11.07.2015 Views

Verbatim Report of - ConstitutionNet

Verbatim Report of - ConstitutionNet

Verbatim Report of - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

10ni hayo tu.Com. Ratanya: Okay asante sana kwa hayo maoni yako Nahuru, kwa hivyo tutaenda kwa mwingine this is Mrs. KenuLekilanu. Kwa hivyo huyu ameleta maandishi yake tutaenda kwa mwingine, Judith Leshamta.Judith Leshampta: Maoni yangu juu ya Katiba. Jina langu ni Judith Leonard Leshampta. Namba ya kitambulisho ni hiyo0661489.Kanuni ya kuongoza sera za Dola; Ni lazima maadili yawe yakutekeleza kisheria. Ukuu wa Katiba; Wananchi wahusikekupitia mikutano ya maoni katika kubadilisha Katiba zile ambazo zinafinya wananchi wa kawaida. Mikutano hiyo iongozwe naTume ambayo imeteuliwa ya marekebisho ya Katiba. Uraia; Atakaye pewa uraia bila swali, ni yule ambaye ana cheti chakuzaliwa na cheti cha ndoa na wazazi wake ni wa mahali pale. Mtoto aliyezaliwa na mzazi mwana mume wa Kenya ambayeanacheti cha ndoa apewe uraia.Vyama vya kisisasa; Kuwe na idadi maalum ya kyama vya kisiasa-viwe tu viwili. Muundo na aina za serikali; Tuwe namuuondo wa serikali ya majimbo ambapo mamlaka ya nchi na Bunge yame gawanywa baina ya serikali kuu na majimbo na piani mipaka iheshimiwe. Kazi ya Mbunge; Kazi ya Mbunge iwe kila siku. Mamlaka ya nchi; Katiba itoe kibali ili Rais awezekuondolewa mamlakani kwa kitendo kisicho halali. Rais awe Mbunge wa jamii aliotoka. Serikali za mitaa; Mayor namwenyekiti wa baraza wachaguliwe na watu au wananchi. Wananchi wawe na haki kurejesha nyumbani diwani au Mbungewao. Madiwani wa ku tueliwa wateuliwe na watu kwa kupiga kura. Muundo wa uchaguzi; Tutafute muundo wa kura ya siri,na aliye pata kura zaidi ndiye mshindi. Tuwe na utaratibu wa kura za siri na tubadilishe utaratibu wa kura za mlolongo mwakahuu wa elfu mbili na mbili. Haki za kimusingi; masharti kuhusu kiKatiba ya kimsingi haitoshi. Haki za jamii kiuchumi, kiafya,kielimu, utamaduni---(interjection)Sasa, haki za makundi yanayo weza kudhuriwa; haki za wanawake zipewe kikao mbele maana wame udhurika miaka mingi.Haki za ardhi; jamii mahali pale, inafaa imiliki ardhi ya mahali pale. Haki ya wanajamii tafauti za kitamaduni na kikabila. Mimindio mimi najichukulia kwamba ni mtu wa kikundi maalum cha jamii ambacho masilahi yangu yanapaswa kulindwa na Katiba.Divorce; Mali yote tuliochuma na yule mume igawanywe sawa. Mali ya family, yaani family property; Majina ya bibi nabwana yaandikwe yote pamoja katika mali ile yote. Maternity leave; Maternity leave iwe miezi mitatu bila kufanya kazi.Domestic violence; Serikali ichukue hatua kwa baba aliempiga bibi yake. Walemavu; Walemavu waangaliwe maanahawakupenda kuwa hivyo. Ulawiti, ama sodomy; Mtu atakaye mlawiti mtoto chini ya miaka kumi na nne afungwemaisha-miaka kumi na tano kuenda juu; afungwe miaka kumi na tano kuenda juu. Mbuga za wanyama wa pori; Ranch ziwegame reserve ili wananchi wafaidike. Ikiwa haitawezekana, asilimia arubaini ingie kwa wilaya----(inaudible).

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!