Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
136

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

KujitunZa na KuMtunZa MtOtO baaDa Ya KujiFunGua

Kama ulivyokuwa unakwenda kliniki kabla ya

kujifungua, hakikisha unakwenda tena kwa uchunguzi

baada ya kujifungua. Kama ulimzalia mtoto wako

nyumbani hakikisha unakwenda kliniki kwa ajili

ya uchunguzi ndani ya siku tatu. Kama ulimzalia

mtoto wako hospitalini nenda baada ya wiki sita ili

mkunga aone kama tumbo lako linarudia hali yake

ya awali. Mkunga anatakiwa pia kuangalia kama

huna maambukizo ya magonjwa au hutokwi na damu

sana.Kama ulipoteza damu nyingi wakati wa kuzaa

mkunga atakupa dawa za madini ya chuma ili kusaidia

kuongeza damu.

Mkunga anaweza vilevile kujibu maswali mengi

utakayokuwa nayo kuhusu kunyonyesha mtoto, kulala,

kinga kwa mtoto, kuzuia mimba na mambo mengine.

Mwanamke aliyezaa kwa mara ya kwanza mara nyingi

anakuwa na maswali mengi hivyo kuongea na mkunga

inaweza kukusaidia.

KuhaRibiKa MiMba

Mara nyingine mimba huwa inaharibika/inatoka yenyewe tu. Tunasema mimba imetoka kwa

bahati mbaya. Fitasi inakufa na inatoka kupitia ukeni. Malaria au magonjwa ya ngono huweza

kusababisha kuharibika mimba. Mimba inaweza kutoka vilevile kama fitasi ina matatizo.

Kama mimba itakuwa imetoka mwanamke anahitaji kumwona mhudumu wa afya ili kuhakikisha

hapati maambukizo kwenye tumbo la uzazi. Mhudumu wa afya anaweza pia akatambua

kilichosabisha mimba kutoka na kutoa matibabu ya magonjwa kama ya ngono.

Mimba inaweza vilevile kutolewa kwa makusudi kwa kupitia taratibu za kitabibu. Mimba inaweza

kutolewa na mganga aliyesomea katika mazingira ya hali ya usafi. Kutoa mimba ni utaratibu

salama kitabibu kwa ujumla na ni salama kuliko kuzaa. Katika nchi nyingi za Kiafrika ni kosa la

jinai kutoa mimba isipokuwa katika mazingira ya matatizo kama kubakwa au kujamiiana kwa

maharimu (ndugu wa karibu) au wakati ambapo maisha ya mwanamke yako hatarini kwa ajili

ya mimba au fitasi si ya kawaida na hata akizaliwa mtoto hataishi. Uthibitisho wa kitabibu

unatakiwa kuwepo kuwa mhusika alibakwa kulikuwepo kujamiiana kwa maharimu au fitasi si ya

kawaida.

Kutoa mimba kinyume cha sheria katika nchi nyingi barani Afrika ni hatari sana. Kutoa mimba

kunafanywa katika mazingira machafu na ya hatari na mara nyingi watu wengi wanaotoa

mimba hawajasomea. Kwa sababu kutoa mimba hakuruhusiwi, mtoaji mimba anaweza kutoa

bila utaratibu, kwa haraka na kuogopa na katika mazingira na vifaa vichafu. Mambo yote haya

yanamuweka mwanamke katika hatari kubwa. Kwa hakika, katika nchi nyingi za Afrika, robo ya

vifo vya wanawake wajawazito vinasababishwa na matatizo ya ama mimba kutoka au kutoa

mimba.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Kutoa mimba kwa kutumia njia isiyo salama

kunaweza kusababisha matatizo ya kiafya.

Kifaa cha kutolea mimba kikiingizwa kwenye

mlango wa mfuko wa kizazi kinaweza

kikasababisha uharibifu kwenye kibofu

cha mkojo au utumbo mdogo au mlango

wa mfuko wa kizazi. Mfuko wa kizazi

ulioharibika utatakiwa uondolewe. Maana

yake, msichana hataweza kupata mtoto tena.

Kutoa mimba kusiko salama vilevile

kunaweza kusababisha kuvuja damu,

maambukizo ya magonjwa na kifo. Kuingiza

kifaa cha kutolea mimba kwenye mlango

wa mfuko wa kizazi na kizazi kunaweza

kusababisha kuvuja sana damu na msichana

anaweza akavuja damu mpaka akafa. Miti

shamba na vifaa vingine vinavyotumika

kuanzisha uchungu mara nyingi siyo safi;

vinaweza kuleta vijidudu vya maradhi katika

mfuko wa kizazi. Kizazi na mirija ya kupitisha

mayai ya mgonjwa vinaweza kuathirika sana

kiasi cha kusababishiwa ugumba au kifo. Miti

shamba, dawa au kemikali ambazo msichana

anameza zinaweza kumfanya awe mgonjwa

sana na anaweza akawa amejipa sumu

mwenyewe.

Je unajua matokeo ya utoaji mimba usio

salama?

Jane alipopata mimba alikuwa na miaka 15

na alikuwa Kidato cha Tatu. Alitaka sana

kuendelea na shule, aliishi na shangazi yake,

ambaye alimpeleka kwa mtu aliyedai ni

mganga anayefanya kazi kwenye hospitali

kubwa mjini Kampala. Mtu huyu aliingiza

kifaa kwenye uke. “Maji” yakatoka. Alisikia

maumivu makali sana, lakini aliambiwa asilie

kwa sababu hata hivyo “alitaka” mwenyewe

kilichomtokea. Shughuli ilichukua dakika 15.

Alirudi nyumbani na alitokwa na damu wiki

nzima, akidhoofu kidogokidogo kila siku.

Tumbo lake liliuma na uke ukawa unatoa

majimaji yenye harufu mbaya. Baadaye

alipelekwa kliniki inayohudumia vijana. Kliniki

waligundua amechanika sehemu kubwa ya

mfuko wa kizazi. Ilibidi afanyiwe upasuaji

na kukaa hospitalini kwa muda wa wiki nne

kutibu kidonda na maambukizo ya magonjwa.

Jane bado hajui iwapo ataweza kupata watoto

baadaye.

Diana kutoka uganda (umri wa miaka 15)

“Kutoa mimba ni hatari sana hasa kwa kutumia miti shamba. Ni

afadhali usishiriki katika ngono kabisa”.

nedina kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Rafiki yangu wa kike akipata mimba nitamkatisha tamaa asitoe

mimba kwa sababu ni hatari. Nitamsihi azae na kisha aendelee na

masomo yake hapo baadaye”

Kutoa mimba kunaweza kuleta matokeo ya kusikitisha kijamii. Watu wengine wakijua kwamba

msichana ametoa mimba, anaweza kufukuzwa shule, kutoaminika au kufedheheshwa na marafiki

au na familia.

Hata hivyo, wasichana wengi wanaishia kutoa mimba kwa njia isiyo salama wanapojikuta

wamepata mimba. Wanasahau hatari za kutoa mimba kwa sababu ya hofu, familia zao

zitakapogundua ujauzito wao. Wanakata tamaa ya kuendelea na masomo. Marafiki zao wa kiume

wanaweza kuwa wamewaacha au kuwalazimisha watoe mimba.

137