Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
88

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Marafiki wa Okakah walimwambia kwamba angempoteza rafiki yake wa kike iwapo asingefanya

naye ngono, lakini ukweli ni kwamba ilikaribia kumpoteza rafiki yake wa kike kwa kumwambia

wafanye ngono! Alichokuwa anaambiwa na rafiki zake haikuwa kweli.

Kumbuka, watu wawili wanaweza kuwa na mahusiano ya karibu sana bila ya hata kufanya ngono.

Wanaweza kubadilishana uzoefu; wanaweza kujifunza mambo mengi ya muhimu kuhusu kila

mmoja wao – jinsi kila mtu anavyoona maisha, jinsi watakavyofanya maamuzi pamoja, kila mmoja

atakuwa mwenzi na mzazi wa namna gani na namna kila mmoja anavyoiona mipango ya maisha ya

mwenzake.

Yote haya ni muhimu kabla hujaanza mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote. Mnatakiwa kwanza

muwe marafiki wa kweli. Ngono bila urafiki wa kweli wakati wote ni hatari kwa afya yako na kwa

moyo wako. Unaweza kuumia. Kwa hiyo kwa ajili ya mahusiano yenye afya na afya ya ujinsia –

kuweni marafiki wa kweli kwanza.

MaPenZi

Ni vigumu kutafsiri mapenzi kwa sababu yanahusu hasa hisia. Mapenzi ni kitu kikubwa na kuna

aina mbalimbali za mapenzi. Mapenzi kwa wazazi na marafiki, mapenzi kwa rafiki wa kiume au wa

kike na mapenzi kwa jamii.

Vile vile mapenzi ni hisia ngumu, na watu wanaweza kueleza maana ya mapenzi kwa njia tofauti

kutegemeana na uzoefu wao na mahusiano yao ya kupenda. Mapenzi ni hisia yenye utata na watu

hutoa tafsiri ya mapenzi kutegemeana na uzoefu wa mahusiano ya kimapenzi.

Godfrey, kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 19)

“Siwezi kuyaelezea mapenzi. Ni vizuri sana kuwa katika mapenzi.”

Patrick, kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Mapenzi ni muungano wa watu wawili ukiwa na sanaa ya

kuelewana na kuwa mwaminifu kwa kila mtu.”

Sherifan, kutoka Ghana (umri wa miaka 15)

“Mapenzi ni kitu ambacho kipo kati ya watu wawili. Aidha

mvulana au msichana. Mapenzi ni kushirikiana katika matatizo

na kujaliana”.

Stabisile, kutoka Zimbabwe (umri wa miaka 19)

“Kuwa na mpenzi ni mojawapo ya vitu vizuri duniani”.

jennifer, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Mapenzi ni wewe, familia yako na marafiki kushirikiana

mawazo pamoja. Hivi ndivyo ninavyofahamu kuhusu mapenzi.”

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Kuwa na mpenzi kunaweza kuwa kama uchawi.

Unakutana na mtu maalumu halafu kila kitu

kinabadilika. Jua linaonekana kung’ara zaidi, nyasi

zinakuwa za kijani zaidi na unajiona kama unatembea

hewani.

Kuwa na mpenzi ni tofauti na kumpata rafiki mpya.

Unapokuwa na mpenzi, unaweza kujisikia joto, na

hisia zilizojaa. Unaweza kujisikia kutabasamu kila

wakati kwa sababu mawazo ya yule unayempenda

yanakufanya uwe na furaha. Unataka kuwa na mtu

huyu kila wakati. Unapata njozi za mchana za tamaa

ya mambo yasiyowezekana kuhusu mtu huyo. Kuna

wakati unaweza kupoteza hamu ya kula au kukosa

usingizi usiku.

Sherry, kutoka Ghana (umri wa miaka 19)

“Ni jambo la ajabu. Huelewi kinachokupata. Huwezi kuelezea.

Unajaribu kuacha kumfikiria lakini unagundua mawazo hayawezi

kutoka. Unaweza ukawa unasoma kwa ajili ya mtihani lakini unaona

akili yako haiendani na macho yanavyoangalia ukurasa wa kitabu.”

Sara, kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Nina miaka 18 na yupo mvulana ninayempenda sana. Anapokuwa

mbali na mimi, ninashindwa kuwa makini na kitu chochote.

Anapokuwepo karibu na mimi ninatetemeka na siwezi kufanya

kitu chochote cha maana,hata kama akiniambia nijifanye kama

hayupo. Hisia hizi zinanifanya nichanganikiwe kabisa.”

angela, kutoka Kenya (umri wa miaka 18)

“Inasisimumua kuwa katika mapenzi.Hutaki kumuumiza.Unajisikia

mpya kama vile kitu kimeongezeka.Wakati mwingine kujisomea

inakuwa matatizo.Akikuandikia barua ,itasomwa kwa masaa.

“Penzi la kwanza” ni mojawapo ya uzoefu mzito wa maisha. Kuwa na mpenzi sio sawa na

uzoefu wowote ulioupata ukiwa mtoto. Ni kitu ambacho unatakiwa kukichukulia taratibu.

Usikimbilie. Tunza moyo wako na wa wale unaowapenda wachukulie kwa uangalifu.

Diana, kutoka Zambia (umri wa miaka 17)

“Ninafikiri kuwa mapenzi yaje kikawaida kuliko inavyotokea kwa

vijana ambao wanaenda kutafuta mapenzi badala ya kuacha mapenzi

yawatafute. Watu wanatakiwa kuangaliana kwa njia chanya.

Mapenzi yanaweza kupatikana bila kulazimisha ili usije ukajuta

baadaye.”

89