11.07.2015 Views

Read - Polis

Read - Polis

Read - Polis

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Uongozi wako, Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limekuwa Bunge laViwango na Bunge ambalo limejitahidi sana kukidhi matarajio ya Watanzania kwakiwango kikubwa. Tumelifikisha Bunge hili mahala ambapo Watanzania wana hamu yakulisikiliza Bunge lakini si kusikiliza tu, wanalifurahia Bunge na Mabunge ya Njeyanakubali kabisa na watu makini wanakubali pia kwamba, Bunge lako ni la Viwango nalinasimamia maslahi ya nchi kwa kiasi kikubwa. (Makofi)Mheshimiwa Spika, nichukue nafasi hii, kumpongeza Waziri Mkuu, MheshimiwaMizengo Kayanza Peter Pinda, kwa utumishi wake uliotukuka, lakini zaidi ninaipongezakazi kubwa ambayo ameifanya kwa muda tangu ameteuliwa na Mheshimiwa Rais. Jimbolangu la Simanjiro haliwezi kumsahau na kusahau mchango wa Mheshimiwa WaziriMkuu, kwa kulitambua tatizo kubwa la maji ya Wilaya ya Simanjiro na kuwa WaziriMkuu wa nchi yetu ndani ya Bunge hili kueleza kwamba, japo Watanzania wanamatatizo makubwa ya maji, lakini Wilaya ya Simanjiro inaongoza. Najua hakupendeleana hana tabia ya kupendelea lakini alieleza hali halisi.Mheshimiwa Spika, ninajua yote haya tumeyafanya na kulifikisha Bunge letumahala stahiki kutokana na uongozi na ushirikiano wa mtu anayeheshimu mgawanyikowa majukumu ya mihimili mitatu ya dola na huyu si mwingine ni Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete. Unaweza kusema lolote unaloweza kusema, lakini MheshimiwaKikwete, kwa miaka yake mitano ya uongozi wa taifa letu, amejitahidi sana kutembeakwenye maneno yake. Hakuna mashaka kwamba, kwa mwaka huu wa uchaguzi,watanzania wakifanya tathmini ya kweli, watakuwa hawana sababu yoyote yakutomrejesha madarakani Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na kwa wale wotewenye nia ya kugombea na Mheshimiwa Kikwete ni haki yao wanakaribishwa ilawafahamu Waswahili wanasema mbuyu hauangushwi kwa kisu cha kukatia nyanya.(Makofi)Mheshimiwa Spika, ni dhahiri pia kwamba, taifa hili linatarajia mara baada yauchaguzi ujao wa mwezi wa kumi, liendelee kuwa na Rais makini na liendelee kuwaBunge litakaloendelea kutetea maslahi ya nchi yetu.Mheshimiwa Spika, ninaamini kabisa Wananchi wa Urambo wakikuchagua wewena nina hakika watakuchagua, sioni ni kwa namna gani Wabunge walioko leo nawatakaokuja wasikuchague kwa mara nyingine kuliongoza Bunge hili la Viwango nakuendelea kuiweka nchi yetu katika rekodi ya Dunia na kuweka mahali ambapo sisitutaendelea kuheshimiwa katika Mabunge ya Kimataifa.Mheshimiwa Spika, najua kwa kutimiza wajibu huu wa Mbunge yeyote makini,upo uwezekano wa kukanyaga vidole vya watu na ninajua kwa miaka mitanotumekanyaga vidole vya watu hasa pale tunapogusa maslahi ya watu wachache.Watanzania walio wengi wameridhika na ndiyo maana nina imani watakuchagua wale waUrambo, Watanzania watamchagua Kikwete na Bunge lijalo Inshallah linawezakuendelea kukuchagua wewe kuwa Spika wa Bunge hili ukisharudi hapa na ninaona afyayako ni nzuri.30

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!