08.06.2013 Views

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Wewe

Maisha Yako

Ndoto Zako

Kitabu cha Vijana balehe

Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako:

Kitabu cha Vijana Balehe

Catherine Watson na Ellen Brazier

i

© Ubora wa Afya kwa Familia Duniani, 2009.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO Shukurani

Taasisi za kujitolea zinaruhusiwa kutumia kitabu hiki kwa kutoa nakala au nukuu lakini

hawaruhusiwi kuuza nakala hizo. Ubora wa Afya kwa Familia Duniani wangependa kuona

wanatajwa kwenye nukuu au nakala hizo kama wamiliki wa kitabu hiki.

Kwa kupata nakala zaidi kitabu cha Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako: Kitabu cha Vijana Balehe,

tafadhali wasiliana na wafuatao:

Family Care International-Kenya

Anwani: S.L.P 45763

00200 Nairobi, Kenya

Simu:. (254-20) 4443167

Simu ya upepo: (254-20) 4443204

Barua pepe: fcikenya@fcimail.org

Tovuti: www.familycareintl.org

Family Care International

588 Broadway,Suite 503

New York,NY 10012

Simu:. (1-212) 941-5300

Simu ya upepo: (1-212) 941-5563

Barua pepe: fcipubs@familycareintl.org

Kitabu cha Wewe, Maisha Yako, ndoto Zako ni tafsiri ya “You, Your life, Your Dreams”

kilichoandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na shirika la “Family Care International”

lenye Makao Makuu Mjini New York, nchini Marekani kwa kushirikiana na shirika la “Straight

Talk Foundation” la Uganda. Toleo la awali kabisa liliandikwa na catharine Watson Mkurugenzi

Mhariri wa “Straight Talk Foundation” kwa kushirikiana na ellen brazier ambaye wakati huo

alikuwa Mkurugenzi wa Programu ya Afrika ya Mashariki katika Shirika la Ubora wa Afya kwa

Familia Duniani.

Tafsiri ya kitabu hiki iliwezeshwa kwa msaada wa shirika la “Tanzania German Programme to

Support Health” (tGPSh) kupitia “Reproductive Health Component (Repro/GTZ)”. Kupiga chapa

kitabu hiki kuliwezeshwa kwa msaada wa Richard and Rhoda Goldman Fund. Japo uratibu wa

kutafsiri kitabu hiki ulifanywa na bi Rehema l. Mwateba, aliyekuwa mratibu wa Shirika la Ubora

wa Afya Kwa Familia Duniani; watu wengi walishirikishwa. Shirika la “Family Care International”

kwa kupitia ofisi yake ya Ubora wa Afya kwa Familia Duniani Tanzania linawashukuru wafuatao

kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha tafsiri hii:-

Kwanza kabisa Shirika la Ubora wa Afya kwa Familia Duniani linawashukuru wafuatao kwa

kufanya tafsri na kupitia maandishi na michoro ya kitabu hiki:-

Bi. Margreth Mtafya Kilembe kwa kufanya tafsiri kutoka lugha ya Kiingereza kuwa Kiswahili.

Bi. Benadicta Maganga kwa kupitia muswada kwa mara ya kwanza.

Bwana Michael Kadege kwa kupitia muswada kwa mara ya pili.

Bwana Abdalla Athumani Mhagama kwa kuratibu shughuli za mapitio ya wasomaji

mbalimbali na kutupatia maoni ya wasomaji.

Bwana Sunnny Kiluvia na Bwana Elikunda Matteru kwa kupitia muswada baada ya wasomaji.

Kwa kuwa si rahisi kumtaja kila mtu aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika uandishi wa

kitabu hiki, shirika linapenda kuwashukuru walioshiriki kuratibu shughuli za wasomaji sehemu

mbalimbali nchini Tanzania:-

Bi. Lucy Ikamba aliyewaratibu wasomaji wa mradi huko Mbeya Vijijini.

Bi. Catherine Ndawi aliyewaratibu wasomaji, Mbeya Manispaa.

Bwana Ole Sepere aliyewaratibu wasomaji, wilaya ya Pangani.

Bi. Emiliana Malambugi aliyeratibu upatikanaji wa maoni ya wasomaji kutoka kwa viongozi

wa madhehebu ya dini.

Bwana Benard Msami aliyewaratibu wasomaji, walimu wa shule za msingi - Turiani, Morogoro

Vijijini.

Bwana Dickson Reginald Ituwe kwa utaalamu wake wa kupanga maandishi katika kompyuta.

Bwana Juma Lugendwa kwa kuchora upya picha zilizoombwa kurudiwa na wasomaji.

Bwana Stanley Matteru na Richard Ndago kwa mchango wao katika utawala.

Bi. Margret Mbede na Bi. Dawa Mhagama kwa mchango wao katika uchapaji.

ii

iii

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO Utanguzi

Shukurani za pekee kwa Bi Cordula Schuemer kwa utetezi kwa vijana na kuhakikisha kuwa vijana

wanapata taarifa sahihi kuhusu masuala ya jinsia na afya ya uzazi.

Kwa kuwa Kitabu hiki ni tafsiri ya kitabu “You, Your life, Your Dreams”, shirika la Ubora wa Afya

kwa Familia Duniani (FCI) lingependa kuwashukuru wale wote waliohusika katika uchapishaji

wa kitabu hiki kwa lugha ya kingereza.Hii inatia ndani udhamini wa shirika la Ford Foundation,

European Commission, William and Flora Hewlette Foundation, John D.and Catherine T.

MacArthur Foundation na Blanchette Hooker Rockefeller Charitable Fund.

FCI ingependa pia kuwashukuru Adolescent Reproductive Health Education Project; CEDPA;

FAWE, Hesperian Foundation na United Nations haswa UNICEF kwa matumizi ya picha zao. FCI

inawapa shukrani Regina C. Faul-Doyle, Timothy Kiwala, Mashet Ndhlovu, ODIA na Philip Odida

kwa michoro yao.

Sehemu mbalimbali za kitabu “You, Your life, Your Dreams”, zilipata mchango kutoka kwa Eva

Agutti, Grace Canada, Claire Mcminn, Edith Mukisa, Dr. Sarah Naikoba na Joy Oguttu. Maandishi,

mifano na michoro ilichambuliwa na Dr. A. Ananie Arkutu, FRCOG, Ghana; Regina Goergen, GTZ,

Tanzania; Muriithi Kinyua, Family Planning Private Sector, Kenya; Dr. Margaret Makumi,Ministry

of Health, Kenya; Dr. Elizabeth Odera, Malezi Preparatory School, Kenya; Rehema Mwateba,

Independent Consultant, Tanzania na Mary Waithaka, Nairobi Primary School, Kenya.

Msaada katika kufanya majaribio ulitolewa na wawakilishi kutoka Ministry of Health Ghana;

Family Planning Association of Kenya;Planned Parenthood Association of Ghana; Young

Christian Women’s Association, Ghana. Shukrani pia kwa wawakilishi kutoka Kenya Association

of Professional Counsellors; Kuleana Centre for Child Rights, Tanzania; Mathare Youth Sports

Association, Kenya; Media Trust for Development, Zimbabwe; Naguru Teenage Health Centre,

Uganda; The New Vision, Uganda na Trendsetters Newspaper, Zambia kwa kuwanukuu vijana

balehe.

FCI inawapa shukrani wafanyakazi wake wote kwa mchango wao mbalimbali katika kufanikisha

uchapishaji wa kitabu ‘Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako’ kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili.

Kubalehe ni kipindi katika maisha ya wanadamu ambapo kijana anabadilika na kuwa mtu mzima.

Kipindi hiki kina msisimko mkubwa, lakini pia ni kipindi chenye kuchanganya sana. Wakati wa

kubalehe utaona mabadiliko mengi ya kimwili na kihisia, pia unaweza kuwa na maswali mengi

kuhusu mwili wako na uhusiano wako na wengine.

Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili ya vijana balehe, ambao wana umri kati ya miaka 14 na 19 ili

kiwasaidie kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokea wakati wa mabadiliko kutoka utoto

kwenda utu uzima.Kitabu hiki kinatoa taarifa sahihi kuhusu mabadiliko yanayotokea katika

kipindi cha balehe, pamoja na mambo mengine, kwa mfano: jinsi ya kuwa na afya njema ya kimwili

na kihisia, kuepuka magonjwa yanayosababishwa na ngono zisizotakiwa, jinsi ya kupambana

na misukumo ya kufanya ngono, na jinsi ya kujiepusha na matumizi mabaya ya vileo na dawa za

kulevya. Pia, kitabu kinatoa ushauri kuhusu uhusiano mwema na wazazi, marafiki, wapenzi, jinsi

ya kuweka malengo ya maisha, mbinu za kufaulu shuleni na maishani na jinsi ya kukabili vikwazo.

Kitabu hiki kina taarifa nyingi lakini si lazima usome kurasa zote. Unaweza kuangalia katika

sehemu inayoonyesha “Yaliyomo” na kuona mada zinazokupendeza zaidi. Ukizimaliza,

unaweza kurudi tena kwenye “Yaliyomo” na kuchagua tena mada inayokuvutia. Pia, unaweza

kufunuafunua tu kitabu na kuangalia sehemu zenye michoro, katuni na nukuu mbalimbali toka

kwa vijana. Unaweza pia kuangalia sehemu maalumu zilizo na kichwa “je, Wafahamu”. Hizi

zinatoa taarifa sahihi kuhusu mambo mbalimbali.

Ingawa kitabu hiki kilikusudiwa zaidi kwa vijana ambao hawajaoa/kuolewa wenye umri wa miaka

14 hadi 19, zipo pia sehemu za kitabu hiki zinazowafaa vijana wenye umri uliozidi na hata walio

kwenye ndoa. Kisome kitabu hiki pamoja na marafiki zako, kaka na dada zako na wazazi wako.

Ongea nao na jaribu kuona wao wanazichukuliaje mada zilizomo kwenye kitabu hiki.

Furahia kitabu hiki na uwe salama!

Molly Anyango

Mshauri rika wa Vijana

Family Planning Association of Kenya

iv

v

Watu wazima wengi hudhani kuwa vijana hawana sababu ya kuwa na wasiwasi wala matatizo. Hata

hivyo, balehe ni kipindi cha kuchanganya na kufadhaisha. Maswali na dukuduku nyingi hutokea

wakati huu wa mabadiliko ya mwili na hisia. Pia, vijana hujiuliza maswali yanayohusu elimu, ajira

na uhusiano kwa marafiki na wazazi. Kipindi cha kubalehe kinaambatana na misukumo toka kwa

marafiki. Vijana huwa na wasiwasi kuhusu maisha yao ya baadaye.

Lakini kubalehe ni hatua muhimu na inayosisimua. Ni kipindi ambacho kijana hukua kimwili, kihisia

na kiakili. Pia, kijana huanza kupata majukumu na kuwa na ndoto kuhusu maisha ya baadaye. Vijana

balehe hujifunza kufanya uamuzi binafsi ambao huweza kubadili maisha yao ya leo, kesho na miaka

mingi ijayo.

Wakati wa kubalehe, kijana anahitaji taarifa sahihi ili zimsaidie kufanya uamuzi wenye nguvu na

usalama. Wazazi, walimu na watu wazima wengine hupata wasiwasi kuhusu uamuzi waufanyao vijana

wao unaohusu uhusiano, ngono,dawa za kulevya na vileo au kupanga maisha ya baadaye.

Hata hivyo, utafiti unaonyesha kuwa vijana wanaweza kupanga mambo yao kwa busara kama wakiwa

na taarifa sahihi pamoja na mbinu mbalimbali za maisha kama vile uwezo wa kufanya uamuzi,

mawasiliano, maelewano, wakisaidiwa na miongozo toka kwa watu wazima.

Kitabu cha “Wewe, Maisha Yako, Ndoto Zako” kinachambua masuala mbalimbali yanayowakuta

vijana balehe katika Bara la Afrika. Yaliyomo humu yameandaliwa kwa kuwashirikisha vijana

wenyewe toka nchi mbalimbali. Kitabu kimebobea katika masuala ambayo vijana wenyewe waliyaona

yana umuhimu: Kuingia utu uzima, kutunza afya, kukabili mifadhaiko, kuelewana na wazazi, kujenga

uhusiano wa kirafiki na kimapenzi, kukabili mifadhaiko na kuvunjika moyo, afya njema ya ujinsia,

kupata mimba, kutoa mimba, kukabili matumizi mabaya ya dawa za kulevya na vileo, masuala ya

elimu na ajira.

Zipo sababu mwafaka za kutaka kuhakikisha vijana wetu wanazo taarifa sahihi kuhusu masuala

haya. Vijana wanakumbana na mambo mengi yanayoongeza changamoto na uwezekano wao wa

kudhurika, ikiwa majumbani, mitaani, shuleni na hata kwenye vyombo vya habari. Leo hii, kijana ana

uwezekano wa kupata matatizo mengi ya kiafya kama vile magonjwa ya zinaa, VVU/UKIMWI, mimba

zisizotakiwa na utoaji mimba usio salama. Kiasi cha asilimia 60 ya maambukizi mapya ya VVU katika

Bara la Afrika yanatokea kwa vijana wa miaka 10 hadi 24. Hii ina maana kuwa vijana wanaambukizwa

VVU kwa kasi zaidi kuliko kundi lolote lingine.

Kijana aliyeko kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa VVU ni yule asiye na taarifa sahihi. Kijana wa aina

hii anategemea zaidi kupata taarifa toka kwa marafiki, video au filamu na muziki wa kizazi kipya,

taarifa ambazo kwa kiwango kikubwa huwa si sahihi. Kwa hiyo, kitabu hiki kimekusudia kuhakikisha

vijana balehe wanapata taarifa sahihi na wanajijengea uwezo wa kukabili misukumo ya kutenda

yasiyofaa, kujenga uhusiano wenye faida na la muhimu zaidi; kuwawezesha vijana wafanye uamuzi

salama na wa busara.

Napenda kuwasisitiza wazazi, walimu na watu wazima wengine wasome kitabu hiki na

wawashirikishe vijana wao na wengineo. Aidha, nawasisitiza watu wazima waongee na vijana kuhusu

taarifa zilizomo na wawashauri vijana inavyopasa. Watu wazima wawasaidie vijana kuwa salama

katika kipindi cha mabadiliko kuingia utu uzima ili waweze kutimiza ndoto zao maishani.

Dr. A. Ananie Arkutu

Kwa Wazazi, Walimu, na Watu wazima wengine

Yaliyomo

ShuKuRani ................................................................................................................................................................... ii

utanGuliZi ....................................................................................................................................................................iv

Kwa Wazazi, Walimu, na Watu wazima wengine ..................................... ....................................................... ......... v

SuRa Ya 1: ujana balehe: baDiliKO KubWa, chanGaMOtO KubWa ....................................................... 1

Nini maana ya ujana balehe? ...................................................................................................................................................... 2

Ukweli kuhusu maisha ..................................................................................................................................................................4

Maadili.......................................................................................................................................... ................................................ ......5

Stadi za maisha................................................................................................................... ............................................................6

SuRa Ya 2: MabaDiliKO Ya MWili............................................................................. ............................................9

Mfoko wa ukuaji: mwanzo wa balehe.............................................................................. ........................................................9

Vichocheo (Homoni).............................................................................................................. .......................................................12

Via vya uzazi - Sehemu za siri............................................................................................ .......................................................13

Nywele za mwilini na mabadiliko ya ngozi....................................................................... .....................................................13

Uwezo wa kufikiri..................................................................................................................... ........................................... .........14

SuRa Ya 3: WaVulana........................................................................................................ .............................. .......17

Umbo na ukubwa wa mwili...................................................................................................... ...................................................17

Sauti yako................................................................................................................................... .............................................. ......18

Via vyako vya uzazi (Sehemu zako za siri)........................................................................ .................................... ...............19

Mazoezi ya usafi...................................................................................................................... ......................................................21

Kudinda kwa uume................................................................................................................... ....................................................22

Kumwaga manii “kukojoa”...................................................................................................... ....................................................23

Ndoto nyevu (“Kutoa manii/ Shahawa ukiwa usingizini”)........................................... ............................ .......................24

SuRa Ya 4: WaSichana.................................................................................................... ............................. ..........27

Maumbile na ukubwa wa mwili............................................................................................ ...................................... ..............27

Matiti yako................................................................................................................................ ............................................. .........27

Sidiria......................................................................................................................................... .......................................................31

Via vya uzazi ( Sehemu zako za siri )............................................................................ ...........................................................31

Kufanya usafi wa mwili vizuri................................................................................. ..................................................................33

Hedhi na mzunguko wa hedhi................................................................................ ...................................................................35

Kutunza kalenda............................................................................................................ ........................................... ...................39

Hedhi inavyokosesha raha........................................................................................ ....................................... ........................40

Ngono na hedhi................................................................................................................. ............................................. ................41

Kujisikia vizuri/ Afya na usafi ................................................................................... ..................................... ........................41

Utatumia nini kujihifadhi na hedhi.............................................................................. .................................... .......................42

SuRa Ya 5: MaMbO Ya MSinGi KatiKa KutunZa MWili........................... ....................... ...........................45

Jiweke safi, nukia vizuri................................................................................................... ......................................... .................45

Utunzaji wa meno yako..................................................................................................... ......................................... ................46

Chunusi.............................................................................................................................................................................................47

Utunzaji nywele................................................................................................................. ........................................... ................48

Lishe nzuri.............................................................................................................................. .............................................. ..........49

Mazoezi.................................................................................................................................. ...........................................................51

Mapumziko mazuri............................................................................................................ ...........................................................53

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO SURA YA 1 | UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA

SuRa Ya 6: utunZaj i aFYa Ya aKili na MOYO............................ ..................................................................55

Kujiheshimu..................................................................................................................... ...............................................................55

Kujiamini............................................................................................................................ ............................................. ................58

Usiwe na wasiwasi, furahi........................................................................................ ...................................... ..........................60

Kukabili huzuni.......................................................................................................... ........................................... ........................63

Kuishi vizuri na watu................................................................................................ ........................................ ...........................64

SuRa Ya 7: ueleWanO na WaZaZi WaKO................................................. .......................... ...............................71

Kuthamini familia...................................................................................................... ......................................... ..........................72

Fahamu yale wazazi wako wanayoyataka........................................................ ................................. ..................................72

Kukidhi matarajio ya wazazi wako...................................................................... ..................................... ...............................74

Mawasiliano na wazazi wako................................................................................ ...................................... .............................74

Vyanzo vingine vya kupata msaada................................................................... ....................................................................78

SuRa Ya 8: uRaFiKi na MaPenZi................................................................... ......................................................81

Urafiki.......................................................................................................................... .............................................. .......................81

Jinsi ya kumtambua mtu ambaye si rafiki wa kweli................................... ............................. .........................................83

Kuelewana na jinsi nyingine................................................................................ ...................................... ...............................84

Kuanza uhusiano na mtu unayempenda ........................................................ ................................... ...................................85

Kujenga uhusiano wa kweli ............................................................................... ........................................................................87

Mapenzi.................................................................................................................... ............................................ ..........................88

Kupumbazika....................................................................................................................................................... ..........................90

Kuachana kimapenzi............................................................................................. .......................................... .............................91

SuRa Ya 9: ujinSia na nGOnO..................................................................... ........................... ..............................93

Ujinsia wenye afya njema...................................................................................... ....................................... ...........................94

Hisia za kijinsia........................................................................................................ ........................................... ..........................96

Punyeto...................................................................................................................... ............................................. ........................96

Ubikira........................................................................................................................... ............................................. .....................98

Kujamiiana..................................................................................................................... ................................................................101

Kuweka kiwango cha kujamiiana........................................................................... ................................................................102

Uamuzi wa kutofanya ngono.................................................................................... ..................................... ........................104

Kuzungumza na mwenzi wako kuhusu ngono......................................................................................... ..........................104

SuRa Ya 10: KutunZa aFYa YaKO Ya KiujinSia ...................................... ....................... ...........................109

Magonjwa ya zinaa....................................................................................................... ......................................... ....................109

Utajuaje kama umepata maambukizi ya magonjwa ya zinaa?......................... .............................................................111

Kwenda kuchunguzwa magonjwa ya zinaa............................................................... ...........................................................112

VVU / UKIMWI....................................................................................................................... .......................................................114

Utajuaje kama una VVU.............................................................................................................................................................116

Kuishi kwa matumaini na VVU....................................................................................... .........................................................118

Ngono salama / Mapenzi salama................................................................................... .......................................................120

Kondomu................................................................................................................................. ........................................................121

Matatizo mengine ya afya ya uzazi............................................................................... .......................................................124

SuRa Ya 11: MiMba na uZuiaji Wa MiMba .................................................... ..................................................129

Mimba inatokeaje?........................................................................................................... .........................................................129

Dalili za mimba.................................................................................................................. ..........................................................130

Hatari za mimba na uzazi kwa wasichana balehe.................................................. ..........................................................131

Kustahimili mimba katika umri mdogo...................................................................... ................................. ........................132

Kujitunza wakati wa ujauzito..................................................................................................................................................134

Mimba na VVU..................................................................................................................... ........................................................134

Maandalizi ya kujifungua................................................................................................ ....................................... ..................135

Kujitunza na kumtunza mtoto baada ya kujifungua............................................. ..........................................................136

Kuharibika mimba............................................................................................................ ..........................................................136

Namna ya kuepuka kupata mimba.............................................................................. .........................................................138

Je vidonge vya kuzuia mimba ni salama?................................................................... ........................................................139

Kuzuia mimba kwa dharura.............................................................................................. .......................................................139

Kinga mara mbili............................................................................................................... ..........................................................141

SuRa Ya 12: nGOnO Ya KulaZiMiShWa na nGOnO bila Ya RiDhaa YaKO..... ....................................145

Shinikizo kutoka kwa rafiki wa kiume au wa kike............................................................ ...............................................145

Shinikizo kutoka kwa watu wazima............................................................................... .................................. ...................146

Unyanyasaji kijinsia............................................................................................................ ........................................ ..............148

Kudhalilisha kijinsia.......................................................................................................... .........................................................150

Ubakaji.................................................................................................................................. .........................................................150

Kitu cha kufanya ubakaji ukitokea.............................................................................. .........................................................154

SuRa Ya 13: MatuMiZi MabaYa Ya DaWa.......................................................... .......................... ...................157

Aina ya dawa na vitu ambavyo vinatumika vibaya................................................ ............................. ............................157

Sigara na pombe.............................................................................................................. ...........................................................159

Kutawaliwa na dawa.......................................................................................................... .........................................................161

Kwa nini watu wanaanza kutumia dawa...................................................................... ........................................................163

Namna ya kushughulikia shinikizo la kutumia dawa.............................................. ............................ ...........................166

Kuacha dawa................................................................................................................................................................... ............168

SuRa Ya 14: KutiMiZa nDOtO ZaKO...................................................................... ............................................171

Kuzitambua ndoto zako............................................................................................................................................ ................172

Mipango ya baadaye kuhusu kazi.................................................................................. ..................................... ..................173

Kuweka malengo.................................................................................................................... ........................................... ..........174

Kufanya uamuzi mzuri (wa busara)................................................................................ ..................................... ..................176

Zingatia bila kuyumba katika malengo na ndoto zako........................................... ............................ ...........................178

Kufanya vizuri katika masomo shuleni........................................................................ .................................. .....................179

Kuacha shule........................................................................................................................ .........................................................181

Kutatua vipingamizi............................................................................................................ ......................................................182

FahaRaSa .................................................................................................................... ........................................ .......187

MaRejeleO...................................................................................................................... ............................................193

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ujana Balehe:

Badiliko Kubwa,

Changamoto Kubwa

Patric, kutoka Kenya(umri,miaka 16)

“Nilichokifurahia katika ujana balehe wangu ni kuwajibika katika majukumu

ya nyumbani hasa wazazi wanapokuwa hawapo. Majukumau haya

nayapenda kwasababu ninadhani nimeshakua na ninaweza kujidhibiti mimi

mwenyewe na wadogo zangu”.

naana, kutoka Ghana. (umri; miaka 17)

“Yapo mambo mengi yanayomhusu kijana balehe ambayo siyapendi. Ninakumbuka

nilipokiwa na umri mdogo nilikuwa na uhuru zaidi kuliko sasa.

Lakini kwa sasa zipo sheria na miongozo mingi.”

Watu wengi duniani wanatafsiri “ujana balehe”

kama kipindi cha maisha kati ya miaka 10 na 19.

Kama una umri wa miaka kati ya 10 na 19, basi

wewe ni kijana balehe. Hongera! Wewe ni mtu

muhimu sasa.

Ni kweli kuwa kwa muda wote uliopita umekuwa

mtu muhimu, lakini kwa sasa hivi umekuwa

mtu muhimu zaidi. Unapitia mabadiliko mengi

sana na unajaribu mambo mengine mapya,

kutoka mwonekano mpya,kujitambua kupya

kama vile kuandamana na marafiki wa jinsi

tofauti,kushikana mikono na kubusiana.

Wazazi wako wanaweza kukuta ujana balehe wako

unautumia vibaya.

1

SURA YA 1

2

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mwonekano wako mpya na kujitambua kwako kunawafanya wazazi, shangazi zako na wajomba

kuwa na wasiwasi kwa sababu wasingependa upate matatizo na wala wasingependa ufanye

makosa makubwa kama vile kupata mimba (au kwa kumpa mimba rafiki wa kike) wakati ungali

unasoma. Zaidi ya yote wanakuwa na wasiwasi kwa sababu wanafahamu kwamba umri kati ya 10-

19 unaweza kuwa na athari kubwa katika ukuaji wako na aina ya maisha utakayokuwa nayo.

nini Maana Ya ujana balehe?

• Ujana balehe ni kipindi ambacho unabadilika na kukua kimwili na kiakili kutoka utoto na

kuingia utu uzima. Wakati wa ujana balehe mambo yafuatayo hutokea:

• Mwili wako utabadilika kwa jinsi unavyopenda uwe au wakati mwingine hata usivyopenda

uwe.

• Utaanza kupata hisia za kutaka kujamiiana, na unaweza usijue ufanye nini baada ya kupata

hisia hizo.

• Utaanza kufikiri bila ya kumtegemea mtu mwingine na kutaka kufanya maamuzi peke yako.

• Hisia zako kuhusu familia na mahusiano yako na wazazi, yanaweza kubadilika kwa uzuri

au kwa ubaya. Wazazi wanaweza kukupa majukumu zaidi ambayo ni dalili nzuri kwamba

wanakuamini na kukutegemea. Lakini wanaweza vilevile wakaanza kuwa wakali hata

kutokuruhusu ukutane na marafiki zako. Wakati mwingine watajaribu kufanya maamuzi

kuhusu masomo na mustakabali wa maisha yako ya baadaye. Wanaweza wakaonyesha

kuwa na upendo mdogo kwako kuliko walivyokuwa huko nyuma na unaweza vilevile usipate

mahusiano yenye upendo kama ulivyokuwa ukiwa mtoto.

• Marafiki zako, na hata yale wanayofikiria, vinaweza kuwa vya muhimu zaidi kuliko ilivyokuwa

awali.

• Hisia zako zinaweza kuwa na utata zaidi kuliko ulivyozoea na wakati mwingine wewe

mwenyewe unaweza usifahamu hasa kile unachohisi au ni kwa nini unahisi hivyo.

• Kwa hakika unaweza kuhisi kutaka kupendwa au kuwa karibu na mtu mwingine.

• Unaweza kukumbana na maamuzi mazito na zinaweza kuwepo nyakati ambapo hujui umtake

nani ushauri.

Ujana balehe ni kipindi maalum kwa kila mtu, kote duniani – mashariki au magharibi,kaskazini

au kusini.Lakini pia ni kipindi chenye changamoto. Hiki ni kipindi cha mabadiliko makubwa, na

mabadiliko makubwa huchukua muda. Utakutana na mambo mengi ya kuyafanyia maamuzi

unapopitia ujana balehe na maamuzi mengine utakayofanya yatadumu nawe katika maisha yako

yote.

Yapo mambo mengi sana ambayo unaweza kuyafanya ili kupitia salama ujana balehe. Hivyo

ni vema uelewe mwili wako na mabadiliko yanayotokea .Ni vema ujielewe na pia uelewe kile

unachokitaka katika maisha. Tumia muda kufikiria maisha yako ya baadaye na kupanga

yatakuwaje. Utu uzima una majukumu makubwa hivyo basi ni lazima kujiandaa vema wakati wa

ujana balehe.

Wakati wa ujana usiwe mpweke na kufanya mambo peke yako. Umezungukwa na watu

wanaoshughulikia matatizo muhimu kila siku. Unao ndugu wengi, kama akina shangazi, wajomba,

binamu na wengi wengineo, amabao unaweza kuwaomba ushauri. Pia kwa vile wewe ni sehemu ya

jamii, zipo mila na desturi nyingi ambazo mafunzo yake yanaweza kukusaidia.

SURA YA 1 | UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA

Mahali pengi ujana umekuwa mgumu kueleweka, na hasa siku hizi vijana wanapata matatizo

ambayo wazazi wao, mabibi hata babu zao hawakuwahi kuyapitia; matatizo hayo ni:

Msukumo wa kutaka kujamiiana.

Madawa ya kulevya shuleni na kwenye jamii.

Wazazi ambao kwa sababu ya shughuli nyingi hawana muda au wanaona aibu kuzungumza

kuhusu mabadiliko yanayowatokea watoto wao.

Magonjwa yaambukizwayo kwa kujamiiana ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI.

Kuwa yatima kwa sababu ya UKIMWI au ajali.

Vita au kuyumba kisiasa kwa nchi.

Ili kuyamudu yote haya na kupitia kipindi cha ujana balehe salama unahitaji kuwa jasiri , mbunifu,

mtafutaji na mwenye kujipa matumaini. Jaribu kujifunza kutoka kwa watu wanaokuzunguka

ambao ni jasiri na watulivu wakati unapokutana na matatizo. Kila wakati jione kuwa utashinda

matatizo yako kama walivyoweza wengine.

Vijana huFiKiRia KWaMba haKuna janGa linalOWeZa KuWaPata

Ni tabia ya vijana duniani kote, katika nchi tajiri na maskini – kufikiria kwamba mambo mabaya

hayawezi kuwatokea. Hujiambia,

“ Haitatokea kwangu”. Wakati mwingine hujiamini sana

na kuhisi wako salama mno.

Je wewe uko hivi? Unadhani unaweza kujaribu kitu cha hatari

na lisikupate jambo? Kwa mfano, wewe na rafiki yako wa kike

(msichana) mnafahamu kuhusu dawa za kuzuia mimba. Lakini

mnadhani kwamba ili mradi hamjamiiani mara kwa mara,

msichana hawezi akapata mimba.

Au unaweza ukawa na ufahamu mkubwa kuhusu

VVU, virusi vinavyo sababisha UKIMWI. Unaweza

ukafahamu kwamba maambukizi yanaweza

kutokea kwa njia ya kujamiiana bila kinga,

lakini unafikiri kwamba rafiki yako wa kiume

hawezi kuwa na maambukizo. Unakataa kufikiri

kuwa unaweza kupata maambukizo ya VVU na

haiwezekani pia kwa wale watu unaowafahamu

kupata ugonjwa huo.

je haya yanakuhusu? Kama ndivyo, hapa kuna

mambo ambayo unahitaji kuyazingatia:

Vijana wengi hujiingiza kwenye vitendo vya

hatari wakidhani kuwa hawatadhurika....

3

4

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mimba inaweza ikatungwa utakapojamiiana kwa mara ya kwanza bila kinga.

Kusema kweli, kila watu wawili wanapojamiiana bila kinga kuna uwezekano wa 1:12 mimba

kutungwa. Maana yake ni kwamba iwapo mtajamiiana bila kinga mara moja kwa mwezi, mnaweza

kukumbwa na mimba isiyotarajiwa.

...mimba huweza tungwa hata kamaumejamiiana

mara moja.inaweza kutungwa utakapojamiiana

kwa mara ya kwanza.

Ili kupita kipindi cha ujana salama unahitaji angalau mambo matatu:

Ukweli Kuhusu Maisha

Kumbuka pia kwamba maambukizi ya VVU

hutokea kwa vijana pia, na hutokea kwa vijana

zaidi kuliko hata kwa wengine. Vijana wanapata

maambukizo ya VVU haraka zaidi kuliko kundi

lingine lolote Afrika. Maambukizi mapya kwa

watu kumi,watu sita huwa ni vijana.

Usiruhusu ukawa mmojawapo kati ya

vijana wenye mimba zisizotakiwa au wenye

maambukizi mapya ya VVU. Soma kitabu hiki

kwa uangalifu ili ujue jinsi unavyoweza kufanya

maamuzi mazuri, ili uwe salama na mwenye afya.

Tafadhali washirikishe marafiki zako kusoma

kitabu hiki ili nao pia wajifunze jinsi ya kuchagua

yale yaliyo mema.

Maadili – Unahitaji kujua yale unayoamini ni ya kweli ili uweze kufanya maamuzi unayoweza

kuishi nayo.

Stadi za maisha, ili utumie ukweli unaoujua na kubakia mkweli ndani ya maadili yako.

uKWeli KuhuSu MaiSha

Nini maana ya “hali halisi/mambo ya ukweli”? Ukweli kuhusu maisha ni upi?

Ukweli ni taarifa zote muhimu za mambo unayotakiwa kuyafahamu ili kuyamudu maisha ya kila

siku na kufanya maamuzi mazuri.

Kufahamu ukweli maana yake ni kufahamu jinsi ya kujitunza mwenyewe – kimwili na kifikra – kwa

kula vizuri; kutunza mwili vizuri; na kutunza vizuri afya ya akili na maono yako. Kufahamu ukweli

vile vile maana yake ni kufahamu jinsi mimba inavyotokea, jinsi VVU/UKIMWI na magonjwa

mengine yatokanayo na kujamiiana yanavyosambaa na jinsi unavyoweza kuzuia usiambukizwe.

Ukweli ni kufahamu ni kwa namna gani madawa ya kulevya na pombe vinaweza kuudhuru mwili na

ubongo na jinsi maisha yako yanavyoweza kuharibika. Ukweli ni kufahamu njia nzuri za kumudu

hali ngumu na matatizo yako, ili uweze kufanikisha ndoto zako.

La muhimu zaidi, kufahamu ukweli ni kubainisha kati ya yaliyo ya ukweli na yaliyo ya uongo. Ni

muhimu sana kujua mambo ya ukweli wakati unapojaribu kuchagua. Chagua lililo la muhimu na

amua la kufanya.

SURA YA 1 | UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA

Unahitaji mambo ya ukweli ili uwe salama. Kitabu hiki kimejaa ukweli, hivyo kitakupa ukweli

kuhusu:

Mabadiliko yanayotokea mwilini mwako (Sura ya 2,3, na 4).

Kutunza afya yako ya kimwili na kimaono (Sura ya 5 na 6).

Mahusiano na watu wengine (wazazi, marafiki wa kike na marafiki wa kiume)

(Sura ya 7 na 8 ).

Ujinsia, ngono, na kutunza afya ya ujinsia.(Sura ya 9 na 10).

Mimba na madawa ya kuzuia mimba (Sura ya 11).

Kulazimishwa na kujamiiana (Sura ya 12).

Madawa ya kulevya na pombe.(Sura ya 13).

Kupanga maisha yako ya baadaye na kufikia malengo yako.(Sura ya 14).

MaaDili

Neno maadili lina maana ya mambo unayoyaamini, unayoyathamini na tabia unazodhani ni

muhimu

katika maisha yako. Maadili mema ni kama yafuatayo:

Kuwa mkweli.

Uwazi.

Uvumilivu.

Ukarimu.

Hisani/Wema.

Kusamehe.

Yaliyotajwa hapa juu ni machache tu kati ya maadili mema, waweza kuwa na mengine; kwa mfano

kusoma kwa bidii, kusaidia wazazi, uaminifu kwa rafiki zako, kujitolea kwenye shughuli za jamii

yako au za kidini.

Maadili yanasaidia kuongoza matendo na maamuzi yako. Yanakusaidia katika kuchagua yaliyo

mema kwako na kwa wengine. Kwa mfano, kijana mkarimu na mvumilivu atamsadia mwanafunzi

mwenzie mlemavu au jirani yake aliyefanyiwa mabaya na watu wengine. Mtu mwaminifu

atachagua kurudisha pesa za muuza duka alizomzidishia wakati akimpa chenji.

Je, una maadili gani? Kipi ni kitu muhimu na chenye thamani kwako? Unaamini katika misingi gani

ya maisha? Unaposoma kitabu hiki, jaribu kujiuliza kuhusu maadili yako.

Kufahamu maadili yako kutakusaidia kufanya maamuzi makini ili uwe salama wakati wote wa

mabadiliko ya ujana balehe.

5

6

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ukijua unachokithamini itakusaidia kuwa mkweli kwako binafsi, hata wakati mtu mwingine

anapokulazimisha kufanya kitendo unachodhani ni makosa. Maadili yako yatakusaidia kuchagua

lililojema kwako; ambalo wakati mwingine, baada ya kuchagua, itabidi uishi nalo daima.

StaDi Za MaiSha

Unahitaji stadi za maisha pia ili uwe salama. Kusema kweli

“Stadi za maisha” zinaweza kuwa stadi za kuokoa maisha,

kama vile uwezo wa :-

Kuelezea hisia zako. Hisia zako ni muhimu, lakini watu

wengine hawawezi kujua unavyojisikia mpaka uwaeleze.

Jifunze jinsi ya kuwafanya watu wengine wajue kile

unachofikiri na unachokitaka kwa kusema moja kwa

moja na kutumia sentensi zinazoanzia na “mimi” – “mimi

ninataka” “mimi ningelipenda” “mimi ninahitaji”“mimi

Sipendi” ………… .” Fanya mazoezi ya kutumia sentensi

zinazoanza na

“mimi” mpaka utakapozoea na kujisikia huru kuzitumia.

tetea hoja yako. Una uhuru wa kufikiri na kujihisi

unavyopenda. Ni vema kujifunza jinsi ya kuwasilisha

mawazo yako kwa wengine bila ya kuwaudhi au kuwafanya

wajisikie vibaya, usionyeshe uadui, ugomvi wala kukosoa

sana.

tetea unachoamini bila kujali wanayosema watu wengine.

Kila mtu ana imani na yaliyo sahihi na yasiyo sahihi, mazuri

na mabaya. Imani hizi zinaitwa kanuni. Wakati mwingine

unaweza ukawa unajua kanuni zako lakini mambo yanaweza

yasiwe wazi sana kiasi cha kukufanya utumie muda

kufikiria lipi ni sahihi kwako na ni kwa nini.

Iwapo unao uhakika wa usahihi wa kile unachofikiria na kwa

nini unakifanya, na kwa nini hupendelei kukifanya utaweza

kusimama imara na lile unaloamini. Hivyo basi msimamo

wa namna hii utakupa heshima mbele za watu.

jihadhari na yanayotokana na shinikizo.

Kuwa na msimamo wa pekee ndiyo

stadi za Maisha.

Jinsi unavyoelekea kwenye utu uzima unatakiwa kufanya maamuzi mengi peke yako. Wakati

mwingine watu wengine wanaweza kukuhimiza na kukusukuma kufanya maamuzi fulani na

ukushawishika kufanya hivyo.

Lakini ufahamu kuwa kufanya maamuzi mazuri maana yake ni kupima chaguo zote zilizopo na

kufikiria matokeo kwa kila chaguo.Inaweza ikawa kazi ngumu iwapo kuna mtu anakuharakisha au

anakushinikiza uamue haraka. Kitu muhimu katika kufanya maamuzi bora ni kuwa na uhakika wa

kanuni zako na malengo yako ya maisha kwa ujumla.

SURA YA 1 | UJANA BALEHE: BADILIKO KUBWA CHANGAMOTO KUBWA

Jambo lingine la muhimu katika kufanya

maamuzi ni kujipa muda wa kutosha.

Kumbuka,unaweza kumueleza mtu kwamba

“ninahitaji kufikiria zaidi kuhusu jambo hili na

nisubiri nitakujibu”

Stadi hizi za maisha zina majina yake, kama

vile “kuongea bila woga wala jazba”

“Mawazo yenye ubunifu” “Kutatua matatizo”,

“Kufanya maamuzi” na“Kujitambua”.

Stadi za maisha ni muhimu sana. Ukweli ni

kwamba stadi za maisha ni muhimu kama

ilivyo kuufahamu “ukweli.” Kuufahamu “ukweli

wa mambo” peke yake hakuwezi kukulinda

hadi uwe pia na stadi za maisha. Kwa mfano

unaweza ukafahamu kwamba kujamiiana bila

kinga kunaweza kukusababisha mimba na

magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU/

UKIMWI. Vilevile unaweza ukawa umeamua

kwamba hutaki kujamiiana, lakini bado ukawa

huna uwezo wa kujieleza na kutetea hoja zako

kwa rafiki yako wa kiume.

Unahitaji Stadi za maisha ili uutumie

ukweli unaoufahamu kusimama imara

katika yale unayoyataka na kuyaamini,

hasa pale inapotokea watu unaowajali na

kuwaheshimuwanatofautiana na wewe.

je, unazo Stadi za maisha? Unaweza

ukasimama imara na kuwa na msimamo kwa

yale unayoyaamini kuwa ni sahihi hata kama

marafiki zako wanawaza tofauti? Unao ujasiri

wa kutosha kutetea afya yako au maisha

yako? Anza kuzitumia stadi zako kadri

unavyoendelea kusoma kitabu hiki.

Kufanya maamuzi mazuri na kusimama imara kwa

unachokiamini ni stadi bora za maisha

7

8

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mabadiliko ya mwili

Wasichana na wavulana wengi wanabalehe kati ya umri wa miaka 10 na 16. Balehe ni kipindi

ambacho unabadilika kimwili, kihisia/kifikra na kiakili kutoka utoto na kuingia utu uzima.

MFOKO Wa uKuaji: MWanZO Wa balehe.

Ipo tofauti ndogo sana kimaumbile kati ya wasichana na wavulana kati ya miaka 9 na 10.

Japokuwa via vyao vya uzazi ni tofauti lakini vifua vyao na misuli vinafanana.

Tofauti kubwa ya kimwili kati ya wasichana na wavulana huanza kujitokeza kipindi cha balehe.

Kwa wastani wasichana wanaanza kuonyesha mabadiliko makubwa ya ukuaji kimwili kati ya umri

wa miaka 10 au 11. Kipindi hiki cha kukua haraka kinaitwa mfoko wa ukuaji. Kwa wasichana kipindi

hiki cha mfoko wa ukuaji hudumu miaka mitatu. Wakati huu wasichana wanakuwa warefu na

wakubwa zaidi ukilinganisha na wavulana wa umri huo huo.

Wavulana wanachelewa kidogo kufikia mfoko wa ukuaji kuliko wasichana, kwa wastani katika

umri wa miaka 12 au 13. Kwa wavulana; mfoko wa ukuaji hudumu muda mrefu kuliko wasichana,

ukweli ni kwamba wavulana wengine huendelea kukua mpaka wanapofikia miaka 19 au 20.

Lakini kumbuka kwamba miaka hii ya ukuaji ni ya wastani tu.

Vijana wengine huanza mfoko wa ukuaji mapema zaidi na wengine

huchelewa. Kuanza mapema au kuchelewa hakuna athari yoyote

katika namna utavyorefuka au namna utakavyokua haraka.Wale

wanaoanza mapema, wengine wanakua haraka wakati wengine

wanakuwa taratibu. Vile vile kwa wale wanaochelewa kuanza

wengine wanakua haraka na wengine taratibu.

Katika kipindi hiki cha makuzi ya haraka, mara nyingi wavulana

na wasichana wanajisikia hovyo. Hii ni kwa sababu sehemu mbali

mbali za mwili hukua kwa wakati tofauti na kwa kiwango tofauti.

Mara nyingi, viganja vya mikono na nyayo huongezeka kwanza

ikifuatiwa na mikono, miguu, kiuno/nyonga na kifua. Vijana

wengi wanaokua haraka hujikuta mara nyingine wakiteguka na

kuanguka. Inashangaza kujiona umeongezeka sentimeta kadhaa

ghafla!

Mfoko wa ukuaji

Mfoko wa ukuaji

9

SURA YA 2

10

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Wavulana na wasichana wengine hukua haraka sana wakati wa balehe kiasi cha kwamba ngozi

yao inashindwa kustahimili ukuaji haraka wa mifupa. Wakati mwingine inapotokea hivyo alama

za misitari hutokea kwenye ngozi. Alama hizi zinaweza kupotea au zisionekane kiurahisi mtu

anavyoendelea kukua, lakini zinaweza zisipotee moja kwa moja.

Hata kama unajiona kukua haraka,bado balehe ni kitendo

cha taratibu mno. Itachukua muda mrefu kabla hujawa

mtu mzima kimwili na kifikra. Kwa wakati huu yafuatayo ni

mambo ya kuzingatia.

Kila Mtu YuKO tOFauti

Kila mtu hufikia balehe kwa wakati tofauti na kwa kiwango

tofauti. Matiti yako yanaweza kuchelewa kukua kuliko ya

rafiki zako lakini wewe unaweza ukavunja ungo mapema

au unaweza kuyapata yote haya baadaye sana. Matiti

yanaweza yakakua na ukavunja ungo akiwa na umri wa

miaka 12 na wewe matiti yanaweza kukua na ukavunja ungo

ukiwa na umri wa miaka 15.

Au kama wewe ni mvulana unaweza ukawa na rafiki yako

ambaye sauti yake ili badilika kuwa nzito akiwa na umri wa

miaka 13. Anaweza akawa ameota mavuzi na misuli wakati

wewe hujakua hata sentimeta moja!

Wavulana hawa wote wana umri wa miaka

13,lakini wanakua kitofauti

Wasichana hawa wote wana umri wa

miaka 13,lakini wanakua kitofauti

Kumbuka kila mtu yuko tofauti na kila yanapokutokea mabadiliko huu ndio wakati muafaka

kwako.

Kila Mtu ana MabaDiliKO YaKe

Kwa kutumia kigezo cha afya, haitegemei kama mwili

wako unakua haraka au taratibu kuliko rika lako.

Mwili wako utabadilika muda utakapofikia. Hakuna

unachoweza kufanya kuhusu muda wa mabadiliko.

Wasichana na wavulana wengine wenye afya nzuri

huchelewa kukua kuliko wenzao wa rika moja.

Wasichana na wavulana wengine wanakua mapema

kuliko wenzao wa rika moja na wala hawana kasoro

yoyote na wana afya nzuri pia.

Lakini hata hivyo unaweza kupata matatizo kama

utakuwa tofauti na wengine.Kwa mfano: inaweza kuwa

vigumu kwa msichana kuwa wa kwanza kuwa na matiti

darasani, au mvulana kuwa wa mwisho kubadilika sauti.

Hii inaweza kusababisha kutaniwa na unaweza kujisikia

upo tofauti sana na kundi rika lako.

SURA YA 2 | MABADILIKO YA MWILI

Sherifan, kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Nilianza kuona mabadiliko katika mwili wangu nikiwa na miaka 11. Matiti

yalianza kuota, nywele zikaota kwapani na kwenye via vya uzazi. Nilijisikia

vibaya sana kwa sababu nilipata mabadiliko haya mapema sana na

nilijiona niko tofauti sana na wenzangu wa rika moja”

Sherry, kutoka Ghana (umri wa miaka 19)

“Nilikuwa darasa la sita(6), sifahamu kama marafiki zangu walikuwa

wanachelewa kukua au mimi nilikuwa nimewahi kukua, lakini nilijisikia

vibaya matiti yalipoanza kukua. Niliwahi kumsikia mama akisema jinsi

walivyokuwa wakitumia tapoli, “kifaa kidogo cha ubao kilichotumika kusaga

pilipili”, kujaribu kuondoa uvimbe kwenye matiti wakati wa enzi zao.

Kwa hiyo nilijaribu, kama mara tatu hivi. Lilikuwa ni jambo la kuchekesha,

lakini hata hivyo haikusaidia kitu. Lakini sasa hivi waliokuwa wananitania

wana matiti makubwa kuliko ya kwangu.”

Kumbuka kuwa mambo haya yanaisha kadri muda unavyopita. Utakapofikisha miaka 20

hakutakuwa na tofauti yoyote kwako au kwa mtu mwingine, iwapo sauti yako ilibadilika ukiwa na

miaka 13 au miaka 17. Hakutakuwa na tofauti iwapo ulivunja ungo ukiwa na miaka 11 au miaka 16.

Sherry, kutoka Ghana (umri; miaka 19)

“Ebu tuyaache mambo yaende kama yalivyopangwa kwani hata kama

hupendi huwezi kubadili kitu isipokuwa kujikubali tu.”

Ingawa huwezi kuubadili mwili wako yapo mambo yanayokuhusu ambayo unaweza

kuyabadili:

1. Unaweza kuhakikisha kuwa wewe ni mtu mzuri. Hakikisha kuwa unafanya kazi kwa

bidiii katika lolote utakalokuwa unafanya (shuleni, kazini na nyumbani). Unaweza

ukakuza haiba yako, ucheshi wako,pia na tabia yako. Angalia kuwa wewe ni nani na

unataka uweje baadaye na wala sio vile unavyoonekana.

2. Jitahidi sana kutotilia maanani utani jaribu kupuuza na usiwaruhusu wanaokutania

waone umefadhaika. Mwishowe watachoka kukutania.

3. Heshima na kukubalika na rafiki zako visije vikakushawishi kufanya mambo ambayo

sio mazuri kwako. Usiruhusu marafiki zako kukulazimisha kufanya mambo ambayo

unajua sio sahihi, kama vile kutania watu wengine, kutumia madawa ya kulevya au

kujiingiza kwenye mambo yanayoweza kukudhuru.

4. Jielimishe mwenyewe kwa kutafuta taarifa sahihi. Hakihisha unafahamu wapi utapata

taarifa unazozihitaji na majibu ya maswali yako yote wakati unapoupitia ujana

11

12

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Pia, weka akilini haya: Watu wa umri wako mara nyingi wanajua taarifa nyingi za uongo kuliko za

ukweli hasa inapokuwa ni za kuelezea balehe na kujamiiana. Marafiki zako wanaweza kukueleza

mambo ambayo si ya kweli, hivyo unahitaji kufahamu wapi uende ili kupata ukweli. Kwa mfano,

unaweza kuambiwa kwamba, matiti au uume utakua iwapo utajamiiana. Au unaweza kutaniwa

kwamba matiti yako ni makubwa kwa sababu umekwishajamiiana. Hali kadhalika unaweza

kusikia kwamba chunusi ni dalili za kwamba unatakiwa ujamiiane. Lakini hakuna lolote katika

haya lenye ukweli. Yote ni uzushi/uwongo.

Uzushi kama huu unaweza kuleta hatari zaidi kwa sababu unaongeza hofu. Uzushi kama huu

unakufanya ufikirie kwamba unaweza kufanya mambo ili kubadilisha yale ambayo huwezi

kuyadhibiti.

VichOcheO (hOMOni)

Ni kitu gani hudhibiti mabadiliko ndani ya mwili wako? Ni kitu gani hufanya ukue haraka au

taratibu? Ni kitu gani hukufanya uongezeke?

Mwili wako wakati wote unatengeneza homoni, ambazo ni kemikali tarishi maalumu ambayo

huuambia mwili namna gani na lini ubadilike na kukua. Mfoko wa ukuaji wako husababishwa na

homoni za ukuaji ambazo zinatoka kwenye ubongo kwa wingi.

Pamoja na homoni za ukuaji, homoni za jinsi nazo huanza kutolewa wakati wa balehe. Kwa

wasichana homoni za jinsia zinatengenezwa ndani ya ovari na kwa wavulana zainatengenezwa

ndani ya korodani. Homoni za jinsi ndizo zinazosababisha tofauti katika maumbile ya mwanaume

na mwanamke. Wasichana wanapoingia kipindi cha balehe nyonga zao huongezeka. Kawaida

nyonga hukua haraka kuliko kifua . Nyonga ya msichana hupanuka na kujiviringa, na kiuno

huonekana kidogo na chembamba. Matiti vilevile huanza kukua.

Kwa wavulana, homoni za jinsia husababisha kifua kupanuka, mikono na miguu inakuwa minene

yenye misuli. Matiti ya wavulana hayabadiliki sana kama ya wasichana yanavyobadilika wakati

wa balehe, lakini hubadilika kidogo. Kwa wavulana wengine, matiti yao hukua kipindi cha balehe

lakini kawaida hupotea kadri muda unavyokwenda.

Homoni huathiri pia hisia zako. Vijana wengi hujisikia kuwa na hisia kali. Dakika moja tu anaweza

kuwa na furaha na msisimko, lakini dakika inayofuata akawa na huzuni karibia kulia. Anaweza

kujisikia vizuri siku moja na vibaya siku inayofuata. Mabadiliko haya katika hisia yanaitwa “hisia

za kuyumba”.

Kipindi cha balehe huwa kina ambatana na hisia kali

SURA YA 2 | MABADILIKO YA MWILI

Jambo hili huwatokea vijana wengi mara kwa mara. Wakati wa ujana balehe, utengenezaji wa

homoni huongezeka ghafla, kitendo ambacho huwafanya vijana wengi wawe na hisia kali za aina

mbalimbali.

Baadaye katika maisha utengenezaji wa homoni utapungua na utajisikia unao uwezo wa kudhibiti

hisia.

Weka akilini kwamba mabadiliko yote ya kimwili, kihisia na kiakili yanayotokea wakati wa balehe

yanasababishwa na homoni zinazotengenezwa na mwili wako. Hakuna unaloweza kufanya

kuharakisha au kuchelewesha utengenezaji wa homoni. Jaribu kukumbuka tu kwamba wewe ni wa

pekee na huna kasoro yoyote.

Via VYa uZaZi “SeheMu Za SiRi”

Pamoja na kuleta mabadiliko katika umbo la mvulana na msichana, homoni hufanya via vya

uzazi kukua. Via vya uzazi maana yake ni zile sehemu za siri za mwili wako ambazo mara nyingi

zinafunikwa na chupi/nguo za ndani.

Kabla hujawa kijana balehe, sehemu za siri zilikuwa kwa ajili ya kujisaidia tu (kukojoa). Wakati wa

ujana balehe hata hivyo, sehemu za siri zinakuwa kubwa. Kwa wasichana ngozi na tishu huwa laini

na yenye mafuta mafuta, kwa wavulana uume huanza kurefuka na kunenepa. Korodani vilevile

hukua na kuanza kutengeneza mbegu za kiume.

Kipindi cha balehe via vya uzazi huanza kutengeneza majimaji pia.

Wavulana huanza kutengeneza shahawa, majimaji yaliyo kama kamasi ambayo mbegu za kiume

huogelea. Shahawa hutoka nje ya uume wakati mvulana anapofikia mshindo. Wasichana vilevile

hutoa majimaji ya ukeni na damu ya hedhi. (soma sura ya 3 na ya 4 kwa maelezo zaidi kuhusu

wavulana na wasichana)

nYWele Za MWilini na MabaDiliKO Ya nGOZi

Ngozi yako na nywele za mwilini hubadilika vilevile katika kipindi cha balehe. Kwa vijana wengi

ngozi inakuwa na mafuta. Ngozi ya utotoni hupotea. Hii hupelekea chunusi kutoka, jambo ambalo

ni tatizo la kawaida kwa vijana wengi (soma sura ya 5 kwa maelezo zaidi kuhusu utunzaji mzuri

wa ngozi).

Dalili nyingine ya balehe ni nywele kuota sehemu mpya za mwili. Wavulana na wasichana wote

wanaweza kuota nywele kidogo miguuni na mikononi. Kwa kuongezea wavulana huota nywele

sehemu za siri, usoni kifuani na kwapani. Wasichana vilevile huota nywele sehemu za siri na

kwapani.

Nywele zinazoota sehemu za siri zinaitwa mavuzi, watu wengine wana mavuzi mengi na wengine

wanayo kidogo. Mavuzi husaidia kufanya eneo la via vya uzazi liwe safi, jambo ambalo ni zuri

sana kwani ngozi inayozunguka via vya uzazi ni laini/nyororo sana na ni rahisi kuumia.Mavuzi

husaidia kuzuia jasho na vitu vingine kutoka kwenye ngozi laini ya via vya uzazi.

13

14

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Vijana wengine hawafurahii nywele mpya zinazoota mwilini hasa mavuzi yanapotokea kwa mara

ya kwanza.

Kumbuka ya kwamba mavuzi ni kitu cha asili na yana kazi yake, kwa hiyo iwapo unayo mengi au

kidogo usihofu sana.

Vilevile, nywele huota kwapani kipindi cha balehe, ingawa mara nyingi ni wakati wa mwisho

wa kipindi cha balehe. Wasichana wengi hawaoti nywele kwapani mpaka baada ya matiti

kuanza kuota na baada ya kuvunja ungo. Kwa wavulana nywele za kwapani kwa kawaida huanza

kujitokeza mwaka mmoja au zaidi baada ya mavuzi kuota. Kama mavuzi, nywele za kwapani

zina kazi maalum.Wakati wa balehe jasho linatoka sana na nywele husaidia kuzuia jasho lisitoke

kwenye ngozi.

Kwa kawaida,kwa wavulana, nywele za usoni huwa za mwisho kuota. Huanza kuota pembeni mwa

midomo ya juu. Nywele zinazoota juu ya midomo ya juu (masharubu) huendelea kuota, na zingine

huota sehemu ya juu ya kidevu na chini kidogo katikati ya midomo ya chini na mwisho zingine

huota kwenye kidevu. Nywele hazioti kidevuni mpaka via vya uzazi vya mvulana viwe vimekomaa

kabisa. Kwa wavulana wengi, nywele za usoni huanza kuota hasa wakiwa na umri kati ya miaka 14

na 18.Lakini zinaweza kuanza kuota mapema zaidi au zikachelewa.

uWeZO Wa KuFiKiRi

balay, kutoka Kenya (umri, miaka 16)

“Nilistushwa! Sikujua kama mtu anaweza kuota nywele

sehemu zake za siri. Nilidhani ninaumwa, na nikamwuliza

mama ambaye alinihakikishia kwamba ilikuwa ni jambo la

kawaida.”

Diana, kutoka Zambia (umri, miaka 17)

“Zilipoota, nilijisemesha mwenyewe kwamba itabidi

nikubaliane na hali halisi”

Doglas, kutoka Zimbabwe (umri miaka 12)

“Yalipoota mavuzi haikunifurahisha yalinifanya nionekane

mbaya”

bernard, kutoka Kenya (umri, miaka 17)

“Marafiki zangu walinicheka ati kwa sababu mavuzi yalikuwa

hayajaota.”

Wakati mabadiliko dhahiri yanayotokea katika mwili kipindi cha balehe, akili nayo pia hubadilika

bila ya kutambulika kiurahisi.Katika kipindi cha ujana balehe, uwezo wa akili unaongezeka sana

hasa katika kufikiri kwa makini na kutoa maoni ya kina. Matokeo ya mabadiliko haya husababisha

utambulisho binafsi kuanza kujengeka.Unaanza kujiona kama mtu wa kipekee. Unapenda kufikiri

mwenyewe na kufanya maamuzi yako binafsi.

SURA YA 2 | MABADILIKO YA MWILI

Mara nyingi, kwa mara ya kwanza utayaona mambo tofauti na wazazi wako wanavyoyaona.

Unaweza kujisikia kutaka kujua imani za wazazi wako na sababu zake. Unaweza kutaka kujaribu

kuishi maisha yako mwenyewe kuliko kutegemea ya kuambiwa na wengine. Unaweza kujaribu

mambo mapya mwenyewe na wakati mwingine kujaribu mambo ya hatari.

Mabadiliko yote haya ya akili ni dalili nzuri za kuonyesha kwamba unaingia utu uzima.

Hata hivyo haina maana ya kwamba tayari umeishakuwa mtu mzima. Ingawa uwezo wako

wa kiakili unaongezeka sana, bado kuna mambo mengi unakuwa hujayajua. Ukweli hutaweza

kuyajua yote, kwa hiyo ni muhimu kujua wapi uende na umwone nani kwa ajili ya taarifa

unayoihitaji. Kutakuwepo wakati ambapo itakuwa muhimu kutumia uzoefu na maarifa kutoka

kwa waliokuzidi umri. Hivyo basi unatakiwa kuuliza maswali, usidhani unayo majibu yote. Jitahidi

kujifunza mengi iwezekanavyo.

Vijana wengine hutaniwa wanapokuwa wameota mavuzi au wanapokosa kuota.

15

16

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 2

MabaDiliKO KatiKa MWili WaKO

Ujana, ambao kawaida huanzia umri kati ya miaka 10 na 16 ni mabadiliko ya hatua kutoka

utoto kuingia utu uzima. Kila mtu anaanza kubadilika wakati wake. Wakati watu wengine

hukua haraka zaidi, wengine hukua taratibu. Tunatofautiana, na hakuna unaloweza kufanya

kuthibiti muda wa mabadiliko hayo.

Ni yapi uyategemee unapobadilika kutoka msichana na kuwa mwanamke au kutoka

mvulana na kuwa mwanaume?

Mfoko wa ukuaji; viganja, nyayo, miguu, mikono, nyonga kifua vyote vitaongezeka

ukubwa mwili utatengeneza homoni, kemikali maalumu ambazo hutoa ujumbe namna

mwili utakavyokua na kubadilika.

Via vya uzazi (au sehemu za siri) vitakuwa vikubwa na vitaanza kutengeneza majimaji

(giligili).

Ngozi inaweza kuwa na mafuta zaidi.

Utaanza kuota mavuzi na nywele kidogo kwapani, miguuni, mikononi na kama ni

mvulana, usoni pia.

Utaanza kupata hisia nzito mbali mbali.

Uwezo wa kufikiri utaongezeka.

Bila ya kujali mabadiliko yanatokea haraka au taratibu, wakati gani yanaanza, jaribu

kukumbuka kwamba mabadiliko haya ni ya kawaida na hayana kasoro yoyote.

Inaweza kuchukua muda mrefu kuyazoea mabadiliko haya kwa hiyo kuwa mvumilivu na

usihofu.

Wavulana

Katika sura ya pili umesoma baadhi ya mabadiliko kadhaa ambayo wavulana wanayapata katika

kipindi cha balehe. Sura hii itakupa maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya.

uMbO na uKubWa Wa MWili

Mfoko wa ukuaji kwa wavulana wengi unaanza kati ya miaka 12 na 13. Hata hivyo wavulana

wengine wanaanza ukuaji mapema zaidi na wengine wanachelewa. Wakati wa mfoko wa ukuaji,

mwili wako utaanza kuwa mrefu zaidi na mkubwa.

Sehemu mojawapo ya mwili wako itakayoanza kukua ni miguu. Ukweli ni kwamba, mifupa ya

miguu inakua haraka zaidi kuliko sehemu zingine za mwili. Hivyo basi miguu inaweza kukua hadi

mwisho kabla ya sehemu zingine kukua sana. Iwapo utajisikia kama vile unakuwa mzito ghafla,

inawezekana ni kwa sababu ya miguu yako imekuwa mikubwa kuliko ilivyokuwa muda mfupi

uliopita. Unatakiwa kuwa mvumilivu kwani hali hii inaweza kukuchukua muda kabla hujaizoea

Mifupa mingine ya mwili nayo itakuwa zaidi kuliko mingine na kusababisha umbo la mwili

kubadilika. Kwa mfano, mabega yatakua zaidi wakati nyonga inaweza kukua kidogo tu. Nyonga

yako inaweza kuonekana nyembamba ukilinganisha na upana wa mabega. Inawezekana miguu na

mikono ikakua zaidi kuliko uti wa mgongo, hivyo basi miguu inaweza kuwa mirefu ukilinganisha

na kifua au kiwiliwili. Matokeo yake umbo lako litakuwa tofauti sana na lile la mvulana mdogo.

Misuli vile vile inakuwa, hasa ile ya miguuni na mikononi. Kadri misuli inavyokua, ndivyo

unavyokuwa na nguvu zaidi. Mlundikano wa misuli na mafuta utasababisha kifua kuwa kikubwa.

Vile vile wavulana wengi hugundua kwamba kuna mabadiliko ya chuchu na matiti katika kipindi

cha balehe. Chuchu huongezeka na kuwa kubwa kidogo. Miduara inayozinguka chuchu nayo huwa

mikubwa na rangi yake kuwa nyeusi kidogo.

Wavulana wengine wanajikuta matiti yao yamevimba na yanauma. Kwa wachache, uvimbe

huzidi, hivyo kuwasababishia wasiwasi kuwa wataota matiti makubwa kama wanawake. Usiwe

na wasiwasi, haya ni mambo ya kawaida uvimbe na ulaini unasababishwa na homoni ndani ya

mwili. Uvimbe unaweza ukadumu mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu, lakini baada ya hapo

hupungua kwa vile mwili unaacha kutengeneza homoni nyingi.

Wakati wa mabadiliko yote haya unatakiwa kuwa mvumilivu kwani mwili wako hauna matatizo

yoyote, na wewe ni wa kawaida kabisa. Hata kama hukui haraka ukilinganisha na rafiki zako

wanavyokua, usiwe na wasiwasi utakua tu, muda bado. Ni wakati gani unaanza kukua na kiasi

gani utakua,inategemea sifa bainifu unazorithi kutoka kwa wazazi wako. Hata ukichelewa

17

SURA YA 3

18

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

kuanza kukua, unaweza kujikuta wewe ni mrefu kuliko wavulana wengine waliopata msukumo wa

ukuaji mapema.

Sauti YaKO

Sauti yako ni dalili nyingine ya uhakika kwamba unaingia kipindi cha balehe. Sauti huanza

kubadilika baada ya mfoko wa ukuaji kuanza, kwa kawaida ni katika umri wa miaka 14 au 15.

Sauti ya wavulana hubadilika kuwa ya chini na nzito katika kipindi cha balehe, kwa sababu ya

homoni inayoitwa “testosterone”.Aina hii ya homoni husababisha zoloto (sehemu ya mwanzo wa

koromeo inayohusika na utoaji wa sauti) kuwa kubwa. Kwa jinsi nyuzi za sauti zinavyokuwa nene

na ndefu ndivyo sauti inavyokuwa ya chini na nzito.

Precious, mvulana kutoka Ghana (umri, miaka 15 )

“Kitu cha kwanza nilichogundua ni kukatika kwa sauti, kupanuka kifua

na mabega. Nilifurahi kwa sababu niliona kwamba sasa ninakuwa

kijana balehe.”

Panaito, kutoka Kenya.

“Nilipata mabadiliko ya sauti mara baada ya kupata ndoto nyevu.”

aloysious kutoka uganda (umri, miaka 19)

“Sauti yangu ilipobadilika nikiwa na umri wa miaka 15. Nilitambua kuwa

nilikuwa ninakua. Nilikua haraka sana na nilifurahi.”

Dalili ya kwanza kuonyesha kwamba sauti yako inabadilika ni kuanza kukwaruza kwa sauti

ghafla. Wavulana wengine hujisikia vibaya sauti zao zinapoanza kukwaruza, kwa vile mara nyingi

haitabiliki itaanza lini.

Sauti huwa ya kawaida na kubadilika katika muda mfupi. Mara inakuwa ya kawaida, dakika

chache baadaye inakuwa ya juu na nyembamba.

SURA YA 3 | WAvULANA

Via VYaKO VYa uZaZi (SeheMu ZaKO Za SiRi)

Uume umetengenezwa na misuli inayozunguka mrija mwembamba. Mrija huu hupitisha mkojo na

shahawa. Uume una kichwa na mwili.Mwili au mpini ni ile sehemu ya uume kama bomba. Kichwa

ni ile sehemu ya juu ya uume. Ni sehemu ambayo ina hisia kali na inahitaji uangalifu mkubwa.

Unapozaliwa kichwa cha uume kinakuwa kimefunikwa

na ngozi nyembamba iliyojikunja. Ngozi hii inaitwa

“govi” Jamii nyingi za Afrika huondoa govi kwa njia

ya upasuaji. Kitendo hiki kinaitwa “kutahiri”. (Angalia

ukurasa wa 20 kwa maelezo zaidi kuhusu kutahiri.)

Ukubwa wa uume unatofautiana kati ya mwanaume na

mwanaume na hauna uhusiano kabisa na ukubwa wa

mwili. Mara nyingi, jinsi uume unavyokuwa mkubwa

ukiwa laini ndivyo unavyoongezeka kidogo unapokuwa

umedinda. Vivyo hivyo, kama ni mdogo unapokuwa

laini unaweza kuongezeka zaidi unapokuwa umedinda.

Vijana wengi wa kiume, “hata wanaume wakubwa”

wanatumia muda mwingi kufikiri na kuwa na wasiwasi

kuhusu uume wao. Je ni mdogo sana? Kwa nini

umepinda kuelekea huku? Je, kuna tatizo lolote?

Sehemu za siri za mwanaume kwa ndani

aloysius kutoka uganda (umri, miaka 19)

“Wakati mwingine tulikuwa tunavuta uume na kulinganisha nani

anao mkubwa zaidi?!”

Iwapo umewahi kujishangaa kama uume wako una ukubwa wa kutosha, kumbuka tu kwamba

tendo la ngono halitegemei ukubwa wa uume. Kwa uhakika ni kwamba ukubwa wa uume hauna

athari zozote kwa mwanamke katika kufurahia tendo la kujamiiana (ngono).

Ukweli ni kwamba kufurahia ngono kwa wanawake na wanaume wengi kunategemea zaidi jinsi

gani kila mmoja wapo anavyompenda mwenzie. Kilicho cha muhimu ni mahusiano na wala sio

ukubwa wa uume.

Kinachoning’inia chini ya uume ni mapumbu. Pumbu ni kama mfuko au kifuko cha ngozi

kinachoshikilia korodani au makende, ambako mbegu za kiume hutengenezwa tangu kipindi

cha balehe hadi uzeeni. Ngozi ya mapumbu ina nywele kidogo na mafuta. Hudaka uchafu ambao

kama haukusafishwa husababisha harufu mbaya.

Katika kipindi cha utoto, mapumbu hujikunja na kuwa karibu na mwili. Lakini, kadri unapopitia

balehe, mapumbu huanza kulegea na kuning’inia chini, ingawa ukijisikia baridi au kuogopa au

kuwa na hamu ya kujamiiana, mapumbu yako yanaweza kujikunja na kurudi karibu na mwili.

Mapumbu yananing’inia chini kwa sababu korodani zinahitaji kuwa katika hali yenye joto chini ya

joto la mwili ili kutengeneza mbegu za kiume.

19

20

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Tohara ni kitendo cha kuondoa ngozi iliyojikunja inayozunguka kichwa cha uume. Ngozi hii huitwa

govi, hufunika kabisa kichwa cha uume lakini inaweza kuvutwa chini ya “mpini” (shafti).

Kufuatana na mila na desturi za waafrika, pamoja na dini fulani fulani kama vile Waislamu na

Wayahudi, watoto wanatahiriwa wakiwa na umri wa siku chache. Katika desturi nyingine za Afrika,

wavulana wanatahiriwa wanapofikia balehe, utaratibu huu unachukuliwa kama utaratibu wa mpito

kutoka utoto kwenda utu uzima.Zipo tamaduni nyingine Afrika ambazo mila haziruhusu kutahiri

kabisa.

Hakuna ubaya wowote wa kutahiri au kutokutahiriwa. Kutahiriwa ni utaratibu wa kidini au

kiutamaduni/kimila. Iwapo katika jamii yenu hawatahiri ni sawa sawa tu.

Je, kutahiri kunaleta tofauti zozote katika hisia ya kujamiiana? Ni vigumu sana kujua jambo

hili kwani kila mwanaume anayo namna yake ya kujisikia. Lililo la uhakika ni kwamba wote,

aliyetahiriwa na asiyetahiriwa wanaweza kufurahia ngono na wanaweza kuwafurahisha wapenzi

wao.

Wakati kutahiri ni utaratibu wa kidini au kimila/ kiutamaduni, watu wengine wanaamini kwamba

kuna faida za kiafya iwapo mwanaume ametahiriwa kwa sababu ni rahisi kusafisha uume wake.

Lakini zipo sababu zingine za kiafya zinazoweza kusababisha watu kutahiriwa. Wapo wavulana na

wanaume wengine ambao govi linakuwa limeshikana sana na kichwa cha uume kiasi cha kwamba

inawia vigumu kuivuta kwa chini. Hii inaweza kusababisha kuvimba kwa uume na maumivu

makali. Namna pekee ya kutatua tatizo hili ni kutahiri.Watu wengine wanafikiri kwamba kutahiri

kunasaidia kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya ngono. Ukweli ni

kwamba, hata kama umetahiriwa unaweza kupata maambukizi ya VVU/UKIMWI na magonjwa ya

ngono. Unashauriwa kufanya mapenzi salama wakati wote.

Mambo yote haya yana maana gani kwako? Kama utamaduni wako hauruhusu wavulana kutahiriwa,

Je, ungependa utahiriwe ili iwe rahisi kuuweka uume wako msafi? Jibu ni hapana unachotakiwa ni

kuwa msafi, kumbuka kusafisha kwa ungalifu chini ya govi. Kwa kawaida haya ndiyo unayotakiwa

kuyafanya. Hata hivyo wavulana ambao hawawezi kuviringisha govi na wale ambao husikia

maumivu uume unapodinda, wanashauriwa kumweleza mfanyakazi wa afya kwa ushauri zaidi.

Sasa hivi watu wengi wanatahiriwa katika vituo vya afya. Lakini sehemu nyingine wanatahiri

wataalamu wa kienyeji (mangariba) kama sehemu ya sherehe. Wakati wowote inapotokea hivyo,

inatakiwa vitumike vyombo visafi, vilivyochemshwa, ili kuua vijidudu kila baada ya kumtahiri

mtu mmoja. Ni hatari sana kutumia kisu kimoja kutahiria wavulana wengi kwa sababu kama

mmojawapo atakuwa na maambuziki ya VVU, kisu kinaweza kueneza maambukizi kwa wavulana

wengine.

Iwapo utatahiriwa kimila, hakikisha utaratibu wa kisasa unatumika ili kuzuia maambukizi ya VVU

na magonjwa mengine yanayotokana na damu. Usikubaliane kabisa na mila/desturi na utamaduni

utakaosababisha maambukizi ya VVU. Taratibu hizo zinaweza kubadilishwa ukawa salama.

Kwa mfano, watu wa Mbale, Uganda walichukua hatua zifuatazo ili kuhakikisha wanatahiri

kiusalama:

• Kila aliyetaka kutahiriwa alilazimishwa kuja na kisu chake.

• Lazima kisu kichemshwa kabla ya kutumika.

• Lazima Mangariba waoshe mikono yao kwa uangalifu kabla na baada ya kumtahiri kila mtu.

MaZOeZi Ya uSaFi

SURA YA 3 | WAvULANA

JE UNAFAHAMU KUHUSU TOHARA? Je, ulikuwa unajua kwamba kuna uzushi mwingi kuhusu uume?

Yafuatayo ni maelezo mbalimbali ya uzushi kuhusu uume:

1. Iwapo huufanyii mazoezi uume kwa kujamiiana, uume wako hautafanya kazi na utakuwa

mdogo. huu ni uongo! Kujamiana sio “mazoezi” ya uume. Uume hauhitaji mazoezi yoyote.

Utafanya kazi vizuri bila hata ya kujamiiana.Kutojamiiana au subira kamwe haviwezi

kuudhuru uume wako.

2. Uume unaongezeka ukubwa kila unapofanya ngono mara nyingi. Sio kweli! Ukubwa wa

uume wako utategemea sifa urizorithi kutoka kwa wazazi wako, na wala sio unachofanya

na uume wako.

3. Uume mdogo hauwezi kumridhisha mwanamke. Sio kweli! Ukubwa wa uume unaathari

ndogo sana kwa mwanamke kufurahia ngono. Hii ni kwa sababu hisia za kutaka kujamiiana

kwa mwanamke zipo kwenye kinembe na eneo linalozunguka uke.Uke wenyewe hauna

mishipa mingi ya fahamu kwa hiyo haujisikii sana

4. Wavulana wenye uume mdogo hawawezi kutumia kondomu. Sio kweli! kondomu

zimetengenezwa kwa jinsi ya kubana, hivyo kila mtu anaweza kuzitumia vema.

5. Lazima ujamiiane kila uume unapodinda. Si kweli! Kwa vyovyote vile hii sio kweli kabisa.

Kwa mfano utafanya nini kama uume wako ungedinda darasani? Uume utalegea wenyewe.

Kamwe huwezi kudhurika kwa kutokufanya ngono uume unapokuwa umedinda.

6. Wavulana wenye dole gumba kubwa wana uume mkubwa. Sio kweli! Watu wengi husema

mambo kama haya ikiwa ni pamoja na wavulana wenye pua kubwa, miguu mikubwa,

masikio n.k, lakini sio kweli. Hakuna mahusiano yoyote kati ya ukubwa wa uume na viungo

vingine vyovyote vya mwili wako. Hakuna jinsi unavyoweza kufahamu ukubwa wa uume

kwa kumwangalia tu.

7. Mbegu za kiume zikizidi zinasababisha mgongo kuuma, kichaa, kichwa kuuma, kuwa

hanithi na kuota chunusi. Sio kweli! Hata kama korodani zinatengeneza mamilioni ya

mbegu za kiume, haiwezekani mbegu hizo kujazana na kusababisha matatizo. Zaidi ya

hapo mbegu za kiume haziwezi kwenda sehemu nyingine ya mwili.

8. Ndoto nyevu ni dalili ya kwamba unahitaji kujamiiana. Sio kweli! Ndoto nyevu ni njia

mojawapo ya mwili kupunguza mbegu za kiume na shahawa. Sio dalili ya kwamba unahitaji

kujamiiana. Mwili wako unaweza kujirekebisha wenyewe bila ya wewe kujihatarisha kwa

vyovyote vile.

Ni muhimu kuosha na kusafisha uume wako kila siku, uwe umetahiri au la. Hii ni lazima iwe

desturi kama unavyofanya kwa sehemu nyingine za mwili wako. Unatakiwa vile vile kuosha

mapumbu, katikati ya mapumbu na mapaja na katikati ya matako.

Kama hujatahiriwa, unatakiwa kurudisha nyuma govi na kusafisha eneo hilo kwa utaratibu.

Unaweza kuhisi viuvimbe vidogo mwanzoni mwa kichwa cha uume viuvimbe hivyo ni matezi

yanayotoa majimaji meupe yanayoitwa smegma. Smegma inasaidia govi kuteleza nyuma

kiulaini. Hata hivyo, iwapo Smegma itajaa chini ya govi inaweza kusababisha harufu mbaya au

maambukizi. Ni muhimu wakati wote eneo la chini ya govi liwe ni safi .

21

22

KuDinDa KWa uuMe

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

iwapo hujatahiriwa rudisha nyuma govi na safisha taratibu chini yake.

Kwa kawaida uume ni laini na huninginia chini. Wakati unadinda, damu nyingi huelekea kwenye

uume isivyo kawaida na damu kidogo hurudi. Hii husababisha uume kuwa mkubwa na mgumu,

na kusimama. Uume uliodinda kwa kawaida hujikunja kidogo kuelekea juu, na unaweza kujikunjia

upande mmoja.

Uume unapokuwa umedinda unaweza ukashindwa kukojoa kiurahisi kwa sababu msuli hufunga

kibofu cha mkojo. Itakubidi usubiri uume ulegee ndipo ukojoe.

Uume unaweza kudinda iwapo utaguswa au kushikwa shikwa, au wakati umepata mhemuko wa

kutaka kujamiiana au kwa kumuona mtu anayekuvutia. Uume unaweza kudinda kwa sababu ya

kuwa na wasiwasi na mfadhaiko. Ni kawaida kwa wavulana kuamka asubuhi na uume uliodinda.

Ukiwa usingizini uume unaweza kudinda mara 5 mpaka 7. Hii ni kawaida kabisa na haina madhara

yoyote.

Kudinda kwa Uume kunawatokea wanaume wote wa umri mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto

wadogo na wazee. Wakati mwingine wavulana huhofu wanapodindisha mara kwa mara. Hali hii

inawasumbua wakiwa darasani, ndani ya basi au hata wakati wa matembezi. Wakati mwingine

zipo sababu za msingi za uume kudinda, kwa mfano, unaweza ukawa umekaa karibu na mtu

anayekuvutia. Hata hivyo, kuna wakati uume unadinda bila sababu yoyote ya msingi.

nfune kutoka Zambia (umri wa miaka 13)

“Kudindisha kwa uume hakuzuiliki na hutokea mara kwa mara.

Wakati mwingine ni dalili ya kuonyesha una msisimko wa

kutaka kujamiiana. Hali hii naichukia sana hasa ninapokuwa

shuleni au hadharani.”

Tafadhali usiwe na wasiwasi, wewe ni wa kawaida, mwenye afya na homoni nyingi. Unaweza

kufedheheka ikitokea darasani au hadharani, lakini wakati wote ni wewe peke yako unayefahamu

kwamba umedindisha.

Wakati mwingine wavulana wanadhani njia pekee ya kuthibiti uume kudinda ni kufanya ngono

Hii sio kweli ni uzushi ikiwa ni sababu ya wavulana kufanya ngono. Uume kudinda sio dalili ya

kwamba unahitaji kufanya ngono, la hasha.

KuMWaGa Manii “KuKOjOa”

SURA YA 3 | WAvULANA

Unapofikia balehe unaweza kuanza kuona majimaji yenye rangi ya maziwa ambayo yananata na ni

mazito, sio mepesi kama mkojo.

Majimaji kama ute hutoka kupitia kwenye uume wakati mwanaume anapofikia mshindo. Kukojoa

manii ni kilele cha msisimko wa kijinsia, wakati mwanaume anapokuwa amedindisha uume.

Kumbuka ya kwamba sio lazima kukojoa manii kila uume unapokuwa umedinda. Kama utasubiri,

uume utalegea wenyewe bila hata ya kukusababishia madhara yoyote.

Majimaji kama ute yametengenezwa na vitu viwili. Karibia 10% ya majimaji ni mamilioni ya

mbegu za kiume. Mbegu za kiume ni ndogo sana kiasi ambacho hatuwezi kuziona kwa macho

labda kwa darubini. Ukiziona zinaonekana kuwa na kichwa cha mviringo na mkia mrefu na

mwembamba.

Asilimia 90 ya ute huo ni majimaji yenye rangi ya maziwa yanayoitwa shahawa. Shahawa

huwezesha mbegu za kiume kuogelea na pia huzipa chakula na kuziwezesha kuwa hai. Shahawa

sio chakula kwa wasichana, kama watu wengine wanavyozusha.

Mbegu za kiume zinatengenezwa katika Korodani/Makende (angalia kielelezo uk 19). Shahawa,

ambazo ni majimaji yenye rangi nyeupe/maziwa zinatengenezwa kwenye vifuko vya shahawa.

Hizi ni tezi zilizopo nyuma ya kibofu cha mkojo. Mwanaume anapofikia mshindo mbegu za kiume

zinachanganyika na shahawa kutoka kifuko cha shahawa. Mchanganyiko huu huitwa manii. Manii

hupitia kwenye mirija ya kupitishia mbegu na kutoka nje ya uume kupitia kwenye tundu dogo

lililopo kwenye kichwa cha uume.

Inaweza kuonekana kana kwamba manii nyingi hutoka wakati mwanaume “anapokojoa” Ukweli

ni kwamba kiasi kinachotoka ni kama kijiko kidogo cha chai kilichojaa. Usije ukadharau uwezo

wa hiki kijiko kidogo cha chai kilichojaa manii;

kinaweza kuwa na mbegu za kiume karibia

milioni mia tano!. Kila mojawapo ya mbegu

hizo inaweza kumfanya msichana apate mimba.

Unapofikiria mbegu za kiume zipatazo milioni

mia tano, utaelewa ni kwa namna gani msichana

anavyoweza kupata mimba kirahisi.

Iwapo mvulana au mwanaume ana maambukizi

ya VVU, kijiko cha chai kimoja kilichojaa

shahawa kinaweza kuwa na mamia kwa maelfu

ya virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Mbegu ya kiume

Kijiko kidogo cha chai kilichoja shahawa kina

mamilioni ya mbegu za kiume na kinaweza kuwa na

VVu iwapo mvulana atakuwa ana maambujizi.

23

24

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Wavulana wengi wanakuwa na wasiwasi kwamba kondomu haiwezi kuhifadhi mbegu za kiume

zipatazo milioni 500. Lakini mbegu za kiume ni ndogo sana na kwa hiyo kondomu inaweza

kuzizuia zote ili mradi inavaliwa kwa usahihi (angalia sura ya 10 kwa maelezo zaidi kuhusu

kondomu).

Wavulana wengine wanakuwa na wasiwasi kwamba wakikojoa manii mara kwa mara

watapunguza kiasi cha shahawa mwilini mwao. Wasiwasi wa kwamba wanaweza kuishiwa

shahawa na hivyo kutokuwanazo za kutosha watakapozihitaji. Hili haliwezi kutokea hata mara

moja kwani mwanaume anatengeneza mbegu za kiume na shahawa tangia kipindi cha balehe

mpaka siku anayokufa.

Vilevile kumbuka ya kwamba haiwezekani mbegu za kiume na shahawa zikalundikana au

zikajenga shinikizo mwilini. Mwili wako ni kama mashine iliyokamilika, unazo njia za kuondoa

mbegu za kiume na shahawa inayozidi, mojawapo ni ndoto nyevu.

nDOtO nYeVu (“KuKOjOlea” KitanDani)

Wakati mwingine wavulana wanakojoa manii

kitandani wakiwa usingizini.Kitendo hiki kinaitwa

“ndoto nyevu” wavulana wengi wanapopata ndoto

nyevu huwa inakuwa ni mara yao ya kwanza shahawa

kutoka mwilini mwao. Wanaweza kuamka na kukuta

doa bichi kitandani au kwenye nguo.

Kama hufahamu lolote kuhusu ndoto nyevu unaweza

kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi. Unaweza

kufikiri umekojoa kitandani au damu inakutoka au

unaumwa, lakini utaona kwamba majimaji yana rangi

ya maziwa/meupe, na sio kama damu au mkojo.

ndoto nyevu kwa mara ya Kwanza

Ndoto nyevu hutokea usingizini tu. Ukisinzia kidogo mchana unaweza kupata ndoto nyevu, lakini

wavulana wengi hupata ndoto nyevu usiku wakiwa usingizini. Wavulana wengi wanapojikuta

wamekojoa manii huwa wanakumbuka kwamba walikuwa wanaota ndoto zinazohusiana na

mapenzi. Lakini unaweza kupata ndoto nyevu hata kama hujaota ndoto za mapenzi.

Karibu wavulana wengi wanafedheheka wakipata ndoto nyevu. Ni sahihi kufedheheka, lakini

kumbuka ya kwamba ndoto nyevu ni za kawaida wakati wa ujana balehe. Vijana balehe wengi

wanapata ndoto nyevu ingawa sio wote.

Mvulana hawezi kujizuia kupata ndoto nyevu; ni za asili na ni za kawaida. Ni njia ambayo mwili

unatoa nafasi kwa ajili ya mbegu za kiume mpya kutoka kwenye korodani. Kupata ndoto nyevu

haimaanishi uanze kujamiiana.

SURA YA 3 | WAvULANA

adamu, kutoka uganda (umri, miaka 13)

“Sidhani kupata ndoto nyevu kunamaanisha ninatakiwa kujamiiana. Ni

kukua tu. Ninaona aibu tu kwa vile inabidi nibadilishe mashuka kila baada

ya siku moja.”

Wavulana wengine wanapoanza kupata ndoto nyevu wanaona ni tukio kubwa sana ambalo

wanalifurahia.

Panaito kutoka Kenya

“Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilijisikia kama nimekomaa

kijinsi. Nilifurahi kuwa mmojawapo wa wale ambao tayari walishapata.

Lakini ningelikuwa sijapata taarifa, ningeweza hata kwenda kumuona

daktari,ninamshukuru Mungu kwamba nilijua kilichokuwa kinatokea”.

adamu kutoka uganda (umri, miaka 13)

“Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilimwambia kaka yangu mkubwa

ambaye alinihakikishia kwamba ilikuwa ni sehemu ya ukuaji.”

Wavulana wengine hawawi na furaha sana wanapoanza kupata ndoto nyevu. Hili ni jambo la

kawaida vilevile.

nfune kutoka Zambia (umri wa miaka 13.”

“Ninaona kama zinanichukiza”

Wavulana wengine wanao marafiki wasio na huruma, ambao huwatania kuhusu kupata ndoto

nyevu. Ni makosa kumtania au kumcheka mtu kwa vile amepata ndoto nyevu. Ndoto nyevu ni

jambo la kawaida.

bernard kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Nilipokuwa darasa la 8, sikutegemea kama ningeanza kukojoa manii

mapema kiasi hicho. Nilimwambia rafiki yangu siri, badala ya kunieleza kwa

nini yametokea, alinicheka. Nilijisikia kufedheheka. Sikutaka mtu yoyote

afahamu, lakini aliwaeleza watu wengine, na wengine wakasema nilikuwa ninapiga

punyeto. Nilimfuata rafiki yangu mwingine ambaye alikuwa mkubwa

kwangu ambaye alinieleza kwamba ndoto nyevu ni kawaida.”

Unatakiwa usiwe na wasiwasi kuhusu ndoto nyevu kwa vile ni jambo la kawaida halina kasoro.

Unavyoendelea kuujua mwili wako ndivyo utakavyokuwa na raha na mabadiliko unavyokuwa

unayapitia. Kwa kuongezea, ukiwa na taarifa iliyokamilika utaweza kuwasaidia wavulana wadogo

kuelewa kitu gani kinawatokea wanapopitia ujana balehe.

Yapo maelezo na mafunzo mengi mazuri ndani ya kitabu hiki,kwa hiyo usiachie kukisoma kitabu

hiki kwa undani.

25

26

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 3

WaVulana

Katika kipindi cha balehe mvulana anategemea mabadiliko mengi kutokea. Mabadiliko

haya ni ya taratibu na hutokea katika umri tofauti kwa wavulana tofauti. Yafuatayo ni

mabadiliko ambayo unaweza kuyategemea:

Mwili wako utakua , hasa mifupa ya mabegani, mikono, miguu na nyayo. Vilevile misuli

itajengeka na utakuwa na nguvu.

Sauti itabadilika halafu itakuwa nzito kadri vinyuzi sauti vinavyokuwa vinene na

kurefuka.

Uume wako utaongezeka na mapumbu yataanza kuninginia chini.

Uume wako utadinda mara kwa mara.

Unaweza kupata ndoto nyevu (kukojoa manii usingizini) usiku.

Unapopitia mabadiliko haya elewa kwamba:

Kila ukubwa wa uume ni sahihi.

Hakuna ubaya wowote kutahiriwa na wala hakuna ubaya wowote kutokutahiriwa kwa

mwanaume.

Oga na kusafisha uume wako kila siku. Kila mara rudisha nyuma govi na kusafisha chini

yake iwapo hujatahiriwa.

Sio lazima kujamiiana eti kwa vile uume umedinda.

Ndoto nyevu ni tukio la kawaida, huwapata wengi, hakuna haja ya kuwa na wasiwasi, sio

dalili ya kwamba unatakiwa kuanza kujamiiana.

Wakati wowote mabadiliko haya yanapotokea mwilini mwako ndio wakati mwafaka. Wewe

ni wa kipekee na uko kawaida kabisa.

Wasichana

Sura ya pili ilielezea kidogo kuhusu mabadiliko ya msichana wakati wa balehe. Sura hii inatoa

maelezo ya kina na naamini utayafurahia kuyasoma.

MauMbile na uKubWa Wa MWili

Wasichana wengi huanza kukua haraka haraka wanapokaribia umri wa miaka 10 hadi 11. Lakini

wapo wasichana wanaoanza kukua wakiwa chini ya umri huu au umri mkubwa zaidi ya huu. Miguu

mara nyingi huwa ndiyo sehemu ya mwili inayokua haraka. Unaweza kuwa mfupi, lakini ukajikuta

miguu yako ghafla imekuwa mikubwa sana! Usijali sehemu nyingine ya mwili itakua na kulingana

na hiyo miguu mikubwa. Mwili wako unakua kwa wakati wake.

Mifupa mingine itaanza kukua pia kila mmoja kwa wakati wake. Mikono na miguu yako inaweza

kutangulia kukua haraka wakati sehemu ya uti wa mgongo ikiwa inakua taratibu zaidi.

Mabadiliko mengine unayoweza kuyahisi ni kuanza kukua nyonga. Mifupa ya nyonga inakuwa

mikubwa, na laini, tishu zenye mafuta hukua kwenye nyonga, mapaja na matako. Kadri nyonga

inavyozidi kupanuka, kiuno kitaonekana chembamba ukilinganisha na sehemu zingine. Mwili

utakuwa wa mviringo, ukionyesha umbo la kike.

Matiti YaKO

catheryn, kutoka Ghana (umri, miaka 15)

“Nilikuwa na miaka 10 nilipoanza kuhisi mabadiliko ya mwili wangu.

Watu waliniambia bila mabadiliko hayo nisingeliweza kuwa

mwanamke kwa hiyo nilifurahi. Nilikuwa naingia katika kundi la

wanawake hivyo sikuwa na budi kujihadhari.”

Wasichana wengine wanaanza kuota matiti wakiwa na umri kati ya miaka 8 au 9, lakini wengine

yanachelewa kuota. Kuota kwa matiti kunasababishwa na homoni inayoitwa estrojeni.

Estrojeni inasababisha tishu ndani ya matiti kukua ili siku moja utakapokuwa na mtoto, uweze

kutengeneza na kuhifadhi maziwa.

Kabla matiti yako hayajaanza kukua, pengine chuchu zako zitakuwa kubwa na kusimama kuliko

zilivyokuwa awali. Mabadiliko mengine unayoweza kuyaona ni duara jeusi na kubwa la ngozi

litakalozunguka chuchu zao.

27

SURA YA 4

28

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unaweza vilevile kuona vinundu vidogo vidogo kuzunguka duara hilo. Hivi vinundu ni tezi ambazo

ni za kawaida. Mwanamke anapokuwa na mtoto, tezi hizi zinatoa kiini kinachosaidia kulinda

chuchu wakati mtoto ananyonya.

Margaret kutoka tanzania (umri, miaka 18)

“Matiti yangu yalipoanza kukua, nilijisikia vizuri japo kuwa

wakati mwingine kulikuwa na maumivu kidogo”

Kadri chuchu na duara vinavyozidi kuwa vikubwa, matiti nayo yanakuwa makubwa na kujaa.

Mabadiliko haya yanavyoanza kutokea, matiti yanaanza kuuma. Unaweza kujisikia maumivu

ukiyabinya au ukiyagonga. Hii ni kawaida, na hakuna haja ya kuhofu. Matiti ni sehemu ya mwili

ambayo ni nyepesi kuhisi kitu. Iwapo kutatokea kiamshi cha namna tofauti, kama kuguswa au

hata ubaridi, chuchu zinakuwa ngumu na husimama.

Kwa wasichana wengine, matiti yao hukua taratibu na kwa wengine hukua haraka. Kwa wastani,

inachukua muda wa miaka 4 matiti kukua kabisa, lakini wasichana wengine matiti yao yanakua

kabisa kabla ya miaka 4, wakati wasichana wengine matiti yanaweza kuchukua hadi miaka 6

kukua kiukamilifu. Hivyo iwapo matiti yako yanachukua muda mrefu kukua tulia tu, yatakua.

Debora kutoka uganda, (umri, miaka 15)

“Matiti yangu yamekua hivi karibuni, lakini ninaogopa jinsi

yanavyoongezeka haraka. Sijali kuwa na matiti, ila ninatumaini

hayatakuwa makubwa sana. Mara ya kwanza nilikuwa

ninashangaa kwa nini yamechelewa kuota, lakini sasa ukubwa

wake unanitisha.”

Kuna matiti ya maumbo na ukubwa mbalimbali. Ukubwa na maumbile ya matiti yanatokana na

tabia vinasaba ulivyorithi toka kwa wazazi wako. Ukubwa pia unategemea tishu zenye mafuta

katika matiti. Hakuna unachoweza kufanya ili matiti yako yawe unavyotaka. Hakuna kiasi

chochote cha mazoezi kinachoweza

kuongeza ukubwa wa matiti yako.

Mazoezi yanajenga misuli lakini matiti

hayana misuli. Kumbuka tu kwamba

matiti yote, makubwa au madogo –

yana kazi kubwa moja - kunyonyesha

watoto.

Pia unatakiwa ujue kwamba, matiti

hayakui yote pamoja sawasawa. Titi

moja linaweza likawa kubwa kidogo

kuliko jingine. Ukweli ni kwamba

hakuna hata mmoja ambaye ana matiti

yanayolingana ukubwa na si rahisi

kuona tofauti hizi.Maumbile ya chuchu

vilevile yanatofautiana sana. Wanawake

wengine chuchu zao zimegeukia

ndani badala ya nje, wengine chuchu

zimezama ndani ya mduara n.k.

Kama matiti yako ni makubwa au madogo,

ni sahihi yalivyo kwako.

SURA YA 4 | WASICHANA

Matiti yana maana tofauti kutoka jamii moja hadi nyingine. Katika utamaduni mwingine

wanawake wanaweza kuacha matiti wazi, wakati katika tamaduni zingine wanashangaa na sio

heshima hata kidogo. Katika sehemu nyingi hata hivyo kuota matiti ni tukio kubwa katika maisha

ya msichana. Ni ishara ya msichana kukua. Wasichana wengi huyapenda matiti yao.

Prossy,kutoka uganda (umri,miaka 13)

“Ninayapenda matiti yangu. Nilikuwa nawahusudu dada zangu

walivyokuwa na matiti. Nilikuwa nachukua soksi na kuzikunja

halafu naweka ndani ya gauni nionekane kama nina matiti.”

barlay kutoka Kenya (umri, miaka 16)

“Nilikuwa ninawahusudu wasichana wanovaa nguo zinazobana

mwili. Nilifurahi nilipopata matiti, hivyo na mimi niliweza kuvaa

nguo zinazobana mwili.”

cathy kutoka uganda (umri, miaka 17)

“Matiti yangu yalikua nikiwa darasa la kwanza .Nilijiona kama

msichana mkubwa kuliko wote darasani. Ilichukuwa muda kukubaliana

na mabadiliko ya mwili wangu. Lakini nilikuwa napenda

nyonga yangu illivyo ya mduara. Marafiki zangu walisema nyonga

yangu inashawishi na hii ilinifanya nijivunie.”

Sherifan kutoka Ghana (umri, miaka 15)

“Nilifurahi sana kwa sababu nilianza kuonekana kama mama

yangu. Nilipokuwa sina matiti nilikuwa ninavaa sidiria ya mama

yangu na kuweka soksi ndani yake nionekane nina matiti kama

mama yangu.”

Baadhi ya wasichana wanajisikia vibaya matiti yao yanapoanza kukua.Pia hii ni kawaida.Hii ni

kwa sababu marafiki zao wa rika moja hawajaota matiti bado.

irene kutoka uganda (umri, miaka 16)

“Wakati matiti yangu yalipoanza kukua, nilikuwa ninavaa flana

zinazobana sana, flana za wadogo zangu. Nilitaka kujisawazisha

mwili nionekane kama sina matiti.”

angela kutoka Kenya (umri, miaka 17)

“Nilikuwa nina wasiwasi mno na nilikuwa ninavaa sweta wakati

wote matiti yangu yalipoanza kuonekana. Nilikuwa sijisikii vizuri

kwani nilikuwa ninasoma shule ya mchanganyiko na sikujua wavulana

wangesema nini.”

Wasichana wengine wanajipinda vibaya kwa kuinamisha vifua vyao kwa sababu ya

kufedheheshwa na kukua kwa matiti yao. Jambo hili linasikitisha kwa sababu kila mtu anatakiwa

kuupenda mwili wake, na kutojali watu wengine wanasema nini. Vyovyote vile matiti yako

yalivyo,kama ni makubwa au madogo yaliyochongoka au ya mviringo ni mazuri jinsi yalivyo.

29

30

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Rita kutoka uganda (umri, miaka 16)

“Ninayapenda matiti yangu kwa sababu yananifanya nijisikie mwanamke

haswa. Wasichana wakubwa ambao hawana matiti hutaniwa na

kufananishwa na wanaume”

Si vema watu kuwatania wasichana kuhusu matiti yao. Huu si ustaarabu. Msichana ajaribu kadri

awezavyo kuwadharau na kutojali matusi yao.

UNAJUA KUWA KUNA IMANI POTOFU NYINGI KUHUSU MATITI?

Watu husema mambo mengi potofu kuhusu matiti, yafuatayo ni baadhi yake:

1. Wasichana wenye matiti yaliyochongoka huvutia kingono. hii Si Kweli. Kuvutia kingono

ipo kwenye akili ya anayejiona hivyo na si kwenye mwili wake.

2. Kuweka jibini kwenye chuchu au kumfanya mdudu ang’ate chuchu hufanya matiti yakue

haraka. hii si Kweli pia. Homoni ndizo zinazofanya matiti yakue. Hamna kitu chochote

zaidi ya hicho kitakachobadilisha matiti.

3. Wasichana wenye ngozi iliyo nyeusi kuzunguka chuchu zao wamewahi kufanya ngono.

huu ni uongo! Kama ilivyo rangi ya ngozi yako, rangi ya mduara wa chuchu inatokana na

tabia vinasaba ulivyorithi kutoka kwa wazazi wako.

4. Matiti yanaweza kuwa makubwa kama wavulana watayashikashika. Si kweli! Ukubwa wa

matiti unategemea tabia vinasaba ulizorithi kutoka kwa wazazi wako.

5. Wasichana wenye matiti yaliyolala wameshawahi kufanya ngono au wameshawahi kutoa

mimba. huu pia ni uongo! Matiti hulala/huanguka kutokana na uzito na maumbile. Kama

una matiti makubwa uwezekano wa kulala au kuanguka kwa sababu ya uzito ni mkubwa

zaidi.

6. Kuvaa sidiria hufanya matiti kuanguka. uongo! Sidiria hushikilia matiti na huzuia ngozi na

tishu za matiti kutanuka na kupunguza kunyumbuka.

7. Wasichana wenye matiti makubwa watakuwa na maziwa mengi kwa ajili ya watoto wao.

uongo! Uzalishwaji wa maziwa hautokani na ukubwa wa matiti; hata matiti madogo huzalisha

maziwa yanayomtosheleza mtoto.

naMna Ya KutunZa Matiti YaKO

Matiti ni sehemu nyeti, kwa hiyo kuna vitu fulani ambavyo unatakiwa uvijue kuhusu utunzaji

wake. Hata siku moja using’oe nywele zinazozunguka chuchu, zinaweza kusababisha madhara.

Ni kawaida kuwa na vinyweleo hivyo. Kuna baadhi ya wasichana wanatokwa majimaji kwenye

chuchu zao: hiki ni kitu cha kawaida. Lakini kama majimaji hayo yana damu au rangi ya kahawia

unatakiwa kumwona daktari maana inaweza kuwa ni uambukizo.

Kutunza matiti ni pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna anayeyashika bila ridhaa yako. Mara nyingi

wavulana na wanaume hugundua kwamba matiti ya wanawake yanavutia sana, lakini hata hivyo

mtu hana ruhusa kuyashika labda upende mwenyewe.

Matiti ya wanawake wengi ni rahisi sana kuhisi yanapoguswa.Kuguswa kunaweza kuleta ashiki ya

kusisimua, na hii inaweza kusababisha utende usilotegemea au uponzeke.

SiDiRia

SURA YA 4 | WASICHANA

Si lazima kuvaa sidiria kama una matiti madogo au yaliyosimama imara. Lakini kama matiti yako

ni makubwa, unaweza ukajisikia vizuri kama ukivaa sidiria ambayo inasaidia matiti yasitikisike

au kurukaruka unapotembea, kukimbia, kucheza dansi au kucheza michezo. Wasichana wengine

waliobalehe wanafedheheka na matiti yao, hivyo kuvaa sidiria kunawafanya kutokuwa na

wasiwasi na pia hupunguza kufedheheka/kujishuku.

Ili kupata kipimo sahihi, wanawake wengi wanajaribisha namba mbalimbali za sidiria kuona ni ipi

itamtosha vizuri. Unashauriwa kufanya hivyo.

Wanawake wengine huwa wanachukuwa vipimo ili waweze kupata saizi ya sidiria. Ili uweze

kupata vipimo vyako, unahitaji kujua saizi ya kifua chako pamoja na saizi ya titi.Pima kifua chako,

chini kidogo ya matiti, ili upate saizi ya kifua. Kisha pima sehemu iliyojaa zaidi ya matiti ili kupata

ukubwa wa titi, kama viko sawa unahitaji kikombe A. Kama kipimo cha matiti ni 2.5 Sm zaidi ya

kifua unahitaji saizi ya titi B. Iwapo kipimo cha matiti ni 5 Sm zaidi ya kifua basi unahitaji saizi ya

titi C.

Via VYa uZaZi/SeheMu ZaKO Za SiRi

Uke ndilo tundu pekee lililo kubwa kuliko matundu yote matatu katika eneo la via vya uzazi.

Mashimo mengine ni tundu la mkojo (mbele ya uke) na mkundu (nyuma ya uke). Uke una kina cha

sm 7 na upana wa sm 3 – 4. Ngozi yake ni laini iliyokunjamana.

Uke wa mwanamke mtu mzima ni imara sana; hutanuka sana na una misuli imara. Wakati wa

kuzaa mtoto uke unatanuka sana kuliko ukubwa wake wa kawaida ili kuruhusu mtoto kutoka

tumboni mwa mama yake. Lakini uke wa msichana ni mwembamba na hauwezi kutanuka

sana. Hii ni mojawapo ya sababu ya madhara

yanayompata msichana aliyezaa angali mdogo.

Uke wa msichana mdogo unaweza kuchanika

au kupasuka wakati wa kuzaa. Hii husababisha

matatizo makubwa sana. (Soma Sura ya 11).

Katika kipindi cha balehe, kuta za uke zinaanza

kutoa majimaji ukeni. Maji maji hayo ni mazito na

yananata kuliko mate na yana kazi yake ambayo

ni kuuweka uke safi, na kutengeneza mazingira

mwafaka ambapo bakteria wazuri wanaozuia

maambukizo ya magonjwa wanaweza kuishi.

Wanawake wengi wanaanza kuona maji maji

ukeni katika nyakati tofauti katika mzunguko

wa mwezi na wakati wanapopata ashiki. Hii ni

kawaida.

Sehemu za siri za mwanamke kwa nje

31

32

Upo uzushi mwingi kuhusu uke:

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Je ? Unajua ukweli kuhusu uke?

1. Uke ni sehemu chafu kuliko sehemu zote mwilini. Si kweli! Mdomo ndio sehemu chafu

kuliko zote mwilini. Ukweli ni kuwa majimaji ya ukeni na damu ya hedhi ni safi. Lakini

mara baada ya kutoka mwilini, bakteria wanaweza kuzaliana kwenye majimaji na damu

na kufanya yatoe harufu mbaya.

2. Uke haujazibwa mwisho, ni tundu lisilo na mwisho. Si kweli pia! Uke umezibwa na mlango

wa tumbo la uzazi. Kondomu au sodo (tampon) haziwezi kusafiri hadi ndani ya kizazi.

3. Ni tabia mbaya kushika uke. Si kweli! Uke ni kama sehemu nyingine yoyote ya mwili

kuishika ni kama kushika sikio. Hata hivyo uke ni sehemu nyeti ya mwili, hivyo unatakiwa

kujishika wakati uko peke yako.

4. Uke ni kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Si kweli! Uke ni sehemu ya mwili wa

mwanamke. Ni yake pekee yake! Usimruhusu mtu yeyote kuushika bila ridhaa yako.

Eneo linalozunguka mlango wa uke linaitwa vulva. Kwa kawaida mlango wa uke umefungwa, na

unalindwa na mashavu ya nje na ya ndani. Mashavu haya yana mikunjo miwili ya ngozi. Kuna tezi

ndogo ndogo katika mashavu, hivyo unaweza kujihisi unatoa jasho na unatoa majimaji meupe

sehemu hizo.

Mbele ya tundu la mkojo, ambapo midomo ya ndani inakutana, kuna kinembe au kisimi. Kinembe

ni kinundu kidogo mfano wa kunde. Kinembe hiki kimejaa neva na ni sehemu ambayo ni nyepesi

kupata hisia/ashiki katika sehemu za via vya uzazi. Kinahisia kali kikiguswa.

Ndani kabisa, mwisho wa uke wako kuna mlango wa mfuko wa uzazi. Mlango wa kizazi unafunga

mwisho wa uke. Upo uwazi mdogo tu kwenye mlango wa kizazi, na uwazi huu unaelekea kwenye

mfuko wa uzazi. Uwazi ni mdogo kiasi kwamba damu za hedhi tu zinaweza kutoka na mbegu za

kiume tu zinaweza kuogelea kwenda juu. Watu wengine huhofia kwamba wakati wa kujamiiana

kondomu inaweza kutoka kwenye uume na kuingia kwenye tumbo la uzazi. Hii haiwezekani kwa

sababu uwazi uliopo kwenye mlango wa mfuko wa uzazi ni mdogo sana. Mlango wa mfuko wa

uzazi unafunguka tu wakati wa kuzaa mtoto ili mtoto aweze kutoka kupitia ukeni na kisha nje ya

mwili.

Ngozi ya mlango wa mfuko wa uzazi ni laini sana, hususani kwa wasichana wadogo na wanawake

wadogo. Mlango wa mfuko wa uzazi unaweza kuharibika au kuambukizwa bakteria na virusi

ambavyo vinaweza kuingia mwilini wakati wa kujamiiana. Hii inaweza ikasababisha saratani

ya mlango wa mfuko wa uzazi. Wasichana wanaoanza kujamiiana mapema au walio na wapenzi

wengi wa kufanya nao ngono, au walio na VVU, wako kwenye hatari ya kupata saratani ya mlango

wa mfuko wa uzazi kuliko wale ambao ni waangalifu katika kufanya ngono. Kutoanza kujamiiana

mapema na kutumia kondomu kunaweza kukulinda usipate saratani ya mlango wa mfuko wa

uzazi, (soma sura ya 10 zaidi kuhusu afya ya uzazi).

KuFanYa uSaFi Wa MWili ViZuRi

SURA YA 4 | WASICHANA

Uke na mkundu vinapaswa kuoshwa mara kwa mara na kubakia vikavu. Ni jambo zuri kuepuka

kuchangia mataulo na ndugu wengine katika familia au marafiki kwani yanaweza kusababisha

kuenea kwa maambukizi ya magonjwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Baada ya kuoga vaa

chupi za pamba zilizo safi. Katika kipindi cha joto, epuka kuvaa chupi za nailoni kwa sababu huwa

zinahifadhi unyevunyevu na joto, hali ambayo husababisha kuota bakteria. Kama huwezi kupata

chupi za pamba, vaa zilizozungushiwa kitambaa cha pamba.

Baada ya kukojoa au kwenda haja kubwa, unapaswa kujisafisha mwenyewe kwa kusafisha

kuanzia mbele ya sehemu zako za siri mpaka kwenye mkundu. Kama ukitumia karatasi la chooni,

karatasi, maji, majani au matawi ya miti kujisafisha, epuka kujisafisha kutoka nyuma kwenda

mbele. Ukijisafisha kutoka nyuma kwenda mbele, kuna hatari ya kuvuta vijidudu vya maradhi

kutoka kwenye mkundu kwenda kwenye uke na kwenye njia ya mkojo. Hii inaweza kukupa

maambukizi ya magonjwa.

Kamwe usijaribu kuosha ndani ya uke labda tu kama umeshauriwa na daktari.

Kwa bahati mbaya wasichana na wanawake wengine wanaosha ndani ya uke kwa kutumia sabuni

kali. Wanawake wengine wanapenda kupaka odorono au kupuliza manukato. Haya yote hayana

umuhimu, na yanaweza kukuletea madhara kwa sababu sabuni, na manukato vikitumiwa ukeni

vinaweza kubadilisha mfumo wa kawaida wa majimaji ndani ya uke na kusababisha ngozi ndani

ya uke kuwasha.

Katika nchi nyingine, kama vile, Zimbambwe na Zambia, wanawake huweka mitishamba, vipande

vya nguo, na vitu vingine ndani ya uke ili kusafisha au kuufanya ubane. Kiafya, hii sio njia nzuri

kwa sababu ngozi ndani ya uke ni laini mno. Unapoingiza vitu vigeni, vinaweza kusababisha

majeraha madogo madogo au michumbuko na uvimbe mambo ambayo yanaweza kukufanya kuwa

na maambukizi na uwezekano wa kukuweka kwenye hatari ya kupata VVU.

Kwa ujumla, ni vizuri kutokuweka kitu chochote ndani ya uke wako, isipokuwa pamba za damu na

dawa kama umeandikiwa na dakitari. Hakikisha tu unafuata maelekezo kwa makini.

Ni vizuri kuchunguza kwa makini majimaji yanayotoka ukeni wakati wa mzunguko wa kila mwezi

ili kuweza kuona dalili na mabadiliko yasiyo ya kawaida. Ukiwa makini , utagundua kwamba

majimaji yanayotoka ukeni sio sawa wakati wote. Wakati mwingine yanaweza kuwa meupe

wakati mwingine yanaweza kuwa meupe kidogo kama ute mweupe wa yai. Wakati wa uovishaji,

majimaji ya ukeni yanaweza kuwa na utelezi zaidi na angavu. Vilevile majimaji ya ukeni yanaweza

kubadilika iwapo mwanamke atashikwa ashiki.

Iwapo majimaji ya ukeni yatakuwa mazito na kubadilika rangi kuwa njano, kijani au kahawia au

yanasababisha muwasho sehemu za siri, unaweza kuwa umeambukizwa maradhi. Harufu mbaya

ya majimaji toka ukeni, maumivu ndani ya uke na damu kutoka wakati hauko katika siku zako

za hedhi ni dalili pia za maambukizi ya ugonjwa. Iwapo utapata mabadiliko yoyote kati ya haya,

itabidi umwone daktari.

Iwapo hushiriki ngono isiyo salama, na kama unazingatia usafi, huwezi kupata matatizo haya.

Ukiutunza vizuri uke wako utajikamilisha kulingana na mazingira. Unachotakiwa kufanya ni

kuosha kwa uangalifu eneo la via vya uzazi kila siku na maji safi au osha kwa sabuni ya kuogea.

Tenganisha mashavu ya nje ili kusafisha uchafu unaojikusanya sehemu hizo.

33

34

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

UNAJUA KUHUSU UKEKETAJI WA WANAWAKE?

Katika mila nyingine, kisimi/kinembe na/au sehemu zingine za via vya uzazi vya

mwanamke zinakatwa au kuondolewa kabisa. Utaratibu huu unaitwa kutahiri

wanawake au ukeketaji wa wanawake. Ukeketaji huu unatofautiana katika nchi

mbalimbali. Wengine hukata kuzunguka kisimi, na wengine hukata kisimi na mashavu

(ya ndani na nje). Kukata kisimi na mashavu na kushona/kupunguza ukubwa wa uke

kunaitwa mfyato, na huu ndiyo ukatili wa kiwango cha juu kabisa.

ni wakati gani unafanyika? Umri ambao wanawake wanakeketwa unatofautiana nchi

moja hadi nyingine. Unafanyika wakati wa uchanga, utoto, ujana balehe, wakati wa

kuolewa au wakati mwanamke ana mimba ya kwanza.

Kwa nini unafanyika? Baadhi ya tamaduni, mila,desturi na imani zinaunga mkono

wanawake kukeketwa, lakini Biblia na Korani haviungi mkono jambo hili. Katika jamii

zingine wanaamini kwamba kukeketa kutalinda ubikira wa wasichana na kuwafanya

wanawake wasiwe wahuni (Malaya). Pia watu wengine wanaamini kwamba kukeketa

kunaongeza raha ya kujamiiana kwa waume zao, na kitendo hiki kinaaminika kuongeza

uwezekano wa wanawake kuolewa na kuimarisha uwezo wa kuzaa.

unafanyikaje? Kwa kawaida wanaofanya kazi hii ni watu wazima/wazee au wakunga

wa jadi wanaotumia visu maalumu, mikasi, vipande vya kioo, nyembe na vifaa vingine

ambavyo si visafi kukeketea. Mara kwa mara ukeketaji unafanyikia katika mazingira

machafu na mwanga hafifu. Kwa kawaida,hazitolewi dawa za kutuliza maumivu, wala

za usingizi,wala dawa za kuzuia maambukizi!

Madhara yake ni nini? Kukeketa wanawake kunaweza kusababisha matatizo makubwa

ya kiafya na kisaikolojia (kihisia):

• Kutoka damu nyingi. Kukata sehemu za via vya uzazi kunaweza kusababisha

kutoka damu nyingi. Hii inaweza kusababisha kifo au upungufu mkubwa wa damu.

• Maambukizi ya magonjwa. Mambukizi ya magonjwa yanaweza kutokea kwa

sababu ya kutumia vifaa vichafu na pia yanaweza kutokea kwa kutumia dawa

za kienyeji za kuponyesha vidonda. Maambukizi yanaweza yakaenea hadi

kwenye tumbo la uzazi, mirija ya kupitishia mayai, na kwenye mayai ya uzazi na

kusababisha maumivu ya mara kwa mara hata ugumba. Mambukizi ya magonjwa

yanaweza kusababisha kifo.

• Mshituko: Mshituko kupita kiasi au kupoteza fahamu kunaweza kutokea kwa

sababu ya kutoka damu nyingi na maumivu makali.

• Kubana mkojo: Baada ya kukeketwa wanawake wanaweza kubana mkojo kwa

masaa au siku kwa sababu ya maumivu au kwa kuogopa kupitisha mkojo kwenye

vidonda. Hata baada ya vidonda kupona mwanamke aliyeshonwa uke, tundu

linaweza likawa dogo mno kuweza kutoa mkojo.

• Matatizo wakati wa siku za hedhi: Kama mlango wa uke ni mdogo sana kiasi cha

kutoruhusu damu ya hedhi kutoka vizuri, damu inaweza kukusanyika ndani ya uke

na tumbo la uzazi. Hii inaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa, na tumbo la

uzazi kuvimba kwa sababu ya damu ya hedhi.

heDhi na MZunGuKO Wa heDhi

SURA YA 4 | WASICHANA

UNAJUA KUHUSU UKEKETAJI WA WANAWAKE? (Endelea)

• Maumivu wakati wa kujamiiana na matatizo wakati wa kujifungua.Wasichana

waliokeketwa wanaweza kupata maumivu wakati wa kujamiiana pia wanaweza kupata

matatizo wakati wa kuzaa iwapo njia ya uke ni ndogo kupitisha mtoto (angalia sura II).

• athari za kisaikologia na kijamii: Ukeketaji kwa mwanamke unaweza kuwa na athari

za muda mrefu kimaisha na kiakili. Anaweza kupoteza imani kwa jamii,wazazi au hata

walezi. Anaweza pia kuathiriwa na hisia za kutokamilika, hofu, mfadhahiko na kupoteza

hamu ya kujamiiana.

Kwasababu ya athari kubwa za kiafya zinazotokea na kwasababu ukeketaji sio hitaji la

kiafya, ndio maana watu wengi sasa huita Ukataji wa via vya uzazi vya mwanamke. (FGM =

Female Genital Mutilation). Tendo hili linachukuliwa kama ni uvunjaji wa haki za wanawake

na wasichana juu ya afya zao kimwili na kiakili na haki za uhuru, usalama na ukamilifu wa

mwili (ujumla na ukamilifu wa miili yao). Kama wewe mwenyewe au unamfahamu msichana

anayelazimishwa kukeketwa, peleka suala hili kwa utawala wa serikali wa mahali ulipo

au mhudumu wa afya ili waweze kuongea na wazazi na ndugu zake juu ya athari mbaya

zinazotokana na kitendo hicho.

Wasichana wengi wanaanza kupata damu ya hedhi au kuingia mwezini kati ya umri wa miaka

10 na 16. Kuvunja ungo (mwanzo wa hedhi) ni dalili ya kwamba mabadiliko makubwa yanatokea

ndani ya mwili wa mwanamke. Vilevile ni dalili ya

kwamba anaweza akapata mimba akifanya ngono na

mwanaume.

Katika kipindi cha balehe, homoni husababisha

ovari ambavyo ni viungo viwili vyenye umbile la

yai kukomaa na kuanza kutoa yai kila mwezi. Kila

mwanamke anazaliwa na mayai ambayo ni madogo

mno kiasi kwamba hawezi kuyaona bila darubini.

Mrija wa falopio

Tumbo la uzazi

Kadri ovari zinavyozidi kukomaa, mfuko wa uzazi

pia unakua, ngozi laini inaanza kutengenezwa

Uke

kuzungukamfuko wa uzazi. Hivi ndivyo mfuko wa

uzazi unavyofanya matayarisho ya kupokea yai

lililorutubishwa.Kama hakuna yai lililorutubishwa,

ngozi laini inayozungukamfuko wa uzazi inakatika

na kutoka kupitia mlango wa mfuko wa uzazi, kupitia

kwenye uke na kutoka nje. Hii ndio damu ya hedhi au Sehemu za siri za mwanamke kwa ndani

“kuingia mwezini”. Kwa vile ngozi laini ya mfuko wa

uzazi imetengenezwakwa mishipa ya damu, inaitwa damu ya hedhi.

Wasichana ambao wameanza kupata hedhi (kwenda mwezini) wanao “mzunguko wa mwezi”.

Katika miaka michache ya mwanzo wasichana wengi mzunguko wao hauna mpangilio

unaoeleweka.

Ovari

Seviksi

35

36

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Hawajui ni lini wataingia mwezini tena. Inakuwa hakuna mfumo maalum, na mara nyingine

wanaweza kukaa miezi kadhaa bila kupata damu ya hedhi kabisa. Hii ni kawaida, baada ya miaka

michache mzunguko wa hedhi unakuwa wa kawaida. Wanawake wengine pia hawapati hedhi zao

kulingana na mzunguko wa kawaida wa kila mwezi, jambo hili ni la kawaida pia.

Hata kama mzunguko ni wa kawaida, muda wa mzunguko wa hedhi unatofautiana kwa

wanawake/wasichana. Kwa wengine mzunguko ni mfupi, siku 21 (hata chini ya hapo). Wengine

mzunguko ni mrefu, siku 35. Wastani wa mzunguko ni siku 28. Tuangalie mzunguko wa hedhi wa

mwanamke wa wastani ambao ni siku 28.

Siku inapoanza kutoka damu, hesabu kuwa ndiyo siku ya kwanza. Katika siku 5 hadi 7 zinazofuata

ukuta wa mfuko wa uzazi unajiachia na damu inatoka kupitia ukeni. Wakati huo huo mwili

unakuwa umeshahisi kwamba hakutakuwa na mimba mwezi huo, na mwili utajua kwamba

unahitaji tena kutayarisha yai jingine.Yai jingine litaanza kuchomoka kutoka kwenye Ovari. Mara,

baada ya hapo tumbo litaanza tena kutengeneza ngozi laini nyingine kuzunguka mfuko wa uzazi.

Katikati ya mzunguko kama siku 14 au wiki 2 hivi tangu damu ianze kutoka ovari inaachia yai

ambalo huanza kubingirika kuelekea kwenye mirija ya falopia. Hiki ni kipindi cha urutubisho.Hiki

kipindi ambacho uwezekano wa mwanamke kupata mimba ni mkubwa. Yai linakaa siku chache

kwenye mirija ya falopia, na kama litakutana

na mbegu za kiume linaweza kurutubishwa na

mwanamke atapata mimba. (Angalia sura ya 11

taarifa zaidi kuhusu mimba).

Kama yai halijarutubishwa linaingia ndani ya

mfuko wa uzazi, kupitia mlango wa mfuko

wa uzazi na uke, na kutoka nje ya mwili. Hii

itakuwa inakaribia siku ya 20.

Karibu wiki mbili hivi baadaye, mwili

unapotambua kwamba yai halikurutubishwa,

ngozi laini ya ukuta wa mfuko wa uzazi

inabomoka tena kama damu ya hedhi na

mzungo unajirudia tena.

ukuta wa tumbo la uzazi uliotayari

kupokea yai

Hivi ndivyo mzunguko wa hedhi unavyokuwa.

Wanawake walio wengi wanadhani kwamba

kipindi cha uzazi nikatikati kabisa ya

mzunguko, lakini hii ni kweli kwa wanawake

wenye mzunguko wa siku 28 tu. Kwa upande wa

wanawake wenye mzunguko mfupiau mrefu,

haiwezekani kuwa katikati ya mzunguko.

Hii ni kwa sababu uovishaji (kutoka kwa

yai) kunatokea karibu siku 14 kabla ya hedhi

nyingine kuanza. Hivyo basi inamaanisha

kwamba mwanamke mwenye mzunguko wa

siku 21 pengine anaovusha siku ya 7, ambapo

mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35

pengine anaovusha siku ya 21. hedhi:Kubomoka kwa ukuta wa tumbo la

uzazi

Mzunguko wa hedhi hautulii katika kipindi cha balehe.Unaweza kuathiriwa na mfadhaiko wa

mawazo, huzuni, kusafiri na mabadiliko mengine katika maisha ya msichana. Kwa hiyo ni vigumu

sana kujua kipindi cha uzazi kitakuwa lini. Wasichana wengi wanapata mimba kwa makosa kwa

sababu wanajamiiana siku ambazo wanafikiri ni salama, siku ambazo wanafikiri uwezekano wa

kupata mimba ni mdogo.

Wasichana na wavulana wengi wamewahi

kusikia kuhusu “siku salama” lakini hakuna

“siku salama” kwa wasichana balehe. Hii ni kwa

sababu mzunguko wa hedhi hubadilika sana

wakati wa ujana balehe. Kama mzunguko wako

ni wa kawaida, unaweza ukabadilika ghafla na

ukawa sio wa kawaida.

Zaidi ya hapo, hakuna siku salama dhidi ya

VVU na magonjwa mengine ya ngono.Unaweza

kuambukizwa magonjwa ya ngono siku yeyote

ya mwezi.

Kusubiri siku salama sio njia nzuri ya kuzuia

mimba au kuzuia magonjwa ya ngono. Kama ni

kijana balehe uliyeanza kujamiiana usitegemee

sana siku salama kama kinga. Kuna njia nzuri

za kujikinga (soma sura ya 10 na 11 kwa taarifa

zaidi kuhusu ngono salama na uzuiaji mimba).

KuVunja unGO

SURA YA 4 | WASICHANA

Hakuna “SIKU SALAMA” kwa vijana balehe

Kupata damu ya hedhi kwa mara ya kwanza ni tukio kubwa sana katika maisha ya msichana.

Wasichana wengi wanakumbuka siku waliyovunja ungo.

Ruvimbo, kutoka Zimbambwe (umri, miaka 13)

“Nakumbuka ilikuwa mwezi Juni tarehe 10 nilipoamka na kukuta

nguo zangu zina damu. Nilimwambia mama. Mama alinipa pamba

na akanielekeza namna ya kuitumia. Aliniambia pia kwamba kama

sina pamba ninaweza kutumia nguo za zamani.”

Kupata hedhi maana yake ni kwamba mwili unakua na unafanya kazi katika njia mpya. Vilevile

kupata hedhi inamaana ya kwamba unaweza kupata mimba endapo utajamiiana. Lakini kupata

hedhi haimaanishi mwili wako upo tayari kujamiiana au kupata mtoto, kwani uke bado ni mdogo

na haujakomaa.Uke hukomaa msichana anapofikia umri wa miaka 18 hadi 20. Isitoshe, nyonga na

mifupa ya nyonga inaweza kuwa midogo sana kumuwezesha kuzaa kwa njia ya kawaida.

Kupata hedhi ni dalili ya afya, lakini wasichana wengi wanashituka na kusikitika wanapovunja

ungo – mara nyingi ni kwa sababu hawakujua kilikuwa ni kitu gani na walidhani kuna kosa

limefanyika.

37

38

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Diana kutoka Zambia (umri; miaka 17)

“Nilishituka nilipopata hedhi kwa sababu sikujua. Lakini mama

yangu akanieleza kwa nini ilinipasa kupitia hatua kama hiyo”

Sherifan kutoka Ghana (umri; miaka 15)

“Sikujua kilikuwa ni kitu gani. Nilifadhaika na kuona aibu kwa

wazazi wangu na marafiki zangu. Nilisali na kumuomba Mungu

aniepushe na mambo hayo. Baadaye nilitambua kwamba ni

sehemu ya maisha.”

Stabisile kutoka Zimbambwe (umri; miaka 19)

“Sikuwa na uhakika kilichokuwa kinaendelea. Sikuwa na ufahamu

wa namna ya kulikabili suala hili. Kupata hedhi kulinifanya

nikose raha.”

Wasichana wanaojua hedhi ni kitu gani na wale ambao mama zao na dada zao wakubwa

wanazungumza nao kuhusu kupata hedhi, inakuwa rahisi kwao kuikubali hali hii.

Sandra, kutoka uganda (umri; miaka 13)

“Bado sijaingia mwezini, lakini hata kama nitaingia, tayari

ninajua hedhi ni kitu gani na kwa vipi unaweza kukabilana na

hali hiyo”

Demitrida, kutoka tanzania (umri; miaka 13)

“Bado sijapata hedhi, nikipata nitamwambia mwalimu mlezi

wangu. Pia nitamwambia mama ili anipatie pamba au kipande

cha nguo.”

Utajua kama umeanza kuingia mwezini utakapoona damu kidogo inatoka kwenye uke. Damu

haimwagiki kama maji yanavyotoka kwenye bomba. Inadondoka taratibu. Kawaida muda

utakaogundua ubichi usio wa kawaida, chupi yako itakuwa imenyonya damu yote, na nguo zako

nyinginezo zitakuwa salama.

Lakini wakati mwingine kunakuwa na damu nyingi au inakuja ghafla. Au inaweza kukuchukuwa

muda mrefu kujionyesha, kinatokea nini. Cathy mwenye umri wa miaka 17 kutoka Uganda

alichafua chupi yake hadi kwenye nguo.

cathy, kutoka uganda (umri; miaka 17)

“Ilinitokea darasani nikiwa na wanafunzi wenzangu. Nilisimama

na kwenda chooni. Nikagundua kuwa nimechafua nguo.

Aah, lilikuwa tukio baya sana. Nilifedheheka sana. Marafiki

zangu walinisaidia lakini ilibidi nikae nyumbani wiki nzima.”

Kama hii itatokea, tulia. Sio kosa lako hukujua kwamba jambo hili litakutokea! Kila mtu

inamchukuwa muda kuelewa namna ya kushughulikia hedhi.

Unaujua Ukweli kuhusu hedhi?

Kila mtu anayo maswali mengi kuhusu hedhi. Yafuatayo ni baadhi ya maswali na majibu yake:

1. Nitapoteza damu kiasi gani kila mwezi? Katika kipindi chote cha kutoka damu ya hedhi

cha mwezi, kiasi cha damu itakayotoka ni kama ml za ujazo 60 hadi 70. Ukipima ml 70. za

ujazo wakati wa kipindi cha Sayansi. utaona kuwa siyo damu nyingi sana. Hata hivyo huo

ni wastani tu, wanawake wengine hupoteza kidogo zaidi- kiasi cha vijiko vichache tu vya

chai. Wengine wanapoteza kikombe kizima kilichojaa.

2.

3.

Kama nikiweka kumbukumbu kwenye kalenda yangu naweza nikajua siku gani ni salama

kwangu, Siku ambazo siwezi kapata mimba?

Hapana, huwezi. Wasichana balehe huwa hedhi yao sio ya kawaida hivyo hawawezi kujua

siku salama ni zipi. Isitoshe, hakuna siku salama dhidi ya maambukizi ya VVU na magonjwa

ya ngono. Unaweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa siku yoyote na usije ukafikiri

siku salama ni njia salama ya kujikinga na maambukizi.

4. Ninaweza kuingia mwezini mara mbili katika mwezi mmoja? Angalia ukurasa wa “40”

Susan alipata damu ya hedhi mara mbili mwezi Aprili.

5. Naweza nikajamiiana wakati niko mwezini? Hili sio jambo zuri, hasa kama ni ngono isiyosalama

(bila Kondom). Kama una VVU vitakuwa kwenye damu yako hivyo mwenzi wako

anaweza kuambukizwa kwa urahisi. Vilevile wewe uko hatarini iwapo utajamiiana wakati

huu na mwanaume aliye na VVU au magonjwa ya ngono. Uko hatarini kuambukizwa kuliko

wakati wowote ule katika mwezi.

6. Je, ngono inatibu maumivu ya mkakamao wa tumbo wakati wa hedhi? Hapana! Ngono

haiwezi kutibu maumivu ya mkakamao wa tumbo wakati wa hedhi. Huu ni uzushi tu ambao

vijana wengi wanaueneza.

KutunZa KalenDa

SURA YA 4 | WASICHANA

Kwa wasichana wengi, inawachukuwa muda kuzoea hedhi. Kujisikia vibaya kuhusu hedhi ni

kawaida kabisa. Jaribu kukumbuka kwamba hedhi ni dalili

ya utu uzima na afya nzuri. Pia unapaswa kujua kwamba

hedhi haita dumu milele. Wanawake wengi wanaacha

kupata hedhi wanapokuwa mwishoni mwa miaka 40 na

miaka ya 50. Umri huu unaitwa “wakati wa kukoma hedhi”

Wasichana wengi wanaona kuna umuhimu wa

kutunzakumbukumbu za tarehe aliyoingia mwezini.

Hata kama hedhi haina mpangilio uliotulia kuweka

kumbukumbu husaidia kutoa mwanga ni lini msichana

balehe ataingia mwezini ili aweze kujiandaa.Unaweza

kununua kalenda ndogo na kutia alama X siku unayoanza

kutoka damu. Kwa kuhesabu siku kati ya X na X utagundua

mzungukowako ni wa siku ngapi na pia kama hedhi yako

ina mpangilio uliotulia au la.

Weka mtiririko wa siku zako za hedhi kwa

kutumia kalenda

39

40

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Susan, mwenye umri wa miaka 19, ana mzunguko wa kawaida wa siku 28. Mwezi Aprili, alianza

kutoka damu tarehe 1, hivyo hedhi nyingine ilikuwa tarehe 29 ya Aprili. Mwezi Mei alipata hedhi

tarehe 27. Mwezi wa sita alipata hedhi tarehe 23. Mwezi wa saba aliingia mwezini tarehe 20

Mwezi wa nane aliingia mwezini tarehe 16 . Umegundua kuwa hedhi inaanza siku tofauti kila

mwezi japo mzunguko wake una mpangilio uliotulia.

Kumbuka, utaratibu wa kuwa na kalenda ni mzuri. Hukusaidia kufanya mandalizi ya kuingia

mwezini lakini sio njia nzuri ya kujua siku salama zitakuwa lini. Kama unapenda sana kufanya

ngono tafuta njia bora ya kujikinga dhidi ya mimba na magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/

UKIMWI.

heDhi inaVYOKOSeSha Raha

Wasichana wengi matiti huvimba na kuongezeka na yanakuwa laini sana kabla ya kuingia

mwezini au wakati yai limerutubishwa.Hali hii haifurahishi, ila ni ya kawaida.Hali hii

inasababishwa na homoni zinazosababisha tishu za matiti kuwa na majimaji zaidi kuliko ilivyo

kawaida. Ukivaa sidiria inayokutosha vizuri itakufanya ujisikie vizuri, na vyakula vyenye chumvi

kidogo vitakusaidia kupunguza kiasi cha maji kinachohifadhiwa na mwili.

Hedhi inaweza kumwathiri mwanamke katika hali yake kitabia. Kabla ya hedhi kuanza kila mwezi,

wasichana wengine hujisikia kulia au kuwa na huzuni. Mara nyingine wasichana wanakuwa na

hasira kwa sababu ya kuvimba matiti yao au mwili kuvimba kidogo au kuvimba sana. Hali hii

mara nyingine inajulikana kama “mahangaiko kabla ya hedhi” na ni matatizo ya kawaida. Jaribu

kuyapuuza yasikusumbue sana.

Wasichana wengine hujisikia maumivu kidogo ya tumbo au mkakamao wa tumbo wakati wa siku

zao za hedhi. Huu mkakamao unatokea kwa sababu misuli ya tumbo la uzazi inabana wakati

ngozi laini inayozunguka tumbo la uzazi inapojiachia na ukuta. Mkakamao huo ni wa kawaida

na unaweza ukavumilika. Iwapo maumivu ni makali lala chini na jaribu kuupumzisha mwili kwa

kuvuta hewa nyingi na taratibu. Vilevile unaweza kuliminyaminya tumbo lako. Njia nyingine ni

kuweka chupa ya maji ya moto tumboni na itakusaidia kupata nafuu. Kama njia hii haikusaidii,

tafuta dawa za tumbo za kutuliza maumivu kwenye maduka ya dawa au dukani.

Mazoezi pia yanaweza kusaidia japo hili halitakuwa jambo la kwanza kulifikiria. Unaweza

kujisikia kama kulala chini, lakini kufanya matembezi au kukimbia huwa kunawasaidia baadhi ya

wasichana kushughulikia tatizo la mkakamao wa tumbo. Ukiweza kupata kisodo aina ya tampoon

unaweza hata kwenda kuogelea. Kuwa katika hedhi kisiwe kikwazo cha kufanya shughuli zako za

kila siku ikiwa ni pamoja na kufanya mambo unayoyafurahia.

Mkakamao wakati wa hedhi na maumivu mara nyingi ndio dalili za awali za balehe na

unapofikisha umri wa miaka 18 au zaidi pengine mambo haya hayatakusumbua sana. Lakini

wasichana wengine hupata maumivu yasiyo ya kawaida wakati wa siku zao. Hawa mara nyingi ni

wasichana wenye hedhi nzito.

Wasichana wenye hedhi nzito mara nyingi wanatumia pedi nyingi usiku na mchana na bado

wanaacha alama ya damu kwenye mashuka au nguo. Mara nyingine wanakosa kwenda shule kwa

sababu wanatoka damu nyingi au wana maumivu makali. Hebu fikiria kukosa kwenda shule kila

mwezi na madhara utakayoyapata katika masomo yako!

Kuna ufumbuzi wa kushughulikia hedhi kali, hivyo usiumie bure. Iwapo kweli una maumivu makali

wakati wa siku zako au unatoka sana damu – kama unakosa kwenda shule kwa sababu ya siku

zako muone muhudumu wa afya. Wahudumu wengine wa afya wanaweza kupendekeza vidonge

vya kuzuia mimba ili kupunguza hedhi nzito yenye maumivu makali. Vidonge vinafanya hedhi

isibadilike badilike ovyo ovyo na vinasaidia kupunguza kiasi cha damu inayopotea kila mwezi.

Iwapo unahitaji kuonana na mganga wako mwulize kuhusu vidonge vya kuzuia mimba. Unaweza

kumeza vidonge hivi hata kama bado ungali hujaanza kufanya ngono. Vidonge vina dozi ndogo ya

homoni ambayo kwa asili inapatikana mwilini. Ni salama kwa vijana wanao balehe.

Kama Mganga hataki kukuandikia cheti cha dawa hizo jieleze,ukipenda mwuulize ufanye nini

kupunguza udhia unaoupata kila mwezi. Usikose kwenda shule kwa sababu ya tatizo linaloweza

kutatuliwa.

Unaweza pia kumwona mhudumu wa afya unapoanza kutoka damu katikati ya mzunguko wa

hedhi au kama siku zako za hedhi zinachukua zaidi ya siku 8.

nGOnO na heDhi

Hakuna ukweli kabisa kuhusu uvumi kwamba ngono inatibu maumivu ya hedhi. Ukweli ni kwamba

kufanya ngono wakati wa hedhi kunaweza kukuongezea uwezekano wa kuambukizwa magonjwa

ya ngono ukiwemo UKIMWI. Damu ya hedhi ni mazingira mazuri kwa bakteria na virusi kukua

haraka.

Iwapo mwanamke aliye katika hedhi amefanya ngono na mwanaume mwenye magonjwa ya

ngono, kuna uwezekano mkubwa kuambukizwa kuliko wakati mwingine wowote wa mzunguko

wake; vilevile kuna uwezekano wa kupata maradhi mengine hatari wakati wa hedhi. Hii ni kwa

sababu mlango wa tumbo la uzazi hufunguka kuliko kawaida ili damu ya hedhi iweze kupita.

Vijidudu vya magonjwa ya ngono vinaweza kusafiri hadi kwenye tumbo la uzazi na kupitia mirija

ya kupitishia mayai, hivyo kusababisha maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke,na

hatimaye kusababisha ugumba.

Kwa mwanaume, kufanya ngono na mwanamke aliye katika hedhi ni hatari vilevile.

Kama ameambukizwa VVU, damu yake itakuwa na virusi vingi vya VVU.

KujiSiKia ViZuRi, aFYa na uSaFi

Katika tamaduni zingine, wanawake walio katika hedhi wanachukuliwa kama wachafu. Lakini

ukweli damu ya hedhi ni safi. Baada ya damu ya hedhi kutoka mwilini bakteria wanaweza

wakakua ndani yake, na kusababisha inuke, ndio maana usafi ni muhimu unapokuwa katika hali

hii. Wakati wa hedhi, oga angalau mara moja ili uwe msafi. Usitumie manukato kwenye via vya

uzazi yanaweza kukusababishia muwasho.

Vidokezi vitakavyosaidia kuzifanya siku zako ziwe nyepesi na starehe:

SURA YA 4 | WASICHANA

Wakati wote kuwa tayari, zijue siku zako za hedhi ili usije ukashitukizwa.

Acha kutumia chumvi nyingi, chumvi inafanya mwili wako uwe na maji mengi, hasa wakati wa

siku zako.Hii inaweza kukufanya kujisikia mwili mzito kuvimba tumbo kutokuwa na raha na

kuwa na mfadhaiko.

41

42

Kunywa maji mengi au juisi ya mtunda.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kula kwa wingi vyakula vyenye chuma nyingi kama samaki, maini, maharagwe, nyama na

mboga za majani. Vyakula hivi vitasaidia kurudishia madini ya chuma yaliyopotea kwa

sababu ya damu iliyotoka.

utatuMia nini KujihiFaDhi na heDhi?

Kihistoria, wanawake na wasichana wakati wote wamepata hedhi na wameweza kuimudu hata

kama kulikuwa hakuna vifaa vya kisasa kuweza kuvinunua madukani kama sasa. Hivyo hata

kama huna fedha ya kununulia pedi na tampons, unaweza kushughulikia siku zako kama kawaida.

Moja ya vitu vya kawaida na rahisi sana kutumia ni vipande vya nguo chakavu. Unaweza

kuvichana kwa ukubwa wa kuenea kwenye eneo la chupi yako na kuvipanga vipande vya nguo

chakavu kimoja juu ya kingine. Hakikisha ni visafi vioshe vizuri na vianike ili viweze kukauka.

Vianike mahali pa siri lakini penye jua ili viweze kukauka. Jua ni dawa nzuri sana ya kuua vijidudu

vya maradhi.

Karatasi za chooni pia siyo aghali, unaweza kununua mabunda matano kwa bei ya bunda moja

la pedi. Itakubidi utengeneze karatasi

nene na refu la kutosha. Mara nyingine

karatasi za chooni zinakwaruza na

zinawezakukusababishia muwasho na uvimbe

kwenye ngozi yako.

Pedi nazo ni nzuri, zimetengenezwa kuweza

kutosha vizurikatikati ya mwili na chupi. Zina

vitu vya kuifanya ijishikizevizuri kwenye chupi

na kukinga tundu la uke.Pedi zinakaratasi

la nailoni kuzuia damu kupenya.Ukitumia

pedi, unatakiwa kuzitupa ndani ya choo cha

shimo au kuchoma moto baada ya matumizi.

Usizitupe ndani ya choo chakuvuta maji kwani

zitakwama na kuziba choo.

Wanawake wengine wanatumia tampon/sodo

ndogo ambayo ni pamba ngumu inayoingizwa

ndani ya uke wakati wa hedhi.Pamba hiyo

hulainika huku ikiendeleakunyonya damu

inayotoka kwenye tumbo la uzazi na kuingia

ndani ya uke. Kuna uzi ambao umefungwa

kwenyesodo ambao unaninginia nje ya uke.

Vuta uzi huu kutoa tampon.

Kitu kizuri kuhusu tampon ni kwamba

haisumbui, hivyo unaweza ukasahau kabisa

kuwa ipo. Lakini tampon zinahitaji uangalifu

zaidi. Wakati wote osha mikono yako kabla ya

kuiingiza. Kama utajiandaa mwenyewe,siku zako za

hedhi hazitakuwa za kutatanisha kwako.

SURA YA 4 | WASICHANA

Unahitaji pia kuzibadili mara kwa mara kwa sababu inaweza kukuletea maambukizi ya magonjwa

ikiachwa muda mrefu kwenye uke. Usiache sodo ndani ya uke zaidi ya masaa 8. Usiitumie usiku

kwa sababu unaweza kulala zaidi ya masaa manane.

Chochote utakachotumia, vitambaa vikuukuu, karatasi za chooni, pedi au sodo vibadili mara kwa

mara kuepuka kuacha damu kwenye nguo au harufu mbaya. Damu ya hedhi inapokutana na hewa,

inaacha harufu mbaya iliyochacha.Chupi zako au nguo zikipata madoa ziloweke kwenye maji

baridi, yenye chumvi kidogo, maji ya moto yanaifanya damu igande na kubakiza doa la kudumu.

Hedhi ni sehemu yako. Ukijiandaa ujio wake, utaona kwamba siyo jambo kubwa la usumbufu,

unaweza kujishughulisha, ukacheza na kufurahi wakati wa siku zako, na hedhi isikukoseshe

kwenda shule au kazini.

43

44

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya Nne

Wasichana

Wakati wa kubalehe, msichana ategemee mabadiliko mengi ya mwili. Yafuatayo ni baadhi

tu ya mabadiliko yanayoweza kutokea:

Mwili utaongezeka urefu; nyonga itapanuka, mifupa ya mikono, miguu itarefuka.

Msichana atapata umbo la mviringo la kike.

Matiti yatakua na chuchu itaongezeka ukubwa na kuwa na rangi nyeusi.

Sehemu za siri zitakomaa na kuta za uke zitaanza kutoa majimaji.

Damu ya hedhi itaanza kuonekana kila mwezi.

Dalili hizi hutokea kwa muda muafaka ambao ni tofauti kwa kila msichana. Wakati

mabadiliko haya yanatokea, kuna vitu vichache vya kuzingatia:

Kwamba matiti yana ukubwa unaotofautiana kwa kila mwanamke. Matiti yote

yanavutia hivyo yalivyo na ni muhimu kwa kunyonyesha watoto.

Safisha sehemu za siri- ila sio ndani ya uke- kila siku. Vaa chupi zilizotengenezwa kwa

kitambaa cha pamba.

Ni muhimu kuifahamu harufu na hali ya kawaida ya majimaji ya uke ili inapotokea

mabadiliko ujue kuwa ni dalili za maambukizi.

Siku za hedhi kwa msichana anayebalehe hubadilika badilika hivyo hakuna “siku

salama’ za kutopata mimba wala hakuna siku salama ambazo hutaambukizwa VVU au

magonjwa mengine ya ngono.

Ingawa wakati wa hedhi ni kawaida kuumwa tumbo, kuvimba au kujisikia vibaya,

hali hii isifanye msichana akakosa raha. Mazoezi na vyakula vyenye chumvi kidogo

husaidia kupunguza maumivu. Kama maumivu yanakuwa makali na damu nyingi sana

inatoka, kamuone mhudumu wa afya.

Mabadiliko Ya Msingi

Katika Kutunza Mwili

Sura hii inazungumzia jinsi ya kutunza afya ya mwili wako kwa ujumla. Hili linaweza kuonekana

kama sio muhimu ukilinganisha na mambo mengine yaliyomo katika kitabu hiki, lakini ni muhimu

kujua jinsi ya kuishi na afya njema. Kwa kweli matatizo mengi ya afya yanaweza kuepukwa kama

ukila vizuri, ukifanya mazoezi, ukiwa msafi na ukijisikia vizuri.

Ni wajibu wako kuangalia mambo haya kila siku, na kuonekana na kujisikia vizuri iwezekanavyo.

Mwili wako ndio utakaokuwa nao katika kipindi chote cha uhai wako. Kwa hiyo unatakiwa

kuutunza kweli kweli!

jiWeKe MSaFi, nuKia ViZuRi.

Kila mtu anataka kuonekana msafi,

lakini kujihisi kuwa na mvuto

inaonekana ni muhimu hususani katika

kipindi cha ujana balehe kwa sababu

ya mabadiliko makubwa yanayotokea

katika mwili. Sio tu mwili unabadilika

umbo wakati wa balehe, lakini vilevile

unaanza kutoa harufu mpya, majimaji

mapya na hofu mpya hasa kwa vijana.

Hivyo kujizoesha kuwa msafi inaweza

kuwa ni njia nzuri ya kujisikia raha ili

kukabiliana na mabadiliko haya yote

yanayotokea.

Oga angalau mara moja kwa siku ili kujisikia

vizuri na safi.

Sandra, kutoka uganda (umri ; miaka 13)

“Siku zote oga, fua na piga pasi nguo ili uonekane nadhifu.”

Usafi mzuri wa mwili hususani wakati wa balehe ni muhimu kwa sababu ngozi yako inaanza

kutoa majimaji zaidi kuliko ilivyokuwa wakati ukiwa mtoto, na baadhi ya haya majimaji yanaweza

kusababisha harufu mbaya kama huogi.

Majimaji utakayoyaona zaidi ni ya jasho. Jasho linatokana na tezi zilizopo kwenye ngozi. Tezi za

jasho zinakuwa hai zaidi wakati unapofikia balehe.

45

SURA YA 5

46

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kwa hiyo, vijana balehe hugundua kwamba wanatoka jasho jingi sana. Pia wanagundua kuwa

jasho lao hutoa harufu na ladha yake ni tofauti kuliko jasho la maji ya kawaida analotoka mtoto

ambaye amekimbia wakati wa jua.

Kwapa zako zina tezi nyingi za jasho, lakini pia una tezi nyingi za jasho katika mikono yako, miguu,

na hata katika via vya uzazi, hivyo utagundua kuwa unatoka jasho sana katika sehemu hizi.

Harufu ya jasho lako itabadilika katika kipindi cha balehe, lakini mabadiliko haya ya harufu ya

mwili ni ya kiasili na kiafya. Ni dalili ya kukua.

Ingawa watu wengi wanahofia harufu ya jasho lao, hasa jasho linalotoka kwapani, kuoga mara

moja au mbili kwa siku, na kuvaa nguo safi inatosha kukuweka nadhifu na safi. Kama unatoka

jasho kwa wingi na linakusumbua, vaa chupi iliyotengenezwa kwa pamba na nguo zisizobana

zilizotengenezwa kwa pamba.Nguo za pamba zinauwezo wa kufyonza jasho kuliko nguo za mpira.

Pia pamba huruhusu hewa kupita hivyo husaidia kuleta ubaridi.Baadhi ya watu hununua odorono

za kupaka au kupulizia marashi ili kuzuia harufu inayotoka kwapani.Hivi vyote vinaweza kuwa

aghali.Kuoga na kuvaa nguo safi kunasaidia vema tu.

Kama lilivyo jasho, majimaji mengine ni damu ya hedhi, majimaji ya ukeni, manii na utoko

(vilainisho vyeupe chini govi) - kimsingi vitu hivi ni safi. Lakini punde tu majimaji haya

yanapokuwa yametoka mwilini, bakteria wanaweza kuota ndani yake, na kusababisha harufu

mbaya au wakati mwingine maambukizi.Kwa hiyo, ni muhimu kusafisha maeneo ya via vya uzazi -

eneo la uke na uume kila siku.Wavulana ambao hawajatahiriwa wanahitaji kuvuta nyuma govi na

kusafisha utoko (Angalia sura ya Tatu).

Wasichana inawalazimu kusafisha katikati ya mashavu ya ndani na nje ya uke, lakini hawahitaji

kusafisha ndani ya uke kwa sabuni kwa sababu uke hujisafisha na kujilinda wenyewe kwa kutoa

uchafu. Usafi ni muhimu hususani wakati wa kipindi cha hedhi (angalia sura ya Nne).

Kwa kusafishia via vya uzazi, sabuni ya kawaida ya kuogea ni nzuri kutumia. Hutakiwi kutumia

sabuni zenye kemikali au zenye kuondoa harufu kwapani, kwenye via vya uzazi kwasababu

zinaweza kusababishia mwasho. Kwa kuongezea, sabuni zenye nguvu za kemikali zinaweza

kuuwa bakteria wazuri wanaoishi sehemu kama za uke ambao wanasaidia kulinda baadhi ya

maambukizi. Baada ya kujisafisha unatakiwa kujikausha na kuvaa nguo safi.

Kama una ngozi inayokauka paka mafuta ya mgando (vaselini) mafuta yeyote mengine au losheni

katika viganja vyako, mikono na miguu itasaidia kulainisha ngozi.Losheni inayopakwa mara

baada ya kuoga inasaidia kuhifadhi unyevu unyevu katika ngozi yako.

Osha mikono yako mara kwa mara. Kila mara nawa mikono yako baada ya kutoka chooni na kabla

ya kula au wakati wa kuandaa chakula. Weka kucha zako safi kwa kuzikata na kuwa fupi.

utunZaji Wa MenO YaKO

Mdomoni mwako ni sehemu ambayo bacteria wanaishi pia. Kwa hiyo utunzaji wa meno ni muhimu

ili kulinda afya. Bakteria wa mdomoni wanaweza kutoboa meno yako.

Kutoboka kwa meno kunaweza kusababisha maumivu makali. Meno yaliyooza yanaweza

kusababisha maambukizi ambayo yanaweza kudhuru sehemu nyingine za mwili wako.

SURA YA 5 | MABADILIKO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Piga mswaki meno yako angalau mara mbili kwa siku,au baada ya mlo na kabla ya kulala. Hii

inaweza kusaidia kuua bakteria ambao wanakula chakula kinachobaki mdomoni kati ya meno

yako na kusababisha kuoza kwa meno au kupata ugonjwa wa fizi. Kuweka meno yako safi

kunasaidia kuwa na uhakika wa kupumua hewa nzuri.

Unatakiwa kusafisha kila jino - kote mbele na nyuma ya mdomo wako. Pia unatakiwa kusafisha

katikati ya meno yako. Miswaki na dawa za meno ni nzuri, lakini kama huna dawa ya meno

unaweza kusafisha kwa maji tu. Unaweza pia kusafisha meno yako kwa kutumia chumvi kidogo

na maji, ili kulinda ufizi na maambukizi ya mdomoni.

Unatakiwa kuepuka kula vyakula vyenye sukari na soda. Licha ya kwamba vinalishe kidogo,

vina sababisha kuoza kwa meno. Ni muhimu kuepuka kuchangia miswaki kwa sababu inaweza

kueneza maradhi.

chunuSi

Wakati wa balehe, tezi za mafuta katika mwili wako zinakuwa hai zaidi, na zinaanza kutoa vitu

vyenye mafuta vinavyoitwa sebum. Unazo hizi tezi za mafuta katika mwili wako wote; zipo zaidi

kwenye uso wako, shingoni, mabegani, kifuani na mgongoni.

Sebum ni vitu vizuri kwa sababu vinasaidia kuufanya mwili wako uwe laini, nyororo na uonekane

kijana. Japokuwa, wakati wa balehe, tezi zako za mafuta zinaweza kutoa sebum nyingi, na

kuwepo sebum kwa wingi kunaweza kusababisha kuziba kwa vitundu vidogo vidogo vilivyopo

katika ngozi yako. Hii inaweza kusababisha matatizo, kama chunusi.

Kuwepo kwa mafuta katika ngozi yako, na kuwa na sebum za ziada zinazotolewa kipindi cha

balehe, inaonyesha ni jinsi gani ambavyo unaweza kupata matatizo ya ngozi. Kuwa na chunusi ni

kitu cha kawaida kwa hakika, angalau vijana 8 kati ya 10 wana chunusi wakati wa ujana balehe.

Chunusi kwa kawaida zinatokea katika umri wa kati ya miaka 14 na 17, lakini hutokea vilevile kwa

watu wazima, wavulana na wasichana.

Baadhi ya vijana wana chunusi nyingi - tatizo linaloitwa “acne”. Chunusi zina kawaida ya kutokea

kutegemeana na familia. Kama wazazi wako au kaka na dada zako walikuwa na chunusi, utakuwa

katika nafasi ya kubwa ya kuzipata. Zinaweza kuendelea kuwa tatizo kwa baadhi ya watu hata

baada ya ujana kupita.

Presha za maisha zinaweza kusababisha chunusi. Vijana wengi wanajikuta wana chunusi

nyingi hususani wakati wa matukio muhimu kama, mitihani, miadi au kitu chochote ambacho

kitamsisimua.

Baadhi ya wasichana wanakuwa na chunusi nyingi wanapokaribia kipindi cha kupata hedhi.

Kuna porojo nyingi kuhusu chunusi, na watu wengine wanasema maneno ya uongo kama: “chunusi

ni dalili ya msichana au mvulana aliye ana hamu ya kufanya ngono.” Sio kweli, ngono haitibu

chunusi.

47

48

utaFanYa nini na chunuSi

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Chunusi ni jambo la kawaida kwa vijana balehe. Kwa bahati mbaya , hakuna jinsi tunavyoweza

kuzikwepa kabisa; wala hakuna matibabu ya ajabu ya kutibu chunusi. Hata hivyo, yapo mambo

kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ili kushughulikia chunusi.

Ni jambo muhimu sana kutunza ngozi yako, hususani kama unaishi sehemu zenye joto, vumbi

na unyevu unyevu. Unaweza kutumia sabuni ya kuogea na maji ya uvuguvugu kuosha taratibu

sehemu za mwili wako zenye mafuta – usoni, shingoni, mabegani, mgongoni na juu ya kifua.

Ukiosha sehemu hizi angalau mara moja kwa siku itasaidia kuondoa mafuta kwenye ngozi na

kusababisha vinyweleo kuwa safi na wazi.

Lakini usisugue sana ngozi yako au kutumia sabuni zenye nguvu na kali kwa sababu zinaweza

kusumbua ngozi yako na kusababisha chunusi zaidi. Kamwe usitumie sabuni za kufulia, sabuni

ya unga na dawa ya madoa, kwani zitaharibu ngozi yako. Jaribu kutoruhusu mafuta unayopaka

kichwani yasifike usoni kwa sababu mafuta haya yanaweza kuzuia vinyweleo vya ngozi yako.

Mwisho, kuwa mwangalifu na matumizi ya krimu za usoni na zile za kung’arisha ngozi. Ingawa

zimeandikwa kwamba ukizitumia ngozi yako itakuwa nyororo na nzuri, krimu zingine zinaharibu

ngozi kabisa. Kwa nyongeza, dawa nyingi za kulainisha ngozi zina vitu ambavyo si vizuri kwa afya

yako.

Ingawa wakati mwingine

unashawishika kuminya

chunusi,sio vizuri. Kama

utafanya hivyo, usaha

unaweza kutawanya

maambukizi kwenye

vinyweleo vingine, na

vilevile unaweza kupata

makovu ya kudumu.

Chunusi zinasumbua,

zinaweza kusababisha

maumivu na uchungu, na

zinaweza kuleta usumbufu

wakati mwingine. Lakini ni

sehemu ya ujana balehe.

Vijana wengi wanajihisi

Hata kama unafikiria kwamba chunusi zako ni mbaya, watu wengine

hawajaziona bado.

kuwa ni wao pekee wenye kusumbuliwa na matatizo ya ngozi, lakini hii ni kwa sababu hawajui

kwamba hata wenzao wa rika moja wanazo chunusi. Za kwako zinaonekana zaidi kwako

kuliko watu wengine wanavyoziona chunusi zako. Unaweza kudhani kilamtu anaziangalia, na

anaangalia ngozi yako mbaya tu na wala hakuangalii wewe. Lakini hii sio kweli. Watu wengine

wanayo mambo mengi ya kufikiria na kwa hakika wanachoangalia ni kujua wewe ni nani na wala

sio ngozi yako inaonekanaje. Kwa hiyo, usivunjike moyo na usiache chunusi chache zikunyime

raha! Hautakuwa nazo milele.

utunZaji Wa nYWele

Tunazo nywele mwili mzima, lakini zaidi kichwani, kwapani na maeneo yanayozunguka via vya

uzazi. Kutunza nywele zako ni sehemu nyingine ya kutunza usafi na kutunza vizuri mwili wako.

SURA YA 5 | MABADILIKO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Nywele zilizopo kichwani mwako ni rahisi kuzitunza hususani kama utakuwa unazipunguza kila

mara. Hata kama unakata nywele kila mara na kuzisuka, unatakiwa kuziosha ili zisiwe na vumbi

na ziwe safi. Kama uko shuleni, jaribu kutochangia chanio kwa sababu unaweza kupata chawa,

maambukizi ya fangasi, na minyoo. Kama utachangia vitana, hakikisha unaviosha vizuri kwa maji

ya moto yenye sabuni kabla na baada ya kutumia.

Watu wengine wana matatizo ya mba, hali ambayo inasababishwa na ngozi ya nywele kuwa kavu

mno.Mba unasababishwa na chembechembe ndogo za ngozi mfu, na watu wengine wenye mba

nyingi wanatumia shampuu maalumu zenye dawa ili kuzuia mba.

Ni vema kuoga mara kwa mara ili kuziweka safi nywele zilizopo kwenye mwili wako, nywele

zilizopo kwenye kwapa, na nywele zilizopo kwenye maeneo ya via vya uzazi. Kama ulivyosoma

sura ya 2 nywele hizi zinasaidia kuondoa jasho na uchafu kwenye mwili wako. Hata hivyo, sehemu

nyingine za Afrika watu wananyoa nywele hizi kwa vile wanajisikia vizuri bila nywele hizo.

Kama mila na tamaduni zako zinapinga kuwa na mavuzi yakate kwa kutumia mkasi. Usiziondoe

zote kabisa kwa kutumia krimu ya kuondolea nywele au kwa kunyoa. Mafuta ya kunyolea nywele

yanasumbua na kuumiza ngozi laini katika sehemu za siri. Pia kunyoa mavuzi kuna madhara

yake. Kama unanyoa mavuzi, uwezekano wa kujikata ngozi ni mkubwa. Iwapo utajamiiana,

mikato hii ni milango ya kupitishia VVU. Hii ni hatari. Tatizo lingine la kunyoa mavuzi ni wakati

mavuzi yanaota tena. Nywele zinakuwa na incha kali kiasi cha kuweza kutoboa kondomu. Vilevile

maeneo yanayozunguka via vya uzazi yaliyonyolewa yanaweza kupata maambukizi kidogo

kwenye vinyweleo au sehemu ambazo mavuzi yanaota. Kunyoa mavuzi kiasi ni salama kidogo,

lakini kuwa mwangalifu usiondoe nywele zote.

liShe nZuRi

Margareth, kutoka tanzania (umri; miaka 18,)

“Nilipokuwa darasa la sita, nilianza kuota nywele sehemu za siri. Mama

yangu aliniambia kuwa, zikikua na kuwa ndefu ninatakiwa nizipunguze na

kuzisafisha vizuri, la sivyo nitanuka.”

lois kutoka tanzania (umri; miaka 13)

“Nimeona nywele kwenye kwapa, kwa vile sio muda mrefu nilipoziona

sijazikata bado”

Lishe nzuri ni muhimu kwa afya njema. Kula chakula chenye virutubisho ni muhimu katika maisha

yote lakini ni muhimu zaidi wakati wa utoto na wakati wa balehe kipindi ambacho mwili wako

unakua na unaongezeka kwa kasi sana.

Mwili wako unahitaji chakula kizuri ili ukue na upate nguvu kwa ajili ya kufanya vizuri shuleni,

kucheza michezo na kufanya kazi.

Wakati mwingine vijana wadogo hawali mlo wenye lishe na wanasahau kula kwa wakati maalum

uliopangwa. Wanaweza kuacha mlo kamili na badala yake wakakazania kula biskuti, chips,

chokoleti, vitu vitamu na soda. Hivi vyakula havina lishe, na mwili wako unahitaji zaidi ya hivi ili

uwe na afya.

49

50

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kila aina ya chakula ina kazi yake mwilini kwa hiyo unahitaji kula milo yenye kila aina ya chakula.

Aina za msingi za vyakula ambayo mwili unahitaji ili uweze kufanya kazi vizuri ni:

“Vyakula vyenye wanga” au vyakula vyenye kuleta nguvu”: Vyakula hivi vinajumuisha ugali,

fufu, mihogo, viazi vitamu, viazi mviringo, mikate, mchele, ndizi, ulezi, na mtama.

“Vyakula vya kulinda mwili”: Vyakula vya kulinda mwili ndani yake vina vitamini na madini

muhimu ambayo mwili wako unahitaji ili uweze kufanya kazi vizuri na uwe na afya. Vitamini na

madini vinapatikana katika mboga za majani, (kama vile spinachi, majani ya maboga, kisamvu),

nyanya, maboga na karoti. Pia matunda ya aina zote kama, papai, embe, chungwa,na nanasi nayo

yana vitamini muhimu.

“Vyakula vya kujenga mwili”: Vyakula vya kujenga mwili vina protini. Protini husaidia mwili

wako uweze kukua na kujengeka vizuri, hususani wakati wa ujana balehe.Pia husaidia mwili wako

ujiponye na kujikarabati wenyewe ukiumia.

“Vyakula vya kujenga mwili” vinajumuisha karanga, njegere, maharage, kunde, nyama, kuku,

samaki wabichi, samaki wa kukaushwa na konokono. Mayai, maziwa, maziwa mgando na jibini

yana protini vilevile. Vyanzo vingine vya protini – nyama, samaki, maharage na njegere, pamoja

na mbogamboga za majani ya kijani kilichokoza – ni vyanzo vya madini ya chuma pia.Madini ya

chuma ni muhimu hususani kwa wasichana na wanawake kwasababu wanahitaji madini ya chuma

ya ziada wakati wakiwa katika hedhi na wakati wakiwa wajawazito.

Mafuta na vitu vitamu: Mafuta ni chanzo cha nguvu mwilini. Baadhi ya mafuta, kama vile ya karanga,

ya nazi, ya mawese yanatokana na mimea wakati mengine kama vile siagi au samli yanatokana

na wanyama. Mafuta yanaleta nguvu nyingi, lakini mwili unahitaji nguvu kidogo tu. Hivyo

basi, ukila mafuta mengi sana unaweza ukapata matatizo ya kiafya siku za usoni.Chanzo kingine

cha nguvu mwilini ni sukari. Kwa ujumla vitu vitamu ni vibaya kwa meno yako.

Fikiria kuhusu mlo wako na hakikisha unapata aina zote muhimu za chakula kama zilivyoonyeshwa

katika ukurasa wa 51, “Vyakula vya kuleta nguvu” vinatakiwa kuwa ni vya msingi katika mlo wako

na unatakiwa ule vyakula hivi. “Vyakula vya kulinda mwili ni muhimu sana pia, kwa hiyo kula kwa

wingi matunda na mboga mboga. “Vyakula vya kujenga mwili” ni muhimu sana, lakini huna haja ya

kula mara nyingi kwa siku. Mwisho ni vyema kula kidogo vyakula vya mafuta na vyakula vitamu.

NI KIASI GANI CHA NGUVU MWILI UNAHITAJI?

Nguvu unayohitaji inategemea na nguvu unayotumia. Ukuaji wakati wa balehe unatumia nguvu

nyingi. Kwa hakika kijana balehe anahitaji nguvu nyingi ukilinganisha na mtu mzima.

Nguvu inapimwa kwa kalori. Kama ukila vyakula vyenye nguvu zaidi kuliko mwili wako unvyohitaji

kwa siku, kiwango cha ziada cha karoli kitabadilishwa na kuwa mafuta na mwili wako utahifadhi

mafuta hayo kwa muda. Watu wengi hudhani kuwa na mafuta mengi ni afya njema na ni jambo la

kawaida, lakini inaweza kuwa ni tatizo kama ukiwa na mafuta mengi. Baadhi ya watu hususani

watu ambao wanakula sana vyakula vyenye kalori nyingi (vyakula vyenye mafuta na sukari) na

ambao hawafanyi mazoezi – wanakuwa wanene sana.

SURA YA 5 | MABADILIKO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Katika baadhi ya miji ya Afrika, wapo wavulana na wasichana wengi wenye uzito mkubwa kuliko

wanavyotakiwa wawe. Hii ni kwa sababu kufanya mazoezi katika miji ni vigumu. Pia vyakula

vingi vya kukaangwa huuzwa mijini. Vyakula vilivyokaangwa vinaweza kuandaliwa kwa haraka

na urahisi - vinaweza kuandaliwa haraka zaidi kuliko vyakula vya asili, kama vile maharagwe

na michuzi. Japokuwa chakula kilichokaangwa kinaweza kuwa na ladha nzuri na kinaweza

kuandaliwa haraka, sio kizuri kwa afya njema. Mlo wa chakula kilichokaangwa kinaweza

kuwafanya watu wawe wanene sana na baada ya muda mrefu, kinawadhuru moyo na mishipa ya

damu.

Jaribu kuepuka kula chakula chenye mafuta na kilichokaangwa. Vilevile epuka chakula na

vinywaji vyenye sukari.

MaZOeZi

Lishe bora inajumuisha mchanganyiko wa vyakula vya aina tofauti, kwa viwango tofauti

Kila mtu anahitaji mazoezi: Watoto, vijana, wazee – wasichana na pia wavulana. Mazoezi

yanakufanya uwe mzuri ung’ae, mwenye umbo zuri na macho maangavu. Yanakufanya uwe

mwenye nguvu kwa sababu yanaimarisha moyo wako na mapafu; hujenga misuli na unene wa

mifupa yako. Yanakufanya uwe na uwezo zaidi wa kupambana na magonjwa kwa kuongeza nguvu

ya mfumowa kulinda mwili.

nfune kutoka Zambia (umri; miaka 13)

“Nina afya nzuri kwa sababu nakula mlo kamili na ninafanya mazoezi

kwa wingi.”

51

52

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mazoezi yana faida nyingine zaidi, yanaimarisha hisia

zako, yanajenga kujiamini, yanakufanya ujisikie vizuri.

Kama unajihisi kuwa na mfadhaiko, hali mbaya au

huzuni, tembeatembea au cheza mchezo wa kurusha

mpira.Fanya mchezo wa kukaa na kunyanyuka. Cheza

mpirawa pete. Endesha baiskeli, ruka kamba, ogelea,

Cheza mpira wa wavu au mpira wa meza. Fanya kitu

chochote kitachofanya moyo wako uende kasi ili

kuongeza morali.

Mazoezi yanaweza pia yakawa njia nzuri ya kukufanya

uwe hodari katika stadi muhimu za maisha, kama

kujiamini, ushirikano na kufanya kazi kwa pamoja. Watu

wengi kwanza hujifunza stadi hizi wakati wakicheza

michezo au wakati wanapojiunga na timu.

Kufanya mazoezi mengi haimaaanishi kuwa lazima

ujiunge na klabu ya michezo. Kusaidia kazi za shambani,

kwenye bustani au kuzunguka nyumba yanaweza kuwa mazoezi mazuri. Shughuli za nyumbani

zinaweza kujenga mahusiano mazuri na wazazi wako.

Baadhi ya watu ni wakimbiaji wazuri lakini wengine

sio. Baadhi ya watu wana vipaji maalum vya mpira

wa miguu, kukimbia kwa kasi au kuogelea vizuri,

kama vile ambavyo watu wengine ni wazuri katika

hisabati au katika kujifunza lugha. Hata kama wewe

si mkimbiaji, unatakiwa kufanya mazoezi kwa wingi.

Kila mtu ana mwili ambao unatakiwa autumie. Kwa

mfano kwa kujinyoosha, kusukuma au kujaribu

mambo kadhaa. Unaweza kujikuta unapofanya

mazoezi unafurahi zaidi na zaidi. Unaweza ukawa

mwana riadha bila ya wewe mwenyewe kujua!

Iwapo hujazoea kufanya mazoezi, inaweza kuwa

vigumu unapoanza. Unaweza kujikuta unashindwa

kupumua wakati wa kukimbia. Mazoezi yanaweza

Kuna njia nyingi nzuri za kufanya mazoezi kukufanya ujisikie vibaya na hivyo kutoendelea

nayo. Kwa hiyo, anza taratibu. Tafuta mchezo

unaoupenda na jenga nguvu zako, hivyo unaweza

kufanya zaidi na zaidi. Nia ni kufanya moyo wako uende kasi, kujisikia kwamba unapumua

haraka kuliko kawaida, na kuwa na joto mwilini. Jaribu kufanya hivi kwa angalau dakika 20, mara

3 kwa wiki.

Fanya mazoezi yako kila mara na utaona maendeleo mazuri.Ngozi yako itang’aa. Macho yako

yatang’aa, utakuwa na furaha na raha. Utajiamini zaidi na kuwa na uwezo wa kuyakabili matatizo.

Na kwa hakika utakuwa na nguvu na mwenye afya pia. Kwa hivyo endelea na mazoezi na usiache

kufanya ati kwa sababu ni kipindi cha mitihani.Wakati wa mitihani ndio unahitaji kufanya mazoezi

zaidi.

SURA YA 5 | MABADILIKO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Ruvimbo kutoka Zimbabwe (umri;miaka 13)

“Naendesha baiskeli ili kujishughulisha na

kwa sababu za kiafya. Vijana wanatakiwa

wajishughulishe, Dunia ina mambo mengi ya

kufanya.”

Godfrey, kutoka Zimbabwe (umri; miaka 19)

“Napenda michezo, Nacheza mpira wa kikapu

kuuweka mwili wangu imara na wenye afya

nzuri.”

Maumbile mazuri hupatikana kwa kufanya mazoezi;

maumbile mabaya husababisha maumivu katika kifua na mgongo.

MaPuMZiKO MaZuRi

endelea na mpangilio wako wa mazoezi na

utaona tofauti !

Pamoja na chakula kizuri na mazoezi ya kutosha, unahitaji kupumzika vya kutosha. Kupumzika

kunaruhusu mwili kuhifadhi zaidi nguvu. Kupumzika kunaweza kuwa katika hali ya kupumzika

kimwili au kulala usingizi

Tumia muda kupumzika kila siku kwa kusoma kitabu, kufanya kitu unachofurahia, kusikiliza redio,

au kwa kutafakari maisha yako. Kwa kiwango kidogo, televisheni inaweza kukufanya upumzike,

lakini usitumie muda mwingi kuangalia televisheni au video.

Kulala ni njia muhimu ya kupumzika. Ni wakati wa kulala tu ndio moyo wako unapunguza mapigo

na misuli yako inapumzika. Hii inaruhusu mwili wako kurudisha na kujiponya na hali ya mfadhiko

au majeraha. Unahitaji kulala sana kipindi cha balehe kwa sababu mwili wako unatumia nguvu

nyingi. Watu wengi wanahitaji kama kiasi cha masaa 8 ya kulala usiku mmoja. Baadhi ya watu

wanahitaji pungufu, na baadhi ya watu wanahitaji zaidi. Kama, unajisikia kuchoka muda wote,

hakikisha unakwenda kulala mapema. Mabadiliko yote yanayotokea mwilini mwako yanachosha,

kwa hiyo hakikisha unaupa mwili wako nafasi ya kupumzika!

53

54

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 5

MAMBO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Kuna vitu vichache, rahisi na vya msingi unatakiwa kuvijua kuhusu kutunza mwili wako.

Utakapofikia kipindi cha balehe, utaanza kutoa jasho zaidi. Kuoga kutakufanya uwe

msafi na kunukia vizuri

Osha meno yako angalau mara mbili kwa siku ili kuepuka meno kuoza na pia ili utoe

pumzi nzuri.

Kama tezi zako za jasho, zinatoa mafuta, unaweza kuwa na chunusi. Chunusi ni sehemu

ya ujana balehe na hakuna njia ya kuziekwepa. Kuuweka mwili wako safi kwa kuoga na

maji na kutumia sabuni ni suluhisho lakini usisugue ngozi yako sana, na usitumie sabuni

ya kufulia kwa sababu itaharibu ngozi yako

Kula mlo wenye lishe ukiwa na vyakula vya “kulinda” na “kujenga mwili”. Epuka kula vitu

vyenye sukari na vyakula vilivyo kaangwa

Fanya mazoezi ya kutosha. Mazoezi yanaimarisha moyo wako, mapafu, na misuli,

yanakuweka imara na yana amsha ari.

Mabadiliko yote unayoyapitia ni muhimu sana, kwa hiyo upe mwili wako nafasi ya

kupumzika kiasi cha masaa 8 kwa usiku.

Kwa kujizoesha kuwa msafi, kula vizuri, kufanya mazoezi vizuri na kupumzika, utaruhusu

mwili wako kufanya kazi vizuri, utajisikia vizuri, kimwili na utajisikia vizuri kiakili.

Utunzaji Afya Ya Akili

Na Moyo

Sura hii inahusu afya ya hisia zako. Afya ya hisia inahusisha mambo mengi, kama kujipenda,

kujiamini, kustahimili wasiwasi, mfadhaiko, na huzuni na kuelewana na watu wengine. Kuwa

mwenye afya nzuri ya hisia maana yake ni kujisikia vizuri wewe mwenyewe. Vile vile maana yake

ni kuwa na nguvu za ndani za kuweza kustahimili raha na shida katika maisha.

Madaktari hawajajua ni kwa nini mtu awe na afya nzuri kihisia na mwingine asiwe nayo.

Inawezekana ni mchanganyiko wa haiba ya kuzaliwa nayo na namna ambavyo ulilelewa ukiwa

mtoto mdogo. Afya nzuri kihisia inategemea pia na mtazamo wako - je upo tayari kutengeneza

afya yako iwe nzuri kihisia?

Kila mtu anaweza kujitahidi awe na afya nzuri ya kihisia. Hii inamaanisha kujienzi na kujiamini.

Vile vile ina maana ya kujenga stadi ili kumudu wasiwasi, mfadhaiko na huzuni. Vile vile

inamaanisha kujenga mahusiano na watu wengine.

KujiheShiMu

Kamusi ya “Oxford inatafsiri “Kujiheshimu” kama “mawazo” mazuri kuhusu tabia ya mtu

mwenyewe” Iwapo unajiheshimu sana, maana yake ni kwamba unajisikia vizuri.Unajua kwamba

unayothamani - mtu unayestahili

kupendwa. Unajiheshimu mwenyewe. Hisia

za namna hii ni nzuri sana, unapojihisi

kupendwa na kuheshimiwa unategemea

hivyo hivyo kutoka kwa watu wengine

vilevile.

Unapojiheshimu sana haina maana ya

kwamba wewe huwezi kujichukia au

kujikasirikia mwenyewe. Kuna wakati kila

mtu hukata tamaa, lakini yule mwenye

kujiheshimu anakubali makosa na kusonga

mbele.

Kujiheshimu ni tofauti na kujidai au kuwa

na majivuno mengi.Watu wanaojienzi

wanajipenda, lakini haina maana ya kwamba

wanajifikiria wao hawana dosari yoyote, au

wao ni bora kuliko wengine.

55

SURA YA 6

56

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kujienzi ni kitu ambacho kipo ndani yako. Lakini hiyo haimaanishi huwezi kuifanyia kazi au

kuhitaji kuikuza na kuijenga. Unaweza kuzingatia yafutayo ili ujenge tabia ya kujienzi:

JE UNAJUA Maana ya kuwa na Afya nzuri kihisia?

Inaweza ikawa vigumu kuelezea afya nzuri ya kihisia. Lakini kawaida utaijua kwa kuona.

Kwa mfano tumchukulie Rose, anaelekea kuwa na furaha wakati wote na anaonekana

kuyamudu maisha ya raha na tabu.

Anapopata maksi za chini anakubaliana nazo na anaongeza bidii.

Akiachwa na mpenzi wake, analia lakini baadaye anaamua kwamba siyo mwisho wa

dunia.

Kipindi cha mitihani, huwa hafadhaiki sana. Hufanya mazoezi na kuzungumza na rafiki

yake mpenzi kukabili mfadhaiko.

Rose anajienzi sana. Hashindwi na hisia anapoachwa na mpenzi wake. Hujitambua kama ni

mtu muhimu. Vile vile anajiamini sana. Ni kweli kwamba alifanya vibaya kwenye majaribio,

lakini anajua anaweza kufanya vizuri zaidi. Hahitaji kumlaumu mwalimu. Njia anayotumia

kupambana na mfadhaiko ni nzuri. Michezo na kumwambia rafiki anayemwamini matatizo

yanayomsibu kunamsaidia kushughulikia wasiwasi na kisha kusonga mbele.

Aidha, watu wengine wanapata shida sana kumudu raha na shida za maisha. Kwa mfano

Emma, ambaye yuko katika mazingira yanayofanana na ya Rose, hufanya kila kitu tofauti.

Hakubali kukosolewa badala yake humlaumu mwalimu kwa kupata alama mbaya.

Akiachwa na mpenzi wake anafadhaika. Hutangaza mambo ya uongo kuhusu mvulana

huyo na huanza kufanya mbwembwe na wavulana wengine.

Anapokuwa na mfadhaiko anaanza kunywa pombe na kuvuta sigara.

Inakuwaje Emma anapata shida sana kuyamudu matatizo haya? Jambo mojawapo ni

kujienzi. Anaumia sana anapoachwa na mpenzi wake na anayamudu maumivu kwa

kumsema rafiki yake vibaya. Anajaribu kujihakikishia kwamba bado anapendwa kwa

kumpenda mvulana mwingine. Njia yake ya kupambana na mfadhaiko haifai kabisa, pombe

na sigara vinaweza kukusahaulisha kwa muda lakini havitatui tatizo.

Epuka kujilinganisha na wengine mara kwa mara. Weka malengo yako, na usijihukumu

mwenyewe kwa kuangalia mafanikio ya mtu mwingine. Maisha ni safari ndefu. Kuna wakati

utaenda mbele na wakati mwingine utarudi nyuma.

Tambua vipaji vyako na kujikubali vile ulivyo.Tengeneza orodha ya mambo unayoyafanya

vizuri. Je wewe ni msanii? Mwanariadha.Mwimbaji, msimuliaji wa hadithi au mnenguaji

(mcheza dansi) Ni masomo gani unayofanya vizuri shuleni?

Fikiria wewe ni mtu wa aina gani na kutengeneza orodha ya sifa ulizonazo. Unapenda nini

kuhusu wewe mwenyewe? Wema wako? Ucheshi? Ubunifu? Umakini?

Fahamu mambo yanayokuhusu ambayo ungependa kuyaboresha, lakini usijikosoe sana.

Kuwa mhalisi na weka malengo ambayo yanatekelezeka na yatakayoonyesha mafanikio ili

uridhike unapoyakamilisha.

Jiamini, na jiambie “ninaweza!”.

Tumia muda wako na watu wanaokujali wanaofanya ujisikie vizuri na kuongeza hadhi ya

kujiheshimu. Kaa mbali na watu wanaojaribu kuharibu heshima yako, hasa kama wanafanya

hivyo kwa sababu fulani.

Kwa vyovyote vile kuifanyia kazi heshima yako haina maana kuwa hutaweza kupata matatizo.

Kuifanyia kazi heshima yako itakusaidia matatizo kuwa mepesi. Kujiheshimu kunakulinda wewe

binafsi. Wakati mtu anakutendea vibaya hisia za kujiheshimu zinapiga kelele “Hee! haya ni

makosa, usiruhusu mtu huyu akakutendea hivi”.

Hebu fikiria kana kwamba marafiki zako wamekuacha. Wamejiunga pamoja na kukuacha peke

yako. Ghafla unajisikia kutetemeka na huna uhakika wa mambo yako. Ni kwa nini hawakutaki

tena? Je kuna makosa umefanya? Heshima yako inaanza kufifia kama ua linavyonyauka.Unaanza

kujisikia vibaya.

Katika mazingira ya namna hii, watu wengine hupata hofu. Wanachukua njia rahisi ya kurudisha

heshima inayoshuka ili apendwe tena, hata kama itamaanisha kufanya jambo ambalo wanafikiria

ni kosa. Kwa mfano, vijana wengine ambao wamekataliwa na marafiki zao wa zamani huanza

kujiunga na makundi ya vijana wanaokunywa pombe, wanaovuta bangi na kujiingiza kwenye

matatizo makubwa. Hivyo wanaanza nao kula madawa ya kulevya, kunywa pombe ili waweze

kukubalika.

Ni vizuri kutafuta kukubalika na kweli inapandisha hadhi lakini haisaidii kutatua matatizo ya

kujiheshimu na wala kukubalika hakudumu. Unaweza kujisikia vizuri kwa muda lakini baada

ya muda mfupi sauti ndogo ndani yako huanza kukusumbua: “Watu hawa hawako makini”. Sauti

hii ni kwamba haujawa mkweli kwako mwenyewe, unajizuia kufanya mambo unayoyataka na

unayoyaweza. Hujisikii vizuri kutokana na yale unayoyafanya kwa mkumbo...” Hiyo sauti ndogo ni

nafsi yako. Ni vema wakati wowote kuisikiliza.

Kurekebisha kujienzi kwako ni kazi kubwa kuliko kujiunga na makundi mapya, au kupoteza

mawazo kwa kutumia pombe, na madawa ya kulevya, (kwa taarifa zaidi kuhusu madawa ya

kulevya na pombe soma sura ya 12). Itakusaidia zaidi kurekebisha kujienzi kwako. Unapopitia

matatizo ya kujienzi, yafuatayo ni mambo machache unayoweza kuyafanya ili yakusaidie:-

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Jaribu kuliweka tatizo lililopo katika mtazamo sahihi. Jaribu kukumbuka kwamba dunia

imejaa mambo ya raha na shida, na kwamba huu sio mwisho wa dunia.

Zungumza na mtu wa karibu yako na unayemwamini kuhusu matatizo yako na hisia

zako. Mtafute kijana mtoa ushauri nasaha au mtu ambaye anakujali na ambaye anaweza

kukusaidia.

57

58

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kumbuka kuwa watu wengine wanakuthamini kutokana na vile ulivyo. Mtafute mtu ambaye

atakuthamini – rafiki mpya, mwalimu, dada, kaka, mzazi au ndugu mwingine.

Kuwa mvumilivu. Kujiheshimu hakujengeki katika siku moja.Unaweza kujisikia vizuri baada

ya siku kadhaa.

KujiaMini

Unapokuwa unajenga kujienzi, unajenga kujiamini pia. Kujiamini ni jambo la msingi katika afya

ya kihisia. Kama kujienzi maana yake kujisikia vizuri na ukamilifu kuhusu tabia yako na namna

ulivyo, kujiamini maana yake kujisikia vizuri kuhusu uwezo wako wa kufanya mambo.

Kujiamini ni jambo kubwa. Watu wanaojiamini

wanajisikia huru kujaribu kufanya mambo

mapya bila ya kuwa na wasiwasi mkubwa

kama watashindwa. Hawaogopi kujiingiza

katika mazingira mapya na kati ya watu wasio

wafahamu. Hawajali hata kidogo watu wengine

watawafikiriaje.

Kujiamini kunavutia sana. Watu wanaojiamini

mara kwa mara wanapendwa sana kwa sababu

wanaonekana kufurahia maisha kwa kiwango

kikubwa wanapopata changamoto mpya na

uzoefu wa mambo mapya.

Kujiamini kunajitosheleza. Kwa maneno mengine,

kujiamini kunasabisha kujiamini zaidi. Hii maana

yake ni kwamba kwa jinsi unavyojaribu kufanya

mambo mapya ndivyo unavyozidi kujiamini. Hii

inasababishwa na sababu mbili zifuatazo:

1. Unajifunza kwamba unaweza kufanikiwa katika mambo mengi ambayo hukuwahi kufikiria

ungeweza.

2. Unajifunza kwamba hata kama unashindwa kufanya jambo fulani hakuna neno.

Unapojiamini, wakati mwingine unaweza kushindwa, lakini mara nyingi utafanikiwa. Hii ni

kwasababu unaposhindwa kufanya kitu, mara kwa mara ni kwa sababu unakuwa na wasiwasi

au kiwewe. Unapojiamini hata hivyo unaweza kufanya mambo mapya. Kwa ujumla, wasiwasi na

kutojiamini hakuleti matatizo makubwa katika kuwa makini kwa lolote unalojaribu kufanya.

Lifanyie kazi suala la kujiamini, itakusaida maisha yako yote. Unaweza:-

Kujifikiria kama mtu unayeweza – yule ambaye unaweza kufanikisha.

Kujiamini kunakuwezesha kujaribu mambo

mapya bila kuhofu kushindwa

Jipe changamoto. Jaribu mambo mapya na uwe muwazi katika mambo ambayo hukuyazoea.

Jizoeshe kusema “sifahamu jinsi ya kufanya kile lakini ningependa kujaribu”

JE? Unafahamu kwa nini wasichana wana matatizo zaidi ya kujiheshimu na

kujiamini kuliko wavulana?

Wakati mwingine wasichana wana matatizo ya kujiamini na kujienzi kidogo kuliko wavulana

wa rika moja. Kwa nini iwe hivi? Je, kujienzi na kujiamini kunahusiana na jinsi ya mtu?

Jibu ni “Hapana” kujienzi na kujiamini hakuhusiani na jinsi ya mtu. Hata hivyo heshima na

imani ya mtu inaweza kuathirika sana kwa namna au jinsi anavyotendewa na watu wengine

– wazazi, wadogo zake, ndugu, walimu, majirani viongozi wa dini na viongozi ndani ya jamii,

n.k.

Kwa bahati mbaya katika utamaduni mwingine wavulana na wasichana wanatendewa

tofauti kabisa; na hii inaweza kuathiri sana namna wanavyojiona na uwezo wao. Kwa mfano;

katika familia zingine wavulana wanaweza kupewa nafasi zaidi katika elimu na mafunzo

ya kazi; na walimu wakati mwingine wanawajali zaidi wavulana. Kwa upande mwingine

wasichana wanaweza wasipate nafasi kama hiyo. Wanaweza wasiruhusiwe kucheza na

wenzao au kucheza michezo kama kaka zao wanavyofanya. Zaidi ya hapo kazi ngumu

wanazofanya nyumbani na shambani zinaweza zisionekane na wala zisitambulike. Matokeo

yake wasichana na wanawake hujiona hawana thamani na wanaweza kuanza kuamini

kwamba thamani yao ni ndogo kuliko ya wavulana na wanaume. Lakini hii sio kweli! Watu

wote ni sawa. Iwapo wote watapata nafasi sawa, wasichana wanaweza kufanya vizuri

shuleni, katika kazi na kitu chochote wanachotaka kufanya.

Inaweza kuwa vigumu sana kama wewe ni msichana na unaishi katika mazingira ambayo

mara kwa mara unajisikia huthaminiwi kama ambavyo mvulana anavyothaminiwa. Haya

hapa ni mambo machache ambayo unaweza kufanya ili kuimudu hali hiyo:

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Wakati wote kumbuka kwamba una thamani kubwa bila kujali watu wengine wanasema

nini. Wewe una akili na uwezo sawa na mvulana yeyote.

Jitahidi mara dufu katika kujenga kujienzi na kujiamini kwako.

Jisifu mwenyewe na ridhika unapofanya kazi vizuri. Usisubiri kusifiwa na watu

wengine ambao wanaweza wasikusifu.

Tumia kila nafasi uliyo nayo kujifunza stadi mpya na fanya mengi kati ya hayo.

Kumbuka, kila unapofanikisha jambo utakuwa unajihakikishia mwenyewe na watu

wengine kwamba unayo thamani kama ambavyo wengine walivyo nayo.

Tambua changamoto unazokumbana nazo; lakini usikate tamaa. Kama unaishi katika

jamii ambayo wanawake wanadharauliwa sana usitegemee hali hiyo kubadilika katika

siku moja, lakini hata hivyo lisikufanye ukate tamaa.

Zungumza na wazazi wako au mtu mzima yeyote anayejali. Kwa mfano; kama wazazi

wanataka kukuachisha shule au wanataka uolewe jaribu kutafuta mtu wa kuzungumza

naye. Eleza namna elimu ilivyo ya muhimu kwako na waombe kama wanaweza

kukusaidia kumudu hali hiyo.

59

60

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kuwa mcheshi. Usiruhusu aibu au wanachofikiria watu wengine iwe ni sababu ya kutofanya

mambo mapya.

Vione vikwazo kama ni nafasi ya kujaribisha na kujifunza mambo mapya, Fikiria mwenyewe

“sawa, nitalishughulikia vipi tatizo hili?”

Ukishindwa kitu, kuwa na mtazamo sahihi. Usiwe na wasi wasi au kuchukizwa nalo. Fikiria

kosa limetokea wapi na ungefanya nini cha tofauti safari nyingine. Halafu achana nacho.

uSiWe na WaSiWaSi, FuRahi

Umewahi kusikia wimbo wenye maneno ya kichwa cha habari hapo juu? Sauti yake ni rahisi na

inavutia. Unadhani ni rahisi kuwa na furaha? Hata hivyo kila mtu anao wasiwasi, na vijana balehe

wana wasiwasi mwingi – wasiwasi kuhusu wao wenyewe namna wanavyoonekana, rafiki zao,

mafanikio shuleni, maisha ya baadaye, n.k.

Wasiwasi unaweza kukukosesha raha. Kwanza jiulize kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi huo.

Mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi usiokuwa wa lazima. Yapo mambo mengine ambayo

hayahitaji kuwa na wasiwasi nayo, kama haya yafuatayo:

Mambo ambayo huna uwezo wa kuyabadili, kama vile sura yako, rangi ya ngozi yako, umbile la

nywele na ukubwa wa matiti au uume. Huwezi ukabadilisha vitu hivi, kwa hiyo ni vema kuvikubali

kama vilivyo. Wewe ni mzuri kama ulivyo. Isitoshe

ni haiba yako ndiyo inakufanya uwavutie watu

wengine. Lenga katika wewe ni nani na wala sio

unavyoonekana.

Mambo ya dunia ambayo huna uwezo nayo.

Unaona gauni zuri dukani. Usibabaike kwa sababu

huna uwezo wa kulinunua. Utahitaji mshahara wote

wa mwezi mmoja kutoka kwa baba yako ili uweze

kulinunua. Kwa kuongezea, hata kama ungelipata

gauni hilo ungejikuta baada ya miezi michache

unahitaji gauni lingine, na hata zaidi. Mambo

ya dunia hayaleti furaha wala kuwa mwisho wa

matatizo; kwa hiyo lenga katika mambo ambayo

yako ndani ya uwezo wako. Ridhika jinsi ulivyo na

kile ulichonacho.

Kama tu ningepata gauni lile zuri, ningekuwa

na furaha zaidi…”

Kutokuwa na rafiki wa kike au kiume. Watu wengine hupata rafiki wa kike au wa kiume kipindi

cha ujana balehe. Lakini wengine hawampati mtu huyo maalumu mpaka baadaye sana katika

maisha. Kwa kuongezea, mapenzi ya vijana hayadumu sana. Inaweza kuchukua muda kumpata

mpenzi wa moyo.

Hivyo kuwa mvumilivu usikimbilie katika mahusiano ati kwa sababu unafikiri unahitaji kuwa na

rafiki wa kike au kiume wakati huo.

Shinikizo kutoka kundi rika ili kufanya kitu ambacho hutaki kukifanya: Fanya mambo yale

tu ambayo unafikiri ni mazuri kwako. Hata siku moja usiruhusu tamaa ya kuwafurahisha watu

wengine ikufanye wewe utende yale ambayo huyataki na unafikiria ni makosa.

• Kuwa mpweke: Upweke ni jambo ambalo

linampata mtu yeyote kwa wakati fulani katika

maisha. Kutatokea muda mfupi utakapojisikia

kama huna mtu yeyote wa kuzungumza naye

au hakuna mtu ambaye anakuelewa vizuri. Kwa

kawaida nyakati kama hizi hudumu kwa muda

mfupi na kila mtu anazipitia.

Lakini bila shaka zipo hali ambazo unastahili kuwa na

wasiwasi nazo. Kwa mfano:

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Wazazi wako hawezi kukulipia karo ya shule na

hujui uende wapi kuomba msaada.

Hili ni tatizo kubwa ambalovijana wengi wanalipata. Zungumza na Mwalimu au mshauri

katika kituo cha vijana kilichopo katika eneo lako kama wana maoni yoyote. Vilevile

zungumza na viongozi wa dini au viongozi wa kijiji ili kuona kama wanamfahamu mtu yeyote

ambaye anaweza kutoa msaada. Labda unaweza kubadilisha shule yenye karo nafuu au

kutafuta kazi ya kufanya mwishoni mwa wiki ili kupata pesa.

Wewe na rafiki yako wa kike mlifanya mapenzi yasiyo salama na sasa anafikiria huenda

akawa amepata mimba.

Huu ni wasiwasi mkubwa. Jambo zuri la kufanya ni kwenda kliniki kupima mimba na kupata

ushauri. Nenda na rafiki yako wa kike kwa ajili ya kumpa moyo. Kama ni mja mzito, usikatae

kwamba sio mimba yako. Wote mnawajibika (angalia sura ya 11 kwa taarifa zaidi kuhusu

mimba).

umesikia tetesi kwamba mmojawapo wa marafiki zako wa zamani ana uKiMWi. huna

uhakika kama ni kweli, lakini je upime?

Huu nao ni wasiwasi mkubwa. Ndio, nenda kwa washauri nasaha na upimaji ili uweze kutuliza

akili yako au uchukue hatua zinazostahili. Nenda na mtu mmoja kwa ajili ya msaada (angalia

sura ya 10 kwa ajili ya taarifa zaidi kuhusu VVU (UKIMWI).

Mtu mzima au mwanafunzi mwenzako amekuwa anakupatia zawadi ndogo ndogo na

starehe. lakini sasa anataka mfanye ngono. anasema anakudai pesa nyingi ambazo

amekuwa anatumia kwa ajili yako.

Usikubaliane na shinikizo hilo. Unaweza kuishia kupata mimba kwa makosa na kuachwa na

mwanaume au mvulana. Kaa mbali naye. Kuwa jasiri na zungumza na wazazi wako, shangazi

au mtu yeyote mzima kuhusu hali hii. Usijaribu kumudu jambo hili peke yako.

Katika hali mbaya kama hizi wasiwasi unaweza kukusaidia. Unahitaji kufikiria sana chaguzi

zote ulizonazo ili kumudu tatizo, halafu unahitaji kuzipima chaguzi na matokeo yake ili uweze

kufanyia kazi yale yanayokufaa.

Hata hivyo wasiwasi juu ya hali mbaya kama hizi unaweza kukuongezea mfadhaiko, yaani pale

unapoanza kujisikia umeelemewa na matatizo yako na wasiwasi. Unapokuwa na mfadhaiko

mwili wako utatoa ishara: Huwezi kuacha kufikiria tatizo. Moyo unadunda kwa nguvu. Unaweza

ukajisikia unakosa hewa. Tumbo linaweza kukuuma. Unaweza kukosa usingizi au unaweza

kuota ndoto mbaya (kupata jinamizi). Unaweza kuwa msahaulifu. Iwapo unazipata dalili hizi za

mfadhaiko chukua hatua zifuatazo:

61

62

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

• Vuta hewa kwa nguvu. Iwapo umefadhaika sana

na unajisikia kukosa hewa na kichwa chepesi, acha

kufanya kile ulichokuwa unafanya na polepole vuta

hewa nyingi, ukiizuia hewa ndani ya mapafu yako

kwa sekunde chache kabla hujaitoa.

• tafuta chanzo cha mfadhaiko Je, unaweza

kuupunguza mfadhaiko? Je, umefaidhaika na

kitu ambacho hustahili kuwa na wasiwasi nacho?

Tengeneza orodha ya vitu vyote vinavyosababisha

uwe na mfadhaiko halafu iangalie kwa makini. Je,

majukumu yamezidi? Je unaweza kufanya lolote ili

kupunguza orodha yako?

• Zungumza na watu. Hakuna haja ya kutatua

matatizo peke yako. Watu wengine wamepitia

wakati mgumu kama wewe na wanaweza kutambua Usijaribu kumudu wasiwasi wako

peke yako. Zungumza na mtu.

namna ya kushughulikia tatizo lako. Anaweza

kuwa mzazi wako, shangazi au wajomba , kaka

au dada, rafiki wa karibu, mwalimu, jirani, mfanyakazi wa afya, kijana mshauri nasaha,

kiongozi wa dini na mzee wa kijiji. Hawa ni watu wachache ambao wanaweza kukupa ushauri.

Wanaweza kupendekeza ufumbuzi ambao hujaufikiria.

• Fanya mazoezi.

Kimbia, cheza mpira wa miguu au tembea haraka haraka, ogelea. Mazoezi ni

njia nzuri sana ya kushinda mfadhaiko.

• Pata usingizi wa kutosha. Jaribu kwenda kulala ukiwa na hali nzuri ya akili. Epuka kuangalia

televisheni (luninga) kabla ya kwenda kulala. Jaribu kupumzisha misuli yote mmoja baada ya

mwingine kadri unavyolala kitandani.

• Kula chakula bora, Zingatia kupata kifungua kinywa, na milo yote ya siku.

• tumia kusali au kutaamali. Hii ni njia nzuri ya kujituliza mwenyewe na kumudu mfadhaiko.

Sala zimejaa mategemeo na hekima kuhusu namna ya kuyaendesha maisha yako ya kila siku.

• Fanya kile unachokifurahia – Hivi ni vitu ambavyo vitakufanya uondokane na mawazo ya

kuwa na wasiwasi, kama kutumia muda wako na rafiki wa karibu, kuchora, kuimba, kulima

bustani, kupika, kusikiliza muziki n.k.

Zifuatazo ni njia chache za kupambana na mfadhaiko ambazo unatakiwa uepukane nazo:

Kutumia pombe na madawa ya kulevya kama njia ya kutuliza mawazo. Hii sio dawa. Pombe

na madawa ya kulevya vinatuliza zile sehemu za ubongo ambazo zinasaidia kufikiria na

kudhibiti tabia yako. Pombe na madawa ya kulevya vinaweza kukufanya utende mambo

ambayo baadaye utayajutia.

Kuficha hisia zako na kuyaweka matatizo yote ndani ya roho yako hakuwezi kukusaidia

kuyamudu na wala kumaliza mfadhaiko wako. Mwisho wake utajisikia kama unayetaka

kupasuka.

Kuhamishia mfadhaiko wako kwa watu wengine. Jihadhari mfadhaiko wako usije ukakufanya

kuwa na kiburi, mkali au mbaya kwa watu wengine. Hii itakufanya wewe mwenyewe ujisikie

vibaya zaidi.

Njia hizi za kukabiliana na mfadhaiko sio nzuri na wala hazifai. Zitazidisha ugumu wa maisha yako

na zinaweza kukuongezea mambo mengine mabaya zaidi ya kukufadhaika. Mfadhaiko ni kitu

unachoweza kukidhibiti, kwa hiyo usiruhusu ukutawale.

KuMuDu huZuni

Wakati mwingine matatizo yanaweza kukufanya ujisikie mnyonge na ukashindwa kupata njia

ya kuyaweka maisha sawa. Hivyo kula matunda na mboga mboga, kucheza michezo na kulala

usingizi wa kutosha kutakufanya ujisikie vizuri zaidi.

Wakati mwingine unayo kila sababu ya kuwa na huzuni. Kwa mfano; ukifiwa na mtu wa karibu

sana, utasikitika sana. Unaweza ukamkumbuka marehemu sana na kupata hisia kali ya

kuhuzunika. Kama umefiwa na rafiki yako wa kiume au wa kike unaweza kujisikia mpweke sana,

na unaamini kuwa hutaweza kumpata mtu mwingine kama yeye.

Kupotelewa kwa namna hii ni kugumu, lakini unaweza kuyakabili matatizo. Baada ya kipindi

cha huzuni, utajisikia uko tayari kuendelea na maisha. Ingawa masikitiko ya kumpoteza mtu

unayempenda yatabakia palepale, mwishowe utakuwa na furaha tena.

Lakini wakati mwingine watu wanakuwa na huzuni kubwa kiasi cha kutoyatamani maisha tena.

Wanadhani maisha hayana maana tena na hakuna faida yoyote ya kuishi. Wanajisikia watupu na

hawafai kabisa. Wanajisikia hawana raha. Wanajiona wamepoteza mwelekeo.

Hisia hizi za kuwa na huzuni sana na kujiona hufai zinaitwa “unyong’onyevu”. Kunyong’onyea au

kuvunjika kwa moyo kunaweza kukasababishwa na jambo linalohuzunisha kama kifo, lakini

mara kwa mara watu wanaopatwa na tatizo hili wanapata shida kutambua sababu maalumu

au kilichosababisha kuvunjika kwa moyo. Matokeo yake wanapata tabu kutambua kama

wamevunjika moyo. Wanaweza kugundua mabadiliko mbalimbali yakiwatokea, kama vile:

Kuwa na huzuni wakati wote.

Kukosa nguvu.

Kushindwa kufikiri vizuri.

Kuumwa kichwa mara kwa mara na matatizo ya tumbo.

Kushindwa kufurahia mambo ambayo mwanzo yalikuwa yanafurahisha.

Mabadiliko katika ulaji, (kama vile kula pelemende) au unywaji (kunywa pombe ili kujaribu

kusahau matatizo).

Je, umewahi kujisikia hivi au kuona mabadiliko kama haya yakimtokea rafiki yako? Kuvunjika

moyo ni jambo la hatari, iwe ni wewe mwenyewe au rafiki yako, hivyo chukueni hatua zifuatazo:-

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Jaribu kutambua ni kitu gani kinachofanya uwe na huzuni.

63

64

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Zungumza na watu wengine kuhusu hisia zako

Fanya mazoezi, na fanya mambo ambayo yanakufanya uwe na furaha na ujisikie vizuri.

Pamoja na haya, jaribu kutoka nje ya nyumba

yenu na pitisha muda na watu wengine. Jihusishe

na shughuli za kanisa/msikitini au kikundi cha

vijana. Kupitisha muda na watu wengine kunaweza

kukusaidia kuondoa fikra za mambo ambayo

yanakufanya uhuzunike sana. Kusaidia kazi

watu wengine kunaweza vilevile kuwa njia nzuri

ya kukufanya ujisikie vizuri. Kwa mfano; jaribu

kumsaidia mtoto anayejifunza kusoma, msaidie

rafiki au jirani yako kazi wanazozifanya. Inaonekana

kama upuuzi, lakini utashangaa namna ambavyo

kumsaidia mtu mwingine kazi kunavyoweza

kukufanya ujisikie vizuri zaidi pamoja na matatizo

uliyonayo.

unapojisikia hovyo, kusaidia watu wengine

kazi kunaweza kukufanya ujisikie vizuri zaidi.

Kama yote hayo hayakukusaidia kiasi cha kufikiria kujiua, tafadhali mtafute mtu wa kuzungumza

naye mara moja. Huyu anaweza akawa ndugu yako, mwalimu au mtaalamu wa ushauri nasaha.

Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengi ni washauri nasaha wazuri, na wanatoa msaada

na ushauri kwa watu wakati wote. Ufumbuzi wa matatizo yako unaweza kupatikana, kwa hiyo

usijaribu kuyatatua peke yako unapojisikia umenyong’onyea sana.

UNAJUA kwamba pombe inaongeza mfadhaiko?

Watu wengi hunywa pombe nyingi wanapokuwa na matatizo wakiamini kuwa inawasaidia

kusahau shida walizo nazo. Pombe hufanya ubongo uwe kama umepata ganzi na kufanya

matatizo kupungua papo hapo.

Kwa bahati mbaya, pombe haiwezi kutatua matatizo yako ya huzuni au kusononeka. Ukweli

ni kwamba pombe inaangukia katika kundi la madawa ya kupunguza uwezo wa ubongo

na sehemu zingine za mwili kufanya kazi vizuri. Pombe na dawa zingine za kupunguza

wasiwasi kwa hakika zinaongezea hali ya kusononeka. Kwa kuongezea, zinamsaidia mtu

akwepe kutatua matatizo yanayomfanya asononeke. Matokeo yake, pombe inaweza kuwa

ngao ya kutegemewa hasa matatizo yanapotokea. Watu wengine wanatawaliwa sana na

pombe kiasi cha kwamba hawawezi kuishi bila kunywa.

KUISHI VIZURI NA WATU

Kuishi na kuelewana na watu ni sehemu nyingine muhimu katika afya ya hisia. Mahusiano

mazuri na wazazi na marafiki zako yatakufanya wewe mwenyewe ujisikie vizuri kwa ujumla na

yatakusaidia kupambana na raha na shida za maisha. Kuelewana na watu wengine kunahitaji

stadi muhimu kama vile:-

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Kujitambua: Kujitambua maana yake ni kuwa na uwezo wa kuelewa hisia zako ni zipi na kwa

nini ziko hivyo. Kujitambua maana yake ni kuwa unapojisikia ovyo ovyo unaachana na kufikiria

kile unachohisi – iwe huzuni, hasira, kukata tamaa, wasi wasi, n.k. Na baada ya kuachana

na unachohisi unaendelea na kufikiria ni kitu gani kinakufanya uwe hivyo. Kwa mfano je ni

wasiwasi juu ya masomo yako? Je unashuku urafiki ambao unaonekana kufifia? Je kuna

mtu amekufanya ujisikie vibaya?

Kujitambua ni muhimu kwa sababu kunakusaidia

uelewe tatizo na chanzo chake. Kwa

kutumia taarifa hii unaweza kuanza kutatua

tatizo. Kama una wasiwasi na kazi za shule,

unaweza kuzungumza na wazazi au mwalimu

wako na kuanza kupata msaada unaouhitaji

ili ujiamini tena. Kama una wasiwasi na rafiki

yako, unaweza kuchukua hatua ya kuzungumza

naye na kumueleza namna urafiki wenu

ulivyo wa muhimu, na kwa pamoja mnaweza

kuangalia namna ya kuufanya uwe urafiki wa

nguvu. Iwapo kuna mtu anakukosesha raha,

unaweza kuamua kukabiliana naye ili afahamu

kwamba unajisikia vibaya anapokutendea

vile, au kama hiyo haisaidii, unaweza kuamua

kukaa mbali na huyo mtu anayekufanya

ujisikie vibaya.

Kujitambua ni uwezo wa kugundua unachohisi na

kinachokufanya uhisi hivyo

Mwisho, kujitambua kunaweza kukusaidia kuujua udhaifu wako, - udhaifu unaotakiwa

kuufanyia kazi mwenyewe. Je, unazo tabia au mwelekeo fulani ambao ungependa kuubadilisha?

Kwa mfano: unaweza kugundua kwamba unapofanya vibaya mitihani yako ya shule

unakuwa na tabia ya kumlaumu mtu mwingine. “Mwalimu hanipendi” unajisemesha mwenyewe.

Au unafikiria “wanafunzi wengine walikuwa wanapiga kelele kwa hiyo nilishindwa

kufikiri.”

Ni rahisi sana kulaumu watu wengine, lakini ni tabia mbaya kwa sababu huwi mkweli na hujiwajibishi.

Labda ulipokuwa mtoto ilikuwa sawa kulaumu watu wengine hasa kwa vile yapo

mambo mengine ambayo watoto hawawezi kuyadhibiti. Lakini unapoingia utu uzima, unahitaji

kuwajibika kwa matendo yako. Kama kuna jambo ambalo haliendi kama unavyotaka ni

juu yako kujaribu kulibadilisha. Kujisikitikia na kujifanya kana kwamba wewe ni mwathirika

wa matendo ya watu wengine haitatatua jambo lolote.

Ushirikeli (uwezo wa kuelewa hisia za mtu mwingine): Uwezo wa kuelewa hisia za mtu

mwingine ni sawa na kujitambua ijapokuwa huu ni uwezo wa kuelewa kile ambacho mtu

mwingine anahisi na kwa nini anahisi hivyo. Kuwa na uwezo wa kuelewa hisia za mtu

mwingine maana yake ni kuwa na uwezo wa kufikiri na kujua pale penye tatizo la mtu

kama - rafiki, mzazi, ndugu, n.k. Unaweza kujua hofu zao,wasiwasi, woga na mahitaji yao, na

unaweza kuelewa wanavyojihisi. Kama ambavyo kujitambua kunavyosaidia ujue mahitaji

yako, ushirikeli unakuwezesha kujua hisia za mtu mwingine. Kwa mfano; kama rafiki yako

ana huzuni, kufahamu tatizo lake kunaweza kukusaidia ujue namna ya kumsaidia kulitatua.

65

66

Kutatua tatizo na kufikiri kwa

ubunifu: Ili kupata ufumbuzi wa

matatizo kunahitaji kufikiri kwa

ubunifu. Kufikiri kwa ubunifu ni uwezo

wa kufikiri ufumbuzi wa tatizo usio

wazi. Ni uwezo wa kusumbua akili

yako ili kupata fumbuzi mbalimbali

bila kujiwekea mipaka ya mazoea

uliyoyasikia ya utatuzi wa jambo fulani.

Kwa mfano: fikiria kuwa umepata

mimba ukiwa unasoma shule. Wasichana

wote unaowafahamu waliopata mimba

waliacha shule na hawakuweza kumaliza

masomo. Kufikiria kwa ubunifu maana

yake ni kutokudhani kwamba lazima

uache shule eti kwasababu wasichana

wengine waliacha. Labda inawezekana

ukakaa shuleni ukiwa na mimba. Au

unaweza kurudi shuleni baada ya

kujifungua mtoto. Labda kipo kituo kwa

ajili ya vijana waliozaa ambako unaweza

kuendelea na masomo au mafunzo.

Kufikiri kwa ubunifu kunahusisha

kuzungumza na watu wengine. (walimu,

vijana washauri wazazi, shangazi,

wajomba marafiki) na kuchunguza

chaguzi zote zilizoko mbele yako.

Stadi za makubaliano. Hizi ni stadi

ambazo unahitaji ili kutatua tatizo au

tofauti ulizonazo na watu wengine.

Kwa mfano, unaweza ukataka kutoka

na rafiki yako, lakini wazazi wako

wanataka ukae nyumbani. Hali kama

hii inahitaji stadi nzuri za makubaliano.

Inaweza ikawa vigumu kukubaliana

na wakati wingine kukatishwa tamaa.

Unaweza kujisikia kama upasuke,

kwamba umevunjika moyo kiasi cha

kusema “potelea mbali” na kuondoka

ukiwa umekasirika na kuchoshwa.

Lakini unahitaji kuwa mvumilivu na

mtulivu wakati unaeleza kwa nini

unajisikia hivyo, na kile unachohitaji.

Vilevile unahitaji kuwa mkweli, mtu

unayeelewa na kuheshimu yale ambayo

watu wengine wanayahisi na kuyahitaji.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Je, unajua maana ya kutatua tatizo kwa

ubunifu bila woga wala jazba?

Anne ana umri wa miaka 16 na ni yatima.

Anaishi na shangazi yake ambaye anamtaka

afanye kazi dukani kwake kila siku baada ya

kutoka shule. Hili ni tatizo kubwa kwa Anne.

Hapati muda wa kutosha wa kujisomea.

Ameanza kufadhaika kwa vile mitihani

inakaribia. Hapati usingizi vizuri usiku kwa

sababu ana wasiwasi sana kuhusu masomo.

Ameanza kumchukia shangazi yake.

Anashangaa iwapo shangazi yake anamwona

kama kitendea kazi na kwamba hampendi

wala kujali maisha yake ya baadaye.

Anne anajitambua. Anajua kuwa anayo

tabia ya kuficha hisia zake mpaka

anapolipuka kwa hasira. Tabia hii haimsaidii

sana. Shangazi yake naye anakasirika na

kusema ameanza kukosa heshima.Safari hii

anaamua kufanya mambo tofauti. Badala

ya kumwambia shangazi yake kiugomvi

“Hunipendi” anamweleza shangazi yake bila

woga wala jazba “Ninawasiwasi sana kuhusu

mitihani yangu lakini nataka pia kukusaidia

kazi za dukani”. Hapa ameonyesha tabia ya

kujiamini.

Kwa kujieleza mwenyewe kwa njia hii,

Anne amesimama imara na kuomba

muda zaidi wa kujisomea. Lakini kwa

wakati huo huo anaelewa shangazi yake

anahitaji msaada wa dukani. Anaonyesha

ushirikiano kwa shangazi yake ambaye ana

majukumu mengine. Akifuata utaratibu huu,

shangazi naye anaelewa pia. Kwa pamoja

wanafikiri kwa ubunifu kutatua tatizo hili.

Wanatengeneza ratiba inayompa Anne muda

zaidi wa kujisomea jioni na pia kumsaidia

shangazi yake jioni inapokuwa lazima.

Inatia moyo kwa jinsi Anne alivyojisikia

vizuri. Ghafla mfadhaiko unapungua na

anaweza kuyafurahia maisha tena.

Hata hivyo sio kila tatizo linaweza kujadiliwa na kufikia maelewano. Wakati mwingine

utalenga katika matokeo ambayo yatakufanya uwe salama, hata kama mtu mwingine

hatafurahia. Mathalani, rafiki yako wa kike au wa kiume amekataa kutumia kondomu

pamoja na kumshawishi kwa nguvu zote. Katika hali kama hii zingatia usalama wako.

Ondoka sehemu hiyo ikibidi.

Msimamo: Msimamo ni stadi ya msingi katika kuelewana na watu wengine. Msimamo

maana yake kutetea na kuyaenzi yale unayoyaamini wewe mwenyewe. Kuwa muwazi na

mwaminifu kwako mwenyewe na watu wengine kuhusu kile unachokihitaji na kukitaka.

Watu ambao hawana msimamo juu ya maisha yao huwa ni wanyenyekevu. Hata kama

wanatendewa vibaya, hawajitetei. Watu ambao hawana msimamo mara kwa mara

wanakosa imani ya kujienzi na kutetea mahitaji yao na kulinda hisia zao au hata miili yao ili

wasiumizwe.

Msimamo ni tofauti sana na kuwa mgomvi. Watu wagomvi ni watundu na hawana huruma,

hawajali watu wengine wanahisi nini. Sio vizuri kuwa mgomvi kwa faida ya afya ya hisia

kwa sababu, kwa undani kabisa, utajisikia vibaya kutokuwa na huruma kwa wengine.

Misingi ya msimamo:

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

• amua unachohisi au unachotaka na kiseme. Usiogope kuwa mkweli kuhusu hisia

zako. Watu wanatakiwa kuziheshimu hisia hizo. Kwa mfano, labda ulijisikia vibaya na

unakosa raha baada ya rafiki yako wa kiume kukugusa sehemu zako za siri. Unatakiwa

kumwambia, “Nilikosa raha uliponigusa sehemu zangu za siri sitaki uniguse hivyo tena”.

Mtu anayekupenda kweli hatataka kufanya vitendo ambavyo vinakukosesha raha.

• Mtazame mtu machoni: Kumwangalia mtu machoni ni kudhihirisha msimamo wako.

Inamjulisha mtu mwingine kwamba hutanii kuhusu kile unachokisema na kwamba

unaangalia kama wanakusikiliza au hawakusikilizi. Tamaduni nyingi haziungi mkono

kumwangalia mtu machoni wakati wa mazungumzo. Wakati mwingine katika maeneo

mengine huliona jambo hili ni ufedhuli (kutokuwa na ustaarabu/heshima) kijana

mdogo anapomwangalia mtu mzima moja kwa moja usoni. Unaweza kufuata mila na

desturi, kama kupiga magoti, kuonyesha heshima lakini kwa wakati huo huo endelea

kumwangalia mtu huyo usoni kama unataka kuonyesha ujasiri/msimamo wako.

• usitoe visingizio. Hisia zako ni sababu tosha. Kwa mfano, kama hujisikii kufanya

mapenzi lakini rafiki yako wa kike au kiume anakulazimisha, epuka kutumia watu

wengine kama kisingizio. Usiseme, “mama yangu karibu atarudi nyumbani au tumbo

linaniuma au ninaogopa kupata mimba au nina kazi ya kusoma kwa hiyo sio muda mzuri

kwangu”. Unaweza ukamchanganya rafiki yako na visingizio hivi. Anaweza kudhani

unataka kwenda sehemu nyingine, au kwamba labda unataka kutumia kondomu.

Anaweza asitambue kwamba unachotaka kumwambia ni “siko tayari kufanya tendo hilo

kwa hiyo sitaki”. Kwa hiyo basi sema kile unachotaka.

• usisemewe na mtu mwingine. Iwapo hutaki kufanya jambo fulani, sema mwenyewe

na usiulize mtu mwingine kama ni sawa. Kwa mfano, kama mtu ana kushawishi unywe

pombe au madawa ya kulevya usiseme; “nisingependa, lakini kama unaona sawa …?

Badala yake sema “Hapana, ninashukuru.

67

68

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sihitaji kitu chochote”. Waonyeshe kwamba unajua unachotaka, hivyo hutafuti kibali chao.

Usibabaishwe na hoja za watu wengine. Endelea kurudia msimamo wako juu ya yale

unayoyataka na usiyoyataka. Labda rafiki yako wa kike anaendelea kukulazimisha mfanye

mapenzi na ana tumia hoja hizi: “Hivi hunipendi?”, “Unajua nilifanya mapenzi na mvulana

wangu wa zamani. Simama imara na usikubali. Mwambie “mimi sio mvulana wako wa

zamani. Mimi ni mimi. Sitaki kufanya mapenzi na wewe.

Kumbuka, unayohaki ya kubadilisha mawazo. Labda wewe na rafiki yako mlizungumza

kuhusu kufanya mapenzi siku chache zilizopita, na ulimwambia mtafanya mapenzi. Lakini

umefikiria kiundani na unaona ni makosa kufanya hivyo. Iwapo atasema; “Lakini ulikubali

mwenyewe kwamba tungefanya mapenzi”. Mwambie: “Nimebadilisha mawazo. Siko

tayari”. Kama kweli anakupenda, ataheshimu maamuzi yako mapya na atasubiri mpaka

utakapokuwa tayari.

Kuwa na msimamo ina maanisha kuwa na uhakika na kile unachotaka

Kuwa na stadi za maisha zilizojadiliwa katika sura hii,kujitambua,ushirikeli,kutatua

matatizo kwa kufikiri, kwa ubunifu,stadi za makubaliano,kuwa na msimamo ni baadhi ya

nguzo za afya ya hisia nzuri.Ukizifahamu stadi hizi utakuwa salama na si ajabu utafanikiwa

katika vitu vingi utakavyojaribisha maishani.

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Sura ya Sita

utunzaji afya ya akili na Moyo

Kuwa na afya njema ya hisia ina maana zifuatazo:

· Kujisikia vizuri wewe binafsi. Ni kujipenda na kujiheshimu. Pia ni kujithamini.

· Kujikubali kuhusu uwezo wako. Unakuwa huna wasiwasi sana kuhusu

udhaifu wako na huogopi kujaribu mambo mapya. Unakuwa unajiamini.

· Kuweza kukabili wasiwasi na mfadhaiko. Unakuwa huna wasiwasi na

mwonekano wako, huna wasiwasi kwa vile eti huwezi vitu fulani, huna

wasiwasi na maneno ya marafiki zako wala huna wasiwasi kwa vile tu

huna mpenzi.

· Kukabili huzuni. Unajitahidi huzuni na hasira zisikutawale na kukukosesha

matumaini.

· Kutambua hisia zako na sababu za hisia hizo. Unapojisikia vibaya (iwe

hasira, uchovu, kukata tamaa) acha kufikiria hisia hizo na sababu zinazosababisha

ujisikie hivyo.

· Kuelewa hisia na sababu wanazotoa watu wengine. Unajiuliza ingekuwa

wewe ungefanyaje? Unakuwa mtu unayejaribu kuelewa wasiwasi, matatizo

au mahitaji ya watu wengine. Huu ni uwezo wa kutambua hisia za watu

wengine.

· Kutatua matatizo na kufikiri kiubunifu. Unakuwa na njia nyingi za

kutatua tatizo linapojitokeza. Pia unatumia njia bora zilizojificha ambazo

hutatua tatizo kwa urahisi zaidi.

· Kumweleza mtu mwingine kuhusu hisia zako, unachokitaka na sababu

zako. Unapojaribu kusuluhisha tatizo au mgongano wa mawazo unakuwa

ni mtu wa kujadili bila kumvunjia heshima mwenzio. Unatafuta suluhisho

lenye manufaa kwa pande zote mbili. Unakuwa ni mtu wa mapatano.

· unakuwa na msimamo wako. Unasisitiza unachokitaka na unachokihitaji.

Unakuwa muwazi na mkweli kuhusu hisia zako. Unakataa kushurutishwa

kwa kitu usichokitaka.

Hisia njema ya mtu mmoja hujengwa na waliomzunguka. Kutakuwa na muda utahitaji

ushauri na msaada toka kwa wengine- toka kwa wazazi, marafiki, walimu,

wajomba, shangazi, kaka , dada, viongozi wa dini au mshauri nasaha. Kitu muhimu

katika kujenga hisia njema ni kuweza kuomba ushauri unapouhitaji.

69

70

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Maelewano Na

Wazazi Wako

Vijana wengine wamebahatika kuwa na wazazi ambao wanaweza wakaelewana na kuzungumza

mambo muhimu. Lakini vijana wengi wanashindwa kuelewana na wazazi wao hasa kipindi cha

balehe. Mahusiano na wazazi wao yanaanza kuwa magumu. Wanaanza kushindana na kubishana

katika kila kitu na wazazi wao. Wanajisikia kama wazazi wao wamepitwa na wakati na wana

mambo ya kizamani. Wanajisikia kama wazazi wao hawawaamini na hawana imani nao.

Gifty, kutoka Ghana (umri, Miaka 14)

“Wazazi wangu wako huru na tunashirikiana katika matatizo

yangu hivyo huwa nakubaliana nao. Kila mara wananifanya

nijisikie mwenye furaha na wananishauri mambo mengi. Ninataka

wazazi wawe na muda mwingi kwa ajili ya watoto wao. Ni vema

wazazi wazungumze na watoto wao na kuwashauri kwa sababu

watoto wanawategemea sana wazazi ili ndoto zao ziwe kweli”.

cathy kutoka uganda (umri, Miaka 17)

“Ukali wa mama yangu na mabadiliko katika mwili wangu

vilijitokeza pamoja. Alinikataza nisijumuike na makundi, wakati

mimi ndio muda niliokuwa nahitaji sana makundi ili kuweza

kubadilishana mawazo.”

Panaito kutoka kenya (umri, miaka 14 )

“Wazazi wangu mara nyingine walinizuia kuchanganyika na vijana

wenzangu”.

barlay kutoka Kenya (umri; miaka 16)

“Wazazi wanajaribu kutufanya tuwe wazuri lakini mara nyingine

huwa wakali. Wanatuchagulia marafiki, na kitendo hicho

sikipendi.”

71

SURA YA 7

72

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

halima kutoka Kenya (umri; Miaka 14)

“Mimi na wazazi wangu mara zote hatukubaliani kuhusu mimi

kutoka nyumbani bila baibui (gauni nyeusi na mtandio wanazovaa

wanawake wa Kiislamu), na baada ya kumaliza mtihani

hawapendi mimi nitoke kila wakati”.

Bila kujali upande uliofungamana nao bado kuna mambo mengi unaweza kufanya ili

kudumisha na kuboresha uhusiano na wazazi wako. Wakati mwingine inaweza kuwa kazi

ngumu lakini ukidhamiria na kujituma jitihada zako zinaweza kufanikiwa, maelewano

yatakuwa mepesi zaidi.

KUTHAMINI FAMILIA

Orodhesha mambo unayoyaenzi na kuyafanya. Pengine unafikiri kuwa ucheshi ni moja

ya sifa zako nzuri. Pengine unapenda unavyotabasamu. Pengine unajisikia vizuri kuhusu

kipaji chako. Pengine unajisikia vizuri kuhusu kipaji chako cha useremala au wepesi katika

hesabu.

Baada ya hapo, jaribu kufikiria wapi hivyo vipaji vilipotoka.. Kwa mfano, Ulijifunza wapi na

toka kwa nani? Unaweza kubainisha baadhi ya tabia hizi kwa wazazi wako, shangazi zako,

na wajomba au ndugu zako wengine? Je, ucheshi ni wa mama yako? Tabasamu ni la baba

yako? Nani alikufundisha mambo ya useremala?n.k

Mara nyingine ni rahisi kuingia katika malumbano na wazazi wako na ndugu wengine

katika ukoo kiasi kwamba sio rahisi kuona ni kiasi gani umerithi toka kwao. Unapata

matatizo ya kuona mambo mnayofanana kwa sababu ya tofauti za mtizamo, tofauti kuhusu

jambo fulani. Mara nyingine unaweza kujisikia unaaibishwa na ndugu zako. Labda wazazi

wako hawana fedha za kutosha, hivyo familia yako wanaishi katika chumba kimoja hata

kukufanya uone aibu kuwaleta marafiki nyumbani.

Ni muhimu kuthamini familia yako na kuikubali kama ilivyo – tajiri au masikini. Lenga

katika kile ambacho ndugu zako wameweza kukupatia, kuliko kile ambacho hawakuweza

kukupatia. Kumbuka kuwa familia yako imefanya kazi kukufanya uwe ulivyo na

utakavyokuwa. Familia yako pia imekupa maadili ya kukuwezesha kuishi kama unavyoishi.

Hii haina maana ya kwamba uko sawa sawa na wazazi wako. Zinaweza kuwepo tofauti

nyingi kati yenu kama kulivyo kufanana kwingi. Kwa kuongezea, kipindi cha balehe ndio

muda ambao vijana wengi wanataka kugundua tofauti kati yao na wazazi wao. Wanataka

kujitegemea, jambo ambalo ni la kawaida na zuri. Hata hivyo, kujitegemea siyo jambo rahisi.

Ukweli linaweza kuwa vigumu sana kwako na hata kwa familia yako.

FAHAMU YALE WAZAZI WAKO WANAYOYATAKA

Unapojaribisha muonekano na tabia mpya na njia mpya za maisha, familia yako inaweza

kuona shida sana. Watashangaa nini kimekupata, wapi umepata mawazo hayo ya ajabu?

Wapi kijana wao wa kiume au kike amekwenda? Huyu kijana ni nani ambaye anapenda

kutumia muda wake mwingi akiwa peke yake au kuzururazurura kwenye vijiwe?

Inaweza kuwa vigumu kwa wazazi kutambua kuwa unakuwa mtu mzima unayeweza kufikiri

mwenyewe na ambaye unayo maoni yako. Bado wanafikiria ungali mtoto. Kuwa mtulivu wakati

wazazi wanajirekebisha kwa mabadiliko yako makubwa.

Grace, kutoka Kenya (umri; Miaka 14)

“Hatukubaliani mara nyingine kuhusu mavazi, kwa sababu wanasema

suruali na jinzi ni kwa ajili ya wanaume. Lakini ninadhani

kuzivaa ni salama kwangu kuliko kuvaa gauni na sketi. Hawataki

pia nisuke rasta. Wanasema ni mtindo wa watu wabaya. Lakini

mimi sifikirii hivyo nachukulia kama mtindo tu”.

bernard, kutoka Kenya (umri; Miaka 17)

“Mara nyingine mawazo yangu yanapingana na ya wazazi wangu.”

Kumbuka kwamba wazazi wako walikua kipindi cha zamani tofauti na wewe. Hata hivyo, kama

wazazi wako wanafuata mila, waonyeshe angalao jambo jipya zuri. Wazazi wako ni kiunganishi

cha utamaduni wa zamani na wa kisasa. Huu ni utajiri kwako. Unaweza kujifunza mengi kuhusu

utamaduni kutoka kwa wazazi wako na wakubwa zako. Litakuwa jambo la kuhuzunisha kama

utapoteza mambo haya:

SURA YA 7 | MAELEWANO NA WAZAZI WAKO

Lugha ya asili au lugha ya mama.

Historia ya watu wako.

Vifaa vya asili vya muziki, nyimbo na hadithi

Ngoma za asili na upishi.

Ingekuwaje kama usingejua hata moja kuhusu

utamaduni wako? Ungelikuwa nani? Ungelikuwa

upande gani?

Jifunze kuhusu historia yako, utamaduni,

mila, muziki, ala, na kucheza ngoma

Bila kuwa na fikra ya utamaduni wetu na historia yetu tutapotea. Wahenga wetu, lugha yao,

utamaduni na imani ni mambo muhimu ya utambulisho wetu. Usiyadharau!

Bila shaka, utamaduni wa kisasa una mambo mengi mazuri - yale yanayofanya maisha yetu

yaonekane bora kama elimu, madawa ya kisasa na mawazo mapya juu ya wajibu wa wanaume na

wanawake.

Kwa mfano, wasichana sasa wanayo nafasi zaidi katika elimu na kazi nzuri ukilinganisha na bibi

zao. Mitazamo ya zamani kama kuamini kwamba wanawake na wasichana wanalazimika kukaa

nyumbani kupika na kuangalia nyumba zinabadilika. Mtazamo kuhusu kuendeleza mila za ndoa

katika umri mdogo nazo zinabadilika.

Kwa sasa unaishi kipindi cha kusisimua. Mambo mengi yamewekwa wazi. Unayo nafasi ya

kutosha kuchagua namna unavyotaka kuishi. Unaweza ukachagua mazuri kutoka kila upande

– mazuri ya utamaduni wa asili na mazuri ya utamaduni wa kisasa. Unaweza kuyakumbatia

unayofikiri ni mazuri, na kuyakataa yale unayofikiri ni mabaya.

73

74

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kadri unavyojaribu kufanya maamuzi yako kuhusu yapi unayotaka kuishi nayo, kati ya kiasili na

ya kisasa jaribu kuwa mwangalifu kuhusu hisia na imani za wazazi na wazee wako. Zungumza nao

ili kujua misimamo yao. Waeleze hisia zako na kile unachowaza.

KuMuDu MataRajiO Ya WaZaZi WaKO

Wazazi wengi wanatarajia mengi kutoka kwa vijana wao. Wanataka uishi maisha mazuri kuliko

walivyoishi, hivyo wanataka ufanye kazi kwa bidii zaidi, ufanye vizuri shuleni, na uwe makini zaidi!

Mategemeo ya wazazi wakati mwingine

yanaweza kuonekana kama mzigo mzito.

Mara nyingine inakuwa kana kwamba

wamelenga sana katika maisha yako ya

baadaye wanayofikiria uwe nayo, kiasi cha

kwambahawasikilizi mawazo na matakwa yako.

Huenda baba yako anataka uwe daktari, lakini

huna uwezo katika masomo ya sayansi. Au

pengine mama yako anategemea wewe uoe na

kuishi kijijini ulikozaliwa, lakini unataka uende

Chuo Kikuu ukawe mwandishi wa habari.

Hali ya namna hii inaweza kuwa ngumu. Wazazi unataka kuwa mwalimu, nasema hapana… atakuwa

wako mara kwa mara wanadhani wakati wote daktari. hivyo ndivyo nataka kijana wangu

wanajua kipi kizuri kwako, hata kama hawajui.

Inaweza kuwa vigumu kwao kutambua kwamba wewe ni mtu unayejitegemea mwenye kipaji

chako, mawazo na ndoto zako. Wanaweza kuwa wanapata shida kutambua kati ya ndoto zako na

ndoto walizonazo wao.

Jaribu kuwa mvumilivu na kumbuka kwamba wazazi wako wanataka maisha yako kuwa mazuri.

Endelea kuzungumza na wazazi wako. Waeleze kuhusu malengo na ndoto zako, na kwa nini

unataka kufuatilia ndoto hizo. Waonyesha jinsi ulivyodhamiria.

MaWaSilianO na WaZaZi WaKO

halima, kutoka Kenya (umri; Miaka 14)

“Mara nyingine wazazi wangu wananipa presha kubwa. Wanategemea

nifanye kila kitu vizuri na nisifanye makosa yoyote.

Wananitegemea niwe sahihi, jambo ambalo halitawezekana,

kwasababu sisi sote ni binadamu ambao tunaweza kufanya

makosa wakati wowote!”.

Kukosekana kwa mawasiliano ya wazi ndicho chanzo cha malumbano kati ya vijana na wazazi

wao. Cha kushangaza ni kuwa inakuwa vigumu kukaa chini na kuwa na mazungumzo yenye

manufaa kwa pande mbili.

SURA YA 7 | MAELEWANO NA WAZAZI WAKO

Wazazi wengi hupenda sana kuwasaidia

watoto waoili wapite salama katika kipindi cha

balehe lakini mara nyingi hushindwa namna

ya kuwasaidia. Wanaogopa kuwaaibisha au

kujiaibisha wao wenyewe. Huenda hata wazazi

wao pia hawakuzungumza nao juu ya balehe na

mabadiliko yote anayopitia kijana. Hivyo ni vigumu

sana kwao kukusaidia wakati wao wenyewe

hawakupata msaada wowote. Kama ilivyo kwako,

wanaweza wasiwe na uzoefu mkubwa katika eneo

hili au wasiyajue majukumu yao.

Kwa vipi kijana anaweza kujifunza kuongea kwa

uwazi na wazazi, shangazi, wajomba, babu na bibi

au jamaa yeyote katika familia? Unajenga vipi

julia, kutoka Ghana (umri: Miaka 22)

“Nilipoanza kuona mabadiliko mwilini mwangu, niliona vigumu

kuyazungumza kwa wazazi wangu. Lakini kadri muda ulivyoenda

nilijisikia huru zaidi na niliweza kuongea nao. Niliwauliza swali

lolote nililotaka kuwauliza.”

Waonyeshe wazazi wako kuwa unajali

kuwafurahisha

uhusiano wakati wanapokuamini na hasa kama mlikuwa mnabishana muda mfupi uliopita?

Utaanzaje kujenga uhusiano huo? Bila shaka hakuna jibu rahisi lakini hapa kuna vidokezo

unavyoweza kujaribu:

• Waonyeshe wazazi wako kuwa unaweza kuwafurahisha. Jitolee kuwasaidia wazazi

wako katika shughuli yoyote wanayoifanya – jikoni, kuzunguka nyumba au bustanini.

Wakati mnafanya kazi pamoja eleza suala lako unalotaka mlijadili.

anthony, kutoka Kenya (umri: miaka 15)

“Njia bora zaidi kukabiliana na wazazi ni baada ya kuwa umefanya

kazi fulani ya kuwafurahisha ndipo unapoweza kwenda kuongea

nao jambo unalotaka.”

• chagua muda mzuri wa kuongea. Uchaguzi wa muda ndio kila kitu! Chagua muda

ambao wazazi wako hawajachoka sana au wakati hawana shughuli nyingi. Yaweza kuwa

vizuri kusubiri hadi mwisho wa wiki wakati wanapumzika na hawafikirii sana masuala

ya kazi.

• anza na mada rahisi. Anza na mada ambayo sio ya kutahayarisha kwako au kwao na

ambayo hamtofautiani nao sana. Katika familia nyingi wazazi na watoto wao huanza

kuongea pale tu kunapokuwa na jambo zito – mfano wakati watoto wanapotaka

kufanya kitu wasichopenda wazazi. Hapa ni mahali pagumu kuanzia.

Unaweza kuanza kujaribu kuzungumza na wazazi wako juu ya hali au tatizo la rafiki yako

kwanza kabla ya kwako.

75

76

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Hii inaweza kuwapa wote wewe na wazazi wako hisia za kumthamini kila mmoja wenu na

inaweza kusaidia kujenga uaminifu na uelewa juu ya hali isiyokuwa ya binafsi sana. Lakini

usisaliti uaminifu wa rafiki yako, pia linda siri zake. Kwa mfano unaweza kuongelea tatizo

la rafiki yako kwa wazazi wako, lakini usimtaje kwa jina huyo rafiki yako aliye katika hali

ngumu.

Waonyeshe wazazi wako kuwa unayajali

mawazo yao. Waulize wazazi wako

wanafikiria nini na kwa nini wanajihisi

hivyo katika hali fulani. Jaribu kuelewa

mtazamo na wajibu wao. Labda unadhani

wazazi wako hawataki uende disko kwa

sababu ni wakali. Lakini huenda kuna kitu

wanakijua kuhusu disko ambacho wewe

hukijui. Huenda wamesikia kuwa wasichana

hubakwa huko au watu huuza madawa ya

kulevya huko. Wanaweza kuwa na sababu

nzuri sana ya kuhisi hivyo na wangependa

uvutiwe na sababu zao na uyajali mawazo

yao.

Waulize wazazi wako nini wanafikiri na kwa

nini. Wanaweza wakawa na sababu nzuri kuhusu

mienendo yao.

• uwe na heshima. Wazazi wako, ndugu zako na wakubwa zako wanajali sana suala la

heshima. Hivyo hata kama unahisi kukatishwa tamaa, jaribu kutopiga kelele na kufanya

wakuone huna heshima. Pia uwe na heshima kwa maadili yao. Wakati baadhi ya maadili

yanaweza kuwa sawa na ya familia yako lakini mengine yaweza kuwa tofauti. Kama

unataka kuishi katika maadili tofauti na ya wazazi wako ni sawa, lakini usiwakosee

wazazi wako juu ya imani zao hata kama kwako zitaonekana kupitwa na wakati au kuwa

za kijadi mno kwako.

• jenga kuaminika. Waonyeshe wazazi wako kuwa unawajibika na kuwa wanaweza

kukuamini. Wakikuambia kuwa uwe nyumbani wakati fulani, hakikisha kuwa unakuwa

nyumbani wakati huo. Uwe muwazi kwao kwa kitu unachotaka kufanya na elezea

sababu zake. Usijaribu kwenda disko kwa siri wakati umewaambia wazazi wako kuwa

unaenda nyumbani kwa rafiki yako. Ukijaribu kuwadanganya huenda wakagundua na

utakuwa umevunja imani yao kwako.

Wazazi wako wanatakiwa kuheshimu mambo yako ya faragha. Lakini usitumie vibaya

faragha hiyo kwa kuishi maisha ya siri na ya hatari. Wazazi wako pia wanatakiwa

waheshimu uchanguzi wako wa marafiki lakini pia unahitaji kuwaonyesha kuwa unaweza

kuchagua marafiki wazuri. Usijihangaishe na watu ambao hawakujali na ambao maadili yao

kimsingi yanapingana na ya familia yako.

aloysious, kutoka uganda (umri: Miaka 19)

“Unatakiwa kufanya ulichoambiwa hata kama hupendi na

usiwafadhaishe wazazi kwa kufanya vitu ambavyo unajua vita

waumiza moyoni. Kwa kufanya yote haya utakapoongea nao

hawatakukatalia lolote utakalowaambia.”

SURA YA 7 | MAELEWANO NA WAZAZI WAKO

• uwe muwazi kwa wazazi wako. Kumbuka

kuwa unabadilika haraka sana kiasi

kwamba wazazi wako wanaweza kuhisi

kuwa hawakuelewi vizuri. Ni wajibu wako

kuhakikisha kuwa wanakuelewa. Ongea

nao kuhusu ndoto zako, matarajio yako,

na mahitaji yako ili wahisi kujiamini kuwa

wanakufahamu wewe na unachokitaka.

Shirikiana nao katika masikitiko na

mashaka yako. Waulize wangekuwa ndio

wenyewe katika nafasi yako wangefanyaje.

Waruhusu wazazi wako wakutane na rafiki

zako ili wajue ni nani unayekwenda naye

matembezini.

Kwa wazazi wako, watambulishe marafiki zako

ili wajue kuwa wanaweza kukuamini.

Wakati wazazi wako wanapohisi kuwa wanakuelewa vizuri, watajisikia vizuri zaidi

wakikuamini. Itawasaidia kuanza kukukubali kama mtu unayeelekea ukubwani na kuacha

kukuchukulia kama mtoto. Itasaidia pia wakuruhusu ufanye maamuzi mengi mwenyewe.

Prisca, kutoka Kenya (umri: Miaka 14)

“Njia nzuri ya kukabiliana na wazazi wako ni kuwaeleza matatizo

yako na kuwaomba kama wanaweza kukusaidia. Ukiwaomba

hawawezi kukataa kwasababu wana mapenzi na uelewa. Unaweza

kupanga siku ya kukaa nao pamoja na kubadilishana nao mawazo

juu ya vitu unavyotaka kuzungumzia kwa sababu hawawezi

kukataa.”

• Waonyeshe wazazi wako kuwa unawajali. Kama unavyotaka wao wakuonyeshe kuwa

wanakupenda, ni wajibu wako kuwaonyesha kuwa unawajali. Wafanyie vitu vizuri

kuonyesha kuwa unawapenda na unataka kuwafurahisha.

Sherifan, kutoka Ghana (umri: Miaka 15)

“Unatakiwa wakati fulani uwanunulie wazazi wako zawadi. Huwa

wanafurahi sana.”

Ni vigumu sana kuelewana vizuri na wazazi wako, na kumudu ukali wao, kuyakidhi matarajio

yao makubwa, na kuyakubali maadili yao ya kiutamaduni. Itachukua muda na subira kubwa.

Lakini kila dakika itakuwa na thamani kwa juhudi kidogo utakayoifanya. Itakuwa ya

thamani kwa sababu kuna wakati marafiki na wenzako hawawezi kukushauri kama wazazi

wako”.

Gifty, kutoka Ghana (umri: Miaka 14)

“Unapaswa uwaheshimu wazazi wako na uweke aibu kando.

Uwaeleze wazazi wako matatizo yako kwa sababu ndio watu

pekee wa kuwa na majibu kwa matatizo yako. Ongea na wazazi

wako mara kwa mara”.

77

78

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

VYANZO VINGINE VYA KUPATA MSAADA.

Wakati mwingine kunatokea tofauti kubwa kati

ya wazazi wako na wewe mwenyewe kuhusu

mitazamo mbalimbali. Umejaribu kuzungumza nao

lakini hukufanikiwa. Wanakataa kukusikiliza na

tatizo linazidi kuwa zito. Kwa mfano, inawezekana

wazazi wakasema kuwa wanataka kukuachisha

shule ili wakuoze kwa mwanaume mzee.

Umejaribu kuwaelezea umuhimu wa shule kwako.

Umewaeleza kuhusu ndoto yako ya kuwa mwalimu

na hawajakusikiliza.

Kuna hali nyingi ngumu kama hizi ambazo huwezi

kuzimudu peke yako. Unahitaji kumtafuta mtu

mzima anayeweza kukusaidia.

jenifer, Kutoka Ghana (umri: Miaka 17)

“Unapaswa kuwasaidia nyumbani katika chochote

wanachokifanya. Katika kuwasaidia mambo yote haya

mapenzi kati yako na wao yatadumu muda mrefu.”

Kama unaona ni tatizo kuongea na

wazazi, jaribu kumuuliza mtu mzima

mwingine kwa ushauri na msaada.

evans, kutoka Kenya (umri: Miaka 16).

“Kama huwezi kuzungumza na wazazi wako kutatua tatizo au

mabishano, unapaswa kuzungumza na ndugu wa karibu, mtu

kama shangazi yako au mjomba ambaye atakusaidia wewe na

kujua lipi zuri kwako.”

Jaribu kuzungumza na mtu mzima mwingine ambaye ni mpole, anayejali na unayemwamini

– mtu anayekufahamu, kama ndugu, kaka, mtu mzima au dada, mwalimu, rafiki wa familia,

baba wa rafiki yako, kiongozi wa dini au afisa jamii. Mwombe akupe ushauri na akusaidie

kuzungumza na wazazi wako kuhusu jambo hilo.

Hata kama huna tatizo kubwa na wazazi wako, lakini unahitaji ushauri, unaweza kujikuta

kuwa ni rahisi zaidi kuzungumza na shangazi, mjomba au ndugu. Wako watu wengi

wanaokujali na wako tayari kukusaidia ukiwaomba.

SURA YA 7 | MAELEWANO NA WAZAZI WAKO

Sura ya 7

MAELEWANO NA WAZAZI WAKO

Ujana balehe ni kipindii ambacho vijana wengi inawawia vigumu kupatana na

wazazi wao. Lakini sio lazima mara kwa mara iwe hivi. Yapo mambo mengi unaweza

kuyafanya kuimarisha uhusiano na wazazi wako:

thamini familia yako. Ikubali familia yako jinsi ilivyo - tajiri au masikini. Tumia muda

wako kufikiria kile ambacho familia yako imekupatia, kama vile nguvu ulizonazo,

kuthaminiwa na vitu vingine vinavyokuhusu wewe mwenyewe. Usiangalie tu nini

hawajakupatia.

elewa imani na vitu wanavyothamini wazazi wako. Wazazi wako walikua kipindi

tofauti na wewe. Hata kama unafikiria wazazi wako wanafuata mila za kizamani,

tafuta yaliyo mema. Jifunze kutoka kwao kuhusu historia yenu, mila na desturi,

muziki na lugha.

Kumbuka kwamba wazazi wanakutakia mema. Kumudu matarajio ya wazazi wako

inaweza kuwa vigumu, hasa ikiwa matarajio ya ndoto zao na zako yanatofautiana.

Zungumza na wazazi wako kuhusu malengo yako na kwa nini unataka

kuyaendeleza. Waonyeshe kuwa unayo nia na unafanya kazi kwa bidii.

Kuwa mwaminifu na muwazi kwa wazazi wako. Angalia wakati mwafaka wa

kuzungumza na wazazi wako. Wape nafasi ya kujua utakuwa mtu mzima wa

namna gani. Waonyeshe kwamba ni mwaminifu na muwajibikaji.

Waonyeshe wazazi wako kwamba unajali hisia zao na unataka kuwafurahisha.

Waulize wazazi wako kwa nini wanahisi wanavyo hisi. Jaribu kuelewa tatizo lao.

Waonyeshe kwamba unapenda na kujali wanachofikiria.

Kuwa na heshima. Hata kama hukubaliani na wazazi wako, jaribu kutokuongea kwa

sauti kali au kuwaonyesha ufidhuli.

Kuwa mvumilivu kwa wazazi wako. Wape muda wazoee ukweli kuwa umeanza kuwa

mtu mzima mwenye maoni na ambaye anayeweza kufikiri mwenyewe.

Kuwa mvumilivu kwako binafsi. Kujenga mahusiano ya karibu na ya wazi na wazazi

wako inachukua muda na ni kazi ngumu. Usivunjike moyo na kukata tamaa, uhusiano

mzuri hauwezi kujengwa kwa siku moja.

Mara nyingine, tofauti ya maoni kati yako na wazazi wako inaweza kuwa kubwa sana.

Tafuta mtu mzima anayejali na unayemwamini – shangazi au mjomba, mtu mzima,

rafiki wa familia, mwalimu, kiongozi wa dini au afisa ustawi na omba ushauri. Pengine

wanaweza wakasaidia kutatua tatizo ulilonalo dhidi ya wazazi wako.

79

80

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Urafiki Na Mapenzi

Sura hii ianahusu urafiki na mapenzi. Kila mtu anahitaji urafiki ulio mzuri na kila mtu

anahitaji kujisikia anapendwa na watu wengine.

uRaFiKi

Marafiki wanachukua nafasi kubwa katika

kutufanya sisi tuonekane kama tulivyo.

Wanatufanya tucheke na wanatufanya tujisikie

wenye furaha. Wanatufahamisha mambo

mapya na mawazo mapya, wanakuza upeo wetu.

Wanashiriki ndoto zetu na kujaribu kutusaidia

kutengeneza mipango ya maisha ya baadaye.

Marakifi zetu pia wanaweza kujibu maswali

yetu mengi hasa katika kipindi cha ujana balehe

na wanatusaidia tujisikie vizuri pamoja na

mabadiliko kadhaa yanayotokea. Tukiwa na

matatizo, wanatutia moyo na kutusadia kutatua.

Wanatusaidia kututhibitishia tulivyo.

urafiki ni muhimu wakati wa balehe na

katika maisha yote

naana, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Marafiki zangu wengi walianza kuona mabadiliko katika miili yao

karibia wakati huo huo nilipoyaona mimi. Kwa hiyo sikuwa na hofu

nayo. Tulijadili mabadiliko na niligundua kwamba tuna matatizo

yanayofanana.”

Grace, kutoka Kenya (umri wa miaka 14)

“Marafiki zangu ni watu wazuri. Tunaheshimiana na kupendana

kama dada na kaka. Wananipenda jinsi nilivyo na kama nimekosea

wananiambia wazi namna ninavyotakiwa kufanya. Wengine

wanafikiri ni vibaya kuwa na marafiki wa jinsi nyingine. Mawazo

yao ni mazuri na tunayajadili, tunaweza kuomba ushauri kutoka

kwao.”

81

SURA YA 8

82

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Gift, kutoka Ghana (umri wa miaka 14)

“Marafiki zangu wananipenda na kuniheshimu sana kwa sababu mimi ni

mwaminifu na ninawashauri kuhusu nini msichana anatakiwa kufanya.”

Unaweza kuwa na urafiki na watu wa jinsi moja au na watu wa jinsi tofauti.

Seif, kutoka tanzania (umri wa miaka 13)

“Ninao marafiki wa kike watatu. Tunakaa na kuongea au kusoma

pamoja. Rafiki wa kike ni kama rafiki wa kawaida tu.”

evans, kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Mimi na rafiki yangu wa kike tunasaidiana kazi za shule na

kubadilishana mawazo kuhusu maisha na namna ya kujiheshimu mbele

za watu wazima.”

halima, kutoka Kenya (umri wa miaka 14)

“Kuwa na rafiki mvulana au msichana maana yake ni kusaidiana na

kufanya maamuzi pamoja. Vile vile kuzungumza kama kuna tatizo.”

Wavulana na wasichana wanaweza kuwa marafiki na wanaweza kuwa na urafiki bila ya

kujamiiana. Wavulana na wasichana wanaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi ambayo

hayahusishi ngono. Kwa hiyo tunapotumia maneno “rafiki wa kiume” na “rafiki wa kike”

haina maana ya kwamba mahusiano hayo ni ya kufanya ngono.

anthony, kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Urafiki wetu sio wa kufanya ngono au kufanya kitu chochote

kitakachotufanya tujute baadaye. Urafiki wetu ni wa kusaidiana kama

marafiki na sio kitu kingine.”

Kwame, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Watu wanafikiri rafiki wa kike ni mtu ambaye unahusiana naye kingono

tu. Rafiki wa kike ni mtu ambaye unaweza kumwomba ushauri, mtu

ambaye unaweza kushirikiana naye kwenye matatizo.”

Urafiki mzuri na wa nguvu unapendeza sana. Unakufanya ufurahi.Unachangia katika kukua

kwa hisia kwa sababu unakufundisha jinsi ya kuwa karibu na mtu.

Urafiki mzuri vile vile unachangia katika kujiheshimu. Ukiwa na rafiki mzuri, unajisikia

vizuri. Inapendeza kuwa na mtu ambaye unaweza kumweleza siri zako. Vile vile inapendeza

kuwa na mtu anayejisikia vizuri kukueleza siri zake. Unaweza kushirikiana naye mawazo

bila wasiwasi wa kuchekwa. Unaweza kushirikiana naye siri na kujua kwamba hazitatoka

nje. Inapendeza kufahamu kwamba rafiki yako atakupenda na kukuheshimu hata kama

hukubaliani naye kuhusu jambo fulani.

Kupitia urafiki wa karibu, unaweza kujifunza jinsi ya kukubali au kukataa mambo tofauti.

Unajifunza pia jinsi ya kuwa na nguvu za kutosha kutetea maoni yako.

Kujiamini ni muhimu kwa maisha ya baadaye na kwa mahusiano na watu wengine. Ukweli ni

kwamba marafiki wanakusaidia kujenga stadi nyingi muhimu ambazo unazihitaji ili kufanikiwa

maishani. Stadi hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa:

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Kuwasiliana vizuri na kuwa muwazi kuhusu hisia zako na mawazo yako.

Kusikiliza na kujua hisia za mtu mwingine na maoni yake.

Kusaidia pale mtu anapokuwa na matatizo au anajisikia hovyo.

Kujadili (kwa mfano, wewe na rafiki yako hamjakubaliana kuhusu jambo fulani, utahitaji

kujadiliana na kuafikiana au kufikia mwafaka).

Kushirikiana, kufanya kazi pamoja na kuwajibika kwa pamoja

Kukubali na kuheshimu tofauti za maoni, imani na mazoea. (Kwa mfano, wewe na rafiki

yako mnaweza msiafiki kuhusu jambo fulani. Ni sawa tu.

Hasa urafiki unajengeka katika kipindi cha ujana balehe kwa sababu vijana wengi wanaona

aibu kuongea na wakubwa. Iwapo wazazi wako wanafikiri kutumia muda wako na marafiki

ni kupoteza muda, jaribu kuwaeleza namna marafiki zako walivyo muhimu kwako na kwa

nini. Unahitaji marafiki.

Urafiki mzuri na wa nguvu unachukua muda na bidii kuujenga. Hautokei usiku mmoja na

huwezi kupata marafiki wa kweli kila siku.

JINSI YA KUMTAMBUA MTU AMBAYE SI RAFIKI WA KWELI.

Inaweza ikatokea wakati mwingine mtu ambaye ulifikiri ni rafiki akageuka kuwa rafiki mbaya.

Kwa mfano rafiki anapotoa siri kwa watu wengine, au anaeneza uvumi wa hovyo kuhusu

wewe, huyu hafanyi vile ambavyo rafiki wa kweli anatakiwa kufanya. Rafiki wa namna hii

anaweza kukuumiza, lakini hayo ndiyo maisha. Jaribu kuzungumza naye na muombe aache

kufanya kitu chochote ambacho kina kukasirisha. Kama rafiki yako haachi kukufanyia

vibaya, kaa mbali naye. Kupoteza rafiki inasikitisha/inahuzunisha, lakini utapata rafiki

mwingine aliye bora zaidi.

ayoo, kutoka uganda (umri wa miaka 15)

“Niliwapoteza marafiki zangu wote kwa sababu

hawakuheshimu

maoni yangu. Sasa ninaye rafiki wa kweli mmoja tu, lakini

tunaheshimiana.”

Marafiki wanaweza kuwa chanzo cha shinikizo – Hasa shinikizo la kundi-rika ambalo ni

chanzo kikubwa cha wasiwasi kwa wazazi. Shinikizo la kundi-rika mara nyingi huwafanya

vijana wafanye makosa, kama kunywa pombe, au madawa ya kulevya. Shinikizo la kundi

rika linaweza kuwafanya vijana wajamiiane wakati kwa kweli hawapendi kufanya hivyo.

Florence, kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Ninapata shinikizo kutoka kwa wasichana wengine

wanapojipamba na wanapotoka na kwenda kwa wavulana.

Ninajishauri mwenyewe nisionyeshe tabia mbaya au kufanya

mambo mabaya.”

83

84

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Katika kipindi cha ujana balehe, ni jambo la kawaida kuona vijana wakiwa katika makundi ya

kirafiki, wakilazimika kufanya mambo fulani fulani katika kundi hilo au kuwa na mtazamo fulani

kama unataka kujiunga au kubaki katika kundi hilo. . Jihadhari na shinikizo la kundi rika kwani

lina nguvu sana kwa sababu unataka kupendwa na unataka kuwa sehemu ya kikundi; na unataka

kuwafurahisha marafiki zako ndani ya kikundi na unataka kuhakikisha hubaki nyuma.

Wakati wote hakikisha akili yako iko sawasawa na

unakuwa mkweli. Usijihatarishe ati kwa sababu unataka

kuwa na kundi la marafiki.

Jambo jingine la kukumbuka: Unaweza ukatokea

wakati fulani kipindi cha ujana ukajisikia kama vile

huna marafiki wa karibu. Hii inaweza kukufanya ujisikie

mpweke, mwenye huzuni na wasi wasi. Usihofu kuwa

una tatizo lolote. Inawezekana wewe umekomaa kidogo

kuliko wenzako wa umri mmoja. Labda unataka mambo

tofauti na rafiki zako wa rika moja. Jinsi utakavyo kuwa

unakua na kukutana na watu wapya, utatengeneza

marafiki wazuri na wa nguvu. Kuwa mvumilivu. Ipo siku.!

KueleWana na jinSia nYinGine

Vijana wengi wanapata shida kuelewana na mtu wa

jinsi nyingine. Hawajui jinsi ya kutendeana kwa heshima na inavyofaa, na hawajui wafanye nini

wanapokuwa wamezungukwa na watu wa jinsi nyingine. Vifuatavyo ni vidokezo kwa wavulana:

Usimwangalie au kumpigia mlunzi msichana kwa sababu ya jinsi anavyoonekana, gauni

alilovaa au namna anayotembea.

Msikilize rafiki yako wa kike anachosema na elewa anaposema “hapana” ana maanisha

“Hapana” na sio vinginevyo. Usijaribu kujishawishi mwenyewe kwamba anamaanisha “labda”

au “ndio” wakati anaposema hapana.

Usipitepite karibu na msalani wa wasichana na/au kuziba njia yao.

Usiwanyanyase au kuwatisha kwa makusudi wasichana usiku au sehemu zisizo na watu.

Usivumishe mambo mabaya kuhusu wasichana.

Wasichana vile vile wanaweza kuwa na mtazamo mbaya kwa wavulana. Vifuatavyo ni

vidokezo vya jinsi ya kuelewana na wavulana:

Usiwatafute wavulana ili upate pesa au zawadi kutoka kwao.

Wakati mwingine vijana wa rika lako

wanaweza kukutenga kwenye kundi lao. hii

inaweza kuwa vigumu na unaweza kufikiri

ufanye lolote ili ujiunge nao. Kuwa mkweli

na usijihatarishe kwa ajili ya kupata

heshima yao.

Kubali kwamba wavulana nao wanashawishika na wanazo hisia kama zako. Usiwacheke,

kuwatania au kuwafanyia mzaha.

Kuwa muwazi kwa wavulana. Yaweke wazi yale unayotaka kuyafanya na yale ambayo hutaki

kuyafanya. Sema yale ambayo kweli unayafikiria na usiogope kujieleza. Kuwa na uhakika,

jiamini, kama hutaki kufanya jambo fulani sema “HAPANA” na ng’ang’ania hivyo hivyo.

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Usianzishe uzushi kuhusu wavulana.

Mara nyingi wasichana na wavulana wanaishia katika mahusiano mabaya kwa sababu hawana

uelewa na uzoefu wa namna ya kuishi na jinsia nyingine. Wavulana hawajui wasichana

wanataka nini kutoka kwa wavulana na wasichana vile vile hawajui wavulana wanataka nini

kutoka wasichana. Hapa kuna vidokezo vichache vitakavyokusaidia:

• Wasichana wanataka upendo, kujaliwa, uaminifu na heshima. Wasichana wanapata

hofu kama wavulana hawawaheshimu. Wanapenda wavulana wanaotumia muda kuwasikiliza

bila mzaha.

• Kuwa pamoja: Wasichana wanaona kwamba kuwa pamoja na kujumuika na wavulana

kunafurahisha na kusisimua. Pia wanawapenda wavulana ambao wanaweza kuwasaidia

wanapopata matatizo na ambao wanaweza kustarehe, kutaniana na kucheka nao.

• uhuru: Wasichana wanataka kupewa nafasi ya kufikiri wenyewe.Wanawapenda wavulana

wanaotambua kwamba wasichana wana akili na wanapenda kuzitumia.

• Wavulana wanaojiamini: Wasichana wanawahusudu wavulana ambao wanajiamini na

ambao hawawaogopi wasichana.

• Wavulana wasiojifanya: Wasichana wanawapenda wavulana ambao hawaigi wengine

na kujifanya wana hali fulani kumbe sio. Wavulana wanataka nini? Wavulana wengi wanayataka

yale yote ambayo wasichana wanayataka katika mahusiano.

• Wavulana wanataka upendo, kujaliwa, uaminifu na heshima. Wavulana wengi wanapenda

kuwa na msichana anayejali na kusaidia – mtu anayesikiliza, aliye na heshima na

asiye na mzaha

• Kuwa pamoja: Kila mtu anapenda kujumuika. Wasichana na wavulana pia wanataka mtu

ambaye wanaweza kutumia muda naye kucheka, kusimuliana hadithi na kuzungumza

kuhusu maoni yao, ndoto na hata malengo.

• uhuru: Wavulana wengi wanasukumwa kutenda mambo kinguvu. Wanatenda kama vile

hawana hisia na hawajisikii kitu. Wanataka mtu ambaye wanaweza kushirikiana naye

kimawazo na kihisia.

• Wasichana wanaojiamini: Tofauti na ambavyo wasichana wengi wanavyoamini, wavulana

wanawapenda wasichana wanaojiamini– wasichana ambao hawaogopi kujieleza

wenyewe kwa uhuru.

• Wasichana wasiojifanya: Wavulana wanawapenda wasichana ambao ni halisi - wasichana

ambao hawaigi mambo ya wengine kama kukomaa, kujisikia au kuringa.

Msingi wa mahusiano mazuri ni urafiki wa nguvu – sio tu jinsi mtu anavyoonekana au mvuto

wa kimapenzi. Katika uhusiano mzuri, hakuna mtu anayejaribu kumdhibiti mwenzake au

kumlazimisha katika kufanya mambo. Pia hakuna mtu ambaye anamnyonya mwenzake au

kumtumia mwenzie kwa namna yoyote ile.

Kumbuka kuwa mahusiano mazuri na ya kudumu hayaji katika muda mfupi. Inachukua muda

kufahamiana kikweli kweli na kujenga urafiki wa nguvu.

KUANZA MAHUSIANO NA MTU UNAYEMPENDA.

Ujana balehe ni wakati ambao unaweza kuanza kujisikia una hamu au unavutiwa na watu

wengine. Unaweza kumuona mtu shuleni kwako ambaye anaonekana mzuri na unafikiria

ungependa muwe marafiki.

85

86

Lakini huna uhakiki utamuanza namna

gani. Hujui kama atapendelea kuwa rafiki

yako. Unachokijua ni kuwa anaweza asiwe

amegundua nia yako.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Prisca, kutoka Kenya

(umri: miaka 14)

“Njia nzuri ya kumwendea

msichana au mvulana

ni kumwendea kwa

upole. Njia nzuri ya

kuanza urafiki ni kwa

kumjali rafiki yako na

kusaidiana naye nyakati

za matatizo.”

Mercy, kutoka Ghana

(umri: miaka 16)

“Kitu cha kwanza cha kufanya ili kuanza urafiki ni kuwa rafiki wa mtu huyo

na mkishafahamiana vizuri unaweza kumuambia kilichoko kichwani au

moyoni mwako kwa kuzungumza na kufungua hisia zako.”

Ni vigumu kumwendea mtu mpya hususani kama unampenda kimapenzi. Unaweza kuogopa

kumwendea msichana au mvulana kwa sababu hutaki kukataliwa na kuumiza roho yako.Kwa

upande mwingine iwapo hutamfuata mtu huyo hutakuwa na mahusiano ya aina yoyote na

mtu huyo kabisa.

Kuna njia mbili za kujua kama mtu anakupenda na

ana hamu na wewe. Unaweza kuzungumza naye

wewe mwenyewe au unaweza kumwomba rafiki

yako aongee naye.

Iwapo utachagua kumpata rafiki wa kumwendea

mtu unayempenda, kuwa mwangalifu kuchagua

rafiki mzuri - mtu ambaye anaaminika sana.

Usingependa kumchagua rafiki ambaye ataishia

kuwaeleza watu wengine kwamba unampenda

mtu fulani. Vile vile usingependa kumchagua rafiki

ambaye ataongea maneno mengi na yule mtu. Kwa

mfano unaweza kutaka rafiki yako ataje jina lako

tu kuona kama yule mtu anakujua wewe ni nani na

kama ana nia na wewe.

ujana balehe ni wakati ambao utaanza kujisikia

kuvutiwa na watu wengine

Kama unavutiwa na mtu, onyesha urafiki na

kuwa mkweli. tafuta nafasi ya kukutana nae.

Ni sawa kabisa kumuomba rafiki yako kumuendea mtu unayempenda, lakini itafikia wakati

ambao utalazimika kuongea naye wewe mwenyewe. Hii inaweza kukuwia vigumu.Unaweza

kuona aibu. Mikono inaweza kulowa jasho. Unapoanza kuzungumza unaweza kusahau

kabisa ulichotaka kusema. Haya yote ni hisia za kawaida kwa mtu anapokuwa na hali ya

wasiwasi au ya kusisimka.

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Jaribu kutulia na kujikumbusha kwamba wewe ni mtu unayevutia unayefurahisha na mwenye

akili. Huna cha kupoteza. Kuwa mwema kwa mtu unayempenda. Anza mazungumzo naye. Tafuta

anapendelea nini na nenda ukamwone. Iwapo msichana au mvulana ni mwema, chukua hatua

inayofuata. Mweleze ungependa mfahamiane zaidi. Muulize kama anaweza kwenda kufanya kitu

na wewe.

KujenGa MahuSianO YenYe nGuVu

Zipo njia nyingi za kumuelewa mtu vizuri na kujenga urafiki wa karibu na mahusiano mazuri.

Mnaweza kwenda kutembea naye, kwenye sherehe, kuangalia sinema au kunywa na kula pamoja.

Mnaweza kucheza michezo na mnaweza kujihusisha katika shughuli za kijamii au za kidini

pamoja. Mnaweza kusoma pamoja. Mnaweza kutumia muda pamoja mnapokuwa kwenye kikundi

cha marafiki.

Kama lengo lako ni kumuelewa mtu vizuri na kujenga mahusiano ya karibu na ya kudumu,

mkifanya shughuli mbalimbali pamoja, ni vizuri zaidi kuliko kujamiiana tu. Ukweli ni kwamba

kuanza kujamiiana kabla mahusiano hayajawa ya karibu na yenye nguvu kunaweza kuharibu

mahusiano. Au mahusiano yenu yanaweza yakawa ya kujamiiana tu.

Kumbuka ngono na upendo ni vitu viwili tofauti. Kujamiiana hakumaanishi watu wawili hawa

wanapendana.

Sherifan, kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Unapofanya ngono, haina maana mnapendana. Mtu anaweza

akawa anakutumia, kwa sababu unapendeza na unamvutia, lakini

sio kwa sababu anakupenda”.

hamson, kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Ngono na kupenda havifanani. Ukilala na msichana haina maana

kwamba msichana huyo anakupenda”.

Watu wengi wanafikiri ngono inafanya mahusiano yawe na nguvu, lakini hii sio kweli.Ngono sio

njia nzuri ya kuweka mahusiano, na wakati mwingine inaweza kuharibu mahusiano kabisa.

Okakah, kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Mmoja wa marafiki zangu wa karibu aliniambia kwamba ningempoteza

rafiki yangu wa kike kama nisingemridhisha kimapenzi.

Kwa kweli hili lilinipa dukuduku sana kwa hiyo nilianza kujaribisha

naye, hata kama hakuwa katika hali ya kutaka. Hili lilinifanya

niwe na dukuduku zaidi. Nilimwuliza kwa nini alikuwa katika

hali hiyo. Alinieleza kwamba kufanya mapenzi kungesababisha

mimba isiyotakiwa na kama ikitokea tungepoteza hadhi yetu

katika jamii. Mwishowe tuligundua kwamba wapenzi wanahitaji

kuheshimiana na kuelewana, na wanahitaji kupuuza shinikizo

kutoka kwa vijana wengine.”

87

88

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Marafiki wa Okakah walimwambia kwamba angempoteza rafiki yake wa kike iwapo asingefanya

naye ngono, lakini ukweli ni kwamba ilikaribia kumpoteza rafiki yake wa kike kwa kumwambia

wafanye ngono! Alichokuwa anaambiwa na rafiki zake haikuwa kweli.

Kumbuka, watu wawili wanaweza kuwa na mahusiano ya karibu sana bila ya hata kufanya ngono.

Wanaweza kubadilishana uzoefu; wanaweza kujifunza mambo mengi ya muhimu kuhusu kila

mmoja wao – jinsi kila mtu anavyoona maisha, jinsi watakavyofanya maamuzi pamoja, kila mmoja

atakuwa mwenzi na mzazi wa namna gani na namna kila mmoja anavyoiona mipango ya maisha ya

mwenzake.

Yote haya ni muhimu kabla hujaanza mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote. Mnatakiwa kwanza

muwe marafiki wa kweli. Ngono bila urafiki wa kweli wakati wote ni hatari kwa afya yako na kwa

moyo wako. Unaweza kuumia. Kwa hiyo kwa ajili ya mahusiano yenye afya na afya ya ujinsia –

kuweni marafiki wa kweli kwanza.

MaPenZi

Ni vigumu kutafsiri mapenzi kwa sababu yanahusu hasa hisia. Mapenzi ni kitu kikubwa na kuna

aina mbalimbali za mapenzi. Mapenzi kwa wazazi na marafiki, mapenzi kwa rafiki wa kiume au wa

kike na mapenzi kwa jamii.

Vile vile mapenzi ni hisia ngumu, na watu wanaweza kueleza maana ya mapenzi kwa njia tofauti

kutegemeana na uzoefu wao na mahusiano yao ya kupenda. Mapenzi ni hisia yenye utata na watu

hutoa tafsiri ya mapenzi kutegemeana na uzoefu wa mahusiano ya kimapenzi.

Godfrey, kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 19)

“Siwezi kuyaelezea mapenzi. Ni vizuri sana kuwa katika mapenzi.”

Patrick, kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Mapenzi ni muungano wa watu wawili ukiwa na sanaa ya

kuelewana na kuwa mwaminifu kwa kila mtu.”

Sherifan, kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Mapenzi ni kitu ambacho kipo kati ya watu wawili. Aidha

mvulana au msichana. Mapenzi ni kushirikiana katika matatizo

na kujaliana”.

Stabisile, kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 19)

“Kuwa na mpenzi ni mojawapo ya vitu vizuri duniani”.

jennifer, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Mapenzi ni wewe, familia yako na marafiki kushirikiana

mawazo pamoja. Hivi ndivyo ninavyofahamu kuhusu mapenzi.”

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Kuwa na mpenzi kunaweza kuwa kama uchawi.

Unakutana na mtu maalumu halafu kila kitu

kinabadilika. Jua linaonekana kung’ara zaidi, nyasi

zinakuwa za kijani zaidi na unajiona kama unatembea

hewani.

Kuwa na mpenzi ni tofauti na kumpata rafiki mpya.

Unapokuwa na mpenzi, unaweza kujisikia joto, na

hisia zilizojaa. Unaweza kujisikia kutabasamu kila

wakati kwa sababu mawazo ya yule unayempenda

yanakufanya uwe na furaha. Unataka kuwa na mtu

huyu kila wakati. Unapata njozi za mchana za tamaa

ya mambo yasiyowezekana kuhusu mtu huyo. Kuna

wakati unaweza kupoteza hamu ya kula au kukosa

usingizi usiku.

Sherry, kutoka Ghana (umri wa miaka 19)

“Ni jambo la ajabu. Huelewi kinachokupata. Huwezi kuelezea.

Unajaribu kuacha kumfikiria lakini unagundua mawazo hayawezi

kutoka. Unaweza ukawa unasoma kwa ajili ya mtihani lakini unaona

akili yako haiendani na macho yanavyoangalia ukurasa wa kitabu.”

Sara, kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Nina miaka 18 na yupo mvulana ninayempenda sana. Anapokuwa

mbali na mimi, ninashindwa kuwa makini na kitu chochote.

Anapokuwepo karibu na mimi ninatetemeka na siwezi kufanya

kitu chochote cha maana,hata kama akiniambia nijifanye kama

hayupo. Hisia hizi zinanifanya nichanganikiwe kabisa.”

angela, kutoka Kenya (umri wa miaka 18)

“Inasisimumua kuwa katika mapenzi.Hutaki kumuumiza.Unajisikia

mpya kama vile kitu kimeongezeka.Wakati mwingine kujisomea

inakuwa matatizo.Akikuandikia barua ,itasomwa kwa masaa.

“Penzi la kwanza” ni mojawapo ya uzoefu mzito wa maisha. Kuwa na mpenzi sio sawa na

uzoefu wowote ulioupata ukiwa mtoto. Ni kitu ambacho unatakiwa kukichukulia taratibu.

Usikimbilie. Tunza moyo wako na wa wale unaowapenda wachukulie kwa uangalifu.

Diana, kutoka Zambia (umri wa miaka 17)

“Ninafikiri kuwa mapenzi yaje kikawaida kuliko inavyotokea kwa

vijana ambao wanaenda kutafuta mapenzi badala ya kuacha mapenzi

yawatafute. Watu wanatakiwa kuangaliana kwa njia chanya.

Mapenzi yanaweza kupatikana bila kulazimisha ili usije ukajuta

baadaye.”

89

90

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kama una mapenzi ya kweli na mtu, mtaheshimiana. Hamtafanya kitu chochote kitakacho

muumiza mmoja wenu. Hutamlazimisha mwenzako kufanya kitu chochote ambacho hakipendi.

Utataka awe na furaha. Linganisha mapenzi yako na pointi hizi:-

Mapenzi yanakufanya wewe na unayempenda kujisikia vizuri mwenyewe na kila mmoja wenu.

Mapenzi ni uaminifu, kujaliana na ukweli.

Mapenzi ni heshima na hadhi

Mapenzi hayaruhusu mtu mmoja kumtumia mtu mwingine.

Mapenzi hayaweki ngono mbele kabla ya urafiki na kamwe mapenzi yasiwe sababu ya

kufanya ngono isiyo salama.

Mapenzi ya kweli yanahusisha hisia ya kuwajibika na kujihusisha kwa watu wengine. Ni hisia

inayotafuta mambo mazuri kwa ajili ya mtu mwingine. Mapenzi hayakasirishi, yana uvumilivu

wala hayana maana ya kushikanashikana. Mapenzi hayana kinyongo. Watu wengine wanadhani

wivu ni dalili ya mapenzi, Si kweli; wivu ni dalili ya kutojiamini na kutoamini kuwa unajali.

Wivu si dalili ya mapenzi. ni dalili ya kutojiamini.

Hata hivyo wakati mwingine wivu ni dalili ya matatizo makubwa zaidi. Kwa mfano, wivu ni dalili

ya kuwa mtu anataka kumdhibiti mtu mwingine. Mahusiano mengi ya unyanyasaji (wanaume

wanapiga wake zao au wanaume wanaobaka marafiki zao wa kike) wanaanza na tabia ya wivu,

ambayo hujengeka kuwa mbaya.

KuPuMbaZiKa

cathy, kutoka uganda (umri wa miaka 17)

“Hisia zangu haziji kwa haraka. Hii ni kwa sababu wakati wote

ninataka kumjua mtu ambaye ananivutia vizuri zaidi. Ninazionyesha

hisia zangu baada ya kuridhika kwamba hayupo

kunitumia bali kwa mahusiano ya kweli.”

Wakati mwingine inakuwa vigumu kufahamu kama mapenzi yenu ni ya kweli. Moyo unadunda na

unajisikia kukosa pumzi na kizunguzungu unapomwona mvulana au msichana fulani.

Unadhani lazima ni mapenzi yanakupa kiwewe! Lakini unapomfahamu mvulana au msichana

huyo, hisia zinatoweka ghafla, na hujisikii kuvutiwa tena na mtu huyo. Hivyo ilikuwa

kupumbazika.

Kupumbazika hakuna ubaya na ni kitu cha kawaida tu. Ukweli ni kwamba vijana balehe

wengi hupumbazika. Kupumbazika kunaweza kusisimua, kufurahisha na hatari isiwepo,

kupumbazika hakugeuki kuwa mahusiano. Unaweza ukawa umepumbazika na mtu na

usitake kuwa na mahusiano naye. Unaweza kufurahi kwa kumtamani kwa mbali. Hiyo ni

sawa tu.

Kuachana KiMaPenZi

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

naana, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Ninafahamu kwamba unapompenda mtu unafanya kile

kilicho

kizuri sana kwa ajili yake na kuwa na yale yote

yanayompendeza moyo wake. Lakini sijawahi kumpenda mtu.

Ninaweza kusema nimewahi kuwahusudu baadhi ya wavulana,

lakini kamwe sijawahi kupenda.”

Sio kila mapenzi hudumu daima. Hisia za kupenda zinaweza kutoweka haraka kama

zinavyokuja, lakini vile vile zinaweza kuwa za kweli na zenye nguvu.

Wakati mwingine, jinsi mnavyokua watu wazima wewe na rafiki yako mnaweza mkajikuta

mmeachana. Ndoto zenu zinawachukua njia tofauti. Mtajikuta yale mnayopendelea

yamebadilika na mnakosa cha kuzungumza. Hamcheki tena pamoja kama mlivyozoea.

Sio vizuri kwa afya yako kihisia kuwa katika mahusiano wakati hakuna mapenzi.

Inahuzunisha na inaweza kuwa vigumu hususani kama mmoja wapo bado ana hisia za

kupenda wakati mwingine hajisikii kabisa.

Iwapo unataka kuvunja mahusiano, kuwa mkweli kuhusu sababu zinazofanya kuvunja

mahusiano. Vile vile kuwa na huruma na mfikirie rafiki yako. Jaribu kutomuumiza, lakini

wakati huo huo maliza mahusiano hayo– usimwache aendelee kutegemea au kufikiria

kwamba utabadilisha mawazo yako.

Iwapo rafiki yako atakuacha, inaumiza sana. Ni vigumu kuacha kufikiria kwamba labda

atabadilisha mawazo kukurudia. Inaweza kuwa vigumu kuamini kwamba hakupendi tena.

Unaweza kujisikia mpweke sana na uliyekataliwa.

Jipe muda wa kumudu maumivu.Usikimbilie kutafuta mahusiano mapya na mtu mwingine

ili ujisikie nafuu. Hata kama utakasirika na kuumia usimlaumu mtu mwingine na kamwe

usieneze uvumi au hadithi mbaya kuhusu mwenzi wako wa zamani. Hizi sio njia nzuri za

kuchukua kwa mtu aliye komaa.

Kupoteza marafiki na kupata marafiki wapya ni sehemu ya maisha. Hatimaye utapata

mpenzi wa kweli ambaye mtaishi naye, hivyo vumilia. Kwa wakati huu lenga katika kuwa

mtu mwenye huruma na anayependeka. Ukijipenda, ni rahisi kupenda watu wengine na

wewe mwenyewe kupendwa.

91

92

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 8

urafiki na mapenzi

Urafiki mzuri na mahusiano mazuri yanakusaidia ujisikie vizuri. Marafiki wazuri

wanakusaidia kutatua matatizo, kukuonyesha mawazo mapya na kushiriki na wewe

katika ndoto za maisha yako ya baadaye.

Wakati mwingine watu unaofikiria ni marafiki zako wanaweza kukushinikiza kufanya

jambo ambalo hulitaki, kama vile kujamiiana au kula madawa ya kulevya. Hii tunaita

shinikizo la kundi rika. Mtu yeyote anayekushinikiza ufanye jambo ambalo hutaki

kulifanya sio rafiki mzuri. Usiruhusu mtu yeyote akakushinikiza ufanye jambo ambalo

unajua ni makosa na ni hatari kwako.

Marafiki wazuri wanaweza wakawa wa jinsi moja au jinsi nyingine. Wavulana na wasichana

wanaweza kuwa marafiki bila ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Maneno

“rafiki wa kiume” au “rafiki wa kike” sio lazima yamaanishe kwamba mahusiano ni ya

kimapenzi. Marafiki wa jinsi tofauti wanaweza kuwa na urafiki wa karibu na kupendana

sana bila ya ngono.

Inaweza ikawa vigumu kuelewana na mtu wa jinsi nyingine kwa sababu wavulana na

wasichana hawana uhakika nini mwingine anataka katika mahusiano. Kumbuka, watu

wengi – wavulana na wasichana – wanataka mambo yanayofanana katika mahusiano.

Wanataka heshima, uaminifu, ukweli, kuelewana na kujali.

Kama unamtaka msichana au mvulana unayempenda, jaribu kuvuta subira na kuwa

mkweli. Kuwa mwema. Toka, nenda ukamwone. Kama anaelekea kupenda nia yako,

mwombe kama mnaweza kwenda kushiriki shughuli fulani kwa pamoja.

Kujenga mahusiano mazuri kunachukua muda na uvumilivu. Ngono sio njia nzuri ya

kujenga mahusiano. Ukweli ni kwamba ngono inaweza kuharibu mahusiano. Kujamiiana

haina maana ya kwamba watu wawili wanapendana au urafiki wao ni wa karibu sana.

Ngono bila urafiki wa kweli ni hatari kwa afya yako na moyo wako.

Kumpenda mtu ni jambo nzuri sana, mapenzi yanakufanya ujisikie vizuri mwenyewe na

mtu mwingine. Furahia hisia lakini usikimbilie jambo lolote. Kumbuka mapenzi yanahusu

heshima na kujaliana. Mapenzi hata siku moja yasiwe sababu ya kufanya jambo

ambalo litaweka afya na maisha yako ya baadaye hatarini. Mapenzi hayawezi kuwa

kisingizio cha kufanya ngono isiyo salama.

Mahusiano hayadumu milele. Kama ukiachwa, sio vizuri kulazimisha mahusiano. Kuwa

mkweli kwa rafiki yako, lakini kuwa na huruma na umfikirie pia. Jaribu usiumize hisia

zake.

Kama mtu amekuacha, unaweza kuhuzunika sana na kujisikia mpweke. Lakini usikate

tamaa. Siku moja utampata mtu mwingine sahihi wa kumpenda. Jipe muda wa kustahimili

ulichopoteza. Usikimbilie mahusiano mapya na usieneze uzishi kuhusu mtu huyo.

Ujinsia Na Ngono

Kuna utata mwingi sana kuhusu neno ujinsia (sexuality) na kujamiiana. Watu wengi wanafikiri

ujinsia maana yake ni kujamiiana. Wengine wanafikiri kwamba huwezi kuwa binadamu hai

mwenye ujinsia na mwenye hisia za kimapenzi hadi uanze kujamiiana.

Imani hizi si za kweli; kila mtu anao ujinsia tangu

kuzaliwa hadi kufa.

Kuwa na ujinsia kunaweza kumaanisha:

Kujisikia unavutia na mwili wako

umejengeka vizuri.

Kujisikia mwenye hisia za kuwa karibu na

mtu fulani.

Kufurahia kuguswa na kukumbatiwa.

Kujishika mwili wako mwenyewe.

Kuvutiwa na mtu mwingine.

Kufikiria hadithi za kimapenzi akilini

mwako.

Kuwa na mawazo au hisia za kimapenzi.

Wakati wa ujana balehe ndio muda ambao

unaweza kuutambua zaidi ujinsia wako -

unavyojisikia, unavyofikiri, unavyojiheshimu

kama mvulana au msichana, na unachokitaka

kuhusu uhusiano wa karibu au pendo la mtu.

Ulipokuwa mdogo pengine hukufikiria kuhusu

mambo haya lakini wakati wa ujana, unaweza

kuanza kufahamu maana ya kuwa mwanaume

au mwanamke. Pia unaweza kuanza kuvutiwa

na watu wengine na kuanza kuona hisia za

kimapenzi, matamanio na ndoto.

UNAJUA maana ya “Ujinsia”?

Ujinsia ni suala lenye utata kueleweka. Ni

zaidi ya kujisikia hisia za kimapenzi au

kujamiiana. Ujinsia ni pamoja na:

Kufahamu na kuwa na hisia kuhusiana

na mwili wako na miili ya watu wengine.

Uwezo wako na nia ya kuwa karibu na

mtu mwingine.

Uelewa wako kuhusu nini maana ya

kuwa mwanamke au mwanaume.

Hisia za mvutano wa kijinsia na watu

wengine.

Uwezo wako kimwili wa kuzaa.

Ujinsia ni muhimu, unafurahisha, na ni

sehemu ya asili ya kuwa mtu. Lakini wakati

mwingine watu wanatumia ujinsia wao

katika namna isiyofaa kwa kushawishi,

kuamuru au kutania watu wengine. Hii ni

pamoja na kuonyesha mapenzi kwa mzaha,

upotoshaji na unyanyasaji kijinsia kama

kubaka/kunajisi n.k. Usitumie ujinsia kama

kifaa cha kupata kitu au kunyanyasa au

kumuumiza mwingine.

93

SURA YA 9

94

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Haya ni mabadiliko ya kufurahisha, lakini yanaweza vile vile kukupoteza – hasa kwa kuwa kuna

miiko mingi kuhusu ujinsia na jinsia. Kwa mfano, watu wengine wanafikiri kwamba kuwa na hisia

ya mapenzi ni dalili kwamba lazima wajamiiane, lakini hii si kweli kwani hisia za kimapenzi ni

sehemu ya kuwa binadamu. Kila mtu anahisia za kimapenzi.

Sura hii inahusu ujinsia na jinsi watu wanavyoonyesha hisia za kijinsia. Kuna mambo mengi

unahitaji kuyajua ili uweze kufanya maamuzi mazuri kuhusu ujinsia na ngono/kujamiiana.

ujinSia WenYe aFYa njeMa

Kuwa mtu mwenye afya njema kijinsia inamaanisha kuwa na uwezo wa kuonyesha hisia zako

katika njia ambazo hazikuhatarishii wewe au mtu mwingine. Yaani huhatarishi hisia na afya yako

na wala huhatarishi hisia za watu wengine na afya zao.

Kama kijana balehe, unaweza kuanza kulifanyia kazi jambo la kuwa kijana mwenye afya njema ya

kijinsia. Unaweza kuhakikisha unajibidiisha kujua kadri iwezekanavyo tofauti kati ya ukweli na

uongo inapokuja kwenye suala la ngono/kujamiiana. Pata muda wa kujifunza kuhusu mwili wako,

hisia zako na namna ya kuwa salama na mwenye afya kijinsia.

Cha muhimu zaidi, pata muda wa kufikiria chaguo lako linaloendana na vitendo vya jinsia yako.

Chaguo lako mojawapo linaweza kuwa “hakuna ngono” au “muda bado”. Unaweza kusubiri kabla ya

hujakimbilia kujamiiana. Unaweza kuhakikisha unaelewa matokeo ya kufanya ngono isiyo salama

na namna ya kujikinga.

Mara nyingine inaweza ikawa vigumu kuwa na afya njema kijinsia. Hakuna mtu

atakayekufundisha kuhusu afya njema, iwe shuleni au nyumbani.

Njia kuu ya kupata habari ni kupitia kwa marafiki, kaka na dada zako, video, miziki, na magazeti.

Hata hivyo njia hizi zinaweza kukuchanganya na kukupoteza.

Magazeti, muziki, vitabu vya hadithi na matangazo yanatoa taarifa

zinazo changanya kuhusu ngono.

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Baadhi ya video nyingine na riwaya za mapenzi, ngono inakuwa kama jambo la kuvutia na halina

matatizo. Ngono inakuwa kama kitu tu kinachotokea na hakuna mazungumzo kati ya watu

wawili kama wanahitaji kufanya mapenzi au la, na watumie kondomu au wasitumie. Hata kama

hawatumii kondomu, watu katika video na riwaya hawaonyeshi iwapo wanapata matatizo ya

kupata mimba zisizohitajika au kupata magonjwa ya zinaa kama VVU/UKIMWI.

Katika muziki, wanaume na wanawake wanaimba kama waliopoteza matumaini na hawajali

kuhusu ngono. Wanaonekana kutojali kuhusu VVU au matatizo mengine. Wanachotaka ni

mapenzi. “Mawazo yangu yananiambia “hapana” lakini mwili unaniambia “ndiyo” unaendelea

wimbo fulani wa rapu. Mwingine unasema: “sijui umenifanya nini hadi ikanisababishia kupenda

kama mwenda wazimu”.

Muziki ni mzuri, unagusa hisia za ndani ya moyo kabisa.Video na riwaya vinaweza kukufanya

uasi maisha yako ya kila siku, lakini havikusaidii ushughulikie mahusiano yako. Havikusaidii

ujue kuzungumza na msichana au mvulana wako kuhusu iwapo mfanye au msifanye ngono. Na ni

ukweli havikusaidii kukuwezesha uzungumze na mwenzi wako kuhusu kutumia kondomu.

Hata mtu unayemfahamu anaweza akakuchanganya kuhusiana na jinsia na ujinsia. Wazazi wengi

hawapendi kuzungumzia maswala ya ngono na watoto wao, hivyo inaweza kuwa vigumu kujifunza

kutoka kwao.

Gifty, kutoka Ghana (umri wa miaka 14)

“Kwa nini wazazi wetu wanaona vigumu kutufundisha mambo ya

ngono? Au ni kwa sababu wanafikiri tutajaribisha au vipi?”

Vijana wengi na marafiki, wanaweza kusema kuwa wameshawahi kufanya ngono hata kama

hawajawahi. Unaweza kuanza kufikiria na wewe ukafanye ngono ili ulingane nao. Wenzako

wanaweza pia wakazua kwamba unahitaji ngono ili upone maumivu ya hedhi au kufanya uume

uwe mkubwa na wenye nguvu. Lakini mambo haya si kweli. Kujamiiana hakuwezi kukuponya

maumivu ya hedhi, na wala hakuwezi kufanya uume uwe mkubwa.

Kwa nyie wavulana, kaka na wajomba zenu wanaweza kuwa walichukua hatua za hatari kuhusiana

na mapenzi ambazo wanazijutia hivi sasa. Cha kushangaza ni kwamba wanawashawishi muanze

ngono kuhakikisha kwamba nyie ni wanaume.

Kwa nyie wasichana, hakuna ambaye amewahi kukusifia huko nyuma, lakini sasa wavulana

wanakuambia wewe ni mzuri, na hii inakufanya ujisikie vizuri. Je, kwa hilo tu unatakiwa uonyeshe

mapenzi kwao na kuwapa matumaini?

Inaweza ikawa vigumu kwako kuona la maana kuhusu maelezo unayopata kuhusu ngono. Hata

hivyo, jambo muhimu kuhusu afya njema ya ujinsia ni kuonyesha tofauti kati ya tabia yenye

mapenzi yenye afya na njia ambazo zina madhara kwako na kwa wengine. Kabla hujachukua

hatua katika hisia zako za kijinsia fikiria matokeo ya hatua za matendo yako. Je wewe au yeyote

yule atakuwa hatarini kupata mimba isiyotakiwa, VVU/UKIMWI au magonjwa ya ngono? Je,

kutenda kutokana na hisia kutasababisha matatizo, kama vile kutoelewana? au kutoeleweka

kimawasiliano katika mahusiano? Je, itasababisha mimi au mwenzi wangu kujisikia vibaya? Je,

hisia za mtu yeyote zitaathirika?Kuwa mwenye afya kijinsia kunamaanisha kupata muda wa

kufikiri kuhusu jambo kabla ya kulifanya ili kufurahisha hisia zako za kijinsia.

95

96

hiSia Za KijinSia

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mambo mengi utayagundua punde utakapoanza kusikia ashiki au kusisimuka kijinsia. Utayahisi

mwili mzima. Kwa wanaume, dalili ya hisia ya kijinsia ni uume kusimama. Kwa wasichana, ni

unyevunyevu ukeni. Hii inatokea kwa sababu damu ya ziada kutoka kwenye mishipa ya damu

inaingia kwenye spongi maalum kwenye tishu ndani ya uke au uume. Kwa wavulana tishu

za spongi zinavimba na kusababisha uume kuwa mrefu, mgumu, mpana na kusimama. Kwa

wasichana, tishu za spongi zinavimba ndani ya kuta za uke na kusababisha utoaji wa majimaji,

ambayo yanalainisha eneo la uchi na kusabisha lilowane.

Unaweza kujisikia hisia za kijinsi zenye kusisimua kwa kusoma riwaya za kimapenzi au kumfikiria

mvulana au msichana unayempenda. Kama ulikuwa na mvulana au msichana na mlikuwa

mnashikanashikana, unaweza kusisimuka zaidi.

Utafanya nini kuhusu hisia za kijinsi? Jambo la kwanza, huhitaji kufanya ngono unapopata hisia za

kijinsi. Kujamiiana ni njia moja wapo ya namna watu wanavyoonyesha hisia za kimapenzi. Lakini

zipo njia nyingi ambazo watu wanaweza kuonyesha hisia zao za kimapenzi - katika mazungumzo,

kushikana mikono, kukumbatiana, kupakatana, kubusiana na kushikanashikana.

Njia hizi za kuonyesha mapenzi zinaweza kuwa za kuridhisha na zina hatari ndogo sana

ya kuambukizwa VVU (soma sura ya 10 zaidi juu ya VVU na magonjwa ya zinaa). Kupumua

na mapigo ya moyo yanaweza kuongezeka. Mwili mzima unaweza ukajisikia kusisimuka na

kuchangamka. Unaweza kuwa na hali hiyo ya kusisimua kwa masaa mengi. Huhitaji kwenda zaidi

ya hapo. Mvulana hahitaji kumwambia msichana kuwa anahitaji kujamiiana nae eti kwa kuwa

amesimamisha. Si kweli. Uume wako utaacha kusimama pindi utakapoacha kumpakata msichana.

Ni muhimu kujua kwamba, si migusano yote inaleta hisia za kufanya ngono. Kama unasukumwa

bila kupenda ili ufanye ngono, hutajisikia vizuri. Msisimko wa kijinsia unatokea watu

wanapokuwa na furaha na wamepumzika (soma sura 12 zaidi juu ya unyanyasaji kijinsia na

vitendo vya ngono visivyotakiwa).

PunYetO

Punyeto ni kitendo cha mtu kushika sehemu zake za siri – uume, uke, matiti au sehemu nyingine

za mwili ambazo zinasisimka kijinsia. Punyeto ni mojawapo ya njia ambayo watu wanaelezea

hisia zao za kijinsia.

Wanaume kwa wanawake wanaweza kupunguza hisia za kutaka kujamiiana na bado wakapata

starehe kwa kupiga punyeto. Kwa kweli watu wengi wanapiga punyeto kipindi fulani katika

maisha yao. Wavulana wanapiga punyeto mara kwa mara kuliko wasichana. Wasichana na

wavulana wengine wanaanza kupiga punyeto wakati bado watoto na wanaendelea kufanya hivyo

maisha yao yote. Wengine wanaanza wanapobalehe; wengine wanaanza wakiwa watu wazima.

Baadhi ya watu hawapigi punyeto, na wengine wanafikiria kuwa starehe ya ngono na kupiga

punyeto ni kinyume na madhehebu yao au imani na utu wao.

Katika mila nyingine, kuna uzushi mwingi

ambao umekusudiwa kuwakatisha tamaa

watu wasipige punyeto. Haya ni baadhi ya

mambo yasiyo ya kweli kuhusu punyeto,

kwamba:-

Kupiga punyeto kunafanya upate kichaa.

Kupiga punyeto kunafanya uote nywele

kwenye kiganja cha mkono wako;

kunasababisha vipele usoni au kupofuka

macho.

Punyeto linafanya upauke rangi ya mwili

na inasabisha utumie mbegu zote za

kiume.

Punyeto linasababisha mtu awe dhaifu

na kufanya mwanaume ashindwe kupata

watoto.

Punyeto linafanya uwe na majivuno na

uwe mbinafsi.

Hakuna ukweli kuhusu uzushi huu. Kutokana

na utalaam wa kitabibu na kisayansi, punyeto

linachukuliwa kama sehemu ya makuzi.

Haijalishi kama utapiga punyeto au hupigi.

Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha

kwamba punyeto ina athari mbaya kimwili

ama kisaikolojia.

Punyeto linaweza kuwa na matatizo iwapo

tu:-

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Limezidi mno – mtu hawezi kufanya kazi

za kutwa mpaka apige punyeto.

Linafanywa maeneo ya watu wote mahali

ambapo watu wengine wanaweza kuona.

UNAFAHAMU maana ya kilele?

Kama ashiki na msisimko vitazidi

kuongezeka, utakuwa unaelekea “kilele”.

Kwa mvulana kuutambua kilele misuli yako

ghafla inabana na kufanya sehemu zote

za uume wako kusukuma mbegu za kiume

nje ya uume. Kwa msichana misuli ya ndani

na inayozunguka uke, mlango wa tumbo

la uzazi na kisimi vinabana. Mara nyingine

majimaji kidogo yanaweza kutoka, lakini

hakojoi kama ilivyo kwa wavulana.

Kilele ni kama kupiga chafya, hisia ya

kukakamaa kwa misuli ikifuatiwa na

kulegea. Kwa watu wengi ni muda mfupi

tu kilele kinadumu kwa sekunde 10, lakini

ni muda ambao unajisikia vizuri na raha na

watu wengi wangependa kukionja.

Kwa wasichana wengi, inawachukua muda

kufikia kilele. Inahitajika kujua wapi na

namna gani washikwe.Na wanahitaji wawe

wanafurahia na kutuliza akili.

Wavulana na wasichana, wote wanaweza

kufikia kilele kwa kupiga punyeto. Hivi ni

vizuri.Uko pekee yako, unaugundua mwili

wako, na majimaji yanayotoka wakati mwili

umesisimkwa hayatampa mtu yoyote

mimba wala uambukizo.

Unapofikia upeo wa raha ya kujamiiana

kwa kushikana na kupakatana, ina ugumu

kidogo. Kweli mko wawili na maji maji

yanayotoka wakati wa kushikana yanaweza

kuwa na VVU au magonjwa ya ngono. (soma

sura ya 10 kuhusu magonjwa ya zinaa na

VVU).

Wataalam wa ujinsia wa binadamu wanaamini

kwamba punyeto ni njia ya kawaida ya watu

kufurahia na kuelezea ujinsia wao bila ya

kujihatarisha katika mimba au magonjwa ya ngono, yakiwemo VVU/UKIMWI. Hakuna tatizo

litakalo tokea mwilini mwako hata kama ukipiga punyeto sana. Kitu pekee kinachoweza kutokea

ni viungo vya uzazi kuvimba kwa sababu ya kuvisugua mno.

97

98

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

KuVutiWa na Mtu Wa jinSi KaMa YaKO

Wakati wa kubalehe ndio wakati watu wengi wanapata kuelewa zaidi mwelekeo wao kijinsi.

Mwelekeo wa kijinsi unahusu mtu ana hisia za kimapenzi na anavutiwa kimapenzi kwa nani.

Watu wengi wanavutiwa kimapenzi na watu wa jinsi tofauti (kama mwanaume anavutiwa na

mwanamke na mwanamke anavutiwa na mwanaume).

Watu wengine wanajisikia kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsi sawa. Wanaume wengine

wanavutiwa na wanaume wenzao na wanawake wengine kuvutiwa na wanawake wenzao. Huku

kuvutiwa na jinsia sawa kunaitwa “ubasha” au “usenge” au “ushoga”.

Nyakati fulani katika maisha yao, baadhi ya watu wanakuwa na hisia za kimapenzi, mawazo,

ndoto na mvuto kwa mtu fulani wa jinsi moja. Marafiki wawili waliokaribu (pengine wavulana

wawili au wasichana wawili) wanaweza kupendana – wanapenda kuwa pamoja na wakati

mwingine wanajisikia kutamaniana kimwili. Watu wengine wanaona hisia hizi zinawachanganya

na kuwafadhaisha. Hisia hizi ni za kawaida, na baadhi ya watu wanazipata hisia hizi wakati fulani

katika kipindi cha maisha yao.

Japokuwa baadhi ya watu wanavutiwa na watu wa jinsi sawa, madhehebu mengine ya dini na mila

zingine zinafikiria ubasha ni jambo baya, si la kawaida na ni tabia ambayo inaweza kurekebishwa.

Watalaam wengi wanafikiria kwamba mwelekeo wa kimapenzi wa jinsi moja si jambo ambalo

wanaweza kulidhibiti kama isivyowezekana kudhibiti rangi ya ngozi au nywele zilivyo. Kwa

maneno mengine ubasha / usenge sio chaguo la makusudi ambalo mtu anachagua, hivyo

haiwezekani kulibadilisha aidha kwa kuswali, kwa utashi au kwa kufanya ngono na mtu wa jinsia

tofauti.

Katika kipindi cha balehe, watu wengine wanajikuta ni mabasha/wasenge. Kujitambua kunaweza

kuwa kugumu. Unaweza kujiona uko tofauti kuliko mtu yeyote anayekuzunguka, na unaweza

kujisikia mpweke mno. Kama unajisikia kitu kama hiki, jaribu kuonana na mtu ili uzungumze naye,

kama mshauri nasaha wa vijana, mhudumu wa afya, mwalimu unayemwamini, au jamaa yako

mkubwa – yeyote atakayeweza kukusaidia kujibu maswali yako na kupunguza hofu yako atakuwa

amekusaidia.

ubiKiRa

Bikira ni mtu ambaye hajawahi kujamiiana. Kila mvulana na msichana amezaliwa bikira. Ubikira

ni kinga nzuri dhidi ya VVU na magonjwa ya zinaa. Siku hizi wavulana na wasichana wengi

wanaamua kubakia bikira hadi siku ya kuoa/kuolewa.

Ruvimbo kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 13)

“Nitataka kutunza ubikira wangu. Sitafanya mapenzi na yeyote

hata kwa kutumia kinga. Rafiki yangu wa kiume ni mtulivu

na ndio maana ni mtu wangu.”

Stabile, kutoka Zimbabwe (umri; miaka 19)

“Bado mimi ni bikira. Bila shaka imani yangu kubwa ya dini

inanisaidia katika suala hili.”

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Susan, umri wa miaka 18 kutoka uganda

“Ubikira ulifanya nionekane mwenye heshima. Wasichana wanatakiwa

kutunza ubikira wao mpaka wanapoona wamepata watu wa kuwafaa.

Ngono ni jambo unaloweza kuahirisha. Yakwepe mazingira yaliyo

kinyume na kanuni ulizojiwekea na utaweza ukadumisha dhamira yako.”

Watu wengi wanachanganyikiwa na kitu kinachosababisha wasichana wapoteze ubikira.

Wanafikiri ubikira wa msichana unadhihirishwa na kizinda, ambacho ni tishu nyembamba ndani ya

mlango wa uke. Kizinda kina shimo dogo na hakizibi kabisa uke kwa sababu damu ya hedhi lazima

itoke kila mwezi. Wasichana wengine hawana kizinda kabisa. Pengine ni kwa vile hawakuzaliwa

nacho au kilinyumbuka na kuchanika kabisa wakati wa michezo.

Wasichana walio na tishu ya kizinda mara nyingine wanatoka damu wanapopoteza ubikira wao.

Wasichana ambao wana tishu ndogo ya kizinda au hawana tishu ya kizinda wanaweza wasivuje

damu watakapojamiiana. Kwa mara ya kwanza hii inawachanganya watu. Watu wanasema:

“Hakuna damu, kwa hiyo hakuwa bikira”. Lakini anaweza kuwa alikuwa, hajawahi kufanya ngono

hapo awali hivyo alikuwa bikira. Ubikira unapotea kwa kujamiiana. Hauwezi kupotea kutokana na

michezo, kwa kutumia visodo, kupiga punyeto au shughuli yoyote ile. Japo ni kweli mambo haya

yanaweza kurefusha au kuchana kizinda, hii haimaanishi msichana sio bikira. Watu wanaofikiria

kuwa kizinda ndio usahihi wa kuwepo bikira wanakosea.

UNAJUA ukweli kuhusu ubikira?

Kuna uzushi mwingi kuhusu ubikira:

1. Nimesikia kwamba msichana anaweza kupoteza ubikira kwa kucheza michezo. Je, hii

ni kweli? Si kweli! Ubikira anaweza kupotea tu kwa kufanya ngono, kucheza michezo ni

kuzuri kwa wasichana na haiwezi kumsababishia kupoteza ubikira.

2. Kuna mitishamba mingine inaweza kurejesha ubikira? Hapana, hakuna mitishamba

inayoweza kurejesha ubikira. Ukipotea, umepotea milele.

3. Rafiki yangu anasema nikibaki bikira kwa muda mrefu, naweza kuugua magonjwa na

mambo yasiyo ya kawaida? Siyo kweli! Unaweza kubakia na ubikira maisha yako yote

bila matatizo yoyote mabaya.

4. Ni kweli kwamba msichana akiwa bikira kwa muda mrefu sana, kizinda chake kitakuwa

kigumu na atapata matatizo ya kufanya ngono? Huu ni upuuzi! Kizinda ni kipande

kidogo na chembamba cha tishu. Hakiwi kigumu kadri unavyokua na wala unaposubiri

kujamiianahudhuriki kamwe.

5. Unawaweza kuwatambua bikira kwa kuwaangalia usoni? Si kweli! Huweza kumtambua

bikira kwa kumwangalia kwa macho. Ni bikira peke yake anayejua hali yake.

6. Baada ya kupoteza ubikira wako, unatakiwa uendelee na ngono. Si kweli. Unaweza

kuacha kufanya ngono ukipenda.

7. Nimesikia kwamba si vema kutumia kondomu ukiwa unajamiiana na msichana ambaye

ni bikira kwa sababu unahitaji kutumia nguvu sana kuvunja ubikira wa msichana

– kiasi kwamba utachana kondomu. Je huu ni ukweli? Hapana! Mvulana na msichana

ambao ni bikira wanaweza kutumia kondomu bila matatizo. Kizinda ni tishu laini sana

inayochanika kwa urahisi mno.

99

100

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kama walivyo wasichana, wavulana wanaweza kupoteza ubikira wao kwa kujamiiana. Watu

wengine wanafikiri sio muhimu kwa wavulana kuwa bikira kama ilivyo kwa wasichana.Zaidi, video

nyingi unazozitazama na riwaya nyingi unazosoma zinafanya ionekane muhimu kwa wanaume

kuwa na uzoefu zaidi wa ngono. Mara nyingine inaonekana kana kwamba ili uonekane mwanaume

lijali lazima ufanye ngono. Lakini kufanya ngono hakukufanyi uwe mwanaume zaidi. Kwa mvulana

au msichana kutunza ubikira wako ni vizuri. Ni njia nzuri sana kwa kinga ya kweli dhidi ya VVU, na

magonjwa ya ngono na mimba zisizotakiwa.

KuPOteZa ubiKiRa

Uwe mvulana au msichana, unapaswa wewe mwenyewe kuamua wakati gani upoteze ubikira

wako. Usije kuwaruhusu watu wengine kukuamulia au kukushinikiza uupoteze. Chagua muda

wako. Na chagua mtu anayefaa. Subiri hadi unakuwa na uhakika kwamba unaweza kujizuia dhidi

ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/UKIMWI na mimba zisizotakiwa.

adam, kutoka uganda (umri wa miaka 13)

“Nafikiri muda mzuri wa kuanza kujamiiana ni wakati nikiwa na umri wa

miaka 20. Nitamaliza masomo yangu na pengine kufanya kazi.Hata kama

muda huo ukifika nitatumia kondomu”.

Mfune, kutoka Zambia (umri wa miaka 13)

“Nitasubiri hadi nioe au nipate fedha za kunisaidia kwa sababu msichana

ukipata mimba nitahitaji fedha za kulelea mtoto”.

Mara nyingine wenzako wanaweza kukulazimisha kufanya ngono.

Douglas, kutoka Zambia (umri wa miaka 12)

“Vijana wengine wakubwa kwetu au waliojaliwa kuwa

na miili mikubwa wanatucheka na kutuambia sisi ni bikira”.

andrew, kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Rafiki yangu wa kiume ananicheka na kunisihi niwe na rafiki wa kike.

Wanasema utaishije bila rafiki wa kike wewe sio mwanaume”.

Mildred, kutoka uganda (umri wa miaka 17)

“Wakati fulani, unajisikia umeachwa na marafiki zako wakianza

kuzungumzia masuala ya ngono. Unaweza tu kuingilia mazungumzo yao

kutokana na ulichosoma kwenye kitabu cha hadithi au ulichoona kwenye

sinema. Kama huna mwelekeo mzuri unaweza ukadanganywa. Nimechagua

kubakia bikira mpaka nimpate mwanaume mzuri wa kunifaa.”

lois, kutoka tanzania (umri wa miaka 13)

“Nazungumza na marafiki zangu kuhusu kufanya ngono. Wapo baadhi ya

wasichana na wavulana wanaosema kwamba ukikataa kufanya ngono

unafanana na mtu ambaye hakusoma”.

Vijana balehe wengi siku hizi wanaelewa kwamba kufanya ngono ni uamuzi wao wenyewe na

kwamba asiwepo mtu wa kuwalazimisha kufanya ngono.

Patrick, kutoka uganda (umri wa miaka 17)

“Marafiki zangu wote wanafanya ngono

na marafiki zao wa kike, na kidogo tu

niwafuate kutokana na kulazimishwa na

marafiki zangu. Lakini niligundua kwamba

sikuwa na uhakika na nilichanganyikiwa.

Isitoshe ninataka kufanya mambo yangu

mwenyewe. Nitasubiri.”

lois, kutoka tanzania (umri wa miaka 13 )

“Hakuna atakayenilazimisha kufanya

ngono. Nitaamua mwenyewe”

Milensu, kutoka Zambia (umri wa miaka

13)

“Sitafanya ngono kwa sababu itabidi nisubiri hadi niolewe nitakapokuwa tayari kwa

matokeo ya kufanya ngono. Sitarajii rafiki zangu kunishinikiza nifanye ngono. Uamuzi ni

wangu.”

andrew, kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Kama nitataka kufanya ngono utakuwa ni utayari wangu mwenyewe. Rafiki zangu

hawatanishawishi kufanya hivyo.”

KujaMiiana

Kujamiiana ni wakati mwanaume na mwanamke wana ileta miili yao karibu na mwanaume

anasimamisha uume na unaingia ukeni kwa mwanamke.

Kwa nini watu wanajamiiana? Kuna sababu nyingi – nzuri na mbaya. Zifuatazo ni baadhi ya

sababu:

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Simama imara dhidi ya shinikizo la kundi

rika. usifanye mapenzi eti kwa sababu rafiki

zako wanafikiri unatakiwa kufanya.

Upendo na mapenzi ya dhati. Kwa watu wawili walio karibu sana, kujamiiana kunaweza kuleta

mapenzi ya dhati na yenye upendo. Hata hivyo watu wengine wanafanya ngono kwa sababu

wanafikiri itawaletea kupendana na mapenzi ya dhati kwenye uhusiano wao. Wanafikiri

kujamiiana kutathibitisha mapenzi kati yao. Hii mara nyingi haisaidii. Mapenzi ya dhati

yanakuja kwa kuzungumza mambo ya uaminifu na kushirikiana katika hisia. Ngono haiwezi

kuwaunganisha watu pamoja kama hawakuwa karibu kabla. Kufanya ngono hakumaanishi

watu wanapendana.

Kuridhisha hamu ya mapenzi na mahitaji ya kimwili. Watu wengine wanafikiri kwamba

unahitaji kujamiiana ili kukidhi hisia za kufanya mapenzi – kama unavyohitaji kunywa

unaposikia kiu. Lakini kujamiiana hakuko hivyo. Ukweli wakati mwingine kujamiiana

hakuridhishi kuliko kushikana mikono, kukumbatiana, kubusu, kama watu wawili hawana

mahusiano ya karibu, kufanya ngono kunaweza kusiwaridhishe.

101

102

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kujaribu kumhodhi mvulana au msichana. Watu wengi wanafanya ngono kwa sababu

wanaogopa kupoteza mahusianao iwapo hawatafanya ngono. Hii ni sababu moja

mbaya ya kufanya ngono. Yeyote atakayekuacha kwa sababu eti hutaki kujamiiana,

hakupendi (soma sura ya 12 kwa maelezo mengi kuhusu hili).

Zawadi: Watu wengine wanafanya ngono kwa ajili ya kupata zawadi, fedha au

upendeleo kama kupata alama nzuri shuleni. Hili linaweza kuwa tatizo gumu, kwa

mfano kama mshirika wako ndiye anayekulipia ada ya shule. Lakini hizi ni sababu zisizo

sahihi za kufanya ngono. Hazitakufanya ujisikie vizuri. Usitumie mwili wako kupata

chochote kutoka kwa mtu yeyote hata kingekuwa kitu gani – fedha au zawadi au

huduma za kipekee – huwezi kuvilinganisha na mwili wako.

Kujisikia umekua. Wengi wanakimbilia kufanya ngono kwa kufikiri itawafanya wajione

wamekua. Lakini kufanya ngono kwa kweli hakubadilishi chochote kuhusu ukuaji wako.

Ngono haitakufanya ukomae na wala haitakufanya uwe mtu mzima.

Kulingana nao au kuwafurahisha wenzio. Watu wengi wanahisi kana kwamba watu wote

wanaowazunguka wanafanya ngono – kana kwamba wao peke yao ndio hawafanyi

ngono. Hii inaweza kuwa tishio na vijana wengine wanafanya ngono kwa sababu

wanafikiri vijana wengine wanafanya hivyo.Ukweli ni kwamba watu wengi hawasemi

ukweli kuhusu ngono, na watu wengi wanatunga tu hadithi kwa sababu wanataka

kuwafurahisha watu wengine.

Kupata mtoto. Kujamiiana ndiyo njia pekee ya kufanya mapenzi ambayo inaweza

kukupatia mtoto.

Watu wengi wanataka watoto wakati fulani katika maisha yao, lakini ni wachache

wanaotaka kuwa na mtoto wakati wa ujana balehe (soma sura 11).

Kujamiiana ndiyo njia ambayo watu wengi duniani wanapa VVU. Kama huko tayari kujikinga

wewe na mwenzio kwa kutumia kondomu wakati wote hujawa tayari kujamiiana.

KuWeKa KiWanGO cha KujaMiiana.

Watu wengine wanafikiri ngono ina nguvu na haiwezi kuzuiliwa na kwamba inatokea

kama radi au mvua. Lakini ukweli ni kwamba – kufanya ngono – ni uamuzi wa makusudi.

Unapofanya ngono sio kwamba ni jambo la asili lazima litokee. Ni wewe unayefanya

uamuzi. Lakini pawe na maamuzi mengi kuhusu ngono. Lini? Nani? Kwa nini? Wapi? Mara

ngapi? Kwa kutumia kondomu? Bila kondomu?

Ngono ni uamuzi mzito. Ni uamuzi wako! Zuia sauti zote zinazosema “kila mtu” anafanya

ngono. Jibu ni kwamba si kila mtu anafanya ngono. Na wewe sio kila mtu. Ni wewe tu.

Kama unafanya uamuzi wa kufanya au kutofanya ngono, fikiria kuhusu hili: Uko tayari

kuvumilia mahitaji ya ngono salama – matumizi sahihi na kutumia kondomu kila mara,

ushauri kuhusu VVU, kupima, na mengineyo? Vijana wengi hawako tayari kubeba wajibu

wote huo; Kuwa mwaminifu kwa nafsi yako. Kama unajiona huko tayari, unaweza kusema

“Hapana” subiri mpaka utakapokuwa mkubwa.

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Unahitaji vile vile kumtunza mwenzi wako, na yeye vile vile anatakiwa akutunze. Kutunzana

kunachukua muda. Urafiki na kuwa karibu haujengeki kwa usiku mmoja. Kama hamjawa marafiki

wa kweli unaweza kuona ngono ni kitu cha aibu. Hii ni dalili tosha kwamba huyo siyo mtu

anayefaa au siyo muda sahihi kwako.

Kama wewe na mwenzi wako hamko tayari kwa kujamiiiana, ishia kwenye kubusiana, kushikana

mikono au kukumbatiana. Weka kikomo na kubaliana nacho usifanye kitu chochote ambacho

mwenzako anakiona hakifai.

Unafahamu kama mahusiano yenu ni tayari kwa kujamiiana?

Jibu maswali yafuatayo kiukweli kadri uwezavyo. Weka tiki kwenye jibu ulilolichagua.

.1. Je, mimi na mwenzi wangu tunafahamiana vizuri

Ndiyo Hapana Labda Sijui

2. Je unajisikia tumeungana pamoja na kila mmoja wetu anajiona kuwa sehemu ya mwenzi katika

maisha.

Ndiyo Hapana Labda Sijui

3. Je, kila mmoja amejikabidhi kwa mwenzie katika uhusiano wenu?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

4. Je, tunaaminiana?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

5. Je, tunawasiliana vizuri?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

6. Je, tunaweza tukazungumza bila wasi wasi kuhusu ngono?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

7. Je, tunafikiria kufanya ngono kwasababu kweli tunataka au kwa sababu tunashinikizwa kufanya

ngono?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

8. Je, tumezungumzia kuhusu njia gani tutatumia kuzuia mimba?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

9. Je, tumezungumzia kuhusu kupima VVU kwetu wote?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

10. Je, tumezungumzia namna ya kujikinga na magonjwa ya ngono pamoja na VVU/UKIMWI?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

11. Je, tumekubaliana kutumia kondomu na njia za kuzuia mimba wakati wa kujamiiana?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

12. Je, mwenzi wangu ataheshimu haki yangu ya kusema “ndiyo” au “hapana” kila tunapofanya

ngono?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

13. Je, nitaheshimu haki ya mwenzi wangu ya kusema “ndio” au “hapana” kwa kila tutakapotaka

kufanya ngono?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

14. Je, ushirikiano wa mahusiano ya kimapenzi yatakuwa salama na ya raha?

Ndiyo Hapana Labda Sijui

Kama ulijibu “hapana” “labda” au “sijui” kwa swali lolote, basi labda wewe na mwenzi wako hamko

tayari kujamiiana. Ni vizuri kungoja.

103

104

uaMuZi Wa KutOFanYa nGOnO

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Vijana wengi wanachagua kutofanya ngono kwa sababu nzuri sana zifuatazo:

Wanaogopa kupata mimba na magonjwa ya ngono virusi vya UKIMWI na UKIMWI wenyewe

na hawapendi kuhatarisha maisha yao.

Bado ni wadogo mno hivyo wanajiona hawako tayari.

Hawataki kuwaudhi wazazi wao.

Wanaona tendo hilo ni kinyume cha maadili ya dini zao.

Wako tayari kusubiri ili kushughulikia masomo yao.

Wanataka kuhakikisha kuwa rafiki yake wa kiume au wa kike anampenda kikweli.

Iwapo unakabiliwa na uamuzi wa kufanya ngono, kumbuka kwamba ngono inaweza kuwa na

matokeo mabaya kama kuambukizwa VVU au mimba zisizotakiwa.Mambo haya yanaweza

kukuharibia maisha yako milele. Unahitaji kufikiri kwa makini uamuzi wako. Kumbuka kuwa:

Kusubiri ndiyo njia nzuri na salama ya kubakia na afya.

Unayo haki ya kusema “hapana” kwa ngono na kushikilia uamuzi wako.

Ukiamua kusema “ndio” kwa ngono, lazima ujizoeze kufanya ngono salama ili kukwepa

mimba, VVU, UKIMWI na magonjwa ya ngono. “Bila kondomu, hakuna ngono”.

KuZunGuMZa na MWenZi WaKO KuhuSu nGOnO

andrew, kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Mimi na marafiki zangu tunazungumza kuhusu ngono.

Tunazungumza pia athari za ngono,kwa mfano iwapo

msichana atapata mimba,tutapata matatizo makubwa,

tutalazimishwa kuoa au kufukuzwa shule!”

halima, kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Sababu nzuri sana za kuchelewa kufanya ngono ni kusubiri

kupata mtu atakayefaa na kusubiri mpaka mnaoana.”

Maamuzi kuhusu ngono yanahusu watu wawili na yanahitaji mawasiliano mazuri na makini. Ni

jambo muhimu kumweleza wenzi wako kitu unachofanya na kitu ambacho hutaki kukifanya.

Watu wengi wanajisikia vibaya na aibu kuzungumza

masuala ya ngono, lakini mambo haya yanakuwa rahisi

baada ya muda na kuyafanyia mazoezi. Hapa kuna

baadhi ya vidokezo:

Fikiri ni kwa nini unataka au hutaki kufanya

chochote: Jua sababu zako ni zipi ili uweze

kuzieleza wazi kwa mwezi wako.

• Fanya mazoezi kabla: Kama huna uhakika

utazungumza nini kuhusu kujamiiana na rafiki

yako wa kike au kiume jaribu kuzungumza na

rafiki wa karibu unayemwamini au mshauri wa

vijana kwanza. Waulize jinsi ya kulizungumzia

suala hilo. Pata maoni ya namna ya

kushughulikia hali hii.

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

chagua muda mzuri na mahali muafaka:

Chagua muda mzuri wa kuzungumza na rafiki

yako wa kiume au wa kike, muda ambao kila

mmoja wenu hana shughuli ya mambo mengine

na wakati ambapo wote mnajisikia mmetulia

na mmestarehe. Ni vizuri pia kuchagua sehemu nzuri. Chagua sehemu ambayo hutajali

hata watu wengine wakiwasikia. Wakati huo huo chagua sehemu ambayo siyo ya kificho

sana ambayo itamfanya msichana wako au mvulana wako apate wasiwasi na kupata

mawazo potofu.

• usingoje mpaka umepata joto la mahaba ndio uanze kuzungumzia ngono: Ni vigumu

sana kuwa na mazungumzo kuhusu kujamiiana wakati mmoja au wote mnajisikia

mmesisimka na katika hali ya kufanya ngono. Hakikisha mnazungumza aina gani

ya mapenzi mnayataka kabla wewe na mwenzi wako kujikuta katika hali ya kuvutia

kimapenzi.

• Kuwa mkweli kuhusu unavyojisikia na jinsi unavyoona. Usiwatumie watu au sababu

mbalimbali kama kisingizio. Kwa mfano kama hutaki kufanya ngono kwa sababu

unataka kwanza kuolewa, usimwambie rafiki yako kwamba sitaki kufanya ngono kwa

sababu naogopa kupata mimba au kwa sababu unaogopa kwamba mama atagundua.

Ukimwambia rafiki yako wa kiume visingizio hivyo atafikiri kwamba unataka utumie

kondomu au unataka uende kwake.Ili kukwepa kutoeleweka, kuwa muwazi na eleza

moja kwa moja hisia zako.

• Simama imara na usikubali kushinikizwa: Hata watu ambao unawaheshimu sana

wanaweza kukushinikiza ufanye vitu ambavyo hutaki kuvifanya. Inaweza kuwa vigumu

sana kuhimili shinikizo kwa sababu ni mtu unayempenda unataka awe na furaha.

Kumbuka hata hivyo kwamba mtu anayekupenda hapaswi kufanya mambo ambayo

yatakukosesha raha. Kama rafiki yako wa kiume au kike anakushinikiza pengine ni

kwa sababu hawajui unajisikiaje au kwa sababu hawajali hisia zako kama ambavyo

inawapasa. Simama kidete, na hakikisha wanaelewa unachokitaka.

105

106

• Zingatia hisia na silika yako: Kama

moyoni mwako hujisikii kwamba

kitu fulani hakikufai usikifanye.

Ngoja mpaka utakapoona huna woga

wowote, wasiwasi au vitu vinavyo

kuhangaisha.

Wakati wote jiruhusu kubadilisha

mawazo. Tuseme ulimwambia rafiki

yako wa kiume kwamba utafanya

ngono naye, lakini ukajiona huwezi kufanya.

Unayo haki ya kubadili mawazo

yako. Unayo sababu nzuri ya kujisikia

unavyojisikia.

Hata kama umewahi kufanya ngono kabla,

unaweza wakati wowote kuamua kuacha.

Hakuna tatizo lolote unapoamua kuacha.

Huna haja ya kutoa sababu za kutosheleza

kueleza kwa nini unaacha. Wewe

kumbuka tu, mtu anayo haki ya kubadili

mawazo yake.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

unayo haki ya kubadilisha mawazo

wakati wowote.

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Sura ya 9

ujinSia na nGOnO

Ujana ndio muda ambao unajitambua wewe mwenyewe kama mtu ambaye unapata

hisia za kijinsia. Unajitambua zaidi kuhusu ujinsia wako – unajisikia, unajiheshimu kama

mwanaume au mwanamke, unajua kitu gani unataka kuhusiana na mahusiano na watu

wengine.

Mtu kuwa na afya kiujinsia maana yake ni kuwa unaweza kuelezea ujinsia wako katika

namna ambayo haikudhuru wewe au mtu mwingine. Ina maana kwamba haujihatarishi

kama vile kufanya ngono isiyo salama, ambayo inaweza kusababisha mimba zisizohitajika

au magonjwa ya zinaa, ukiwemo VVU/UKIMWI.

Kila mtu ana hisia za kiujinsia na huhitaji kufanya ngono unapokuwa na hisia za kiujinsia.

Ngono ni njia mojawapo ambayo watu wanaweza kuelezea hisia za kijinsia, kama

kuzungumza, kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana n.k.

Bikira ni mtu – msichana au mvulana – ambaye hajawahi kufanya ngono. Wasichana

hawawezi kupoteza ubikira wao kwa kucheza michezo au kuvaa kisodo au shughuli

nyingine yoyote.

Kutunza ubikira wako na kusubiri kufanya ngono kutakuweka salama. Haitakuumiza

kusubiri. Vijana wengi wanaamua kutofanya ngono, wanajiona ni wadogo mno na wanajisikia

bado. Unayo haki ya kusema “hapana” kwa ngono.

Watu wengi duniani wameambukizwa VVU kwa kupitia ngono. Kama huko tayari kujikinga

wewe na mwenzi wako kwa kutumia kondomu kila mara,basi ujue huko tayari

kufanya ngono.

Kuzungumza kuhusu ngono na marafiki zako wa kike au kiume inaweza kuonekana kazi

ngumu na ya aibu mwanzoni lakini ni vizuri kumwambia mwenzio unataka nini na kipi

hutaki ili isije ikatokea kutoelewana. Chagua muda mzuri wa mazungumzo na usisubiri

mpaka uwe “katika joto la mahaba”. Kuwa mkweli kuhusu hisia zako, na usijirahisi au

kushinikizwa kufanya kitu ambacho hukihitaji.

Kumbuka, hata kama umewahi kufanya ngono kabla, unaweza wakati wote ukaamua

kuacha kufanya ngono. Hakuna matatizo yoyote yatakayokupata. Kama huwezi kujikinga

na mimba zisizotakiwa, VVU/UKIMWI na magonjwa ya ngono, itakubidi uache

kufanya ngono.

107

108

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kutunza Afya Yako

Ya Kiujinsia

Stabisile kutoka Zimbabwe (umri: miaka 19)

“Mwili wangu ni wa pekee kwangu. Ninaulinda dhidi ya magonjwa

ya ngono, VVU na mimba.”

Mwili wako vile vile ni wa pekee. Je, unaulinda? Yapo mambo mengi unayotakiwa kuyajua

kuhusu kuishi na afya nzuri na kujilinda mwenyewe dhidi ya matatizo ya afya ya uzazi.

Watu wengi wanapofikiria matatizo ya afya ya uzazi, wanafikiria magonjwa ya ngono na

VVU/UKIMWI tu. Haya ni matatizo ya hatari kwa hiyo ni wazo zuri kujua namna ya kujitunza

na jinsi ya kuepuka majanga.

MaGOnjWa Ya nGOnO

Magonjwa ya ngono ni magonjwa ambayo

yanaambukizwa kwa njia ya kujamiiana

au kwa kufanya ngono. Yapo magonjwa ya

ngono yanayosabisha vidonda, uvimbe au

malengelenge wakati yapo mengine ambayo

hayaonyeshi dalili zozote.

Magonjwa ya ngono yanaenea kwa kupitia

mgusano wa majimaji ya watu wawili – shahawa,

majimaji ya ukeni na damu – na kupitia mgusano

na ngozi iliyoathirika. Magonjwa ya ngono

yanaweza kuenezwa kutoka kwa mwanaume

kwenda kwa mwanamke, na kutoka kwa

mwanamke kwenda kwa mwanaume na hata

kati ya watu wawili wa jinsi moja.

Ugonjwa uenezao kwa ngono uliombaya zaidi

kuliko yote ni VVU/UKIMWI. Hakuna sindano

ya kinga na hakuna dawa unapokuwa umepata

maambukizi. Watu wengi wanakufa ndani ya

miaka 10 mpaka miaka 20 baada ya maambukizi

ya VVU.

109

SURA YA 10

110

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Magonjwa mengine ya zinaa kama kaswende, klamidia na kisonono ni hatari vilevile. Magonjwa

haya yanatibika na tunaweza kuyathibiti. Lakini yanaweza kuleta athari za muda mrefu:

Kusababisha ugumba yaani kushindwa kupata watoto.

Kusaidia virusi vya UKIMWI kuingia mwilini kwa urahisi.

Kwa ufupi, zipo njia tatu za kuepuka magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU.

1. Usifanye ngono. Ahirisha kufanya mapenzi au acha kabisa kujamiiana.

2. Unapojamiiana, hakikisha unatumia kondomu tangu mwanzo mpaka unapomaliza kitendo.

3. Nenda na mpenzi/mwenzi wako kupima VVU. Kabla ya kuanza kujamiiana. Unaweza kupima

VVU zaidi ya mara moja kutegemeana ni lini ulifanya ngono isiyo salama (bila kinga) ili

kuhakikisha huna VVU. (Angalia ukurasa wa 116 kwa maelezo zaidi). Hakikisha kati yenu hakuna

aliye na maambukizo ya VVU kabla ya kuanza kujamiiana. Kila mmoja wenu abakie mwaminifu

kwa mwenzie.

Mambo haya yanaonekana kuwa rahisi. Njia za kuwa salama ni hizo tatu. Lakini, yapo mengi ya

kufikiria. Iwapo ulifanya ngono na baadaye ukaamua kuacha, bado utatakiwa kupima. Unaweza

kuwa na ugonjwa uenezwao kwa ngono bila ya kujitambua.

je, unajua kwa nini wasichana wako hatarini zaidi kupata maambukizo ya

magonjwa ya zinaa hasa VVu/uKiMWi?

Ingawa wote, wanaume na wanawake, wanaweza kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa,

wanawake na wasichana wanapata maambukizo kwa urahisi zaidi kuliko wanaume/wavulana.

Zipo sababu kadhaa kwa nini iwe hivyo:

1. Uume wa mwanaume unaingia ndani ya uke na shahawa zake zinaweza kuwa na maambukizo.

Zikikaa ndani ya mwili wa mwanamke zinaongeza uwezekano wa kupata maambukizo ndani ya

tumbo la uzazi, mirija ya falopia na ovari.

2. Kwa ujumla, wasichana wako hatarini kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa kwa sababu

mlango wa mfuko wa uzazi wa msichana balehe ni laini zaidi kuliko wa mwanamke mtu mzima. Uke

unaweza ukachanika wakati wa kujamiiana jambo ambalo linaweza kuongezea hatari ya kupata

maambukizo ya magonjwa ya ngono.

3. Wasichana wengi na wanawake wanafundishwa kuwa watiifu na wanyenyekevu kwa wanaume.

Hawana stadi ya kujiamini ili kuwashawishi wenzi wao kutumia kondomu kwa ajili ya kinga.

Wasichana balehe wengi, walioolewa au wasioolewa, wenzi wao wana umri mkubwa kuliko wao

wenyewe. Mwenzi anapokuwa na umri mkubwa kuliko msichana, inaweza kumuwia vigumu hasa

msichana kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa na mimba. Katika jamii nyingi inaweza

kumwia vigumu mwanamke kukataa kujamiiana na mme wake au kumsisitizia watumie kondomu

hata kama anafikiri mwanaume wake anaweza akawa na mwanamke mwingine.

4. Wanawake na wasichana wako kwenye hatari ya kufanya ngono bila kutaka. (kwa kulazimishwa

au kubakwa), kuliko wanaume na wavulana. Katika mazingira magumu kama haya, inaweza kuwa

vigumu kujikinga na maambukizi.

5. Mambo ya kimila na utamaduni kama vile kufanya ngono kavu na kuweka dawa za kienyeji, nguo

na vitu vingine ndani ya uke ili “kusafisha” au “kuubana” vyote hivi vinamwongezea mwanamke

hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono. Kukausha uke kabla ya kujamiiana

kunaweza kuongeza uwezekano wa kuchanika na kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Kama wewe na mwenzi wako mnatumia kondomu wakati wote mnapojamiiana ni vizuri sana.

Endelea!Watu wengi wanaanza kwa kutumia kondomu. Lakini baada ya muda wanaanza

kufikiri. “Ninamwaminimwenzi wangu, tunaweza kuacha kutumia kondomu”. Hii siyo sawa!

Kabla hamjaacha kutumiakondomu, wote wawili mnahitaji kupima kwa ajili ya magonjwa ya

ngono pamoja na angalau, kipimokimoja cha VVU. Hata kama wewe na mwenzi wako mmepima

na hamna maambukizo ya magonjwaya ngono, ni vizuri zaidi kuendelea kutumia kondomu. Je,

ikitokea kwamba mmoja wenu amejamiianana mtu mwingine? Vilevile unahitaji kuzuia mimba.

utajuaje KaMa uMePata MaaMbuKiZO Ya MaGOnjWa Ya Zinaa?

Watu wengi hasa wanawake ambao wamepata maambukizo ya magonjwa ya zinaa

hawaonyeshidalili zozote zile. Kwa mfano, hakuna dalili yoyote ya kuonyesha kwamba umepata

maambukizo yaVVU kwa mara ya kwanza. Magonjwa mengine ya ngono vilevile hayana dalili za

wazi, kwa hiyo kilamtu inabidi afikirie hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya zinaa. Kama

umeshafanya ngonobila kinga unaweza kuwa umejiweka katika hatari ya kupata maambukizo.

Ukipata kidonda au kiupele sehemu za siri ambacho kinapotea, unahitaji kumwona mhudumu

wa afya.Yapo magonjwa ya zinaa mengine ambayo yana dalili zinazokuja na kupotea. Kidonda

cha kaswendewakati wote kinapona na vidonda vinavyotokana na malengelenge vinapona na

kujirudia. Kama umewahikupata kidonda, kiupele au lengelenge kwenye via vya uzazi, unatakiwa

kumwona mhudumu wa afya.Hata kama dalili za ugonjwa wa ngono zinapotea, maambukizo

yanakuwepo na wala hayawezi kuponabila kupata tiba sahihi.

Kwa vyovyote vile,kama

umeshaanzakujamiiana au bado, ni

vizuri kufahamuvia vyako vya uzazi

vikoje. Ikiwa unajuavikoje ukiwa mzima,

itakuwa rahisikugundua tatizo mapema.

Tumia kiookujiangalia sehemu zako za

siri kiurahisi.Kwa mfano, kidonda cha

kaswendehakiumi, kwa hiyo unaweza

usigundueisipokuwa kama ukiangalia.

Kwa wasichana, ni vema kufahamu

mwonekano na harufu ya kawaida

yamajimaji yako ya ukeni. Majimaji

yaukeni ya kawaida:. Ni kama majimaji

meupe ya yai.

• Ni maangavu au meupe.

• Yanatoa harufu ya kawaida au yenye

afya na isiyochukiza.

• Hayawashi.

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Magonjwa ya ngono mara kwa mara

husababisha majimaji ya ukeni kuwa na

rangi ya njano au kijani na hutoa harufu

mbaya na kali.

je, unazijua alama na dalili za magonjwa ya

zinaa?

Magonjwa mengine ya zinaa hayana dalili za wazi,

hasa kwa wanawake, lakini mengine yanazo.

Dalili za magonjwa ya zinaa kwa wanaume ni

pamoja na:-

• Kidonda, vidonda, upele au malengelenge juu

aukuzunguka uume.

• Uume kutoa usaha.

• Maumivu makali wakati wa kukojoa.

• Maumivu wakati wa kujamiiana.

• Maumivu na kuvimba mapumbu.

• Uvimbe usio wa kawaida au kuota vitu kwenye

via vya uzazi

Dalili za magonjwa ya zinaa kwa mwanamke:

• Kutoka kwa majimaji ukeni ambayo ni mazito;

yanawasha au yana harufu na rangi isiyo ya

kawaida.

• Maumivu sehemu za chini ya kitovu. . Maumivu

wakati wa kujamiiana.

• Kutokwa kwa damu ukeni kusiko kwa kawaida

na bila mpangilio.

• Kuwasha maeneo ya via vya uzazi.

• Uvimbe usio wa kawaida na kuota vitu kwenye

via vya uzazi.

111

112

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Magonjwa mengine ambayo hayaambukizo kwa njia ya ngono vilevile husababisha kutoka kwa

majimaji yasiyo ya kawaida. (soma mwisho wa sura hii kwa taarifa zaidi). Hata bikira anaweza

kupatabaadhi ya maambukizo haya. Ukiona kitu chochote cha tofauti, mwone mhudumu wa afya.

Iwapomwenzi wako ameona kitu chochote cha tofauti kwenye sehemu zake za siri unatakiwa na

wewe uende ukafanyiwe uchunguzi wa afya hata kama unajisikia una afya nzuri.

KWenDa KuchunGuZWa MaGOnjWa Ya Zinaa.

Kama umefanya ngono bila kinga, unahitaji kwenda kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa,

hatakama unazo au huna dalili zozote.

Kwenda kuchunguza magonjwa ya ngono kunaogopesha. Kwa bahati mbaya wahudumu wa

afyawengine wanahukumu na huwa hawana huruma kwa vijana balehe. Wanafikiri hawatakiwi

kufanyangono na wanawafahamisha hivyo! Siku hizi, kliniki nyingi zinatoza gharama kubwa kwa

matibabu yamagonjwa ya zinaa, lakini zipo chache ambazo zinatoa huduma kwa gharama nafuu

kwa vijana balehe.Kwa hiyo, ulizia na ujaribu kutafuta kituo cha afya vinavyowajali vijana balehe.

Hata kama wahudumusiyo wema, shikilia msimamo wako na endelea kuomba unachokitaka.

Haiwezekani kwamba watakataakukuhudumia. Kuwa jasiri.

Kwenye vituo vya afya vizuri utapata vilevile elimu nasaha kuhusu uamuzi muhimu kama:-

Je, unataka kuendelea kufanya ngono?

Je, unataka kupima VVU?

Je, utazungumza vipi na mwenzi wako kuhusu kutumia kondomu?

Je, unatakiwa kutumia uzazi wa mpango? Njia ipi ni sahihi kwako?

Kliniki nyingi zinatoa kondomu bure, kwa hiyo anza kuzitumia kiukweli na hakikisha mwenzi wako

anapata matibabu yanayostahili.

Ikiwa umepata maambukizo ya magonjwa ya

ngono:

Mwenzi ambaye hajatibiwa

atakuambukizatena. Hata kama

umeachana naye badounatakiwa

kumweleza aende kufanyiwauchunguzi

na kutibiwa. Kama huwaambiina kama

hawana dalili zozote, hawawezikujua

kama wana maambukizo ya magonjwaya

ngono mpaka hapo ugonjwa

utakapokuwaumesababisha madhara ya

kudumu kwenyevia vya uzazi. Inaweza

ikawa vigumukumweleza rafiki yako

wa zamani lakiniunahitaji kuwa jasiri

kuongea na kumwelezamtu huyo kwamba

aende kufanyiwauchunguzi. Kumwambia mwenzako inaweza kuwa

vigumu lakini ni muhimu.

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Hakikisha unameza dawa zote ulizopewa na mhudumu wa afya.

• Usifanye ngono mpaka utakapoelezwa na mhudumu wa afya kwamba wewe na mwenzi wako

mmepona.

• Jadili kuhusu afya ya kijinsia na mwenzi wako ili muweze kujikinga.

Kamwe usijitibu mwenyewe magonjwa ya ngono. Unahitaji kupata dawa sahihi au dawa kutoka

kwa mhudumu wa afya. Ukitumia dawa isiyo sahihi itafanya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa

kuwa sugu.

Kamwe usichangie dawa na rafiki yako. Kunywa dozi yote peke yako. Iwapo utakunywa sehemu

tu ya dozi utawafanya wadudu wanaosababisha ugonjwa wawe sugu na vigumu kutibika.

Unajua kuhusu magonjwa ya zinaa?

Magonjwa yote ya zinaa yanawezesha kupata maambukizo ya VVu kiurahisi. Baadhi ya magonjwa ya zinaa

ambayo yanasababishwa na vijidudu vya bakteria na yanaweza kutibika ni:-

• chankroidi: Ugonjwa huu husababisha vidonda vyenye maumivu kwenye via vya uzazi na wakati

mwingine kuvimba kwa tezi kwenye kinena. Tezi za limfu zinaweza kuvimba hadi kupasuka. Vidonda

vinavyohusiana na chankroidi vinaongeza hatari ya kupata maambukizo ya VVU.

• Klamidia – Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya kujamiiana na unaweza kukaa bila kujitokeza kwa muda

halafu ukaanza kuleta matatizo. Dalili zake ni pamoja na uume au uke kutoa uchafu, maumivu wakati

wa kujamiiana (kwa wanawake) na uvimbe au maumivu kwenye mapumbu. Mara nyingi, ugonjwa huu

hauonyeshi dalili – 70% ya wanawake na 25% ya wanaume hawaonyeshi dalili kabisa. Kama klamidia

haijatibiwa, maambukizo yanaweza kuenea na kusababisha uvimbe ndani ya mfuko wa kizazi na

unaweza kupata ugumba. Kwa wanaume, klamidia isipotibiwa inaweza kusabisha ugumba.

• Kisonono: Ugonjwa huu husababisha kutokwa usaha wa rangi ya njano/kijani na maumivu makali wakati

wa kukojoa. Hata hivyo, wanaume wengine hawapati dalili zozote. Wanawake wengine wanaweza kutoa

uchafu lakini wengi wao hawana dalili. Iwapo maambukizo hayajagundulika na kutibiwa, yanaweza

kuenea na kusababisha ugumba/utasa. Kama kisonono hakijatibiwa husababisha pia upofu kwa watoto.

• Kaswende: Ugonjwa huu husababisha kidonda kidogo kisichouma. Dalili zinatokea kwenye via vya uzazi

au mdomoni. Kidonda hutokea siku 9 mpaka siku 90 baada ya maambukizo. Kidonda hiki hupotea baada

ya siku chache na kinaweza kisionekane tena. Maambukizo yanaweza kukaa bwete kwa muda. Baadaye

kipele kisichowasha hutokea. Dalili nyingine ni pamoja na homa kiasi, uchovu, vidonda kooni, nywele

kunyonyoka, kupungua uzito, kuvimba tezi, na misuli kuuma. Iwapo kaswende haikutibiwa inaweza

kuleta matatizo makubwa maishani kama ugonjwa wa moyo hasa katika hatua za mwisho. Maambukizo

yanaathiri ubongo pia. Wanawake wajawazito wanaweza kumwambukiza kaswende mtoto tumboni na

hii inaweza kusababisha mimba kuharibika au kuzaa mtoto aliyekufa. Watoto wanaozaliwa na kaswende

wanakuwa wagonjwa sana. Matibabu yanaweza kufanyika wakati wowote kaswende inapogundulika,

lakini ikigundulika mapema matibabu yanachukua muda mfupi na yanafanikisha kutibu ugonjwa huo.

• “trikomoniasisi” husababisha kutoka uchafu unaonuka, kuwasha na vijidonda kwa wanawake.

Wanaume kwa kawaida hawaonyeshi dalili kabisa. Dalili zinaanza siku 3 mpaka siku 28 baada ya

maambukizo.

Magonjwa mengine ya zinaa yanasabishwa na virusi. Haya hayawezi kutibika kiurahisi au hayawezi kutibika

kabisa. Nayo ni:-

• Malengelenge (herpes): Hayawezi kutibiwa na Viuavijasumu. Ugonjwa huu unaenezwa kwa njia ya

kujamiiana na kwa kugusana na ngozi iliyoathirika. Malengelenge husababisha vidonda vidogo kutoka

kwenye via vya uzazi au kuzunguka mdomo. Vidonda vinaweza kuambatana na homa kali, maumivu ya

kawaida na kuvimba tezi. Malengelenge hupasuka baada ya siku 2 hadi siku 4 na mwishowe hupona. Mtu

akipata maambukizo hubakia hivyo maishani. Marudio ya mashambulizi yanategemea afya ya mtu. Watu

wenye VVU wanashambuliwa mara kwa mara na malengelenge. Mtoto aliye na maambukizo ya ugonjwa

wa malengelenge yuko hatarini kupata upofu, ubongo kuharibika na kifo kutokea. Kwa kuongezea,

malengelenge huongeza hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema (uaviaji).

113

114

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unajua kuhusu magonjwa ya zinaa? (Inaendelea)

Virusi vya “human Papilloma,” Vinundu sehemu za siri (genital warts)

Virusi hivi husababisha sugu kuota kwenye via vya uzazi. Virusi hivi vilivyofunikwa

vinaweza visionekane kwa urahisi, hususani kama vitatokea kwenye njia ya uzazi ya

mwanamke. Kawaida vinajitokeza wiki 3 hadi wiki 9 baada ya maambukizo. Kipindi hiki

kirefu vijidudu hukaa tuli mwilini kabla ya kusababisha ugonjwa. Inamaanisha kwamba

inaweza ikawa vigumu kufahamu maambukizo yalikotokea na yanaweza kuenea kwa watu

wengine bila kujua. Vinundu sugu vinaweza kutibiwa na maji ya tindikali na hairuhusiwi

kujamiiana mpaka vinundu vyote vimepotea. Wenzi wote wanatakiwa kuchunguzwa ili

kuona kama hawana vinundu sugu. Wanawake wenye maambukizo haya wako katika hatari

kubwa ya kupata kansa ya kizazi.

• VVu/ uKiMWi : Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. VVU vinapoingia mwilini

hushambulia kinga ya mwili ambayo kwa kawaida inalinda mwili usipate maambukizo.

Inaweza ikachukua miaka mingi kuona dalili za maambukizo, lakini baada ya muda mrefu

mtu anashindwa kuzuia maambukizo na hata magonjwa yaliyozoeleka ambayo

VVu/uKiMWi

VVu (Virusi Vya uKiMWi) ni Virusi vinavyosababisha UKIMWI (upungufu wa Kinga Mwilini)

UKIMWI ni ugonjwa ambao kinga ya mwili dhidi ya magonjwa inaharibiwa hatua kwa hatua.

VVU vikiingia kwenye mwili wa mwanadamu vinashambulia kinga ya mwili ambayo kwa kawaida

inalinda mwili usipate maambukizo. Watu wenye maambukizo ya VVU wanaitwa watu wanaoishi

na VVU/ UKIMWI. Baada ya muda mrefu mtu aliyepata maambukizo anashindwa kuzuia

maambukizo hata ya magonjwa yaliyozoeleka ambayo kwa vyovyote vile yasingefikia hali mbaya.

Mwili unaposhindwa kujikinga na magonjwa tunasema mtu ana UKIMWI. hakuna chanjo ya

maambukizo ya VVu, na hakuna tiba mara utakapokuwa umepata maambukizo hayo.

Inachukua muda mrefu mpaka dalili za VVU kuonekana. Matokeo yake ni kwamba, mtu ambaye

ana maambukizo ya VVU anaweza akawa na afya nzuri kwa miaka mingi na anaweza asijue

kwamba anayo maambukizo. Katika kipindi hiki anaweza kueneza VVU bila yeye kujua.

Muda ambao mtu anaanza kuona dalili za virusi unategemea na uwezo wa nguvu ya kinga ya mwili

na uimara wa virusi. Yapo makundi mengi ya VVU. Makundi mengine humfanya mtu augue haraka

kuliko mengine. Kwa wastani inachukua miaka 5 hadi 10 kabla dalili zozote za VVU hazijajitokeza.

Kwa vile virusi vinashambulia kinga ya mwili na kumfanya mtu ashambuliwe kiurahisi na

magonjwa, dalili zinatofautiana sana kutegemeana na ugonjwa gani mtu anaougua.

Hata hivyo dalili za kawaida ni:-

Kuvimba tezi za limfu

Kifua kikuu.

Kupungua uzito sana na kuchoka .

Kutoka jasho, hasa usiku.

Homa za mara kwa mara

Kuharisha kwa mfululizo.

Kichefuchefu na kutapika.

Kikohozi kikavu cha mfululizo.

Upele mwilini na vidonda mdomoni.

Hakuna dawa inayotibu VVU/UKIMWI. Lakini zipo dawa zinazowasaidia watu waishio na VVU

kwa miaka mingi bila kuumwa na zinazopunguza makali ya VVU/ UKIMWI. “Anti – retrovirals”

(ARVs) ni dawa zinazopunguza kuendelea kwa virusi. “ARVs” zinawawezesha watu kuishi maisha

ya afya nzuri. Dawa hizi haziuwi virusi moja kwa moja. Zaidi ya hapo dawa hizi ni ghali sana,

ingawa zipo kampuni ambazo zimeanza kutengeneza dawa zenye gharama nafuu na zenye ubora

uliosawa na dawa zilizo ghali. Hata hivyo, ni vigumu kununua dawa hizi ambazo ni nafuu katika

nchi nyingi za Afrika. Matokeo yake ni kuwa watu wengi hawazipati. Dawa hizi sasa zimeanza

kupatikana katika nchi nyingi za Kiafrika kwa bei nafuu.

Kwa hiyo, kitu cha kwanza ni kuzuia VVU kuingia mwilini mwako.

UKWELI KUHUSU VVU

Zipo aina mbili za VVU zinazojulikana kama VVU 1 na VVU 2. VVU 1 inapatikana zaidi, na VVU

2 inapatikana zaidi Afrika ya Magharibi kuliko VVU 1. Vyote, VVU 1 na VVU 2 vinasababisha

UKIMWI. Hata hivyo, kipindi cha kuanzia maambukizo mpaka kufikia UKIMWI ni kirefu

zaidi kwa yule mwenye aina ya VVU 2 kuliko VVU 1. Sasa hivi hakuna kinga kwa aina zote za

VVU wala hakuna dawa ya UKIMWI. Watu wengi wanaopata maambukizo ya VVU wanafikia

UKIMWI baada ya kuishi na VVU kwa miaka 5 hadi miaka 10. Kipindi hiki cha muda ni cha

wastani, inategemea na mambo kadhaa, kama:-

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Aina ya VVU (VVU 1 au VVU 2).

Upatikanaji wa dawa na kutibu dalili zinazojitokeza sana, na pia kujiweka wazi na

magonjwa mengine.

Msaada wa kisaikolojia anaopewa mgonjwa.

Kumbuka kwamba maambukizo ya VVU/ UKIMWI huibuka kwa njia tofauti kutegemea na

maelezo binafsi. Mtu akigundulika ana virusi vya UKIMWI haimaanishi atakufa tu. Wapo watu

ambao walipata maambukizo miaka 20 iliyopita na hadi leo hawajafikia hatua ya UKIMWI.

Matumaini yapo!

Kamwe usidhani mtu anavyoonekana ni salama kwa sababu ya vile anavyoonekana.

Subiri vya kutosha kabla ya kuanza ngono kwa sababu kujamiiana ndiyo njia kuu

inayoambukiza VVU.

Kama unafanya ngono, tumia kondomu kila maraKondomu inaweza kukukinga usipate VVU

na magonjwa mengine ya ngono.

Wakati wote pima VVU kabla ya kuanza uhusiano wa kijinsia na mtu mpya na hakikisha

mwenzi wako naye anapima VVU.

Usichangie nyembe, sindano, vifaa vya kutogea au visu vya kutahiria.

115

116

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

VVu VinainGiaje MWilini?

Njia kuu inayoeneza VVU ni kujamiiana na mgusano wa moja kwa moja na majimaji ya mwilini.

Katika Afrika, zaidi ya asilimia 90 ya watu wanaoambukizwa VVU wanaambukizwa kwa njia

ya kujamiiana. Ni rahisi sana kwa mwanamume kumwambukiza mwanamke kuliko mwanamke

kumwambukiza mwanamume. Hii ni kwa sababu ngozi na misuli ya uke, kuzunguka kinembe na

kuzunguka mashavu ya nje ya uke ni laini sana. Ngozi hii inapata michubuko, vidonda na kuchanika.

Michaniko na michubuko ni midogo sana kiasi kwamba huwezi kuona kwa macho, lakini ni mikubwa

kutosha VVU kupita kama ngozi laini inagusana na shahawa kutoka kwa mwanaume ambaye ana

maambukizo.

Mwanamume anapofanya ngono na mwanamke aliye na maambukizo ya VVU yuko hatarini vilevile

kupata maambukizo. Uume unakutana na majimaji ya ukeni ambayo yana VVU. Kama mwanamke

ana VVU, vinasafiri kupitia kwenye mrija wa uume. Iwapo hajatahiriwa VVU vinaweza kupita

kwenye ngozi hii laini hususani kama vipo vidonda, michubuko au mikato.

VVU vinaweza kuenea kwa njia nyingine vilevile. Njia hizi ni pamoja na:

Mama kwa mtoto wakati wa mimba, au wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha.

Mgusano wa damu ya mtu ambaye ana maambukizi. Inawezekana ikawa wakati wa kuongezewa

damu, kujikata na kisu cha kuchangia au wakati watu wanaotumia dawa za kulevya

wanachangia sindano.

Siku hizi damu inayotumika kuwaongezea wagonjwa inachunguzwa kwa makini kuhakikisha

kwamba haina maambukizo.Hata hivyo, sherehe nyingi za kimila kama kutahiri na kukata vitu

mwilini zinaendelea kutumia njia ambazo siyo salama kama vile kuchangia kisu kimoja au wembe

kwa watu wote wanaotegemewa kufanyiwa. Kamwe usichangie wembe na ndugu zako au marafiki

zako na wala usichangie visu visivyochemshwa wakati wa sherehe ya kutahiri au tukio lolote la

kimila.

Bado haijathibitishwa kama mtu anaweza kupata VVU kupitia kwenye mate wakati wa kubusu.

Hata hivyo, iwapo mtu ana mkato/kidonda mdomoni anaweza kupata maambukizo kwa kumbusu

mtu ambaye anayo maambukizo ya VVU na anavyo vidonda vilevile. Kwa vile VVU vipo ndani ya

shahawa na majimaji ya ukeni, kujamiiana kwa njia ya mdomoni hakuepushi hatari. Iwapo mtu ana

mchubuko au kidonda mdomoni na wakati huohuo akapata shahawa au majimaji ya ukeni mdomoni,

anaweza kupata VVU .

VVU havienei kwa kugusana kwa kawaida kama vile kukumbatiana, kushikana mikono au kumgusa

mtu mwenye maambukizo. VVU vinaishi kwa muda mfupi sana vinapokuwa nje ya mwili, kwa hiyo

haviwezi kuenezwa kwa njia ya kumgusa mtu aliye na maambukizo au kuchangia vitu – kama beseni,

vyombo vya kulia chakula, nguo, vitabu n.k.

Wengi wetu tunao wagonjwa wenye UKIMWI ndani ya familia zetu na tunatakiwa kuwatunza

wanapougua. Ni muhimu unapomhudumia mgonjwa kujikinga ili usipate maambukizo. Unachotakiwa

kuhofia ni majimaji ya mwilini kama vile, majimaji yanayotoka kwenye vidonda, damu ya hedhi na

uharo. Jilinde mwenyewe kwa kuvaa glovu unapomsaidia kuoga au unaposafisha kitu chochote

chenye damu au majimaji yoyote ya mwilini.

utajuaje KaMa una VVu?

Huwezi kujua kwa kujiangalia mwili. Huwezi kutambua kama watu wengine wana VVU kwa

kuwaangalia. Hata kama watu wana UKIMWI – walipata maambukizo ya VVU muda mrefu na

wamekuwa wagonjwa – huwezi kujua kama ni UKIMWI kwa kuwaangalia labda kama wewe ni

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

mhudumu wa afya. Hii ni kwa sababu

magonjwa mengi yanayoambatana

na UKIMWI yanaweza kujitokeza

yenyewe kwa watu ambao hawana

VVU. Kwa mfano, unaweza kuugua

kifua kikuu ukiwa na VVU au

usipokuwa navyo.

Ipo njia moja tu ya kujua kama una

VVU. Katika nchi nyingi upimaji

wa VVU unaambatana na ushauri

nasaha – majadiliano ya undani na

mtu aliyesomea, mwenye huruma

na ambaye anaweza kukusaidia

ili uweze kumudu hali yako ya

kuwa na VVU na kujifunza jinsi

ya kujihudumia. Kama hujapata

maambukizo, mshauri anaweza kukuelimisha ufanye hadhari ili usipate maambukizo.

Vipimo vya UKIMWI vinaaminika ni sahihi, salama na haviumi. Mhudumu wa afya anachukua

damu kidogo kutoka kwenye mkono wako. Unaweza kupata majibu katika muda wa saa moja, au

unaweza kuambiwa urudi baada ya wiki

moja au mbili kutegemeana na kipimo

Vipimo vya VVU vinafanyaje kazi?

kinachotumika.

Ili kujua kama ni kweli huna VVU,

utaambiwa urudi kupima tena baada

ya miezi 3 hadi 6 wakati kipindi cha

kusubiri kimepita.

KWa nini uPiMe VVu?

Zipo sababu nyingi za kupima VVU.

Iwapo mara kwa mara unakuwa na hofu

kuhusu maambukizo ya VVU na una

wasiwasi kutokana na mabadiliko ya

afya yako mara kwa mara inawezekana

njia pekee ya kutuliza akili ni kupima.

Iwapo ulifanya ngono na mtu ambaye

anaumwa na umesikia ana UKIMWI,

hapo utahofu zaidi. Labda njia pekee

ya kutuliza akili ni kupima na kujua

kama umepata maambukizo au la.

Kamwe usidhani kwamba umepata

maambukizo, pima ili ujue.

Mtu yeyote anaweza akawa ameambukizwa VVu

bila kuwa na dalili. usitegemee muonekano wa

mtu kuamua kuwa fulani hana VVu.

Mtu anapokuwa na maambukizo mwili hushituka

na kutoa askari ili kupigana na maambukizo.

Kipimo cha VVU kimetengenezwa kutambua kama

askari wa VVU wapo au hawapo ndani ya mwili wa

binadamu. Ikiwa wapo wengi, maana yake mtu huyo

ana maambukizo ya VVU na kwamba mwili unajaribu

kupigana na maambukizo.

Kwa kawaida askari wanaopimwa na kipimo

cha VVU huonekana mwezi mmoja baada ya

maambukizo. Hata hivyo, mara nyingi askari wa

VVU hutokea baada ya muda zaidi – kama miezi

3 hadi miezi 6 baada ya maambukizo. Katika

kipindi hiki kipimo cha VVU hakitaona askari. Kwa

maneno mengine, miezi 3 mpaka miezi 6 baada ya

maambukizo, mtu anaweza kupima na kuonekana

hana maambukizo ingawa anayo maambukizo.

Vile vile, mtu huyu anaweza kuambukiza watu

wengine katika kipindi hiki kabla askari wa VVU

hawajaonekana kwenye kipimo.

Kwa hiyo,- kama mtu yuko hatarini kupata VVU

na akapima na kuonekana hana VVU, bado

anashauriwa kurudia baada ya miezi 6 ili kuwa na

uhakika kama hana maambukizo.

117

118

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unafahamu kuhusu kuishi kwa matumaini na VVU? V

Hamza alijua ana VVU miaka minne iliyopita. Wakati huo alikuwa ana umri wa miaka 18 naye

anaeleza hadithi yake: “Nilitoka viupele mwilini. Hii ilinisukuma nikapime. Ulikuwa wakati

mgumu sana kwangu, lakini kwa msaada wa ushauri nasaha nilikubaliana na hali halisi.

Niliweza kumaliza kozi yangu ya ufundi magari. Ushauri nilioupata uliniwezesha kuishi mpaka

hivi sasa. Nimeweza kubadili tabia. Nimeacha kuvuta sigara na kunywa pombe. Ninaye rafiki

wa kike ambaye ana VVU vilevile. Ili kuepuka kuongezea maambukizo, tunafanya ngono

salama – tunatumia kondomu.

Vilevile ninaepuka kuwa na mfadhaiko na ninatibu magonjwa madogomadogo

yanayonishambulia. Kitu kimoja cha muhimu nilichojifunza ni kuepuka kujionea huruma,

na hili ndilo linalonifariji. Ninajihusisha sana katika michezo ya kuigiza ambayo inatumika

kuelimisha vijana kuhusu kujizuia na VVU/UKIMWI na kuwahudumia waathirika.

Ninawashauri vijana wasubiri kufanya ngono mpaka watakapokuwa wakubwa. Wale ambao

wamepata maambukizo wanatakiwa kuikubali hali na kujiunga katika mapambano ili kuokoa

maisha ya wale ambao hawajapata maambukizo”.

Hamza anaishi salama na VVU. Amekuwa jasiri na amekubaliana na hali yake. Anautunza

mwili wake. Anaendelea na shughuli zake ametingwa, hapotezi muda. Ana upendo na maisha.

Ana rafiki wa kike. Lakini anahakikisha hamwongezei maambukizo na wala yeye mwenyewe

haongezewi maambukizo anatumia kondomu. Kuishi kwa matumaini kunaweza kukusaidia

kuwa hai kwa muda mrefu.

KuiShi KWa MatuMaini na VVu

Kugundua kuwa una maambukizo ya VVU, siyo kitu rahisi kustahimili lakini unaweza kujifunza

kumudu kuishi navyo. Utahitaji kupewa ushauri nasaha. Ni jambo zuri vilevile kumweleza mtu wa

karibu yako ili usibebe mzigo peke yako.

Kwa watu wengi ugonjwa unaendelea polepole, na wanaweza kuishi na VVU kwa muda wa miaka

10 hadi 20. Kuwa na matumaini. Wanasayansi wengi wanalifanyia kazi suala la VVU. Siku moja

wataweza kufanikisha utafiti huo.

Ukigundua umepata maambukizo ya VVU ni muhimu sana “kuishi kwa matumaini”. Kuishi kwa

matumaini kunaweza kuboresha sana nafasi yako ya kuwa na afya kwa muda mrefu. Kuishi kwa

matumaini na VVu maana yake ni:-

Kumweleza mwenzi wako (unayeshirikiana naye ngono kuwa wewe ni mwathirika).

Kuwatunza kwa upendo wale wote unaowapenda, na kushiriki ibada za dini yako.

Tumia muda wako katika kumcha Mungu.

Kula chakula bora kama vile mboga za majani, maharage, samaki wa kukausha kwa sababu

hivi vinasaidia kuboresha kinga ya mwili.

Kuishi kwa matumaini, kuikubali hali ilivyo na kutokunyanyapaliwa.

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

unafahamu kinachotokea unapokwenda kupima?

Susan ana umri wa miaka 19, aliamua kwenda kupima na sasa

anaeleza kilichotokea. “Niligundua kwamba rafiki yangu wa

kiume amefanya ngono na msichana mwingine. Niliachana

naye. Lakini bado nilikuwa na hofu kwamba ningeweza kuwa

nimepata maambukizo ya VVU. Tumekuwa tukifanya ngono

isiyo salama (bila kinga). Hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana.

Sasa nimegundua.

Nilihofu sana kuhusu VVU! Nilijua kuna njia moja tu ya kutuliza

akili yangu: kwenda kupima. Siku moja nilipata ujasiri wa

kwenda. Nilienda kwenye kituo cha maelezo kuhusu UKIMWI

mjini Kampala. Nilipofika getini, niliogopa. Nilisimama pale

kwa muda mrefu. Mwisho niliingia ndani.

Niliandikishwa, nikapewa namba yangu na nikaambiwa

nimsubiri mshauri. Baada ya dakika tano, alikuja na

akanichukua pamoja na wengine wanne tukaenda kwenye

chumba kingine. Tulipewa ushauri nasaha kama kundi.

Alituuliza tulikuwa tunajua nini kuhusu VVU/UKIMWI na alijibu

maswali yetu.

Kilichofuata, mimi na mshauri tulikutana faragha. Aliniuliza lini

nilifanya ngono kwa mara ya mwisho, nilikuwa na marafiki wa

kiume wangapi na kama nilitumia kinga. Aliniambia ninaweza

kutoka nje wakati wowote kama ningaliamua kutopima. Lakini

nilimweleza kwamba nataka kupima. Baada ya hapo alinipeleka chumba kingine ambako

alinitoa damu kidogo kutoka kwenye mkono. Alifanya haraka sana na wala haikuuma.

Baada ya damu kuchukuliwa nilienda kwenye chumba cha ushauri nasaha na mshauri

alizungumza na kila mtu kuhusu nini maana ya kuwa na VVU au kutokuwa na VVU. Alituuliza

ni kwa jinsi gani tutamudu iwapo majibu yatakapoonyesha kuwa tumeathirika, na jinsi

tutakavyojilinda tusipate maambukizi zaidi au tusiwaambukize wengine. Alituuliza namna

gani tutahakikisha tunabakia watulivu iwapo majibu yatatokea kuwa hasi.

Baada ya kupewa ushauri nasaha kwa kikundi, tuliitwa kwenye chumba cha faragha kupewa

majibu yetu. Nilikuwa wa kwanza kuitwa. Jasho lilikuwa linanitoka na mapigo ya moyo

yalikuwa yanaenda mbio. Nilitaka kukimbia nitoke, lakini niliyahitaji majibu.

‘Majibu yako ni mazuri, huna VVU’, niliambiwa na mshauri. Nilifumba macho, nikasali sala ya

shukurani. -Niliapa kutofanya ngono tena bila kusisitizia matumizi ya kondomu. Mshauri

aliniambia kwamba, kwa vile ni zaidi ya miezi sita tangu nilipofanya ngono kwa mara ya

mwisho, ninaweza kuamini majibu haya na nisingehitaji kipimo kingine cha kuhakikisha

kwamba nilikuwa sina VVU.

Nilipotoka nje, nilijisikia nafuu na mwenye furaha. Na yote haya yalifanyika kwa muda wa

saa moja tu”

119

120

Tibu magonjwa yote yanapojitokeza.

Pumzika na fanya mazoezi mepesi.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Jiunge na jumuia au vikundi vya kusaidia watu wanaoishi na VVU/UKIMWI.

Fanya ngono salama ili usimwambukize mtu mwingine virusi au mwenyewe kujiongezea

virusi vipya mwilini mwako.

Kuishi chanya maana yake ni kuishi kwa kadiri ya upeo wako kila siku. Kuishi chanya ni kitu

ambacho kila mtu anatakiwa kufanya hata kama hatuna maambukizo ya VVU.

Vilevile ni muhimu kuwasaidia watu wengine waishi kwa matumaini na VVU. Usiwaite watu

wenye VVU au UKIMWI “waathirika” kwa sababu siyo waathirika. Ni kama watu wengine, walio

na vitu vingi vya kufanya. Wanaweza kufanya kazi na kuchangia maendeleo. Wanahitaji upendo

na kusikilizwa kama watu wengine. Mara kwa mara wanahitaji msaada wa pekee kutoka kwa

marafiki wa karibu. Inawapasa ndugu kuwa na mtazamo unaowajali / usiowabagua watu wenye

VVU. Kamwe usiwatanie, kuwanyanyapaa au kuwasumbua katika jamii.

Ulikuwa unafahamu kwamba:

nGOnO SalaMa / MaPenZi SalaMa

UKWELI KUHUSU VVU/UKIMWI

Watu milioni 42 duniani wanaishi na VVU kwa sasa. Kati ya hawa karibu robo wana umri

wa miaka kati ya 15 na 24. Watoto na vijana chini ya miaka 18 wanawakilisha zaidi ya

asilimia 10 ya wanaoishi na VVU*.

Nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara zimeathirika sana na VVU/UKIMWI, na

UKIMWI ndiyo ugonjwa unaosababisha vifo vingi. Kati ya watu wote wanaoishi na VVU,

milioni 29.4 ni kutoka eneo hili na kulikuwa na maambukizo mapya ya watu milioni 3.5.

Kwa ujumla, VVU vinaenea kwa njia ya kujamiiana. Asilimia 90 ya maambukizo Afrika

yanatokana na kujamiiana.

Duniani kote, wapo watoto milioni 14 ambao ni yatima kwa sababu ya UKIMWI na kati ya

hawa milioni 12.1 wanaishi Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Ugonjwa huu wa mlipuko unapunguza matarajio ya muda wa kuishi katika Afrika.

Mwishoni mwa miaka ya 1990, watu Afrika walitarajia kwa wastani kuishi miaka 59. Lakini

kutokana na VVU/UKIMWI, matarajio ya muda wa kuishi kwa watu wa Afrika itashuka

hadi miaka 45 tu kufikia mwaka 2010.

Ngono salama maana yake ni kufanya mapenzi ambayo yanapunguza uwezekano wa wewe

kupata magonjwa ya ngono, ikiwa ni pamoja na VVU au mimba. Ukitaka mapenzi salama kwa

asilimia mia moja (100%) basi uchaguzi ulio bora zaidi ni kupiga punyeto na kuacha kabisa

kujamiiana. Kama ukisoma sura ya 9 utafahamu kwamba punyeto ni salama kabisa, upo peke

yako. Majimaji ya sehemu za siri ni yako mwenyewe. Huwezi kupata maambukizo kutoka kwa mtu

yeyote na wala huwezi kujipa au kumpa mtu mwingine mimba.

Kubusu au kumkumbatia mwenzi wako

ni mapenzi salama. Mpaka sasa hivi

haijathibitishwa kama VVU vinaenezwa kwa

njia ya kubusu au kukumbatia. Hata hivyo, kama

mmojawapo ana maambukizo ya VVU na ana

vidonda mdomoni anaweza kumwambukiza

mwenzake. Vilevile kuna uwezekano wa

maambukizo kutokea iwapo mtagusana via vya

uzazi na kupata majimaji ya ukeni au shahawa

mikononi. Kama una mikato au michubuko

mikononi unaweza kupata maambukizi ya VVU

kama mtu mwingine ana maambukizi.

Kujamiiana kati ya watu wawili ambao wote

hawana maambukizo ya magonjwa ya zinaa au

VVU ni mapenzi salama. Lakini, bila shaka bado

patakuwa na hofu ya mimba.Watu wengi hufikiria

kwamba kwasababu wamekuwa na uhusiano na

mtu kwa muda mrefu, wanaamini kuwa hawana

VVU na magonjwa mengine ya ngono. Lakini

mmoja wao akipima ndipo ukweli unadhihirika.

Watu unaowaamini na kuwapenda wanaweza

kukuambukiza magonjwa ya zinaa. Wanaweza

wakawa hawajui kuwa wamekuambukiza.

andrew kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Ninajiamini mwenyewe; sina maambukizo ya magonjwa ya ngono

kwa sababu sijawahi kujamiiana na mtu yeyote.”

anthony kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Sababu nzuri kuliko zote ya kumfanya kijana acheleweshe kuanza

ngono ni kwamba ana uhakika wa kutopata UKIMWI na magonjwa

mengine ya ngono.”

Milensu kutoka Zambia (umri wa miaka 13)

“Kusema “HAPANA” sitaki kujamiiana ni njia mojawapo ya kujikinga

na hatari ya kupata magonjwa na inakufanya udhibiti maisha yako.”

Kondomu vilevile ikitumika vema hufanya tendo la ngono kuwa salama. Kwa kweli kondomu ni

muhimu katika kukulinda wewe na mwenzi wako. Hata kama hujaanza kujamiiana, ni vema usome

somo linalofuata kwani kuna siku utahitaji kuzifahamu kondomu.

KOnDOMu

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Hujachelewa kuanza kutumia kondomu.

Kondomu ni mfuko laini uliotengenezwa kwa mpira ambao unavalishwa kwenye uume kabla ya

kuanza kujamiiana. Mwanaume anapofikia mshindo, anakojoa shahawa ambazo hunaswa kwenye

chuchu ya kondomu. Kwa vile shahawa zinakusanyika kwenye kondomu ina maana majimaji ya

mwanaume hayamwingii mwanamke na wala uume haugusi majimaji ya ukeni kwa sababu uume

umefunikwa na kondomu.

121

122

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kama ikitumika kiusahihi na kwa kukubaliana, kondomu ni kinga

kamili dhidi ya magonjwa ya ngono, ikiwa ni pamoja na VVu na

uzuiaji wa mimba. Kondomu zinazuia vijidudu, bakteria na virusi

vilivyo ndani ya uke kukutana na uume, na huzuia mbegu za kiume,

bakteria na virusi ndani ya shahawa kuingia ukeni.

Ijapokuwa kondomu zinaonekana nyembamba sana,

zimetengengezwa na mpira imara (lateksi) na zimejaribiwa kwa

kutumia nguvu za electroniki ili kuhakikisha kwamba kiwango chake

ni cha juu. Watu wengine wanasema kwamba kondomu zina matundu

madogo sana ambayo yanaweza kupitisha VVU. Hii siyo kweli. VVU

haviwezi kupita kwenye kondomu. Hata hivyo, kondomu inaweza

kuwa na matundu kama muda wa kutumika umekwisha au imetunzwa

vibaya au imewekwa visivyo.

Ni muhimu sana kufuata taratibu za matumizi ya kondomu kila mara

na kila wakati unapozitumia:

1.

2.

3.

4.

Seif, kutoka tanzania(umri wa miaka 13)

“Ngono salama ni kutumia kondomu. Niliyasikia haya kutoka

kwa watu na vilevile kwa kusoma magazeti. Sijawahi kufanya

ngono”.

Sospita, kutoka tanzania(umri wa miaka 13)

“Nimesikia kuhusu kondomu. Nilisoma kwamba zinakukinga

usipate maambukizo ya magonjwa ya ngono na VVU”.

Godfrey, kutoka Zimbabwe(umri wa miaka 19)

“Sina uhakika kama nitafanya mapenzi na mtu yeyote bila ya

kutumia kondomu. Sioni kama hilo linaweza kutokea”.

Chana pembezoni mwa pakiti kwa uangalifu. Usitumie meno na

hakikisha kucha hazichani kondomu.

Usiikunjue kondomu harakaharaka. Iweke kwanza kwenye kiganja

chako na itasimama kama kofia.

Valisha kondomu mara uume unapodinda vizuri na kabla

haujagusa uke. Shika chuchu ya kondomu ukiwa unaiviringisha

chini ya uume. Kondomu inatakiwa iende yenyewe kiurahisi. Kama

haishuki kiurahisi basi jua umeigeuza ndani nje. Itupe kondomu

hiyo na uchukue mpya. Usitumie kondomu iliyogeuzwa ndani nje

kwa sababu inaweza ikawa na shahawa ambazo zina mbegu za

kiume au vijidudu vinavyoambukiza magonjwa ya ngono.

Endelea kushika chuchu ya kondomu wakati unaendelea

kuiviringisha kondomu mpaka uifikishe kwenye shina kabisa. Hii

nafasi ya ziada (chuchu) ni kwa ajili ya shahawa baada ya kukojoa

(kufikia mshindo).

5.

6.

Baada ya kukojoa, shika ukingo wenye bangili wa kondomu na toa

uume toka kwenye uke. Hii itasaidia kuzuia kondomu isiteleze.

Tupa kondomu kwenye choo cha shimo, choma au fukia ardhini.

Usiache kondomu mahali ambapo watoto wataiona na wala usitupe

kwenye choo cha kuvuta maji kwani itaelea.

Yafuatayo ni maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia kondomu kwa usahihi ili

zisipasuke na wala zisiteleze na kutoka.

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Angalia juu ya pakiti tarehe ya kwisha matumizi au tarehe ya

kutengenezwa. Kama tarehe ya kwisha matumizi imepita, usiitumie!

Kama tarehe ya kutengeneza ni zaidi ya miaka mitatu iliyopita,

usiitumie! Kumbuka kuwa hata kondomu zinazotumika kuzuia mimba

zisitumike zaidi ya miaka miwili baada ya tarehe ya kutengenezwa.

Kamwe usitumie kondomu ambayo pakiti yake imetoboka. Zaidi ya

hapo usitumie kondomu ambayo ganda lake lina rangi zilizochujuka

au halina rangi kabisa au kama ganda ni gumu limekakamaa au linanata sana.

Tunza kondomu sehemu ambayo kuna ubaridi kiasi, kiza na pakavu. Joto, mwanga na

unyevuunyevu vinaharibu kondomu. Usitunze kondomu kwenye pochi au mfukoni.

Ikiwezekana tumia kondomu zenye vilainishi au tumia vilainishi kama kondomu siyo laini.

Vilainishi vinaweza kusaidia kondomu isipasuke au kuchanika wakati wa kujamiiana. Tumia

vilainishi vyenye asili ya maji tu. Vilainishi vizuri ni pamoja na maji na dawa za kuulia mbegu

za kiume. Majimaji ya ukeni ya asili yanaweza kuwa kilainishi. Kamwe usitumie vilainishi

vyenye asili ya mafuta. Usitumie vaselini, mafuta ya maji (ya kupikia, ya watoto, ya nazi,

petroli), jeli ya petroli, vipodozi vya aina zote, siagi, malai ya kokoa au majarini. Vyote hivi

vinaweza kudhoofisha uimara wa kondomu.

Usikunjue kondomu kabla ya kutumia. Kondomu ambayo imeshakunjuliwa ni vigumu kuivaa.

Tumia kondomu mpya kila unapofanya ngono baada ya mshindo. Kamwe usitumie kondomu

zaidi ya mara moja na usivae zaidi ya moja.

Watu wachache wanadhurika kiafya na mipira aina ya “lateksi”. Hivyo kondomu hizi

zinawasababishia viupele na ngozi kuwasha. Kama unalo tatizo kama hili, zipo kondomu ambazo

hazitengenezwi kwa kutumia mpira wa “lateksi”. Tumia hizo. Zungumza na mhudumu wa afya

namna ya kuzipata.

Watu wengi wanaotumia kondomu wanasema zinawafanya wenza wote wawili wafurahie ngono.

Wenza wote wanaweza kupumzika na kutulia zaidi wanapokuwa hawana hofu ya mimba au

kupata magonjwa ya ngono. Wanaume wengine wanasema kondomu zinawasaidia wasifikie

mshindo “wasikojoe” haraka na kuwafurahisha wenzi wao.

Lakini pia wapo wanaume na wanawake ambao hawapendi kutumia kondomu kwa sababu wana

hofu kuwa hawatafurahia ngono vizuri. Hivyo, mwanaume anaweza kumdanganya mpenzi wake

kwamba hana ugonjwa hivyo kumtaka amwamini na asiwe na sababu yoyote ya kuwa na hofu.

123

124

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Anaweza kumfanya mwanamke ajisikie vibaya kwa kumuuliza ni kwa nini hamwamini. Lakini

ikumbukwe kuwa yeyote anaweza kuwa na maambukizo ya magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja

na VVU kutokana na uhusiano uliotangulia hata bila ya kuona dalili zozote. Kwa hiyo, ni kwa faida

ya wote kutumia kondomu.

Kondomu inatoa kinga kwa wale watakaohusika. Kuitumia kondomu ni alama ya kuaminiana,

kuheshimiana na kujaliana.

MatatiZO MenGine Ya aFYa Ya uZaZi

je, unazifahamu kondomu za kike?

Umewahi kusikia kuhusu kondomu za kike? Hii ni njia

nyingine ya kujikinga dhidi ya VVU, magonjwa mengine

ya ngono na mimba. Hiki ni kimfuko kilicholainishwa

kama kondomu ya kawaida ya wanaume. Lakini, badala

ya kufunika uume, inakinga uke kama kizuizi dhidi ya

maambukizo.

inavyofanya kazi: Kuna pete ndogo mbili; moja ni pete

ndogo ndani ya kondomu na ya pili ipo upande uliowazi ambayo hukaa nje ya mwili. Pete hizi

hushikilia kondomu ya kike ikae mahali pake. Kondomu ya kike, kama kondomu ya kiume

inazuia mbegu za kiume kukutana moja kwa moja na uke. Kama uume unabakia ndani ya

kondomu na pete ya nje inabakia mahali pake basi kondomu itafanya kazi.

jinsi ya kutumia: Inaweza kuchukua muda ili kuweza kuivaa kondomu vizuri kama mazoezi

yalivyo kwa kondomu za kiume. Lakini mwisho utazoea. Kwanza ikunje pete ya ndani iwe

na alama ya nane (8). Kisha isukume ndani kiasi utachoweza mpaka utakapoona huwezi

kuisukuma zaidi. Kondomu itakapokuwa imekaa sehemu yake, ongoza uume wa mwenzi

wako ndani ya kondomu. Tumia kondomu ya kike moja kwa wakati mmoja. Usirudie kuitumia

kondomu hiyo.

jinsi ya kuitoa: Ni rahisi sana kuitoa. Sokota pete ya juu ili shahawa zisimwagike, halafu vuta

kondomu nje na itupe ndani ya choo cha shimo au choma moto au fukia ndani ya shimo.

Faida yake: Kondomu ya kike ni njia pekee ya kujikinga ambayo inadhibitiwa na mwanamke

mwenyewe ili imlinde dhidi ya maambukizo ya magonjwa ya zinaa, VVU/ UKIMWI na mimba.

Inakaa taratibu ndani ya uke na haibani uume unapoingia.

Yapo matatizo ambayo yanatokea kwenye via vya uzazi lakini siyo magonjwa ya zinaa. Hata

kama hujawahi kufanya ngono, yapo maambukizo ambayo unaweza kuyapata sehemu zako

za siri. Unaweza ukapata maambukizo kwenye njia ya mkojo ambayo husababisha kuwashwa

au maumivu unapokojoa mkojo. Ukiona uchafu wa ajabu unatoka au maumivu au damu wakati

unapokojoa, unatakiwa kumwona mhudumu wa afya.

KanDiDiaSiSi”

Kama sehemu zako za siri zinawasha na unatokwa na uchafu wa ajabu ukeni unaweza ukawa na

“kandidiasisi”. Hili ni tatizo la kawaida. Ugonjwa huu vilevile unaitwa maambukizo ya hamira na

unasababishwa na kuvu wanaofanana na hamira wanaoitwa “kandida albicans”. Ugonjwa huu

unawasumbua wasichana na wanawake wengi. Wavulana wanaweza kupata kandida chini ya govi.

Kandida ni kiumbe kimojawapo ambacho kwa asili kinaishi juu ya mwili. Kwa kawaida kandida

hakisababishi matatizo yoyote. Kinadhibitiwa na kinga ya mwili na bakteria wengine ambao

kwa kawaida wanaishi ukeni. Lakini ikiwa kinga ya mwili imeshaharibiwa na haifanyi kazi vizuri,

viumbe kandida huzaliana haraka . Mara kwa mara tatizo hili hutokea kabla au baada ya damu ya

hedhi kutoka na wakati wa mimba.

“Kandidiasisi” inaweza kuenea kwa njia ya kujamiiana na mtu ambaye ana kandida wengi. Lakini

inaweza kusababishwa na mambo mengine vilevile. Mfadhaiko, kama vile mitihani, kifo ndani ya

familia au mabishano yanaweza kuwa kichochezi cha “kandidiasisi”. Wakati mwingine unaweza

kupata kandidiasisi ukinywa kiuavijasumu – Viuavijasumu vinaua bakteria ambao kwa kawaida

wanaishi ukeni. Watu wanaoumwa kisukari na wale wenye VVU wanapata kandidiasisi mara kwa

mara.

“Kandidiasisi” si ugonjwa wa ngono kwa sababu hata bikira wanaupata. Joto linapozidi na

unyevunyevu kuzunguka eneo la via vya uzazi vinaweza kusabisha kandidiasisi. Hii ina maana ya

kwamba unaweza kujiletea mwenyewe “kandidiasisi” kwa kuvaa nguo zisizofaa. Kama, kwa mfano

ukivaa nguo za nailoni, kaptura za kubana au suruali aina ya jeans zinazobana na kukaa kwa saa

kadhaa huku umebananisha miguu, pengine kwenye basi, unatengeneza unyevuunyevu na joto

ambalo kandida wanahitaji ili waishi.

Dalili za kandidiasisi ni:-

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Zungumza na mwenzi wako kuhusu matumizi ya Kondomu. eleza unavyojisikia na unachotaka.

Kuwashwa kwenye via vya uzazi, wote; wasichana na wavulana.

Usaha kutoka ukeni au chini ya govi unaofanana na maziwa yaliyoharibika.

Kuvimba na kuwepo kwa utando telezi wa uke na midomo ya ndani au kichwa cha uume kuwa

chekundu.

Iwapo utapata mojawapo ya dalili hizi omba msaada kutoka kwa mhudumu wa afya mwenye ujuzi

ambaye atakupatia matibatu yanayotakiwa. Matibabu yanayotakiwa kawaida ni:-

125

126

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Dawa za kupaka zinazotibu kuvu au wakati mwingine kidonge kinachotumbukizwa ndani ya uke. Iwapo

umeishaanza ngono, mwenzi wako anatakiwa kutibiwa pia ili asikuambukize tena.

Vilevile, unaweza kusafisha taratibu eneo la via vya uzazi na maji yenye chumvi kidogo. Kuwa safi

kwa kusafisha mara mbili kwa siku. Usifute via vya uzazi kwa sababu utasababisha vidonda ambavyo

itabidi vitibiwe. Usikune uke, na nawa mikono baada ya kushika sehemu za siri. Vaa nguo safi

zilizokauka na chupi za pamba. Kumbuka kuanika chupi juani.

Iwapo maambukizo ya “kandidiasisi” yanajirudiarudia ni vema kwenda kupima VVU. Maambukizi

yanayojirudiarudia ni alama ya kinga kuwa dhaifu.

MaaMbuKiZi KWenYe njia Ya MKOjO

Wanawake na wanaume wanaweza kupata maambukizo kwenye njia ya mkojo, lakini zaidi kwa wanawake

kwa sababu ni rahisi bakteria kuingia kwenye njia ya mkojo. Dalili za maambukizo ni:

• Kutaka kukojoa mara kwa mara

• Kusikia maumivu makali wakati wa kukojoa

• Mkojo kuchanganyikana na damu.

Maambukizi haya yanaweza kuepukwa kwa kujiweka safi hasa kwa kusafisha eneo la via vya uzazi kila siku

na kuhakikisha unanawa baada ya kwenda haja kubwa. Wakati wote unasafisha kutoka mbele kuelekea

nyuma. Ukisafisha kutoka nyuma kwenda mbele unaweza kusambaza bakteria kutoka kwenye mkundu

kwenda kwenye tundu la mkojo. Hatua nyingine za kuchukua ili kuepuka maambukizo haya ni kunywa

maji mengi; kukojoa mkojo mara kwa mara (usijaribu kubana mkojo kwa muda mrefu) na hasa baada ya

kujamiiana, na kuvaa chupi za pamba na nguo pana zinazoweka sehemu za siri kavu.

Iwapo unafikiri unayo maambukizo kwenye mrija wa kupitisha mkojo, kunywa maji mengi na nenda

kamwone mhudumu wa afya kwa ajili ya matibabu. Usijamiiane mpaka dalili zote ziwe zimetoweka.

KanSa / SaRatani Ya ShinGO Ya MlanGO Wa KiZaZi

Saratani ya shingo ya mlango wa kizazi inaathiri mlango wa mfuko wa kizazi. Seli zinapokuwa na saratani

zinaongezeka haraka kuliko seli za kawaida mwilini mwako. Seli za Saratani zinavamia na kuchukua nafasi

ya tishu zilizo na afya mwilini mwako na hatimaye ugonjwa unaweza kuua. Ugonjwa huu unawapata sana

wanawake wakubwa (zaidi ya miaka 40). Lakini sasa hivi unajitokeza hata kwa vijana wa umri mdogo.

Saratani ya shingo ya mlango wa mfuko wa kizazi inaweza kuonekana mapema kwa kutumia utaratibu

unaoitwa “Pap smea”. Mhudumu wa afya atatakiwa akusanye seli kwenye mlango wa mfuko wa kizazi. Kwa

kutumia darubini, seli ambazo si za kawaida na ambazo zinaweza kuwa na saratani zinaangaliwa kama

zipo. Ikiwa zipo seli ambazo si za kawaida zinaweza kuondolewa. Saratani ya mlango wa mfuko wa kizazi

inatibika iwapo itagundulika mapema. Kwa vile ni muhimu kugundua mapema saratani hiyo, madaktari

wanashauri kwamba wanawake wote ambao wanajamiiana wapime kipimo cha “pap smea” kila baada ya

miaka mitatu mpaka mitano.

Kama harufu mbaya au uchafu unatoka ukeni au kama damu inatoka unapojamiiana, mwone daktari kwa

sababu hizi zinaweza kuwa dalili za kuwa na tatizo kwenye mlango wa mfuko wa kizazi.

Unajiweka kwenye hatari ya kupata kansa ya kizazi ikiwa utaanza kufanya ngono katika umri mdogo (kabla

ya miaka 20) au kama utashiriki ngono na watu zaidi ya watatu katika kipindi cha uhai wako.

Kuweka sugu sehemu za siri kunaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata kansa ya kizazi. Ugonjwa wa

kansa ya kizazi ni sababu ya msingi ya kukufanya uamue kusubiri hadi ufike miaka 20 ndipo ufanye ngono.

Pia, ni sababu ya kukufanya uamue kuwa na mpenzi mmoja na utumie kondomu kila mara.

Sura ya 10

Kujali na Kuhudumia afya yako ya kijinsia

Magonjwa ya zinaa au maambukizo yatokanayo na ngono ni maambukizo ambayo yanaenea

kwa njia ya kujamiiana. Yanaenea kwa njia ya majimaji ya watu wawili kama vile shahawa,

majimaji ya ukeni na damu.

Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika, lakini bado yanaweza kuharibu via vya uzazi na

kufanya mtu asizae. Dalili za magonjwa ya ngono ni pamoja na:-

Vidonda, malengelenge, uvimbe na vipele sehemu za siri.

Usaha kutoka kwenye uume.

Usaha wenye rangi ya ajabu na harufu mbaya kutoka ukeni.

• Maumivu wakati wa kujamiiana au wakati wa kukojoa.

Magonjwa mengine ya ngono hayatibiki. UKIMWI ni mmojawapo wa magonjwa ya ngono

ambayo hayatibiki. VVU husababisha upungufu wa kinga mwilini. Maambukizo ya VVU

yanasababisha UKIMWI. (Upungufu wa Kinga Mwilini) Ugonjwa huu unasababisha kinga ya

mwili (mfumo wa kinga mwilini dhidi ya magonjwa) ushindwe kufanya kazi. hakuna dawa ya

kuzuia maambukizo ya VVu, na hakuna dawa ya kutibu uKiMWi.

haiwezekani kumtambua mtu mwenye maambukizo ya VVu kwa kumwangalia tu. Mtu

anaweza kuwa na afya yake kwa muda mrefu kabla dalili hazijaanza kujitokeza. Mtu anaweza

asifahamu kama amepata maambukizo kwa miaka kadhaa. usije ukadhani kwamba mtu

hana VVu, na usije ukadhani kwamba mtu anavyo VVu. ni muhimu kupima.

Iwapo una wasiwasi kuhusu magonjwa ya ngono, ni jambo jema kwenda kupima na kupata

matibabu kama yanatakiwa. Usije ukajitibu mwenyewe na dawa na wala usichangie dawa na

mtu mwingine.

Iwapo utafahamu kwamba umepata maambukizo ya VVU, pata ushauri. Usijaribu kukabili

tatizo hili peke yako. Kama utajitunza vizuri unaweza kuwa na afya nzuri na kuishi maisha

yenye manufaa.

Zipo njia zitakazokuepusha kupata maambukizo ya magonjwa ya ngono pamoja na VVU:-

SURA YA 10 | KUTUNZA AfYA YAKO YA KIUJINSIA

Acha kabisa kujamiiana. Ishia kubusu na kukumbatiana tu.

Iwapo umeshaanza kujamiiana tumia kondomu kila mara ili kujikinga. Hakikisha unajua

jinsi ya kutumia kondomu kiusahihi.

Siyo kweli kwamba matatizo yote yaliyopo kwenye via vya uzazi ni magonjwa ya ngono. Yapo

maambukizo kama kandidiasisi na maambukizo ya njia ya mkojo ambayo hayasababishwi na

kujamiiana. Haya husababisha pia matatizo katika sehemu za siri. Kwa ujumla, maambukizo

haya yanaweza kuepukwa kwa kuimarisha usafi sehemu za siri. Iwapo unasikia maumivu au

muwasho sehemu za siri mwone mhudumu wa afya.

127

128

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Mimba inatokana na watu wawili, mwanaume na mwanamke. Wote wawili wanawajibika. Sura

hii haihusu wasichana peke yao. Wavulana wanatakiwa kusoma pia. Mimba na kuzuia mimba

zisizotakiwa ni wajibu wenu wote wawili msichana na mvulana.

MiMba inatOKeaje?

Mimba na uzuiaji wa

mimba

Mwanamume na mwanamke watakapofanya

ngono isiyo na kinga, kuna uwezekano wa

mwanamke kupata mimba. Mwanamume

anapokojoa shahawa ndani ya uke, shahawa

hizo zinaingia kwenye uke na kuogelea kwenda

kwenye mlango wa mfuko wa kizazi. Zikitoka

kwenye mfuko wa kizazi zitaogelea hadi kwenye

mirija ya kupitisha yai na hapo zinaweza kuishi

kwa muda wa siku 3 hadi 5

Kama yai litakuwa limeshaingia kwenye mirija

ya kupitisha yai au litafika hapo katika kipindi

cha siku 3 hadi 5, moja ya mbegu za kiume

inaweza kuliingia yai na kulirutubisha. Seli mpya

ijulikanayo kama Zaigoti inaundwa ikiwa ni

muungano wa yai na mbegu ya kiume. Zaigoti

hugawanyika sehemu mbili kutengeneza seli

mbili zinazofanana. Seli mbili hizi zinagawanyika

kufanya seli 4, nazo seli nne zinagawanyika mara

mbili kutengeneza seli 8, na kuendelea. Mara

kibonge cha seli nyingi kinatokea.

Kibonge cha seli kinasafiri kutoka kwenye mirija

ya kupitishia yai kwenda kujishikiza kwenye

kuta za mfuko wa kizazi. Kitendo cha seli

kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi

kinaitwa “Upandikizaji”. Upandikizaji unatokea

wiki 3 baada ya hedhi yako ya mwisho. Huu ndio

mwanzo wa mimba.

Mbegu za kiume zikiogelea kwenye ukuta wa

tumbo la uzazi kwenda kwenye yai

Mwanzo wa mimba: yai lililoovushwa

likipandikizwa kwenye ukuta wa tumbo la uzazi

129

SURA YA 11

130

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kumbuka kuwa mimba inaweza kutokea kama utafanya ngono isiyo salama mara moja tu.

Mimba inaweza kutokea kama mwanamume atakojoa shahawa zake karibu na uke hata kama

hamkujamiiana! Shahawa zikimwagwa nje ya mlango wa uke bado zinaweza kuogelea hadi

kwenye mlango wa mfuko wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi na kwenye mirija ya kupitisha yai.

Utadhani hakuna uwezekano, lakini inatokea.

Dalili Za MiMba

Dalili ya wazi kuwa mimba imetungwa ni kukosa kupata hedhi. Hii ni kwa sababu ukuta wa mfuko

wa kizazi hautoi damu mwanamke akiwa na mimba. Utando laini unabaki ndani ya mfuko wa

kizazi na unatengeneza kiota laini kwa ajili ya mtoto kukua. Kukosekana kwa hedhi haina maana

kuwa umepata mimba. Wasichana waliobalehe wanaweza kuwa na hedhi isiyo ya kawaida. Kwa

miaka mingi siku za hedhi kwa baadhi ya wasichana balehe, zinaweza kuchelewa au zikakosekana

mwezi mzima bila sababu yoyote.

Dalili nyingine za mimba:

Matiti kuwa laini

Kichefuchefu (hali ya kutaka kutapika) na kuwa na mate mdomoni.

Uchovu (kujisikia umechoka sana)

Kutaka kukojoa mara kwa mara

Kupendelea kula vitu fulani,wakati mwingine visivyo vya kawaida.

Wanawake wachache huwa hawaoni dalili zozote kati ya hizo hapo juu. Kwa mfano, wanawake

wengine hutoa damu kidogo sana wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya mimba zao na hivyo

wanaweza kufikiri hedhi imekuwa na damu kidogo kuliko kawaida.

Kama huna uhakika kuwa umepata au hujapata mimba, unaweza kufanya kipimo cha mimba.

Katika sehemu nyingine, unaweza kununua kipimo cha mimba kwenye maduka ya dawa. Vilevile,

unaweza kufanyiwa kipimo cha mimba kwenye kliniki. Mara nyingine kipimo kinafanywa kwa

kupima mkojo na unaweza kugundua viini fulani ambavyo vinatengenezwa na mwili wakati wa

mimba. Dakitari au nesi wa kituo cha afya anaweza vilevile akakufanyia uchunguzi wa mwili ili

kuona kama una mimba au la.

Mimba inachukuwa wiki 40 kabla ya mtoto kuzaliwa(toka mwanzo wa hedhi yako ya mwisho).

Hadi utakapokosa hedhi yako - kama siku 28 baada ya siku ya mwisho ya siku zako za hedhi

iliyopita - kibonge cha seli nyingi, yaani kiinitete kitakuwa kinakua katika mfuko wa kizazi kwa

karibu wiki nzima.

Kiinitete kinakua haraka sana. Wiki sita baada ya hedhi yako ya mwisho, ubongo na uti wa

mgongo vinakuwa vimeanza kutengenezwa na moyo unaanza kupiga. Katika wiki 9 kiinitete

kinaitwa fitasi. Katika wiki ya 12 fitasi inatambulika kama binadamu ila inakuwa na kichwa

kikubwa. Katika wiki 20 (miezi 5) mwanamke anaweza akajisikia fitasi inachezacheza au

kuzunguka ndani ya tumbo lake. Fitasi inaweza kugeuka au kusogea na inaweza pia ikashituka

kukiwa na kelele zenye sauti ya juu.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Ukuaji na maendeleo ya mtoto ndani ya tumbo la uzazi

hataRi Za MiMba na uZaZi KWa WaSichana balehe

Mimba ni hatari kwa kila mwanamke lakini ni hatari zaidi kwa wasichana balehe. Tatizo kubwa

kwa wasichana chini ya miaka 20 ni nyonga. Mifupa inayozunguka mfereji wa kutolea mtoto

haujakua vizuri. Wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo wanapata taabu katika kuzaa

kwa sababu mlango wa uzazi kwenye mifupa ya nyonga ni midogo mno na mtoto hawezi kupita.

Tatizo hili linaitwa uzazi wa kukwama.

Kama mtoto hawezi kutoka nje inabidi mtoto atolewe kwa njia ya upasuaji. Vijijini, wanawake

wengi wenye matatizo kama haya huwa hawawezi kufika hospitali kwa muda unaotakiwa. Mtoto

anaweza kufia tumboni. Isitoshe mfuko wa kizazi unaweza kuchanika kwa sababu ya kipindi

kirefu cha uchungu na mwanamke anaweza kufa kwa kuvuja damu nyingi. Hii ni sababu mojawapo

inayowafanya wasichana balehe wengi wadogo kufa wakati wa kuzaa.

131

132

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Uchungu wa muda mrefu unaweza kusababisha matatizo mengi. Baada ya saa nyingi za uchungu,

kichwa cha mtoto kinaweza kunyoosha au kuchana uke, na kusababisha shimo kati ya uke na

kibofu cha mkojo au kati ya uke na mkundu. Shimo hili linaitwa Fistula. Kwa sababu ya shimo

hilo, msichana au mwanamke hawezi kuzuia mkojo au kinyesi. Mkojo au kinyesi wakati wote

vitakuwa vinavuja kupitia shimo hilo na kushuka chini ya miguu. Matokeo yake msichana au

mwanamke atakuwa ananuka vibaya na anaweza kuvimba miguu kutokana na mwasho wa mara

kwa mara unaosababishwa na mkojo kwenye ngozi. Katika jamii zingine msichana au mwanamke

wa aina hiyo hutengwa na jamii. Jibu pekee ni kumtafuta mganga mtalaamu wa upasuaji kuweza

kuziba shimo. Inaweza kuwa vigumu kumpata mtalaamu wa operesheni hii, na siyo mara zote

inafanikiwa.

Pia kutokana na uchungu wa muda mrefu kwa wasichana wadogo kuna hatari ya kupungukiwa

damu (damu dhaifu), kupata shinikizo la damu na kifafa cha mimba. Mambo haya yanaweza

kusababisha uchovu, maambukizo ya magonjwa, kuumia na kifo. Wasichana wadogo pia wako

hatarini kuzaa kabla ya wakati wake au kuzaa watoto wenye uzito wa chini kuliko inavyotakiwa.

Kupunguza hatari ya matatizo haya unahitaji kujitunza vizuri wakati wa ujauzito mimba isije

ikaharibu mwili wako na kukusababishia ulemavu wa maisha.

KuStahiMili MiMba KatiKa uMRi

MDOGO.

Miezi tisa ya mimba ni muda wa uchovu

mkubwa kwa mwili wa msichana. Kinaweza

pia kuwa kipindi cha msongo na uchovu.

Hata kwa wasichana walioolewa ambao

wanataka kuanzisha familia, kipindi cha

mimba ni kipindi ambacho matunzo maalumu

yanahitajika.

Kupata mtoto kwa msichana asiyeolewa

kunaweza kukawa na matatizo mengi

mbalimbali. Mara nyingine familia ya

msichana inaweza kutoa msaada na

kumsaidia katika hali ngumu aliyonayo.

Kwa wasichana wengi,mimba inamaanisha

mwisho wa masomo yao

Watamsaidia kulea mtoto, watampeleka shule kumalizia masomo yake. Ni jambo zuri sana

familia wanapotoa msaada. Lakini kwa bahati mbaya, si jambo la kawaida.

Mara nyingi, mimba isiyotakiwa inasababisha msururu wa matukio. Wazazi wa msichana

wanaweza ama kumwachisha shule kwa sababu ya kukasirishwa na kukatishwa tamaa, anaweza

kupigwa na kufukuzwa nyumbani au anaweza kutishwa mno na vitisho vya wazazi wake akaamua

kutoroka yeye mwenyewe. Maisha yake yanakuwa ni ya huzuni, maisha ya baadaye ya mtoto

yatakuwa hatarini, kwa vile amezaliwa na msichana mwenye huzuni ambaye hakuwa tayari kulea.

Wasichana wengi wanaokabiliwa na mimba zisizotakiwa wanajaribu kuzitoa kinyume cha sheria.

Pamoja na kwamba wanajua kutoa mimba ni hatari, wanapendelea kuhatarisha maisha yao kuliko

kufukuzwa shuleni au nyumbani. Kila mwaka barani Afrika, maelfu ya wasichana wanakufa au

wanaharibu viungo vyao vya uzazi kwa sababu ya kutoa mimba zisizo salama. Katika nchi nyingi

za Afrika kutoa mimba ni kinyume cha sheria (soma zaidi mwisho wa sura hii).

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Wakati mwingine mvulana aliyempa mimba msichana anaweza

kupata matatizo pia. Anaweza kupigwa na baba au kaka wa msichana.

Anaweza kufukuzwa shuleni au kwenye jamii. Anaweza kulazimishwa

kumwoa msichana na kumtunza mtoto na hivyo hataweza kuendelea

na masomo yake na malengo yake ya kazi. Pengine atalazimika kulipa

faini kubwa kwa wazazi wa msichana.

Ukigundua unakabiliwa na mimba isiyotakiwa, usijihukumu

mwenyewe, na usijaribu kuikabili hali hiyo kimyakimya. Mtafute mtu

yeyote anayeweza kukusaidia kufanya uamuzi mzuri uzungumze naye.

Katika hali hiyo usifanye uamuzi wa haraka bila kutafuta maelezo na

ushauri unaotakiwaau bila kufikiri kwa makini uchague lipi.

Japo itaonekana ni vigumu, ni muhimu kuwataarifu wazazi wako

au walezi kuhusu hiyo mimba. Utahitaji msaada wao wakati huu na

baadaye, hasa kama utahitaji kuendelea na masomo. Unayo haki ya

kupata elimu lakini unaweza kuhitaji msaada wa watu wengine ili

urudi shuleni.

Je, unajua kuwa mvulana naye anawajibu kuhusu mimba?

Usijaribu kukaa kimya

unapopata mimba.

Unahitaji matunzo

mengi na msaada.

Wavulana wengi hawafikirii kuhusu uwezekano wao kuwa baba wakati wanapojamiiana. Hata

hivyo, watu wawili wanahusika ili kupata mimba na kwa hiyo mvulana anao wajibu sawa na

msichana.

Kama umekwishaanza kujamiiana unatakiwa kuwajibika na kuwa mwangalifu. Usitegemee

kalenda kwamba ni njia inayoweza kukusaidia kujikinga wewe na rafiki yako wa kike. “Hakuna

siku salama kwa wasichana balehe”. Unaweza kumpa mimba kwa urahisi rafiki yako wa kike na

mimba ya utotoni inaweza kuwa hatari na ikahatarisha maisha na afya ya rafiki yako wa kike.

Inaweza kuwa vibaya pia kwa maisha yake ya baadaye, na maisha yako pia kwa kulazimishwa

kuacha masomo ili umtunze mtoto. Kwa hiyo, usifanye mambo ya hatari kijinsi. Kama ukiamua,

fanya ngono salama kama kukumbatiana au hakikisha kwamba wewe na rafiki yako wa kike

mnatumia njia za kuzuia mimba vizuri kila mnapojamiiana. Ni afadhali kuwa mwangalifu

kimwenendo, kimatendo, kifedha na vyovyote inavyowezekana kuliko kujutia baadaye.

Kama utakuwa baba bila kutarajia, kubali kuwajibika kwa vitendo vyako. Jifikirie kama

baba mwenye wajibu na tenda kama baba. Zungumza na rafiki yako wa kike kuhusu jinsi

utakavyosaidia kumtunza mtoto. Muulize jinsi utakavyoweza kusaidia ili aweze kuilea vema

mimba yenu (kama vile kumsindikiza kliniki, kumsaidia kazi n.k). Hata kama wewe na msichana

hamna uhusiano wa karibu, usimkimbie, zungumza naye jinsi utakavyohusika katika maisha ya

mtoto.

Unatakiwa pia kuwa mwazi kwa wazazi wako kuhusu jambo hili na waeleze wakusaidie katika

mazungumzo ya kushirikiana na wajibu wa kumlea mtoto na matunzo ya mama na mtoto. Zaidi

ya yote usirudie kufanya kosa kama hilo tena.

133

134

KujitunZa WaKati Wa ujauZitO

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kwa sababu mimba inaleta uchovu mkubwa katika mwili wako na ni hatari kwa afya yako ni vizuri

upate matunzo yanayofaa.

Anza kwenda kliniki ya wazazi mapema unapojijua umepata mimba; usingoje hadi mimba

ionekane. Sababu za kuwepo kliniki ya wazazi ni kuhakikisha wewe na mtoto wako mko

katika hali nzuri. Kliniki ya wazazi ni muhimu kuweza kutambua matatizo mapema na

kuyatibu mapema.

Jiwekee utaratibu. Fuata ratiba ya kwenda kliniki ya

wazazi.

Nenda mara nyingi kadiri wakunga watakavyokwambia.

Tumia chandarua ili kujikinga na malaria.

Pata mapumziko kwa wingi

Fikiria utakula nini na hakikisha unakula vyakula vya

kujenga mwili kama maharage na mayai. Kula matunda

kwa wingi na mboga za majani. Utahitaji vilevile madini

kama kalsiamu. Kalsiamu inapatikana katika maziwa

lakini ile yenye gharama nafuu inapatikana toka kwenye

samaki wadogo wanaoliwa na miiba yake (dagaa).

Pata madini ya ziada ya chuma yanayotolewa hospitalini au kliniki. Mwili wako unahitaji

madini ya chuma kwa wingi ili uwe na nguvu na afya wakati wa ujauzito.

Hakikisha unakwenda kliniki ya akina mama na unapata chanjo za lazima mapema.

MiMba na VVu

cissy kutoka uganda (umri wa miaka 17)

“Haikuwa rahisi mara ya kwanza nilipogundua nilikuwa na mimba. Sikuwahi

kufikiria ingeliweza kunitokea. Nilizungumza na rafiki yangu wa

karibu akanishauri nionane na mshauri ambaye alinisihi nisitoe mimba,

kitu nilichotaka kufanya. Niliwapoteza marafiki zangu, lakini niliyakubali

makosa yangu, na sasa nina mtoto wa kike. Sitakubali kurudia tena kosa”.

Hakikisha unakwenda kliniki ya akina

mama na unapata chanjo za muhimu

mapema.

Ni muhimu mno kujikinga dhidi ya maambukizo ya ugonjwa wa UKIMWI wakati una mimba na

baadaye wakati unanyonyesha. Hii ni kwa sababu ukiambukizwa nyakati hizi, kuna uwezekano

wa kumwambukiza mtoto VVU. Sisitiza matumizi ya kondomu na mwenzi wako. Wewe na mwenzi

wako mnaweza kwenda kupima VVU pamoja. Kama mmoja wenu au wote mna VVU, mnatakiwa

kutumia kondomu wakati wote mnapojamiiana. Iwapo wote vipimo vitaonyesha hamna VVU

mnatakiwa kuwa waminifu na kuendelea kutumia njia ya uzazi wa mpango ya chaguo lenu ikiwa ni

pamoja na kutumia kondomu.

Ukigundua una VVU wakati wa ujauzito, mwambie daktari. Siku hizi kuna dawa ambayo unaweza

kutumia ukiwa mjamzito ili kupunguza maambukizi kwa mtoto. Kwa kawaida, karibu asilimia 30

ya watoto waliozaliwa na mama walio na virusi vya UKIMWI / VVU wanakuwa wameambukizwa

VVU. Lakini kwa kutumia dawa, unaweza kupunguza hatari ya maambukizo hayo.

Vilevile unatakiwa kuzungumza na tabibu wako kuhusu kunyonyesha mtoto kwa sababu kuna

hatari ya kumwambukiza VVU kupitia kwenye maziwa ya mama. Huduma za dawa za kupunguza

makali ya VVU kwa mama wajawazito zinapatikana. Watoa huduma katika vituo vya tiba

wanaweza kukueleza jinsi mpango wa huduma hizo ulivyo katika ngazi ya Wilaya.

MaanDaliZi Ya KujiFunGua

Kama kijana balehe, unatakiwa kufanya maandalizi ya kujifungulia mtoto hospitalini ambako

wapo wataalamu wa kutosha na vifaa vya kutosha kuweza kushughulikia matatizo yoyote

yanayoweza kujitokeza.Usijaribu kujifungulia nyumbani au kwa wakunga wa jadi. Jitahidi kadiri

iwezekanavyo kujifungulia katika kituo cha afya chenye vifaa bora, mahali ambapo wanaweza

wakafanya upasuaji kuondoa mtoto kupitia tumboni kama italazimu.

Mkunga au mwanamke wa makamo atakushauri vitu unavyovihitaji kwa ajili ya mtoto wako

kama: nepi, nguo na blanketi. Hii itategemea sehemu unayoishi na utaratibu wa afya wa nchi

hiyo. Unaweza kuhitajiwa upeleke vifaa kama pamba, glavu za plastiki, wembe mpya, sirinji

mpya, sindano, sabuni na dawa za kuua wadudu. Unaweza kulazimika kuandaa usafiri wa kwenda

hospitali.

Jaribu kuwa na mwanamke wa makamo mwaminifu wakati wa kipindi cha uchungu, pengine mama

yako mzazi, dada yako mkubwa au shangazi. Hii inaweza kukuliwaza na kukusaidia kwani uchungu

unaweza kuchukua muda mrefu. Mkunga anaweza asiwe na wewe muda wote.

Je, unafahamu kuwa wanawake waliokeketwa wana mahitaji

maalumu wakati wa kujifungua?

Tohara ya wanawake ambayo pia inajulikana kama “female genital mutilation (FGM)” inaweza

kusababisha matatizo ya kipekee kwa wanawake wenye mimba. Tohara mbaya sana ni

“mfyato/ ufyataji”, ambayo uke unashonwa na linaachwa tundu dogo tu kwa ajili ya mkojo na

damu ya hedhi kupita. Tundu hilo lazima lifunguliwe wakati wa kuzaa mtoto ili kichwa cha

mtoto kiweze kupita. Utaratibu huu, lazima ufanywe na mtaalamu wa mambo ya afya ili kuzuia

matatizo zaidi. Makovu yatokanayo na tohara yanaweza vilevile kusababisha viungo vya uzazi

kuchanika wakati wa kuzaa, kwa sababu ngozi haiwezi kutanuka kirahisi. Damu nyingi inaweza

kuvuja.

Kama mtoto hawezi kutoka, inawezekana kukawa na matatizo makubwa. Wakati mtoto

amezuiwa, kuta za uke, kibofu au mkundu vinaweza kupasuka. Kutokana na hali hiyo mkojo na

kinyesi vinaweza kuwa vinavuja wakati wote kupitia ukeni. Wanawake wengi wametengwa na

wenzi wao kwa sababu ya harufu mbaya.

nini cha kufanya.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Jiandae mapema kwa ajili ya kujifungua. Wakati wa nusu ya kipindi cha pili cha mimba,

unatakiwa umwone mkunga kwenye kituo cha afya ambaye amesomea kuzalisha wanawake

waliotahiriwa. Mkunga anaweza akakueleza kama kuna hatari ya kupata matatizo, au uke

unatakiwa kuongezwa. Panga kuzalia katika mazingira mazuri ya afya. Kujifungulia mtoto

nyumbani ni hatari mno.

135

136

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

KujitunZa na KuMtunZa MtOtO baaDa Ya KujiFunGua

Kama ulivyokuwa unakwenda kliniki kabla ya

kujifungua, hakikisha unakwenda tena kwa uchunguzi

baada ya kujifungua. Kama ulimzalia mtoto wako

nyumbani hakikisha unakwenda kliniki kwa ajili

ya uchunguzi ndani ya siku tatu. Kama ulimzalia

mtoto wako hospitalini nenda baada ya wiki sita ili

mkunga aone kama tumbo lako linarudia hali yake

ya awali. Mkunga anatakiwa pia kuangalia kama

huna maambukizo ya magonjwa au hutokwi na damu

sana.Kama ulipoteza damu nyingi wakati wa kuzaa

mkunga atakupa dawa za madini ya chuma ili kusaidia

kuongeza damu.

Mkunga anaweza vilevile kujibu maswali mengi

utakayokuwa nayo kuhusu kunyonyesha mtoto, kulala,

kinga kwa mtoto, kuzuia mimba na mambo mengine.

Mwanamke aliyezaa kwa mara ya kwanza mara nyingi

anakuwa na maswali mengi hivyo kuongea na mkunga

inaweza kukusaidia.

KuhaRibiKa MiMba

Mara nyingine mimba huwa inaharibika/inatoka yenyewe tu. Tunasema mimba imetoka kwa

bahati mbaya. Fitasi inakufa na inatoka kupitia ukeni. Malaria au magonjwa ya ngono huweza

kusababisha kuharibika mimba. Mimba inaweza kutoka vilevile kama fitasi ina matatizo.

Kama mimba itakuwa imetoka mwanamke anahitaji kumwona mhudumu wa afya ili kuhakikisha

hapati maambukizo kwenye tumbo la uzazi. Mhudumu wa afya anaweza pia akatambua

kilichosabisha mimba kutoka na kutoa matibabu ya magonjwa kama ya ngono.

Mimba inaweza vilevile kutolewa kwa makusudi kwa kupitia taratibu za kitabibu. Mimba inaweza

kutolewa na mganga aliyesomea katika mazingira ya hali ya usafi. Kutoa mimba ni utaratibu

salama kitabibu kwa ujumla na ni salama kuliko kuzaa. Katika nchi nyingi za Kiafrika ni kosa la

jinai kutoa mimba isipokuwa katika mazingira ya matatizo kama kubakwa au kujamiiana kwa

maharimu (ndugu wa karibu) au wakati ambapo maisha ya mwanamke yako hatarini kwa ajili

ya mimba au fitasi si ya kawaida na hata akizaliwa mtoto hataishi. Uthibitisho wa kitabibu

unatakiwa kuwepo kuwa mhusika alibakwa kulikuwepo kujamiiana kwa maharimu au fitasi si ya

kawaida.

Kutoa mimba kinyume cha sheria katika nchi nyingi barani Afrika ni hatari sana. Kutoa mimba

kunafanywa katika mazingira machafu na ya hatari na mara nyingi watu wengi wanaotoa

mimba hawajasomea. Kwa sababu kutoa mimba hakuruhusiwi, mtoaji mimba anaweza kutoa

bila utaratibu, kwa haraka na kuogopa na katika mazingira na vifaa vichafu. Mambo yote haya

yanamuweka mwanamke katika hatari kubwa. Kwa hakika, katika nchi nyingi za Afrika, robo ya

vifo vya wanawake wajawazito vinasababishwa na matatizo ya ama mimba kutoka au kutoa

mimba.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Kutoa mimba kwa kutumia njia isiyo salama

kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya.

Kifaa cha kutolea mimba kikiingizwa kwenye

mlango wa mfuko wa kizazi kinaweza

kikasababisha uharibifu kwenye kibofu

cha mkojo au utumbo mdogo au mlango

wa mfuko wa kizazi. Mfuko wa kizazi

ulioharibika utatakiwa uondolewe. Maana

yake, msichana hataweza kupata mtoto tena.

Kutoa mimba kusiko salama vilevile

kunaweza kusababisha kuvuja damu,

maambukizo ya magonjwa na kifo. Kuingiza

kifaa cha kutolea mimba kwenye mlango

wa mfuko wa kizazi na kizazi kunaweza

kusababisha kuvuja sana damu na msichana

anaweza akavuja damu mpaka akafa. Miti

shamba na vifaa vingine vinavyotumika

kuanzisha uchungu mara nyingi siyo safi;

vinaweza kuleta vijidudu vya maradhi katika

mfuko wa kizazi. Kizazi na mirija ya kupitisha

mayai ya mgonjwa vinaweza kuathirika sana

kiasi cha kusababishiwa ugumba au kifo. Miti

shamba, dawa au kemikali ambazo msichana

anameza zinaweza kumfanya awe mgonjwa

sana na anaweza akawa amejipa sumu

mwenyewe.

Je unajua matokeo ya utoaji mimba usio

salama?

Jane alipopata mimba alikuwa na miaka 15

na alikuwa Kidato cha Tatu. Alitaka sana

kuendelea na shule, aliishi na shangazi yake,

ambaye alimpeleka kwa mtu aliyedai ni

mganga anayefanya kazi kwenye hospitali

kubwa mjini Kampala. Mtu huyu aliingiza

kifaa kwenye uke. “Maji” yakatoka. Alisikia

maumivu makali sana, lakini aliambiwa asilie

kwa sababu hata hivyo “alitaka” mwenyewe

kilichomtokea. Shughuli ilichukua dakika 15.

Alirudi nyumbani na alitokwa na damu wiki

nzima, akidhoofu kidogokidogo kila siku.

Tumbo lake liliuma na uke ukawa unatoa

majimaji yenye harufu mbaya. Baadaye

alipelekwa kliniki inayohudumia vijana. Kliniki

waligundua amechanika sehemu kubwa ya

mfuko wa kizazi. Ilibidi afanyiwe upasuaji

na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki nne

kutibu kidonda na maambukizo ya magonjwa.

Jane bado hajui iwapo ataweza kupata watoto

baadaye.

Diana kutoka uganda (umri wa miaka 15)

“Kutoa mimba ni hatari sana hasa kwa kutumia miti shamba. Ni

afadhali usishiriki katika ngono kabisa”.

nedina kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Rafiki yangu wa kike akipata mimba nitamkatisha tamaa asitoe

mimba kwa sababu ni hatari. Nitamsihi azae na kisha aendelee na

masomo yake hapo baadaye”

Kutoa mimba kunaweza kuleta matokeo ya kusikitisha kijamii. Watu wengine wakijua kwamba

msichana ametoa mimba, anaweza kufukuzwa shule, kutoaminika au kufedheheshwa na marafiki

au na familia.

Hata hivyo, wasichana wengi wanaishia kutoa mimba kwa njia isiyo salama wanapojikuta

wamepata mimba. Wanasahau hatari za kutoa mimba kwa sababu ya hofu, familia zao

zitakapogundua ujauzito wao. Wanakata tamaa ya kuendelea na masomo. Marafiki zao wa kiume

wanaweza kuwa wamewaacha au kuwalazimisha watoe mimba.

137

138

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Utoaji mimba usio salama ni hatari sana. Unaweza kupoteza maisha yako.

Kama wewe au yeyote unayefahamu anakabiliwa na mimba isiyotakiwa, tafuta msaada. Kuwa

mwaminifu kwa wazazi /walezi kuhusu hali hiyo. Kama wazazi wako hawakusaidii tembelea kituo

cha vijana na mwombe mshauri wa vijana ushauri kuhusu suala lako. Mwombe mshauri wa vijana

akuelekeze wapi unaweza kwenda kuzungumza na mhudumu wa afya anayejali na mpole.

Kama wewe au yeyote unayemjua alitoa mimba na hajisikii vizuri, nenda hospitali haraka. Kuvuja

damu, homa ya baridi, homa na/au kutoka majimaji yenye harufu ni dalili kwamba kuna mahali

pana matatizo makubwa. Afya yako na maisha yako yapo hatarini hivyo uchunguzi wa waganga

ni muhimu sana. Hata kama sheria ni kali kiasi gani, wahudumu wa afya wana miiko ya kitalaamu

ya kumsaidia yeyote atakayekuwa na matatizo. Usiache woga ukuzuie kupata matibabu na

hatimaye ukapoteza uhai.

Njia nzuri ya kujikinga mwenyewe dhidi ya matokeo ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama ni

kukwepa kupata mimba isiyopangwa ama kuepuka ngono nzembe.

naMna Ya KuePuKa KuPata MiMba

Njia ya uhakika kabisa ya kutopata mimba ni kuacha kufanya ngono. Uzuiaji huu una uhakika wa

asilimia 100, na ni salama kihisia na kimwili. Kama hujamiiani, hakuna jinsi unavyoweza kupata

mimba au kumpa mimba msichana.

Ikiwa unajamiiana, hakikisha pia kuwa wewe na mwenzi wako mnatumia kondomu kujikinga dhidi

ya mimba na magonjwa ya ngono. Unatakiwa pia kuomba msaada kutoka kliniki ya uzazi wa

mpango. Unahitaji kuchukuwa hatua ili mwenzi wako asipate mtoto ambaye huwezi kumtunza

kwa wakati huu.

Kuna aina nyingi za dawa za kuzuia mimba ambazo ni salama kabisa kwa vijana (angalia

kisanduku ukurasa wa 140). Njia yoyote utakayotumia, hakikisha unaitumia inavyotakiwa. Kwa

mfano, kusahau kumeza kidonge kunaweza kusababisha upate mimba.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

je, ViDOnGe VYa KuZuia MiMba ni SalaMa?

Uvumi kama huu ni uwongo na si wa

kisayansi. Tangu miaka ya 1950, mamilioni

kwa mamilioni ya wanawake wametumia

dawa za vidonge za kuzuia mimba. Vidonge

vya kuzuia mimba vimefanyiwa uchunguzi

mkubwa katika historia ya dawa. Kwa

kuyafuatilia maisha ya maelfu ya wanawake

kwa miaka mingi waganga sasa wanajua

kwamba vidonge vya kuzuia mimba havileti

saratani. Uwezekano wa wanawake

wanaomeza vidonge kupata saratani ya

kokwa la mayai na uwezekano wa kupata

saratani kwenye ngozi laini ya kuta za

tumbo la uzazi ni mdogo kuliko wanawake

ambao hawajawahi kutumia vidonge hivyo.

Kuna uvumi mwingine kwamba kutumia vidonge vya kuzuia mimba wakati wa ujana balehe

kunaweza kuharibu kokwa la mayai na kusababisha isiwezekane kupata mimba baadaye. Huu pia

ni uzushi.Mwongozo wa kimataifa wa kutumia dawa za kuzuia mimba unasema vidonge ni vizuri

kwa wanawake ambao bado hawajapata watoto. Ukweli ni kwamba ,mara nyingine vinatumika

kuwasaidia vijana balehe kuwapunguzia maumivu makali wakati wa hedhi. Huhitaji kuwa na

mtoto kwanza ndipo uanze kumeza vidonge. Vidonge havitaharibu kokwa la mayai.

Wasichana na wanawake wengine wanapata kichefuchefu, matiti kuwa laini na kuongezeka

uzito wanapoanza kumeza vidonge. Matokeo haya huwa yanatoweka baada ya mwezi mmoja au

zaidi. Karibu wanawake wadogo na wanawake wa makamo wote wanaweza kumeza vidonge. Ni

wanawake wa makamo tu ambao wanaovuta sigara, walio wanene sana au wanashinikizo la damu

au magonjwa fulani kwenye mfumo wao wa damu wanashauriwa wasitumie njia ya homoni kuzuia

mimba (vidonge vya kuzuia mimba, sindano na vipandikizi). Unatakiwa kumwona mtoa huduma ili

akupime kama huna vidokezo vya mteja wa dawa za kuzuia mimba.

KuZuia MiMba KWa DhaRuRa

christine kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Nimesikia kwamba vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha

saratani au pia ulemavu kwa mtoto”.

Kuna njia moja zaidi ya kuzuia mimba ambayo hapana budi kuijua. Hii ni njia ya dharura ya kuzuia

mimba. Njia ambayo unaweza kuitumia kuzuia mimba haraka baada ya kufanya ngono isiyo

salama. Kwa mfano kama ulisahau kutumia kondomu au kama kondomu ilipasuka au ilitoka kwa

bahati mbaya (jambo ambalo ni nadra sana kama ikitumika vizuri).

Kinga ya dharura ya kuzuia mimba imeanza kupatikana sehemu nyingi siku hizi. Kama ukifanya

ngono bila kinga na una wasiwasi wa kupata mimba unaweza kwenda kwa muhudumu wa afya na

kumwomba kinga ya dharura ya kuzuia mimba. Ikiwa umebakwa omba kinga ya dharura ya kuzuia

mimba kutoka kwenye kliniki ya mpango wa uzazi au kituo cha vijana karibu na wewe katika

kipindi cha saa 72 (siku 3).

139

140

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Je, unajua njia zipi za kuzuia mimba ambazo ni salama kwa vijana?

Njia zote hizi za kuzuia mimba ni salama kwa vijana:

Kondomu: Kondomu ni mpira laini ambao huwekwa kwenye uume

uliosimama kabla ya kujamiiana. Mwanaume anapotoa shahawa (“anafikia

mshindo”) zinanaswa nchani mwa kondomu. Majimaji toka kwa mwanaume

hayamwingii mwanamke na majimaji toka kwa mwanamke hayagusi uume

wa mwanaume. Kondomu zinatoa kinga nzuri dhidi ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/ UKIMWI

na huzuia mimba. Bei ya kondomu ni ndogo na zinawasaidia wanaume wengine kuchelewa kutoa

shahawa mapema.

Vidonge: Vidonge vina kiasi kidogo sana cha homoni. Homoni hii huzuia uovishaji

kutoka kwenye makokwa ya mayai. Mwanamke aliyeingia kwenye hedhi

anapomeza kidonge lakini kidonge kinafanya hedhi ya mwanamke kuwa nyepesi

na maumivu kuwa mepesi. Pia matokeo ya kuzuia mimba kwa kutumia vidonge

ni mazuri sana, lakini lazima umeze kila siku. Ukikosa kumeza zaidi ya siku moja

unaweza kupata mimba kwa sababu rutuba inarudi pindi unapoacha kumeza

vidonge. Vidonge havizuii VVU au mangojwa mengine ya zinaa. Kwa hiyo, ni vizuri

iwapo unatumia kondomu, uwe na mwenzi mmoja tu na wote muwe mmepima na kuthibitisha hamna

magonjwa ya ngono/VVU.

Sindano: Sindano ina homoni ambazo zinazuia yai kurutubishwa. Huanza

kufanya kazi katika muda wa saa 24 na hutoa kinga dhidi ya mimba kwa

muda wa miezi mitatu. Kudunga sindano ni rahisi kwa sababu huhitaji

kukumbuka kumeza kidonge kila siku au kufanya chochote kabla ya

kujamiiana. Sindano pia inatunza siri, hakuna anayeweza kujua kwamba

unatumia mtindo huu kwa kuzuia mimba. Sindano zinafanya siku zako za

hedhi ziwe nyepesi na zenye maumivu kidogo ambapo zinaweza kuwasaidia

vijana wanaopata maumivu au hedhi nzito. Unapoacha kudunga sindano, huwi na rutuba tena mara

moja, kwa sababu homoni zinakaa mwilini kwa muda . Wanawake wengi wanakuwa na rutuba tena

ndani ya mwaka mmoja wanapoacha kutumia sindano, lakini wengine wanapata mimba mapema.

Sindano hazizuii magonjwa ya zinaa/VVU hivyo zinafaa tu kama unatumia kondomu au kama unaye

mwenzi mmoja na wote mmepima magonjwa ya ngono/VVU.

Vipandikizi: Vipandikizi ni vimrija vidogo vinavyowekwa ndani ya ngozi kwenye

mkono chini kidogo ya bega. Vimirija hivyo huwa vinatoa homoni inayozuia yai

kurutubishwa. Kama ilivyo kwa sindano huhitaji kukumbuka kumeza vidonge

au kufanya lolote kabla ya kujamiiana. Vipandikizi vinadumu miaka mitano.

Lakini vinaweza kuondolewa mapema. Ni kinga nzuri sana kuzuia mimba, lakini

haizuii magonjwa ya zinaa/VVU. Kwa hiyo unatakiwa kutumia kondomu au kuhakikisha kuwa wewe na

mwenzi wako hamna magonjwa ya ngono/VVU.

Dawa ya kuulia mbegu za kiume (vidonge mafuta au krimu na povu): Dawa

hizi zinaua mbegu za mwanaume kabla hazijaingia ndani ya mfuko wa kizazi,

lakini hazimuumizi mwanaume au mwanamke. Zipo aina mbalimbali za dawa

na zinaingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Dawa hizi zitumike na kondomu kwa

sababu zina kinga ndogo sana dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU. Zaidi ya hapo,

hazina kinga madhubuti kama ya vidonge au sindano katika kuzuia mimba.

Tofauti na vidonge na sindano, huhitaji kuzipata kutoka kwa mhudumu wa afya; unaweza kupata moja

kwa moja toka kwenye maduka ya dawa. Hii inaweza kuwa bahati kama una aibu kwenda kliniki, lakini

kumbuka kutumia kondomu.

Unapotumia vidonge vya dharura inakubidi umeze kiasi cha mchanganyiko wa vidonge vya kuzuia

mimba baada ya saa 12 katika kipindi cha saa 72 za kufanya ngono bila kinga. Kinga ya dharura ya

kuzuia mimba haifanyi kazi mimba inapokuwa imetungwa. Ndio maana ni muhimu kuipata haraka

baada ya ngono isiyo na kinga. Usijaribu kunywa dawa hizi bila ushauri wa mhudumu wa afya

mwenye ujuzi.

KinGa MaRa Mbili

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Je, unafahamu kuwa wanawake waliokeketwa wana mahitaji

Kuchomoa/kurusha: Kuchomoa au kurusha ni wakati mwanaume anatoa uume nje ya uke

kabla ya kukojoa shahawa. Njia hii sio salama kwa sababu wanaume wengi hawawezi kuutoa

uume kwa wakati unaotakiwa. Mara nyingi wanaume hawajui kwamba wanakaribia kukojoa

mpaka wanapokuwa wamekaribia sana. Pia, matone machache ya shahawa yanaweza kutoka

kabla ya kukojoa na matone machache haya yanatosha kusababisha mimba. Kuchomoa

hakuleti kinga dhidi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.

“Siku salama”: Wanawake wengine wanasubiri siku ambazo wanajua kwamba hawana rutuba.

Utaratibu huu unafaa kwa wanawake ambao hedhi zao ni za kawaida na wenzi wao wana

ushirikiano. Wasichana wa umri mdogo wengi hawana hedhi za kawaida hivyo si rahisi kujua

siku salama. Kama ilivyo kwa njia ya kuchomoa, siku salama hazileti kinga dhidi ya magonjwa

ya zinaa/VVU.

Kitanzi: Kitanzi kinatumbukizwa kwenye tumbo la uzazi na mhudumu wa afya. Ni rahisi

kukiingiza kwa mwanamke ambaye amewahi kuzaa, kwa hiyo haipendekezwi kwa vijana.

Kitanzi kinaweza kusababisha ugonjwa wa ngono ukue na kufikia hali ya kutisha. Kwa vile

vijana ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa ya zinaa, wasitumie kitanzi. Kitanzi hakitoi kinga

dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Kufunga kizazi: Kukata au kufunga mirija ya kupitishia mbegu ya wanaume na wanawake ni

njia ya kudumu ya kuzuia mimba. Unafanyika upasuaji ambapo mirija ya kupitishia shahawa na

yai inazibwa. Njia hii inawahusu wanaume na wanawake ambao wanafikiri wamepata idadi ya

watoto inayowatosha. Njia hii haifai kwa vijana kwa sababu huwezi kupata watoto baada ya

upasuaji. Kufunga kizazi hakutoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Ugonjwa wa UKIMWI umebadilisha mawazo ya watu wengi kuhusu njia za kuzuia mimba.

Zamani watu walilenga katika kuangalia ni njia zipi zinaleta matokeo bora katika kuzuia mimba.

Hawakujali sana kama njia ya kuzuia mimba ilitoa kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Leo mambo ni tofauti. Kupata VVU ni maafa makubwa kuliko kupata mimba isiyotakiwa. Siku

hizi watu wanazungumzia kuhusu kinga mara mbili. Kinga mara mbili ni wakati unatumia njia

ambayo matokeo yake hupunguza hatari ya mambukizo ya magonjwa ya zinaa/VVU/UKIMWI, na

wakati huohuo, unatumia njia nyingine ambayo matokeo yake ni mazuri katika kukinga mimba

zisizotakiwa.

Angalia njia mbalimbali hapa chini uone jinsi zinavyotoa kinga dhidi ya mimba na magonjwa

mengine ya ngono pamoja na VVU.

141

142

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Hata hivyo, njia pekee nzuri ya kujikinga ni kuacha kujamiiana au kuacha zinaa. Lakini kama

unavyoweza kuona hapo juu, yeyote ambaye anajamiiana, njia nzuri ya kuzuia mimba ni kutumia

vipandikizi, sindano na kondomu.

Stabisile kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 19)

“Kama mwanamume anakataa kutumia kondomu, huyo anapoteza

muda.

” cathy kutoka uganda (umri wa miaka 17)

“Ninapendekeza matumizi ya kondomu ili kukwepa maambukizo

ya VVU/UKIMWI, magonjwa ya zinaa na kuzuia mimba

zisizotakiwa”.

Kondomu ni nzuri kwa kuzuia mimba, na zinakusaidia kukukinga wewe na mwenzi wako dhidi ya

magonjwa ya zinaa/UKIMWI. Unaweza kufanya ziwe kinga nzuri zaidi kwa kuchanganya vidonge

na njia nyingine ya kuzuia mimba.

iwapo yeyote anasema hataki kutumia kondomu jiandae kwa jibu zuri! na jiandae kuondoka kama

atakataa kutumia kondomu.

Sura ya 11

Mimba na uzuiaji wa mimba

Wakati wote mwanaume na mwanamke wakijamiiana bila kinga, mimba inaweza kutokea.

Mimba inaweza ikatokea mara ya kwanza tu mnapojamiiana bila kinga.

Mimba inaweza kutungwa kama mbegu moja inakutana na yai na kulirutubisha ndani ya

mwanamke. Kama yai litarutubishwa, linajishikiza kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Huu ndio

mwanzo wa mimba.

Dalili za mimba ni pamoja na:

Kukosa siku zako za hedhi

Kujaa na kuuma kwa matiti

Kichefuchefu

Kuwa mchovu

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Kutaka kukojoa mara kwa mara.

Mimba ni hatari hasa kwa wasichana balehe kwa sababu miili yao bado haijakomaa.

Wasichana wadogo wanakabiliwa na matatizo makubwa ya afya wakati wa mimba na wakati

wa kuzaa kuliko wanawake wa makamo. Kwa hiyo, ni jambo la muhimu hasa kwa msichana

mdogo kupata matunzo sahihi wakati wa mimba. Inashauriwa kuzalia hospitalini mahali

ambapo kuna wahudumu wa afya wa kutosha na vifaa vinavyoweza kumudu matatizo yoyote

ya uzazi.

Wasichana balehe wengi wanapata mimba kwa makosa. Wanaamua kutoa mimba kwasababu

wanataka kuendelea na shule au kwa sababu hawataki kuwaaibisha wazazi wao. Hata hivyo,

katika nchi nyingi za Afrika kutoa mimba ni kinyume cha sheria na si salama hata kidogo.

Kutoa mimba kusiko salama kunaweza kusababisha matatizo makubwa kiafya, kuanzia

maambukizo ya magonjwa, uharibu wa via vya uzazi, kuvuja damu sana, ugumba na vifo. njia

sahihi ya kukwepa mimba ni kuacha ngono. Kuacha kabisa ni salama kwa asilimia 100.

Iwapo unashiriki kujamiiana, wewe na mwenzi wako mnatakiwa wakati wote kujikinga dhidi

ya mimba na magonjwa ya ngono pamoja na VVU/UKIMWI. Njia zote za kuzuia mimba ni

salama kwa vijana.

Kama umesahau kutumia kinga ya mimba au kama kondomu itatoka au kupasuka, nenda

haraka kwenye kliniki waombe kinga ya dharura ya kuzuia mimba. Inaweza kuzuia mimba

ikiwa itatumika katika kipindi cha saa 72 cha kujamiiana bila kinga.

Mimba inahusu watu wawili yaani mwanamume na mwanamke. Wavulana na wanaume pia

watu wazima, wote wanalo jukumu la kuzuia mimba.

143

144

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ngono ya kulazimishwa na

Ngono bila ya ridhaa yako

Wakati mwingine watu yaani wanaume kwa wanawake na wavulana kwa wasichana wanajamiiana

huku kiukweli hawapendi kufanya hivyo. Wanaweza kushinikizwa na rafiki wa kiume au kike

kujamiiana kama ushahidi wa mapenzi yao. Wanaweza kushinikizwa kufanya ngono ili kulipa

zawadi au pesa walizopokea. Au wanaweza kulazimishwa kujamiiana na mtu ambaye ni mkubwa

au ana nguvu zaidi.

Ngono isiyotakiwa ni hatari. Itakuweka katika hatari ya kupata mimba na magonjwa ya ngono

ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Vilevile, inakuweka katika hatari ya kupata magonjwa ya hisia.

Unaweza kupata maumivu makali sana ya kihoro iwapo utajamiiana bila ridhaa yako.

Njia nzuri ya kukwepa ngono za namna hii ni

kuyakimbia mazingira mabaya yanayoweza

kusababisha ukaingia katika mtego.

ShiniKiZO KutOKa KWa RaFiKi Wa

KiuMe au Wa KiKe

Wakati mwingine wavulana wanawaambia wasichana

wajamiiane kama ushahidi wa mapenzi yao. Vilevile,

wasichana wanawaambia wavulana vivyohivyo.

Watu wengine wanafikia hatua ya kutishia kuvunja

uhusiano pindi mwenzi atakapokataa kujamiiana.

Inaweza kuwa vigumu iwapo mtu unayempenda na

kumjali akikwambia mjamiiane. Unaweza kudhani

njia pekee ya kuendeleza urafiki ni kumkubalia

mfanye ngono. Unaweza kudhani ni vema kumkubalia

kwa sababu unamjali na unataka afurahi.

Ngono kamwe isitumike kama ushahidi wa

mapenzi.

145

SURA YA 12

146

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Katika mazingira kama haya, inaweza kuwa vigumu sana kujua tofauti ya kile anachokitaka na

kile wewe unachokitaka. Ni rahisi kuchanganyikiwa lipi ni sahihi kwako.

Iwapo rafiki yako wa kiume au wa kike anashinikiza mjamiiane, fikiria maswali yafuatayo:

Unathamini nini? Je, unaamini kwamba ni sahihi kujamiiana wakati huu katika maisha yako?

Au je, huoni ni vyema usubiri mpaka baadaye, kama vile utakapoolewa au kuoa?

Unajisikia vizuri kuhusu wazo la kujamiiana au wazo hilo linakufanya ukose raha?

Unajisikia kama unaweza kukataa kujamiiana au hili linaenda kinyume na kile unachofikiri

ni sahihi kwa msichana au mvulana kufanya? Kwa mfano, katika maeneo mengine, ni vigumu

sana msichana kusema “HAPANA” kwa mvulana au mwanaume kwa sababu amefundishwa

kwamba wakati wote anatakiwa kuwa mnyenyekevu kwa mwanaume. Katika maeneo

mengine inaweza kuwa vigumu sana kwa mvulana kusema “HAPANA” kwa sababu amelelewa

kuamini kwamba mwanaume wakati wote anatakiwa kujamiiana. Hivyo mtu anaweza kuhisi

kwamba kwa kusema hapana inaweza kuleta matatizo.

Unafikiri mwenzi wako ataendelea kukupenda na kukuheshimu kama ukikataa?

Majibu ya maswali haya yatakueleza mengi kuhusu kama ujamiaane au usijamiiane na rafiki

yako. Uwe msichana au mvulana, wote mnayo haki ya kukataa kujamiiana. Ni wewe unayetakiwa

kufanya uamuzi mwenyewe kuhusu kujamiiana. Kama huamini kwamba ngono inakufaa wakati

huu wa maisha yako, usifanye; bila hata kujali rafiki yako wa kiume au kike anasema nini.

Kama hujisikii kufurahia wazo la ngono na hauko tayari kufanya, usifanye. Iwapo unafikiria rafiki

yako wa kike au wa kiume hatakupenda ukikataa kujamiiana, ukweli ni kwamba hakupendi kama

atakuchukia. Hakuna mtu ambaye anakupenda kweli atakulazimisha kufanya jambo ambalo

unahisi ni baya kwako.

Iwapo huna uhakika kama rafiki yako wa kike au wa kiume atakuwa na wewe ukikataa kujamiiana,

labda jambo la maana la kufanya ni kusubiri na kuona. Mwambie rafiki yako kwamba unampenda

lakini umeamua kwamba hauko tayari kujamiiana. Kama akisema ni sawa, basi unaweza ukatuliza

moyo na kutulia. Unaweza kufurahia uhusiano wenu mzuri bila kukimbilia kufanya ngono.

Hata hivyo, iwapo rafiki yako wa kike au kiume ataamua kukuacha, hii inaweza kuwa ngumu kwa

sababu inakuonyesha kwamba rafiki yako alikuwa hakupendi. Unaweza kujisikia una huzuni na

mpweke. Unaweza kufikiri ulifanya uamuzi usio sahihi, lakini hukufanya! Ulifanya kilichokuwa

sahihi kwako. Katika kufanya uamuzi ukakuta rafiki yako wa kiume au wa kike alitaka kukutumia

na wala hakuwa anakujali, bila shaka uvumbuzi huu utakuhuzunisha, lakini ni afadhali kuvumbua

mapema kwani ingekuwa vibaya zaidi kama ungegundua baada ya kujamiiana.

ShiniKiZO KutOKa KWa Watu WaZiMa

Wakati mwingine watu wazima ikiwa ni pamoja na waliooa au kuolewa, wanawalazimisha vijana

kufanya ngono. Mara nyingi wanaume, watu wazima (wazee) wanapenda kuwa na uhusiano wa

kimapenzi na wasichana wadogo.

SURA YA 12 | NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO

Wakati mwingine vilevile wapo wanawake watu

wazima wanaopenda kuwa na uhusiano wa

kimapenzi na wavulana wa umri mdogo.

Mara kwa mara mtu mzima hutoa zawadi, pesa

au huduma maalumu kwa kijana. Mtu mzima

anaweza kutoa pesa kwa ajili ya karo, nguo au

peremende. Iwapo mtu mzima ni kama mwalimu

au dereva wa basi, anaweza kuahidi kumpa

alama nzuri au kumpakia kwenye gari bure.

Lakini zawadi zote hizi siyo bure. Baada ya

muda mtu mzima atadai “malipo” kwa zawadi

alizotoa. Kawaida kijana “atalipa” kwa njia ya

ngono.

effie Kutoka Kenya ( umri wa miaka 16)

“Nilikuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa na umri wa miaka

15. Rafiki yangu alikuwa na uhusiano na mtu mzima ambaye

alikuwa anampa kila alichotaka, na mama yake alifahamu kuhusu

uhusiano huo na wala hakujali. Siku moja akiwa anaelekea shuleni

aliona gari la mzee huyo. Aliamua kumpa lifti mpaka shuleni,

lakini wakiwa njiani kuelekea shuleni yule mwanaume alipita njia

nyingine na akampeleka msichana kwenye nyumba ya kulala

wageni na akajamiiana naye kwa nguvu”.

Ingawa inaweza kufurahisha kuona mtu mzima anavutiwa na wewe na inaweza kukufanya ujisikie

unapendeza na ni wa maana, uhusiano wa namna hii ni mbaya sana. Unaweza kuwa hatari kwako

kwa vile:

Unaweza kupata maambukizo ya magonjwa ya

zinaa, VVU/UKIMWI na mimba.

Unaweza kukatisha masomo yako.

Unaweza kuwa chanzo cha hasira kwa mke wake

au mume wake ambaye anaweza kukushambulia

au kukudhuru.

Umri unapopishana sana na kipato kinapotofautiana,

vilevile uhusiano hauwi sawa. Unaweza kujisikia

huna mamlaka. Unaweza kuogopa kusema hapana

unapoombwa ngono kwa sababu unajua ulichukua

pesa au zawadi. Unaweza vilevile kuogopa

kumwambia mtu mzima kutumia kondomu.

Huu ni uhusiano wa hatari sana unaweza kuharibu

maisha yako ya baadaye au milele!

Watu wazima wanaweza kukupatia pesa au

zawadi kwa ajili ya ngono. uhusiano huu ni

hatari kwako

KWa nini unaniPa

MiMi hiZi PeSa?

SitaZichuKua!

aSante.

Kataa kupokea zawadi na pesa. usijiingize

katika deni na mtu.

147

148

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unaweza kushawishika kuingia katika uhusiano na mtu mzima, hususani kama huna pesa za

matumizi na wazazi wako hawawezi kukununulia vitu vya kukufurahisha na vilivyo vizuri. Hata

hivyo, hakuna zawadi au kiasi cha pesa chenye thamani ya gharama utakayolipa.

Iwapo mtu mzima, mwanaume au mwanamke anajaribu kukupatia zawadi au pesa na anashinikiza

mjamiiane, kuwa jasiri. Sema “hapana” na ondoka bila kuchelewa. Waeleze wazazi au shangazi

au mjomba au mwelimisha rika kilichotokea. Waombe wakusaidie uweze kuimudu hali hiyo.

Usijaribu kutatua peke yako.

Vijana wengine wanaingizwa katika uhusiano wa namna hii na wazazi wao. Hii ni kwa sababu

wazazi ni maskini na hawawezi kulipa karo, chakula, nguo na vitu vingine. Hali kama hii ni ngumu

kwa kijana yeyote. Iwapo utakuwa katika mazingira kama haya unahitaji kufikiri kiubunifu:

Ni nani unaweza kumwendea kwa ajili ya msaada? Unaweza kuzungumza na ndugu wengine

kama vile shangazi, mjomba, babu, bibi au kaka au dada? Huenda wakakulipia karo au

wakawasaidia wazazi wako kufanikisha yote. Unaweza kuzungumza na mtu yeyote ndani

ya jamii, kama vile mtu wa kanisani, msikitini au kutoka kituo cha vijana? Hawa wanaweza

kufahamu namna ya kutatua tatizo lako.

Je, unaweza kuzungumza na mwalimu au mkuu wa shule? Waulize namna unavyoweza

kulishughulikia tatizo lako. Pengine wanaweza kukusaidia kwa kukusamehe karo au kwa

kukupatia kazi ya kufanya shuleni ili uweze kulipa karo.

Je, unaweza kupata pesa? Unaweza kufanya kazi, kama kuuza mboga, karanga, bisi au

peremende baada ya shule ili kupata pesa?

Wapo watu wengine wanaokuzunguka ambao wanaweza kukusaidia ikiwa watajua tatizo lako.

Kwa hiyo omba msaada na usijaribu kulitatua peke yako.

unYanYaSaji KijinSia

Margaret kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 17)

“Kitu kimoja ninachojua kuhusu wanaume ni kwamba wengi

huwania kujifurahisha na mtu wa jinsi nyingine, na katika kufanya

hivyo wanaweza kukuahidi hazina zote za maisha. Kwa

hiyo, nimesema HAPANA kwa wanaume wengi na nitaendelea

kufanya hivyo.”

neema kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Alikuwepo mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anajaribu

kufanya urafiki na mimi lakini nilikataa. Mwanaume huyo alikuwa

anawatuma wasichana wengine kujaribu kunishawishi,

lakini nilikataa.”

Aina yoyote ya kuguswa au kushikwashikwa kimapenzi bila ridhaa ya anayetendewa hivyo ni

unyanyasaji kijinsia. Inaweza ikawa kushikwa matiti au sehemu za siri. Inaweza vilevile ikawa

kujamiiana. Aina yoyote ya kukutana kimapenzi bila ya kupenda ni unyanyasaji pia.

SURA YA 12 | NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO

Unyanyasaji kijinsia mara nyingi unafanywa na

mtu mzima anayemjua kijana na ana madaraka juu

yake. Mtu mzima anaweza kuwa jirani, rafiki wa

familia, mwalimu, kiongozi wa dini au kiongozi wa

jamii. Mtu mzima anaweza akawa ndugu, kama vile

mzazi, mzazi wa kambo, mjomba au shangazi, kaka

au dada.

Unyanyasaji kijinsia unaweza kuhusisha tishio,

rushwa, udanganyifu, ujanja na vurugu. Mtu mzima

anaweza kukutishia, au mtu mzima anaweza

kukupatia zawadi ili kukufanya utoe ushirikiano.

Mtu mzima anaweza pia kukudanganya au

kukutegea ufanye jambo. Mtu mzima anaweza

kukutishia kukudhuru wewe au familia yako iwapo

utamwambia mtu yeyote kuhusu unyanyasaji

kijinsia. Mtu mzima anaweza kukuchanganya akili

kwa kusema uhusiano utakuwa wa siri.

Unyanyasaji kijinsia ni jambo baya sana na linaweza kukufanya uchanganyikiwe. Hapa kuna

mambo machache ya kuyaweka maanani:-

Mwili wako ni wako.

Unayo haki ya kuamua nani akushike, akushike vipi na wakati gani.

Kugusana kwa aina yoyote kusikokubalika ni

unyanyasaji kijinsia.

Mtu yeyote asiangalie au kukushika sehemu zako za siri kwa namna ambavyo utajisikia

vibaya.

Amini hisia zako kuhusu kuguswa na amua nini kilicho chema kwako. Usimsikilize mtu

anayejaribu kukushawishi vinginevyo.

Mtu akikugusa ambavyo hupendelei, sema “hapana” kwa nguvu na kwa sauti. Kuwa jasiri.

Tafuta mtu wa kumweleza kuhusu tukio. Ongea na mzazi, shangazi au mjomba, babu, bibi, rafiki,

mwalimu au mama wa rafiki yako. Pata msaada.

iwapo yupo mtu anakunyanyasa kijinsia au anakushinikiza ufanye naye ngono, tafuta msaada. Ongea

na wazazi au mtu mwingine anayejali.

149

150

KuDhaliliSha KijinSia

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unyanyasaji kijinsia hauishii katika kushikashika au kugusa mwili. Wakati mwingine matusi ya

nguoni na utazamwaji wa kifuska vinaweza kumfanya mtu ajisikie vibaya.

Aina yoyote ya kitu kisichovutia kijinsia unaitwa udhalilishaji kijinsia. Mifano ya udhalilishaji

kijinsia ni:

Kumwita msichana “mchafu”,anajirahisisha au mkarimu kwa sababu tu ya uvumi kwamba

amekuwa na wapenzi wengi.

Kupiga miluzi au kutoa maoni juu ya mwonekano wa mtu anapopita mbele yako.

Utani wa kimapenzi kama vile utani kuhusu matiti au mwili wa msichana.

Udhalilishaji kijinsia unaweza kutokea mahali popote – shuleni, mtaani, sokoni, kanisani au

nyumbani.Udhalilishaji kijinsia mara nyingi unatokea kwenye mabasi wakati wa kwenda shuleni

au wakati wa kurudi nyumbani. Wadhalilishaji wanaweza kuwa wageni au watu unaowafahamu,

kama mwalimu, jirani, ndugu au mtu mnayefanya naye kazi au mwanafunzi.

Udhalilishaji kijinsia ni jambo zito. Maneno tu yanaweza kuharibu heshima yako. Yanaweza

kukufanya ujisikie kudhalilika na kukosa raha. Yanaweza vilevile kukufanya uogope.

Kuogopa kwa sababu ya kudhalilishwa kijinsia ni jambo la kawaida na la asili. Hisia hizi ni silika

inayokueleza uwe mwangalifu. Watu wanaotoa maneno mabaya kijinsia, kwa vyovyote vile

hawajali hisia zako. Hawajali kama yanakuumiza. Maneno machafu ya kijinsia yanaweza kuwa ni

onyo kwamba, jambo baya zaidi linakuja.

Njia nzuri ya kumudu udhalilishaji kijinsia ni kuwaepuka watu wanaotoa maneno machafu ya

kijinsia. Usionyeshe unaogopa. Kuwa mtulivu na mwenye kujiamini, na ondoka sehemu hiyo.

Jaribu kuepuka hali kama hii baadaye. Kwa mfano, kama kuna mtu anakusumbua unapokwenda

shuleni, jaribu kubadilisha njia au muda unaokwenda.

Njia nyingine za kumudu udhalilishaji kijinsia ni pamoja na:

Kutojilaumu. Kumbuka, hakuna mwenye haki ya kukunyanyasa kwa vile unavyoonekana,

ulivyovaa au tabia yako ya mapenzi iliyopita.

Kuongea na mtu. Usinyamaze kimya; zungumza na mzazi, shangazi, mjomba, mwelimishaji

rika au mwalimu unayemwamini. Waombe wakusaidie kuishughulikia hali hiyo.

ubaKaji

Ubakaji ni kitendo cha kutumia nguvu ambacho mtu analazimishwa kujamiiana.Waathirika wa

ubakaji mara nyingi ni wanawake, hata hivyo, wakati mwingine wavulana na wanaume wanabakwa

vilevile.

Ubakaji ni kitendo cha kulazimisha, utumiaji wa nguvu, kufedhehesha na ukatili. Watu wengi

wanadhani kwamba wabakaji ni wageni wenye vurugu. Hata hivyo hili ni jambo ambalo sio la

kawaida, kubakwa na mtu asiyejulikana ni mara chache sana. Wengi waliobakwa wanawafahamu

SURA YA 12 | NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO

waliowashambulia. Kawaida mshambuliaji anaweza kuwa ni rafiki wa kiume, jirani, ndugu au rafiki

wa familia.

beth kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Ilikuwa tarehe 16 mwezi wa Novemba nilipomtembelea rafiki

yangu. Hakuwa mpenzi wangu, alikuwa rafiki wa kawaida. Kawaida

nilikuwa ninaenda huko na kukaa naye siku nzima. Lakini siku

hiyo alibadilika. Alinivutia kitandani na tukaanza kupambana.

Alitaka kunilazimisha tujamiiane lakini nilikataa. Baadaye alianza

kusema maneno matamu na hakutaka kunisikiliza. Kisha niliruka

pembeni na kumweleza kwamba sitaki nipate mimba kwa sababu

mimi ningali mdogo. Nilitoka nje ya nyumba nikimuaga kwa heri.

Tangu siku hiyo sijarudi tena kwenye nyumba ya mvulana huyo.”

Ubakaji mwingi kwa vijana ni ule wa miadi na rafiki yako na ule wa watu uliowazoea. Ubakaji

wa aina hii hutokea pale rafiki wa kiume anapomlazimisha rafiki wa kike wajamiiane bila ya

ridhaa yake. Pengine walikuwa wanakumbatiana na kubusiana lakini baadaye rafiki wa kiume

akamlazimisha msichana wajamiiane.

Ulikuwa unafahamu kwamba mambo mengi yanayozungumzwa

kuhusu ubakaji siyo ya kweli?

Kuna uzushi kuhusu ubakaji kama ifuatavyo:

• Wasichana wanafurahia. hii siyo kweli! Ubakaji unatisha na unaleta kihoro. Unaumiza

kimwili na kihisia. Hakuna mtu ambaye anaweza kufurahia kubakwa.

Wasichana wanaomba kubakwa wanapovaa nguo zinazochochea ashiki au

wanapotembea kwa namna ya kuchochea ashiki. Siyo kweli! Hakuna mtu anayeomba

kubakwa.

Mwanaume hawezi kushitakiwa kwa vile msichana au mwanamke alikuwa amemchochea

kwa nguo yake fupi au kwa kukaa kifuska. Siyo kweli! Wanaume wote wanao uwezo wa

kudhibiti hamu ya kujamiiana. Wale wanaosema hawawezi, wanadanganya na lazima

waadhibiwe.

• Msichana au mwanamke akisema “hapana” ukweli anamaanisha “ndiyo”. Siyo kweli!

Mwanamke akisema “hapana” anamaanisha “hapana” Hamaanishi “ndio” au “labda”.

Iwapo msichana au mwanamke amebakwa, yeye ndiye wa kulaumiwa kwa sababu

angeweza kuzuia. uongo! Mwathirika kamwe hawezi kulaumiwa. Mbakaji anawajibika

kwa kubaka na ana makosa. Kamwe usimlaumu aliyebakwa.

Ubakaji wa miadi na ule wa watu uliowazoea ni ubakaji wa kutumia nguvu, unaumiza, unakosesha

raha na ni makosa. Hata kama mvulana na msichana walikuwa wanaelewana, mvulana hana haki

ya kumlazimisha msichana kufanya zaidi ya kile anachotaka.

151

152

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Hata kama wameshawahi kujamiiana kabla, lakini kwa sasa msichana hataki, mvulana hana haki

ya kumlazimisha. Hata kama msichana alikuwa anavaa nguo zinazochochea ashiki, mvulana hana

haki ya kumlazimisha. Katika mazingira yote haya, kitendo cha mvulana kubaka ni kosa la jinai.

naana kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Rafiki yangu alijamiiana kwa sababu rafiki yake wa kiume

alimlazimisha. Hakutaka kujamiiana lakini hakuwa jasiri kwa

sababu mpaka rafiki yake anafikia kushika matiti yake hakukataa.

Kwa hiyo, kijana aliendelea na kumwingilia na akashika

mimba.”

Wakati mwingine wasichana wanaonyesha ishara zinazochanganya. Wanaweza kujionyesha

kama vile wanafurahia kinachotokea, kwa hiyo mvulana anakuwa haelewi ni wakati gani anasema

hataki aendelee zaidi. Hata kama msichana hatoi ishara za wazi, mvulana hana haki ya kumbaka.

Kamwe kubaka si adhabu halali kwa msichana ambaye alikuwa anatoa ishara zinazochanganya.

Wavulana wengine ambao wanawabaka marafiki zao wa kike wana imani potofu kwamba

mwanaume atafanya kile anachotaka bila ya kujali msichana anataka nini. Wavulana wengine

wana imani potofu kwamba wasichana wanaposema “hapana” wanamaanisha “ndiyo”. Hakuna

lililo la kweli kati ya haya.

Mwanaume wa kweli anajali na kumfikiria mtu mwingine. Husikiliza mwenzi wake anachosema na

hafanyi mzaha. Wavulana wanahitaji kujifunza kuamini yale wasichana wanayoyasema. Msichana

akisema “hapana” anamaanisha “hapana”. Msichana akisema “acha” mvulana lazima aache.

Regina kutoka uganda (umri wa miaka 15)

“Nilikuwa na rafiki wa kiume. Siku moja alinialika nyumbani

kwake kwa ajili ya chakula cha mchana. Nilipokwenda, nilimkuta

anashughulika kutengeneza chakula. Tulikula chakula

pamoja na kuosha vyombo. Nilimweleza kwamba ningependa

kuondoka, lakini alinisisitizia nikae kwa muda. Aliniambia

kwamba kulikuwa na sinema moja nzuri sana; kwa kweli

ilikuwa ni nzuri na inavutia. Lakini katikati ya sinema aliniomba

nimbusu na kujaribu kunilazimisha tujamiiane. Lakini

nilikataa. Nilimwambia siwezi na kumwomba aniache, ama

sivyo ningepiga kelele ya kuomba msaada. Alihofu sana na

akaniacha. Nilimwambia kwamba, kwasababu ya tabia yake

urafiki wetu umekwisha”.

Kila mtu anaweza kujifunza jinsi ya kupunguza uwezekano wa kubakwa. Kama ni msichana

au mvulana, kitu cha muhimu zaidi ni kuamini hisia zako. Kwa mfano, kama mtu anakufanya

ukose raha au anakutishia, zingatia hisia zako na zifanyie kazi. Mwache huyo mtu au ondoka

katika mazingira hayo mara moja, hata kama hakuna sababu iliyowazi ya kukufanya ukose raha.

Unaweza ukawa unapata dalili zenye hila ambazo ni ishara muhimu za kukuonya. Kamwe usipuuze

hisia hizi. Zisikilize hisia zako na uzifanyie kazi.

SURA YA 12 | NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO

Njia Nyingine za kujilinda dhidi ya ubakaji:

Usikae peke yako na mtu usiyemjua na kumwamini. Ukienda kutembea fuatana na kikundi

cha marafiki na kaa na kikundi hicho.

Usiende au kuendelea kukaa nyumbani

kwa mtu kama hakuna mtu mwingine.

Usiende sehemu za upweke ambako

hakuna watu wengine jirani.

Iwapo katika eneo lenu watu wanabakwa

sana, beba mchanganyiko wa mchanga

au pilipili iliyosagwa ili uweze kumtupia

machoni mtu anayekusumbua.

Kama una matembezi, hakikisha (wazazi

marafiki, shangazi, mjomba) wanajua

unakokwenda na muda unaotegemea

kurudi.

Kuwa jasiri na kusema “HAPANA” kwa

Ijue mipaka yako. Kabla hujaenda

sauti na kwa nguvu

kwenye miadi yako, fikiria kile

unachotaka kukifanya na kile ambacho hutaki kukifanya. Usijaribu kufikiria wakati tayari

upo na rafiki yako na mnakumbatiana na kubusiana.

Kuwa mwazi kuhusu mipaka yako. Ikiwa hutaki kujamiiana mweleze rafiki yako bila kuficha,

hasa uhusiano unapoanza ili kuhakikisha kwamba wote mna mategemeo yanayofanana.

Unapotoka kwa ajili ya miadi; hakikisha unazo pesa za kwako ili uweze kurudi nyumbani

kama miadi itageuka kuwa michungu.

Gawana gharama na rafiki yako. Usimwache akafikiri anakudai ngono kama malipo ya pesa

alizotumia kwa ajili yako.

Usinywe pombe wala dawa za kulevya. Pombe na dawa za kulevya zinaweza kukufanya

ushindwe kuwa mwazi kuhusu mipaka yako. Unaweza kushindwa kujimudu.

Usikubali kinywaji kutoka kwa mtu usiyemjua na usiache kinywaji chako unapokwenda

chooni kwa sababu mtu anaweza kuweka dawa za kulevya ndani ya kinywaji chako.

Kama umetoka na rafiki yako naye akaanza kukushinikiza, kataa kwa nguvu. Usimwachie

mwanya wowote wa yeye kudhani unamaanisha ndio wakati unaposema hapana. Sema

kwa nguvu na kwa sauti kubwa na mwangalie moja kwa moja machoni. Usitabasamu wala

usiangalie pembeni kwa aibu. Usimwonyeshe rafiki yako alama ya kuwa unataka ushawishike

au kubembelezwa.

Iwapo upo katika hali mbaya na kuna mtu anajaribu kukuzidi nguvu unaweza kupigana naye,

bila kujali jinsia na ukubwa wa umbo. Unazo nguvu na akili ya kupigana. Tumia kila ulichonacho

kujilinda. Piga ukelele mkubwa kwa mfululizo kuomba msaada.

153

154

Njia za kujilinda ni pamoja na:

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Silaha nzuri uliyonayo ni vidole vyako na kucha. Mchome kwa nguvu kwa kutumia vidole

ndani ya macho ya mshambuliaji. Usihofu kumuumiza. Alikuwa na nia ya kukuumiza.

Tumia goti kumpiga teke la nguvu kwenye sehemu za siri. Iwapo utatumia nguvu, ataumia

sana na kumsababishia maumivu mara mbili.

Iwapo mtu huyo yuko juu yako na anausukumiza uso chini kwenye ardhi, tumia kisigino

kumpiga teke kwenye mifupa ya chini ya mgongo, juu kidogo ya matako.

Iwapo unazidiwa nguvu, tulia, jaribu kumdanganya mshambuliaji kwa kumshikashika. Halafu

mchome machoni au piga mapumbu. Kimbia mara mbakaji atakapotulia kidogo kwa sababu

ya maumivu.

Kitu cha KuFanYa ubaKaji uKitOKea

Wakati mwingine pamoja na jitihada zote za kujaribu kujitetea ubakaji unatokea, msichana au

mvulana anaweza kuzidiwa nguvu na mshambuliaji na ukashindwa kujinasua. Hii ni hali mbaya

sana, kwa hiyo ni muhimu kujua cha kufanya baada ya hapo.

Ubakaji ukitokea kwako au kwa mtu unayemfahamu, haya ndiyo unatakiwa kufanya:

Tumia nguvu zako zote kumsukuma na kupigana

Pata huduma ya matibabu haraka iwezekenavyo. Lazima upime vipimo kuhakikisha kwamba

upo salama na kwamba majeraha yote yanatibiwa.

Mwombe mzazi, shangazi, mdogo wako au rafiki wa karibu akusindikize kliniki / hospitalini

au polisi ili ukapate msaada. Mtafute mtu ambaye ana nguvu, anajali na anategemewa.

Mtu unayemwamini na ambaye hatasema kwa watu wengine.

Usioge kabla ya kwenda kutibiwa. Ingawa wazo la kwanza la mtu ni kuoga vizuri, siyo vizuri

kufanya hivyo. Watalaamu wanashauri kwamba mtu aliyebakwa asinawe hata mikono yake

kwa sababu inaweza kuharibu ushahidi (uchafu, shahawa, majimaji ya mwili, nywele n.k.)

ambavyo vingetumika kuhakikisha kwamba ubakaji umetokea na ni nani aliyefanya hivyo.

SURA YA 12 | NGONO YA KULAZIMISHWA NA NGONO BILA YA RIDHAA YAKO

Vaa au weka ndani ya sanduku, nguo zilizovaliwa wakati ubakaji unatokea. Nguo hizi

zitatumika kama ushahidi kuhakikisha kwamba ubakaji umetokea.

Jaribu kumtafuta mhudumu wa afya ambaye ni wa jinsi yako akuchunguze mara utakapofika

kituo cha afya. Iwapo wewe ni msichana mwombe mhudumu msichana akuchunguze.

Mhudumu anatakiwa achunguze kama kuna mikato, michaniko au michubuko. Na anaweza

kuchukua sampuli ya shahawa ukeni.

Omba dawa za dharura za kuzuia mimba (angalia Sura ya 11 kwa taarifa zaidi kuhusu

kuzuia mimba kwa dharura). Omba vilevile upime vipimo vya magonjwa ya ngono na VVU.

Kipimo cha VVU utahitajika kukirudia baada ya miezi 3 hadi 6 ili kuhakikisha maambukizo

hayajatokea. (angalia Sura ya 10 kwa taarifa zaidi kuhusu VVU na magonjwa mengine ya

zinaa).

Mwombe mhudumu wa afya aandike kila kitu anachokiona. Taarifa hii inaweza kusaidia

kuhakikisha kwamba ulibakwa.

Mwombe mhudumu wa afya akushauri wapi uende kutoa taarifa ya kubakwa. Iwapo

mhudumu wa afya hajui, nenda kwenye kituo cha vijana au kikundi cha wanawake. Waombe

ushauri namna ya kutoa taarifa kuhusu ubakaji na wapi unaweza kupata ushauri wa kisheria

kama unataka kumshitaki mbakaji.

Iwapo unataka kutoa taarifa kuhusu ubakaji fanya hivyo mapema iwezekanavyo. Nchi nyingi

zimeweka sheria na adhabu kali kwa mtu atakayepatikana na kosa la kubaka. Ukiamua kutoa

taarifa polisi au kwa viongozi wa kijiji, fanya hivyo bila kuchelewa. Unahitaji kuwa jasiri kutoa

taarifa ya ubakaji kwa sababu inaumiza na kuhuzunisha kuzungumzia yaliyotokea lakini

lazima utoe taarifa hiyo. Usipofanya hivyo ataondoka na kuwa huru na anaweza kumuumiza

mtu mwingine.

Pata nasaha. Lazima umpate mtu wa kuzungumza naye kuhusu hisia zako za hofu, huzuni,

hasira na maumivu. Mtaalamu wa nasaha anaweza kukusaidia kuchambua hisia zako ili uweze

kuendelea na maisha yako ya kila siku.

Ni muhimu kujua kwamba katika nchi nyingi ni kosa mwanamke kutoa mimba ambayo ni matokeo

ya kubakwa. Iwapo unafikiri kwamba umepata mimba, zungumza na mhudumu wa afya au waone

kikundi cha akina mama ili kujua uchaguzi ulionao.

Inaweza ikakuchukua muda mrefu kupona kimwili na kihisia baada ya kubakwa. Kuwa mvumilivu.

Jambo la muhimu zaidi usijilaumu au kufikiria uliwajibika kwa ubakaji huo. Halikuwa kosa lako.

155

156

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 12

ngono ya kulazimishwa na ngono bila ridhaa yako

Ngono isiyotakiwa ni hatari; inakuweka katika uwezekano mkubwa wa kupata mimba

isiyotakiwa na magonjwa ya zinaa na VVU/UKIMWI. Inaweza kuwa mbaya vilevile kwa afya

ya hisia zako. Inaumiza sana na kuleta kiwewe ukijamiiana bila ya ridhaa yako.

Ngono isiyotakiwa inajumuisha mambo mengi tofauti. Inaweza ikawa:

Kushikwa au kuguswa kijinsia bila ya ridhaa yako. Hii ni kunyanyaswa kijinsia.

Matusi ya kijinsia yasiyotakiwa ni udhalilishaji kijinsia.

Kulazimishwa ngono; huu ni ubakaji. Mbakaji anaweza akawa mgeni kabisa, lakini

kawaida ni watu ambao wanafahamika kwa anayebakwa – kama rafiki wa kiume, rafiki,

jirani au ndugu.

Njia nzuri ya kujilinda ni kujifunza jinsi ya kugundua na kuepuka mazingira ambayo utakuwa

hatarini kulazimishwa ngono:

Epuka uhusiano na watu wazima. Uhusiano huu unakuweka katika uwezekano mkubwa

wa kupata magonjwa ya ngono na mimba kwa sababu uhusiano huu hauna usawa.

Unaweza usiwe na nguvu ya kusema “hapana” ukiombwa ngono au kumlazimisha mtu

mzima atumie kondomu.

Amini hisia zako. Iwapo kuna mtu anakufanya ujisikie vibaya au uwe mwenye wasiwasi,

mwache mtu huyo mara moja. Hisia zako ni ishara muhimu, usizipuuzie.

Usije hata siku moja ukawa peke yako na mtu ambaye humwelewi vizuri na kumwamini.

Usiende nyumbani kwa mtu kama hakuna mtu mwingine. Fuatana na kundi la marafiki na

kaa nalo.

Jua mipaka yako na hakikisha rafiki yako wa kiume au wa kike anaielewa mipaka hiyo.

Usiwaruhusu watu wengine wakupatie zawadi au watumie pesa kwa ajili yako kwa

sababu wanaweza kukuomba urudishe msaada huo kwa kufanya nao ngono.

Usinywe pombe au kutumia dawa za kulevya.

Kuwa jasiri, usiwachanganye watu kwamba unaposema hapana unamaanisha ndio.

Usitoe ishara yoyote kwamba unataka kushawishiwa na kubembelezwa kwanza.

Wakati mwingine ubakaji unatokea licha ya mtu kujitahidi kujilinda. Iwapo hili litatokea,

unahitaji kupata matibabu na ushauri moja kwa moja. Mhudumu wa afya anaweza kukupatia

dawa ya dharura ya kuzuia mimba. Usioge kwanza kwa sababu itakuwa vigumu kuhakikisha

kwamba ulibakwa. Tunza nguo ulizokuwa umevaa wakati ubakaji unatokea.

Jambo la muhimu zaidi, usijilaumu. Halikuwa kosa lako. Jipe muda wa kupona kimwili na

kihisia.

Matumizi mabaya ya dawa

Mara nyingine watu hutumia dawa na viini kadhaa ambavyo haviponyi magonjwa. Dawa hizi

zinabadili jinsi mtu anavyojisikia na anavyofikiri. Zinaweza kumfanya mtu awe mcheshi zaidi,

mwerevu, mpole, jasiri na anayefurahisha kuwa naye. Dawa hizi zinaweza kumfanya mtu asiwe

mwoga na asifadhaike. Lakini hisia hizi zinadumu kwa muda mfupi sana na hivyo kutumia dawa

kama njia ya kujifurahisha na kufanikisha mambo yako ni hatari sana. Kutumia dawa kwa njia hii

kunaitwa “matumizi mabaya ya dawa.”

Matumizi mabaya ya dawa ni tatizo kubwa linalotukabili. Dawa zingine kama pombe na sigara ni

sehemu katika maisha yetu ya kila siku kiasi kwamba hatufikirii kama ni dawa za kulevya. Lakini

pombe na sigara ni dawa za kulevya na mara nyingi watu wanazitumia vibaya.

Dawa zinadhuru akili yako, mwili wako, na uhusiano wako na watu wengine. Zinaweza kukufanya

mgonjwa na usipate mafanikio katika maisha yako yote. Zinaweza kusababisha ufanye

vibaya shuleni, upoteze marafiki na ukosane na wazazi wako. Zitakufanya utumie pesa yote

utakayofanikiwa kuipata.

Dawa zinaweza kufanya iwe vigumu kwako kufanikisha mpango wa kufanya ngono salama.

Wakati wote unatakiwa kuwa makini kuhusu ngono. Unahitaji kuwa na uwezo wa kusema “Hakuna

kujamiiana, hakuna kabisa”.; au “ninataka busu tu na sitaki kujamiiana,” au “nitatumia kondomu

tu.” Dawa zinafanya ubongo usifanye kazi vizuri. Zinaweza kukufanya ufanye mambo ya hatari

kama kufanya ngono isiyo salama. Kutokana na hiyo unaweza ukaishia kupata magonjwa ya zinaa

pamoja na VVU/UKIMWI. Unaweza ukaishia kupata mimba au kumpa mimba msichana.

aina Ya DaWa na Vitu aMbaVYO VinatuMiKa VibaYa

Kuna aina nyingi za dawa zinazotumiwa vibaya na watu.

Zinaweza zikasababisha matatizo ya kweli. Zifuatazo ni baadhi tu ya dawa zinazojulikana na

baadhi ya matatizo yanayoweza kukupata.

Marijuana ambayo majina yake kadhaa ni bangi, hashi, poti, majani, gugu, acapulco gold au

fimbo ya thai. Dawa zote hizi zinatokana na mimea. Kwa kawaida watu wanavuta majani lakini

mara nyingine ipo dawa ya nguvu zaidi inayotengenezwa kutokana na mashina ya mimea.

157

SURA YA 13

158

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Bangi inaweza kumfanya mtu ajisikie ameburudika na kufurahi, au inaweza kumfanya mtu ajisikie

kutetemeka sana na kuogopa. Kuvuta bangi kunaweza kusababisha macho yawe mekundu,

midomo na koo kuwa mikavu na hamu ya kula kuongezeka. Unaweza kujisikia usingizi, na

wasiwasi wako kutoweka katika muda ambao ulevi umekolea. Lakini ujue utashindwa kufanya

uamuzi hata ule ulio mdogo!

Kuvuta sana na matumizi ya muda mrefu ya bangi yana madhara kwenye mapafu na yanaweza

kusababisha saratani. Uvutaji unaweza vilevile kuathiri kumbukumbu na uwezo wa kuwa makini

na kuelewa mambo. Inawezekana kuwa vigumu kuendelea na masomo au kuwa na maendeleo

mazuri ya kazi kwa sababu kumbukumbu na usikivu vinakuwa vimepungua.

Khat, gat, miraa au mirungi ni aina ya jani linalotafunwa maeneo ya pembezoni mwa Afrika na

karibu Afrika ya Mashariki yote. Hii ni dawa maarufu sana katika baadhi ya jumuia kwa sababu

inafanya ujisikie kuwa macho zaidi, mwenye nguvu na mwenye kujiamini. Vilevile, inapunguza

njaa. Athari mbaya za kutafuna jani hili ni pamoja na kuwa na wasiwasi, uchokozi, uhanithi (kama

mwanaume hawezi kusimamisha uume) na maono ya vitu

ambavyo havipo.

Petroli, gundi, rangi, tina na bidhaa za viwandani

zinazowekwa kwenye makopo ya kupuliza. Mara nyingine

zinavutwa ili kujiweka katika hali ya ulevi. Vitu hivyo vinaweza

kufanya ujisikie joto, njaa kidogo, hupunguza woga na

kukufanya mwenye furaha angalau kwa muda. Baada ya kuvuta

vitu hivyo, unajisikia usingizi na unajiona haupo kabisa kwenye

mazingira yanayokuzunguka. Kwa kuwa vitu hivyo ni rahisi sana

kununua, vinakuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa mitaani.

Dawa hizi zinaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika.

Unaweza kupoteza mwelekeo na ukachanganyikiwa na

usiweze kudhibiti hatari zinazokuzunguka. Kwa hiyo, unaweza

kugongwa na gari kwasababu utashindwa vitu rahisi kama

kuvuka barabara.

Kuvuta kwa muda mrefu kunaweza kusababisha ukakosa

fahamu (kuzimia au kufariki), kukabwa roho (kushindwa

kupumua) na kifo. Matumizi ya mara kwa mara ya vitu hivi

yanaweza kukuharibu mapafu, ubongo na viungo vingine

muhimu vya mwili.

Dawa za kutuliza ni pamoja na valiumu na mandraksi: Dawa

hizi zinaweza kukufanya ujisikie mwenye usingizi au kama

umepumzika vile na uko shwari. Zinapunguza mapigo ya moyo na kupunguza kupumua.Ukizidisha

zinaweza kukuua kwa haraka na kiurahisi.

Dawa zenye kuleta njozi, kama “angel dust,” LSD (pia yanaitwa tindikali, mchemraba wa sukari,

dragoni na magugu yanayoua). Dawa hizi zinaweza kukufanya uhisi mambo ambayo hayapo.

Dawa hizi zinasababisha kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kupoteza usingizi na kupandisha

joto la mwili. Mtumiaji anaweza pia kuwa na wasiwasi, tabia ya vurugu, mfadhaiko na wazimu

(ugonjwa wa akili usiotibika.) Wakati uko katika hali ya ulevi kwa sababu ya dawa na unahisi

kwamba unaweza ukajiumiza. Matumizi ya muda mrefu yanaweza kuleta matatizo ya kupoteza

kumbukumbu, na ukizidisha zinaweza kusababisha kutetemeka, kupoteza fahamu na hatimaye

kifo.

“Dawa kali” (narcotics) zikijumuisha dawa kama heroini (pia inaitwa junki, sukari ya kahawia

na smak) na kokeini (inaitwa koki, crak na barafu). Katika Bara la Afrika dawa kali ni matatizo

makubwa, na watu wengi wanazitumia. Mara nyingi zinatumika kwa kujidunga sindano inayoenda

moja kwa moja kwenye mishipa ya damu. Dawa hizi ni rahisi sana kuzizoea mwilini. Ukianza

kuzitumia inaweza ikakuwia vigumu kuziacha. Watu ambao wamezizoea wanaona kana kwamba

hawawezi kuishi bila dawa hizo.

Dawa hizi zimepigwa marufuku kabisa, na ili kuzipata shurti ufuatane na watu ambao wanavunja

sheria. Dawa hizi ni ghali sana hivyo watu wengine wanaozitumia wanaanza kuiba fedha ili

wapate fedha ya kutosha kuweza kuzinunua. Watu wengine wanauza miili yao ili kupata fedha

ya kutosha kununua dawa hizi. Watu wengine wanaotumia dawa hizi hutumia sindano kwa

kujichoma ili waweze kuzizoea mwilini. Wale wanaochangia sindano wana hatari kubwa ya kupata

mambukizo ya VVU.

SiGaRa na POMbe

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

Watu wengi wanapofikiria dawa za kulevya huwa hawaorodheshi pombe na sigara. Hata hivyo,

pombe na sigara mara nyingi vinatumiwa vibaya kama dawa nyingine za kulevya na zina athari

zake.

tumbaku, sigara (vilevile zinaitwa, dragis, batis, na fegi) na “mitemba”. Nikotini ni kiambato

kichochezi katika tumbaku, sigara na mitemba. Nikotini haikufanyi ujisikie uko juujuu kama ilivyo

bangi au pombe na wala haiharibu uwezo wako wa kuamua. Inaweza kukufanya ujisikie mwenye

nguvu nyingi na inapunguza hamu yako ya kula.

Hatari moja kubwa ya nikotini ni kwamba inazoeleka sana mwilini. Umewahi kuona wavutaji

wakitaka kuacha kuvuta?. Wanakuwa wanyonge, hawawezi kulala au kuunganisha mawazo,

wanaudhika upesi na wanakuwa na hasira na wasiwasi. Kujisikia kwa namna hii kunaudhi kiasi

kwamba watu wengi wanashindwa kuacha kuvuta na wanajaribu tena na tena kabla ya kufanikiwa

kuiacha tabia hii.

Siyo tu kwamba nikotini inazoeleka sana mwilini bali pia ni hatari kwa afya yako.Uvutaji

umeonekana kusababisha matatizo mengi ikiwa ni pamoja na saratani ya koo, ulimi, mapafu,

matiti na utumbo mkubwa. Uvutaji unaharibu moyo na mishipa ya damu katika mwili na inaweza

kuleta hatari ya kupata shinikizo la damu, kiharusi na ugonjwa wa moyo.

Pia uvutaji sigara umeonekana kusababisha uhanithi kwa wanaume. Hii ni kwa sababu uvutaji

unaharibu mishipa ya damu katika uume kama unavyoharibu mishipa ya damu mingine mwilini.

Pombe ni dawa ya kulevya maarufu sana Afrika na kwa kweli dunia nzima. Tofauti na dawa

zingine za kulevya, pombe imehalalishwa kisheria na inapatikana kwa aina mbalimbali na kwa bei

ndogo.Kwa hiyo pombe ni dawa ya kulevya ambayo kuna uwezekano wa kukumbana nayo. Mara

nyingi ndani ya nyumba, mmoja wa wazazi wako au wote wanaweza wakawa wanakunywa pombe.

Inaweza ikawa rahisi kwako kuipata na haitaonekana kama kitu cha kutisha kwa sababu ni kitu

cha kawaida katika jamii.

159

160

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ni rahisi kuanza kunywa pombe na usiifikirie sana kuhusu jambo hilo. Lakini fikiria tena! Pombe

ni dawa ya kulevya kama dawa nyingine za kulevya. Pombe inadumaza mfumo wa mwili. Baada

ya kunywa pombe kidogo, matendo yako yanaweza yakawa ya taratibu na inaweza ikakuwia

vigumu kufikiri vizuri. Ukiongeza kidogo tena, unashindwa kusema vizuri na unaweza kuwa mkali

na mchokozi. Kama siyo mzoefu wa pombe au kama unakunywa sana unaweza kutapika sana au

ukapoteza fahamu.

Athari za muda mrefu za unywaji sana pombe ni mbaya. Nadhani unawafahamu watu katika

jamii ambao ni walevi sana na ambao hawawezi kuishi bila kunywa. Unaweza ukawa umeona jinsi

inavyoharibu familia, watu kupoteza kazi, na inasababisha afya kuwa mbaya, kama kuharibu

ubongo na kuleta ugonjwa wa ini.

Pombe ni dawa ya kulevya maarufu sana

ambayo inawafanya watu wastarehe na

kusahau taabu zao. Hata hivyo, kujiona

umestarehe mno na kutojitambua si jambo

zuri kwani kunaweza kukufanya upate

matatizo.

Pombe kama ilivyo kwa dawa nyingine za

kubadili hali ya mtu, inaondoa uwezo wa

kujizuia na mambo unayoona yatakutia aibu

mbele ya wenzio. Pombe inakupa ujasiri wa

kuzungumza mambo ambayo baadaye utakuja

yajutia.

Kwa mfano, wasichana wengi wakiwa

hawajanywa hawana ujasiri wa kwenda kwa

mwanaume na kumbusu kwenye mdomo lakini

msichana akiwa amekunywa pombe anaweza

kujisikia huru sana; anajisikia kumbusu

mvulana na anafanya hivyo.

Pombe inaweza pia kumfanya mvulana afanye

vitu ambavyo kwa kawaida asingelifanya. Kwa

mfano, mvulana anaweza akaamua kutaka

kujamiiana na msichana baada ya kunywa

pombe. Hata kama rafiki yake wa kike anataka

au hataki, anaweza kujaribu kumlazimisha

kujamiiana naye. Pombe inamfanya asiweze

kumfikiria rafiki yake wa kike anavyojisikia;

inamfanya pia asiweze kufikiria matokeo ya

jambo analotaka kutenda.

Unapokunywa pombe, sheria zinazotawala

tabia yako ya kawaida zinapungua. Uwezo

wako wa kuamua mambo mazuri unapungua.

Kwa hiyo, unapoteza uwezo wa kupima

mambo. Kijana mmoja anasema haya kuhusu

pombe:

Pombe inaathiri uwezo wako wa kufanya

uamuzi salama

lazarus kutoka Zambia (umri wa miaka 15)

“Ninapokunywa ninasahau hatari zote zinazonizunguka. Ninasahau kila

kitu kuhusu kondomu. Hivyo huwa ninafanya ngono bila kinga kwa sababu

ya kishawishi cha pombe. Ninajua nina uwezekano wa kuambukizwa.”

Iwapo kinywaji cha kawaida kama pombe kinaweza kukuletea matatizo makubwa kama hayo,

hebu fikiria kinachoweza kutokea kama ukitumia dawa kali zaidi kama kokeni.

KutaWaliWa na DaWa

Kadiri mtu anavyoanza mapema kutumia dawa, ndivyo anavyojiwekea nafasi ya kujenga matatizo

makubwa yanayohusiana na dawa baadaye. Athari za dawa nyingi zinaongezeka kadiri muda

unavyopita. Athari zinajijenga mwilini, kama bomu lililotegwa kwa muda maalumu likisubiri muda

ufike lilipuke.

Kuna dalili nyingi zinazojitokeza matumizi ya dawa zinapofikia kuwa matatizo makubwa.

Dalili hizo ni:-

Je, unajua kwamba matumizi ya dawa za kulevya zina matatizo ya kipekee kwa

wanawake na wasichana?

Wakati dawa za kulevya zote zina madhara mwilini, nyingi zinawaathiri zaidi wanawake

na wasichana kuliko wanaume. Kwa mfano, kuvuta sigara kunaleta madhara ya pekee kwa

wanawake. Kunaweza:

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

Kuleta matatizo ya kiafya kama mwanamke anatumia vidonge vya kuzuia mimba.

Kupunguza miaka ya mwanamke ya kuzaa watoto kwa sababu tukio la hedhi kukoma

litatokea mapema

Kuongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya mlango wa mfuko wa kizazi na tumbo

la uzazi.

Kusababisha mifupa ya mwanamke kuwa dhaifu.

Kusababisha iwe vigumu kwa mwanamke kupata mimba.

Kuongeza hatari ya mimba kutoka kwa mwanamke mjamzito.

Kufanya mwanamke azae mtoto mdogo sana au mtoto azaliwe mapema kabla ya wakati.

Kumeza dawa na kunywa pombe wakati mwanamke ana mimba ni hatari kwa sababu inaweza

kusababisha matatizo makubwa ya kiafya na ya mtoto kuzaliwa na kasoro, kama kuundwa

vibaya kwa moyo, mifupa, kichwa na viungo muhimu vya ndani. Mtoto pia anaweza kuzaliwa

na uzito mdogo, kukua taratibu na kutokuwa na uwezo wa kujifunza darasani. Matumizi

mabaya ya dawa wakati wa ujauzito yanaweza kusababisha uzae mtoto ambaye tayari

ameathirika na dawa na hivyo kuzoeleka mwilini mwake.

Kumbuka, ukiwa unatumia dawa wakati wa ujauzito, mtoto wako pia anapata kiwango

kikubwa kuliko wewe. Athari kwa mtoto zitakuwa kubwa zaidi kuliko kwako.

Kuongopa kuhusu kiasi cha dawa unachotumia. Hii ni pamoja na kujidanganya mwenyewe

kiasi gani cha dawa au pombe unayotumia.

161

162

Kuficha dawa ili watu wengine wasizione.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kuwa na matatizo ya fedha kwa sababu zote zimetumika kwa dawa.

Kujiaibisha mwenyewe na wengine hadharani kwa kufanya vitendo vya aibu.

Iwapo wewe au mtu yeyote unayemfahamu anaanza kuacha kufanya mambo anayoyapenda,

anatumia muda kidogo kwenye kazi za shuleni, anakwepa kuwajibika, anataka sherehe na

anataka kupigana baada ya kunywa au akiwa amelewa basi matumizi ya dawa yanamfanya aingie

katika matatizo makubwa na anahitaji asaidiwe ili aache au unahitaji kusaidiwa ili uache.

irinne kutoka Zambia (umri wa miaka 16)

“Rafiki yangu alikuwa anatumia dawa, na dawa zikamzoea

mwilini. Hakuwa anaweza kukaa hata saa moja bila kuzitumia.

Alizizoea hadi wakati fulani akizikosa alikuwa anapigana hovyo

na ndugu zake na majirani.”

Moja ya matatizo makubwa ya kutumia dawa ni mwili kutawaliwa

na dawa hizo. Mwili unapozoea dawa hizo inabidi uzitegemee ili

uweze kufanya kazi za kila siku. Dalili za mwili kuzoea dawa ni

pamoja na:

Kujisikia kana kwamba dawa ni muhimu ili kukamilisha siku.

Kutaka zaidi na zaidi dawa ili uweze kujisikia ipasavyo.

Kuanza kuona mabadiliko mabovu ya tabia kama vile hasira,

wasiwasi, vurugu za ghafla.

Kupoteza fahamu (kuzimia) baada ya kuzitumia.

Salome kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Mmoja wa marafiki zangu ambaye alizoea

kutumia dawa aliugua sana. Pua yake ilikuwa

inatoa damu wakati wowote. Mara nyingine

alikuwa anaanguka chini.”

Mara mwili unapokuwa umetawaliwa na dawa, unahitaji zaidi na zaidi dawa hizo ili uweze

kujisikia vizuri. Hii ni gharama na inaharibu mwili wako. Kwa dawa kali kama kokeini na heroini,

mara zinapozoeleka mwilini, ukizikosa unaugua sana. Ukiacha kutumia, moja kwa moja, utapata

dalili zisizopendeza, kama kutetemeka, kichefuchefu, kutapika, maumivu na shida katika kupata

usingizi na kula. Hali hii inaweza ikawa mbaya kiasi kwamba utataka kurudia tena kutumia dawa

hizo.

Dalili hizi za kujisikia vibaya zinaitwa “dalili za kujitoa”. Ni hisia za mwili kutokana na dawa

kuondolewa mwilini. Kwa sababu mwili wako umekuwa tegemezi kwa dawa hizi, mwili unaugua

kwa kukosa dawa hizo.

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

julia kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Niliacha kutumia dawa rafiki yangu mpenzi aliponishauri kuhusu

hatari za dawa. Mara ya kwanza nilidharau, lakini baada ya muda

nilijaribu kujidhibiti mwenyewe. Niliambiwa na rafiki yangu nisizitumie

kwa wiki moja, lakini nilimweleza nisingaliweza bila dawa

hizo. Hata hivyo, namshukuru Mungu kwamba wiki nzima sikuzitumia

na sasa najua naweza kuishi bila dawa hizo.”

Kuyashinda mazoea ni vigumu sana na watu tofauti wanao uzoefu tofauti. Watu wengine wana

uwezo wa kuacha kutumia dawa mara moja. Watu wengine wanahitaji kuacha taratibu, kwa

kupunguza kiwango cha kutumia. Hii inasaidia kuulinda mwili kutokana na mshituko wa kuacha

ghafla. Kuacha kidogo kidogo kunasaidia kuruhusu mwili kuanza kujitoa kwenye dawa.

Omari kutoka tanzania (umri wa miaka 18) “

Niliacha kutumia dawa baada ya kushuhudia athari zinazotokana

na kujihusisha katika kutumia dawa. Baadhi ya marafiki zangu

wamefariki kutokana na maambukizo ya kifua au maradhi mengine.

Ilibidi niende kupata ushauri dhidi ya dawa na kwa kufanya

hivyo nimeweza kuacha.”

Kushinda utegemezi wa dawa za kulevya kunahitaji nguvu kubwa na dhamira, ujasiri na

uamuzi thabiti. Kuna wakati ambapo utajisikia kama vile huwezi. Kwa hiyo ni jambo muhimu

kutafuta msaada na kuungwa mkono. Zungumza na mshauri wa vijana au mhudumu wa afya

kuangalia kama kuna msaada wa vikundi au mpango unaoweza kujiunga nao. Jambo la muhimu

zaidi usishirikiane na watu ambao watakurudisha nyuma. Usishirikiane na watu ambao

hawatakusaidia kuacha tabia yako.

KWa nini Watu WanaanZa KutuMia DaWa?

Njia iliyo wazi na sahihi ya kuepuka kupata matatizo ya kutawaliwa na dawa ni kutokuanza

kutumia dawa kabisa. Kwa hiyo, ni vizuri kuelewa ni kwa nini watu wanaanza kutumia dawa, ili

uwe mwangalifu na kuhakikisha kuwa kamwe huangukii katika mitego hiyo.

Kuna sababu nyingi zinazowafanya vijana kuanza kutumia dawa kama

kokeini na heroini au hizi zilizozoeleka kama pombe na sigara:

Kwanza, vijana wengi wanatumia dawa kwa sababu wenzao

wa rika moja wanafanya hivyo na kwa sababu

wanataka kuonekana sawa katika kundi.

Makundi mengine yanatumia dawa

kama sehemu ya utambulisho wa kundi

lao. Kama unataka kuwa sehemu ya

kundi, unaweza kupata msukumo wa

kutumia dawa kama wanayotumia

wenzako.

163

164

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Wenzako wanaweza kukuomba ujaribu kutumia dawa na kudharau athari zake. Wanaweza

wakakasirika au wakakutukana kama hujaribishi kuvuta.

Margaret kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Nilikuwa na miaka 13 nilipoanza kutumia dawa. Marafiki zangu

walianza kuvuta bangi. Waliniambia nivute pafu moja tu, lakini

nilikataa. Wakaanza kunicheka, na kwa vile sikutaka kuambiwa

kuwa ni mwoga, niliamua kuvuta pafu moja.”

Pili, wengi wanatumia dawa kwa sababu wanataka kukwepa matatizo katika maisha yao.

Labda waligombana na wazazi wao au pengine marafiki wamewaumiza kihisia. Wanaweza kuwa

wanajisikia wenye huzuni, wasiwasi au wamezidiwa na matatizo. Dawa zinaweza kuonekana

kama njia rahisi ya kuepukana na matatizo.

Marion kutoka Zimbabwe (umri wa

miaka 17)

“Baadhi ya marafiki zangu walianza

kutumia dawa kwa sababu ya

matatizo nyumbani au nje.”

Francis kutoka uganda (umri wa

miaka 15)

“Baadhi ya marafiki zangu

wamepoteza wazazi wao kutokana

na UKIMWI na wanatumia dawa

kusahau matatizo yao.”

tatu, wengine wanatumia dawa za kulevya kwa sababu

wanataka waonekane tofauti na vile walivyo. Vijana

wengi hawajisikii ni wazuri vya kutosha kama walivyo.

Wanataka wawe na ujasiri wa ajabu, waongee kwa sauti ya

juu, waonekane wanavutia na wamekua. Dawa zinaweza

kuwafanya wawe watu tofauti.

juma kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Ninao marafiki ambao wanatumia dawa kila wakati, kama

dawa zinazoathiri akili na bangi. Wanatumia dawa hizi ili

wajisikie watu wazima na bora kuliko wenzao. Lakini dawa hizi

zimewasababishia wasizingatie kazi zao, ndoto, malengo na

tamaa zao za baadaye.”

nne, watu wengine wanafikiri dawa zitawafanya wapate ujasiri wa kufanya mambo ambayo

wanaogopa kuyafanya. Kuna mazingira mengi katika maisha yanayohitaji ujasiri. Unaweza

ukawa mwoga kuongea darasani au unaweza kuwa mwoga kumwendea msichana au mvulana

unayempenda. Dawa zinaweza kuonekana kama njia rahisi kuushinda woga huu.

tano, vijana wengine wanaamini kuwa dawa zitawafanya wawe werevu zaidi. Wanafikiri dawa

zitawasaidia wakae macho ili waweze kujisomea kwa muda mrefu na vizuri

Sita, vijana wengi wanatumia dawa kwa sababu ya kuchoshwa na maisha. Wanataka kuwa na

furaha na hawajui kitu gani kingine kitawafurahisha.

Saba, vijana wengine wanatumia dawa kwa sababu wamepoteza matumaini. Hawajisikii kama

wana mpango wa maisha ya baadaye. Wanatumia dawa kwa sababu wanajiona kana kwamba

hawajali kitakachowatokea.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za baadhi ya vijana kutumia dawa za kulevya. Lakini hakuna sababu

hata moja inayothibitisha uhalali wa matumizi ya dawa. Kutumia dawa ni njia mbaya ya kutatua

matatizo. Dawa zinafanya matatizo kuwa magumu zaidi. Ujana ni kazi ngumu, na kuna mambo

mengi ungetaka kufanikisha unapokuwa kijana shuleni na nje ya shule. Unahitaji kujifunza namna

ya kuvumilia matatizo, namna ya kushughulikia hisia zako, namna ya kuwa na urafiki usio na

madhara, namna ya kushughulikia mabadiliko ya mwili wako. Orodha ya mambo unayopaswa

kuyashinda au kuyaweza wakati wa ujana wako haina mwisho.

Tatizo la dawa ni kwamba zinaweza kuingilia utaratibu wako mzima wa kupata stadi na utaalamu.

Zinakusimamisha kujifunza namna ya kuvumilia mfadhaiko wa kila siku. Zinakuzuia kujifunza

stadi za maisha utakazozihitaji utakapokuwa mtu mzima.

Kumbuka:

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

Huhitaji dawa ili upendwe na watu.

Huhitaji dawa kuwa jasiri na shupavu.

Huhitaji dawa ili kumudu huzuni au maudhi.

Maryann kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Rafiki yangu Katty aliambiwa na msichana mwingine kwamba

akivuta bangi anaweza kumuuliza mwalimu maswali magumu ambayo

hawezi kuyajibu. Lakini mambo yalimgeukia Katty upande

mwingine. Akaanza kushindwa kuyamudu masomo. Sasa hivi ni

mtu aliyekata tamaa na kuacha shule. Angependa apewe nafasi

tena kurudia shule lakini baba yake hataki kusikia habari hizo.

Anasema kwamba alishindwa alipopewa fursa.”

Unaweza ukaishi bila dawa na pombe. Ndani yako unazo nguvu na nyenzo za ndani za

kushughulikia hali na matatizo yoyote yale. Unahitaji kutafuta nguvu za ziada ndani yako ili

kushinda tatizo hili.

Kwa tatizo lolote unaloliona, msaada unaweza kupatikana. Unaweza kuzungumza na mshauri

wako, mwalimu unayemwamini au mtu katika kanisa lako au msikiti wako. Zungumza na wazazi,

shangazi au mjomba, kaka mkubwa au dada au rafiki unayemwamini. Msaada unapatikana

ukiutafuta.

165

166

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

naMna Ya KuShuGhuliKia ShiniKiZO la KutuMia DaWa

Kumudu shinikizo kutoka kwenye kundirika linalotaka utumie dawa kama wao ni vigumu sana.

Hapa kuna hadithi fupi ya kijana mmoja:-

Je, maelezo haya yanakukumbusha wewe pia hali ambayo imewahi kukutokea ukiwa na wenzako?

Hawa marafiki walikuwa wanahitaji sana Jeckton avute. Kwa nini walimshinikiza?

Watu wengi wanataka kuungwa mkono wanapofanya jambo wanalofikiri siyo sahihi. Wanafikiri

makosa yao yanakuwa madogo kama mtu mwingine anafanya nao. Marafiki zao wanapofanya

jambo la kijasiri pamoja nao, hawajisikii kuogopa sana kuhusu hatari iliyopo. Kama wako katika

kikundi wanajisikia kustarehe na kufurahia burudani wanazozipata kwenye dawa. Ndiyo maana

watakushinikiza sana wewe.

Hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kushughulikia hali hiyo:

jeckton kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Nilipokuwa na miaka 13, nilikuwa naelekea nyumbani nikiwa na

baadhi ya marafiki zangu. Tulipita sehemu ambayo marafiki zangu

mara nyingine wanaenda kukutana na baadhi ya marafiki zao.

Tulipofika pale waliwakuta marafiki zao na wakapewa kifurushi

cha bangi. Bila kupita muda, msichana mmoja akaanza kuvuta

na akaniambia nivute pafu moja. Nilikataa, wakaanza kunicheka.

Waliniita majina mabaya na wakaniambia niache kuwaaibisha.

Waliniambia ilikuwa tamu sana na ingenifanya nijisikie vizuri. Kwa

sababu sikutaka waelewe kwamba nilikuwa naogopa, niliamua kuvuta

kidogo. Baada ya kuvuta kidogo, siwezi kusema yaliyotokea

baada ya hapo maana sikumbuki tena. Nilichanganyikiwa kwa

muda wa karibu siku tatu.”

Kumbuka kwamba huhitaji kumfanya rafiki ajisikie vizuri kwa kumuunga mkono kufanya

mambo ambayo siyo mazuri kwako.

Kama ni rafiki wa kweli, unaweza kumwambia rafiki yako kuwa mambo anayoyafanya ni ya

hatari.

Uwe mwazi kwa wenzio kwamba hutaki kutumia dawa au kitu. Waonyeshe rafiki zako

kwamba unazijua akili zako zilivyo na kwamba hata wakikusihi vipi hutabadilisha mawazo

yako.

Ondoka kama rafiki yako anazidi kukushinikiza au anaanza kukutukana ama kukucheka.

Usiendelee kujadili suala hilo zaidi. Subiri hadi atakapokuwa hatumii dawa ndiyo mwanze

kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Kofi kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Huwa nashinikizwa na marafiki zangu kutumia dawa za kulevya

ninapokuwa nao, lakini ninajizuia mwenyewe na kuwaeleza kwa

ujasiri kabisa kwamba nimeridhika bila ya kutumia dawa.”

Mara nyingine tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kuliko kukataa shinikizo toka kwa marafiki.

Unaweza kugundua kwamba rafiki yako analo tatizo kubwa la dawa au pombe, tatizo ambalo

unaona linamharibia maisha yake. Hili nalo ni gumu kulitatua. Haya ni mambo machache

unayoweza kufanya:

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

Zungumza na rafiki yako kuhusu matumizi ya dawa wakati hajanywa au hayuko katika hali ya

ulevi.

Usimlaumu au kumkosoa rafiki yako. Hii itazua mabishano baina yenu. Badala yake lenga

katika matatizo ya dawa na mwonyeshe rafiki yako kwamba unaogopa. Jaribu kumsaidia

rafiki yako aelewe kwamba ana matatizo.

Jaribu kumsaidia rafiki yako apate msaada na jaribu kumsaidia akwepe sehemu ambayo

atapata shinikizo la kutumia dawa au pombe.

Margaret kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Wengi wa marafiki zangu walikuwa wameshaharibiwa na dawa;

lakini baada ya kujua hatari na ukweli kuhusu dawa niliamua kuwasaidia

marafiki zangu. Wengi wamebadilika na mimi ninafurahi.”

Wakati mwingine watu wenye matatizo kutokana na dawa hawako tayari kukusikiliza wewe na

ushauri wako. Wanaweza kuzikataa juhudi zako za kusaidia na wanaweza kukukasirikia. Mnaweza

mkaishia kuwa na mabishano makali na rafiki zako, lakini angalau dhamira yako itakuwa wazi na

utakuwa umejitahidi kuwasaidia.

Wakati wote upo uwezekano wa urafiki kuvunjika kutokana na tabia yako ya kutokubaliana na

tabia zao.

hanifa kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Nilikuwa na rafiki ambaye nilimwamini sana kwa kipindi kirefu,

lakini sikujua mambo aliyokuwa anayafanya kwa kificho. Siku

moja nilimkuta na watu wenye sura za ajabu, macho yake yalikuwa

mekundu. Niligundua alikuwa ananuka bangi. Nilijaribu kuzungumza

naye mara kwa mara lakini hakunisikiliza. Hivyo nilimtaka

achague ama kuacha kutumia alichokuwa anatumia au kuacha

kuzungumza na mimi. Nilifikiri angefanya uamuzi sahihi lakini

nilikuwa nimekosea aliacha kuzungumza na mimi.”

Inaweza kuwa vigumu sana kumpoteza rafiki lakini angalau ulisimama kwenye kanuni zako,

ulijaribu kumsaidia rafiki na wewe binafsi hukujihusisha na hatari ya dawa. Mara chache, baada

ya muda, rafiki atabadilika.

hanifa kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Baada ya miezi kadhaa, rafiki yangu aligundua madhara ya dawa

hizo kwa maisha yake, na akaniomba tuendelee kuwa marafiki

tena. Kwa sababu nilimwonea huruma nilikubali.”

167

168

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kama una wasiwasi kuhusu rafiki yako, jaribu kumsaidia lakini kama rafiki anakataa msaada

wako urafiki hautadumu, usijilaumu. Ulifanya jambo ulilopaswa kwa kadiri ulivyoweza.

Kuacha DaWa

Vijana wengi wanakua katika mazingira ambayo yanazungukwa na aina mbalimbali za dawa

za kulevya. Lakini siyo kila kijana katika sehemu hizi anajihusisha na dawa hizo. Wengine

wanajihusisha, baadhi hawajihusishi. Wengi wanakataa dawa na shinikizo kutoka kundirika kwa

sababu wanayaona matatizo yanayoletwa na dawa za kulevya. Vijana hawa wana msimamo,

wanafikiri wakati wote, na wanajitegemea. Wanakaa kimya, safi na wanafanya mambo

wanayoyaona mazuri kwao.

anthony kutoka Zambia (umri wa miaka 16)

“Nafikiri vijana wanapaswa kujishughulisha na mambo wanayoyapenda

na siyo kukaa bila shughuli kwasababu ubongo

usioshughulishwa ni karakana ya kufikiri maovu. Wanatakiwa

kuwakwepa marafiki wabaya na makundi mabaya. Vilevile, ni

vizuri kwa afya yako kukaa mbali na dawa za kulevya.”

Prisca kutoka Kenya (umri wa miaka 14)

“Yakwepe makundi mabaya yanayotumia dawa na jihusishe na

shughuli za vijana.”

Dawa na pombe zipo tele kila mahali na zinaweza kuwa rahisi kupatikana. Lakini kuwepo

kwa dawa haimanishi kwamba ni lazima uzitumie. Unaweza kuwa mtulivu, fanya mambo yako

mwenyewe na kaa mbali na dawa za kulevya.

Kuwa thabiti. Jitazame kwa uaminifu kujijua wewe ni nani na jinsi unavyotaka uendeshe maisha

yako. Jua kipi ni muhimu kwako, na malengo yako ya baadaye ni yapi na utayapataje malengo

hayo? Fikiria wapi dawa na pombe vinaingia katika mipango yako. Je, vitakusaidia ufanikishe

mipango yako ya baadaye au vitakuzuia?

Vifuatavyo ni vidokezo kutoka kwa vijana kuhusu namna ya kuepukana na dawa:

• Jishughulishe: Jihusishe katika shughuli mbalimbali kama vile michezo au vikundi vya sanaa.

Shughuli hizo zitachukua muda wa kukaa bure na zitakufanya ujisikie vizuri. Hutachoshwa na

hutahitaji kutafuta dawa za kulevya kama kiburudisho.

• Kuwa tofauti: Usitumie dawa ili ufanane na makundi. Kuwa mwenyewe. Fanya yale

yanayokupendeza.

• Jiheshimu: Usitumie dawa za kulevya au pombe kwa ajili ya kufurahisha watu wengine au

kupata ujasiri wa kufanya kitu. Jiheshimu na watu wengine watakuheshimu. Na ukishajua

watu wanakuheshimu utapata ujasiri kwa lolote unalotaka kufanya.

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

• Tafuta kukubalika kwenye manufaa: Kuna njia nyingi za kujisikia umekubalika na unapendwa

na watu wengine. Kuna njia nyingi zinazokubalika kuliko kutumia dawa au pombe. Jiunge

na makundi ya watu waliokusudia kufanya jambo fulani, kama kuimba, michezo, maigizo,

kusoma au kusafisha maeneo ya jirani. Tafuta watu watakaokupenda vile ulivyo. Tafuta nini

unaweza kufanya. Tafuta watu ambao hawapotezi muda wao kubwia dawa.

• Jithamini:

Tambua thamani yako. Itetee thamani hiyo.

• Kuwa na nia ya kufanikiwa katika mambo yako: Je, nini ndoto zako? Tazama maisha yako ya

baadaye na ona wapi unataka kwenda. Dawa hazitakusaidia kwenda unakotaka kufika.

• Tumia kila chembe hai ndani ya ubongo wako: Usiruhusu chembe hai za ubongo wako

zikauawa na dawa za kulevya. Soma kwa bidii na fanya vizuri katika kazi zako za shuleni.

• Pata msaada wa kitaalamu: Kama unapata shinikizo la kutumia dawa, nenda kazungumze

na mshauri wa vijana.Pata msaada kama unafikiria unalo tatizo la dawa. Jaribu kutafuta

mshauri na matibabu. Hujachelewa sana kuacha kutumia dawa za kulevya hata kama

umekuwa unatumia muda mrefu. Msaada unapatikana lakini unatakiwa kuchukua hatua ya

kwanza kuutafuta msaada huo.

169

170

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 13

Matumizi Mabaya ya Dawa

Kutumia dawa bila sababu za kiafya na kupata hali ya aina fulani kunaitwa matumizi

mabaya ya dawa. Kuna aina nyingi za dawa na vitu vinavyotumika vibaya kama bangi,

miraa, petroli, gundi na dawa kali kama kokeini na heroini. Pombe na sigara nazo pia ni

dawa na mara nyingi zinatumika vibaya.

Dawa zinaweza kuwa na athari nyingi zenye kuleta madhara. Matumizi ya dawa hufanya

mwili uzoee hali ambayo huwezi kufanya chochote bila ya kuzitumia. Dawa pia zinaweza

kuharibu ubongo wako, moyo, mishipa ya damu, na mapafu. Matumizi ya dawa wakati wa

ujauzito yanaweza kuleta matatizo makubwa kwa mtoto.

Vilevile dawa zinaweza kusababisha matatizo mengine. Dawa nyingi zinaweza kukufanya

usifikiri vizuri na usiwe na uamuzi mzuri. Kutokana na hilo, unaweza kuwa hatarini kupata

matatizo ya muda mrefu. Unaweza kufanya ngono bila kinga na kuishia kupata mimba

zisizotakiwa au kumpa msichana mimba na magonjwa ya zinaa kama VVU/UKIMWI.

Zipo sababu nyingi zinazowafanya vijana watumie dawa:

Kujumuika na kundirika.

Kuyakimbia matatizo.

Kuishinda huzuni.

Kujaribu kujibadilisha walivyo ili kuonekana tofauti.

Kutafuta ujasiri wa kuhimili hali ngumu au changamoto.

Kujifurahisha.

Kumudu hali ya kupoteza matumaini.

Hakuna hata sababu moja ambayo ni nzuri ili kuhalalisha matumizi ya dawa. Dawa

zitafanya matatizo yako kuwa magumu zaidi.Unaweza wakati wote kuyavumilia matatizo

bila kuwa na dawa ndani yako. Una utashi wa kuyashughulikia matatizo au hali yoyote ile.

Dawa zinaweza zikaharibu maisha yako ya baadaye. achana na dawa na jishughulishe.

Jihusishe na michezo na mambo mengine ya jumuia. Hutahitaji kutafuta tena furaha au

burudani kutokana na dawa. Kuwa tofauti. Usifanye jambo la hatari ili ulingane na wenzio.

Jiamini na fanya kilicho sahihi kwako. Kama unajiheshimu watu wengine watakuheshimu

pia.

Kama unapata msukumo wa kutumia dawa au kama unafikiri una tatizo la dawa, pata

msaada. Dawa ni kitu chenye nguvu. Usijaribu kupigana na dawa peke yako. Msaada upo

wakati wote, lakini unapaswa kuchukua hatua ya kwanza ya kuomba msaada.

Kutimiza ndoto zako

Kila mtu anazo ndoto za maisha yake ya baadaye, ndoto za kufanya jambo kubwa na kuwa mtu

muhimu na aliyefanikiwa. Ndoto hizi zinaonyesha lengo la kupata kitu fulani. Haya ni malengo

yetu na matamanio yetu. Ni maono tuliyonayo kwa ajili yetu wenyewe na kwa ajili ya maisha ya

baadaye.

Zifuatazo ni baadhi ya ndoto chache za vijana balehe:

Sherifa kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Ninataka kuwa bibi shamba na ninataka kuwa mtu maarufu.”

Omari kutoka tanzania (umri wa miaka 18)

“Ningependa niwe mtu ambaye watu wanakuja kwangu kwa ushauri,

mtu mwenye ndoa imara na pengine kazi kama meneja ofisini.”

naana kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Ninataka kuwa daktari, hususani kushughulikia wanawake na watoto.”

Patrick kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Ninafikiria kuwa na shamba dogo

la mifugo lenye ardhi ya kutosha ili

wazazi wangu wakae huko pamoja

na mimi. Ningependa niwe na mke na

nipate watoto watatu.”

Milensu kutoka Zambia (umri wa miaka

13)

“Ninafikiria kuwa na nyumba yangu

mjini ikiwa na sofa sebuleni. Ninataka

kuwa muuguzi, niwe na kliniki yangu na

niheshimiwe na jamii yangu.”

171

SURA YA 14

172

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ndoto yako ni nini? Ungependa uwe nani? Unajifikiriaje mwenyewe katika miaka mitano ijayo?

Katika miaka15? Utakuwa nani na utakuwa unafanya nini?

Sura hii inahusu kutimiza ndoto zako. Inahusu kuzifikiria ndoto zako na kutafakari ni kwa vipi

unaweza kuzifikia. Inahusu kufanya uamuzi mzuri wa busara na utakaokufikisha karibu na ndoto

zako. Aidha, inahusu namna ya kumudu vipingamizi vitakavyojitokeza katika maisha.

Si jambo rahisi kufanikisha ndoto. Inahitaji kufanya kazi kwa bidii na kuwa na dhamira/nia. Kwa

hiyo, jambo muhimu ni kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii. Fanya vitendo! Usikae chini na

kusubiri mambo yakutokee. Unatakiwa kuyajenga maisha yako ya baadaye.

KuZitaMbua nDOtO ZaKO.

Watu wengine wana ndoto nyingi sana na zinabadilika kila wakati. Kwa mfano mchukue Remijia

wa Tanzania:

Alipokuwa na miaka 6 alitaka kuwa ofisa wa polisi.

Alipokuwa na miaka 8 alitaka kuwa kapteni wa meli.

Alipokuwa na miaka 10 alitaka kuwa rubani wa ndege.

Alipokuwa na miaka 13 alitaka kuwa mwalimu.

Sasa ana miaka 19 anataka kuwa mhandisi.

Kwa nini ndoto hubadilikabadilika? Je, ni vibaya kuwa na ndoto nyingi

zilizo tofauti? Hapana! Ndoto ni nzuri, zinatia hamasa na zinakufanya

ufanye kazi kwa bidii. Zinakufanya uangalie maisha ya baadaye na

uwe na mipango thabiti.

Watu wengine wanaelekea kuwa na ndoto chache. Hawajui

wangependa wawe nani wakiwa wakubwa. Wanapata shida kujifikiria

watakuwa vipi miaka 5 ijayo.

Kama yanakugusa, usihofu. Hili ni jambo la kawaida! Haina maana

kuwa huna ndoto, bali ina maana kuwa bado hujafikiria ndoto zako ni

zipi. Lakini, unaweza kuanza sasa kuzitambua ndoto zako.

Ndoto za watu wengi zinaathiriwa na watu wanaowazunguka. Kwa

hiyo, kwanza angalia unazungukwa na nini. Fikiria kuhusu watu

walio ndani ya jamii. Ni nani unaowahusudu? Ni watu gani

unaowaheshimu? Mtu anaweza kuwa mwalimu

ambaye anajua majibu ya maswali yote

yanayoulizwa. Anaweza kuwa ni daktari

ambaye alijua kilichokuwa kinakufanya

uumwe miezi michache iliyopita.

Anaweza akawa mchungaji wa kanisa

lako. Wanaweza kuwa wazazi wako.

Pata muda wa kutafakari ndoto zako za baadaye

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Pili, usiruhusu ndoto zako zikakwamishwa na mambo unayoyaona. Angalia hata nje ya jumuia

yako. Kuna mtu ambaye umemsoma kwenye gazeti au kitabuni ambaye alifanya jambo ambalo

linakushangaza? Pengine ni mwanasayansi ambaye anajifunza jinsi tembo wanavyowasiliana wao

kwa wao. Pengine ni muuguzi anayewahudumia wakimbizi katikati ya uwanja wa vita. Wapo watu

wengi wanaofanya mambo mengi mazuri yanayovutia na yenye manufaa na maisha yao. Watu

hawa wanaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa. Wanaweza kukuanzishia ndoto kuhusu maisha

yako ya baadaye.

Tatu, yaruhusu mawazo yako “yapae angani” usijiwekee mipaka ya vitu ambavyo unaweza

kufanya au ambavyo huwezi kuvifanya. Kwa mfano, usiiache ndoto kwa sababu ya mawazo

yaliyopitwa na wakati, kama mawazo kuhusu kazi wanazoweza kufanya wanaume pekee au

wanawake pekee. Mambo yanaenda yakibadilika. Wanawake siku hizi wanafanya kazi ambazo

mama zao hawakuwahi kufikiria kuzifanya. Sasa hivi wanawake wanaweza kuwa wahandisi,

marubani, madaktari, wanariadha, wanasayansi, maprofesa, wanaanga, Marais, waandishi wa

habari n.k. Kama ni mvulana au msichana, unaweza kuwa mtu unayetaka kuwa, ikiwa utadhamiria

na kufanya kazi kwa bidii.

MiPanGO Ya baaDaYe KuhuSu KaZi

Vijana balehe wachache wana vipaji vya ziada katika taaluma fulani, kama hisabati, muziki au

kuchora. Utafikiri kipaji kimewachagua. Wanakuwa wataalamu wazuri wa hisabati, wasanii,

walimu na viongozi wa kwaya au wasanifu majengo.

Watu wengine wanapendelea kitu kimoja tangu utoto wao, na mvuto huo mkubwa unarahisisha

sana wakati wa kutoa uamuzi kuhusu watakuwa nani. Unaweza kumsikia mzazi akisema “wakati

wote tulijua kwamba John atakuwa mganga wa mifugo. Alianza kuwahudumia wanyama wadogo

alipokuwa na umri wa miaka minne tu.

Watu kama hawa, maisha yao yanaonekana kuwa rahisi. Inaonekana kana kwamba njia yao ya

kazi imenyooka. Uamuzi wao unaonekana kuwa ni rahisi kwa sababu wanajua kabisa wanataka

kufanya nini, na wanacho kipaji katika eneo hilo maalumu.

Wengi hatuko hivyo. Wengi ni watu wa kawaida, wenye akili ambao tunaweza kufanya vizuri

katika mambo tofauti. Uwezekano wa kuwa nani au kufanya nini ni matokeo ya mchanganyiko wa

yale tunayoyapenda na tusiyoyapenda, uwezo wetu na utayari wa kufanya kazi kwa bidii na fursa

tunazopata.

Kufanikisha ndoto kwa watu wengi ni njia ndefu yenye kona nyingi. Wakati wote siyo moja kwa

moja na hatua sahihi za kuchukua haziko wazi. Zaidi ya hapo vikwazo visivyotegemewa vinaweza

kujitokeza njiani. Ni mambo ambayo yanatakiwa kushughulikiwa kwa makini sana.

Jitahidi kujitokeza kwenye kazi nyingi iwezekanavyo. Bila kufanya hivyo huwezi kufahamu nafasi

gani zipo duniani kwa ajili yako? Katika nchi nyingine, vijana balehe wanajitolea kufanya kazi

katika mashirika mbalimbali wakati wa likizo. Wakati mwingine wanapata malipo kidogo ya

kutosha usafiri kwenda na kutoka nyumbani. Lakini mara nyingi hawapati chochote. Wanajitolea

tu.

Usifikiri kwamba kwa vile jambo fulani siyo la shule na siyo la kazi ya kulipwa basi halina

thamani. Iwapo unaweza kupata kazi ya kujitolea, pengine unaweza kupata uzoefu mzuri na

wenye manufaa.

173

174

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kwa mfano unaweza kupata fursa ya kuona jinsi utaratibu wa kazi za ofisini zinavyokuwa na

utaweza kupata hisia nzuri kuhusu kazi wanazozifanya. Unaweza kujua kwamba kazi hiyo

inakufaa au haikufai. Kwa vyovyote itakavyokuwa, uvumbuzi utakuwa muhimu. Kwa jinsi

utakavyokuwa unaendelea utajifunza stadi mpya, utajenga mvuto mpya na utajiamini.

Unapofikiria kuhusu aina ya kazi ambayo ungependa kufanya, vilevile fikiria kuhusu hatua

utakazozichukua. Kwa mfano, fikiria kuhusu watu wenye sifa nzuri uliowachagua. Unafikiri

walifanya nini hadi kufikia hapo walipo? Walihitaji aina gani ya elimu? Aina gani ya mafunzo kwa

vitendo waliyapata?

Njia bora ya kujua namna gani watu walivyofikia hapo walipo ni kuwauliza. Iwapo wapo watu

ambao unawaheshimu na ambao mafanikio yao unayahusudu, waulize kama wanao muda

wakuambie jinsi walivyofikia pale walipo. Kabla hamjakutana, andika orodha ya maswali ambayo

ungependa kuwauliza, Kwa mfano; ni kitu gani kilisababisha kuchagua kazi wanayoifanya na ni

aina gani ya elimu na mafunzo waliyapata. Wanapenda nini zaidi kuhusu kazi yao? Ni kitu gani

hawakipendi?n.k.

Watu wengi wanafurahi sana na kujisikia sifa wakati mtu mwingine anavutiwa na mafanikio yake

na pale wanapoombwa ushauri. Kawaida watu watakuwa na shauku ya kukueleza habari zao na

kukusaidia njia utakayochagua. Unahitaji ujasiri kumwendea mtu mzima ambaye humjui vizuri,

lakini utashangaa wengi wao watakuwa wazuri na watakusaidia, wanaweza kukushauri jinsi ya

kupanga kazi yako.

KuWeKa MalenGO

Ni vema kuweka malengo, mambo unayoyategemea kwa maisha ya baadaye. Vilevile, unahitaji

kujiwekea malengo mahususi ambayo yanaweza kukamilishwa katika muda mfupi.

Lengo ni kuwa na jambo unalotaka kulifanyia kazi. Kuna aina mbili za malengo. Malengo ya muda

mfupi na mrefu. Ndoto zako ni malengo ya muda mrefu. Haya ni mambo unayoyawazia kutokea

baadaye katika muda mrefu.Malengo ya muda mfupi ni mambo ya muda mfupi. Ni mambo

yatakayotokea kesho, juma lijalo au mwaka kesho. Malengo ya muda mfupi ya baadhi ya vijana

balehe ni haya yafuatayo:-

Sofia kutoka uganda (umri wa miaka 14)

“ Itakapofikia mwisho wa mwaka wa kwanza wa sekondari,

ninataka kushika namba za juu, nusu ya darasa.”

essie kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Nitakapofikia umri wa miaka 16 ninataka kujua jinsi ya kutumia

kompyuta.”

Francis kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Mwakani ninataka kupiga solo katika kwaya ya kanisa”.

Miriam kutoka Zambia (umri wa miaka 16)

“Ninataka kufanya vizuri katika mitihani yangu ili niandikishwe

katika shule nitakayoichagua.”

Patrick kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 18)

“Ninataka kujifunza jinsi ya kuzungumza mbele ya kadamnasi.”

Una malengo gani? Ni mambo gani ambayo ungependa kuyafanya ifikapo mwisho wa mwaka

huu? Je, mwisho wa mwaka ujao?

Malengo yana manufaa sana. Unapokamilisha lengo

unaweza kulifuta kwenye orodha. Inakupa hisia ya mafanikio

na furaha ya kukamilisha jambo. Inakufanya ujisikie

vizuri. Inakuonyesha kwamba unapofikiria kitu unaweza

kufanikisha.

Malengo yanatakiwa yawe halisi na ambayo yanawezekana

kutekelezeka- mambo ambayo unaweza kufanikisha. Wakati

mwingine watu huweka malengo ambayo si halisi, kama vile

kuwa tajiri sana. Watu wengi hawawi matajiri na hata wale

wanaokuwa matajiri pengine walikuwa na malengo halisi

kama vile kuanza biashara zao. Waliendesha biashara kwa

muda mrefu kiasi cha kufanikiwa sana.

Wakati mwingine watu wanaweka malengo yasiyofaa,

mathalani kuhusu mambo ya kufanya mapenzi. Vijana balehe

wengine wanajiambia:

“Likizo hii lazima nipoteze ubikira wangu.”

“Lazima nijamiiane nikifikisha umri wa miaka 16”

Nitajaribu kujamiiana na msichana mwingine zaidi ya rafiki yangu wa kike.”

Malengo kama haya hayana manufaa. Ukiyafanikisha pengine hutajisikia vizuri. Hebu fikiria:

Hivi kweli kujamiiana ndilo lengo lako? Je, umeweka lengo hili kwa sababu tu unapata shinikizo

ili usiwapoteze marafiki? Je, unafikiri marafiki zako wote wanajamiiana, hivyo wewe unabaki

nyuma? Hizi siyo sababu nzuri za kujiwekea malengo.

Fikiria kile ambacho wewe mwenyewe unataka kufanikiwa na weka maanani mwongozo huu wa

kuweka malengo:-

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Hakikisha malengo yako ni mazuri na yana manufaa.

Hakikisha malengo ni halisi na yanatekelezeka.

Hakikisha hayakuingizi katika hatari yoyote

Hakikisha ni malengo yako wewe na siyo ya mtu mwingine.

Ukifanikisha lengo utajisikia vizuri

175

176

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Baada ya kuyatambua malengo yako, fikiria jinsi utakavyoyafanikisha. Weka mpango mzuri

mwenyewe. Halafu jiulize maswali haya manne:

Kwa nini? Ni sababu gani zinakufanya uwe na lengo hili?. Kwa nini unataka kulifanikisha?

namna gani? Hatua gani utakazozichukua kufanikisha lengo hili? Utafanya nini?

lini? Utamaliza lini kila hatua uliyoiweka katika kufanikisha lengo? Utafanikisha lengo lako lini?

nini? Utahitaji nini ili kufanikisha lengo lako?

Kwa mfano: Tuchukulie labda unataka kufanya vizuri zaidi katika somo la Hisabati. Kwa nini

unataka kufanya vizuri zaidi? Pengine ni kwa sababu unajua unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko

ulivyowahi kufanya siku za nyuma. Unafaulu sana katika masomo mengine isipokuwa Hisabati.

Una akili, na wala huhitaji kusoma sana ili ufanye vizuri masomo mengine. Hata hivyo, unaona

Hisabati ni ngumu zaidi.

ni kwa namna gani utaboresha alama zako

za Hisabati? Labda utaanza kufanya marudio

zaidi, kwa kupata msaada wa ziada baada

ya masomo na baada ya mazoezi ya maswali

zaidi.

lini utachukua hatua zote hizi? Labda

utaamua kutumia saa moja nzima kila siku

kujifunza Hisabati baada ya kutoka shule na

saa mbili siku za mwisho wa wiki.

utahitaji nini kikusaidie uboreshe alama

katika Hisabati? Labda unahitaji muda zaidi.

Pengine huwa unamsaidia shangazi yako

shughuli za dukani kila siku jioni. Mweleze

shangazi yako kuhusu lengo lako na mwombe

kama anaweza kukuachia mapema ili uweze

kujisomea. Pengine unahitaji maswali mengi

ili ufanye mazoezi. Mwombe mwalimu wako

akupe maswali ya ziada ya kufanya nyumbani.

Ukipanga vizuri na kufanya kazi kwa bidii unaweza kutimiza malengo yako.

KuFanYa uaMuZi MZuRi (Wa buSaRa).

Panga mipango vizuri ili uweze kufikia

malengo na ndoto zako

Kufanya uamuzi mzuri kunaweza kukusaidia kutimiza malengo yako na hatimaye kufanikisha

ndoto zako. Uamuzi mzuri haimaanishi kuwa ukiwa na miaka 13 unaweza kufanya uamuzi sahihi

kuhusu utakuwa nani maishani mwako. Kufikiria utakuwa nani siyo uamuzi. Hiyo ni ndoto na ni

lengo la muda mrefu.

Kufanya uamuzi ni tofauti. Uamuzi ni uchaguzi kati ya njia moja au nyingine zinazowezekana

kutumika. Kufanya uamuzi ni kitendo cha kila siku. Utafanya mamia ya uamuzi mpaka ufikie

mafanikio ya ndoto zako.

Je, uende nyumbani baada ya masomo

ukajisomee au ubaki shuleni kucheza

na wenzako? Je, ukubali kujamiiana

na rafiki yako wa kike au usubiri?

Unatakiwa ufanye uamuzi wa busara

kila siku.

Mojawapo ya mambo muhimu katika

kufanya uamuzi ni kuangalia mbele

na kuona kitu gani kinaweza kutokea

iwapo utafanya kitu fulani. Tunaita

kutabiri matokeo yanayoweza kutokea.

Jinsi unavyoweza kutabiri matokeo

mapema ndivyo utakavyofanya

uamuzi mzuri utakaoleta matokeo

unayoyataka.

Kwa mfano, labda unataka kuamua

uende nyumbani kwa rafiki yako baada

ya kutoka shuleni. Iwapo utaenda

nyumbani kwao itasaidia kuimarisha

urafiki wenu kwa vile msichana

huyu anajulikana sana shuleni na

amewaalika wasichana wengi kwao.

Kwa muda mrefu umekuwa unataka

kuwa rafiki na kikundi hiki kwa hiyo

unafurahi sana kualikwa ili kupata

wasaa wa kuwa nao.

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

1.

2.

3.

4.

5.

6.

7.

Je, Unafahamu hatua muhimu za kuchukua

unapofanya uamuzi?

Fafanua tatizo, hali au suala ambalo unahitaji

kufanyiwa uamuzi.

Tambua uchaguzi wote wenye kuwezekana au

njia utakazotumia.

Fikiria matokeo ya kila utakalochagua.

Fikiria maadili na imani yako kuhusu

kinachostahili na ambacho hakistahili ni jambo

gani la kufanya linaloendana na maadili yako.

Fikiria jinsi uamuzi wako unavyoweza kuathiri

watu wengine.

Chagua jambo la kufanya ambalo kigezo chake ni

ufahamu wako, maadili, thamani, malezi ya kidini

na malengo yako.

Tathmini uamuzi wako na jinsi unavyojisikia amua

kama ulifikiria kwa uangalifu na chunguza tena ili

uweze kujisikia safi na uchaguzi ulioufanya.

Kwa upande mwingine, mama yako anaweza kukasirika kama ukienda bila ya kuomba ruhusa.

Zaidi ya hapo unakabiliwa na mtihani wiki ijayo na ulikuwa umeahidi ungeanza kujisomea

mapema. Ukienda nyumbani kwa huyu msichana, utakuwa na muda mfupi wa kujisomea kwa ajili

ya mitihani, na unaweza kupata maksi chache.

Toa uamuzi wako binafsi. Usiruhusu watu wengine wafanye kwa ajili yako.

177

178

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Uamuzi kama huu unaweza kuwa mgumu. Masomo yako na uhusiano mzuri na mama ni muhimu

kwako. Lakini wakati huohuo, unataka kuwa na urafiki na kikundi hiki cha wasichana. Hayo ni

muhimu kwako vilevile. Vyovyote vile, itabidi upime vipengele vyote na kuona ni kipi kizuri

kwako. Kitu gani kitakuwa kizuri kwa muda mrefu. Lolote utakaloamua hakikisha ni uamuzi wako.

Hakikisha unachagua jambo moja kwa sababu ndilo unalolitaka – siyo kwa sababu kuna mtu

anakulazimisha kufanya hivyo.

Mara kwa mara tathmini uamuzi wako na jinsi unavyojisikia kuhusu uamuzi huo. Je, unajisikia

kama uliyefanya uamuzi sahihi? Kama sio, utafanya nini ili uyabadilishe? Kwa mfano, labda

unaamua kuanza kujamiiana na rafiki yako wa kiume lakini unajua ulikuwa siyo uamuzi sahihi

kwako. Unahofu kubwa ya kupata mimba na kuwasikitisha wazazi. Unajua kwamba wewe na

rafiki yako wa kiume mngetumia dawa za kuzuia mimba lakini kitu ambacho kingefaa zaidi ni

kutojamiiana.

Uamuzi mwingine unaweza kubadilishwa. Kwa hiyo, ni muhimu kutathmini mara kwa mara.

Unaweza kuamua kuacha kujamiiana. Kamwe usiseme nimechelewa kufanya uamuzi mzuri.

ZinGatia bila KuYuMba KatiKa MalenGO na nDOtO ZaKO.

Wakati mwingine inakuwa vigumu kubaki umelenga katika makusudio au ndoto zako. Wakati

mwingine matokeo unayoyataka yanaonekana kuwa mbali na hayafikiki. Unaweza kuhisi

kushawishika kufurahia maisha sasa na kuacha maisha ya baadaye yawe yatakavyokuwa.

Unaweza kuamua kuacha kusoma kwa bidii, na

badala yake ukawa unafurahi na marafiki zako

tu.

Wakati mwingine watu wanaweza kukukatisha

tamaa. Wanaweza kukufanya ufikiri hutaweza

kufikia ndoto zako. Kwa mfano, vijana wengine

wanapata msukumo mkubwa wa kuoa au

kuolewa mapema na kuanza kuzaa watoto.

Vilevile inaweza kuwa vigumu kama unafuata

njia ambayo siyo ya kawaida - kufuatilia ndoto

ambayo iko tofauti na za rika lako. Inaweza kuwa

vigumu zaidi kama unafuatilia kazi ambayo watu

wengi wa jinsi yako hawapendi.

Simama imara katika ndoto yako.

usikubali kuyumbishwa

aromo kutoka uganda (umri wa miaka 19)

“Rafiki zangu mara kwa mara wananitania kwamba kazi ya uhandisi

na umakanika ni kazi ya wanaume na kwamba hakuna mwanaume

atakayenioa. Lakini ninataka kufika hapo na kuona itakavyokuwa.

Siwasikilizi na ninasoma kwa bidii. Mambo mengine yatafuata

baadaye.”

Sherry kutoka Ghana (umri wa miaka 19)

“Ninataka kuwa mhandisi sanifu majengo. Baba yangu ni mkandarasi

wa ujenzi na aliniambia ni fani nzuri. Jinsi Ghana inavyobadilika,

kutakuwa na ujenzi mwingi na fani hii itakuwa nzuri.

Lakini itakuwa vigumu kwa mwanamke pekee. Kutakuwa na ubaguzi.

Hata mjomba hakubaliani na jambo hili kwa sababu anasema

wanawake ni dhaifu. Anasema asingemwajiri mwanamke kama

angepata nafasi ya kuajiri. Ananishauri niende kusoma fani ya

uhasibu.”

Inaweza kuwa vigumu kuendelea na malengo yako wakati watu wengine wanakukatisha tamaa

na kukwambia huwezi kufanya kitu hicho. Vivyohivyo, ni ngumu kubakia na lengo wakati watu

wengine wanakwambia fanya upesi na uwe na furaha. Bila ya kujali watu wengine wanasema nini,

bakia mkweli na ndoto zako.

Iwapo watu watakwambia kwamba

huwezi kufanya kwa sababu ni

mwanamke au ni mwanaume, zidisha

kufanya kazi mara mbili ya ulivyozoea.

Unaweza kufanya kazi yoyote ambayo

akili yako inakutuma na unayoimudu.

Wanaume na wanawake wana uwezo

sawa wa kufanya kazi, hata kama

hawapewi nafasi sawa wakati wote.

Iwapo unashinikizwa na wazazi wako

uolewe au uoe au uache masomo

mapema, jaribu kupata ushauri kutoka

kwa mwalimu, shangazi, mjomba,

kiongozi wa jamii ama mtu mmoja kutoka

kanisani kwako au msikitini. Waombe watu hawa ushauri na uone kama wanaweza kukusaidia

uzungumze na wazazi kuhusu umuhimu wa elimu na mafunzo. Ndoto zako ni muhimu, na itakuwa

vigumu kuzifuatilia wakati unahudumia familia.

KuFanYa ViZuRi KatiKa MaSOMO Shuleni

Kufanya vizuri shuleni kunahitaji bidii na nia. Elimu ni ufunguo wa maisha. Welewa ni zawadi

nzuri zaidi ambayo unaweza kujipatia mwenyewe. Jaribu kubaki shuleni kwa muda mrefu

iwezekanavyo. Kila mwaka utapata ufahamu zaidi na stadi zaidi zitakazokusaidia ufanikishe

ndoto zako.

Vifuatavyo ni vidokezo vichache vya kukusaidia kufanya vizuri katika elimu:

Jiwekee utaratibu mzuri wa kufanya mambo yako.

Jiandae kwa ajili ya masomo. Usiache muda wa mazoezi ya masomo hadi dakika za mwisho.

Weka muda wa kujisomea

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Weka muda wa kujifurahisha na kupumzika. Kufanya kazi wakati wote bila ya kucheza

kunamfanya mtu achoke na asiwe mchangamfu. Kwa hiyo, kuwa mwangalifu kupanga muda

wa kujifurahisha, kufanya mazoezi na muda kwa ajili ya marafiki na familia.

Kula vizuri na pata muda wa kulala usingizi ili usisinzie darasani.

iwapo unashinikizwa kwamba uolewe “mapema”

zungumza na mtu mmoja kama mwalimu,

ambaye anaweza kukusaidia.

179

180

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Shiriki darasani. Hata kama unaona aibu, unahitaji kujifunza kuzungumza. Mwonyeshe mwalimu

wako kwamba unasikiliza kwa makini na unafanya kazi kwa bidii. Hii ni muhimu kwa wasichana.

Wasichana wengine wanaogopa kuongea darasani na wanawaacha wavulana peke yao

wasikilizwe.

Unajua jinsi ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya mitihani?

Katika shule nyingi, mambo mengi yanategemea matokeo ya mitihani, kama ilivyo Kidato cha

Nne na cha Sita. Hapa kuna vidokezo vichache vya namna ya kujiandaa kwa ajili ya mitihani:

Wasichana zungumzeni darasani msikae tu kimya na kuwaacha wavulana peke yao

wasikilizwe na mwalimu

Pitia tena madaftari kila siku kwa makini. Usisubiri mpaka siku ya mwisho.

Panga ratiba yako ya kila siku na kumbuka muda wa kufanya kazi za shule.

Andika muhtasari “tini” ili uweze kukumbuka vipengele muhimu siku ya mitihani.

Tumia muda wa ziada katika masomo yanayokushinda na jaribu kupitia marudio kwa

msaada wa mwalimu.

Ukianza kupata mfadhaiko, pumzika. Cheza michezo au soma kitabu cha hadithi. Karuke

kamba au nenda katembee ili kutuliza mishipa ya fahamu.

Kitu muhimu siku ya mtihani ni kutulia!

Fika kwenye chumba cha mtihani muda uliopangwa. Ukichelewa utakuwa na wasiwasi na

itakuwa vigumu kufikiri kwa makini.

Ukipewa karatasi za mtihani usifanye kitu chochote dakika chache za mwamzo. Acha

mapigo ya moyo wako yashuke kidogo kwa sababu ukirukia moja kwa moja kujibu maswali

unaweza kufanya makosa ya kijinga.

Soma maelezo na maswali kwa uangalifu mkubwa ili kuhakikisha umeelewa maswali.

Mtahini atakayesoma majibu yako ataangalia ni jinsi gani umetafsiri swali. Panga majibu

na weka hoja zako vizuri.

Anza kujibu maswali ambayo ni rahisi kwako. Hii itakuongezea hali ya kujiamini. Watahini

hawatakuadhibu kwa kutojibu maswali kwa mpangilio uliopo ili mradi umejibu maswali

vizuri na umeandika namba ya kila swali. Usianze na swali gumu kuliko yote kwani

litakufanya upoteze matumaini ya kujiamini. Pia, utapoteza muda mwingi kufikiria majibu.

Kuacha Shule.

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Unajua jinsi ya kujiandaa vizuri kwa ajili ya mitihani? (Endelea)

Usiangalie huku na huku unapofanya mtihani. Unaweza kupata wasiwasi na hofu ukiona

wanafunzi wenzako wanaandika haraka. Usitetemeke unapoona watahiniwa wengi

wanaomba karatasi za ziada. Walimu hawaangalii kiasi gani ulichoandika bali ni kwa

namna gani umelijibu swali na kwa jinsi gani mawazo ya majibu yako yalivyopangiliwa.

Watu wengine wanaandika upuuzi mtupu!

Kumbuka mwandiko ni muhimu uwe mzuri kwani mtahini anahitaji kusoma ulichoandika.

Baada ya mtihani, epuka kujadili majibu na wenzako. Ukizungumzia unaweza ukajikuta

unajihisi kwamba majibu yako siyo mazuri ya kutosha na hii haitakusaidia kujiandaa kwa

mitihani itakayofuata.

Utakapopata karatasi za majibu ziangalie kwa makini. Angalia maswali ambayo ulikosea

kujibu ili ujue wapi unatakiwa kufanya kazi kwa bidii. Fikiri kuhusu aina ya maswali

yanayokupa matatizo ili ujiandae vizuri zaidi safari ijayo. Usisahau kuangalia maswali uliyojibu

kiusahihi na kujipongeza kwa kazi nzuri.

Vijana balehe wengi wanalazimika kuacha shule kabla ya kumaliza masomo. Labda wazazi

hawana uwezo wa kuwalipia karo au pengine wanapata mimba kwa makosa na wanalazimika

kuacha shule.

Hali hizi ni ngumu, lakini haimaanishi kwamba utashindwa maisha sehemu nyingine. Itakubidi

kufikiria upya ndoto na malengo yako. Kama ni mbunifu na unayo maarifa unaweza kushinda

maisha. Usifikiri maisha yako sasa yamekwisha, ila:

• angalia watu wanaokuzunguka. Vijana wengine ambao hawapo shuleni wanazikamilisha vipi

ndoto zao? Wanafanya nini?

• angalia nafasi na rasilimali zilizopo kwa ajili yako. Hata kama huwezi kuendelea na shule,

zipo njia nyingine za kupata mafunzo mazuri. Kwa mfano, kama uliacha shule kwa sababu

ya mimba, tafuta kama kuna kituo cha akinamama ambako unaweza kwenda kwa ajili ya

mafunzo na kozi. Pengine kunaweza kuwa na mfuko wa mkopo kwa jamii wa kusaidia watu

kuanza miradi midogomidogo ya kuongeza kipato.

• Omba ushauri kwa watu. Kutoka kwa wazazi, mjomba, shangazi, majirani, viongozi ndani

ya jumuia au hata mwalimu wako wa zamani. Watu hawa wanaweza kuwa na maoni mazuri

kuhusu kazi au mambo ambayo ungeweza kuyafanya.

• Fikiria upya malengo yako na mikakati kwa ajili ya kuyatimiza. Labda haitawezekana

kuwa daktari, lakini kuna mambo chungu nzima ambayo unaweza kuyafanya vizuri. Unaweza

kuamua kuanzisha biashara ndogo. Je, utafanyaje? Labda unaweza kuunda kikundi na rafiki

zako. Mwombe kila mtu achangie kwenye mfuko wa pamoja utakaotumika kama pesa za

mtaji kwa ajili ya biashara. Pengine unaweza kuzungumza na wafanyabiashara wakupe

ushauri jinsi walivyofanikiwa na namna ya kuanza. Unaweza ukawaalika wawekezaji kwenye

biashara yako kama unaweza kuwashawishi kwamba ni wazo zuri.

181

182

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

• Kuwa mbunifu.

Kama rafiki zako wote wanauza magazeti mitaani au kwenye taa za

barabarani, unaweza kufikiria kuuza kitu kingine au kufanya jambo jingine. Kuungana nao

kuuza magazeti kunaweza kufanya usipate kipato cha kutosha ili kuweka akiba ya pesa ya

kuanzishia shughuli nyingine.

Kutatua ViPinGaMiZi

Kama upo shuleni au upo nje ya shule, siyo kila mara mambo yataenda kama ulivyopanga. Wakati

mwingine kizuizi kikubwa hutokea katika mchakato na kusababisha ugumu katika kufanikisha

malengo uliyojiwekea. Vizuizi hivi

vinasababisha ugumu na mara nyingine

vinakurudisha nyuma kabisa.

Unafahamu jinsi ya kuvikabili vipingamizi?

Vipingamizi vinaweza kuwa vigumu na

kukatisha tamaa, lakini vinatokea kwa

kila mtu. Jinsi utakavyochukulia vizuizi

vya maisha visivyoepukika ndivyo jinsi

vitaamua ni kwa namna gani utafanya

vizuri kuzifikia ndoto zako yawezekana

isiwe ile ndoto yako ya mwanzo lakini

ikawa ni ndoto nzuri pia.

Vipingamizi vinaweza kutokea kwa

sababu ya matukio yaliyo nje ya

uwezo wako – mambo ambayo huwezi

kuyadhibiti, kama vile mabadiliko

katika hali ya kiuchumi ya familia

yako. Pengine biashara ya baba yako

imeanguka au mama yako ameugua

na hivyo hawawezi kulipa karo. Jambo

kama hili likitokea itabidi utumie nguvu

zako zote ulizo nazo kupata ufumbuzi.

Je, yupo ndugu yeyote ambaye

anaweza kukusaidia kulipa karo? Je,

shule inaweza kukupunguzia karo kwa

sababu umekuwa mwanafunzi mzuri?

Je, unaweza kuhamia shule ambayo ni

nafuu kidogo?

Wakati mwingine unaweza kupata

vipingamizi ambavyo viko nje kabisa ya

uwezo wako. Labda zipo nafasi 20 za

Chuo Kikuu kwa wanafunzi wa wilaya

yako kusomea uhandisi. Ushindani ni

mkubwa mwaka huu. Wanafunzi 80

wanashindania nafasi hizo. Wewe ni wa

21 katika mitihani.

Unafahamu jinsi ya kuvikabili vizuizi? Wakati

wote Tom alitaka kuwa daktari. Lakini vita

vilitokea katika eneo lake alipokuwa na umri

wa miaka 15, na hakufanya mitihani. Hatimaye

alipofanya hakuweza kumudu kununua kitabu cha

Kemia na ilibidi asome muhtasari “tini”. Hakufaulu

kuingia shule ya udaktari.

Tom alisikitika sana lakini aliendelea kupendelea

mambo ya afya. Kwa hiyo wazazi wake

walimhimiza afanye kozi ya mambo ya elimu ya

afya. Tom alijisikia mbadala huu ni dhaifu. Lakini

alifanya kazi kwa bidii na baada ya miaka miwili

alifuzu kozi hiyo. Baada ya hapo alipata kazi kama

mkaguzi msaidizi wa afya katika eneo dogo la

Wilaya iliyoko nje ya mji. Alifanya vizuri kazini

kwake na baadaye aliajiriwa na shirika moja

ambalo walimpeleka kupata mafunzo kadhaa.

Mwaka jana Tom alipandishwa cheo akawa

Mratibu wa mradi wa Shirika la Afya kwenye

wilaya tatu. Anawasimamia madaktari watatu.

Tom amefanikiwa. Siri ya mafanikio yake ni

pamoja na:

Kuwa mkweli kuhusu kupendelea masuala ya

afya.

Kukubali na kuwa tayari kufanya jambo

lingine baada ya mpango wa kwanza

kushindikana.

Uwezo wake mkubwa wa kufanya kazi na

kujituma katika yote anayofanya.

Hii inaweza kukuwia vigumu. Utalishughulikia namna gani tatizo hili? Tukio mojawapo ni

kufadhaika sana na kukata tamaa. Njia ya ufumbuzi ni kuwa na mtazamo wa kushinda. Unaweza

kushughulikia namna gani hali hii? Umekosa nafasi hii kwa pointi moja tu! Je, ipo kozi nyingine

Chuo Kikuu ambayo unaweza kuanza nayo halafu uhamie uhandisi baadaye? Je, kuna Chuo Kikuu

kingine? Unaweza kurudia mitihani? Wanafunzi wote 20 wataenda Chuo Kikuu? Je, ukifuatilia

kwa karibu zaidi utaipata nafasi hiyo au la?

Kipingamizi chochote kitakachokupata kisikuvunje moyo na wala usikate tamaa. Jaribu kutatua

tatizo. Upo usemi kwamba “penye nia pana njia” ambao unamaanisha kuwa endapo una nia ya kitu

utatafuta njia ya kufanikisha.

Wakati mwingine vipingamizi

vinatokea kwa sababu ya matatizo

uliyonayo. Aidha, nguvu yako

haiendani na njia uliyochagua au kwa

sababu ya mtazamo wako na namna

unavyolishughulikia jambo lenyewe.

Vipingamizi vinavyosababishwa

na udhaifu wako ni vigumu

kuvishughulikia. Moyo wako unaweza

kutaka kufanya kitu lakini ikatokea

kuwa hufai kufanya jambo hilo.

Kwa mfano, moyo wako ulipenda

kuwa daktari lakini biolojia na

kemia unashindwa kumudu. Huwezi

kukumbuka mambo haya hata

kama utakariri masomo hayo mara

kwa mara. Unafanya vibaya katika

majaribio ya masomo haya, ingawa

unafanya vizuri katika masomo

mengine.

Jambo kama hili likitokea unatakiwa

kujikosoa mwenyewe. Fikiria kuhusu

uwezo wako na udhaifu wako.

Wapi unafanya vizuri. Ufanye nini

kitakachokuwa sawa na uwezo wako?

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Kutambua uwezo wako na jinsi ya

kufanya zaidi ya uwezo wako inaweza

kuwa vigumu. Ni vigumu kujiona

wewe mwenyewe, na kujua aina zako

za uwezo. Kama unapata matatizo

kutambua jaribu kuzungumza na mtu

unayemfahamu – mzazi, kaka, dada,

shangazi , mwalimu au mshauri. Watu

hawa wanaweza kuwa wameona uwezo wako ambao wewe hujauona.

Ni kwa vipi utautumia uwezo wako wote?

Susan alikuwa na uhakika kuwa atakuwa mwandishi

wa habari. Alipata kazi ya kujitolea kwenye gazeti

moja la wanawake. Wafanyakazi wenzake walimpa

kazi ya kuandika na kumpa mapendekezo ya namna

ya kuandika makala. Lakini kila alichoandika

kilikuwa kibaya japo alijitahidi sana. Mawazo

yalipotea kila alipojaribu kuandika, na ilimchukua

saa nzima kuandika aya moja.

Alikaa hapo kwa muda wa miezi mitatu bila ya

kuandika makala yoyote. Susan alianza kuingiwa na

hofu. Alikuwa anatumaini kufanya kozi ya uandishi

wa habari baada ya kumaliza Kidato cha Sita.

Ingawa wafanyakazi wote pale walikuwa wazuri

kwake, mwanamke mmoja ambaye alibuni gazeti

alikuwa mzuri zaidi. Susan aliamua kwenda

kuzungumza naye na kumwomba ushauri. Yule

mwanamke alimwambia Susan asihofu sana. Vilevile

alimshauri Susan ajaribu mambo mengine pale.

Halafu akamwacha Susan ajaribu mikono yake

kwenye kompyuta na ikatokea kwamba Susan

alikuwa na jicho zuri kwa picha na ramani. Kwa

furaha, Susan alibadilisha na kusoma kozi ya usanifu

wa grafu.

Ingawa uandishi wa habari hakuufanikisha, Susan

alipata kazi nyingine ambayo aliipenda kweli. Susan

alikuwa na uwezo wa kubadili mawazo. Hakukata

tamaa badala yake alifanya kila kazi kwa uwezo

wake na kwa nafasi iliyojitokeza.

183

184

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kitu kibaya kuliko vingine vyote na ambacho kitakachokurudisha nyuma ni mtazamo wako

mwenyewe. Siku nyingine unahisi kama hutaki kujaribu zaidi. Umechoka au unajisikia hufai ama

ghafla unafikiri njia uliyochagua ni ngumu mno na kwamba matunda na mafanikio viko mbali

sana.

Mtazamo wako mwenyewe unaweza kuwa kikwazo. Vikwazo vyenyewe ni:

• MaWaZO MabaYa. Unajiambia mwenyewe kwamba una bahati mbaya na kwamba u mjinga.

Hapohapo unatumia mawazo haya kuwa sababu ya kushindwa kufanya jambo lolote.

• KuOGOPa KuFanYa MaKOSa. Unahofu sana kufanya makosa kiasi cha kutojaribu kufanya

kitu chochote.

• KuOGOPa MaFaniKiO. Hujaribu kwa sababu unahofu kuwa mafanikio yatakufanya kivutio.

• laKini SiWeZi. Unajiambia mwenye kwamba huwezi kabla hata ya kujaribu.

• KuOGOPa KutORiDhiSha MateGeMeO Ya Watu WenGine. Unahofu sana kuhusu

kuwasikitisha watu wengine kiasi cha kuchelea kujaribu.

Jihadhari na vikwazo hivi: Usiruhusu vikunase.

Kamwe hutajua una uwezo wa kufanya jambo mpaka ufanye bidii ya kufanya jambo hilo.

Usilizungumzie tu au kutarajia kwamba litatokea. Anza kuyafanyia kazi malengo yako.

Mara nyingi tunafikiri kwamba watu tunaowasikia wamefanikiwa wamezaliwa na vipaji vyao

pamoja na stadi kiasi kwamba ilikuwa rahisi kwao kufikia pale walipo. Hata hivyo, ukiangalia

walichofanya watu hawa utashangaa kiasi cha juhudi zao binafsi walizoweka katika kufanikisha

ndoto zao.

Wakati mwingine, tunadhani kwamba watu waliofanikiwa wana bahati. Upo msemo usemao:

“Bahati ipo pale maandalizi yanapokutana na nafasi”.

Hakikisha kwamba unajiweka tayari kwa lolote wakati wote. Ipo siku bahati itakuangukia

Kumbuka kuwa mafanikio si kuwa nyota wa uigizaji ama kuwa na gari la kifahari au kuwa na pesa

nyingi. Mafanikio ni jambo la nafsi. “Mafanikio yana maana tofauti kwa watu tofauti. Hata hivyo,

watu wengi wanatafsiri mafanikio kuwa ni kujihisi vizuri na kile unachokifanya.

Mwenye kuamua kiwango cha mafanikio yako ni wewe mwenyewe. Usisubiri watu wengine

wakutafutie mafanikio. Mafanikio yako yataamuliwa na furaha yako, utajiri wa kiroho, busara

zako, uwezo wako wa kubadilika kutegemeana na hali, ubunifu wako, nia na mtazamo wako

kwa watu wengine. Umeshika funguo za maisha yako ya baadaye na ndoto zako. Fanya

linalowezekana leo, usingoje kesho.

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Sura ya 14

Kutimiza ndoto zako

Kutimiza ndoto zako kunategemea kufanya kazi kwa bidii sana na kwa nia. Usisubiri

mambo yakutokee. Haya ni maisha yako ya sasa na ya baadaye. Unahitaji kuyajenga kwa

dhati.

Watu wengine wanajua wanataka kuwa nani na wanataka kufanya nini. Wanajua ndoto zao.

Wengine hawajui wanataka kuwa nani. Hii haina maana kuwa hawana ndoto. Ina maana

bado hawajajijua ni akina nani. Unaweza kuanza kutambua ndoto zako leo.

• angalia watu wanaokuzunguka katika jumuia yako. Nani unamhusudu na

kumheshimu? Watu hawa wanaweza kuwa mfano mzuri kwako.

• angalia nje ya jumuia yako. Wapo watu wanaofanya mambo yanayovutia na yenye

thamani kwa maisha yao. Hawa wanaweza kuwa mifano mizuri kwako.

• Ziache fikra zako za ubunifu zipae angani. Usijiwekee mipaka kuhusu nini unaweza

kufanya na kipi huwezi. Kama ni mvulana au ni msichana unaweza kufanya karibu kila

kitu unachotaka kufanya kama jambo ukiliweka akilini na kuongeza juhudi.

Zungumza na watu wanaofanya mambo yanayokuvutia. Waulize walifikaje pale walipo?

Walihitaji elimu gani? Mafunzo gani walipata. Wanapenda nini zaidi kuhusu kazi zao? Na ni

kitu gani hawakipendi sana kuhusu kazi zao?

Ndoto zako ni malengo yako ya muda mrefu – mambo ambayo unafikiria kuyakamilisha

baada ya muda mrefu. Lakini unahitaji vilevile malengo mahususi— mambo ambayo

unaweza kuyakamilisha katika muda mfupi. Fikiria unachotaka kufanikisha wiki hii,

mwezi huu na mwaka huu. Ukifanikisha malengo haya utajisikia vizuri. Utaona kuwa

unapokiweka akilini kitu unaweza kufanikisha.

Kuzifikia ndoto zako si jambo rahisi na siyo jambo la moja kwa moja lililonyooka.

Hatua sahihi za kuchukua hazitakuwa wazi na unaweza kujikuta unakutana na vipingamizi

ambavyo hukuvitegemea. Utahitaji kuwa na uwezo wa:

• Kufanya uamuzi mzuri kwa kuangalia matokeo ya uchaguzi uliopo mbele yako.

• Kulenga ndoto zako na kutoruhusu kujikatisha tamaa au kupotezwa na watu wengine.

• Kufanya kazi kwa bidii kama upo shuleni au haupo shuleni. Tumia nafasi uliyonayo

vizuri.

• Kumudu vikwazo (mambo yatakayokurudisha nyuma), na kutokata tamaa. Palipo na

nia pana njia.

Mafanikio yako yanaamuliwa na wewe mwenyewe. Nia yako, ubunifu, busara, uwezo

wa kukubali mabadiliko, mtazamo kuhusu watu wengine ni ufunguo wa maisha yako ya

baadaye na ndoto zako.

185

186

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Faharasa

amali [kutaamali] matendo, kazi, mazowea

angavu -eupe, safi, -enye kuelimika, enye akili nzuri

ari hali ya kuwa na moyo wa hima katika kukamilisha jambo,

kutokubali kushindwa

ashki tamaa ya kiume au kike, hamu, nyege, uchu

asi kataa kutii amri, pinga kanuni au sheria

baini [kubainisha] tambua au fahamu jambo lililokuwa limefumbwa

bwete bure, rahisi

changamoto kitu au jambo linalotia ari

chunusi [Acne] ugonjwa wa uvimbe

dinda kwa uume simama kwa uume, disa, inuka

disisha/ dindisha [kusimamisha] simama kwa uume, inuka

enzi [Kujienzi] onyesha heshima au mapenzi, penda

fufu fuvu/bupuri, bakaa ya mifupa baada ya mwili kuoza

ghali -enye bei kubwa, siyo rahisi

giligili kioevu kizito kinachoteleza, ute au gole

govi ngozi ambayo huziba dhakari kwa mbele kwa asiyetahiriwa

187

188

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

haiba heba, uvutio wa heshima, mwenendo wa kupendeza, sura

nzuri, urembo, uzuri

harimu [ma] ndugu wasioweza kuingiliana kimwili kwa mfano mtu

na dada yake

hasi ondoa au haribu mapumbu ya mwanaume au mnyama dume

kinyume cha kitu -(chanya)

hadhari uangalifu

hedhi damu inayomtoka mwanamke katika siku zake za mwezi

hodhi jirundikia mali au bidhaa

homoni kemikali zinazosisimua mwili

ishi kwa matumaini kuishi kwa matumaini. Hali ya mwathirika kuendelea

kuishi kwa kujipa moyo

jinsi, jeni Kijinsi viini urithi ambavyo hurithisha tabia na maumbile ya

kiumbe, -a kike au a-kiume

Jinsia uhusiano kati ya wanawake na wanaume unaojumuisha

mambo mengi, mfano mgawanyo wa kazi n.k.

kalori [Calories] kipimo cha joto

kandida [albicans] aina ya kuvu ambayo hupatikana mdomoni, ngozi, utumbo,

ukeni

kandidia [kandidiasisi] vijidudu/ vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kuvu

kanuni desturi, sheria, amri, taratibu za lazima

kemi muziki/ nyimbo zenye mahadhi ya rapu.

kiambato kitu kinachoambatanakihoro huzuni kubwa kwa ajili ya

kufiwa au jambo la msiba,

kilele sehemu ya juu kabisa, kiwango cha juu cha mafanikio,

kufikia kilele katika mapenzi (mshindo)

kilenge, kijusi, [Fitasi] mimba changa ya wiki tano au zaidi

fARASA

kinembe kinyama kilichojitokeza kwenye tupu ya mbele ya

mwanamke (kisimi)

kipindi fiche kipindi ambacho mwenye virusi vya UKIMWI/ VVU

hajaonyesha dalili za ugonjwa

kiwango cha kujamiiana idadi ya matendo ya ngono mtu ayafanyayo kwa muda

fulani

kizinda kizuizi chembamba cha nyama au mwili

kojoa toa mkojo, toa shahawa, katika ngono ni mshindo.

kokwa [la Mayai] mbegu za uzazi za mwanaume

konokono Mnyama anayeteleza na anayetambaa polepole

kuvu fangasi, husababisha vimelea na vijidudu

Kuzitambua ndoto zako Kuwa na mawazo halisi ya kufikirika kimaisha

kweza [Kujiweka Juu] kujitukuza, kutaka watu wakuone,

lateksi gundi

limfu kioevu ambacho asilimia kubwa ni maji yenye virutubisho

mbalimbali mwilini

malai mafuta yanayotumika kupaka usoni

manukato marashi ya majimaji ya urembo yanayonukia

mavuzi nywele ziotazo manenani

mfoko kutoka kwa kitu ghafla na kwa nguvu

mfyato kushona uke na kuacha tundu dogo kwa ajili ya kutolea

mkojo na hedhi

miadi makubaliano ya kukutana, ahadi

189

190

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

mkakamao msinyao/kushupaa kwa mwili, kujikaza kwa musuli wa

mwili baada ya jambo fulani

morali msisimko anaopata mtu

mshindo Tendo la kumwaga shahawa kwa mwanaume

msongo kuwa au kutingwa na mawazo mengi yasiyo na utatuzi wa

papo hapo

mustakabali uelekeo wa jambo baadaye

nasaha mawaidha, mwongozo anaopewa mtu kuhusu jambo fulani

nata shika na gandaganda kama vile gundi na ulimbo gandama

ndoto nyevu kutoka shahawa (mbegu za uzazi) mvulana akiwa usingizini

ngono tendo la kuingiliana kimwili kati ya mwanamke na

mwanamume.

nyonga umbo la mfupa lenye umbile la beseni lililopo katika kitako

cha mgongo

nyumbuka kuvutika kama mpira

odorono mafuta ya manukato yapakwayo kwapani

ovisha/ uovishaji kuachiwa kwa yai / kutoka kwa yai kutoka kwenye mfuko

wa mayai kwa ajili ya kurutubishwa. Lisiporutubishwa huwa

hedhi.

pangusa ugonjwa uenezwao kwa njia ya ngono unaojitokeza kama

kidonda sehemu za siri.

“pap smea” kipimo cha saratani

pumbaa [pumbazika] zubaa bila kusema neno, bumbuwazi

punyeto kitendo cha kujichua na kufika kilele ili kukidhi haja ya

mapenzi

riwaya hadithi ndefu yenye visa zaidi ya kimoja.

fARASA

sebamu “Sebum” mnyeso wa mafuta kutoka kwenye tezi za kwenye ngozi

shankaroidi[Chankroidi]pangusa ugonjwa wa zinaa unaoleta maumivu makali sehemu za siri,

wakati mwingine kuvimba kwa tezi hadi kupasuka.

sifa-bainifu maelezo ya pekee yanayotambulisha kitu kilivyo

sirinji bomba la kupigia sindano

smegma mnyeso wa mafuta kutoka kwenye tezi za kwenye ngozi

kwenye paji la uso

sodo [tampon] kifaa kinachotumiwa na wanawake kujihifadhi wakati wa

hedhi (pedi)

sponji sifongo

stadi maarifa ya utendaji wa jambo fulani

thamini familia heshima na kupenda familia

ugumba hali ya kushindwa kuzaa - utasa

uhanga [dalili za kujitoa] kufanya jambo kwa nia nzuri au mbaya kwa faida/ hasara ya

wengine

ujinsia hali ya kuwa na jinsia moja

ungo hali ya uzima anayokuwa nayo msichana kabla hajaingiliwa

na mwanaume

unyong’onyevu hali ya kuchoka anayokuwa nayo mtu

uovishaji utaratibu wa kujitoa kwa yai kutoka katika mirija ya uzazi

ushirikiali hali ya kuhisi au kuelewa hisia za mtu mwingine

utashi hali ya kutaka (matamanio)

utoko uchafu wa ukeni

uvumi jambo linalosemwa lisilo na ukweli

via vya uzazi viungo vya uzazi

191

192

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

virigua fanya ghasia, fujo, sumbua

vunja ungo hatua inayoendana na mabadiliko ya kibiolojia kutoka

utoto kwenda utu uzima (msichana)

VVU virusi vya UKIMWI

wajibu [Kuwajibika] jukumu, kazi, shughuli

weka wasilisha kitu mahali, tua, peleka

Marejeleo

Am I ready to have sex? Planned Parenthood of New York City, Inc., New York. 1998.

Je, niko tayari kufanya ngono?

Birth Control Choices for Teens. Planned Parenthood Federation of America, New York, 1997.

Njia za Kupanga Uzazi Kwa Vijana?

Changing Bodies, Changing Lives, edited by Ruth Bell and the Teen Book Project, 3rd Edition,

RandomHouse, 1998.

Mabadiliko ya Miili, Mabadili ya Maisha

Choose a Future! Issues and Options for Adolescent Girls. Centre for Development and Population

Activities (CEDPA), Washington, D.C., 1996.

Chagua Maisha yako ya Usoni! Masuala na Maamuzi ya Wasichana balehe

Contraceptive Technology. 17th ed., written by R.A. Hatcher et al. Ardent Media, Inc., New

York,1998.

Tekinolojia ya Uzuiaji Mimba

The Education of Girls and Women in Africa, Forum for African Women Educationalists (FAWE),

Nairobi, Kenya.

Elimu ya Wasichana na Wanawake Afrika

“Feeling Good about Growing Up.” Planned Parenthood Federation of America, New York, 1993.

Kujisikia Vema Kuhusu Kuwa Mtu Mzima

Filling the Gaps: Hard to Teach Topics in Sexuality Education. Sexuality Information and Education

Council of the United States (SIECUS), New York, 1998.

Kuyajaza Mapengo: Mada Nyeti kufundisha katika Elimu ya Kijinsia

Guidelines for Comprehensive Sexuality Education. 2nd ed. Sexuality Information and Education

Council of the United States (SIECUS), New York, 1996.

Maelekezo ya Elimu Mwafaka ya Mambo ya Kijinsia

Healthy Women, Healthy Mothers: An Information Guide, written by A.A. Arkutu. Family Care

International, New York, 1995.

Wanawake wa Afya Bora, Akina Mama wa Afya Bora: Habari ya Maelekezo

193

194

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

HIV Testing. Straight Talk, Vol. 7, No. 8, August 1998.

Kupima Virusi vya Ukimwi

Life Planning Education: A Youth Development Program. Advocates for Youth, Washington,

D.C., 1995.

Elimu ya Kupanga Maisha:Mradi wa Maendeleo wa Vijana

Now What do I do? How to Give Your Pre-Teens Your Messages. Sexuality Information and EducationCouncil

of the United States (SIECUS), New York, 1996.

Sasa Nifanye Nini? Jinsi ya Kuwapa Habari Vijana Wako Ambao Hawajabalehe

The Preteen’s First Book about Love, Sex and AIDS, written by Michelle Harrison, M.D., American

Psychiatric Press, Inc., Washington, D.C., 1995.

Kitabu cha Kwanza kwa Vijana ambao Hawajabalehe Kuhusu Mapenzi, Ngono and Ukimwi

Red Card or Yellow—Are You Still in the Game? Being Young and Coping with Sexual and

Reproductive Health in Tanzania. Swedish Association for Sex Education (RFSU), Stockholm,

1995.

Kadi Nyekundu au ya Kijani- Je Ungali Mchezoni? Kuwa Mchanga na kukabiliana na Afya ya

Uzazi Tanzania

Responsible Teenage Sexuality, Planned Parenthood of South Africa (PPASA), 1992.

Afya Bora ya Kijinsia kwa Vijana balehe

Sexually Transmitted Infections: The Facts. New York: Planned Parenthood Federation of

America, 1997.

Magonjwa ya Zinaa: Ukweli wa Mambo

Stay off drugs and Alcohol. Straight Talk, Vol. 7, No. 9, September, 1999.

Usiyakaribie Madawa ya Kulevya na Pombe

Sugar Daddies and Sugar Mummies. Straight Talk, Vol. 7, No. 10, October 1999.

Baba na Mama Sukari

Talking with our Children about Sex and Growing up, Unicef and Government of Uganda, Kampala,

Uganda.

Kuzungumza na Watoto Wetu Kuhusu Ngono na Utu Uzima

What’s Happening to My Body? A Book for Boys, written by Lynda Madaras. Newmarket Press,

New York,1988.

Ni Nini Kinachofanyika katika Mwili Wangu, Kitabu cha Wavulana

What’s Happening to My Body? A Book for Girls, written by Lynda Madaras. Newmarket Press,

New York,1988.

Ni Nini Kinachofanyika katika Mwili Wangu, Kitabu cha Wasichana

Where Women Have No Doctor: A Health Guide for Women, written by A.A. Burns et al. The

Hesperian Foundation, Berkeley, 1997.

Mahali Wanawake Hawana Daktari, Maelekezo ya Afya kwa Wanawake.

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!