You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
Moyo.

Kwa Kiarabu Moyo ni Qalb; yaani kitu cha kubadilika badilika,

leo hivi kesho vile. Na kutokana na maana hiyo Mapinduzi ni Inqilaab.

Pia ni yenye kukokotezwa kumuomba Mnyezi Mungu mwenye

kuzipindua nyoyo kila siku baina ya vidole vyake viwili – azithibitishe

nyoyo zetu ndani ya Twa`a yake.

Moyo umefananishwa au nasibishwa na Arshi yake Mnyezi

Mungu; kwani mambo yote huanzia hapo. Kadhalika ndani ya Moyo

ndipo panapoanza mambo yetu yote, na mengi tunashangalia sana hivi

leo. Tunayaona ya ajabu, na hiyo peke yake ni Ajabu. Mnyezi Mungu

hajaumba sanaa ya ajabu kuliko Mtu, na papo mtu huyo huyo anaona vitu

vingine alivyovitengeneza yeye mwenyewe kua ni Ajabu. Bwana Mtume

SAW amesema katika hadithi ambayo ni mashuhuri sana kua:-

“Ndani ya mwili lipo pande la nyama Jeusi; likitengemaa

basi hutengemaa mwili mzima, na likifisidika basi

hufisidika mwili wote; (Basi haliwi pande hilo la nyama ila

kua ni Moyo)”

Pia amesema SAW:-

“Hakika amali zote ni zenye kutegemea nia yake mtu; na

nia pahala pake ni moyoni”.

Na Mnyezi Mungu haangalii sura za watu wala watoto wao na

mali zao, lakini Mnyezi Mungu anaangalia nyoyo za watu na matendo

yao. Fikra zote za maana ambazo mtu huzihangaikia, huanza Moyoni.

Mambo yote aliyoyakusanya mtu ni kutokana na Moyo. Mambo mfano

wa Ilimu au Ujuzi wowote kila alichohifadhi, kila chenye kuhitaji

kumbukumbu na kadhalika.

25.