Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
22

KuDinDa KWa uuMe

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

iwapo hujatahiriwa rudisha nyuma govi na safisha taratibu chini yake.

Kwa kawaida uume ni laini na huninginia chini. Wakati unadinda, damu nyingi huelekea kwenye

uume isivyo kawaida na damu kidogo hurudi. Hii husababisha uume kuwa mkubwa na mgumu,

na kusimama. Uume uliodinda kwa kawaida hujikunja kidogo kuelekea juu, na unaweza kujikunjia

upande mmoja.

Uume unapokuwa umedinda unaweza ukashindwa kukojoa kiurahisi kwa sababu msuli hufunga

kibofu cha mkojo. Itakubidi usubiri uume ulegee ndipo ukojoe.

Uume unaweza kudinda iwapo utaguswa au kushikwa shikwa, au wakati umepata mhemuko wa

kutaka kujamiiana au kwa kumuona mtu anayekuvutia. Uume unaweza kudinda kwa sababu ya

kuwa na wasiwasi na mfadhaiko. Ni kawaida kwa wavulana kuamka asubuhi na uume uliodinda.

Ukiwa usingizini uume unaweza kudinda mara 5 mpaka 7. Hii ni kawaida kabisa na haina madhara

yoyote.

Kudinda kwa Uume kunawatokea wanaume wote wa umri mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto

wadogo na wazee. Wakati mwingine wavulana huhofu wanapodindisha mara kwa mara. Hali hii

inawasumbua wakiwa darasani, ndani ya basi au hata wakati wa matembezi. Wakati mwingine

zipo sababu za msingi za uume kudinda, kwa mfano, unaweza ukawa umekaa karibu na mtu

anayekuvutia. Hata hivyo, kuna wakati uume unadinda bila sababu yoyote ya msingi.

nfune kutoka Zambia (umri wa miaka 13)

“Kudindisha kwa uume hakuzuiliki na hutokea mara kwa mara.

Wakati mwingine ni dalili ya kuonyesha una msisimko wa

kutaka kujamiiana. Hali hii naichukia sana hasa ninapokuwa

shuleni au hadharani.”

Tafadhali usiwe na wasiwasi, wewe ni wa kawaida, mwenye afya na homoni nyingi. Unaweza

kufedheheka ikitokea darasani au hadharani, lakini wakati wote ni wewe peke yako unayefahamu

kwamba umedindisha.

Wakati mwingine wavulana wanadhani njia pekee ya kuthibiti uume kudinda ni kufanya ngono

Hii sio kweli ni uzushi ikiwa ni sababu ya wavulana kufanya ngono. Uume kudinda sio dalili ya

kwamba unahitaji kufanya ngono, la hasha.

KuMWaGa Manii “KuKOjOa”

SURA YA 3 | WAvULANA

Unapofikia balehe unaweza kuanza kuona majimaji yenye rangi ya maziwa ambayo yananata na ni

mazito, sio mepesi kama mkojo.

Majimaji kama ute hutoka kupitia kwenye uume wakati mwanaume anapofikia mshindo. Kukojoa

manii ni kilele cha msisimko wa kijinsia, wakati mwanaume anapokuwa amedindisha uume.

Kumbuka ya kwamba sio lazima kukojoa manii kila uume unapokuwa umedinda. Kama utasubiri,

uume utalegea wenyewe bila hata ya kukusababishia madhara yoyote.

Majimaji kama ute yametengenezwa na vitu viwili. Karibia 10% ya majimaji ni mamilioni ya

mbegu za kiume. Mbegu za kiume ni ndogo sana kiasi ambacho hatuwezi kuziona kwa macho

labda kwa darubini. Ukiziona zinaonekana kuwa na kichwa cha mviringo na mkia mrefu na

mwembamba.

Asilimia 90 ya ute huo ni majimaji yenye rangi ya maziwa yanayoitwa shahawa. Shahawa

huwezesha mbegu za kiume kuogelea na pia huzipa chakula na kuziwezesha kuwa hai. Shahawa

sio chakula kwa wasichana, kama watu wengine wanavyozusha.

Mbegu za kiume zinatengenezwa katika Korodani/Makende (angalia kielelezo uk 19). Shahawa,

ambazo ni majimaji yenye rangi nyeupe/maziwa zinatengenezwa kwenye vifuko vya shahawa.

Hizi ni tezi zilizopo nyuma ya kibofu cha mkojo. Mwanaume anapofikia mshindo mbegu za kiume

zinachanganyika na shahawa kutoka kifuko cha shahawa. Mchanganyiko huu huitwa manii. Manii

hupitia kwenye mirija ya kupitishia mbegu na kutoka nje ya uume kupitia kwenye tundu dogo

lililopo kwenye kichwa cha uume.

Inaweza kuonekana kana kwamba manii nyingi hutoka wakati mwanaume “anapokojoa” Ukweli

ni kwamba kiasi kinachotoka ni kama kijiko kidogo cha chai kilichojaa. Usije ukadharau uwezo

wa hiki kijiko kidogo cha chai kilichojaa manii;

kinaweza kuwa na mbegu za kiume karibia

milioni mia tano!. Kila mojawapo ya mbegu

hizo inaweza kumfanya msichana apate mimba.

Unapofikiria mbegu za kiume zipatazo milioni

mia tano, utaelewa ni kwa namna gani msichana

anavyoweza kupata mimba kirahisi.

Iwapo mvulana au mwanaume ana maambukizi

ya VVU, kijiko cha chai kimoja kilichojaa

shahawa kinaweza kuwa na mamia kwa maelfu

ya virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Mbegu ya kiume

Kijiko kidogo cha chai kilichoja shahawa kina

mamilioni ya mbegu za kiume na kinaweza kuwa na

VVu iwapo mvulana atakuwa ana maambujizi.

23