You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
MAISHA YAKE.

Sasa naanzia:

Utajo wa kuzaliwa kwake Mwenyi Ezi Mungu atakase siri

yake Bwana Al-Maarufu alizaliwa mwaka Saf 1270 Hijra katika

mtaa wa Bajanani, Moroni Ngazija.

Alizaliwa katika nyumba iitwayo "Shashanyongo". Baba

yake ndiye aliyemlea. Alisoma kuran Ngazija akawa anasoma

kwa Tajwidi.

Baadaye Baba yake alimpeleka Zanzibar si kwa

jingine lolote ila kutafuta ilmu. Alikaa Unguja kiasi ya miaka

mine, takriban akazijua vilivyo fani za Tajwidi, Fiqih, Nahw na

kiasi cha kutosha katika ilmu za hadithi na kuran. Ilmu zote hizi

alizichukua kutokana na mjomba wake Sayyid Ali Bin Sultan

Ahmad.

Wakati wa safari yake, Babu yake upande wa mama

yake Sultan Ahmad alimwambia; "Tutafutie ilmu ya haqiq

(undani wa mambo yaliyohusiana na Uungu) kwani sisi hatujui

vilivyo".

Baada ya kusoma ilmu hizo alirejea Ngazija, akashughulika

kukunjua ilmu zote hizi na kuita watu kwa Mwenyi Ezi Mungu

katika msikiti wa Ijumaa. Alianza kusomesha katika tafsiri ya

kuran Jalalain katika wanafunzi wake waliosoma kwake fanni ni

mwalimu wake wa Tajwidi Musa Bin Ahmad.

Muhimu:

Baba yake Sayyid, Mungu amuie Radhi ilikuwa

hakupata mtoto mwanaume. Basi alipohiji akakusudia Madina

kumzuru babu yake, Rehema ya Mwenyi Ezi Mungu na Amani

yake ziwe juu yake, alimuomba Mwenyi Ezi Mungu katika Quba

la mtume (SAW) amruzuku mtoto mwanaume kwa mke wake

mlahirifu Mwana mkuu Bint Sultan Ahmad. Aliweka nadhiri

hapo ikiwa Mwenyi Ezi Mungu kamruzuku mtoto mwanamme

1.