Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Energiewende ya Ujerumani | 27

© Paul Langrock

Hifadhi ya hewa iliyobanwa ni chaguo lingine la kuhifadhi nishati

kwa muda mrefu zaidi. Inatumia nishati isiyotumika kubana hewa

kwenye nafasi chini ya ardhi kama mapangoni katika makuba ya

chumvi. Ikihitajika, hewa iliyobanwa inaendesha jenereta, hivyo

kuzalisha umeme.

Kugeuza nishati kuwa katika hali ya gesi ni njia mpya ya kuhifadhi

nishati kwa muda mrefu. Mbinu hii inatumia mchakato wa

elektrolisisi mbapo umeme hugeuzwa kutoka katika hali ya nishati

endelevu kuwa haidrojeni au gesi asili sanisi. Manufaa ya mbinu hii

ni kuwa haidrojeni na gesi asili zinaweza kuhifadhiwa, kutumiwa

mara moja au kusambazwa kwenye gridi ya gesi ya asili. Gesi hizi ni

rahisi kusafirisha na zinaweza kutumika kwa njia nyingi. Viwanda

vya nishati vinaweza kuzirejesha kuwa umeme na joto kama

inavyohitajika, na watumiaji wanaweza kuzitumia kupika, kupasha

joto au kuendesha gari.

Lakini mifumo mingi ya kuhifadhi nishati bado ni ghali mno, kwa

hivyo Serikali ya Ujerumani inarahisisha utafiti na maendeleo

kwenye suala hili. Katika mwaka wa 2011, serikali ilizindua

mkakati wa kuwekeza kwenye hifadhi. Tangu mwaka wa 2013, pia

imekuwa ikiwekeza kwenye mifumo midogo anuwai ya kuhifadhi

inayohusiana na fotovolti (PV). Kurekebisha upungufu mdogo kwa

haraka kwenye gridi ya umeme ni njia mpya ya kutumia betri.

Uzinduzi kwenye soko wa mifumo hii ya betri utaendeleza utafiti na

ubunifu na kupunguza gharama.

Hata hivyo, wataalamu wanasema matumizi ya mifumo mipya ya

kuhifadhi mwanzoni yatakuwa machache. Gharama nafuu za mifumo

ya teknolojia zote za kuhifadhi zitapatikana tu baadaye wakati nishati

endelevu zitakapo kuwa sehemu kubwa ya uzalishaji nishati. Katika

muda mfupi au muda wa kati, machaguo mengineyo ndiyo afadhali kwa

kuwa ni nafuu zaidi. Machaguo haya yanajumuisha upanuzi wa gridi au

kudhibiti uzalishaji na matumizi ili kutumia nishati kwa ufanisi.

Kugeuza umeme kuwa gesi

Kwa kutumia elektrolisisi na kutengeneza methani; matumizi yanayoweza kutokea

Uzalishaji wa kupindukia

wa nishati endelevu

ELEKTROLISISI

KUTENGENEZA METHANI

H 2

CH 4

H 2

H 2

Mtandao wa gesi asili

Mifumo ya kuhifadhi gesi

Matumizi ya viwanda Usafiri

Uzalishaji umeme Utoaji joto

Miradi 15 ya majaribio inayoendelea; miradi 6 inayojengwa au iliyopangwa

2014

Ujerumani ilibadilisha Sheria ya Vyanzo Endelevu vya Nishati. Sheria sasa inajumuisha malengo ya ukuzaji wa kila mwaka na inalazimisha ushirikiano

kwa soko. Umoja wa Ulaya ulikubaliana kuhusu malengo ya nishati na tabianchi kufikia mwaka wa 2030: kupunguza viwango vya gesijoto kwa asilimia

40, kuongeza kiwango cha nishati endelevu kuwa angalau asilimia 27 na kupunguza matumizi ya nishati kwa angalau asilimia 27. Ujerumani ilipitisha

Mpango wa Utendakazi wa Taifa wa Ufanisi wa Nishati na ilizindua Mpango wa Utendakazi wa Tabianchi wa 2020. Zikiwa na kiwango cha asilimia 27.4

katika uzalishaji wa umeme, nishati endelevu zakuwa chanzo muhimu zaidi cha nishati nchini Ujerumani kwa mara ya kwanza.