11.07.2015 Views

Read - Polis

Read - Polis

Read - Polis

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

kuzifanyia ubadhilifu fedha hizo. Waheshimiwa Wabunge ni madiwani katikaHalmashauri za wilaya, lakini licha ya malalamiko ya wabunge kwamba vikao muhimuvya maamuzi ndani ya Halmashauri vinafanyika kwa wakati wabunge wakiwa Bungeni!Wakati mwingine vikao vinaahirishwa hadi wabunge waondoke majimboni, lengo nikuondoa mchango wa mbunge hasa katika uwezo wake wa kuchambua mipango nataarifa za utekelezaji zinazotolewa katika vikao.Mheshimiwa Spika, bado mbunge ni kiongozi wa Kata zote katika Jimbo lakiniDiwani mmoja kwa Kata moja tu anapewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Halmashauriau Meya na kujijengea mazingira ya kuwa na madaraka makubwa zaidi hata kulikoMbunge wa Jimbo. Baadhi ya wenyeviti hao elimu na uwezo wao wa kiutendaji nimdogo sana na kwa hali hiyo watendaji waovu hutumia nafasi hiyo kufanyawanavyotaka na hata kudiriki kuandika Taarifa za uongozi za utekelezaji wa miradi nakuziwasilisha hata mbele ya kamati za Bunge akiwepo mwenyekiti wa Halmashauriwilaya.Mfumo huu kama ambavyo nimeueleza katika Bajeti za 2008/2009, 2009/2010 nasasa 2010/2011, unahitaji kufanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na kuona jinsi yakupunguza wingi wa akaunti za fedha katika Halmashauri zetu za wilaya.Kwa matarajio makubwa ya uchambuzi wa mapungufu kwa lengo la kuimarishaufanisi katika halmashauri zetu.Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.MHE. MWADINI ABBAS JECHA: Mheshimiwa Spika, katika hotuba yaMheshimiwa WaziriMkuu, amegusia hatua mbalimbali ambazo zimeanza kuchukuliwana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kufanikisha maandalizi ya Uchaguzi huo.Miongoni mwa hatua ambazo zinachukuliwa ni pamoja na kuboresha Daftari la kudumula Wapiga Kura.Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu shughuli za uandikishaji wa wapigakura kwa upande wa Tanzania Zanzibar unasimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar(ZEC). Daftari hili ndilo ambalo pia linatumiwa na NEC katika Uchaguzi wa Rais waJamhuri wa Muungano wa Tanzania na Wabunge. Lakini kumekuwa na malalamiko yamuda mrefu kwamba maandalizi ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa upande waZanzibar umegubikwa na matatizo mengi sana, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wananchikunyimwa haki hiyo kwa visingizio mbalimbali. Aidha kuna baadhi ya wananchiwanaandikishwa zaidi ya mara moja ama kwa kutumia majina tofauti na katika vituotofauti vya kujiandikisha.Kadhalika kuna baadhi ya wapiga kura majina yao kuachwa kwa makusudi aukuhamishwa na kupelekwa vituo vingine vya mbali na wanapoishi.Mheshimiwa Spika, matatizo haya pamoja na mengine ambayo sikuyataja hapalengo lake kubwa ni kuwanyima baadhi ya wananchi haki yao ya kikatiba ya kuchaguaviongozi wanaowataka. Aidha baadhi ya wananchi wanapewa fursa zaidi ya moja yakuchagua viongozi ili viongozi Fulani wachaguliwe kwa kura za kishindo kinyume nataratibu zinazokubalika. Kuna baadhi ya watu hasa mipakani na raia wa Msumbiji48

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!