You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
KUZALIWA KWANGU NA MALEZI YANGU:

“Naona afadhali nielezee kwanza msingi wa malezi.

Nilizaliwa Zanzibar mwisho mwaka 1917 yaani

December kwa mujibu wa Sheikh, yeye atakuwa anamjua

Mzee wangu vizuri kwani alikua ameoa kwao, kwa Babu na

Mama wote Masharifu walozaliwa Ngazija. Babu Abu-Bakkar

Bin Salim, Mama Lydiid Jamallilleye.

Babu mkubwa Sayyid Abdul-Hassan baada ya miaka

miwili yaani 1938 Baba yangu huyo alifariki-Mungu

amrehemu. Na baada ya miaka mitano ya umri wangu mama

alifariki - Mungu amlaze mahali pema . Nikalelewa na Mume

wa Khaalal Ibin Khaalat wa Mama yangu Seyyid Abdul-

Fattaah Bin Ahmed Jamalilley akiitwa sharifu Abudu.

KUANZA KUSOMA:

Nilipelekwa chuoni kwa Al-Mar-hum Seyyid Sheikh

Bin Abdul-Rahman Babake Seyyid Hassan Sheikh nikawa

nasoma, na Sala nimesoma kwa Bibi mkubwa mwana-Ashata

kama alivokua akiitwa Aisha lakini wakimwita Mwana-

Ashata.

Nikabaki baada ya kuhitimu nasomesha watoto chuoni huko

huko na Khalafu nikawa nakwenda nasomesha watoto chuoni kwa

Sharifu Abudu, na wakati huo huo tena nikatiwa Skuli, lakini kwa

sababu ya kukawia kuingia Skuli, sikupata Mnazi mmoja.

Nikapelekwa Mwembe-ladu kutoka Kisiwandui asubuhi, ninarudi

halafu nakwenda saa nane tena mpaka mwisho nikaja zangu Mnazimmoja.

Baada ya kusoma miaka mitatu Mwembe-ladu na mwalimu

wa mwanzo wa Skuli hiyo alikuwa Juma Mohamed, wakimwita

Juma Mohamed Mushte - sijui kwanini Mwalimu Juma Allahu-

Yarham.

1.