Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
92

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Sura ya 8

urafiki na mapenzi

Urafiki mzuri na mahusiano mazuri yanakusaidia ujisikie vizuri. Marafiki wazuri

wanakusaidia kutatua matatizo, kukuonyesha mawazo mapya na kushiriki na wewe

katika ndoto za maisha yako ya baadaye.

Wakati mwingine watu unaofikiria ni marafiki zako wanaweza kukushinikiza kufanya

jambo ambalo hulitaki, kama vile kujamiiana au kula madawa ya kulevya. Hii tunaita

shinikizo la kundi rika. Mtu yeyote anayekushinikiza ufanye jambo ambalo hutaki

kulifanya sio rafiki mzuri. Usiruhusu mtu yeyote akakushinikiza ufanye jambo ambalo

unajua ni makosa na ni hatari kwako.

Marafiki wazuri wanaweza wakawa wa jinsi moja au jinsi nyingine. Wavulana na wasichana

wanaweza kuwa marafiki bila ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Maneno

“rafiki wa kiume” au “rafiki wa kike” sio lazima yamaanishe kwamba mahusiano ni ya

kimapenzi. Marafiki wa jinsi tofauti wanaweza kuwa na urafiki wa karibu na kupendana

sana bila ya ngono.

Inaweza ikawa vigumu kuelewana na mtu wa jinsi nyingine kwa sababu wavulana na

wasichana hawana uhakika nini mwingine anataka katika mahusiano. Kumbuka, watu

wengi – wavulana na wasichana – wanataka mambo yanayofanana katika mahusiano.

Wanataka heshima, uaminifu, ukweli, kuelewana na kujali.

Kama unamtaka msichana au mvulana unayempenda, jaribu kuvuta subira na kuwa

mkweli. Kuwa mwema. Toka, nenda ukamwone. Kama anaelekea kupenda nia yako,

mwombe kama mnaweza kwenda kushiriki shughuli fulani kwa pamoja.

Kujenga mahusiano mazuri kunachukua muda na uvumilivu. Ngono sio njia nzuri ya

kujenga mahusiano. Ukweli ni kwamba ngono inaweza kuharibu mahusiano. Kujamiiana

haina maana ya kwamba watu wawili wanapendana au urafiki wao ni wa karibu sana.

Ngono bila urafiki wa kweli ni hatari kwa afya yako na moyo wako.

Kumpenda mtu ni jambo nzuri sana, mapenzi yanakufanya ujisikie vizuri mwenyewe na

mtu mwingine. Furahia hisia lakini usikimbilie jambo lolote. Kumbuka mapenzi yanahusu

heshima na kujaliana. Mapenzi hata siku moja yasiwe sababu ya kufanya jambo

ambalo litaweka afya na maisha yako ya baadaye hatarini. Mapenzi hayawezi kuwa

kisingizio cha kufanya ngono isiyo salama.

Mahusiano hayadumu milele. Kama ukiachwa, sio vizuri kulazimisha mahusiano. Kuwa

mkweli kwa rafiki yako, lakini kuwa na huruma na umfikirie pia. Jaribu usiumize hisia

zake.

Kama mtu amekuacha, unaweza kuhuzunika sana na kujisikia mpweke. Lakini usikate

tamaa. Siku moja utampata mtu mwingine sahihi wa kumpenda. Jipe muda wa kustahimili

ulichopoteza. Usikimbilie mahusiano mapya na usieneze uzishi kuhusu mtu huyo.

Ujinsia Na Ngono

Kuna utata mwingi sana kuhusu neno ujinsia (sexuality) na kujamiiana. Watu wengi wanafikiri

ujinsia maana yake ni kujamiiana. Wengine wanafikiri kwamba huwezi kuwa binadamu hai

mwenye ujinsia na mwenye hisia za kimapenzi hadi uanze kujamiiana.

Imani hizi si za kweli; kila mtu anao ujinsia tangu

kuzaliwa hadi kufa.

Kuwa na ujinsia kunaweza kumaanisha:

Kujisikia unavutia na mwili wako

umejengeka vizuri.

Kujisikia mwenye hisia za kuwa karibu na

mtu fulani.

Kufurahia kuguswa na kukumbatiwa.

Kujishika mwili wako mwenyewe.

Kuvutiwa na mtu mwingine.

Kufikiria hadithi za kimapenzi akilini

mwako.

Kuwa na mawazo au hisia za kimapenzi.

Wakati wa ujana balehe ndio muda ambao

unaweza kuutambua zaidi ujinsia wako -

unavyojisikia, unavyofikiri, unavyojiheshimu

kama mvulana au msichana, na unachokitaka

kuhusu uhusiano wa karibu au pendo la mtu.

Ulipokuwa mdogo pengine hukufikiria kuhusu

mambo haya lakini wakati wa ujana, unaweza

kuanza kufahamu maana ya kuwa mwanaume

au mwanamke. Pia unaweza kuanza kuvutiwa

na watu wengine na kuanza kuona hisia za

kimapenzi, matamanio na ndoto.

UNAJUA maana ya “Ujinsia”?

Ujinsia ni suala lenye utata kueleweka. Ni

zaidi ya kujisikia hisia za kimapenzi au

kujamiiana. Ujinsia ni pamoja na:

Kufahamu na kuwa na hisia kuhusiana

na mwili wako na miili ya watu wengine.

Uwezo wako na nia ya kuwa karibu na

mtu mwingine.

Uelewa wako kuhusu nini maana ya

kuwa mwanamke au mwanaume.

Hisia za mvutano wa kijinsia na watu

wengine.

Uwezo wako kimwili wa kuzaa.

Ujinsia ni muhimu, unafurahisha, na ni

sehemu ya asili ya kuwa mtu. Lakini wakati

mwingine watu wanatumia ujinsia wao

katika namna isiyofaa kwa kushawishi,

kuamuru au kutania watu wengine. Hii ni

pamoja na kuonyesha mapenzi kwa mzaha,

upotoshaji na unyanyasaji kijinsia kama

kubaka/kunajisi n.k. Usitumie ujinsia kama

kifaa cha kupata kitu au kunyanyasa au

kumuumiza mwingine.

93

SURA YA 9