12.07.2015 Views

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

Read - Al-Faqeer

SHOW MORE
SHOW LESS
• No tags were found...

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

YAAl Faqeer,Ahmad Sheikh,Majaalis El-Ulaa,Dar es salaam Tanzania,Muharram -21-1421- ( 26 April,2000).

YALIYOMO:No.Uk.1. Yaliyomo…………………………………………i.2. Utangulizi………………………………………...ii.3. Dibaji……………………………………………..vi.4. Uongofu…………………………….......................1.5. Jibu la kwanza………………………………….....1.5. Jibu la pili……………………………………........11.6. Maneno ya hikma……………………………… 18.

بسم هللا الر حمن الر حيمUTANGULIZI:Bismillah wal khayru wash sharru Bimashiyatillah.Allahumma swalli ala habibika sayyidna Muhammadkhaatamul Anbiyaail-lah waalihi wa swahibihi wa sallam.Wa baad, liliulizwa swali ambalo jibu lakelilisababisha kupekua zaidi hakika yake, na kufikiauzinduzi wa kijitabu hiki kipetopeto ili wale ambaohawakuwepo zama za kutupa mas-ala haya nao piawaelimike na kufaidika nalo kama kweli ndani yake zipofaida. Kwa kadiri ya ujuzi alotupa Mnyezi Mungutumejaribu kulijibu kwa kuchegemeza hoja zote kwa njiaya kurejea ndani ya Qur-an kitabu cha Mnyezi Munguambacho ndani yake zipo hakaik kuhusu yote yahitajiwayondani ya mapito ya uhai wa kila siku hapa dunianina pia mraa-ja-a katika hadithi za Bwana MtumeS.A.W. kwani tumeamriwa kufanza hivyo kila tunapokosakuafikiana au kukubaliana katika jambo lolote lile. MnyeziMungu ametuambia kua amedhibiti kila kitu ndani ya kitabuchake hicho yaani Qur-an, kwa hiyo upo umuhimu mkubwakatika kutuwezesha kutatua mambo yetu.Halkadhalika hadithi kwani Bw. Mtume ndiyealokabidhiwa shughuli za kubainisha Qur an kwa watu. Nando maana Mnyezi Mungu anatuamrisha kumtwii MtumeSAW na kupokea lolote analotuamrisha au analotukatazanalo. Ipo hatari ya kuvukwa na Uislam pindi tukiyapingahayo. Anaemtii Mtume basi, ndo amemtii Mnyezi Mungu.Sababu si za kuelezwa bali akili yake mtu inamtoshakumfunulia hakika ya jawabu.Qur an 4:59.ii

"Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Munguna mtiini Mtume na wenye mamlaka juuyenu, walio katika nyie (Waislamuwenzenu). Na kama mkikhitilafianajuu jambo lolote basi lirudisheni kwaMwenyezi Mungu na Mtume, ikiwaMnamwamini Mwenyezi Mungu na sikuYa mwisho. Hiyo ndiyo kheri, nayo inaMatokeo bora kabisa".Kwa hiyo tunaomba Tawfiq kwa Mnyezi Mungu naMtume S.A.W. ili tuwezeshwe kuandama haki nakuongozwa katika kuitetea Dini yake ilonyooka.Twabaani vikwazo vitakuwepo lakini kila tukiangalianyuma tunaona kua Maswahaba walikutwa na misukokoskomizito kuliko sisi. Wengi ya watu hutaka wasiguswe kwasababu wamesilimu na wanaswali. Jee vyeo na darajahawataki? Na ni nani ambae angemudu kutangua katiba yaMnyezi Mungu alieumba mauti na uhai ili atupe balaa iliaweze kujulikana kama ni nani atakua na matendo mema?Qur an 67:2.”Ambaye ameumba mauti na uhaiKukujaribuni (kukufanyieni mtihani):Ni nani miungoni mwenu mwenyevitendo vizuri zaidi. Naye ni mwenyenguvu (na) mwenye msamaha”.Hii ni njia moja ya kukumbushana kama tumetokeakusahau. Kutokana na udhaifu wa binadamu hatuwezikujigamba kuwa yote tuliyo yaandika ndo yametimia walahaihitaji mkono wa mtu mwingine, laaiii

Tunawaomba ambao watakuta makosa au upungufu wowotewasiache kuturekebisha kwa sababu moja tu, Al-kamaalLillahi Wahdahu; na sisi ni wenye Takwsiri nyingi.Suala lilikua juu ya: Uongofu ni wa Mnyezi Munguau kiumbe? Bila shaka ni suala kubwa, la maana kabisa nalenye kumhusu kila mwenye akili, na alie mnyenyekevu kwaMola wake kikweli. Nina shauku nzito kutaka kuwashukuruwalowazia na kutaka darsa kama hizi tuzianzishe pale Ilalamtaa wa sadani, miongoni mwa kina Akh Fuad, SharifKarama na wote wahudhuriao Darsa hizo kila jumatano.Juhudi zao katika kuchapisha nuskha hizi ni yenyekushukuriwa ghaya. Mnyezi Mungu atawajazia na kuwapakila walitakalo katika ya kheri hapa Duniani ndani ya maishana kwa kesho yawmul Qiyama Insha Allah hawatakuwakama ambao wataomlilia Mnyezi Mungu wakisema :-Qur an 20:125.“Yaa Rabi kwa nini (vipi tena) umenifufuakipofu hali nilikuwa na macho yangu?”.Waambiwe:- Qur an 20:126.“(Mungu) Atasema: “Ndiyo vivyo hivyo.Zilikuja Aya zetu ukazizahau, (ukazipuuza)na kadhalika leo utasahauliwa (utapuuzwa)”.Mnyezi Mungu anapenda kuombwa na anachukiaasipoombwa, Kwa hiyo, napitia tena kwa Bwana Mtumekumtaka rukhsa au yeye mwenyewe SAW achukue nafasi yakutuombea kwa jina lake A-lim na A-leem atufungue akilina kutuelimisha kwa njia ambayo tutamudu kua Wajaahid nawahitaji watu katika Dini yake-Islam.iv

Waswalla Llahu wasallam alaa habiibihil aadhwamSeyyidna Muhammad waalihi wal hamdu lillahi Rabbilaalameen.Al Faqeer Ahmad Sheikh,Rajabu 28 – 1415,December 31, 1994,Majaalis El Ulaa,El Qadiriyya.Dar es salaam.v

DIBAJI.Tunamshukuru Mwenyeenzi Mungu kwa neema zakealizotuneemesha. Nazo ni nyingi sana kama alivyosema Subhanahu wa Taala katika Kurani Takatifu Surat Ibrahimkuwa:Qur an 14:34."Na Akakupeni kila mlichomuomba na (msichomuomba). Na Mkizihesabu neema za MwenyeenziMungu hamzidhibiti, hakika mtu ni mwenyekujidhulumu sana na kafiri sana”.Na akatiya mkazo wa hayo wakati aliposema katika SuratulAl Nahl:Qur an 16 :18“Na mkizihesabu neema za MwenyeeziMungu hamzidhibiti, hakika MwenyeenziMungu ni msamehevu sana na mrehemevu”.Katika neema zote alizotuneemesha Mola wetu hakunaneema kubwa nzuri na muhimu kama neema ya uongofu waImaan na Uislamu.Ni neema inayohusika na vitendo vilivyo vema hapaduniani na kulipwa na Mwenyeenzi Mungu siku ya malipokama ni matokeo ya vitendo vyema malipo mema zaidi.Amesema Mwenyeezi Mungu katika Kurani takatifu SuratIsrah.Qur an 17:15.vi

DIBAJI :"Anayeongoka basi anaongoka kwa nafsiyake mwenyewe na anayepotoka anapotokakwa hasara ya nafsi yake mwenyewe, walahatabeba mbebaji mzigo wa mwingine. Nasisi (Mwenyeezi Mungu) si wenye kuwaadhibu(viumbe) mpaka tuwapelekee mitume".Kwa hivyo basi Mwenyeenzi Mungu amejiona kuwaamewajibika kuwatuma Mitume na Manabii tofauti kwalengo la kumuamini, kumuabudu na kuwaongoza kwaMwenyeenzi Mungu aliyewaumba na atawarejesha tenakwake, na kuwalipa kila mmoja kwa aliyoyatenda. NaManabii na Mitume yote watakuwa mashahidi waMwenyeenzi Mungu kwa umma wao kwa kufikisha ujumbewake kwao. Amesema Mwenyeenzi Mungu katika Surat AlNisai. Qur an: 4:41."Basi itakuwaje tutakapoleta shahidikutoka kilau umma na tutakuleta wewe(Muhammad) uwe shahidi juu ya huuumma wako".Uwongofu unatoka kwa Mwenyeenzi Mungu peke yake.Yeye ndiye anayeongoza, Manabii na Mitume ni wafikishajitu wa uwongofu huo. Sheikh Ahmad Sheikh amenukulukatika kitabu chake hiki ukurasa wa pili maneno yaMwenyeenzi Mungu katika Kurani Takatifu akimuambiyaMtume Muhammad SAW kuwa: Qur an 28:56vii

DIBAJI:"kwa hakika wewe huwezi kumuongoaumpendaye, lakini Mwenyezi Munguhumuongoa amtakaye, naye anawajuawaongokao".Na yeye Bwana Mtume Muhammad SAW katika hotubayake aliyeitowa katika Hija ya kuaga na iliyoitwa "Hotubaya kuaga" Imeitwa hotuba ya kuaga kwa sababu aliwaagaMaswahaba wake aliokuwa nao hapo kuwa karibuni ataiyagadunia. Na alikuwa mara kwa mara akitamka kuwa: "EweMola mimi nimefikisha basi shuhudia"Mwenyeenzi Mungu anawataka Waislamu woteulimwenguni kwa kuwa ameshawaongoza katika Dini yahaki na ya kweli, wazidi kumuomba duwa ya kuzidikuwaongoza kwa kun`gan`gania na kushikilia Dini hiyo nakufa nayo na kufufuliwa na kuhesabiwa na Dini hiyo.Wakati kila aliye Muislamu anapomuabudu MwenyeenziMungu katika ibada ya Swala na anaanza kwa kumsifia sifaanazostahiki, na halafu anamuomba kwa kusoma:Qur an 1:5-6."Tuongoze njia iliyonyooka, njia yawale ambao umewaneemesha juu yaousiyowaghadhibikia wala wasiyopotoka"Anayasoma hayo katika Surat (Al Faatiha) kila siku maratano, katika Swala za fardhi na mara nyinginezo katikaSwala za Sunna.Mwenyeenzi Mungu utuzidishiye uwongofu wa Diniviii

DIBAJIya Islam na utuwafikiye katika kutenda yaliyo mema nautukubaliye nayo na utulipe malipo mema kesho akhera. Naumkubalie mtungaji wa kitabu hiki Sheikh Ahmad Sheikh naujaalie utungo wake huu kwa ajili yako tu, ili umlipeanayostahiki kulipwa mwenye kufanya kwa ajili yako.Ahmad Haydar MwinyimvuaDar es salaam.ix

UONGOFU:Mnyezi Mungu akiwa kwa mapenzi yake ndoalowaumba wana Adam, kwa nini tena aje kuwatia motoni,huu uongofu si wenye kutoka kwake bali ni kwa mtumwenyewe?Suala hilo lilifikia karibu na kufanana na lilelililoulizwa katika Interview muhimu fulani lilosharitiwakua ndio au hapana. (yaani jibu liwe ndiyo au hapana). EtiMnyezi Mungu anaweza kuumba jiwe moja mfano wa hiidunia?. Je anaweza kuumba jiwe kama hilo halafu ashindwekulibeba?. Hili ni suali tatanishi na ni lenye mtego ndaniyake, kiasi cha kuonyesha kwamba kwa pande zote zamajibu mja anakua ameshaingia ndani ya kufru bila kujijuakama ni mwenye akili ndogo. Majibu ya suali hilo yalikuamawili :Jibu la Kwanza:Mnyezi mungu anamsamehe amtakae, naanamuadhibu amtakae. Mnyezi Mungu anapomtakia mjawake kheri; basi humuongoza katika dini; kwa nini? Kwasababu yeye humuongoza amtakae katika njia iliyonyookanayo ni dini (Islam).Pengine Mnyezi Mungu humuacha kupoteayule amtakae. Minighayr kujulikanwa na mwinginepalikuwepo mkataba gani katika siku za ahadi na mithaki(za genetic life) Uhai kabla ya kuvaa mwili waudongo huu wa kidunia) baina yake Mnyezi Mungu nayule mja.Katika hakika kama hizo hizo aliambiwa Bw. Mtume (SAW)Kuwa: Qur an 61:5.“Na wakumbushe (Nabii) Musa alipowaambiawatu wake: “Enyi watu wangu! Mbonamnaniudhi, hali mnajua kuwa mimi ni1

Mtume wa Mwenyezi Mungu (niliyeletwa)kwenu? Basi walipoendelea na uovu wao,Mwenyezi Mungu aliziachilia nyoyo zaozipotoke (kama walivyopotoka wenyewe);na Mwenyezi Mungu hawaongoi watuwaovu (wenye Kutoka katika ta`a yake)”.Vile vile katika:Qur an: Qasas 28:56."Kwa hakika wewe huwezi kumuongoaumpendae, lakini Mwenyezi Munguhumuongoa amtakae nayeanawajua waongokao. (Kwa hiyoanawaongoa na anawajua wasiotakakuongoka kwa hiyo anawaachiliambali) Mwenyezi Mungu ndie ajuayeni nani anaeongoka."Na yule ambaye Mnyezi Mungu amemuacha apoteehatoweza kupata wa kumuongoa, mtu ataachwaakitangatanga ovyo tu. Katika hadithi ya Bwana MtumeSAW iloelezwa na Swahaba mashuhuri kabisa (Bw)Abdallah Ibn Mas-ud R.A. katika kuumbikamwanadamu ndani ya tumbo la mama yake kuanzia tone lamanii mpaka kupuliziwa roho; Hakika hii inajitokeza kamahivi mwishoni mwake:“…Naapa kwa yule ambae roho yangu (Nafsiyangu) iko mikononi mwake, hakika mmojawenu ataishi akifanza amali za watu wa peponi,hata haitabaki kati yake na hiyo pepo Illadhiraa moja tu – kitamtangulia kitabu(kilichoandikwa siku ile ya kupulizwa roho)2

atafanza amali za watu wa motoni aingie (huomoto). Na hakika mmoja wenu ataishi akifanzaamali za watu wa motoni hata haitabaki bainayake na huo moto Ila dhiraa moja tu,kitamtangulia kitabu; atafanza amaliza watu wa peponi aingie”.Yote yaliyotajwa mwenye hadithi hiyo hakuna hatamtu mmoja ambaye anaweza kuyajua kabla ya mja muhusikana muhusishwa kwayo, bali yeye tu Mnyezi Mungu pekeyake. Wale wenye kupata vizuri kisa cha mwana chuonimkubwa wa Kiyahudi zama za Sydna Musa A.S. akiitwaBal – a’m watapata vizuri hakika ya uongofu na husunulkha-tima„Mwisho mwema‟ ni vipi kusudio lake.Yasemekana kua wanafunzi wake alfu moja walikuawanaruka angani husemei ndege, walakini mwisho wakealifia juu ya mti wa adhabu akiwa amemsujudia Ibilisi –Alayahi laanatul – Llah. Husunul kha-tima ndo jambo lakuzingatia mno katika suala zima la Uongofu. Baadhi yaaya zenye kushadidia suala la uongofu kutoka kwa MnyeziMungu.Qur an 10:25“Na Mnyezi Mungu anaweta (viumbe vyakewende) katika (hiyo) Nyumba ya amani nahumuongoa amtakaye njia iliyonyooka(maadam anakubali Uongofu)”Darisalaam ilokusudiwa hapa sio jiji kuu la nchini Tanzania.Bali ni moja ya pepo zake Mnyezi Mungu ambayo ndaniyake muna amani isiyotarajiwa kubadilika hata siku mojakatika Aya 93 ya suratul Nahal tunasoma.Qur an 16:93.3

“Na Mwenyezi Mungu angalitaka kwa yakiniangelikufanyeni kundi moja tu (mnamtii nyotekama alivyowafanya malaika lakini kakufanyenimfanye mtakavyo) lakini anamuacha kupoteaanayemtaka na anamuongoa anayemtaka kwahakika mtaulizwa kwa yale mliyokuamkiyafanya (kwani mmepewa ujuzi wa kujuajema na baya)”Vile vile Mnyezi Mungu anasema mwisho mwa aya ya 17 yasuratul-Kahf : Qur an 18:17.“….Ambaye Mweyezi Mungu anamuongoza basiyeye ndiye anayeongoka; na anayemwachakupotea, basi hutampatia mlinzi mwongozi”.Hakika ya wazi wazi dhwahiri sha-hir ni hiyo lakiniba-tween ya mambo hakuna aijuae illa yeye Sub-hana waTaala. Katika aya ya 8 ya sura 35 Fa-Tweer Mnyezi Munguanatwambia:- Qur an 35:8."Je! aliyepambiwa a`mali zake mbaya naakaziona njema (mtamwambia nini mpakaasikie?). Bila shaka Mwenyezi Munguhumwacha kupotea amtakae (kwa kua4.

hataki mwenyewe kuongoka); na humuongoza amtakae, basi roho yako isitoke kwamajonzi juu yao; kwa yakini Mwenyezi Munguanayajua (yote) mnayoyafanya.Na tutizame yaliyomo ndani ya aya 22 ya Sura ya 39 Zumarambayo hatukosi kuona ukweli ya kua uongofu kwa sehemukubwa uko mikononi mwa Mnyezi mungu:Qur an 39:22.“Je! Mtu ambaye Mwenyezi Munguamemfungulia (amemfungua) kifuachake kuukubali uislam, akawa yukokatika nuru itokayo kwa Mola wake (nisawa na mwenye moyo mgumu)? Basiadhabu kali itawathibitikia wale wenyenyoyo ngumu wasimkumbuke MwenyeziMungu. Hao wamo katika upotofu(upotevu) ulio Dhwahir.Mapatano kati ya mja na Mnyezi Mungu mpaka ajekumfunga kifua chake kusikubali Uislamu ni khabari zenyekujulikanwa na yeye tu Sub-hana wa Taala, na hawezimwingine, kilicho muhimu ni kudumisha unyenyekevu kilasiku pamoja na kumuomba Mnyezi Mungu atubakishe ndaniya Uislam mpaka siku ya kuitoka dunia iwe tumo ndaniyake, Mfano wa Seyyidna Ibrahimu ASW kwa wanawe naSeyyidna Yaaqubu AS katika kuwanasihi watoto wao:Kwanza:-.Qur an 2:132.5

“…Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia Dini,basi msife illa (Ilhalan) ni waislamu”.Pia katika Aya hii:- Qur an 3:102.“Enyi mlioamini Mcheni MwenyeziMungu kama ipasavyo kumcha; walaMsife isipokuwa mmekwisha kuwaWaislamu kamili.”. Mnyezi Mungu anapopitisha hukumu hiyo huahamuhusishi mtu yoyote tu akajua kua fulani nafulani kamuongoa na kampotoa. Na mwenyekuongolewa na Mnyezi Mungu hakuna awezaekumpotoa kama mwenye aya ya 37 ya sura hiyoya Zumar:Qur an 39:36-37."Je, Mwenyezi Mungu hamkifii (hamtoshei),mja wake? Na wanakuogofisha(wanakukhofisha kwa wale walio kinyumechake, (masanamu; kuwa watakudhuru kamahutawaabudu. Wanaweza wapi kukudhuru,licha kukunufaisha). Na aliyehukumiwa na6

Mwenyezi Mungu kupotea, basi hana wakumuongoa Na ambaye Mnyezi Munguanamuongoa hakuna wa kumpoteza. Je!Mwenyezi Mungu si mwenye nguvu anayewezakulipa kisasi”.Kwa hakika hiyo ni yenye kuonyesha Dhwahir shaahirya kua Uongofu wa kweli ni wa Mnyezi Mungu:"Inna Hudallahi Huwal Huda"Na sio rahisi mtu kumtibua. Si siku nyingi zilizopitaWaislamu wa China walichomewa Misahafu yao na Vitabukadhaa vya dini na Misahafu mingine na mingine iliwezakuandikwa kwa urahisi kabisa, sababu Qur an ilikua vifuanimwa watu. Dhanna yao kua kwa kuichoma Misahafu yaWaislamu wa kichina ndio wangefaulu vizuri sana katikakuupotosha Uislamu na waumini wake, ilipiga chini nakufedheheka. Amma kwa upande wa Ammi yake BwMtume SAW - Abu-Lahb Ibn Abdul Mutwalib yapo mengiya kuzingatia juu yake, yeye Abu-Lahb alipinga sura kadhawa kadhaa, lakini tangu ilipoteremshwa Suratul “Lahb”yaani: “Tabbat-Yadaa” Sura ya 111 hakuweza kufunuamdomo wake kabisa. Na ajabu zaidi ni kwamba aliishi kwamuda wa miaka kumi ndio akafa bila kusilimu hata kiuongotu, ili ipatikane ufifilishi na kutangua kauli ya MnyeziMungu ilokwisha hukumiwa juu yake. Tizama vipi MnyeziMungu anaelezea katika hakika ilomo mwenye:Qur an 40:33“….Siku mtakapogeuka nyuma (mkimbie nahamna pa kwenda) hamtakua na mlinzi kwaMwenyezi Mungu, na mwenye kuhukumiwa na7

Mwenyezi Mungu kupotea, basihuyo hana mwongozi yoyote”.Kadhalika kauli yake ifuatayo mwenye:Qur an 42:46.“…wala hawatakua na marafiki wa kuwasaidiambele ya Mwenyezi Mungu. Na ambayeMwenyezi Mungu anamwacha kupotea hananjia yeyote (ya kutengemea)”Swadaqallah - Mnyezi Mungu amesema kweli, ammasivyo ikiwa kwamba Uongofu hauko Mikononi mwake, Abu– Lahb angeweza kujirekebisha ndani ya miaka kumi aloishibaada ya kusikia Suratul Lahb, yaani: “Tabaat YadaaAbi Lahabin Watabb”.Mnyezi Mungu haangalii sura ya mtu wala mali nawana bali moyo wake mja na matendo yake.Anapopitisha hukumu yake juu ya mja hua ni yenyeuadilifu, lakini hakuna wa kumuingilia kwa lolote lile.Tizama jinsi gani anapofikia mtu kuhukumika katikamatendo yake pindi aliposema:Qur an 45:23“Je umemuona yule aliyefanya yale anayoyatakeyeye kuwa ndie Mungu wake, na Mwenyezi Munguakamuacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi naakapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake8

na kumtia kitanga machoni pake;basi nani atamuongoza baada yaMwenyezi Mungu? Je; hakumbuki?”.Pengine tunaambiwa hivi ifuatavyo :Qur an 6:39.“Na wale waliokadhibisha hoja zetu ni viziwina mabubu na wamo gizani. AmtakayeMwenyezi Mungu humwachia kupotea; naamtakaye humweka katika njia iliyonyooka “.Mfano wa aya 6:39 kama hizo umejaa ndani ya Qur an.Masikio, Macho, Moyo ni sehemu ya Akili kwa hiyo MnyeziMungu anapokwishapiga muhuri ndani ya Akili ya mjahakuna wa kufuta, hiyo ni hakika tosha lakini siyakuwezekana kushuhudika kwa macho ya mtu. Na ajabu nikwamba hata anayehusika haiwi rahisi kwake kujijua kuwaameishapigwa muhuri na kwamba baas, hana chakuongokewa tena katika maisha yake. Hizo sio hakaik zotemwenye Quran ambazo zinashuhudia kwamba MnyeziMungu anamwokoa amtakae bali alal akalli ni toshakukumbusha mtu katika kukokoteza mazingatio na imaniyake anapokua mtu Mwislam na anatekeleza yatakiwayo,basi si kwa ujanja wake au nguvu zake lakini ni kwakutakiwa na Mnyezi Mungu kheri kama hio, kwa hiyoazidishe mtu ule unyenyekevu na kuzidi kuomba kila sikumtu abakishiwe kheri hiyo mpaka mwisho wa uhai wake.Wapo ambao wanaowahusu katika jamaa zaowanawaendea mbio huku na kule ili waache yaleyaliyowavaa angalau waingie msikitini siku moja tu lakiniwaapi! Wanashindwa, pamoja na kutakiwa na kutaka kwaokujitoa katika machafu yao (mambo maovu walokwishayazoea na kubobea ndani yake). Kwa nini basi, sababu nikwamba Mnyezi Mungu muumba wa viumbe wote amejaalia9

wengine kua makafiri na wengine kua muumin. Mapatanokati ya wote hao na Mnyezi Mungu hamna wa kujua.Qur an 64:2.“…Yeye ndiye aliye kuumbeni (nyote) nakuna wengine wenu ni makafirina wengine wenu ni waislamu, Munguanayaona (yote) mnayoyafanya".Makusudio yaliyomo ndani ya aya hiyo si yenyekuhitaji sherehe ili kuelewa bara-bara hakuna wa kukatarufaa dhidi ya uamuzi wa Mola, na hasa ukizingatia jinsimambo yenyewe yanavyojieleza na kujisherehesha wenyewewazi wazi na kinagaubaga ilobaki ni kuomba kwa MnyeziMungu atupe Taufiki tudumishwe ndani ya Uislam kunaliHusunulkha-tima Bijahi Rasuli Llah Swallal – Lahu AlayhiWasalaam.10

Jibu la pili:Amma katika upande wa pili wa jawabu katikasuala la uongofu, ni kama lifuatavyo katika kuanza kwake nakawli ya Mnyezi Mungu:-Qur an 10:108.“Sema: “Enyi watu!Haki imekwisha kujieni kutoka kwa MolaWenu basi anaeongoka anaongoka kwa(faida) Nafsi yake,na anaepotea kwa(khasara ya) Nafsi yake, (mwenyewe) na mimisi mlinzi juu yenu (mimi ni mtoaji khabari tu)”Mnyezi Mungu hamtii mtu motoni bali mtu ndomwenyewe anajitia motoni. Sababu ni kwamba MnyeziMungu anataka kila kiumbe na hasa Bin Adam na Majiniwamwabudu yeye tu ili aje awalipe pepo. Na akatoa chombomadhubuti cha kufahamia haki na batil, nayo ni akili, kwahiyo baada ya kuleta mitume kuja kukukmbusha nakufahamisha zaidi na zaidi nini anachotaka.Ametarajiwa mtu kua ataongoka akitumia Akili yake,kwa hiyo anaeongoka kwa faida yake mwenyewe, naanaepotea basi ni kwa hasara yake mwenyewe. Na MnyeziMungu si mwenye kudhulumu waja wake:"Hakua mola wako mwenye kudhulumu waja".Pamoja na kua Mnyezi Mungu humwongoa amtakae nahumwacha kupotea amtakae, lakini ameacha nafasi kubwakwa mja mwenyewe aonyeshe kua anataka kuongolewa auhataki. Nafasi hiyo imo kwenye Akili yake mtu, kwa hiyo:Qur an 17 : 15.11

“Anaeongoka basi anaongoka kwa maslahiya nafsi yake mwenyewe, na anaepoteabasi ni kwa khasara (ya nafsi) yake walahatabeba mbebaji mzigo wa mwingine nasisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe)mpaka tuwapelekee Mitume (awafahamisheyaliyo ya haki. Basi wakiyakataa ndipowanapoangamizwa)”.Katika Surat Ja thiya 45:15 Mnyezi Mungu anayohaya ya kusema:-Qur an 45 : 15.“Mwenye kutenda mema basi ni kwaajili ya nafsi yake (mwenyewe) namwenye kufanya uovu ni juu yake(mwenyewe pia) kisha mtarudishwakwa mola wenu".Ndo kusema kila jema analofanya mtu ataliona nakila ovu atalofanya mtu ataliona. Khabari hizo hakika yakeinashuhudiwa na aya zenye kumalizia Surat zilzala 99: 7na 8. Mnyezi Mungu anatuhadharisha kwa kusema:-Qur an 99: 7-8."Basi anayefanya wema (hata) wa kiasi chauzito wa mdudu chungu ataona jazaa yake12

Na anayefanya uovu (hata) wa kiasi chamdudu chungu ataona jazaa yake"Qur an: 2 : 281.“Na iogopeni siku ambayo mtarudishwakwa Mwenyezi Mungu kisha viumbe wotewatalipwa kwa ukamilifu yote waliyoyachuma,nao hawatadhulumiwa”.Atasema nini mtu wakati mambo yote aliyoyafanyakwa Akili yake yamedhibitiwa vizuri na kwa uadilifu kabisa.Na hoja zake mtu zitazidi maana yake mtu atakua mbishikatika kuania kujitetea basi atazibwa mdomo, na viungovyake mwenyewe ndo vitazungumza kumtolea ushahidi:-Qur an 36:65."Siku hiyo tutaziba vinywa vyaoitazungumza mikono yao na itoeushahidi miguu yao kwa yale (yote)waliokuwa wakiyachuma".Ushahidi kama huo lau ungeruhusika kutumiwahapa duniani basi fedheha zingekithiri kwa watu, na penginewengi wangekua wasafi kuliko walivyo leo takribanulimwengu mzima, hata katika nchi ambazo katiba yao niQur-an mfano wa Saudia, lakini Mnyezi Mungu mwingi warehema, na mwingi wa kusubiri.Mtu ataambiwa haya ingia moto wa jahannam leokwa yale uliokuwa ukiyakufuru. Basi kwa sababu ya ukafiriwako ukakataa kupokea uongofu. Hujaambiwa wewekuambiwa kwamba:- Qur an 45:11.13

“Huo ni uongofu, na wale waliozikataa ayaza mola wao watakua na adhabu kubwayenye kutokana na adhabu iumizayo”.Au:“Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu,nazo niUongofu na rehma kwa watu wanaoyakinisha”.Bila shaka uliambiwa, sasa kilichokuzaini mpakaukaacha Kuongoka ni kitu gani? ukisema ni shaytwani bilashaka utajibiwa:-Qur an 36:60-61.“Je! Sikukuagizeni (sikukuusieni) enyi wanadamukuwa msimuabudu shaytwani? hakika yeye niadui aliyedhahiri kwenu. Na ya kwambaniabuduni MIMI, hii ndio njia iliyonyooka”Ukisema ni pesa, utakumbana na kauli kama hii iliyokomwenye surat Humazah: Qur an 104:1-7."Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kurambakisogo msengenyaji ambae amekusanya mali nakuyahesabu (tu bila ya kuyatumia katika njia za14

kheri) anadhania kua mali yakeyatambaki kisha milele. Hasha! Bilashaka atavuru mishwa katika (motounaoitwa) Hutwamah?na ni jambo gani litakalokujulisha (hataukajua) ni nini (huo moto unaoitwa)hutwamah? ni moto wa Mungu uliowashwa(kwa ukali barabara ambao unapanda)moyoni".Kama wewe ni mwenye akili na umepania kuongoka, basiutaacha yote hayo, ambayo hakika yake ni pambo tu lamaisha ya kidunia na ni mitihani ambayo Mnyezi Munguatakutizama umefaulu au umefeli mitihani hiyo. MnyeziMungu anamtizamia aliyemneemesha mali kuzidikumshukuru na fakiri kusubiri.Amma kuacha kwako huko bila shaka si vingine bali nikuudhiddi Moyo au Nafsi yako na kurudi kwa mola wako,nawe umepewa nguvu ya kuweza kupinga matamaniomatakwa ya nafsi ambayo ni adui yako mkumbwa – weweni mtawala wa mwili wako mzima ambao ni dunia kamiliambayo ndani yake ndiko unakoanza huo – ulimwengumkumbwa mno ambao ndo Mnyezi Mungu alotukuka.Uwezo uliopewa umeelezwa vizuri katika aya hii:Qur an 79:40-41“Na amma yule ambaye aliyeogopakusimamishwa mbele ya Mola wake,akaikataza nafsi yake na matamanio(maovu). Basi (huyo) pepo ndiyo itakuwamakazi yake”.Mnyezi mungu anatwambia ndani ya Qur-an suratInsaan kwa jina jingine inaitwa suratil – Dahar:Qur an 76:3.15

“Hakika sisi tumemuongoa (tumembainishia)njia (zote mbili hizi kua hii ndio ya kheri nahii ndio ya shari) basi (mwenyewe tena)atakua mwenye shukurani (sio kwakusema Al-hamdullillah kama wengiwanavyoichukulia, bali ni kutekeleza amrizote ambazo Mnyezi Mungu ametuagiza nakuacha makatazo yake yote) awe mwenyekukufuru (kukanusha)”Basi hapo khiyari ni yako ukitaka kua Muislamuutakua umechagua njia ya: kushukuru, au ukitaka kua kafiriutakua umechagua kukufuru na Mnyezi Mungu ndiyeHakimu wa mahakimu wote, siku ambayo hakunaatakaetamba hata mmoja bali yeye tu peke yake. Hakunaawezae kutoa hukumu juu au dhidi ya Mnyezi Mungu katikasheria zake. Lakini kuna kuyatizama mambo yalozunguukasheria hizo zenye kufanya mambo ya Uislamu kisha uonenjia sahihi ya kupita.Maudhui ya mada hii imekusanya mambo makubwayafuatayo katika uongofu kua: “Ni wa Mnyezi Mungu”.Mwanadamu ana khiyari, fursa nyembamba ya kuchaguabaina ya kuongoka au kupotea. Mkataba wa tangu na tangukatika ahadi na mithaki kati ya Mnyezi Mungu na viumbewaliohusishwa na amana – yaani Uislam, Al habib Omaraliisemea amana hiyo katika magazine mashuhuri wakati ule"African events" (The trust that is Islam) – Alisema:"Angels were there and God left them and appointedhuman beings to be vicegarents on earth". Mamboyote hayo yalituka kabla hatujaja duniani kuitekeleza amanahiyo. Hakika ya mambo yote hayo kuanzia la mwisho nikwamba hata mtu mwenyewe hana uwezo wa kuyakinishakua alitwaa ahadi ya kuukubali Uongofu muda wake wotewa maisha mafupi na ya mda ya hapa duniani au alichaguauongofu mwanzo tu lakini mwisho kupotoka, amma kwafursa finyu ya kuchagua hawezi kuyakinisha atadumu akiwamwongofu au atabadilika katikati au vinginevyo yaani:-Aongoke, apotee, aongoke au tena apotee aongokeapotee au anaendelee na kuongoka moja kwa moja au apoteemoja kwa moja.16

Na aidha kwa Uongofu wa Mnyezi Mungu, ni yeye tundiye anayejua nani na nani aongoke au laa. Hii ni kwasababu Mnyezi Mungu hashirikiani na kiumbe yeyote katikakupitisha mambo yake – yeye hufanya apendavyo –haingiliwi hahojiwi wala hazuiliwi katika kupitishaayatakayo.Ikiwa ni hivyo basi kiumbe ana haki au wajibu wakuridhia juu ya kadhwaa ya Mnyezi Mungu na kuwekamatarajio na matumaini katika rehma zake kubwa mnozisojua mipaka. Na kwa vile Uislamu ni kusalimu amri nakunyenyekea kwa kadiri ya uwezo wake, basi mtuakiwafikishwa katika Uongofu basi la wajibu ni kuzidishaunyenyekevu wake na kuzidi kumuomba Mnyezi Munguambakishe Uislamuni na kumfariji kwa Husunul kha –tima asione kuwa kuswali kwake na kadhalika kutokana nauhodari wake katika kutumia nafasi ya ufinyu wa hiyarikuliko kua amependelewa kheri na Mnyezi Mungu.Mnyezi Mungu ni: Muqallibal Qullub. Mwenyekuzipindua nyoyo atakavyo, leo hivi kesho vile basiusijitukuze eti kwa sababu uko kwenye twa-a ya Mola wako,wala usimlaani na kumcheka ambae yuwamuhasi MnyeziMungu badala ya kumuombea Uongofu ili aongokewe kamawewe – kumbuka ya kua Mnyezi Mungu amemficha waliiwake baina ya watu, kwa hivyo si rahisi kumjua yuleunaemdharau yu vipi mbele zake Sub-hana wa Taala.Kama alivyoficha ridhaa yake katika Twa-a yake;na machukio yake katika maasi yake. hawezi mtu kujua niTwa-a gani anayoifanza ambayo itamridhisha MnyeziMungu au maasi gani anayofanza ambayo yatamchukizaMnyezi Mungu kwa hiyo asidharau thamma asidharau katikaTwa-a kitu chochote wala katika maasi kitu chochote.Kwa hiyo tumuombe Mnyezi Mungu atuwafikishekatika kheri zake, na katika yale anayoyapenda nakuyaridhia. Mambo yake mtu yote yameshaandikwa siku ileya kupulizwa roho akiwa ndani ya tumbo la mama yake:Riziki yake, Amali yake, Ajali yake, na kua kwakeMwema au Shakiyyi- yaani Muovu – (hadithi mashuhuri).Lakini Mnyezi Mungu ni mrehemevu na msamehevu kupitakiasi hakuna wa kuweza kukadiria. Na hakuna dhambiinayomshinda kusamehe – Illa-shirk. Basi tusikate tamaana rehema zake.WABILLAHIT - TAWFEEQ.17

Maneno Ya Hikma:*** Mtu ni kuendeshwa (msayyir), si mwenye khiyari*** Muumini wa kweli hana khiyari katika ambayoMnyezi Mungu na Mjumbe wake wameamua.*** Uislamu ni Dini ya maumbile*** Kila kizaliwacho huzaliwa katika ncha ya Uislamu.*** Husunul kha-timani kukata roho na "La-ilaha allalLahu" – Malipo yake ni pepo.*** Bwana Mtume SAW. Ametwawafu na kauli yamwisho: "Ummati – Ummati" (Umma wanguUmma wangu).*** Uwongofu ni wake yeye Sub-hana wataala.Bwana Mtume S A W amesema:-“Nimepewa elimu koche koche.Katika hizo ni elimuambayo nimeamrishwa niwafundishe watu wote. Na katiyake ni elimu ambayo nimeamrishwa niwafundishe watumahsusi. Na miongoni mwa elimu hizo zipo ambazonimeamrishwa nisimfundishe (mtu) yeyote”.Bwana Mtume S A W amesema:-“Mwenye kuchukua maji ya mvua akayasomea ndani yakeSuratil:Fa-tiha………..………………….………….70Suratil – Naas………………..........………...70Suratil – Falaq………………….…………...70Suratil – Ikhlas…………………….……..…70Na swalatu alan naby…………….....…........70Basi nina apa kwa yule ambae roho yangu iko mikononimwake, hatokunya maji hayo ambaye ana ugonjwa wowoteilla Mnyezi Mungu atamponesha”.(Hadithil Quds).Kasema Bwana Mtume S A W kua:-“Mwenye kutaka kuelezea maovu ya mwenzakebasi na atangulize kueleza maovu yake yeyemwenyewe kwanza.(Kwa kua kila mtu ana makosa tu, maadam sio maaswun-yaani alokingwa na kufanza maovu) nawalo bora katika watenda makosa ni wale wenyekutubia”.18

Mtungaji(Al marhum)AL- FAQEER AL -HABIB AHMAD SHEIKHSecond additionToleo la pili19

Vitabu vilivyokwisha toka ni:*1. Maana halisi ya Imaan. (i) (1 st 2 nd & 3 rd addition ).*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako.*3. Njia nyepesi ya kujua kitu juu ya uongofu.*4. Knowledge vision & ecstacy.*5. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu.*6. Waislamu na Sayansi - Ulu-m.*7. Kuhifadhi Burda.*8. Maana halisi ya Imaan (ii).*9. Muhammad SAW katika ulimwengu wa ghayb.*10. Siri ya Balaa.*11. El makhlouq (Viumbe)*12. Njia nyepesi ya kujua juu ya uongofu. (2 nd addition)Vitabu ambavyo tunategemea kuvitoa muda si mrefu(Insha Allah) ni:*1. Waislamu na Sayansi - Ulu-m. (2 nd addition)*2. Njia nyepesi ya kuijua nafsi yako. (2 nd addition).*3. Mwinyi Baraka katika ulimwengu wa kiislamu. ( 2 nd .addition).*4. Some aspects of concepts of facility in medevial IslamicPhilosophy by Mwinyibaraka.*5. Manaqib ya Al habbib Ma`aruf.Kwa maulizo kuhusu vitabu wasiliana nasi:Majaalis El Ulaa El Qadiriyya – Sinza,P.o. Box 15170,Tel: 0748595958.Tel: 0744 023703.Tel: 0741 235091.Tel: 0744 299597.Dar es salaam

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!