Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Alirejea tena Mtsamudu, lakini hakukaa hapo mda mrefu

akatakiwa kwenda Bombo akaenda pamoja na baadhi ya Muridi,

akakaa huko siku kadha wa kadha aliwapa Ijaza huko watu wengi

akafanya khalifa juu yao Sayyid Jaafar baadae alirejea Mtsamudu

akadumu katika Masjid Ar hmani katika kumtaja Rabbu wake.

Hakuwa akienda msikiti wa Ijumaa ila siku ya Ijumaa.

Kupingwa na Sheikh Fadhil na Jawabu ya Sayyid na

yaliyopita baina yao kwa ufupi.

(Mungu awalie Radhi wote wawili na atunufaishe kwa wote)

katika muda huu Sheikh Fadhili alimpinga Sayyid katika

kuwapa Ijaza ya Tarika watu wa Hunzuwani pamoja na kuwa

wao si Ahli kama alivyodai yeye hali ya kutoa Dalili kwa hadithi

"Msiwape hekima wasiostahiki msije mkadhulumu" na katika

hadithi nyingine au utimilifu wa hii au hadith khutba na mimi

ndie Mufti wa Sawahil yote tangu Ras hafun mpaka Ras torfi na

mimi nimezuia dhikri juu yenu au kuisoma mbele yangu. Seyyid

alisimama akasema "Huna njia ya kuzuia dhikri", wakati huo

zogo lilizuka kwa wingi msikitini watu walisimama na kelele

zikaja juu. Kila mmoja akakamata silaha yake, Sayyid nae

alinyanyua upanga wake Sayyid Abdallah Bin Sheikh alitoa nje

upanga wake Sayyid Abdallah Bin Omar Khajar lake akelekea

kwa Sayyid Abdallah Bin Omar aliyeitwa Abood Bin

Muhammad Bin Omar, mtoto wa nduguye Abdallah Bin Omar ni

katika Muridi wa Sayyid. Hapo hapo alimpiga kofi Ami yake

kwa sababu ya wivu juu ya Sheikh wake hivi ndo anavyokuwa

Muridi. Sultan Abdallah alikuwapo msikitini askari wake

wakamzunguka Sayyid akatoka nje ya msikiti akanadi anaetaka

Ijaza na ahudhurie wakahudhuria mbele yake wengi na yeye

pamoja waliokua pamoja naye wanataka jina la Mwenyi Ezi

Mungu. Baadae alitoa sauti akatoa nje upanga wake mbele ya

Sultan Abdallah. Askari walipoona upanga walikimbia, Sayyid

alimshika Sultan mkono akamwambia: "Sema Allah" akawa

anasema pamoja naye wakafuatana nyumbani na waliokuwapo

waliwafuata na wote wanataja jina tukufu mpaka Sultan akaingia

nyumbani kwake.

Assayyid alielekea Mirontsi na kikundi katika Muridi wake

walimfuata lakini hawakufika pamoja naye kwenye msikiti wa

8.