11.07.2015 Views

Read - Polis

Read - Polis

Read - Polis

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

MHE. TATU M. NTIMIZI: Mheshimiwa Spika, ahsante na nakushukuru kwahuruma.Mheshimiwa Spika, kwanza naipongeza hotuba ya Waziri Mkuu na naiungamkono. Nawashukuru kwa utendaji wao wa kazi kuanzia Waziri Mkuu na watendajiwake wote kwa kazi ambayo wameifanya kutokana na hotuba hii, tunajua kwamba kwakweli wana haki ya kupongezwa.Mheshimiwa Spika, naomba nimkumbushe Waziri Mkuu kuhusu jambolililofanyika kwenye Jimbo langu la kutaka Halmashauri, Waziri Mkuu alipokuja Jimbonikwangu wananchi walimweleza katika kijiji cha Kigwa, kwamba ana furaha sana kazizote zimefanyika, utaratibu kuanzia Vijiji, Kata mpaka Wilaya tayari maelekezo yoteyamefanyika kisheria na sasa wanangojea hatma ya kupata Halmashauri yao. Chondechonde Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui yako mbali, wananchi wangu watapata tabusana kama hawakupata Halmashauri, naomba Halmashauri hii kwa sababu ya manufaa yawananchi wetu na jambo hili lipo katika ofisi yako tafadhali iliangalie kwa macho yahuruma ili Jimbo la Igalula lipate Halmashauri yake liweze kujitegemea katika kupatahuduma za jamii.Mheshimiwa Spika, Rais alipokuja mwaka jana wananchi waliomba umemekatika maeneo muhimu, hasa Kigwa ambayo ni center kubwa sana na barabara ya Itigindipo inapopita na hapo pia kuna sekondari ya Kisanji, hapo ilikuwa makao makuu yawakimbizi, kuna miundombinu mingi sana. Rais akasema kwamba Wizara hii ifanyeutaratibu wa kuviwezesha vijiji hivi kupata umeme kwa sababu umeme umeingia Uyuiambako ni Makao Makuu Isikizya lakini kuna kijiji kinaitwa Mayombo, Mayombompaka Kigwa ni kilomita ambazo hazizidi tano, ni rahisi kuteremsha umeme pale kutokaKigwa kuja Igalula na Igalula kuja Igoweko angalau center kubwa kama hizi zipateumeme. Lakini watalaam kila mara wamekuja kutazama wanapita katika Jimbo zimauwezekano wa kuanza kuteremsha umeme lakini imekuwa ni safari za utalii wanaingia nakutoka kila mwaka si chini ya miaka mitatu, je ni nini hatma ya kupata umeme?Mheshimiwa Spika, Jimbo hili ni kubwa, umaskini tunao lakini bila kuwa naumeme kwa kweli itatuletea matatizo, nitashukuru sana kama suala hili la umeme badoliko katika maandalizi yao angalau tuone hatua gani inafanyika.Mheshimiwa Spika, lingine mwaka juzi na mwaka jana nilizungumzia kuhusumajengo yaliyojengwa ya zahanati, wananchi wamejitolea, Serikali imetusaidia,niliendelea kuzungumza katika Bunge lako, kwa hiyo majengo haya yamekamilikampaka nyumba za wauguzi zimekamilika na wananchi wamejitolea sana kufanya kazi hii,lakini kwa kweli miaka mitatu hospitali ya Itundaukulu, Nzigala, Kalangasi ni maeneoambayo sasa hivi mwisho tunaweka wafanyakazi wengine, wananchi wanapata taabu.Maeneo ambapo zahanati zipo ni mbali kutoka katika maeneo yao, ndiyo maana Serikaliikahimiza kwamba kila kijiji kuwe na zahanati angalau wananchi wapate huduma hizi,lakini kwa masikitiko kila mara Waziri akisema kwamba tunajitahidi kupelekawahudumu lakini kila mwaka inakuwa ni ahadi.38

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!