Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
98

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

KuVutiWa na Mtu Wa jinSi KaMa YaKO

Wakati wa kubalehe ndio wakati watu wengi wanapata kuelewa zaidi mwelekeo wao kijinsi.

Mwelekeo wa kijinsi unahusu mtu ana hisia za kimapenzi na anavutiwa kimapenzi kwa nani.

Watu wengi wanavutiwa kimapenzi na watu wa jinsi tofauti (kama mwanaume anavutiwa na

mwanamke na mwanamke anavutiwa na mwanaume).

Watu wengine wanajisikia kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsi sawa. Wanaume wengine

wanavutiwa na wanaume wenzao na wanawake wengine kuvutiwa na wanawake wenzao. Huku

kuvutiwa na jinsia sawa kunaitwa “ubasha” au “usenge” au “ushoga”.

Nyakati fulani katika maisha yao, baadhi ya watu wanakuwa na hisia za kimapenzi, mawazo,

ndoto na mvuto kwa mtu fulani wa jinsi moja. Marafiki wawili waliokaribu (pengine wavulana

wawili au wasichana wawili) wanaweza kupendana – wanapenda kuwa pamoja na wakati

mwingine wanajisikia kutamaniana kimwili. Watu wengine wanaona hisia hizi zinawachanganya

na kuwafadhaisha. Hisia hizi ni za kawaida, na baadhi ya watu wanazipata hisia hizi wakati fulani

katika kipindi cha maisha yao.

Japokuwa baadhi ya watu wanavutiwa na watu wa jinsi sawa, madhehebu mengine ya dini na mila

zingine zinafikiria ubasha ni jambo baya, si la kawaida na ni tabia ambayo inaweza kurekebishwa.

Watalaam wengi wanafikiria kwamba mwelekeo wa kimapenzi wa jinsi moja si jambo ambalo

wanaweza kulidhibiti kama isivyowezekana kudhibiti rangi ya ngozi au nywele zilivyo. Kwa

maneno mengine ubasha / usenge sio chaguo la makusudi ambalo mtu anachagua, hivyo

haiwezekani kulibadilisha aidha kwa kuswali, kwa utashi au kwa kufanya ngono na mtu wa jinsia

tofauti.

Katika kipindi cha balehe, watu wengine wanajikuta ni mabasha/wasenge. Kujitambua kunaweza

kuwa kugumu. Unaweza kujiona uko tofauti kuliko mtu yeyote anayekuzunguka, na unaweza

kujisikia mpweke mno. Kama unajisikia kitu kama hiki, jaribu kuonana na mtu ili uzungumze naye,

kama mshauri nasaha wa vijana, mhudumu wa afya, mwalimu unayemwamini, au jamaa yako

mkubwa – yeyote atakayeweza kukusaidia kujibu maswali yako na kupunguza hofu yako atakuwa

amekusaidia.

ubiKiRa

Bikira ni mtu ambaye hajawahi kujamiiana. Kila mvulana na msichana amezaliwa bikira. Ubikira

ni kinga nzuri dhidi ya VVU na magonjwa ya zinaa. Siku hizi wavulana na wasichana wengi

wanaamua kubakia bikira hadi siku ya kuoa/kuolewa.

Ruvimbo kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 13)

“Nitataka kutunza ubikira wangu. Sitafanya mapenzi na yeyote

hata kwa kutumia kinga. Rafiki yangu wa kiume ni mtulivu

na ndio maana ni mtu wangu.”

Stabile, kutoka Zimbabwe (umri; miaka 19)

“Bado mimi ni bikira. Bila shaka imani yangu kubwa ya dini

inanisaidia katika suala hili.”

SURA YA 9 | UJINSIA NA NGONO

Susan, umri wa miaka 18 kutoka uganda

“Ubikira ulifanya nionekane mwenye heshima. Wasichana wanatakiwa

kutunza ubikira wao mpaka wanapoona wamepata watu wa kuwafaa.

Ngono ni jambo unaloweza kuahirisha. Yakwepe mazingira yaliyo

kinyume na kanuni ulizojiwekea na utaweza ukadumisha dhamira yako.”

Watu wengi wanachanganyikiwa na kitu kinachosababisha wasichana wapoteze ubikira.

Wanafikiri ubikira wa msichana unadhihirishwa na kizinda, ambacho ni tishu nyembamba ndani ya

mlango wa uke. Kizinda kina shimo dogo na hakizibi kabisa uke kwa sababu damu ya hedhi lazima

itoke kila mwezi. Wasichana wengine hawana kizinda kabisa. Pengine ni kwa vile hawakuzaliwa

nacho au kilinyumbuka na kuchanika kabisa wakati wa michezo.

Wasichana walio na tishu ya kizinda mara nyingine wanatoka damu wanapopoteza ubikira wao.

Wasichana ambao wana tishu ndogo ya kizinda au hawana tishu ya kizinda wanaweza wasivuje

damu watakapojamiiana. Kwa mara ya kwanza hii inawachanganya watu. Watu wanasema:

“Hakuna damu, kwa hiyo hakuwa bikira”. Lakini anaweza kuwa alikuwa, hajawahi kufanya ngono

hapo awali hivyo alikuwa bikira. Ubikira unapotea kwa kujamiiana. Hauwezi kupotea kutokana na

michezo, kwa kutumia visodo, kupiga punyeto au shughuli yoyote ile. Japo ni kweli mambo haya

yanaweza kurefusha au kuchana kizinda, hii haimaanishi msichana sio bikira. Watu wanaofikiria

kuwa kizinda ndio usahihi wa kuwepo bikira wanakosea.

UNAJUA ukweli kuhusu ubikira?

Kuna uzushi mwingi kuhusu ubikira:

1. Nimesikia kwamba msichana anaweza kupoteza ubikira kwa kucheza michezo. Je, hii

ni kweli? Si kweli! Ubikira anaweza kupotea tu kwa kufanya ngono, kucheza michezo ni

kuzuri kwa wasichana na haiwezi kumsababishia kupoteza ubikira.

2. Kuna mitishamba mingine inaweza kurejesha ubikira? Hapana, hakuna mitishamba

inayoweza kurejesha ubikira. Ukipotea, umepotea milele.

3. Rafiki yangu anasema nikibaki bikira kwa muda mrefu, naweza kuugua magonjwa na

mambo yasiyo ya kawaida? Siyo kweli! Unaweza kubakia na ubikira maisha yako yote

bila matatizo yoyote mabaya.

4. Ni kweli kwamba msichana akiwa bikira kwa muda mrefu sana, kizinda chake kitakuwa

kigumu na atapata matatizo ya kufanya ngono? Huu ni upuuzi! Kizinda ni kipande

kidogo na chembamba cha tishu. Hakiwi kigumu kadri unavyokua na wala unaposubiri

kujamiianahudhuriki kamwe.

5. Unawaweza kuwatambua bikira kwa kuwaangalia usoni? Si kweli! Huweza kumtambua

bikira kwa kumwangalia kwa macho. Ni bikira peke yake anayejua hali yake.

6. Baada ya kupoteza ubikira wako, unatakiwa uendelee na ngono. Si kweli. Unaweza

kuacha kufanya ngono ukipenda.

7. Nimesikia kwamba si vema kutumia kondomu ukiwa unajamiiana na msichana ambaye

ni bikira kwa sababu unahitaji kutumia nguvu sana kuvunja ubikira wa msichana

– kiasi kwamba utachana kondomu. Je huu ni ukweli? Hapana! Mvulana na msichana

ambao ni bikira wanaweza kutumia kondomu bila matatizo. Kizinda ni tishu laini sana

inayochanika kwa urahisi mno.

99