You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
YALIYOMO:

No.

Uk.

1. Yaliyomo………………………………………….……..iii.

2. Dibaji……………………………………………………iv.

3. Utangulizi…………………………….………..……...….vii.

4. Nafsi………………………………………..………….…1.

5. Roho/Nafsi…………………………………….…….……9.

6. Tiba ya Nafsi Khabbith…………………………………..13.

7. Akili……………………………………..……….…...…...19.

8. Moyo………………………....……………..………...…...25.

9. Jedwary la Nafsi…………………………………………...28.

10. Jinsi ya kuachana na Mwili……………………...………...29.

iii.
DIBAJI:

Bismillahir Rahmanir Raheem.

Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu,

Mfalme wa siku ya malipo yeye peke yake ndiye anayesitahiki kuabudiwa

na hakuzaa wala hakuzaliwa.

Anasema Mwenyezi Mungu katika Kurani Takatifu Surat

Yusuf Aya ya 53:

“….Nami sitakasi Nafsi yangu, kwa hakika kila

Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa

ile ambayo Mola wangu ameirehemu”.

Maneno haya ya katika Kurani Takatifu aliyoyaelezea kumueleza

Mtume Muhammad (SAW) yanamhusu Mtume Yusuf Bin Yakuwb (AS)

alipokua anajitetea kuwa hakumtaka mke wa Mfalme wa Misri.

Anamhakikishia kuwa “Nafsi ni yenye kutuamrisha sana maovu”

isipokuwa iliyorehemewa na yeye Mola. Na hii iliyorehemewa na Mola

ndiyo Nafsi ambayo yenye muelekeo mzuri yenye kumtii Mwenyezi

Mungu na kumuabudu na ndiyo inayoitwa “Al Mutmainna” aliyoitaja

Mwenyezi Mungu katika Kurani Takatifu Surat Alfajr:

Ewe Nafsi iliyotulia rejeya kwa Mola wako

hali ya kuwa utaridhika (kwa utakayoyapata)

na Mwenyezi Mungu aridhike na wewe, basi

iv.
Kupigana Jihadi na Nafsi ni jukumu kubwa linalotukabili katika

maisha yetu ya hapa Duniani. Mfano alivotupigia Sheikh Ahmad katika

kitabu hiki Uk. 11 wa Sheikh Abdul – Kaader Jeylani (Q.A.S.A)

kuwa alichukua miaka kumi na tano maporini akifanza majaribio

kuishinda Nafsi yake. Na akaishinda na kuitawala barabara. Na kuitawala

huko ni kufikia kilele cha ucha Mungu na akawa mmoja wa Mawalii wa

Mwenyezi Mungu. Na kabla yake alikuwepo Walii nchini Alyaman jina

lake Abuwmuslim Al khawalaniy aliyempinga Al aswad Al ansiy

aliyekuwa akijidai Unabii na Utume wakati wa Mtume Muhammad

(SAW) alikamatwa na wafuasi wa Al ansiy na wakamtiya katika shimo la

moto ili aunguwe. Moto haukumuunguza wala haukumchubuwa kama

ilivyotokea kwa Mtume Ibrahim (AS), hii ni karama alizozionyesha walii

huyu Abuwmuslim kwa kuishinda Nafsi yake. Kwa hivyo basi na

tujitahidi kuzipiga Jihadi Nafsi zetu kwa sababu ndizo

zitakazotusababishiya kuingizwa ima Peponi au Motoni. Amesema

Mwenyenzi Mungu katika Kurani Takatifu

Surat Al – Imraan, 185 :-

“Kila Nafsi itaonja mauti na bila shaka mtapewa ujira

wenu kamili siku ya kiyama, na aliyewekwa mbali na moto

na akaingizwa peponi, basi amefuzu, na maisha ya Dunia

hii ni starehe idanganyayo”.

Mwenyenzi Mungu amjaze kheri Sheikh Ahmad kwa juhudi zake

za kuandika kitabu hiki kwa kuwanufaisha na kuwazindusha ndugu zake

Waislamu.

WAMA TAWFIYQIY ILLA BI LLAAH.

AHMAD HAYDAR MWINYIMVUA,

DAR ES SALAAM.

vi.
Bismillahir Rahmanir Raheem.

UTANGULIZI:

Al-hamdulillah na si vingine bali ni ukweli usiokanushika kua

Mnyezi Mungu ndiye pekee mstahiki wa kila Swifa njema na Rehma zake

Mola pamoja na amani zimwendee mjumbe wake wa mwisho Bw. Mtume

Muhammad (SAW ) Mwalimu mkuu mno, aliyefundisha Umma huu wa

mwisho Ilimu zote tunazozijua kuanzia siku zile za jahilia mpaka leo hii

ambapo huyu humfundisha huyu na kuendelea mpaka siku ya mwisho

ambayo kiitikadi tunaimani kua ipo na itawadia tu bila khilafi wala

khiyari.

Suala lililochukua uzito katika kitabu hiki Akili ni moja

miongoni mwa Mas-la mazito na lilo muhimu sana. Na mwenye akili

hushughulishwa mno na yote yenye kutaalaki na Akili maana kama

iwavyo vyovyote vile.

Wana wa Elimu ya Viumbe vyenye Uhai (Biologists) wa kileo

wanakubali kutoijua khassa Akili ni nini. Hatua moja kubwa walopiga

katika suala zima la akili ni kua kwake Ubongo wa mbele ya kichwa

(Cerebrium) ni kitovu cha akili. Hii imepatikana kutokana na majaribio

ya muda mrefu.

Wana sayansi hao wameelezea ndani ya vitabu kadhaa-wakadhaa

mfano wa “The Exploring Biology” ambapo ndani yake wameelezea

kua hatua moja kubwa walioifanza kutokana na majaribio kadhaa ni

katika kugundua ya kua akili Mahir (ile ilo kusanya mambo matano –

macho, pua, sikio, ulimi, na mikono) na hiyo ni akili (isio julikana kua

kitu gani) ni vilowekwa katikati ya hiyo Cerebrium.

Akili yenyewe ikiwa ni matenda kazi ya hiyo Cerebrium kama

vile uhai ni matenda kazi ya nyanja muhimu za uhai (Protoplasm).

Linapoulizwa suala la akili na wapi katika mwili wa mtu ambapo

Mnyezi Mungu ameiweka. Wengi huona kua akili ipo kichwani, lakini

Mwendawazimu pia anacho. Hakuna

vii.
Mwendawazimu ambae hana kichwa lakini matendo yake siyo ya mtu

mwenye akili.

Akili bila shaka ni lazima tuijue amma sivyo haitokuwa rahisi

kudai kua nayo. Kutokana na kujiingikiwa nayo wengi katika ndugu

zangu tumeona kuwepo umuhimu mkubwa kuandika fatwa kwa njia ya

kipetopeto.

Hakuna shaka kabisa kua baada ya kupata hakika yake itakua

tumepiga hatua kubwa kiasi ilobaki ni wewe kutafuta njia za kuiongeza.

Njia zipo basi mwenye akili hataziacha bali atazitafuta kwa udi na

uvumba, na usiku na mchana.

Tunamuomba Mnyezi Mungu atunufaishe kwa kijitabu hiki na

kutufungulia kila lenye kuhitajika katika kutujenga kua watu wenye Akili

kweli.

Nahisi siwezi kukwepa kuwashukuru wote ambao walioandaa

darasa la kila Juma tano pale Ilala kwa Akh Fuad Batarfy, Sharif Karama,

Ba Ally Bin Mkhashshe, Seyyid Hussein

El Bayti, Sheybob, Akh Said Okash, Moh’d Batarfy, Saleh Hariz, Ababili

Abdallah na wengineo ambao si rahisi kuwaorodhesha majina yao hapa.

Bidii yao katika kuzishughulikia nuskha hizi kuzichapisha katika

Computer na kadhalika ni moja inayoonyesha wazi kua ni wenye kupenda

ilmu. Na haidhaniwi kua mwenye raghba ya ilmu si mwenye akili.

Mnyezi Mungu atawajaza ziada ya vile ilivyoelezwa kua ni bora kuliko

wenye kupigana vita vya jihadi, na Mahujaji na wafanzao Umra.

Huwatakia maghfira ( hao wapendao ilmu) Mbingu na Ardhi na

bahari miti na wanyama, pia mawe, na kila chenye kuchomozewa jua juu

yake, na huko akhera malipo yao anayajua Mnyezi Mungu Sub hana

wa Taala.

“Ishi hapa duniani ukiwa Alim au

Mutaallimi (mwenye kujifunza), au

Mustamian (mwenye kusikiliza ilmu)

usiwe mtu wa nne utahiliki.”

viii.
Hii ni kawli yake Alayhi Afdhalus Swalatu Was Salaam, Bwana Mtume

Muhammed (. S. A.W).

Al Faqeer Ahmad sheikh,

Majaalis El Ulaa,

El Qadiriyya, Sinza

Dar es salaam,

Tanzania

Swafar – 21

9 may 2000.

ix.
Nafsi na Sifa zake:

Al hamdullilah, waswalaatu lilahi taala wa salaamuha ala rasulillah.

(S.A.W).

Amma baad, Suala la Nafsi hii ambayo tunayo ndani ya miili yetu

ni kubwa na pia zito, kwa hiyo basi haitakuwa jambo la akili kulipita hivi

hivi tu minighayri ya kujishughulisha na kulijua kwake.

Bwana Mtume (S.A.W) amelisemea hivi:-

“Man arafa nafsahu

faqad arafa Rabbahu”

“Mwenye kuijua nafsi yake bila

shaka ameishamjua Mola wake”

Sababu ya kusema hivi kumjua Mnyezi Mungu ni wajibu wake

mtu wa kwanza katika uhai, na njia nyepesi ya kumjua mola ni katika mtu

kuijua Nafsi yake.

Kuijua Nafsi ni kujua makamu za Nafsi. Hii ina maana ya kujua

manzili zake saba kwa swifa na matendo yake.

Ya kwanza:

Nafsi Ammaara.

Ambayo Mnyezi Mungu Sub-haana wa Taalah ameisema ndani

ya Qur an kama:- S:12:53

1.
“Mimi sijitakasi nafsi yangu, kwa hakika (kila)

nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu, isipokuwa

ile ambayo Mola wangu ameirehemu. Hakika Mola

wangu ni mwingi wa kusamehe (na) mwingi

wa kurehemu”

Hii ndiyo nafsi ovu na khabbithi kupita zote, kwa mujibu wa kauli yake

Alayhis-swalaatu Llahi Taala waa-lihi.! “Nafsi hii ni khabbithi zaidi

kuliko mashetwani sabini”

Inakutosha kuangalia zile sifa zake, ili kuthibitisha kauli yake

bwana Mtume S.A.W wewe mwenyewe uelewe ya kwamba kila

unapojishughulisha na kuifuatilia kwa karibu zaidi ndiyo jihadi kubwa

kwako na kukuingizia thawabu nyingi ndani yake.

Sifa za Nafsi Ammaarah

Kupenda kula sana

Ubakhili

Kuhangaika

Kua na tamaa

Kuwa na kiburi (Wall yadh Billah)

Matamanio

Hasada na

Ghafla

Sifa zote hizi ni zenye kumpeleka mtu kwenye kuhiliki kwa adilla

na ushahidi madhubuti toka kwa Bwana Mtume Alayhi

swala waatul-Lahi wa salaamuhu.

Ya pili: Nafsi Lawwaama.

Hii ni Nafsi inayojilaumu laumu, Seyyid Umar Bin Abdallah Bin

Al-ba-shaikh Abiibakar Bin Salum ( Mwinyi- Baraka) akisema :- “Haina

njia nyingine, ni kujilaumu”

Lakini Mnyezi Mungu ameisemea vizuri. Ameiapia:- 75:1-2

2.
“Naapa kwa siku ya kiyama tena naapa kwa nafsi

inayojilaumu. (Kuwa imefufuliwa na mtalipwa)”

Sifa za Nafsi Lawwaama:

Kujilaumu laumu.

Fikra.

Kujizuia (Qabdh).

Ujubi

Lalamika lalamika

Asili ya kuwa na sifa hizo ni kwamba ni kutaka kujiondosha

kabisa katika Nafsi Ammaara kwa vitendo vyake vyenye kwenda

kinyume na maamrisho ya Mnyezi Mungu.

Nafsi Mul-hama.

Ya tatu:

Nafsi zote takribani zimetajwa hakika zake mwenye Qur an. Hii

imetajwa ndani ya:- Suratish-shams. 91:7-8-9-10.

“Na kwa nafsi (roho na aliyeitengeneza kisha

akaifahamisha uovu wake na wema wake. Bila

shaka amefaulu aliyeitakasa ( Nafsi yake) na

bila shaka amejihasiri alieiviza (Nafsi yake)”.

3.
Sifa za Nafsi Mul-hama.

Ilmu.

Tawaadhui.

Tawba.

Subrah.

Tahaamul - kuvumilia adha.

Kiakili tu ukizilinganisha swifa hizo na zile za nafsi ya kwanza

utaona ipo tofauti kubwa mno ndani yake. Ndani ya nafsi hizi unaona

wazi kuwepo Uislamu ndani yake, kama unavyoweza kuona kuwepo

ukafiri ndani ya nafsi ya kwanza. Hiyo ni hatua

kubwa katika kujijua. Ni hatua kunjufu katika jihad ya nafsi

ambayo Bwana Mtume (S.A.W) ameihimizia.

Nafsi Mutmainna.

Ya nne:

Hii ndiyo Nafsi pekee ya kwanza iliyotulizana kabbisa, haina vituko

ndani yake, na, “Iliyosemezwa na Mnyezi Mungu Khasa”. Qur an

89:27.

“Ewe Nafsi yenye kutua.”

Huko ni kunadiwa na Mnyezi Mungu mwenyewe lakini bila shaka

ukiweka mazingatio ya kweli utaona kuwa ni miujiza mikubwa imo

mwenye mnada huu kwa wenye akili.

4.
Sifa za Nafsi Mutmainna:

Ukarimu.

Tawakkul.

Hikam.

Ibaada

Shukar na Ridhaa.

Hizo ni miongoni mwa sifa nzuri mno ambapo mtu anakua nazo

ndani ya Uhai wake hapa duniani. Mawalii wote bila shaka ni wakarimu

kwa hiyo kila anaye tamassak na sifa hii basi ametammasak na sifa ya

Mnyezi Mungu. Nasi tumeusiwa na Bwana Mtume S.A.W. tujitabiishe na

sifa nzuri nzuri za Mnyezi Mungu. Amma katika kushukuru kuna Uislam

mzima ndani yake.

Nafsi Radhiya.

Ya tano:

Nafsi hii imetajwa mara tu baada ya Mutmainna ndani ya Suratil Fajar

katika juzuu ya “Amma.” Nafsi iliyo ridhiya.

Sifa za Nafsi Radhiya:

Zuhdi (Kuipa nyongo dunia).

Ikhlas.

Wara`a.

Kuacha yasomuhusu mtu.

Wafaa`i – Kutekeleza.

Miungoni mwa sifa njema ambazo zimeibeba Nafsi hii hamna kama

Ikhlas ambayo Shaytwani anaikhofu mno. Qur an imesema hivyo siyo

mwandishi. Pia katika msururu wa utajo wa Nafsi tatu hizo, hii ndiyo

yenye kukamilisha yaani:-

5.
Nafsi Mardhiyya.

ya sita:

Nafsi hii imetajwa mara tu baada ya Nafsi Radhiya yaani ilo ridhiwa

na Mola Sub-hana wa Taalah. Amma mtu akisha ridhiwa na Mnyezi

Mungu basi hua hana haja ya kuogopa chochote tena.

Sifa zake:

Husnul khuluq – Tabia njema

Lutf kwa viumbe.

Taqarrab ila Llah – Kuacha yote yasiokuwa ya Mnyezi Mungu.

Tafakkur - Katika utukufu na ukubwa wake Mola.

Kuridhika na alokugawia Mnyezi Mungu Sub-hana wataala.

Nafsi hiyo inatakiwa kurudi kwa Mola wake Radhiyya.

Hali ya kuwa Mardhiyya hivyo basi, inatakiwa iingie katika kundi la waja

wake Mnyezi Mungu.

Waja wote ni wa Mnyezi Mungu lakini wapo ambao ni speshel.

Amma katika walioukubali uja hakuna kama Bwana Mtume Alayhi

Afdhalu Swalaat Was-salaam.

Mtume Muhammad S.A.W Ni mja wake na mjumbe wake. Mitume

wengine wote wanamfwatia Nabii Muhammad .S. A W. kama Sayyidna

Issa AS. ametajwa pia kama Abduhu warasuluhu lakini wamepitana

kwa daraja na fadhila. Na pamoja na hayo yote pia Mtume SAW anasema

ya kuwa…..“Hajifakharishi- Katika kuwa kwake Bwana wa watoto

wote wa (Nabii Adam A.S.W).”

Nafsi Kaamila.

Ya saba:

Pengine huitwa Nafsi Swafiyya, yaani iliyokuwa safi

6.
kabisa. Kwa nini? Kwa kuwa sifa nzuri nzuri zote zimo ndani yake.

Sifa zake:

Sifa zote njema zilizotajwa katika Nafsi tano ukiacha Nafsi ya

kwanza ambayo ni Ammara.

Bwana Mtume S.A.W amesema:- “Kupigana na Nafsi ndiyo jihadi

kubwa”

Hakuna juu yake Jihadi nyingine yaani ile Jihadi ya Panga ambayo

humfanya anayekufa ndani yake kuhisabiwa kuwa “yuko hai” haifui dafu

kabisa hapa.

Nafsi na makamu zake:

Mpaka kufikia hapa bila shaka umeishaipatapata kiasi ambacho

hakukupi shaka ndani ya moyo wako. Nini wamesema Maulamaa

wakubwa wakubwa katika Uislam?.

Wachache tu mfano wa akina Ghazzal, Busri na labda Habibi

Ahmed Bin Abubakkar Bin Sumeit aliyekuwa Zanzibar katika karne ya

kumi na nane mwishoni na kumi na tisa.

Imam Ghazzal ameelezea vizuri sana mas-ala ya Nafsi, Roho na

akili ndani ya vitabu vyake vya “Ihyaa ulumud deen”.

Imam Busri ameelezea vizuri ndani ya “Burda” kitabu mashuhuri

ambacho Waislamu wengi wanakijua na kukifanzia kazi katika matukio

kadhaa wa kadhaa ndani ya uhai wa kila leo, katika Tawassul za kila

siku. Yeye amesema kuwa:-

“Nafsi ni kama mtoto mchanga ukimwacha

atapondekea kunyonya na ukimzuia ataacha”.

Nafsi haina cha ujana haina cha uzee, ikimshika mtu hua hasikii

kitu katika waadhi wala nasaha. Tazama katika kuiachia kula sana kama

Punda inavokutia uvivu na kadhalika.

7.
Amma Habib Ahmed ndani ya Kitabu chake. “ kawkabur zaahir”,

anasema.:- “ Nafsi ni kama smaku”. Chunguza smaku utaona inayo

pande mbili. Upande wa kuvutia, upande wa kufukuzia. Ule wa kwanza

ndiyo wenye kukufanza ukamili katika maovu na ule wakuzuia ndiyo

unaokukataza kufanya maovu.

Qur an 79.40-41

“ Na amma yule anechelea kusimamishwa mbele ya

Mola wake akaizuia nafsi yake na matamanio

basi pepo ndio mashukio yake”

Suala la kujizuia ni muhimu mno na ni Jihadi ya kila mmoja, kwa

hiyo siyo mambo ya Sheytwani bali “Wewe binafsi yako”.

Na kila unapoanza amali njema inakuwa inatakata sehemu kwa sehemu

mpaka inang’aa kama Nuru, na hapo ndipo unapohesabika kua mtu

kamili. Amma sivyo, basi wewe ni kama wanyama wengine wowote

(mammals).

Mnyezi Mungu atuwafikishe katika kheri.

8.
ROHO/NAFSI

Qur an: 17:85.

“Na wanakuuliza habari ya roho. Sema, roho ni jambo

lililohusika na Mola wangu (Mnyezi Mungu) nanyi

hamkupewa katika ilmu (Ujuzi) ila kidogo kabisa”.

Ushahidi wa aya hii ni wenye kuonyesha wazi wazi kua upo ujuzi

wa Roho. Na pamoja na kua kidogo au kiduchu tu. Ndiyo makadirio

ambayo Mnyezi Mungu ameonelea kua ni yenye kutosha kabisa kwa hapa

duniani.

Katika misemo yetu ya Kiswahili ni ule msemo:- “Maji ya kifuu ni

Bahari ya chungu” (yaani yule mdudu mdogo na mwepesi sana – mdudu

wa sukari pengine mdudu chungu).

Huo ni mfano mmoja tosha kwa mtu mwenye akili ya kujisaidia nayo

angalau kidogo tu; ni wazi kuwa hatahitaji maelezo marefu ya aina

yoyote.

Tukiangalia kwa mazingatio kauli ya Bw. Mtume S.A.W juu ya

Rehma za Mnyezi Mungu tunaelewa fika kua ni “moja kwa mia moja”

kwa jumla tangu dunia ianze mpaka kufikia kiyama. Bila shaka moja kwa

mia ni sehemu ndogo mno, na hapo mpaka leo hii karne ya Ishirini na

moja mwaka huu wa Elfu mbili watu bado wangali wanarehemeana bado.

Na hasa ukiongezeka usemi wake kua:

“Warehemuni walioko ardhini atakurehemuni

aliyeko mbinguni”.

9.
Basi kidogo hiyo ni yenye kutosha kabisa. Pengine ingekuwa ni

Rehma mbili katika zile mia ndo ziloshushwa ungesema watu

wangeshindwa kufanza mambo mengine yoyote bali wangekuwa

wanarehemeana tu. Wapo watu wengine wanafikia kuikanusha kisirisiri

au kipumbavu kiuchache wa ilmu. Aya hiyo: 17:85 wao wakidai kua

hamna anaejua mambo ya roho illa Mnyezi Mungu .

Mnyezi Mungu anaijua mno hiyo Roho; anasema kua ametupa ujuzi

nayo lakini ni kuduchu. Si busara kuchukua kidogo ya Mnyezi Mungu

ukaifanza kua ndo hiyo hiyo kwako wewe Mwanadamu, na huku ukidai

kuamini kua: –

“Hana anayefanana naye hata mmoja”.

Kuna hatari ya kufikia kujichukua wewe kama Alim-Sameeun

(Unaesikia ) Basweerun (Unaeona) na kadhalika, kua ndo hiyo hiyo ya

Mnyezi Mungu (Mnyezi Mungu apishilie mbali fikra kama hizo kwetu).

Mnyezi Mungu anamuona na kumsikia sisimizi michang’ato yake

chini ya ardhi ndani ya giza la usiku, Je Shekhe, wewe wasikia hivo hivo?

Mnyezi Mungu anayajua ya siri na yalofichika ndani ya siri katika vifua

vya watu. Jee na wewe Sheikh ni hivo hivo? Basi Staghfiru kwa Mola

wako na ukithirishe Kalima ya Tawheedi usije ukahiliki kwa kujifanya

kichwa Mchungu. Uislamu unataka unyenyekevu (Sub-Mission).

Na isisahaulike kua Bwana Mtume SAW amekataza malumbano na

kwamba mwenye kuacha kulumbana (kubishana na hali ya kua yeye ndio

mwenye haki basi (malipo yake) siku ya kiama Mnyezi Mungu

atamjengea Nyumba ya Dhahabu). Na ikiwa kwa waliopewa Chuo (Ahlil-

Kitab) Basi malumbano yawe “Bil-lati Hiya Ahsan” kwa njia ya wema

sana. Kwa nini?; kwa sababu ni mara chache tunakumbuka kua mtu

anapopinga jambo hua na maana ya kufru. Kwa hiyo basi huenda mtu

akawa na Sijda yake usoni lakini ni Kafiri.

10.
Lau kabla ya kubishia jambo ambalo amelisema ambae hana ushuhura

katika Jamii, tungezingatia katika kawli aizungumziayo kua ni yake au ya

Mnyezi Mungu ingekuwa rahisi kuyahukumu mambo kwa njia ya Amani

na busara ya hali ya juu ambayo haingemgandamiza mtu. Ilmu iwe ya

manufaa siyo ya fadhuli.

Al Habib Seyyid Umar akisema:- “Suala la Nafsi / Roho si la

kusemea kidogo tu kisha ukaliacha, utapoteza watu”. Yeye

mwenyewe ilimchukua masaa matatu kuelezea juu ya Nafsi alipotoka

Makerere University Uganda ambako alikua na kina Nyerere, Obote,

Yusufu Lule na wengine kadhaa aliowataja ambao baadae walishika

nyadhifa kubwa kubwa katika Serikali za Afrika Mashariki.

Sheikh Abdul-Qa dir Jeylani (Q.A.S.A) alichukua miaka kumi na

tano maporini akifanza majaribio ya kuishinda Nafsi na hatimae

akaishinda na kuitawala barabara. Na miungoni mwa natija ni ile ya

kufunguliwa mambo mengi makubwa makubwa yalojaa karama, yote

hayo hayajaja kwa upendeleo bali Mujaahada.

Na katika mda wote huo alikua akifunga kila siku - labda siku moja

tu alifungua kwa sababu ya maskini mmoja alietaka kumuombea mtu Dua

lakini kwa sharti ale nae pamoja, Basi alifungulia kwa ajili hiyo -

Chambulecho Al Habib:-

“Nini Swaumu ya miaka kumi na

tano kwa Dua ya masikini huyu”.

Nafsil Ammaara haina inapopata taabu kama katika Swaumu. Basi

kwa apendae kupata Sa’ada ya Nafsi yake na aanze na tabiya hii ya

kufunga funga.

Swaumu za Twaa (Tatwa-w-u’e) kama vile Jumatatu na Al-Khamisi

na siku za mwezi kumi na tatu kumi na nne na kumi na tano za kila

mwezi. Huenda ukahisabiwa kama aliyefunga Dahar nzima. Kumbuka

kauli ya Al - Mustwafa S.A.W:-……

“Mwenye kufunga Ramadhani akafatanisha na Sittatish-

Shawwaal (Siku sita za Shawwal) hua kama aliyefunga Dahar….”

Sababu ni Basweet kwa kuchukua malipo ya kila jambo jema

11.
Thawabu 10; Jumla ya siku thelathini na sita kwa Thawabu kumi

inafanza siku za mwaka mzima (Dahar) yaani siku mia tatu na sitini, na

hali kadhalika funga ya Ayyamul-Beydh 13, 14 na 15 ya kila mwezi kwa

miezi kumi na mbili ya mwaka mzima inafanza siku 36 zenye Thawabu

kila moja inakuja ile ile mia tatu na Sitini ambazo ndo Dahar. (Tazama

Hikma ilivyo ajabu kiasi gani ndani yake).

Amma katika Khatwir (mapenzi ya jambo lenye kuvutia moyoni)

yake Bw. Mtume SAW Alivutiwa mno na Swaumu ya Nabii Daudi

Babake Nabiy-Allah Suleiman A.S - ambae alikuwa akifunga siku moja

na kula siku moja.

Majaribio hayo yote hassa si vingine Illa ni yenye makusudio ya

kumtengeneza mtu ili awe mwema na mwenye Swifa za kuwa

Mtawala alokusudiwa na Mola Subhana wa Taala hapa Duniani (The

divine’s viceregent).

Njia nyepesi mno katika kushinda Nafsi hii ilokwisha

kukudhihirikia ukhabith wake mda mrefu sasa tangu ubaleghe hadi hii leo

hakuna kama kwenda kinyume ya swifa zake ambazo tayari

umeishazifahamu .

Maswahaba zake Bwana Mtume SAW, Radhya-Allah Anhum

wakifanza majaribio katika kila jambo lililohitaji muamalla zama za

kuteremshwa wahyi toka kwa Mola wa ulimwengu zote.

Tukumbuke la maana angalau moja katika natija na faida nzuri katika

majaribio (Experimantations) nalo ni kuongezeka akili.

Sasa hebu na tuangalie katika ya kuhitaji kuyafanzia kazi leo kabla kesho

kuhusu hii Nafsi khabith.

12.
Jinsi ya kuitibu Nafsi khabbith.

Kupenda kula sana: Basi dhidi yake ni kufunga – Swawmu. Bw.

Mtume SAW alisema:-

“Sisi ni wale ambao hawali mpaka wawe na

njaa na pindi tulapo basi hatushibi huondosha

mkono hali ya kuwa hatukushiba na hatuna njaa”.

Mfalme mmoja aliita matabibu ili wampe dawa ya kuondosha maradhi

yote. Wakamwendea mabingwa katika fani ya Twiba toka Arabuni , India

na Afrika (Sudan) Mwarabu alimwambia kuwa ni Habba Soda. Muhindi

alimwambia kua ni maji ya moto Asubuhi kabla ya Stiftahi na usiku

wakati wa kulala. Pakapita kimya kiasi ambacho kilimpelekea amuulize

Twabib Mwafrika vipi mbona uko kimya au umeshindwa? Bwana

Mwafrika akasema:- “Bwana Mfalme, ni kweli Habba Soda imesemewa

na Bwana Mtume SAW kua inatibu maradhi yote ila mauti, na lau na

mauti yangekuwa na dawa, basi Mnyezi Mungu angeweka mwenye

Habba Soda. Amma kwa maji ya moto tumbo hulainika na mafuta

mwilini huyeyuka hivo basi, mtu upunguza unene. Lakini dawa ya

maradhi yote hakuna kama kula wakati mtu una njaa, na kuondosha

mkono kabla hujashiba (na kuvimbiwa), njia hii huwa ni kinga kabla

kujitibu.”

(Preventetion is Better than Cure).

Mfalme akasema kuaTwabib Mwafrika ameswibu na kuhibu yaani

ndiye aliyepata.

Ubakhili: Kinyume chake ni ukarimu – Sukhaa.

Bakhili ni Aduwwal-Llah hata kama ni mchaji mtaabbadi

Mkubwa, na karimu ni kipenzi cha Mnyezi Mungu hata kama

ni faasik.

Kuhangaika: Dhidi yake ni utulivu ambao unaandamana na Nafsi

Mutmainna.

13.
Kua na tamaa: Zingatia ule usemi “Tamaa mbele mauti nyuma”.

Kinyume chake ni kinaa na kule kukinai ni utajiri mkubwa, anasema

Mtume wa Mnyezi Mungu.

Kuwa na kiburi: (Mola atuepushe nacho) Dhiddi ni kujitupa chini

kua Mnyenyekevu.

Hata ikibidi kufanza aina ya shughuli ambazo lau atakuona yeyote

yule basi hatakosa kupata hisia kama za kudharauliwa. Hiyo ina kheyri

zaidi kuliko kutukuzwa ukapata kiburi.

Matamanio: Lau huanguka kwa kufunga Swawmu tu. Lakini ziada

ni katika kuyakumbuka mno Mauti. Bwana Mtume SAW alieleza

kua katika kuyakumbuka mauti imma itamfanza mtu apungunze

maasi au atazidisha Ibada.

Mfano utabiri wa Pope mwaka 1959 kua 1960 ingekua mwisho

wa Dunia, wa Moshi Kilimanjaro walibakia Makanisani kuanzia Krismas

mpaka January, ni wenye kutosha kuthibitisha ukweli wa kuyakumbuka

mauti ni waadhi kamili, na ambae hawaidhiki kwa mauti, basi huyo hana

waadhi.

Hasad: Amma kuhusu Hasad ambayo Bw. Mtume SAW amesema:

“Ni ugonjwa usio na Dawa”. Illa kuacha tu kule kuhusudu, mtu wa

akili anatakiwa kuyazingatia sana maanani huenda akanusurika.

Maisha ya hapa Duniani yamejaa majaribu, kwa hiyo mtu mwenye

akili nae anatakiwa afanze majaribio kwa kila jema alolijua. Akili haina

njia ya kuzidi kama katika mtu kua na ungi wa Tajiriba (Frequent

Experimentation Culculation and So on and so Forth) katika

majaribu makubwa tulonayo hasa katika zama zetu hizi hakuna kama

“Wanawake”. Bwana Mtume SAW akisema :-

14.
“Sijakuachieni baada yangu fitna ashaddu

kuliko wanawake”

Tuondoshe au tupunguze habari za: “Aa!! Sikataka mwenyewe!” Al-

Habib (Mwinyi Baraka) akisema :- “Itafaa wapi si kataka

mwenyewe“. Ni nzuri mtu kua mwema hasa anapokua kijana aliyejaa

Ghururi ambazo daima humzunguka kweli kweli. Wakati wa ujana ndo

aghlabu huvutiwa na mambo ya ajabu ajabu ya maisha ya ghururi.

“Haingii peponi ambae ndani ya moyo

wake ana punje ndogo ya kiburi.

Kadhalika Ubakhili umuaduisha (humfanza awe adui wa Mnyezi

Mungu ) Na pia adui wa Nafsi yake yeye mwenyewe. Na vipi mtu huyo

kua rafiki ya mwingine? Amma ni kweli kua:

“Sakhii alie Faasik ni Mahbub mbele za Mnyezi

Mungu, kuliko Bakhili mchaji Mungu”.

Juwa ewe mtafuta matukufu kwa Mnyezi Mungu Mtukufu ya kua

Mnyezi Mungu anapotaka kufanza mmoja ya waja wake kua Walii

(Rafiki) Basi, humpamba kwa sifa hiyo ya ukarimu na tabiya njema.

Tumeishaona jumla ya sifa njema katika Nafsi sita, sifa ambazo ni

zenye kumtosha mtu kujipamba nazo ili afanikishe katika kua mja wa

Mnyezi Mungu wa kweli kweli.

Na mtu anapofikia kua kipenzi cha Mnyezi Mungu basi hua hana

hofu juu yake na kila siku hua ni mtu wa mafanikio mazuri. Kila

analolitaka Mnyezi Mungu atampa thamma atampa. Hivyo ndivyo

asemavyo yeye mwenyewe Sub-Hana wa Taala katika hadithi takatifu

(Hadithil- Qudsi)

Kila unaemsikia kua ni walii basi kafikia Daraja hiyo kwa

maagizo hayo yaliyomo mwenye Hadithil-Quds, na kwa kumpenda mno

Bw. Mtume Muhammad Alayhi Swalawatullah Wa Salamuhu. Nasi

Inshaallahu Taala tupate Tawfiqi ya kweli ndani ya kupigana jihadi

kubwa hii dhiddi ya Nafsi vile alivyotuusia Bwana wa Mabwana, Bwana

wa Watoto wote wa Sayyidna

15.
Adam . ASW. Bwana Mtume S.A.W. amesema:

“Lau ningechaguzwa juu ya Utume ninataka kitu

gani nisingechangua isio kua tabiya njema kwani

kila cha ziada (Fadhila) ni chenye kuondoka na

kwisha, isipokuwa sifa njema; Kwani hizo hubaki

na wewe (milele)”.

Ni nani baada ya Mnyezi Mungu na Mtume wake mkweli wa

mambo kuhusu yote yamuhusuyo mtu hapa Duniani? Swifa nzuri na tabia

njema ndo zimfanzazo mtu kuonekanwa mtu amma sivyo, mtu hua ni

mnyama tu (Mammals-Biologists wanasema).

Na pengine mtu huzidiwa na Wanyama kibaadhi ya sifa. Matendo

yote ayafanzayo mtu pia Mnyama huyafanza pamoja na kutokuwa na

akili. Lakini wakati asiyekuwa na akili anamsabihi Mola muumba na

kuswali swala ambayo Mnyezi Mungu na huyo Mnyama anaijua, basi

mwenye akili mtu hua chini ya Mnyama. Na hivyo ndivyo ilivyosimuliwa

mwenye:

Qur- An- 7:179.

“ Na bila shaka tumewaumbia Moto wa Jahan-nam

Wengi katika Majini na wanadamu (kwa sababu

hii) Nyoyo wanazo lakini hawafahamu kwazo

(hawataki kufahamu kwazo) na macho wanayo

lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo, lakini

hawasikii kwayo. Hao ni kama Wanyama, bali wao

ni wapotofu ( Wapotevu) zaidi – hao ndio

walioghafilika”.

16.
Suala la pepo na Moto si suala la mtu kujipangia, amma sivyo hangeingia

yeyote Motoni. Lakini suala la kufananishwa mtu ambaye Mnyezi Mungu

amemtukuza kupita viumbe vyote hapa Duniani aje kufananishwa na

Mnyama asiye na akili na papo awe mpotevu zaidi, hilo ni tusi zito sana.

Mambo ya kweli kama haya inataka mtu aweze kuyazingatia na

kuazimia azma ya kweli kujibadilisha kwa kadri ya uwezo wake pamoja

na kumuomba Mnyezi Mungu amuongoze kwa Rehma zake.

Mnyezi Mungu anajua sana jinsi uzito wa Mitihani yake ulivyo kwa

mtu katika mapambano yake na Nafsi yake, Matamanio, Dunia na

Sheytwani, Basi, hakuna haja ya kukata tamaa na Rehma zake Sub-Hana

Wataala.

Tazama vile Mnyezi Mungu atuambiavyo katika: Qur an 39:53

“Sema, “Enyi waja wangu mliojidhulumu Nafsi

zenu, msikate tamaa na Rehema ya Mwenyezi

Mungu bila shaka Mwenyezi Mungu husamehe

Dhambi zote. Hakika yeye ni mwingi wa kusamehe

(na) mwingi wa kurehemu”.

Al –Habib (Mwinyi Baraka), Akisema: “Hakuna dhambi

inayomshinda kuisamehe ila Shirk”. Kawli hii ukiitia maanani

unapata matumaini ya moyo kua Mnyezi Mungu ni mzuri mwenye

huruma mno kuliko Mama kwa kichanga chake.

Tusisahau pia vile alivyotuusia Bwana Mtume S.A.W. katika

maneno yaliyojaa hikma ndani yake kua:

“Mtu ni hadithi (Mazungumzo tu) baada yake,

basi (Tu) jitengenezee hadith nzuri kwa

watakaokuja kusimulia (Baadae)”

17.
Tena na tena na tumuombe Mnyezi Mungu atupe Tawfiqi na mioyo yenye

nguvu katika kuishinda mitihani yake kwa wingi wa Subra na shukurani

kwa Jaha ya Bwana Mtume Muhammad Swallallahu Taala Alayhi wa

Alihit-wahiraati-Ummahaatil Muslimiina. DUNIANI. (Amin).

18.
AKILI:

Ni Nuru ya kung’aza, Mnyezi Mungu ameiweka ndani ya Moyo

wa mtu na daima hunga’ara kwenye ubongo ambao uko kichwani katika

mtu.

Mfano wa karibu kabisa ambao mtu wa kawaida anaweza

akaipata-pata kirahisi ni ule wa Projector na Screen katika kufanza

kazi pamoja, bila ya ushirikiano si rahisi. Ndo kusema tumuonapo mtu

kaharibikiwa basi huwa hiyo Johari ya akili ndo iliyoathirika kwa hiyo

huo ubongo wenye Awnsi kumi na sita hua haufanzi kazi kabisa.

Bw.Mtume SAW amesema:-

“Usimlilie aliyekufa mlilie ambae amepungukiwa

na akili yake”.

Chombo pekee kilo Azizi kwa mtu hakuna kama Akili, na hiyo

ndiyo yenye kutafautisha baina ya mtu na Mnyama.

Ukifungua Qur an utaona sehemu nyingi imetajwa Akili. Na ni

kutokana na matendo gani hasa ndo mazingatio ya dhati

yanapochukuliwa. Aya ifwatayo ina mengi ya kuzingatia

Qur an 2:164:-

19.
“Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi,

na katika kuandamizana usiku na mchana na katika

(mwendo wa) vyombo ambavyo hupita katika bahari

kwa (kuchukua vitu) vifaavyo watu, na (katika

kumiminika ) maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu

kutoka Mawinguni na kwa (Maji) hayo akaihuisha ardhi

baada ya kufa kwake Na akaeneza humo (Ulimwenguni

kwa ajili ya maji hayo) kila aina ya Wanyama, na katika

mabadiliko ya upepo na mawingu yanayoamrishwa

kupita baina ya mbingu na ardhi, Bila ya shaka

(Katika haya) zimo Ishara kwa watu wenye akili

(kuwa yuko Mwenyezi Mungu na ni mmoja).

Na kweli ikiwa tofauti ya pekee kubwa kati ya mtu na Mnyama ni

akili ni wazi kua Mnyama hawezi kua na habari yeyote ya vyombo

vinavyotembea baharini, kinachobadilisha usiku na mchana na kadhalika,

basi mtu ambae hana habari ya hayo yote bila shaka hataachana futi moja

na Mnyama mwenyewe. Hilo ni tusi kubwa ambalo ukimweleza mtu basi

mtapigana sana pengine akwambie: “… ngoja leo ndo utauona huo

unyama wangu…”

Akili imesemwa kua inazidi na kupungua. Kuzidi kwake ni

kutokana na wingi wa majaribio katika mambo mbali mbali ambayo

umeanza kuyajua hivi sasa. Na humo humo Mnyezi Mungu

anakufundisha yeye mwenyewe ambayo hukua unayajua.

Ni ajabu kubwa kwa mwenye akili, lakini kwa asiyekuwa na akili hataona

chochote cha maana ndani yake.

Amma kupungua kwake akili ni zama za kufanza makosa akili

huondoka, na ndo maana ya kauli yake Bw. Mtume SAW kua:-

“Hawi muumini anaiba, zama zile za kuiba (kwake)

kua ni muumin, au anazini zama zile za kuzini kua ni

muumin, au anauwa zama zile akiuwa kua ni muumin”.

20.
Na wale ambao zama Sheytwani anapowashika hukumbuka basi

saa hiyo hiyo huwa wanaona (Mno) akili ndo huwa macho,

ikamkumbuka na kumtaja Mnyezi Mungu.

Na azingatie mtu juu ya vitu ambavo tunadai tunavijua mno na

kutokana na kuvijua huko na mazoeya tunahisi ati havitupi taabu hata

kidogo: Radio, Tepu, Tv, Magari, Kamera, Taa za Stimu, Kompyuta,

Mobitel, Inter-net na kadhalika: jee viliteremka moja kwa moja toka

Mbinguni kama mvua?.

Hili ni suala tosha kukuwezesha kuichemsha Akili yako ambayo

labda unatumia sehemu yake moja tu ya – kumi na sita (1/16). Daima

usipoichemsha, itabaki hivyo hivyo mpaka kiyama ambapo itaonekana

kua ulipewa Akili lakini hukuitumia!!.

Sifa za mwenye Akili:

Mnyezi Mungu aliyetukuka amejaalia kila kitu kua na swifa zake

kwa makusudio maalumu ili kipate kujulikana kwa wepesi na

kutambuliwa kwa njia iso na shaka hata kidogo. Halikadhalika Akili nayo

imepewa swifa zake maalumu ambazo zinakujulisha wazi kua mwenyewe

ni mtu mwenye Akili.

Hizi ndo swifa za Akili kutokana na mafunzo alofundisha Bw.

Mtume SAW, katika hadithi iliyopokelewa kutokana na Bi. Aisha (R.A)

hakika amesema:-

Akili inayo Swifa kumi (10) kati yake zimegawika ndani ya mafungu

mawili:- Dhwahiri na Batwin.

Dhwahiri Ni zile zilizo wazi wazi kabisa mtu akiziangalia anaziona,

nazo ni :-

1. Swamt: yaani ukimya, Bw. Mtume SAW katika Swifa hii

pia amesema kua: “ Mwenye kuzidisha maneno yake

basi huzidi kuanguka kwake” (Speech is Silver,

Silence is Gold) (Kusema sema ni fedha na

kunyamaa ni dhahabu – kinaong`arisha.)

21.
2. Hilm: Upole.

3. Tawadhu’i : Yaani ule Unyenyekevu ikiwa ni ile hali ya kujitupa

chini na hata kama Mnyezi Mungu amekufanza kuwa

Mfalme mbele za watu kwani hapo hasa ndo pahala

pake. Amesema Bw. Mtume SAW “Mwenye kujiweka

chini, Basi Mnyezi Mungu humrufaisha ( Humnyanyua

humpandisha juu)”.

4. Kuamrisha mema.

5. Kukataza mabaya: Daima hutakia wenzake mambo ya

kheri kila anapokueko baina ya watu.

Al- Habib Sayyid Umar akiwa katika safari za Ulaya kwenye

meli, safari hiyo alijiwa na kijana wa kizungu akawa anamtolea nasaha

na kumueleza juu ya Mnyezi Mungu na kumsomea Al-Hamdu na

Qul-Huwallahu kwa taabu. Al-Habib alimuuliza ni mda gani tangu

amekua Mwislam? akamwambia miezi sita. Lakini aliahidi kwa Mnyezi

Mungu kua akikutana na mtu yoyote atamwelezea juu ya Mola Sub-hana

Wataala, na hali kadhalika katika kukataza Mabaya ambayo watu

huyafanza, uzuri zaidi ni kuwahi kabla ili mtu aweze kujiandaa na

kuyakwepa.

Sifa za batwin:

6. Tafakkur: Yaani hali ya kufikirifikiri hasa katika dalil nyingi

zilizojaa na kutapakaa katika maumbile, kuanzia mbingu

na viliomo juu na ndani yake. Ardhi na viliomo ndani

yake, mfano wa milima, wanyama, majani, maji na

madini mbali mbali. Kwa mtu wa Tafakkur bila shaka

ndani ya Machache hayo angeweza kuandika vitabu vya

Ilimu fani mbali mbali tele na nyingi ni zenye umuhimu

kweli kweli ndani ya maisha ya hapa duniani.

22.
Bwana Mtume SAW amesema:

“kutafakkur katika maumbile ya Mnyezi Mungu

saa moja ni bora kuliko Ibada (ya sunna) ya

mwaka mzima”.

7. Ibra: Katika maajabu mazito ya akili, swifa hii imetiya

fora kwani katika maisha yake huenda mwenye

akili ndogo akamwelewa vibaya na kumtabiri

ambavyo sivyo alivyo – pengine aseme ni

mchawi.

8. Khofu: Kumkhofu, kumuogopa Mnyezi Mungu peke yake. Amma

kwa yule asie mkhofu Mnyezi Mungu. Basi itafaa kumkhofu

zaidi, kwani haachi kutomuogopa Mnyezi Mungu illa moto

mdogo au mwendawazimu peke yao hao. Inatosha kuonyesha

kua mtu anamkhofu Mnyezi

Mungu kwa kutekeleza kwa kadiri ya uwezo wake yale yote

aloamrishwa ayafanze na kuacha yale yote alokatazwa nayo.

Haiwezi kua ni khofu “eti mbona havui nguo

akatembea uchi au kuhujumu watu.” Wazimu upo

aina saba akichunguza lazima atapata ncha

ilonasibiana nae, na anaemjua mwendawazimu

kisha usimkhofu basi ipo hatari ya kua yeye ni zaidi.

9. Kuyaadhimisha madhambi:

Yaani ayaone mazito hata, yawe madogo vipi kwani hawezi

akajua ni dhambi ipi aifanzayo ambayo itamfanza Mola wake

achukie na kumfuta katika waja wake warehemewa. Zingatia

juu ya moto mkubwa ambao mwanzo wake ni cheche ndogo

ndogo kabisa

10 Kudhalilisha nafsi:

23.
Abadan.

Nafsi kila siku inataka makuu na kutambuliwa na wewe

kua inayo haki kwako, ni kama vitimbi vya mtoto mdogo

nyumbani kwao na hasa wanapokuwepo wageni. Na kama

ilivyo maalumu nafsi ukiitukuza ni lazima mwisho wake

itakuliza, kwani daima haikutizamii maslahi kwako

Nafsi ilokusudiwa hapa si ingine bali ile Al ammara.

Mnyezi Mungu ameelezea kua daima ni yenye kuamrisha

maovu tu haibadiliki hata siku

moja. Kwa kifupi mwenye Akili lazima awe na mifano

iliyotajwa kwenye swifa kumi hizo. Na si rahisi kwa

asiekuwa nazo kudai kua na Akili.

Tunamuomba Mnyezi Mungu mjuzi wa kila jambo atufungulie

Tafhuma katika kuielewa na kuitumia vyema Akili jambo ambalo Mola

Sub-hanalaah amelisema kua ni azizi. Kwani hakuna baada Nuru ya

Bwana Mtume SAW, jambo azizi kuliko

A K I L I.

24.
Moyo.

Kwa Kiarabu Moyo ni Qalb; yaani kitu cha kubadilika badilika,

leo hivi kesho vile. Na kutokana na maana hiyo Mapinduzi ni Inqilaab.

Pia ni yenye kukokotezwa kumuomba Mnyezi Mungu mwenye

kuzipindua nyoyo kila siku baina ya vidole vyake viwili – azithibitishe

nyoyo zetu ndani ya Twa`a yake.

Moyo umefananishwa au nasibishwa na Arshi yake Mnyezi

Mungu; kwani mambo yote huanzia hapo. Kadhalika ndani ya Moyo

ndipo panapoanza mambo yetu yote, na mengi tunashangalia sana hivi

leo. Tunayaona ya ajabu, na hiyo peke yake ni Ajabu. Mnyezi Mungu

hajaumba sanaa ya ajabu kuliko Mtu, na papo mtu huyo huyo anaona vitu

vingine alivyovitengeneza yeye mwenyewe kua ni Ajabu. Bwana Mtume

SAW amesema katika hadithi ambayo ni mashuhuri sana kua:-

“Ndani ya mwili lipo pande la nyama Jeusi; likitengemaa

basi hutengemaa mwili mzima, na likifisidika basi

hufisidika mwili wote; (Basi haliwi pande hilo la nyama ila

kua ni Moyo)”

Pia amesema SAW:-

“Hakika amali zote ni zenye kutegemea nia yake mtu; na

nia pahala pake ni moyoni”.

Na Mnyezi Mungu haangalii sura za watu wala watoto wao na

mali zao, lakini Mnyezi Mungu anaangalia nyoyo za watu na matendo

yao. Fikra zote za maana ambazo mtu huzihangaikia, huanza Moyoni.

Mambo yote aliyoyakusanya mtu ni kutokana na Moyo. Mambo mfano

wa Ilimu au Ujuzi wowote kila alichohifadhi, kila chenye kuhitaji

kumbukumbu na kadhalika.

25.
Bwana Mtume SAW amesema:-

“Hufa Mtu Kwa Yale Aloishi Nayo, na

hufufuliwa Mtu Kwa Yale Alokufa nayo”.

Katika hoja hii wametokea walomili upande wa hakika ya

Talqini (ile asomewayo maiti baada kwisha fukiwa) kua haina umuhimu

kwake kwa sababu kama aliishi akiwa anamjua Mnyezi Mungu na Mtume

wake, anaijua Dini aloridhiya Mola wake, Kibla chake, Imamu wake

(yaani muongozo wake kwa maana ya (Qur an) na ndugu zake, basi

hatahitaji kukumbushwa chochote.

Na hali kadhalika ameishi hayajui hayo mpaka amekufa, basi hatoweza

kujifunza chochote kutokana na Talqini. Anayeweza kujifunza ni yule

aliye hai. Kwa upeo wa Taammul za kweli hutakosa kuona jinsi gani

Moyo ulivo muhimu.

Hebu na atizame na kutaammal mtu, ya vijana wadogo tu

waliohifadhi Qur an yenye aya zisizopungua alfu sita mia sita na sitini na

sita (6666) ndani ya nyoyo zao bila kukosea kitu!.

Kwa msaada wa Moyo ndiyo tunajifunza na kuzihifadhi Ilimu na maarifa

kadhaa wa kadhaa; jee hiyo si ajabu ilo kweya mipaka?.

Suala linakuja, “Jee Moyo huo wenye maajabu makubwa kama

hayo, ambao unamwezesha mtu kuyajibu masuala ya Munkar na

Nakiir baada ya kufa – ukitokea kubakizwa Hospitali kwa

uchunguzi wa sababu za kufa kwa marehemu vipi atakabil

masuali ya Malaika hao. Yote aloyahifadhi moyoni mwake ndo

yamebakia kwenye maabara za Hospitali vipi itakua hukmu ya

maiti wake?”

Hapo ndo maulamaa mfano wa kina Imam Ghazzali walipoenda

kite zaidi na zaidi hadi kufikia kuona kua moyo ulokusudiwa hapo ni ule

wa Nuru ambao pengine ndo mtu mwenyewe, na ambao ndani yake

ndo Mnyezi Mungu ameiweka Akili. Sio Moyo ambao wengi wetu ndo

kwa mazowea tunaojua, ukiwa na kazi ya kuendesha damu ukisaidiwa na

mapafu!.

26.
Amma ilaaka kati yake na Moyo uloachwa Hospitalini ni yenye

kujulikana na Mnyezi Mungu peke yake, kwani Moyo wa

Hospitali unaweza ukaoza kwa vile asili yake ni udongo uliodhihiri

kama nyama. Lakini moyo wa Nuru ni wa swifa za juu ambao

umekusudiwa maisha ya milele na si wenye Kufa hata siku moja.

Ajabu kubwa jinsi unavyoshirikiana na Akili na Ubongo katika matenda

kazi zake ndani ya maisha yetu ya kila siku!!.

Mambo kama haya ndo anotakiwa mtu, na hasa vijana

wajishughulishe nayo ili kujiandaa kupokea matukufu toka kwa Mnyezi

Mungu, alotukuka.

Vijana ndo wenye nafasi nzuri ya kukaribishwa chini ya kivuli cha

Mnyezi Mungu siku ambayo hapatakuwepo kivuli illa hicho ikiwa

watapondokea katika kumtii Mnyezi Mungu tu peke yake wakaacha balaa

na ghasia chungu nzima zilizowazingira maishani mwao.

Inshallah baada ya kujua moyo huo wenye asrari zisoidadi,

huenda mambo yetu yakawa na mwelekeo wa mabadiliko mazuri.

Wafaqanal Lahu lima yuhibbu wa yardha.

27.
Makamu za Nafsi.

No

Nafsi Sifa Nyuradi

1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

Al Ammara.

Lawwama.

Mul hama.

Mutmainna.

Radhiyya.

Mardhiyya.

Kamila.

Kupenda kula sana, Ubakhili,

Kuhangaika,

Kua na tamaa, Kuwa na

kiburi (Wall yadh Billah).

Matamanio, Hasada na

Ghafla.

Lalamikalamika, Kujilaumu

laumu, Fikra, Kujizuia

(Qabdh), Ujubi.

Ilmu,Tawaadhui, Tawba.

Subrah,Taamul - kuvumilia

adha.

Ukarimu,Tawakkul, Hikam,

Ibaada, Shukar na Ridhaa.

Zuhdi (Kuipa nyongo dunia),

Ikhlas, War-l, Kuacha

yasomuhusu mtu, Wafaai.

Husnul khuluq – Tabia

njema, Lutf kwa viumbe,

Taqarrab illa Llah – Kuacha

yote yasiokuwa ya

M/Mungu, Tafakkur- Katika

utukufu na ukubwa wake

Mola.

Kuridhika na alokugawia

M/Mungu Sub-hana wataala.

Sifa zote njema zilizotajwa

katika nafsi tano, Ukiacha

nafsi ya kwanza ambayo ni

Ammara.

La ilaha illa

Llah.

Allah.

Huwa.

(Ismuh Dhwamir).

Hayyu.

Ahad

A`ziz

Wadud.

28.
Namna au mambo muhimu katika

zoezi la kuachana na mwili.

Muhadhiri: Al Faqeer Ahmad Sheikh.

Katika suala zima la kujigawa kuna mambo makubwa ya kuzingatia

mawili: Transmission and Receiving.

What we require to consider, in which way did we receive

that message and then we are going to deal with it. If the

transmission was spiritual: then we must act accordingly.

Otherwise the message will be VOID. No spiritual message

shall ever be valid in another way. Look; take this example of

material in which a Human-being was created – SOIL. But we

taking bath every now and then! And yet we are not dissolving -

Why? – Ask your mind.

Katika mambo haya saba ndio msingi wa kuachana na

mwili – Separation:

1. Lazima kudumu na udhu kwa masaa 24.

2. Kuwa na tumbo jepesi – Mtu na aepukane na mambo ya kula

kupita kiasi. Na hapa ni budi kutumia hadithi ya Bwana Mtume

S.A.W pale aliposema: “Sisi hatuna haja ya Twabibu, kwa

sababu hatuli mpaka tusikie njaa. Na pale tukila hatuli

tukashiba”.

29.
Jambo lingine la kuzingatia, ni aina ya chakula. Ni vyema

kuepukana na vyakula vyote vyenye kutia nyege. (Ashki ya

kufanya tendo la ndoa) na ikiwezekana ni bora mtu ajiepushe na

vyakula vinavyotokana na Roho.

3. Tuondoe woga kwa viumbe: Mtu na ajaribu kutoka usiku mpevu

nje ya mji na alale popote bila ya kuogopa kuwa linaweza

kutokea jambo dhidi yake.

4. Mtu na aendelee kumtaja Mnyezi Mungu mara kwa mara. Na

amkimbize Sheytwani Ibilisi kwa kutamka Kalimat Tawheed.

Na pale anapoitamka Kalimat hiyo ni budi itoke ndani ya Roho.

Kwa hakika ya mambo ya Kiroho hupatikana kwa kuyafanya

Kiroho hayo mambo yenyewe.

5. Mtu na aangalie Wakati. Hasa kati ya majira ya saa kumi na saa

kumi na moja za Al fajir. Basi, atakuta kuna Wakati umesimama

hauendi kama nyakati nyingine. Si vingine juu ya hakika ya

jambo hilo, isipokuwa Mnyezi Mungu SWT anadhihiri katika

wingu na Dunia akinadi : Je! Nani mwenye haja zake ili

nimkidhie?, Nani mwenye haja ya kufutiwa Dhambi zake

Nimfutie? Nani mwenye kutaka Pepo yangu Nimpatie?”.

Wengi ya watu wanakuwa wamelala katika wakati huo. Basi

kama wewe umefanikiwa juu ya jambo hilo ukawa hadhiri, basi

nyanyuka na utarakai – Rakaa mbili za wakati huo ni bora

kuliko Dunia na vilivyomo.

6. Jitahidi kujiweka katika hali ya kati ya kuwa macho na kua

katika Usingizi. Na ni katika hali hiyo ambapo unaweza

kufungukiwa na mambo mengi – kwani ukifanikiwa jambo hilo

utakuwa ukimiliki Coscious Mind na Sub–Conscious Mind. Na

moja kati ya mambo yaliyo muhimu kabisa katika ku-develop ili

uweze kujigawa.

7. Shart lingine kubwa kabisa ni kumwogopa Mnyezi Mungu

Kikweli kweli. Ndipo ambapo yeye Mnyezi Mungu atakiogopesha

kila kiumbe dhidi yako. Na ndio maana ikapendelewa mtu afanye

Haluwa zake nje ya mji.

30.
Mahali ambapo ataweza kuziepuka sauti za watu. Jambo hili

litampelekea mtu kuweza kuidhibiti barabara Nafsi yake. Na ile

akili yenye nguvu Sub Conscious Mind inaingia kazini katika

zile sehemu za hatari hatari. Hivyo ili kuizowesha kutumika akili

hiyo budi kutingishwa tingishwa. Wengi katika watu hutumia

kiasi cha 1/16. cha akili alopewa na ndio maana Bwana Mtume

SAW akasema: “Watu wamelala”. Kwani sehemu kubwa ya

akili zetu hatuzitumii. Hivyo na ajitahidi kila mmoja wetu

kujipandisha Daraja kwa kuyafanzia kazi yale anayojua, ili angaa

tuweze kutumia japo 3/16. ya akili zetu. Na papo ukifikia kutumia

kiasi hicho, wengi katika watu watakupanga wewe katika kundi la

wenda wazimu. Ama watakuona umechanganyikiwa (Ndio maana

unasema au unatenda yasiyowezekana). Kwa kuwa maono yako

yatakuwa mbali na maono ya watu wengine, na ni kweli utakuwa

ukiviona vitu kwa asili yake, siyo kwa mfano ambao wengi wetu

tumezoea kuona. Utakuwa unaishi katika ulimwengu wa Hakika

na muda mrefu utakuwa katika jitihada za kumridhisha Mnyezi

Mungu, na hapo ndipo penye kufuzu.

“Hakika yetu sisi Hatukuwaumba Majini na Watu ila

kwa kuniabudu Mimi. (Kunitambua mimi)”.

31.
Mtungaji:

(Al marhum)

AL- FAQEER AL - HABIB AHMAD SHEIKH

32.
Vitabu vilivyokwishatoka ni:

*1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st , 2nd & 3rd addition).

*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako.

*3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu.

*4. Knowledge vision & ecstacy.

*5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu (i) .

*6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m.

*7. Kuhifadhi Burda.

*8. Maana halisi ya Imaan (ii).

*9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb.

*10. Siri ya Balaa.

*11. El makhlouq (Viumbe)

*12. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu. (2nd addition)

*13. Manaqib ya Al habbib Sayyeid Al Ma`aruf.

*14. Some aspects of concepts of facility in medevial Islamic

Philosophy by Mwinyibaraka.

*15. Njia nyepesi ya kuijua Nafsi yako. (2nd addition).

Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu

(Insha Allah) ni:

*1. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2nd addition)

*2. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu (ii).

*3. Muhammad SAW katika ulimwengu wa Ghayb.

Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:

Majaalis El Ulaa - El Qadiriyya Sinza,

33.

P.o. Box 15170,

Tel: 0747 483553

Tel: 0748 595958.

Tel: 0744 023703.

Tel: 0741 235091.

Tel: 0744 299597.

Dar es salaam.
Al habib Al Faqeer Ahmed Sheikh Mohamed Sheikh Msiha, amezaliwa

Singida mkoa wa Dodoma, mwaka 1938. Amepata elimu ya sekula Unguja na

amebahatika kupata elimu ya juu katika chuo maarufu Afrika ya Mashariki

Makerere Uganda.

Elimu yake ya Dini ameipata hapo hapo Unguja toka kwa Masheikh mbali mbali,

baadhi yao ni:

Sheikh Sleiman Alwi (Muhib Rasul) (Al Marhum).

Sheikh Seyyid Mansab.

Maalim Himid (Al marhum).

Maalim Hemed Muhamed El Buhry.

Sheikh Seyyid Qamus.

Sheikh Muawwiya Ibn Abdul Rahman.

Sheikh Ally Muhamed Comorian.

Sheikh Ibrahim Mzee Ahd.

Sheikh Haj Mzee Ahmad Msiha.

Amma Elimu ya Nafsi na Roho Amepata Ijaza yake toka kwa A`limu mkubwa

Duniani Al Habib Sayyid Omar Bin Abdallah (Mwinyi Baraka).

Sheikh Ahmad amewahi kufanya kazi katika jeshi la Polisi Tanzania Bara

katika mikoa mbali mbali mpaka alipostahafu.

Katika umri wake wote Sheikh Ahmad alijahid katika kuendeleza Uislamu

kwa kusomesha na kuandika vitabu vya mada na maudhui mbali mbali katika

Uislamu. Pia alianzisha Majaalis Sehemu mbali ambazo ziko mpaka leo, Mtaa wa

Pemba, Sinza, Bungoni, kijito nyama, Sadani (Ilala) na Kibaha (Misugusugu)

ambapo ndipo ilipo Dhwarihi yake (alipozikwa).

Sheikh Ahmad ametwawafu 27. 8. 2001. ( Mwezi 7 jumadda thany 1421

H.R.). Akiwa na umri wa miaka 63, vile vile alivyokuwa akiomba aishi umri ule

ule alioshi kipenzi chake Bwana Mtume Muhammad SAW.

Insha Allah Mnyezi Mungu amjaze kheri na alitie Nuru kaburi lake (Amin).

Khalifa: Sheikh Issa Othman,

Majaalis El Ulaa El Qadiriyya, Sinza Dar es Salam.