Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
16

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 2

MabaDiliKO KatiKa MWili WaKO

Ujana, ambao kawaida huanzia umri kati ya miaka 10 na 16 ni mabadiliko ya hatua kutoka

utoto kuingia utu uzima. Kila mtu anaanza kubadilika wakati wake. Wakati watu wengine

hukua haraka zaidi, wengine hukua taratibu. Tunatofautiana, na hakuna unaloweza kufanya

kuthibiti muda wa mabadiliko hayo.

Ni yapi uyategemee unapobadilika kutoka msichana na kuwa mwanamke au kutoka

mvulana na kuwa mwanaume?

Mfoko wa ukuaji; viganja, nyayo, miguu, mikono, nyonga kifua vyote vitaongezeka

ukubwa mwili utatengeneza homoni, kemikali maalumu ambazo hutoa ujumbe namna

mwili utakavyokua na kubadilika.

Via vya uzazi (au sehemu za siri) vitakuwa vikubwa na vitaanza kutengeneza majimaji

(giligili).

Ngozi inaweza kuwa na mafuta zaidi.

Utaanza kuota mavuzi na nywele kidogo kwapani, miguuni, mikononi na kama ni

mvulana, usoni pia.

Utaanza kupata hisia nzito mbali mbali.

Uwezo wa kufikiri utaongezeka.

Bila ya kujali mabadiliko yanatokea haraka au taratibu, wakati gani yanaanza, jaribu

kukumbuka kwamba mabadiliko haya ni ya kawaida na hayana kasoro yoyote.

Inaweza kuchukua muda mrefu kuyazoea mabadiliko haya kwa hiyo kuwa mvumilivu na

usihofu.

Wavulana

Katika sura ya pili umesoma baadhi ya mabadiliko kadhaa ambayo wavulana wanayapata katika

kipindi cha balehe. Sura hii itakupa maelezo zaidi kuhusu mabadiliko haya.

uMbO na uKubWa Wa MWili

Mfoko wa ukuaji kwa wavulana wengi unaanza kati ya miaka 12 na 13. Hata hivyo wavulana

wengine wanaanza ukuaji mapema zaidi na wengine wanachelewa. Wakati wa mfoko wa ukuaji,

mwili wako utaanza kuwa mrefu zaidi na mkubwa.

Sehemu mojawapo ya mwili wako itakayoanza kukua ni miguu. Ukweli ni kwamba, mifupa ya

miguu inakua haraka zaidi kuliko sehemu zingine za mwili. Hivyo basi miguu inaweza kukua hadi

mwisho kabla ya sehemu zingine kukua sana. Iwapo utajisikia kama vile unakuwa mzito ghafla,

inawezekana ni kwa sababu ya miguu yako imekuwa mikubwa kuliko ilivyokuwa muda mfupi

uliopita. Unatakiwa kuwa mvumilivu kwani hali hii inaweza kukuchukua muda kabla hujaizoea

Mifupa mingine ya mwili nayo itakuwa zaidi kuliko mingine na kusababisha umbo la mwili

kubadilika. Kwa mfano, mabega yatakua zaidi wakati nyonga inaweza kukua kidogo tu. Nyonga

yako inaweza kuonekana nyembamba ukilinganisha na upana wa mabega. Inawezekana miguu na

mikono ikakua zaidi kuliko uti wa mgongo, hivyo basi miguu inaweza kuwa mirefu ukilinganisha

na kifua au kiwiliwili. Matokeo yake umbo lako litakuwa tofauti sana na lile la mvulana mdogo.

Misuli vile vile inakuwa, hasa ile ya miguuni na mikononi. Kadri misuli inavyokua, ndivyo

unavyokuwa na nguvu zaidi. Mlundikano wa misuli na mafuta utasababisha kifua kuwa kikubwa.

Vile vile wavulana wengi hugundua kwamba kuna mabadiliko ya chuchu na matiti katika kipindi

cha balehe. Chuchu huongezeka na kuwa kubwa kidogo. Miduara inayozinguka chuchu nayo huwa

mikubwa na rangi yake kuwa nyeusi kidogo.

Wavulana wengine wanajikuta matiti yao yamevimba na yanauma. Kwa wachache, uvimbe

huzidi, hivyo kuwasababishia wasiwasi kuwa wataota matiti makubwa kama wanawake. Usiwe

na wasiwasi, haya ni mambo ya kawaida uvimbe na ulaini unasababishwa na homoni ndani ya

mwili. Uvimbe unaweza ukadumu mwaka mmoja au mwaka mmoja na nusu, lakini baada ya hapo

hupungua kwa vile mwili unaacha kutengeneza homoni nyingi.

Wakati wa mabadiliko yote haya unatakiwa kuwa mvumilivu kwani mwili wako hauna matatizo

yoyote, na wewe ni wa kawaida kabisa. Hata kama hukui haraka ukilinganisha na rafiki zako

wanavyokua, usiwe na wasiwasi utakua tu, muda bado. Ni wakati gani unaanza kukua na kiasi

gani utakua,inategemea sifa bainifu unazorithi kutoka kwa wazazi wako. Hata ukichelewa

17

SURA YA 3