You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
wa Mwenyi Ezi Mungu ananiamrisha nitaje Ismul-Jalala".

Sayyidat Alawiyya huyu ndiye ambaye Sheikh Abdallah

Darwesh alisema katika kumtaja kumpa cheo chake:

"Wangegawika Muridi mimi ningekuwa pamoja na kikundi

alichomo Sayyidati Alawiyya".

Katika siku hizo alikwenda Sayyid kwenye Bustani ya

mama yake ijulikanayo kwa jina la Buzini akakaa huko siku

nyingi awemo ndani ya Khalwa (Muepukano na kila kitu kwa

kushughulika na Mwenyi Ezi Mungu) Hapo ilimjilia kwa daraja

kubwa hali wapatao Mawalii wakubwa ilirejea nayo Mironi

akaingia nyumbani kwa Sheikh Abdallah Bin Himid, akabaki

pamoja naye huko siku tatu bila ya kuingia huko nyumba yoyote.

Baada ya hapo alitoka Sheikh Abdallah Bin Himid

na Sayyid akapanda juu ya sakafu ya nyumba akafika ukingoni

akaanguka, nduguye Sayyid alimchukua mpaka nyumbani kwa

mama yake akabaki nyumbani kiasi ya miezi sita na Ahwal zake

zikizidi hatuwezi kukisia aliyoyapata katika yajayo kutoka na

Mwenyi Ezi Mungu pamoja na yanayoteremka na miminio

alipokuwa katika hali hiyo mara yumo ndani ya صحو mara

nyingine محو pengine huwa عينةkatika na pengine katika

(Maneno haya hayafasirika kwani ni Istilahi za Mabwana حضو ر

Masufi. Hayana maana ya lugha wenyewe wanatambua kwa

Dhawq. Kuyaonja na ekspiriense. - Mfasiri). Aliendelea hata

akapata ambayo hatwezi kuyatambua vilivyo na tunahemewa na

kudiriki hakika yake.

Jadhba hii ni mash-hur Ngazija kwa Muridi wote. Yeye

Sayyid alisema wakati katika Jadhba yake "Mimi ni kitu Azizi

mimi ni kitu kilichotokana na Mtume (S.A.W) na ni hasha

Mtume kumpa baba yangu kitu kidhalilifu". Alisema:

(Mwenyi Ezi Mungu atunufaishe kwa baraka zake ) "Ingekuwa

bahari ni wino na miti kalamu ili kudhibiti niliyoyaona

bahari ingekwisha na miti ingemalizika kabla ya kumalizika

mambo niliyoyaona katika Jadhba yangu hii".

Baada ya hapo alirejea kukaa na watu kama ada yake ya

mwanzo akasafiri kwenda Hinzwani akateremka Mtsamudu.

Sultan Abdallah alikuwa Bambao alimtaka Sayyid aende huko na

yeye akenda pamoja na baadhi ya Muridi. Sultan Abdallah

akampokea kwa taadhima na mtukuzo, na yeye alikuwa

akijihisabu kuwa ni katika jumla ya Muridu. Katika baadhi ya

10.