat llahi ni Babtism ya Mungu Ka-precise kua

ambae kwa Wakristo Sharti Abatizwe.

Padri ambatize mtu. Na unaona katika Uislamu laa - Mungu

mwenyewe anakubatiza. Mambo ya Roho hayo Bin Adam

mwenzake hayagusi. Mnyezi Mungu anasema, ukimwamini kuna

Mjarad wa kuamini namna hiyo tu. Kama inavohitajiwa uamini

Mungu mwenyewe. Amma kubatiza.

“…Waman Ahsan Mina-llahi Swibghata wa Nahnu

Lahu A-bidu-n”.

“Na mimi mwema zaidi kuliko Mnyezi Mungu

kwa Swibgha, na sisi kwa yeye ni wenye kumuabudu”.

Qur an: 2:138.

Mtu mwengine akutengenezee wende ukamuabudu

mwengine. Akufanye unafaa-kuabudu, wende ukamuabudu

mwengine. Huyo huyo unofaa kumuabudu ndiye ataekutengeneza

akupokee, atengeneze mambo yako, kuonyesha Utolerence wa

Uislamu, kukaa pamoja na watu wa dini nyingine kama Qur an

inavyosema:-

“Walaa Tujaadil Ahlil – kitaab Illa Billati

Hiya Ahsan”.

“Usijadiliane na watu wa chuo illa kwa namna iliyo

nzuri (watu wa chuo Yahudi na Kristo) ilaa kwa namna

iliyo nzuri kabisa”.

Qur an: 29:46

Haya katika Radio, katika Maklasi, katika mashangwe katika

kila pahala mtu akipata fursa anatoa aya hizo na aya zinginezo

11.
waafikianazo.

“Wa Qu-lu A-manna Billahi Unzila Ilayna Wamaa

Unzila Ilykum Wailaahana Wailaahukum

Wa-hid Wanahnu Lahu Muslimuun”.

“Na useme tumeamini ambacho kilichoteremshwa

kwetu na kilichotelemshwa kwenu nyinyi

na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja na

sisi kwa yeye peke yake tumesilimu”.

Qur an: 3:84

Hiyo ndiyo Qur an tukufu tuliitumia sana. Nikitoa khutba

katika Lottery Clubs katika Clubs za namna kwa namna na vikundi

vya wanawake, mjini na mashambani kuna Associations za

wanawake na mambo yao hayo, nkawaambia khutba.

Mtu bila shaka nkaonyesha kuona wapi katika Uislamu

katika hayo nkawaambia ulietajwa kwa uzuri katika Qur an kuliko

zaidi kuliko Sayydatna Maryam na wanadhania kua yeye anavunjwa

na Uislamu. Waislamu ni mtu wao mamake Mtume na anatajwa

ndani ya Qur an vizuri kabisa.

Sadatna Maryam na alivotajwa vizuri katika Qur an hakua si

chochote illa ni Mamake Naby Isa aliyeambiwa kua amemzaa hali

ya kua yu Bikra inatosha sikwambii miujiza yake. Tunda, siku si

zake mengine na wema wake katika Lottery inataka wasaa kusema

na Politician wakubwa wakubwa. Kusema na watu juu ya mambo

makubwa unawaambia hatari ya Colourbar Discrimination si kwa

kuwatukana wala kuwaogopa, kuwaambia hatari unafanya hatari

yaani kama jeuri.

Mmarekani mmoja anainua kidole namwambia Mmarekani

aache Colorbar aache kwa mmoja Myahudi alikua katika Group

yetu akaja akawaambia mngekua mnajiona we mwenyewe

unapokua unasema-ajabu. Na alil-hasil fursa hizo zimechukulika

Insha-Allah zisifutike ziwe zimethbitika.

Khutba kadhaa wa kadhaa nimejaribu kuzikumbuka mambo

makhsusi yalosemwa–Maelezo makhsusi yalokamatana na Uislamu

ambao ulikua nao – Hawafahamu nimejaribu kuwafahamisha kadiri

ya uwezo nimekwenda hata tukafika pahala, hapo kuna Camp kuna

vijana wa Jamal – kadhaa wa kadhaa wameekwa hapo wageni wa

Vice Chairman wa Serikali ya Kimarekani, tukachanganishwa

12.
nao sasa yule aliyetuchukua Marekani akasema kwamba: “Naona

kama kwamba Jumapili hii Wakristo wasiende Kanisani – badala

yake watachanganyika na Waislamu na Mayahudi pamoja wafanye

jambo la kiibada pamoja.

Kila mtu asome kitu katika Dini yake. Mayahudi wasome

Taurati, Wakristo wasome Zaburi na Dua ya Zaburi na Waislamu

wasome Qur-an. Mambo yafanyike ki-njia ambayo Wayahudi

hawatowaudhi Waislamu wala Wakristo. Na Wakristo watafute vile

vile kwamba hawatakwenda kinyume na Waislamu na Wayahudi”

Wakatupa shauri hilo, mimi nikamwambia yule Kijana wa

Kimasri Muegyptian kua apande ahubiri, yeye afanye kazi ile, lakini

akakataa . Mimi nikamwambia: “Lakini lini wataisikia Qur an na

hatuna woga wowote wa kuonyesha kua Qur-an ndio sawa

kuonyesha kua Qur-an itafunikwa au itazidiwa kabisa ndo sawa

kuonyesha kua ndo kitabu cha Mnyezi Mungu hasa cha kweli

kweli”. Alipokataa mimi nikafanya, wale walosoma vitabu vyao na

dua zao hapana alothibitika. Quran iliposomwa na aya gani

ilosomwa.

“Walaa Tastawi-l Hasanatu Walas Sayyiatu Id-Faa

Billati Hiya Ahsan Faidhal Ladhi Bainaka wa

Baynahu Ada-Watan wa Maaka Annahu Waliyyul

Hamiid Yulaqi Qa-ha Illa-ladhiina Swabaru

Wamaa Yulaqqa-ha Illa Dhu-Hadh-Dhin Adhiim”.

Hiyo ndiyo Qur an, ni Aya mbili hizo zilizosomwa. Haiwi sawa

Kiingereza ikifasiriwa:-

“It can never be equal evils and virtue it will never be equal”.

Tenda kwa lilo zuri kabisa jema kabisa, mtu akifanya ovu hutafuta

lilo jema kabisa atende. Push away what whatever is the best

what is the worst and all of a sudden that one who was your

bitter enemy between you and him you will discover he has

turned into a faithfull friend almost – irreletive. Mlipe mema

mara utamuona amebadilika amekua rafiki mwema. Wala

hawakutanishwi na hayo illa wenye kusubiri wala hawakutanishwi

na hayo illa wenye fungu kubwa kwa Mungu.

“Laa Ilaha Illallah wa Maa yulaqqa-ha Illal ladhina

13.
Swabaru wa Maa Yulaqqa ha Illa Dhuhadh-dhu

Adhiim”.

Wameathirika utastaajabu kabisa, ajabu mmoja Mmarekani

akanijia akaniambia: “Is that the Qur an?” Nikamwambi: “O

yes, there is a lot in that”. Nkamwambia-mmekawia kujua.

Ni moja katika mambo yalotokea halafu akanijia yule

Muegyptian akaniambia “You, anta adhym, anta tahmil

elamaana”. Nikamwambia: “Alhamdu-Lillah”. Basi

tukaondoka hapo tukasogea mbele pengine. Mtu asome aya

katika katibu chake inahitajia asome na Dua ya Kitabu chake

mimi nilichagua Aya hii:-

“Rabbana Laa Tua-khidhna innasiina Aw-kh-twaana

Rabbana wala tahmil elayna iswran kamaa hamal

tahu ala-lladhina min Qablina Rabbana wala tahmilna

maa Laa Twa-qata Lala bihi wa af anna-waghfir lana

war hamna Anta Mawla-na fan-Swurna alal-qawmil –

ka firiina”.

“Bwana wetu, e! Rabbu wetu usitupatilize tukisahu au

Tukikosa e! (Rabbu wetu) usituchukulie uzito kama

ulivowachukulia walio kabla yetu usitubebeshe

tusioweza kuyachukua yalo mazito kwetu ya Rabb

utuafu utughafirie uturehemu we ndo ulo tawalia

mambo yetu utunusuru juu ya watu (Qawm) yenye

kukufuru”.

Hiyo Amerika katika Camp ile ilikusanya watu namna kwa

namna. O! our Lord, kwa hakika nilifasiri Lord, hapana neno

jingine lililotumika sana kwa Rabbana kama Lord, lakini haina

maana ya Lord peke yake yaani ina maana nyingine. Creator

Envoilver Lord Prossessor – kila kitu kimo katika neno Rabb –

Avenger – mtengenezaji, kama sisi, kwa kiswahili utasema

mtengenezaji, katutengenezea yote. Rabb ukifasiri, “Bwana”

haitoshi hata kidogo au si Wafaransa “Laa tua-khidhna in nasiina

aw-akhtwaana”.

Maana Muislamu makosa yake yanakuja kwa kusahau,

anarukwa na akili anasahau. Huo ndio Uungu, anasahau Pepo

anasahau alokatazwa kwa kufanya makosa kama ilivyodhihiri kwa

14.
Babu yetu, Mzee wetu Adam. Akikumbuka anarejea anasikitika na

anamuomba Mungu asimchukulie. Muislamu mwema, kinyume

mbaya hutampa kufanya ni fahari huyakimbilia akayatengenezea

tena.

Basi unataka ujue kua hapana haya kwa kucha kwa Dini zao

nyingineo, kwanza kwa Kikatholic lazima wende wakamtafute

Priest. Akupe kurudi halafu ndo usamehewe kwa wasta wake.

Wanaita wenyewe To Confess! kukubali ubaya wake mtu.

Kiislamu hapana, unakubaliwa na Mnyezi Mungu na

unamuomba asikuchukulie. Basi mpaka mwisho hapo ikaja

mizunguko tena tulikokwenda.

Sasa si sharti niseme kwa mujibu wa taratibu uliopita lakini

kwa namna yoyote ile kwa kiasi ntavyokumbuka tulipofika New

York usiku tulichukuliwa tukatiwa katika Meli tukaitizame New

York kwa nje Baharini. Inatisha, ina haiba inapendeza Sky Scrapers.

Majumba ya mamia makumi kwa makumi, Ghorofa mia na kitu

Mataa jumba la United Nations, na hii inaathir sana kuonyesha Bin

Adam vipi anaweza kutumia uwezo aliopewa akafanya kazi akafikia

hali ile.

Jitihada yao yote watu fikra nzuri juu ya Marekani na kwa

sababu hiyo ndo maana nyumba tulizokaa nyingi mimi nafsi yangu,

nyumba nilizokaa ni kumi na nane. Kumi na sita ndani yake hakuna

hata tone la ulevi, na wanavunja ulevi vile vile, ili kutaka

kutuonyesha ya kua wako watu hawalewi huo Amerika. Akili yao

imewaambia ulevi una hatari na si wa kutumiwa kwa sababu ya

uzima, kwa sababu ya akili, kwa sababu ya mwili.

Basi na huku vile vile kila wanalolipata na kutufanyia wema

kwa kadiri wanavoweza katika majumba. Na hivi hata huko South

Atlanta imewekwa nao kwenyewe kulikuwa ndo wakati huo

kwenye Racial Discrimination kubwa – Colorbar – na niliwekwa

katika nyumba ya mmoja katika weupe wenye hadhi lakini alikua

haamini hayo.

Wakanitazama vizuri, mwisho wakanifulia nguo zangu.

Wakaniniuliza wenyewe nguo zako za taka ziko wapi, hebu lete.

Ndivo walivo hao juu ya majumba hayo, watu namna nyingi katika

nchi moja na wako wengine wakikutizama unaona kua

wanakutizama kwa jicho la adhabu.

Basi tukenda tukafika New york tukaingia katika meli

tukaingia katika Bahari. Nilipoona nikakumbuka Qur an kama Aya

15.
Aliyoitumia Sayyidnal Imma Sheikh Abdo Bakathir Abdallah Bin

Mohamed Bakathir Sheikhe wa Mashekhe zetu Aleyhum

Ridhwaanullah, alipokuja akaonyeshwa Aeroplane mwanzo inapita

Aeroplane watu katika Zawiya yake akatolewa alipoiona

hakutaharaki wala lolote alisema.

“Falamma nasuu maa dhukkiru bihi fatahna lahlim

Abwa-ba shiy hatta idhaa farihu bi maa uwtu

akhadhnahum baghtatan faidha-hum mublisun

faqutwi a daabiral qawmul ladhiina dhwalamu-wal

hamdu Lillahi Rabbil A-lamina”

Ikanijia Aya hiyo na nikaisoma:-

“Waliposahau hayo walionyeshwa kwayo tuliwafungulia

Milango ya kila kitu (Allah Akbar) hata walipokwisha

furahi kwa waliyopewa tuliwachukua kwa ghafla (Adhabu

ikaja kwa ghafla) waka haribikiwa kwa ghafla”

Kama tunavoona mambo ya Kiulaya huja yakenda kama bofu

likawa juu hivi mara likapasuka vita au nini au nini.

“…Faidhaahun Mublisuun”. mara wamekata tamaa hata kusema

hawawezi. Wamekaa tu nyuma ya watu wenye kudhulumu wenye

kuweka mambo si pahali pao ndo maana ya dhulma. “Dhulma”

wanaweka kitu si mahali pake Al-Hamdulillah. Basi nilipotizama

pale ilinijia Aya hiyo nikaisoma:-

“Falamma nasuu maa dhukrini bihi fatahna lahum

abwaaba kulli shiy hatta idhaa farihu bima uwtu

akhadha hum baghttan faidha-hum mublisuna

faqutwia daabral qawmil ladhiina dhwalamu wal

Hamdu lillahi Rabbil A-lamiina”

Yule Muegyptain akamwambia yule Mmarekani:

“Mwambie akutafsirie Aya hiyo”. Nikaona taabu kubwa. Hawa

wenyewe masikini wanataka waonyeshe kua hapana watu kama

wao. Wamefika pakubwa pa kukua, hii Aya inaonyesha wapuuzi

kabisa na wako katika hatari. Nikamwambia: “Haya we mtajie”,

16.
Akaniambia: “Hapana usikubali”. Akashikilia, nikamsafiria

akanywea. “Basi twende zetuni” Imekua yale aliyoyataka siyo yale

aliyoyapata. Qur an mimi sina mastaajabu na kua kuna kitu

kushinda Qur an na iko pale hata kitu kimoja. Kila kitu kiko pale.

Haya tuliporudi New York tena.

Sasa mimi nafikiri kua afadhali sehemu hii niifanye Part one

hii niliokwisha sema nikae nifikiri namna ya kukaabili sehemu

nyingine. Safari hii ya Amerika ilikua safari ndefu ina karibia miezi

mitatu, kwa hiyo ndiyo ina mambo kadhaa wa kadhaa”.

17.
SEHEMU

YA

PILI

18.
SAFARI YA PILI AMERIKA:

“Tuliingia mji wa Nishilin na kila mtu akawekwa katika

nyumba fulani, mimi nikawekwa katika Fiski University – pamoja

na President wa Unit Squad Farsuk University pamoja na

President wa hiyo Fiski University alikua ndo anahishimiwa kabisa

New York na ni Mnegro. Hapo alikua na mkewe vile vile wote

watu wahishimiwa sana. Ndo mwenye nyumba nzuri kubwa kabisa.

Wakati wa kula akanambia “Jee! Grace?”; Wakristo

husema kabla ya kula, inaitwa “Grace”, sisi Grace yetu ni:-

“Bismillahir-Rahmanir-Raheem”. Hii ndo kwa ufupi, lakini watu

wajuao kuna vitu zaidi katika vinavosemwa kabla ya kula, lakini

hilo niliona ni refu na “Bismillahir-Rahmanir-Raheem” inatosha

nikafasiri kwa Kiingereza:-

“In the name of God the most compassionate the

most merciful”.

“O! hii sasa tutakua tukiitumia hii inatosha kabisa”. Na

wanao wanafunzi walotoka nchi nyingine za Kiislamu katika

University yao. Baada ya kula wakaniambia vile vile niseme kitu

cha kushukuru kama wanavyofanya wao nikawaambia, siye yetu

nyepesi tunasema:- “Al-hamdulillahi-Rabil-alameen”. “Haya

sema” nikawaambia:-

“All praises are due to God - the Lord the Evolver

of the Universe the Sustainer of the Universe”.

Tukakaa mwisho tukaondoka. Ajabu, namna walivyokaa na

mimi kwa uzuri, mwisho wa mtu kukaa na mtu kwa uzuri sana, tena

hawanijui mwanzo wala mwisho - tena kwa vizuri sana. Nikitaka

kuondoka wemekataa, “Usiondoke”. Hatimae nikaondoka kama

desturi ilivotengnezwa katika Programme.

Nilipofika London nimewaandikia barua, katika barua

nikasema nikatia maneno ya Kiarabu.

“Maa Fil Maqaam Lidhyl Aql Wadhil Adab”

19.
“Hapana katika kukaa moja kwa moja usisafiri kwa mwenye akili na

mwenye adabu, anaetafuta adabu namna ya kuishi vizuri duniani.

Safiri, katika safari kuna faida tano:-

i. Tafrijil Ham - Kutokwa na hamu,

ii. Wa Kasbil Maaisha - Na kuchuma maisha. Mimi hapa

nimeondoka na suti mbili nzuri

kabisa - first class - katika maduka

yaliyo bora kabisa.

iii. Wa Ilmun - Na Ilmu. Huyo alikua Sociologist

mkubwa ana vitabu kadhaa

vya Sociology.

iv. Wa a-dabun - Na adabu, namna ya kujua kukaa na

watu na kusema na watu.

v. Wa Sub-hati Maajidin-Na Sub-ha ya Watu Watukufu.

Watafrijil Ham, Waktisaabul Maa-i-sha, wa Ilmun, wa

A-da-bun, Nikaja nikafasiri kwa Kiingereza, halafu katika barua ile

nikaandika kwa Kiingereza, mambo yote matano hayo nimeyakuta

katika nyumba moja, nikamwambia:-

“Is n‟t it wonderful that one could find all those five

under one roof?.

“Alaysa Ha-dha Ajaban Annal Insaan Yajid Hadhal

Khamsa Tah-ta Saqf Wahid?”.

Akaniletea barua akasema:- “Usiseme hivyo, kwenu kwa pili huku, njoo

tena”. Mimi sikwenda njia hizo tena, nilikwenda Amerika tena lakini

sikwenda upande huo, ni ajabu mtu kuyakuta yote matano haya mahali

pamoja. Na ziko nyingine zinahimizwa kusafiri kama:-

“Sa-firu fainna fil Asfa-ri tajid iwadhan

amman tufa-riquhu”.

“Safiri utapata badala ya yule uliyemfariki”.

Wa Ansub (Ujitayarishe) Fa Inna Ladhatil Maaisha (Utamu wa

maisha), Fin nusub (katika tabu), Inni ra-aytu fi Khisaai fil maai

yufsiduhu (Mimi naona kusimama maji huyafisidi), In-sa-la Twabahu

(Hua mema yakichuruzika yakiteremka), Twa-ba (Hua mema

na yakitulizana huharibika), Muftalasatwal usud law laa Firaqu

20,
Lagha-b-masim-ba Law (Ingekuwa hawajafariki vichaka

wasingepata visindika). Wal-ud fi ardhiha Naw-un minal hatwab

(Na udi pahali pake ni namna tu ya mti katika miti na ukiondoka

pale ndo unatiwa ndani ya moto unatoa harufu nzuri). Watu

wakihimizwa sana kusafiri lakini safari haijaachwa kua taabu “Qitatun

minal adhab” yuko mtu mmoja anasema:-

“Balil Adha-b qit-a minals safar”

“Bali adhabu ni sehemu ya safari”

Na zamani ilikua raha yake kubwa ya safari mnafwatana

mnakua ndugu wamoja, kitu kimoja, mnasaidiana mnashirikiana

mnaona raha katika safari, mnokofika mnapokewa kwa wema, sasa

watu wote kila mmoja kashughulika na lake. Hilo ni moja katika

pahala pamoja tulipowekwa.

Sasa tulipokua huko New York tuliwekwa nyumba inaitwa

„International House‟. Siku moja nimekaa nje pale ninamuona

Mmarekani mmoja kaingia na karatasi anadhania “Islam and

Religion” (Islam na Dini) nikasema huyu amedhania Uislamu si

Dini? nitajaribu kiasi nnachoweza kumfahamisha kua Uislam ni

dini; tena ni dini kuliko dini nyingine zozote bali mbele ya Mnyezi

Mungu hapana inayoweza kuitwa dini illa Uislamu.

“Innad-Deena Indallahil Islam”

“Hakika dini kwa Mnyezi Mungu ni Uislamu)”.

Qur an: 3:19.

Si kwa kua tunaambiwa na Qur an tu, lakini mafundisho yake na

namna zake na maisha yake inaonyesha dini ya kweli, na kwa

Mnyezi Mungu ni Uislamu.

Basi nikaanza nnaingia ninamfahamisha tukenda mpaka

njiani akaniambia: “Basi, basi, mimi ni Muislamu mwenzako, hii

khutba nnakwenda kuitoa YMCA, na namna ulivonieleza, wewe,

naona wewe utaeleza vizuri kuliko ntavoelezea mimi kwa hivo

wewe utakwenda ukaitoe khutba hii na ili nisiikose hukai hapa tena

utakuja kukaa nyumbani”.

Nikamwambia si kitu lakini mimi nimewekwa hapa.

Akawapigia simu walioniweka, yeye yule akataka kujua mie

nimekubali, akanipigia simu akataka kujua Adresi, akapigiwa na

21.
simu kua niko huko nyumbani nnakokwenda nkakae. Bila shaka

nikakaa akaja na mimi nikaenda nikahamia. Namna tulivyozoeana

kwa muda mchache. Akastaajabu vipi Mmarekani si Muislamu ama

mnaona leo udugu wa Kiislamu, nikamwambia laa ni udugu wa

Kiislamu:

“Innamal Muuminanuna Ikhwana”

(Hakika si jinginelo ni kuwa waumini wote ni ndugu)

“Fa Aslehu baina Akhawaykum”

“Patanisheni baina ndugu zenu”

Qur an: 49:10.

“Wat Taqul Llaha……..”

“Na wamche Mnyezi Mungu”.

Nikamuuliza wakati mmoja alikueko, ajabu, akiitwa Bwana

kheri ni jamaa yake Marehemu Maallim Mohamed Ahmed wa

Zanzibar anafanya kazi Melini. Nilipopata kuja London nikamuuliza

pana watu wa Kingazija huko. Akanipa Adresi, Mohamed Ahmed

Jae. “Laa Ilaaha Illal Lah” Akanipa Adresi kwa kua nikienda

Amerika nitajaribu kuuliza nayo ni kuuliza tu. Lakini pahali kama

Amerika, Umtafute mtu wapi!.

Huyu nilipomuona Muislamu nikasema nitamuuliza alaa

kulli hali. “Oo! yule Mzanzibari?” Hakujua kuwa ni Mngazija au

Mnini – maadam katoka Zanzabar basi ni Mzanzibari akasema

“Utamuona lakini kwanza twende tukakae nyumbani asije

akakuchukua. Tukakaa akatengeneza khutba yake, akamaliza.

Akaniambia “leo tutakwenda, Alkhamisi usiku utamuona pahala”.

Tukaenda katika majumba ya Sky Scrapers moja za New York tena

kuna Maulidi wanasoma kila Alkhamisi tukafika kwenye “Yaa

Naby Salaam Alayka Yaa Rasul Salaam Alayka” nikamwambia:

“Amma wewe Yaa Naby umefika mbali mpaka Huku!”.

Baada ya Maulidi yule Mzee yuko hapo. Huyo Mzee

mwenyewe Mruwada wa Jumbe Fumu. Nikamwita huyo mtu wa

huko nikisikia mtu ananiambia. “Huyu mtu wa huku lakini

anaonyesha Mngazija”. Nikamwambia: “Wee nani?” akaniambia

“Mimi Mruwada wa Jumbe Fumu”. “Nani jamaa zako?”

22.
“Mahmudu wa Jumbe Fumu, ni katika walionilea Mimi, anaitwa

Mahmudu wa Jumbe Fumu na wamenikhusu kwa upande wa

ukeni”.

Mtu akiitwa: Mahmudu Bin Kimwana Jumbe Fumu au

Abdul-ghanii wa Jumbe ndo mwanzo akiitwa wa Jumbe Fum.

Nikamwambia: “Hawa ndugu zako ndo walonilea!”. Basi pale pale

akaanza kujifakharisha kwa wale – “Huyu mwanangu” – “This is

my son I have rasied him, my Brothers have raised him”

wamemnyanyua - yaani wamemlea – “He must come and stay with

me (Aje nyumbani akae na miye), Na hivo twende zetu sasa hivi”

Nikamwambia” “Haiyumkiniki nimechukuliwa kwa hishma na kwa

azma, na azma zenyewe bado hazijatekelezeka, itakuwaje!” - Laa

Ilaaha Illa llah - akakubali.

Basi tukaenda mpaka baada kutengenezwa tena ikatiwa

tukenda Maulidini, tukaenda tukafanya ile khutba ikawa Ghas-ya

kwenye khutba. Kuonyesha nini Uislamu, ni kama khutba ile

niliotoa katika – King Abdul-Azeez University – “What is Islam”

Hii nimesema: “The real meaning of Islam” lakini ile nimesema

na watu si Waislamu – iko tofauti sana.

Katika niliowaonyesha usawa katika Uislamu na umoja na

undugu nime Emphasise sana na yale niliokua nikielezea huko

nyuma huko, na kwengineko kama: “Qu-lu, a-manaa Billahi

wama unzila ilayna” (sema tumeamini Mnyezi Mungu na

yaloteremshwa kwetu) – na hiyo – “Yaa ayyuhaa Naas inna

khalaqna-Kum min dhakarin wa untha” – Sote ni namna hiyo

hatujui sisi tofauti ya Rangi wala Nchi wala Nasabu – wala nini.

Ikiwa kuna watu hawatumii, hawataki, pale mbali, lakini

Uislamu umeamrisha kama hawaongei mawazo mengine ambayo

watu hawayataki au hawawezi kuyafwata lakini wamejua Uislamu

umeamrisha.

Katika kuuliza ilipokuja katika usawa, kwenye usawa

ilivokwisha ikaja suala, Akainuka Mnegro mmoja akasema “Wewe

unasema katika Uislamu unasomesha Usawa mbona kuna watumwa

katika Uislamu unakubali tu?” Nikamwambia “Ukristo

hayakubaliwi hayo au hapana? wewe Mnigro umekujaje huku

Amerika? umetekwa, umetiwa kamba, umetiwa katika atlantic

Ocean, umefanywa mtumwa kwa nguvu, na hivi umeletwa huku,

umeelimishwa umefanywaje!” Aaa! wakamvamia Wanegro

wenzake wakamwambia – “We ndo wa kusema maneno namna

23.
hiyo, maneno gani hayo!”. Nililetewa barua kua walisilim watu kwa

sababu ya khutba zile zilotolewa YMCA.

Tukarudi England lakini ilitokea ilikua na hamu sana kurudi

kwa Meli. Kwa Meli kutoka New York mpaka Southampton, nilikua

kila nnapokwenda naambiwa hapana Meli asilani sasa shauri gani?

hata siku moja hiyo tukalala nikaona “Queen Elizabeth” Meli

kubwa lile linakuja New York kutoka Southmpton (London)

asubuhi nikaambiwa kua siku ya pili au ya tatu kuna safari, kuna

Queen Elizabeth ipo, inatoka New York inakwenda London.

Basi nikapanda Queen Elizabeth toka New York kwenda

London bila shaka kwanza unafika Southampton. Meli pandikizi la

Meli naona ni katika Meli kubwa zilokuweko wakati wake duniani.

Ilikuepo “United States” ilikuwepo “France, Normandee”

ilikuwepo Queen Elizabeth na Queen Mary!

Sasa safarini tumo ndani ya Queen Elizabeth nikaona katika

Atlantic Ocean Baharini kama Jabali katika Bahari nikauliza

nkasema “Kuna Jabali katika Atlantic Ocean?” nikambiwa “Laa, ile

ni Queen Mery inatoka Southampton inakwenda New York?.

“Aajib, ni kama Qur-an ilivosema, Quran inasemaje?”

“Walahul Jawaaril, Manshaa-ji Fil Bahri Kal

Aalaam”

“Na vitokuja kuzaliwa (havipo sasa) (Vitakuja kuzaliwa)

katika bahari vitakua utadhani jabal”.

Qur an: 55:24

Nikaona Quran haijabakisha kitu “Walahuljawaaril Munsha-a-ti

kal Aalaam fa Biayyi a-Laai Rabbikum a-tukadhdhiba (Ipi

katika Miujiza ya Mwenyezi Mungu mnaikadhibisha?).

Hata safari moja neno husemwa pamoja na neno jingine.

alikuja Sheikh Shuayb, ndo alokua Mwanachuoni Mkubwa kabisa

Uganda akaja Unguja. Kwanza alichukua Uislamu tu kwa Sheikh

Abdus-Swamad, mmoja alikua zamani – Zama za Seyyid Ma-jid

akenda kule. Mimi nimemkuta Mzee – Sheikh akaja akawa anataka

kusoma hasa akataka kusoma “Mantiq” na ndo alosimamia Maulidi

sana baada ya Shekh Abdur-Rahman Bin Aqeed – Aloyatia Maulid

Uganda wakasilimu watu kwa maelfu siku hiyo.

Mwanzo wa kusomwa Maulidi walisilimu watu kwa maelfu.

24.
Watu walivosikia Matwari na nini, wamekimbilia

kusikiliza na waliposikia khutba na kuona wameyumba,

wamefanyaje, walipoondoka pale watu kwa maelfu wamekua

Wailsamu. Hata wakataka kushitakiwa kua wamepiga ngoma

kwa jina la Dini. Ikafanywa kesi – Seyyid Ahmed Ibn

Abdur-Rahman akafanya, akasimamisha, akashinda.

Basi tangu wakati huo wanaingia watu ndani ya

Uislamu kwa Maulidi na Matwari. Wanavalia watu

wanakwenda waganda wanavaa vizuri mpaka huenda

wanakutana kutwa wanakaa pamoja wanasoma Maulidi,

wanakula wanawafikiana, wanasilimu, wanaalika wakubwa

wa nchi wanasheherekea.

Mwanzo nilimuona Iddi Ameen huko katika Maulidi namna

hayo pamoja na yule President – Alotolewa Karibu, walikuja

pamoja punde baada ya Revolution ya Mutesa kabaka Mutesa –

Mkutano mkubwa Sub-hana watu wanoshughulika na Uislamu na

mambo ya kheri wanastarehe sana.

Twayyib, basi alikuja Unguja ye Sheikh Shuyb lakini kaja

baada ya kua kasoma namna hiyo tangu hapo – Fiqihi, kasoma na

Nahaw, kasoma namna hiyo kasoma Mantiq na kiasi alivosoma,

akaja mwisho akaja akachukua Twariqatish Sha-dhiliya

Shurtwiya kwa Seyyyid Aly Bin Ammi yangu.

Vile vile Seyyid Mohamed Bin Shekh El-Maaruf, Seyyid

Aly ye yuko hapa hapa Babake She Hamadi. Hao wote Baba zao

ndugu – yeye Seyyid Aly Bin Sheikh Seyyid Abdur-Rahaman na

Babangu. Hata Sheikh Shuayb alipata kuniambia: “Nchi hii kama

mmeekewa nyiye, Sayyid Abdur-Rahman kaja kaleta Maulidi,

Sayyid Aly kaleta Twariqa-Sha-dhiliya, wewe umekuja

umenisomesha”.

Basi akaja nikamchukua Beyti-Ras kama unavojua baadhi

ya watu – kumejengwa Msikiti mkubwa – mkubwa kwa sababu ya

Watoto wa Boarding. Zamani Boarding ilikuwa Dole, na mimi

nilianza kusomesha Dole mbali kidogo, Meli kumi unakwenda kwa

mutkari halafu unakwenda kwa miguu. Au Bakhti yake upate gari

ikuchukua mpaka juu huku pakiitwa Dole.

Ikahamishwa halafu ikaja hapa Pwani Beyti-Rasi pahala

Seyyid Saeed Bin Sultan alifikia hapo akitoka Oman, Zamani

mwanzo akifika hapo pakajengwa skuli kubwa – Skuli Techers

25.
Trining na Primary ni Dole Class na ikabidi uwepo Msikiti. Sheikh

Shuayb alipokuja nikamchukua Msikitini nikamtaka atoe Mawaidha

– Hodari wa kusema sana, Faswih na anajua kuchagua maneno, na

nini; na mtu kakulia Uganda lakini anasema Kiswahili vizuri kabisa.

Kaja akasema, pale ni iko karibu na bahari pale, ile Skuli na Msikiti

uko karibu na Bahari, anawaonyesha ukweli wa Uislamu.

Anawaambia “Tazama Qur an inavokwambieni unaona Meli

zinavopitapita hapa nyiye mnastaajabu kua wazungu wamezua zile.

Zile Mnyezi Mungu ameziumba kwa hikma yake; Akawasomea:

“Walahul jawa-ril munsha-atifil fil bahri kal

A‟Alaam”

Allahu yar-ham Sheikh Shuayb. Hiyo ndo ya njiani kwenda

Southampton nikarudi nikaenda zangu London kuendelea na

masomo.

Kukaa London yametokea mambo mengi bila shaka,

Mahudhurio Mikutano ya Waislamu, kufurahikia Maulidi, Sifa za

Maulidi kuzifurahikia kushughulika kwa mambo kadhaa hata katika

mambo niloyakumbuka siku za mwanzo mwanzo nilipokwenda

nkayashughulikia.

Mlokuemo katika Dini ni Miraji ilifanzwa London na mtu

alochaguliwa atoe khutba mbele hapo – alikuwa Seyyid Ahmed Bin

Kirami wa India akisomesha Skuli of Oriental African Studies.

Nilikutana na Maalim Zuberi Allahu yar-ham tukenda. Akasema

akatoa khutba na kuonyesha Miraji kua imetokea na hawezi kuitia

wasi wasi, mtu anajua uwezo wa Mnyezi Mungu na Mnyezi Mungu

kusudi kaonyesha kua mambo haya si mambo ya kidesturi kwa

kuanza kutaja kisa, kasema:-

“Sub-hana ladhi asra bi abdihi layla, minal

masjidil haram ilal masjidil-aqswaa”.

Tazama Mnyezi Mungu kaanza kwa kusema “Sub-hana”

katakasika na kila lisilo Laykiana na yeye – yaani msije mkajipima

nyiye mkaona madam nyiye hamtaweza kujifanyia mambo haya

ndo basi hayakufanyika. Haya yamefanywa na yule ambaye

ametakasika na kila lisilolaikiana na yeye Kampeleka usiku mmoja

Mtumwa wake, huyo Abdi wake Asra biabdih Yaani msiri wake

alokiriana nae, yeye kamkiri kua ni Rabb na Rabb kamkiri kua

yeye

26.
ni Abdi wake – Anampa siri zake anamwendesha sio mwendo

anaowaendesha watu wengine.

Imetoka: “Masjidil Haraam Ilal Masjidil Aqswa Alladhii

ba-rakna hawlahu”. Akasema mpaka akalia akaliza watu

nakumbuka ni katika mambo nlomuandikia Al-Habib Barua

nilipokua kule na kitu kingine nilichomuandikia ni mkutano wangu

na Yusuf Aly, Mkutano wangu na Yusuf Aly alo Translate Quran,

na Translation yake ndo inohishimiwa sana.

Nilikwenda nkamtafuta nnamuulizia nkaambiwa yuko

England, wapi,! ikabidi nizunguuke nnamtafuta hata nkapambana,

nkaambiwa nenda mahali fulani labda utamkuta.

Hapo nkenda nkaonana nae - Ni klabu ya watu wanofanya

kazi katika Empire, Empire Club. Nilipokwenda nikaonana na

Receptionist akaniambia: “Je nani, yule Mzee anokaa pale afanzi

lolote anajikalia tu?” Nikamwambia: unaona ni wewe tu kua

kajikalia, ni yeye nnahaja nae. Nkaenda nkaja siku nyingine

nikampata nikamwambi: “Nna haja na wewe”. Akaniambia: “Ndo

wewe ndo unaekuja hapa ukiniuliza nimeambiwa?” nikamwambia

“Naam” “Njoo unataka nini - Come Along what do you want?”

“Sit down” Nkamwambia: “I have read your translation of the

Quran and I was very much Impressed, very much indeed I

Admire you”. I thought since you are here - still I must come

and see you”. He was Old man Almost mystical, kua sufi mkubwa

kawa na Mnyezi Mungu tu hata kusema na watu hasemi na watu.

Akanambia “Naam - Yes you are right”. Nkamwambia: “Nadhani

ulivokua ukiandika tafsiri ile umemuona usingizini Mtume mara

nyingi”. Akanambia:-

“Yes, and I saw him, I felt this was coming from

Heaven to tell me what I should Write and I wrote

that tranlation it took me three years to write the

translation. I was going round and round, I was

busy writing the translation and I visited almost

every place mentioned in the Qur an in my attempt

to write that translation”

Nikamwambia: “What are you doing here, you are so old?”

akanijibu: “Yes where shall I go? Lahor used to be a city of

Islam, Now It‟s no longer. I have a small room here by myself

27.
and literaly intersted in europe and here its easy for people to

contact me”

Ni ajabu namna ninavyoyakumbuka maneno yake,

nimeyakumbuka very cleary na kwa kuya-repeat lakini nikayasema

kwa namna clearly na Admiration yangu imenisaidia

niyakumbuke maneno ndo ilivyo hivyo.

Nikamwambia: “wewe ni mtu wa wapi asili yako wapi”

akanambia: “Mimi ni mtu wa Yemen, Northern Yemen, Baba

yangu alikua mtu wa huko, akaja India akawa mtu wa huko. Na si

yeye tu bali hata Babu yake pia waliishi huko wakaowa, wakaishi

huko”.

Nikamwambia: “How did you manage to combine both

types of Education – Islamic and European secular and

Religion?” Akanambia: “Okey yes, I had a wise Father a learned

person whose wisdom was greater than his knowladge, he told

me: “learn anything you want but mind you would never find".

He is wise who takes what is truth and leaves what is the

incidental”.

Hiyo ndo jawabu yake sasa nkasema kua – “Qur an

imekusaidia sana. Watu walikaa kwa uovu na wewe, lakini Qu ran

imekusaidia namna ya kukabiliana na watu. Aya gani imekusaidia

sana kuliko aya zote?” Akanambia: “Suratil Fati-ha”.

“There is northing like Al-hamdu, in the whole of

World litrature”.

Akawa anaingia, anaisoma akaisoma yote, akaisoma kama

asili ilivyo, halafu akaifasiri. Halafu nikaona huyu Mzee leo

nisimweke sana halafu nikija tena ataniona huyu mtu matata. Huyu

afadhali nimuondoe njiani, nikamwambia leo basi afadhali tupige

Fat-ha. “Unataka nini?” Nikamwambia: “General” akatia Fat-ha

tukasoma Al-hamdu, akasoma yeye kwa sauti, unaona maana mpya

inakuja kwa msomo wake Yusuf Aly Allahu yar-ham.

Siku nyingine tena nikamwambia vipi kwa sababu yeye ni

Mwalimu wangu nikimuona mtu alokua akinisomesha Islamic Law

mzungu Christian English akinistaajabisha nkamwambia: “Vipi

duniani kuwa Prejudice namna hii. Mtu namna ile anatarajiwa

aseme kitu haki tupu”.

28.
“What don‟t you – you mustn`t be surprised to see

people with prejudices… you and I have our own,

let others have their own prejudices”.

Katika maneno alonambia hapa basi tukaendelea hivo hivo

tukicheka, tunazungumza.

Wakati mwingine nikamuona hasemi asilani. Nakaa kimya

namuuliza naona hajanitambua! Ananiambia “Nakutambua si yule

anokuja hapa. “You come here from time” Nikajua leo hayupo

afadhali niende zangu. Msafara wangu wote na yeye hapo

nilipokwambieni karibu na Trafalgel Square. Afadhali niende zangu

nikamwacha. Hayo ndo mambo yalopita nilipokua London.

Mambo mengi yamepita ya mfahamisho baina ya Waislamu

na Wakristo. Pameambiwa katika yalokamatana na Science,

mengine yamekamatana na Politics. Mie kila nkipata nafasi

kuonyesha Uislamu unasema nini nasema, naandamana na mikutano

ya Eastend na mengineyo. Na siku zile kulikuwepo mahali

panaitwa East African House ilikodiwa na nchi za East Afrika,

vijana hupata mahali pa kwenda kupumzika, pakapatikana na

mjumbe wa kukaa nikahamia huko huko. Pahali pazuri karibu na

katikati ya London.

Muda mwingi nilioupitisha London niliupitisha na mimi

nakaa hapo, na halafu, unajua tena Waislamu na vikundi vyao, na

tukikutana wengine wanatualika. Tulikua pamoja na Salim akiitwa

Bwana Awadh Bin Salum Masud alikua akipenda mambo hayo ya

dini, huyazungumza na kuyaeleza.

Anakwenda tunakutana na watu wa Pakistan wapi wapi,

wazee wengine wametoka Suudia Hijaaz. Wamekuja Madaktari,

wazee wengine Madaktari wa zamani wa asili huja mara moja tu,

Alha-sil siku za fursa. Mpaka mwisho ikapita miaka ilopita

tukafanya mtihani miaka 1 – 3 nilikaa kwa sababu ya kusoma hivo

nikafanya mtihani ikabidi nirudi kwetu East – Africa.

Lakini wakati nilikueko Ulaya kila Vication nilichukua fursa

kwenda Ulaya. Nikisikia kuna Group mpya ya watu wanakwenda

“Europe” nami „nikiwajoin‟ tukiingia pamoja kwenda kutembea,

kwenda kutizama Qur an inasema nini. “Siru Fil-ardhi” (nendeni

kwenye ardhi) “Fandhuru” (mtizame) “Kayfa Baada-alkhalq”

(Mnyezi Mungu vipi kaanza kuumba) “Thumma Allahu Yanshiu

Nashatal Ukhra” (Baada ya hapo Mnyezi Mungu anazua mzuo

29.
mwingine kabisa sio ule alioumba mwanzo). Mnyezi Mungu ni

“Latwiif” anajua kabisa undani wa mambo namna ya kutengeneza

na kufanya. “Yarham Man Yashaa” (Anamrehemu amtakae) “Wa

maa antum bi muujiziina fil ardh” (Na nyiye si wenye kumshinda

Mnyezi Mungu kwenye ardhi). Hizo safari zangu za Europe

nimezifanya ngapi, tunakwenda kunapotolewa Notice hapa na huko

katika University halafu unapeleka Application yako kama

umekubaliwa unakuwemo.

Zote mbili nimekwenda nami simjui mtu yeyote, wote watu

wageni namna kwa namna. Bali kuna moja tukaenda tukapita njia

moja zote bila shaka watu wanachukulia mpaka Paris. Hii moja

tukaenda mpaka Spain, Tukarudi France, tukaingia nchi nyingine za

Europe lakini kwa hiyo kwa njia hiyo nikaona nchi zote za Europe

zote Western Countries. Zote nikazipita, kuzitambua na kuziona.

Safari nyingine ndo ntakuja nende kwenye nchi za Eastern

Countries.

Katika fursa kubwa na faida nilizopata nilipokuwepo

England mara ya mwanzo ni kuingia ndani ya msafara

uliotengenezwa kuzunguuka Europe, ndani ya Coach inakwenda

mbio mbio na kwa raha. Nilikua ndani yake, hii ilitengenezwa na

mmoja katika Walimu wa London University, tukaenda tukapita

English Channel tukaenda France tukafika mpaka Paris tukakaa

baada ya Paris tukateremka kwenda Spain. Tukaenda tukafika

Spain. Hiyo Spain kwa wakati mkubwa ilikuwa nchi ya Kiislamu,

Endlus Waislamu wakatawala, wakajenga, wakakaa wakazaliana

ikawa kama nchi ya Kiislamu.

Kila nchi watu wakawahusudu, wakatamani wawe kama

wao, wakawaiga kama huku. Mwisho walivyokuja watu wakaja

wakawaiga Wazungu – hata wanaandika waandishi wa Kiulaya,

wengine wakasema kua wazee wa wakati ule walikua Wakristo

wakisema: “Ama tumepigwa. Watoto wameharibika namna hii,

wanafwata mambo ya Kiislamu na Kiarabu na kuvaa Kiislamu

na hivi”. Na ustaarabu wao wote kama siye tunavopiga kelele

kuhusu uzungu, na wao walikua namna hivyo hivyo.

Waffaqana llahu Limaa Yuhibb wayardha

Wal - Hamdu Lillahi Rabbil a-lameen.

30.
Katika

ulimwengu

wa

Uislamu

(i)

31.
Vitabu vilivyokwishatoka ni:

*1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st , 2nd & 3rd addition).

*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako.

*3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu.

*4. Knowledge vision & ecstacy.

*5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu (i) .

*6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m.

*7. Kuhifadhi Burda.

*8. Maana halisi ya Imaan (ii).

*9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb.

*10. Siri ya Balaa.

*11. El makhlouq (Viumbe)

*12. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. (2nd addition)

*13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf.

*14. Some aspects of concepts of facility in medevial Islamic

Philosophy by Mwinyibaraka.

*15 maana halisi ya Imaani I (3rd. Addittion)

*15. Njia nyepesi ya kuijua Nafsi yako. (2nd addition).

*16. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa Uislamu ii.

*17. Maana halisi ya Imaani ii (2 nd . Addition)

*18. Mwinyi Baraka katika Ulimwengu wa Uislamu i (2 nd . Addi.).

Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu

(Insha Allah) ni:

*1. Muhammad SAW Bwana wa Mabwana

*2. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition)

*3. Muhammad SAW katika ulimwengu wa Ghayb.

Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:

Majaalis El Ulaa - El Qadiriyya Sinza,

P.o. Box 15170,

Tel: 0747 483 553

Tel: 0748 595 958.

Tel: 0744 023 703.

Tel: 0741 235 091.

Tel: 0744 299 597.

Dar es salaam.

32.
Al habib Seyyid Umar bin Abdallah bin Seyyid Ahmad Al Sheikh Abu

Bakar bin Salim (Mwinyi Baraka ). Amezaliwa Zanzibar katika mwaka

1918. Naye alikuwa ni miongoni mwa vijana walionyanyukia katika malezi

kamili ya Uislamu. Alipomaliza masomo yake ya mwanzo katika Qur an

Aliendelea kuhudhuria Majaalis za jioni katika misikiti mbalimbali mjini hapo.

Alikuwa ni kijana ambaye uwezo wake katika kuhifadhi Qur an na uzingatiaji

katika masomo ya skuli ulikuwa ni wakupigia mfano. Katika skuli, masomo

yake ya msingi na yale ya sekondari aliyapata katika shule za kawaida za

Serikali ya Zanzibar.

Baada ya kufanya vyema katika masomo ya Cambridge, aliweza kuendelea

katika Chuo kikuu cha Makerere Uganda. Kwa muda wa miaka mitatu

alikuwepo chuoni hapo kuweza kuhitimu Shahada ya: “Diploma in Bias and

Biology”. Mara baada ya kuhitimu masomo yake, alirejea Zanzibar ambapo

alianza kufundisha masomo ya Dini ya Uislamu, na pia alifundisha Biology

katika Vyuo Vya Waalimu Dole na Beitil El Rass.

Kwenye miaka ya hamsini mwanzoni, Al Habib alienda tena kusoma

London Uingereza katika School of Oriental And African Studies. Ambapo

alipewa Shahada ya Diploma katika Islamic and Comperative Law. Na pia

alitunukiwa Shahada ya Diploma katika Lugha ya Kiarabu. Aliporejea tena

Unguja katika mwaka 1955, Al Habib aliteuliwa kushika Wadhifa mwingine

tena Principal katika Muslim Academy, kuanzia mwaka 1960 – 1963. kisha

alipatiwa Schoolarship kutoka Commonwealth kwenda Oxford Univesity

Uingereza. Huko alifaulu vyema katika masomo yake “Comperative Religion

And Philosophy”. Hapo akatunukiwa Degree ya Ph.D.

Al habib Umar alikuwa ni miongoni mwa masheikh wanaotuminiwa

katika kuzilea Roho/Nafsi za waumini. Ambao pia wanajulikana kuwa ni

Masheikh wa Kisufi (Taswauf). Miungini mwa Masheikh zake ni pamoja na Al

Habib Umar Bin Abu Bakar Bin Sumeity, na pia Al Habib Ahmad Bin Hussein

Bin Abu Bakar Bin Salim.

Siku ya tarehe tatu March 1988, Sawa na Mwezi 17, Rajab, 1408, Mwaka

wa Kiislamu ilikuwa ni siku nzito iliyojaa majonzi kwa wale wote waliokuwa

wakimfahamu Al Habib Umar Bin Abdallah (Mwinyi Baraka). Kwani

Alitwawafu akiwa huko katika Visiwa vya Comoro.

“Tunamuomba Mwenyezi Mungu Sub hanahu Wata`ala, ainyanyue

juu Roho yake, Yeye pamoja na Masheikh wote wengine, Maulamaa

pamoja na watu wema wote ambao wametangulia katika Imaan”.

“Amin”