Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
mwenye kutizamwa kwa jicho la kusaidiwa na kutengenezewa

kutokana na bwana Muumbaji khalafu alisafiri kwenda Zanzibar

akakutana na Sheikh Uways na akachukua Tarika ya Qadiria

kutokana naye akarejea Ngazija baadaye akenda Nzwani wakati

huo anadhikri kwa Tarika ya Qadiriya wala hakumpa yeyote Ijaza

ya Tarika hiyo, bali baadhi ya nyakati alikuwa hujitenga faragha

akadhikiri peke yake baadae hurejea kwa wapenzi wake.

Aliporejea Ngazija haikuchukua muda mrefu ila alifika

Sheikh Abdallah Darwesh alikuwa kafuatana na ndugu yake

Sayyid Abdal Rahman Bin Sheikh na mama yake Sayyidat

Mwana Mkuu wakaja katika jahazi moja.

Sayyid alikutana na Sheikh Abdallah Darwesh alie

mchukulia amana na pakapatikana baina yao mahaba kwa

mtizamano wa mwanzo.

Hayo yalitokea kwa hekima ya Mwenye Ezi Mungu

aliyeumba akatengeneza kila jambo na vipawa vya kukusudiwa.

Sheikh Abdallah alitelemka kwenye kisiwa cha Ngazija

akaingia katika vingi katika vijiji vyake. Alipokuwa anazunguka

katika vijiji hivyo aliona katika baadhi ya njia zake ndege wawili,

mmoja akatoa ubait huu:

شرتث شراب السر مه خمر الصفاء

Wapili nae akatoa ubait huu:

فسكرت لو حقا ومالي منا زعا

Sheikh akaongeza juu ya ubait huu Abyat nyingine kama ilivyo

katika kasida ijulikanayo Ubait wa mwanzo wa qasida hiyo ni:

سقاء في سعاىاالحثية فلم ارى

سواه علي اال طالقا فىاكون المع

mpaka mwisho.

Baadae Sheikh Abdallah alifanya makazi mahali alipozaliwa.

Itsandaa mjini (Huko ndiko alipozaliwa mrithi wa Ahwal za

Mawalii na Maqamat yao Seyyidna Al-Habib Omar Bin Ahmad

Bin Sumeit رضوان هللا عايو na baba yake alizaliwa huko huko,

babu yake Al-Habib Abubakar ndiye aliyetoka Shibam

Hadhramaut kuja Ngazija- Mfasiri).

Huko kwao Itsandaa Sheikh Abdallah alifungua chuo

cha kusomesha watoto kur-an tukufu na baadhi ya vyuo vidogo

vidogo. Baadhi ya watoto walikua wakikhitimu kuran takatifu

kwa muda wa chini ya miezi sita kwa baraka zake hata wengi

4