08.06.2013 Views

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

24

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Wavulana wengi wanakuwa na wasiwasi kwamba kondomu haiwezi kuhifadhi mbegu za kiume

zipatazo milioni 500. Lakini mbegu za kiume ni ndogo sana na kwa hiyo kondomu inaweza

kuzizuia zote ili mradi inavaliwa kwa usahihi (angalia sura ya 10 kwa maelezo zaidi kuhusu

kondomu).

Wavulana wengine wanakuwa na wasiwasi kwamba wakikojoa manii mara kwa mara

watapunguza kiasi cha shahawa mwilini mwao. Wasiwasi wa kwamba wanaweza kuishiwa

shahawa na hivyo kutokuwanazo za kutosha watakapozihitaji. Hili haliwezi kutokea hata mara

moja kwani mwanaume anatengeneza mbegu za kiume na shahawa tangia kipindi cha balehe

mpaka siku anayokufa.

Vilevile kumbuka ya kwamba haiwezekani mbegu za kiume na shahawa zikalundikana au

zikajenga shinikizo mwilini. Mwili wako ni kama mashine iliyokamilika, unazo njia za kuondoa

mbegu za kiume na shahawa inayozidi, mojawapo ni ndoto nyevu.

nDOtO nYeVu (“KuKOjOlea” KitanDani)

Wakati mwingine wavulana wanakojoa manii

kitandani wakiwa usingizini.Kitendo hiki kinaitwa

“ndoto nyevu” wavulana wengi wanapopata ndoto

nyevu huwa inakuwa ni mara yao ya kwanza shahawa

kutoka mwilini mwao. Wanaweza kuamka na kukuta

doa bichi kitandani au kwenye nguo.

Kama hufahamu lolote kuhusu ndoto nyevu unaweza

kuchanganyikiwa na kuwa na wasiwasi. Unaweza

kufikiri umekojoa kitandani au damu inakutoka au

unaumwa, lakini utaona kwamba majimaji yana rangi

ya maziwa/meupe, na sio kama damu au mkojo.

ndoto nyevu kwa mara ya Kwanza

Ndoto nyevu hutokea usingizini tu. Ukisinzia kidogo mchana unaweza kupata ndoto nyevu, lakini

wavulana wengi hupata ndoto nyevu usiku wakiwa usingizini. Wavulana wengi wanapojikuta

wamekojoa manii huwa wanakumbuka kwamba walikuwa wanaota ndoto zinazohusiana na

mapenzi. Lakini unaweza kupata ndoto nyevu hata kama hujaota ndoto za mapenzi.

Karibu wavulana wengi wanafedheheka wakipata ndoto nyevu. Ni sahihi kufedheheka, lakini

kumbuka ya kwamba ndoto nyevu ni za kawaida wakati wa ujana balehe. Vijana balehe wengi

wanapata ndoto nyevu ingawa sio wote.

Mvulana hawezi kujizuia kupata ndoto nyevu; ni za asili na ni za kawaida. Ni njia ambayo mwili

unatoa nafasi kwa ajili ya mbegu za kiume mpya kutoka kwenye korodani. Kupata ndoto nyevu

haimaanishi uanze kujamiiana.

SURA YA 3 | WAvULANA

adamu, kutoka uganda (umri, miaka 13)

“Sidhani kupata ndoto nyevu kunamaanisha ninatakiwa kujamiiana. Ni

kukua tu. Ninaona aibu tu kwa vile inabidi nibadilishe mashuka kila baada

ya siku moja.”

Wavulana wengine wanapoanza kupata ndoto nyevu wanaona ni tukio kubwa sana ambalo

wanalifurahia.

Panaito kutoka Kenya

“Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilijisikia kama nimekomaa

kijinsi. Nilifurahi kuwa mmojawapo wa wale ambao tayari walishapata.

Lakini ningelikuwa sijapata taarifa, ningeweza hata kwenda kumuona

daktari,ninamshukuru Mungu kwamba nilijua kilichokuwa kinatokea”.

adamu kutoka uganda (umri, miaka 13)

“Nilipopata ndoto nyevu kwa mara ya kwanza nilimwambia kaka yangu mkubwa

ambaye alinihakikishia kwamba ilikuwa ni sehemu ya ukuaji.”

Wavulana wengine hawawi na furaha sana wanapoanza kupata ndoto nyevu. Hili ni jambo la

kawaida vilevile.

nfune kutoka Zambia (umri wa miaka 13.”

“Ninaona kama zinanichukiza”

Wavulana wengine wanao marafiki wasio na huruma, ambao huwatania kuhusu kupata ndoto

nyevu. Ni makosa kumtania au kumcheka mtu kwa vile amepata ndoto nyevu. Ndoto nyevu ni

jambo la kawaida.

bernard kutoka Kenya (umri wa miaka 17)

“Nilipokuwa darasa la 8, sikutegemea kama ningeanza kukojoa manii

mapema kiasi hicho. Nilimwambia rafiki yangu siri, badala ya kunieleza kwa

nini yametokea, alinicheka. Nilijisikia kufedheheka. Sikutaka mtu yoyote

afahamu, lakini aliwaeleza watu wengine, na wengine wakasema nilikuwa ninapiga

punyeto. Nilimfuata rafiki yangu mwingine ambaye alikuwa mkubwa

kwangu ambaye alinieleza kwamba ndoto nyevu ni kawaida.”

Unatakiwa usiwe na wasiwasi kuhusu ndoto nyevu kwa vile ni jambo la kawaida halina kasoro.

Unavyoendelea kuujua mwili wako ndivyo utakavyokuwa na raha na mabadiliko unavyokuwa

unayapitia. Kwa kuongezea, ukiwa na taarifa iliyokamilika utaweza kuwasaidia wavulana wadogo

kuelewa kitu gani kinawatokea wanapopitia ujana balehe.

Yapo maelezo na mafunzo mengi mazuri ndani ya kitabu hiki,kwa hiyo usiachie kukisoma kitabu

hiki kwa undani.

25

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!