You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
askari ambao walitafuta baadhi ya watu wajulikanao

wakawachukua baadhi yao. Walimtafuta As-Sayyid lakini yeye

alijificha hawakuweza kutambua alipokuwa. Mitsamhuli

ilikuwapo jahazi inakwenda Zanzibar, Sayyid alipanda usiku

wakati ambao wanaomtafuta wameghafilika walipokuwa

hawakumpataSayyid, nchi kavu wazungu walipanda kwenye

jahazi ili watizame ikiwa hajajificha humo jahazini. Walipoingia

jahazini wakaanza kupekua, palivuma upepo mkali na mawimbi

yakachafuka, hapo hapo waliteremka bila ya kumuona, "Na wapi

jicho pofu litaona jua?" wakati huo mnyororo uliofungiwa jahazi

na nanga ulikatika na Jahazi ikaingia baharini matanga

yakapandishwa na jahazi ikatweka kuelekea Zanzibar.

Imewachukua Sayyid na Muridi wake wawili Ahmad

Nakhodha na Abdul-R-rabb jahazi ilipokuwa mbali na nchi kavu

Sayyid alisimama juu ya sitaha akababaika mmoja katika muridi

wake akasema: "Eeh bwana wangu, umejitokeza watu watakuua

iwe sababu ya sisi kuangamia", akajibu "Usihuzunike na sisi kwa

kupenda Mwenyi Ezi Mungu baada ya salat aljumaa tutaingia

Zanzibar. Safari yake ilikuwa jioni ya jumanne. Ikatokea vile vile

kama alivyosema kwani waliingia Zanzibar baada ya salat

aljumaa.

Aliishi Sayyid Unguja hata mpaka alipotolewa Sultan

Sayyid Ali Ngazija Dola ya kifaransa ndio iliyomtoa. Hapo

alirejea Ngazija na hakusafiri kamwe. Hakuondoka huko hata

Mwenyi Ezi Mungu akamchukua hali ya kuwa yeye Sayyid

karidhia na karidhiwa.

منا فيو رض هللا عنو

12.