You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
YALIYOMO

No.

Ukurasa.

1. Yaliyomo-------------------------------------------------- i.

2. Utangulizi------------------------------------------------- ii.

3. Dibaji------------------------------------------------------- iv.

4. Siri ya balaa------------------------------------------------ 1.

5. Nini siri ya hizi balaa?------------------------------------ 4.

6. Nini cha kufanya?------------------------------------------ 9.

7. Sehemu ya pili “Wakati”----------------------------------- 15.

8. Tukio la kiyama---------------------------------------------- 19

9. Nyakati za Mnyezi Mungu---------------------------------- 24.

i.
بسم

هللا الر حمن الر حيم

UTANGULIZI

Al-hamdullilahi wal khayru wash-sharru bima

shiyati Llah. Allahu mma swalli a`laa habibika Seyyidna

Muhammad wa alih waswahbihi ajmaina wat tabi ina lahum

biihsa nin ilaa yawmid dina. Waba`ad:

Inaonyesha kuwa watu wengi wanaishi bila kujua vipi kuishi.

AJABU. Kufa kila mtu anajua, hata mtoto mdogo haitaji

maelezo yoyote kwa suala hilo la kufa. Kutokana na illa hiyo,

tumeonelea iko haja ya kuandika kijitabu kama hiki ambapo

mtu anaweza kustafidi mengi katika suala la kuishi na

kupambana na mitihani ambayo ndiyo hasa lengo lake. Baada

ya kusoma kitabu hiki utashangaa kuona kuwa umefunukiwa

na akili kiupana ambao labda ingekuchukua siku nyingi

kuelewa hakika yake. Balaa, mitihani, fitna na majaribu ni

neno moja ambalo katika kiswahili hatuna sawa yake. Na hata

tukisema misukosuko haitoshelezi kuwa ndiyo balaa, kwa

sababu misukosuko ni neno jingine kabisa. Mnyezi Mungu

ametaja vifwatavyo kama fitna kubwa kwa mtu ; pesa, mke,

watoto, mali, njaa, mauti, upungufu wa mali na kadhalika.

Lakini wengi watashangazwa na listi hiyo pamoja na kuwa

navyo vitu hivyo siku nyingi sana zilizokwisha kupitia

maishani mwetu. Kila kitu kinategemea ilmu na hakuna lolote

ambalo tunalifanza halina ilmu ndani yake.

Qur an Suratul Twaha 20:50.

"(Musa) akasema: “Mola wetu ni yule liyekipa

kila kitu umbo lake kisha akakiongoza (kufuata kinachowafiki

umbo lake hilo).”

Bila ilmu hatuwezi kuongoza njia - Ndo maana Bwana Mtume

SWA. katuambia:

طَلب العلم فريضة على كل مسلم ومسلمة

ii
(Kutafuta ilmu ni lazima kwa kila muislamu

mume na mke).

Na mambo yote yafanywayo bila ilmu ni yenye

kurudishwa hayakubaliwi. Tutapungukiwa na shida nyingi

tukijua jinsi gani Mnyezi Mungu anavyowajaribu waja

wake na kuwa imara zama za mabalaa kwani:

خيزه وشزه من هللا تعالي

(kheri na shari zote zinatoka kwake Mnyezi

Mungu SWT).

(Amin).

Al-Faqeer,

Ahmad Sheikh,

Majaalis

Sinza,

Shaaban 24 – 1415,

25 – 1 – 1995.

iii
DIBAJI

بسم

هللا الر حمن الر حيم

Tunamshukuru Mwenyeenzi Mungu kwa fadhila zake na neema zake nyingi

sana zisizohesabika. Na Swala na Salaam zimfikie Mtume Muhammad (SAW)

pamoja na ali zake na awaridhiye maswahaba wake wote – Amin.

Amma Baad : Amesema Mola katika Quran takatifu surati Al Ankabuut:

Qur an 29 : 1 – 3.

“Watu wanadhani kuwa wataachiwa pindi wakisema kuwa

tumeamini bila ya kupata misukosuko. Hakika tuliwatiya

katika misukosuko wale ambao waliyokuwa kabla yao wao,

kwa yakini mwenyeenzi Mungu atawatambulisha wale walio

wakweli na atawatambulisha wale ambao ni warongo”.

Ni katika moja ya hekima zake Mwenyeenzi Mungu katika kuwapima waumini

kwa viwango vya imani zao kwake yeye kwa kuwaletea aina mbali mbali za

misukosuko na mabalaa. Na ingawa anavijua Kabla ya kuvipima viwango hivyo.

Na Mwenyeenzi Mungu anafanya hivyo kwa kudhihirisha mapenzi yake kwa

anayemleteya misukosuko na mabalaa, kama alivyosema Mtume Muhammad

(SAW):

ان هللا اذااحب عبدا ابتاله فاذاصبر نجاه واذارضا اصطفاه

(Hakika Mwenyenzi Mungu akimpenda mja humpa mabalaa

na kama akisubiri anamuokowa nayo na akiridhika nayo

humchaguwa (kuwa mja wake wa karibu).

Kwa hivyo basi, muumini wa kweli amewajabika kuridhika na hukumu ya

Mwenyenzi Mungu kwake yeye hata ikiwa ina uchungu wa namna gani. Amesema

Mtume Muhammad (SAW) katika Al-Hadithi Al- kudsiyy;

من لم يزض تقضاى فا لىتجذر تا سوا ى

iv
DIBAJI

“Asiyeridhika na hukumu yangu, basi na

awe na mola asiyekuwa mimi”.

Kupendwa na Mwenyenzi Mungu kwa njia ya kuteremshiwa mabalaa na

misukosuko ni moja wapo ya neema zake ambayo inazalisha ndani yake

neema nyinginezo zilizo nzuri na muhimu kwa maisha ya muumini hapa

duniani, ikiwemo neema na sifa ya subira. Na subira kama alivyosema Mtume

Muhammad (SAW):-

ا لصثز نصف ا ال ى مان

Sote tunaelewa kuwa Mtume Muhammad (SAW) ni kipenzi cha

Mwenyeenzi Mungu kuliko watu wote. Na katika historia ya maisha yake

kama Mtume wa Mwenyeenzi Mungu alifiliwa na mke wake wa kwanza bibi

Khadija RA na kufuatiliya kufa ami yake na mlezi wake Bwana Abiy twaalib

katika mwaka mmoja. Na Bwana Mtume aliusiya kwa kuwita mwaka huo ni

mwaka wa huzuni.

Na alipokwenda mjini Twaaif katika mwaka huo huo kuwahubiriya watu

wake ujumbe wa Mwenyeenzi Mungu wa Dini ya Islam walimpiga mawe na

kuukataa. Na kwa kuwa ni kama alivyoamrishwa na Mwenyeenzi Mungu

katika Qurani Takatifu Surat Al Ahkaaf kuwa awe mwenye subira: Qur an

46:35.

“ Subiri (ewe Muhammad) kama walivyosubiri Mitume

Uwlu-Al-Azim. Nao ni: Mitume Nuhu, Ibrahim, Mussa

na Isa (AS)”v

Subira aliyokuwa nayo Mtume Muhammad (SAW) ndiyo iliyokuwa

moja wapo ya silaha aliyotumia Mtume Muhammad (SAW) katika

kuufanikisha kwa kuufikisha ujumbe wa Mwenyeenzi Mungu kwa watu wote

kama Nabii wa mwisho na Mtume kwa watu wote.

Mwenyenzi Mungu amkubaliye Al Marhuum Sheikh Ahmad Sheikh wa

Majaalis – Sinza athari yake hii aliyetuachia na nyinginezo kwa manufaa ya

ndugu zake Waislam, na alijaaliye Kaburi lake (Kibaha ) bustani miungoni

mwa mabustani ya peponi- Amin.

v

Ahmad Haydar Mwinyimvua,

Dar es salaam Tanzania.

14 Ramadhani 1424,

9 November, 2003.
بسم

هللا الر حمن الر حيم

SIRI YA BALAA:

Bin Adam hana pahala ambapo hupata utakaso wa moyo kama

anapofikwa na balaa. Mfano ambao ameuelezea Mnyezi Mungu

mwenyewe ndani ya Qur an hakuna kama ule anapotokea mtu kuwamo

ndani ya chombo baharini na ghafla ikaanza mchafuko wa hali ya hewa.

Dharuba toka kila upande, mawimbi mazito na makubwa kama mlima

hakuna nchi yeyote karibuni bali ni bahari pana tu, ambayo mwisho wa

mandhari yake mtu kila upande ni ile ya maji kukamatana na mawingu

tu. Mandhari hiyo lau tofauti ni ndogo na ile ya siifu (khasf: yaani:

“ Quick sends” ), ambaye anayetumbukia ndani yake hukiona kifo ni

chenye kumvaa bila ubishi wowote, lakini mtu hujiona kabisa anakufa

na kukata tamaa ya kunusurika kama aliyoipitia Edmond Dause.

Alisema:

“The angry waves and the sight of dangerous

rocks told me that death was near. and the

thought of death made me afraid. I used all my

powers as a man and as a sea man to ascape.

But I did so because I was happy, because I

didn`t coated death, and because I didn`t

wish that I, a living thing made by the service

of God, should became food for the birds and

beasts of the sea……..”.

“mawimbi ya ghadhabu na mandhari ya majabali ya

hatari yaliniambia kuwa kifo kilikuwa kimekaribia, na

mawazo ya kifo yalifanza niogope. Nilitumia uwezo

wangu wote kama mwanamme na baharia hasa, ili

kuikwepa ajali hiyo. Lakini nilifanya hivyo kwa sababu

nilikuwa na furaha; kwa sababu sikuwa nimefunikwa na

kifo. Na kwa sababu sikutegemea kuwa mimi kiumbe

chenye uhai uliotengenezwa kwa huduma yake Mnyezi

Mungu, nije kuwa chakula cha ndege na wanyama wa

baharini…“

1
Katika hali kama hiyo mwanaadamu humuomba Mnyezi Mungu kwa

hali ya unyenyekevu na utakaso mkubwa kweli kweli. Qur an Surat

Yunus: 10:22.

“Yeye ndiye anayekuendesheni katika bara na baharini.

Hata mnapokuwa katika majahazi na yanakwenda nao

Kwa upepo mzuri na wakafurahi nao; mara upepo mkali

Unayajia na mawimbi yanawajia kutoka kila upande, na

wanaanza kufikiri ya kwamba wametingwa. ( Hapo ndipo)

wanapomuomba Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia

utii, (wakisema): “Ukituokoa katika haya, bila shaka tutakuwa

miongoni mwa wanaoshukuru.”

Lakini anapookolewa na akawasili katika ardhi salama kabisa hapo

hapo humfanzia mola wake chungu ya washirika kama siye yeye

aliyekiomba kwa hali ya Ikhlaas kubwa moyoni mwake. Quran Surat

Hud 11:9 –10.

2
“Na kama tukimuonjesha mwanaadamu rehema

inayotokana nasi; kisha tukaiondoa kwake, mara

moja anakuwa mwenye kukata tamaa kabisa na

asiyekuwa na shukurani. Na kama tukimuonjesha

neema baada ya dhara iliyompata mara husema:

“Taabu zimekwisha ondoka kwangu”. (Wala

hashughuliki kufanya mema wala kumshukuru

Mnyezi Mungu). Basi huwa (sasa) ni mwenye

kufurahi sana (na) mwenye kujivuna kabisa”.

Pengine mtu hupewa balaa katika neema, naye mtu hufurahia

na kukongoea kule kukirimiwa kwake. Na anapobalaiwa (tiwa balaa)

katika upungufu wa neema, mara hupayuka akadai kuwa Mnyezi

Mungu amemsahau. Qur an Surat Fajr 89:15-16.

“Lakini mwanaadam, mola wake anapomfanyia

mtihani akamtukuza na kumneemesha, basi husema :

“Mola wangu amenitukuza;” (wala hashughuliki

kufanya mema ili kutengeneza akhera yake). Na

Anapomfanyia mtihani Akampunguzia rizki yake,

husema: “Mola wangu amenidhalilisha, (nikifanya

mema au mabaya ni sawa sawa, hatayashughulikia,

basi naendelea kufanya mabaya)”

3
Kwa nini yapatikane yote haya? Bila shaka sababu ya msingi si

nyingine illa ni ile iliyoelezewa mwenye surat Mulk na nyingine kadhaa

mwenye Qur an. Qur an Mulk 67:2.

“Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni

(kukufanyieni mtihani); ni nani miongoni mwenu

mwenye vitendo vizuri zaidi. Naye ni mwenye nguvu

( na) mwenye msamaha”.

Katika katiba zake Mnyezi Mungu hapa duniani ni kuwajaribu

waja wake. Kwa hali hii neema ni mtihani na nakma ni mtihani pia. Yule

anayeneemeshwa, anatarajiwa kushukuru; na yule alonakamishwa

anatarajiwa kusubiri. Asiyeweza hayo, basi Mnyezi Mungu anasema:

“……….Na atafute Mola asiyekuwa Mnyezi Mungu na pa kuishi

pasokua hapa duniani.” Hadithi hiyo ina mafumbo mazito ndani yake.

NINI SIRI YA HIZI BALAA.

Bwana Mtume S.A.W anatuambia:

4
(Hakika Mnyezi Mungu alotukuka anapompenda

mja wake humpa mabalaa. Basi akisubiri humuepusha

na balaa hilo. Na akiridhia basi humchagua

(kuwa mja wake).

Hadithi hii inatupa maarifa mazuri ndani yake, nayo si

mengine bali ni yale yanayotuwezesha kugundua siri ya kupendwa na

Mnyezi Mungu imo ndani ya kujaribiwa. Tofauti na mapenzi ya

binadamu anayekuletea kisababu, balaa basi huyo hakupendi. Na

anayekukunjulia mkono basi huyo ndiyo anayekupenda na

kukuhurumia

Mnyezi Mungu anafahamisha mwenye Qur an 2: 155-156.

“Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi

ya mambo haya); hofu na njaa na upungufu wa

mali na watu na wa matunda. Na wapashe habari

njema wanaosubiri. Ambao uwapatapo msiba

husema: “hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na

kwake yeye tutarejea (atatupa jaza yake).”

Hiyo: “…Wape bishara njema wenye kusubiri…

Wapashe habari njema…” Inagusia pale pale katika kutarajiwa

yule alonakamishwa kuwa atasubiri. Kusubiri ndiyo jawabu la

mtihani, au majaribio, au balaa.

Bwana Mtume S.A.W. amesema:

"....وماجزاءالصبر االالجنو

5
(Hatukujua jaza (malipo) ya subra kingine

chochote illa ni pepo tu.)

Amesema pia katika hadithi nyingine kuwa:

(Muumini hana, anachokosa akineemeshwa

hushukuru (na si vingine,mwenye kushukuru

huzidishiwa huzidishiwa),na akitahiniwa

husubiri (na malipo ya subra ni pepo).

Kwa hivyo huku anapata na huku anapata. Mnyezi Mungu anaonyesha

ndani ya Qur an kuwa lau angekuwa anawapa kila mtu kwa ayafanyayo,

basi wale wenye kumkufuru na kumshirikisha ndiyo angewapa nyumba

nzuri nzuri za dhahabu na fedha na kadhalika kila wakitakacho. Kinyume

nyume mambo yake Mnyezi Mungu. Sisi huona tukineemeshwa sana

ndiyo eti tunapendwa mno, kumbe huwa ni hatari.

Seyyidna Daud As alikaa mwaka mzima bila ya mtihani wa aina

yeyote, basi alishtuka akamuuliza Mnyezi Mungu VIPI? Au amekuwa

miongoni mwa waliochukiwa mbele yake Sub hana wa Taala?. Na ambao

huwa na mitihani mikubwa kupita watu wote hakuna kama mitume. Basi

na warithi wa mitume nao wasishtuke na kuanza kubabaika yanapowafika

mabalaa. Qur an 2:214.

“Mnadhani kuwa mtaingia peponi na hali

hamjajiwa na mfano wa (yale yalowajia)

wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata

6
mashaka na madhara na wakatetemeshwa

sana hata mitume walioamini pamoja nao

wakasema: “Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika

lini?”. Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu

iko karibu”.

Zipo balaa za kujitafutia mtu mwenyewe- mathalan mtu

kutumbukiza kidole mwenye sega la nyuki na wenyewe wamo ndani.

Zipo balaa nyingine Mnyezi Mungu anaelezea mwenye Qur an

2:195

“Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala

msijitie kwa mikono yenu katika maangamizi –

zo. Na fanyeni wema, hakika Mwenyezi Mungu

huwapenda wafanyao wema”.

Na mifano kama hiyo mingi Mnyezi Mungu kwa rehma zake

atukinge nayo. Mnyezi Mungu anafundisha tena jinsi ambavyo

tutaweza kufaulu katika kukabiliana na mitahani yake. Ni kama

anaetoa jawabu zake mbele kabla ya mitihani kuletwa: Qur an

2:153

7
“Enyi mliomini jisaidieni (katika mambo

yenu) kwa subira na sala, bila shaka

Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri.”

Mnyezi Mungu ndiyo huba kubwa (The greatest love). Na kila

anayependa hua hapendi kuwa (kukaa) mbali na mpenzi wake. Basi ikiwa

amri ya mambo ndiyo iko hivyo, basi ni budi kuzidisha subra zetu kila

siku. Fakhri iliyoje kwa watu kusikia kuwa Rais au Mfalme wa nchi yuko

kwa fulani. Siyo yeye yuko kwa Rais au Mfalme, Aa! Rais au Mfalme ndo

yuko kwake au yuko pamoja naye.

Hakuna njia ambapo anafikilia mja katika bahri ya mapenzi yake

kwa Mnyezi Mungu ila kwa kupitia mabalaa. Lakini kwa sababu nafsi ya

neno lenyewe Balaa siyo kiswahili, uzito wake umekuwa na sura ya

tofauti na vile lilivyo hasa. Katika lugha ya kiswahili Balaa inatupa

tafhuma ya hatari isiyoweza kusubiria ndani yake. Na pia inapotafsiriwa

kuwa ni Fitna ndiyo kabisa na inapotafsiriwa kuwa ni mitihani hapa

kidogo ule mmeremeto wa ubaya unapungua kasi. Kadhalika Majaribio

yote ikiwa ni neno lile lile lakini uzito unazidi kupungua, pamoja na kuwa

kwake maneno yote hayo –Balaa, Fitna, Mitihani na Majaribio hakuna

hata moja la kiswahili. Sasa ikiwa hatujapata neno la kiswahili kwa –

“Balaa”- vipi tunaelewa tutakavyo tu. Mnyezi Mungu anatwambia: Qur

an 47:31.

“Na tutakufanyieni mitihani mpaka

tuwadhihirishe (wajulikane ) wale

wanaopigania dini miongoni mwenu na

wanaosubiri, nasi tutadhihirisha habari

zenu.”

8
Mnyezi Mungu hataacha kuwajaribu waja ili kuona ni nani wa

kweli mpaka dunia imalizike. Sasa wapi tutakwenda ambako hakuna

Mitihani Fitna na Balaa?

NINI CHA KUFANYA:

Baada ya kwisha kupatapata siri ya Mabalaa sasa na

tujiulize nini la kufanya ndani ya ule muda wa kusubiri?. Lazima

turudi kwenye ile Aya ya 153 ya sura Al Baqrah ambapo

tunashauriwa tujisaidie katika mambo yetu kwa Kusubiri na Kusali.

La muhimu ni huko kusali. Kusali kuna maana si moja tu, ya

kusimama, kurukuu na kusujudu. Lakini swala ina sehemu kubwa ya

Dua, nayo ni maombi kwa Mnyezi Mungu. Swala ni Bridge (daraja)

yenye kumuunganisha Mtu na Mola wake, na Ibada maalumu. Sala

ni rehma, na ndiyo maana katika kumswalia Bwana Mtume SAW

hakuna kusimama, kurukuu wala kusujudu, pia katika sala ya maiti.

Kujisaidia mambo yetu kwa sala, tunapata kauli ya Bwana Mtume

SAW kuwa:

(Mnyezi Mungu amejaalia kila kitu silaha,

na silaha ya muumini ni Dua).

Mnyezi Mungu anafundisha vipi tutamuomba; amma kwa jina lake

Allahu au kwa jina lake Rahman Kwingine anatutaka tumuombe

kwa unyenyekevu na kwa khofu, pengine kwa khofu na kwa kutumai

(confidence) na kwa siri au kwa fakhri au kwa sauti ya juu wala si

kwa sauti ya chini lakini baina yake. Qur an 17:57.

“Hao wanaowaomba (wenyewe) wanatafuta

ukaribiano na mola wao; (hata) walio karibu

miungoni mwao (na Mungu, kama malaika wao

wanafanya yaya haya) wanatumai rehma Zake

na wanaogopa adhabu yake. Hakika adhabu ya

Mola wako ni ya kuogopwa.”

9
Wengine hufanza Tawasssul nyingi nyingi tu, kwa sababu

Mnyezi Mungu ni mwenye kupenda kuombwa na huchukia asipoombwa.

Kinyume na sisi. Tusipoombwa hufurahi, na tunachukia - illa wachache tu

labda, tunapoombwa. Mnyezi Mungu anawataja waja wake wema kwa

kutuambia: Qur an 51:19

“Na katika mali zao ilikuwako haki ya kupewa

maskini aombaye na ajizuiaye kuomba.”

Pia katika Suratul Ma’arij 70:24-25.

“Na ambao katika mali zao iko sehemu maalumu.

Kwa ajili ya aombaye na anayejizuilia kuomba

(japo muhitaji)”.

Sisi tunajitoa katika sifa tukufu kama hizo kwa kuchukia kuombwa.

Kwa hiyo kumuomba Mnyezi Mungu ndiyo jawabu tunapokuwa mwenye

mabalaa. Siku nyingi zilizopita waliteseka baadhi ya watu kwa sababu ya

kumuomba Mnyezi Mungu mpaka ikafikia kuambiwa: Qur an 22:40

10
“Ambao wametolewa majumbani, (mjini) Mwao

pasipo haki ila kwa sababu wanasema: “Mola

wetu ni Mwenyezi Mungu.” Na kama Mwenyezi

Mungu asingaliwakinga watu, baadhi yao kwa

wengine, bila shaka yangalivujwa mahekalu na

makanisa na nyumba nyingine za ibada na

misikiti ambamo Jina la Mwenyezi Mungu

hutajwa kwa wingi. Na bila shaka Mwenyezi

Mungu humsaidia yule anayesaidia Dini Yake.

Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na

Mwenye kushinda.”

Subra ikienda na dua na matendo mema, ndipo Mnyezi

Mungu huepushia watu mabalaa yao. Na miongoni mwa jawabu

hakuna kama ISTIKTHAAR (kufanza wingi ) mambo ya swadaka na

ISTIGHFAAR (kutaka msamaha) kwake yeye Mnyezi Mungu.

Mambo mawili hayo yanapata ( Support ) kutiwa nguvu na aya : Qur

an 71:10-12

"Nikawaambia: Ombeni msamaha kwa

Mola wenu. Hakika yeye ni mwingi wa

Msamaha. Atakuleteeni mawingu yanyeshayo

mvua nyingi. Na atakupeni mali na watoto,

na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito.”

Vile vile Mnyezi Mungu amesema: Qur an Suratul Anfal 8:33

11
“Lakini Mnyezi Mungu hakuwa wa kuadhibu

maadamu wewe ( Nabii MUHAMMAD )

umo pamoja nao ( Hapa Makka ), Wala Mnyezi

Mungu hakuwa wa kuadhibu pia hali ya kuwa

(Baadhi yao wamesilimu ) wanomba msamaha.”

Mtu angetaka aambiwe na nani zaidi ya Mnyezi Mungu hakaik

za namna hiyo ili asikie na kutekeleza. Tazama fadhila za ISTIGHFAAR

zilivo pewa ubora na faida. Mnyezi Mungu anaacha kuwaadhibu

washupavu watenda dhambi katika mji wanapopatikana wenye kuleta

ISTIGHFAAR. Kutokana na wao Mnyezi Mungu anastahi kuwaadhibu –

Ni madogo Hayo ? – Lakini ndiyo kwa vile watu hawataki kutambuwa

wala kuwathamini.

Jambo la pili ni swadaka ambapo Mnyezi Mungu

katika hadithi aliyofahamisha Bwana Mtume SAW kuwa:

الصدقة تدفع غضة الزب

(Swadaka hukinga ghadhabu ya Mnyezi Mungu).

Jee hatuoni fawaida zake ndani ya uhai na maisha

yetu ya kila siku? Inataka mtu achunguze na kufanza

majaribio, hiyo ni ibada tosha na ya uhakika (Creative

worshiping).

Jinsi gani Mnyezi Mungu anavyojaalia mitihani kwa

waja wake. Mwenye mali mitihani yake mingi ni kwenye

mali yake na dhidi ya hali yake, ndiyo kusema masikini.

Wengi wenye mali walizipoteza kwa sababu ya

kuwanyanyasa masikini. A`lim mtihani wake katika ilmu na

dhidi yake kwa wajinga. Bwana Mtume SAW alisema kuwa:

(Ilmu hupata maafa wakifundishwa wasiokuwa watu

wake).

12
Halkadhalika masikini na mahakimu nao wana mitihani yao.

Watu wanne hao tumewaonyesha kwa kuwa wao ndio nguzo

zilokamatia ulimwengu jinsi vile alivyosema Bwana Mtume SAW.

Kwa ujumla Mnyezi Mungu hukinga balaa zetu na

hupunguza ghadhabu zake kwetu kwa ajili ya swadaka. Basi jambo

hilo lingefaa lidumishwe kwa sababu faida zake ni za kuonekanwa

kwa macho hasa, na mambo yetu yamghadhibishayo Mnyezi Mungu

ni mengi. Mambo haya wapo wengi ambao hawana habari nayo

pengine hizo swadaka huchukulia kuwa ndiyo ZAKA.

Lakini tofauti ni kule kuwa swadaka ni ya hiyari, na zaka ni

ya lazima. Swadaka unaweza kumpa mtu yeyote, lakini zaka ni

lazima muislamu anaestahiki kule kupata zaka. Amma sivyo

itakuwa haijaswihi na utakuwa hutahisabiwa kuwa umelipa, na

itabidi kuirudishia tena.

Insha Allah Mnyezi Mungu atuwafikishe katika

kheri tuongokewe kwa yetu, sisi na waislamu wenzetu.

Na tuweke matumaini ya dhati kuwa tutajibiwa kwa

lolote tunaloliomba. Na ndio maana Mnyezi Mungu

akatuambia kuwa: Hadithil Quds:

“Lau wangekusanyika pahala pamoja watu

wote wa mwanzo na wa mwisho, binaadam

na majinni kila mmoja akaomba alitakalo

kwa Mnyezi Mungu katika shida zake, basi

Mnyezi Mungu angempa kila mmoja na

isingekuwa imepungua chochote katika

hazina yake”.

Labda kiasi kile kile cha uzi uliotumbukizwa baharini,

ukanyonya maji na kushirabu barabara.

Huyo ndiye Mnyezi Mungu aliye mkarimu mno na mwenye huruma

isiyomithilika kwa viumbe, Mkwasi mwenye kuneemesha waja wake

atakavyo, wengine anawakunjulia wengine anawakadiria.

Mambo yote tuloyataja na kufahamisha ndani humu ni yake

na kule kuyatekeleza na kuyafuata ndiyo maana ya uislamu.

Qur an 3 : 83

13
“Je! Wanataka dini isiyokuwa ya

Mnyezi Mungu, na hali kila kilichomo

mbinguni na ardhini kinamtii yeye,

kikipenda kisipende? Na kwake

watarejeshwa wote”.

14
Sehemu

ya

Pili

15
WAKATI

Na tarehe yetu yote ni daraja sekunde dakika na saa – SAA!

Wakati umegawika katika mafungu matatu, manne :

i. Uliopita ( Past )

ii. Uliopo ( present )

iii. Ujao ( future )

iv. Milele ( Eternal or Eternity ).

Waliopita huenda waliyajua ya kwetu kama: yajayo; na

wajao hawajui ya kwetu wala waliopita na yajayo. Kwa hivyo

sisi tumekuwa bora kuliko waliopita. Mnyezi Mungu anasema

(ili kuthibitisha ubora wetu kwa kawli fupi kama hii): Qur an

3:110.

“Nyinyi (ndio mmekua ) umma bora (miongoni mwa

nyumma) zilizoletwa kwa watu------“.

Hadithi:

Imetokana na Seyyidna Omar (R.A) alisema:

“Siku moja tulikuwa tumekaa na Bwana Mtume

SAW. Hapo alitokea mtu ambaye nguo zake

zilikuwa nyeupe Pepe na nywele zake zilikuwa

nyeusi sana; hakuwa na alama ya machofu

ya safari na wala hapakuwa na hata mmoja

katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu

na Bwana Mtume SAW. Akiweka magoti yake

karibu na magoti ya Bwana Mtume SAW aliweka

viganja vyake juu ya mapaja yake, akasema

“Ewe Muhammad nambie kuhusu Uislamu.”

Mtume wa ALLAH SWT alisema: “Uislamu ni

Kukiri kuwa hakuna Mungu isipokuwa ALLAH

16
Na Muhammad ni Mjumbe wake, kusali, kutoa

zaka, kufunga Ramadhani, na kwenda Ma

kka ukiweza”. “Umesema kweli”, alisadikisha

yule mgeni. Tulipigwa na mshangao kwa kumuuliza

na kisha yeye muulizaji kusadikisha.

Akauliza tena “Nambie kuhusu Imaan”. Akamjibu

Ni kumwamini Mnyezi Mungu, Malaika

Wake, vitabu Vyake, Mitume wake, Siku ya

kiyama na kuamini kuwa kheri na shari zote

Zinatoka kwake.” “Umesema kweli” akasadi-

Kisha yule mgeni. Akauliza tena: “Hebu

Nieleze juu ya Ihsan”. Alisema SAW: Ni kumuabudu

Mnyezi Mungu kama vile unamuona japokuwa

humuoni yeye anakuona.” Akauliza

tena. “Niambie juu ya kiyama”. Bwana Mtume

SAW alisema: “Anaeulizwa hajui zaidi

Kuliko aneuliza”. Yule mgeni akasema: “Nambie

alama zake”. Alisema SAW “Kijakazi atamz

aa bwana wake na utaona wachunga wenda

miguu chini, wenda uchi, mafukara (wasiokuwa

na hata makazi) wakishindana kujenga majumba

ya fakhri. Muda mfupi baada ya yule mgeni

kuondoka, Bwana mtume SAW akauliza:

“Ewe Omar jee unamjua ni nani yule aliekuwa

akiuliza? “ Nilisema “Mnyezi Mungu na Mjumbe

wake wanajua zaidi.” Alisema ni Jibril

alikuja kuwafundisha Dini yenu (Kwa njia ya

maswali)”.

Imepokewa na Muslim.

17
Wakati seyyidna Jibril AS (The holy ghost ) alipomshukia Bwana

Mtume SAW ( katika karne ya saba) ili amfundishe DINI (ISLAM) kwa

njia ya kumuuliza maswali, akawa anasadikisha kila alipojibiwa, swala

lilikuwa moja zito sana. Lakini aliomba afahamishwe dalili zake tu baada

ya kujibiwa kua “Hakuwa mwenye kuulizwa kwacho ( hicho kiyama)

mwenye kujua kuliko muulizaji”. Bwana Mtume SAW alielezea dalili

zake tu, nazo zilikuwa kama hivi:

i. Mjakazi ( Amati – pia ni jam-u ya umma) yaani: mama.

ii. Utaona wenda miguu chini na uchi, wachunga

mbuzi (cowboys) wakipitana kwa majumba marefu marefu

(Zama ambapo sky scrappers za USA hazikuwepo).

iii. Wanawake wanapokosa haya na kuota mikia.

iv. Qur an itapodharauliwa na kudhalilika.

Bwana Mtume SAW aliendelea mno kuelezea watu juu ya dalili za kiyama baadae

kiasi cha kujenga picha kama hii:

v. Mbali itapokuwa karibu. - ( Ibara hii inadhihirisha umuhimu

wa usafiri kwa vyombo viendavyo mbio kuliko ngamia na

farasi - Kwani wakati farasi anakimbia mfano wa masafa ya

maili sitini kwa saa, roketi itafunika masafa yenye maili

ishirini na tano elfu kwa muda huo huo), na mara mbili ya

roketi, challenger inakwenda maili hamsini elfu katika saa

moja.

vi. Chuma kitapotamka.- ( Mfano wa redio, simu na Telex ambazo

hazikuwepo katika zama zile ).

vii. Mtu mweusi kutawala – ( labda katika zama zile mtawala

mweusi alikuwa ni Mfalme Nagash wa Ethiopia, na katika karne

ya kumi na tisa dunia imejaa watawala weusi, aliyajuaje Bwana

Mtume Muhammad SAW haya?).

18
TUKIO LA KIYAMA:

Tofauti kati ya mwislamu na kafiri ni kuamini mambo ya ghayb ( fact

in exisence) mwislamu ni lazima aamini kiyama kuwa kitakuja bila

shaka yeyote (without any doubt) lau sio lazima kujua kuja kwake.

Qur an Naziat 79:42-44

“Wanakuuliza kiyama kutokea kwake

kutakua lini?. Uko wapi na kuweza

kutaja (wakati wa kuja kiyama ). Mwisho

(wa ujuzi ) wake uko kwa Mola wako.”

Mnyezi Mungu anamweleza Mtume wake Nabii Muhammad

SAW kwa kawli ya wazi wazi kua kipo, hicho kiyama, lakini wale tu

wanaokiogopa ambao watakumbushika, wengine laa !. Na katika dalili

za wazi wazi ambazo ni muhimu kuzijua kwa jicho la mazingatio ya

hali ya juu kabisa ni hizi:

1. Kudhihiri Mahdi

2. Kutokea kwa Dajjaal (Atazaliwa akiwa na jicho moja

kama walivyokuwa kawmu NISA. (Amerika katika noti

yao ya dola 100 ambapo inaonyesha picha ya jicho moja,

utadhani walipata habari zake).

Huyo mlaghai mkubwa jitu moja lenye fitna kubwa kabisa,

ambaye atadai uungu kama alivyodai Firauni wa zama za Nabii Mussa

AS, na tofauti ya muda wa Firauni miaka mia nne, Dajjaal atadumu

duniani kwa muda wa siku arubaini ambazo ni tofauti na siku ya

kawaida. Siku kumi za mwanzo kila siku moja itakuwa kama mwaka

(kwa hiyo ni miaka kumi) siku kumi za pili kila siku moja kama mwezi.

Siku kumi za tatu kila siku yake ni kama wiki moja Na siku kumi za

mwisho kila siku ni kama siku ya kawaida.

Kwa hiyo, siku kumi za mwanzo ni kama miaka kumi. Kumi la pili ni kama

miezi kumi. Kumi la tatu ni siku sabini, ( yaani miezi miwili na siku kumi). Na kumi la

nne ni siku kumi. Jumla ni miaka kumi na mbili na siku ishirini.

19
Dajjaal ataingia kila nchi duniani kudanganya na kufitinisha watu.

Ulaghai atoutumia kama vile kumfufua aliekufa siku nyingi na kuleta

mvua na kuotesha mazao mashambani utavutia watu mno kiasi cha

kumwamini kuwa mungu. Yeye atakuwa na pepo na moto. Wataomkubali

atawatia ndani ya pepo yake, wataomkataa atawatia motoni. Lakini ukweli

wa mambo ni kinyume nyume. Watoingizwa peponi ndiyo watoingia

motoni, na wale watoingia motoni ndiyo watoingia pepo ya Mnyezi

Mungu wa kweli. Nchi pekee ambazo hataingia Dajjaal ni Makka na

Madina.

3. Kuteremka seyyidna Isa AS. (Ambaye

atakuja kumpiga vita na kumuondoa (huyo

Dajjaal). Baadaye ataishi siyo kama Mtume, bali

kama mja mwema aliye mchaji ). – Ataoa ataishi

miaka arubaini atakufa, na Madina katika Rawdha

karibu ya Bwana Mtume SAW ndipo atazikwa.

4. Kutokea Juju wa Majuju. (Ambao Dhyl Qarneyn)

aliyewafungia ndani ya ukuta fulani tangu siku hizo hadi leo

hii bila shaka.

5. Kutokea kwa Dabba. (Mnyama wa ajabu ). Mnyama huyu

atawasemeza watu yale ambayo wanakataa kuyakinisha.

Hakika hii .inafahamishwa kwetu na Qur an ya Mnyezi

Mungu; kwa kila mtu kujipatia mwangaza wa mbele kabla

kuwadia wakati wake ambao kutokea karne hii ya ishirini na

moja sio mbali tena.

Tunaanza kuzoeshwa kumzowea mnyama huyo kabla ya kufika

kwake ili tu, tusifikie mshtuko ambao unaweza kuitoa roho ya mtu mbichi

mbichi. Mfano wa “Mapi show” Unajihusisha vizuri sana.

Mnyama huyo atakuwa na mwendo mkali mno, hatakikosa

atakachokifukuza wala hakitampata kitachomfukuza. Ataandika usoni

mwa muumini: “huyu ni mtu wa peponi”. Na uso wa mtu huyo utang`aa

sana. Na katika uso wa mtu wa motoni ataandika: “huyu ni ka fir” na uso

wake utapiga weusi. Na leo praktizi za kujitia weusi zimeanza hali ya

kuwa huyo Dabba wenyewe hajaja. Dabba atakuwa miungoni mwa dalili

za mwisho tena.

6. Kuchomoza jua magharibi ya ardhi:

Hii ni ishara ya wazi wazi yenye kuogofya ( kuogopesha)

mno – Allahu Akbar. Bila ya shaka ionekanapo hitilafu

katika maumbile bin adam hushangaa,

20
hushtuka na pengine humiliki hali fulani akataka afanze

ambalo uwezo wake ungeruhusu.

Viumbe vyote vimezoea kuona jua likichomoza toka mashariki ya

dunia kwenda magharibi. Lakini siku hiyo litachomoza toka magharibi

na kuja zake hadi katikati ( kama inavyokuwa saa sita, saa za kulingana

kinvuli ), na litarudi huko huko maghribi.

7. Utapodhihiri moshi: Moshi uliokusudiwa hapa ni ambao

utaenea dunia nzima. Moshi huu utakuwepo duniani muda wa

siku arubaini. Moshi utakuwa ukitoka puani, machoni na

kwenye duburi ( tupu ya nyuma ) ya kila kafir mpaka

ataonekana kama mlevi.

Hali hii ya kuonekana watu walevi na hali hawakunywa pombe,

bali ni adhabu ya Mnyezi Mungu ni kali. Imetajwa ndani ya Qur an

ikiashiria juu ya dalili za kiama vile zitavyojionyesha. Taathira ya

moshi kwa muumini itakuwa kama mafua mafua tu hivi. –

Hizi ni miungoni mwa taabira ( prophecies ) alizozielezea Bwana

Mtume SAW. Na kila mtu ni muhimu azijue mapema na kuwafundisha

watoto wake.

8. Kuharibika Al Kaaba: Baada ya kufa nabii Isa AS. Na

kuzikwa Madina, Al kaaba itaharibika juu ya mikono ya

Habash.

Katika karne ya saba wakati wa uzawa wa Bwana Mtume SAW

Al kaaba ilitaka kuharibiwa na Abraha – Ambaye alikuwa mfalme

muhabesh aliyeweka jeshi lake Yemen. Mnyezi Mungu alituma jeshi la

ndege -Ababiil - wakiwa na vijiwe midomoni idadi ya jeshi zima la

Abraha, wakawa kama majani yaliyotafunwa na kisha yakatemwa.

Baada ya tukio hilo hakuna nchi yeyote duniani iliyojasiri kutaka

kuihujumu nyumba ya Mnyezi Mungu mpaka hii leo. Lakini

ipo kawli toka kwa Bwana Mtume SAW kuwa katika akheriz zaman

madola makubwa ya dunia yatapata kishawishi kutaka kuihujumu

lakini Mnyezi Mungu atawateremshia mabalaa mjini mwao washindwe

kujitambua nafsi zao. Hakika ya Al kaaba inabaki kuwa ni nyumba ya

Mnyezi Mungu ambayo iliyojengwa na Seyyidna Ibrahim ASW.

akisaidiana na mwanawe Seyyidna Ismail AS. Na ni pahala pa amani

siku zote, na hilo limetimia tangu wakati wa seyyidna Ibrahim ASW

mpaka leo, si chini ya miaka elfu sita iliyokwishapita.

21
9. Kunyanyuliwa Qur an: Qur an ndiyo kitabu cha mwisho

kwa wanaadam duniani, na kiliteremshwa kwa Bwana

Mtume Muhammad SAW katika karne ya saba, wakati

dunia ilikuwa imezama katika ujaahili. Ikiitwa “Dark age”.

Bwana Mtume ndiyo Mtume wa mwisho aliyeteremkiwa na roho

mtakatifu (The holy ghost ) naye hakuwa msomi wala kuandika hakuwa

anajua. Hakika hiyo ilikuwa hoja kubwa na yenye nguvu kweli. Lakini

haikusaidia kuwafanya wapinzani wa uislamu wajizuie kumtuhumu kuwa

ameiandika yeye. Ajabu ni kwamba wenye ilmu hata wakikusanyika

pamoja kuandika mfano wake wasingeweza na wala hawataweza

Pambano liko wazi kama watapatikana wa kuandika wajitokeze.

Wengine wamemsingizia kuwa Bwana Mtume SAW alijitangazia

utume yeye mwenyewe. Kwa wenye kujua vipi mitume

inavyotayarishwa, madai kama haya hayawapi taabu kwa vile

yaliyodaiwa na majaahili waliorubuniwa na mabwana zao watafanya

nini?. Miungoni mwa kawli zake Bwana Mtume SAW kuhusu mfano

kama huo uliobeba kichwa cha maneno, ni ule wenye kuelezea kuwa:

“Zitakuja zama hautabaki uislamu illa jina

lake tu, na haitabaki Qur an illa maandishi

yake tu ( Rasmuhu )”.

Usemi huo unaonyesha kuwa zama hizo ( na huenda zimeshafika )

watu hawatajishughulisha na kusoma Qur an, kwa hiyo Qur an itafanana

na nyumba iliyohamwa - lakini kunyanyuliwa Qur an ni yenye uzito

tofauti kabisa, kwani hata vifuani haitakuwepo na katika kurudi watu wa

ardhini kuwa makafiri hiyo ndiyo hatari zaidi. Mfano wa kuidharau Qur

an mpaka kufikia wazee kuwashughulikia mno watoto wao kwa masomo

ya kizungu kuliko Qur an ambayo ni rahisi mno, ni moja miungoni mwa

dalili za wazi ambazo zinatuonyesha wapi tunakwenda!.

Pia kupuuza sala kwa nyudhuru za nguo chafu na kila siku

tunazifua kwa masabuni chungu mbovu. Vipi Bwana Mtume SAW

asemee juu ya sala kuwa ndiyo nguzo kuu ya uislamu, kwa hivyo

mwenye kuisimamisha (Iqamu swalat ), basi amesimamisha dini

(Uislamu ), na mwenye kuitupa akaipuuza, basi ameivunja dini. - Halafu

mtu ajifanze hamnazo na kwa makusudi aiche hiyo sala?. Basi kama

imedaiwa kuwa watu wa ardhini watarudi kuwa makafiri, basi, ni wazi

kuwa zoezi lake limeshatwaa nafasi.

22
Amma kwa dalili za kiyama, kila muislamu anajua kwa hiyo siyo

rahisi kuvutiwa na hadithi za dhana dhana na kudanganya watu. Mfano

wa utabiri wa Pop wa 1959 kuwa mwaka 1960 ingekuwa mwisho wa

dunia. Miaka arubaini baadaye utabiri wa Nishel Nostrodamus kwa july

4 na kama hizo. Kiama hakitatokea ila chini ya bendera ya uislam.

Kiama hakitatokea mpaka akosekane katika uso wa ardhi ambaye

anasema: “Allah, Allah"; Lau baadhi ya dalili zimeisha jitokeza,

mfano wa kwenda uchi, wanawake kukosa haya, wanawake kuwa na

mikia, na nundu kama ya ngamia kichwani, mbali kuwa karibu, vyuma

kuzungumza na mtu mweusi kutawala. Lakini hizo tisa bado kuanza

hata moja. Mambo yatakapokuwa tayari, bila shaka yeyote tutaanza

kuzishuhudia moja baada ya moja kama tutakuwepo.

23
NYAKATI ZA MNYEZI MUNGU:

Mnyezi Mungu ndiye aliyeutoa wakati ambao yeye haumuhusu

kitu chochote. Wakati wanasayansi wanaitakidi kuwa ili ufanzike wakati

ni budi kuweko ( vitu vitatu ) Nafasi yaani Volume. Mnyezi mungu

kaenea kila pahala, kwa nafasi haimhusu chochote. Masafa yaani

Distance ( hapa na kule ), Mnyezi Mungu haitaji masafa. Na ili upatikane

wakati vile vile ni lazima kuwepo Kasi yaani Speed, au mwendo, ( bila

ya shaka ni wa kuzunguka). Kwa hoja hii wamehusisha maumbo yaliyoko

mbinguni ambayo yote ni yenye kuzunguka. Mnyezi Mungu haimpasii

jambo hilo hata siku moja. Mnyezi Mungu ameelezea juu ya wakati katika

Qur an: Suratus sajadah 32:5

“Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya

mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake

kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni

miaka elfu mnayotumia nyinyi katika

kuhisabu kwenu”.

Katika mfumo huo mwenye akili timamu hatakosa kuona hizi saa

24 zetu ni fupi mno kiasi cha kumaanisha kuwa saa 1 yake ni miaka 41. 16

au miaka 42.4. Tukitizama katika sura ya pili inayoelezea wakati. Tutaona

ndani ya: Quran suratul ma`arij 70:4

“Malaika na roho hupanda kwake katika

siku ambayo muda wake ni miaka elfu

hamsini”.

24
Katika sura hii tunaona kuwa saa moja yake ni sawa na miaka

2083-2088. Mtu mwenye akili timamu hakosi kuona kuwa katika saa

yake hiyo ni kiasi ambacho kinamfikia Nabii Zakari AS, Yunus AS, nk.

Mtu akitafakuri juu ya mtoto wa digi digi aliozaliwa na baada ya saa

moja tu anaenda mbio na mama yake, wakati binadamu labda miaka

miwili na zaidi ndio aje kumudu zoezi hilo, basi ni sawa na kusema:

“Saa moja ya digi digi ni sawa na miaka

miwili ya mwanaadam”.

Ndani ya nyakati mbili hizi mtu yoyote mwenye akili

hatokosa kuona kuwa suala la: “kupitwa na wakati”, kama

ilivyozoeleka mno kwa vijana wa leo, ni kama upumbavu

mtupu. Msemo huu unawaandama masikini wa kutafakari

katika jamii.

Katika wakati wa kwanza na wa pili walioudiriki ni Seyyidna

Adam ASW na Mama Hawwa AS. Katika wanaadamu. Na pia

wamediriki huu wakati wetu wa masaa 24. Wakaishi hadi miaka 1001

(elfu moja na moja ) hapa duniani.

Wanasayansi waliochunguza na wakakubaliana kuwa ndiyo

hakika kwamba mwanga wa jua unatembea miaka 186 elfu kwa sekunde

moja, nyota aina ya GALAXY katika muda huo huo inakwenda kiasi

cha maili 105 ya mwanga, ambapo kila mwaka wake mmoja ni sawa na

miaka Trillion sita (6, 000,000,000,000,000,000 ). Suala la kupitwa na

wakati hapa ni la kipumbavu kabisa.

Mfano wa Betilquise ( Beyt jawzaa ), nyota moja

kubwa mno, imethibitishwa kielimu ( Science ). Mwanga

wa jua kwa spidi yake ya 186,000 maili kwa sekunde,

itakuwa kiasi cha miaka 32 elfu kufikia mara moja na si tena

illa baada ya miaka elfu 32 mingine. Na papo zipo nyakati

ambazo haziwezi kuingia ndani ya akili ya mtu. Dakika

moja ni sawa na miaka mia tano ya anga.

Na upo huo wakati wa milele ambao ndani ya akili

ya mtu haufikirikiki kabisa. Mnyezi Mungu ndiye anayejua

– Wallahu ya`alam bi swa waah.

WABILLAHIT TAWFEEQ.

25
Al habib Al Faqeer Ahmad Sheikh Mohamed Sheikh Msiha,

amezaliwa Singida mkoa wa Dodoma, mwaka 1938. Amepata elimu ya

sekula Unguja na amebahatika kupata elimu ya juu katika chuo maarufu

Afrika ya Mashariki Makerere Uganda.

Elimu yake ya Dini ameipata hapo hapo Unguja toka kwa Masheikh

mbali mbali, baadhi yao ni:

Sheikh Sleiman Alwi (Muhib Rasul) (Al Marhum).

Sheikh Seyyid Mansab.

Maalim Himid (Al marhum).

Maalim Hemed Muhamed El Buhry.

Sheikh Seyyid Qamus.

Sheikh Muawwiya Ibn Abdul Rahman.

Sheikh Ally Muhamed Comorian.

Sheikh Ibrahim Mzee Ahd.

Sheikh Haj Mzee Ahmad Msiha.

Amma Elimu ya Nafsi na Roho Amepata Ijaza yake toka kwa A`limu

mkubwa Duniani Al Habib Sayyid Omar Bin Abdallah (Mwinyi

Baraka).

Sheikh Ahmad amewahi kufanya kazi katika jeshi la Polisi

Tanzania Bara katika mikoa mbali mbali mpaka alipostahafu.

Katika umri wake wote Sheikh Ahmad alijahid katika kuendeleza

Uislamu kwa kusomesha na kuandika vitabu vya mada na maudhui

mbali mbali katika Uislamu. Pia alianzisha Majaalis Sehemu mbali

ambazo ziko mpaka leo, Mtaa wa Pemba, Sinza, Bungoni, kijito nyama,

Sadani (Ilala) na Kibaha (Misugusugu) ambapo ndipo ilipo Dhwarihi

yake (alipozikwa).

Sheikh Ahmad ametwawafu 27. 8. 2001. ( Mwezi 7 jumadda thany

1421 H.R.). Akiwa na umri wa miaka 63, vile vile alivyokuwa akiomba

aishi umri ule ule alioshi kipenzi chake Bwana Mtume Muhammad

SAW.

Insha Allah Mnyezi Mungu amjaze kheri na alitie Nuru kaburi lake

(Amin).

Majaalis El Ulaa El Qadiriyya,

Sinza Dar es Salam.