08.06.2013 Views

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

66

Kutatua tatizo na kufikiri kwa

ubunifu: Ili kupata ufumbuzi wa

matatizo kunahitaji kufikiri kwa

ubunifu. Kufikiri kwa ubunifu ni uwezo

wa kufikiri ufumbuzi wa tatizo usio

wazi. Ni uwezo wa kusumbua akili

yako ili kupata fumbuzi mbalimbali

bila kujiwekea mipaka ya mazoea

uliyoyasikia ya utatuzi wa jambo fulani.

Kwa mfano: fikiria kuwa umepata

mimba ukiwa unasoma shule. Wasichana

wote unaowafahamu waliopata mimba

waliacha shule na hawakuweza kumaliza

masomo. Kufikiria kwa ubunifu maana

yake ni kutokudhani kwamba lazima

uache shule eti kwasababu wasichana

wengine waliacha. Labda inawezekana

ukakaa shuleni ukiwa na mimba. Au

unaweza kurudi shuleni baada ya

kujifungua mtoto. Labda kipo kituo kwa

ajili ya vijana waliozaa ambako unaweza

kuendelea na masomo au mafunzo.

Kufikiri kwa ubunifu kunahusisha

kuzungumza na watu wengine. (walimu,

vijana washauri wazazi, shangazi,

wajomba marafiki) na kuchunguza

chaguzi zote zilizoko mbele yako.

Stadi za makubaliano. Hizi ni stadi

ambazo unahitaji ili kutatua tatizo au

tofauti ulizonazo na watu wengine.

Kwa mfano, unaweza ukataka kutoka

na rafiki yako, lakini wazazi wako

wanataka ukae nyumbani. Hali kama

hii inahitaji stadi nzuri za makubaliano.

Inaweza ikawa vigumu kukubaliana

na wakati wingine kukatishwa tamaa.

Unaweza kujisikia kama upasuke,

kwamba umevunjika moyo kiasi cha

kusema “potelea mbali” na kuondoka

ukiwa umekasirika na kuchoshwa.

Lakini unahitaji kuwa mvumilivu na

mtulivu wakati unaeleza kwa nini

unajisikia hivyo, na kile unachohitaji.

Vilevile unahitaji kuwa mkweli, mtu

unayeelewa na kuheshimu yale ambayo

watu wengine wanayahisi na kuyahitaji.

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Je, unajua maana ya kutatua tatizo kwa

ubunifu bila woga wala jazba?

Anne ana umri wa miaka 16 na ni yatima.

Anaishi na shangazi yake ambaye anamtaka

afanye kazi dukani kwake kila siku baada ya

kutoka shule. Hili ni tatizo kubwa kwa Anne.

Hapati muda wa kutosha wa kujisomea.

Ameanza kufadhaika kwa vile mitihani

inakaribia. Hapati usingizi vizuri usiku kwa

sababu ana wasiwasi sana kuhusu masomo.

Ameanza kumchukia shangazi yake.

Anashangaa iwapo shangazi yake anamwona

kama kitendea kazi na kwamba hampendi

wala kujali maisha yake ya baadaye.

Anne anajitambua. Anajua kuwa anayo

tabia ya kuficha hisia zake mpaka

anapolipuka kwa hasira. Tabia hii haimsaidii

sana. Shangazi yake naye anakasirika na

kusema ameanza kukosa heshima.Safari hii

anaamua kufanya mambo tofauti. Badala

ya kumwambia shangazi yake kiugomvi

“Hunipendi” anamweleza shangazi yake bila

woga wala jazba “Ninawasiwasi sana kuhusu

mitihani yangu lakini nataka pia kukusaidia

kazi za dukani”. Hapa ameonyesha tabia ya

kujiamini.

Kwa kujieleza mwenyewe kwa njia hii,

Anne amesimama imara na kuomba

muda zaidi wa kujisomea. Lakini kwa

wakati huo huo anaelewa shangazi yake

anahitaji msaada wa dukani. Anaonyesha

ushirikiano kwa shangazi yake ambaye ana

majukumu mengine. Akifuata utaratibu huu,

shangazi naye anaelewa pia. Kwa pamoja

wanafikiri kwa ubunifu kutatua tatizo hili.

Wanatengeneza ratiba inayompa Anne muda

zaidi wa kujisomea jioni na pia kumsaidia

shangazi yake jioni inapokuwa lazima.

Inatia moyo kwa jinsi Anne alivyojisikia

vizuri. Ghafla mfadhaiko unapungua na

anaweza kuyafurahia maisha tena.

Hata hivyo sio kila tatizo linaweza kujadiliwa na kufikia maelewano. Wakati mwingine

utalenga katika matokeo ambayo yatakufanya uwe salama, hata kama mtu mwingine

hatafurahia. Mathalani, rafiki yako wa kike au wa kiume amekataa kutumia kondomu

pamoja na kumshawishi kwa nguvu zote. Katika hali kama hii zingatia usalama wako.

Ondoka sehemu hiyo ikibidi.

Msimamo: Msimamo ni stadi ya msingi katika kuelewana na watu wengine. Msimamo

maana yake kutetea na kuyaenzi yale unayoyaamini wewe mwenyewe. Kuwa muwazi na

mwaminifu kwako mwenyewe na watu wengine kuhusu kile unachokihitaji na kukitaka.

Watu ambao hawana msimamo juu ya maisha yao huwa ni wanyenyekevu. Hata kama

wanatendewa vibaya, hawajitetei. Watu ambao hawana msimamo mara kwa mara

wanakosa imani ya kujienzi na kutetea mahitaji yao na kulinda hisia zao au hata miili yao ili

wasiumizwe.

Msimamo ni tofauti sana na kuwa mgomvi. Watu wagomvi ni watundu na hawana huruma,

hawajali watu wengine wanahisi nini. Sio vizuri kuwa mgomvi kwa faida ya afya ya hisia

kwa sababu, kwa undani kabisa, utajisikia vibaya kutokuwa na huruma kwa wengine.

Misingi ya msimamo:

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

• amua unachohisi au unachotaka na kiseme. Usiogope kuwa mkweli kuhusu hisia

zako. Watu wanatakiwa kuziheshimu hisia hizo. Kwa mfano, labda ulijisikia vibaya na

unakosa raha baada ya rafiki yako wa kiume kukugusa sehemu zako za siri. Unatakiwa

kumwambia, “Nilikosa raha uliponigusa sehemu zangu za siri sitaki uniguse hivyo tena”.

Mtu anayekupenda kweli hatataka kufanya vitendo ambavyo vinakukosesha raha.

• Mtazame mtu machoni: Kumwangalia mtu machoni ni kudhihirisha msimamo wako.

Inamjulisha mtu mwingine kwamba hutanii kuhusu kile unachokisema na kwamba

unaangalia kama wanakusikiliza au hawakusikilizi. Tamaduni nyingi haziungi mkono

kumwangalia mtu machoni wakati wa mazungumzo. Wakati mwingine katika maeneo

mengine huliona jambo hili ni ufedhuli (kutokuwa na ustaarabu/heshima) kijana

mdogo anapomwangalia mtu mzima moja kwa moja usoni. Unaweza kufuata mila na

desturi, kama kupiga magoti, kuonyesha heshima lakini kwa wakati huo huo endelea

kumwangalia mtu huyo usoni kama unataka kuonyesha ujasiri/msimamo wako.

• usitoe visingizio. Hisia zako ni sababu tosha. Kwa mfano, kama hujisikii kufanya

mapenzi lakini rafiki yako wa kike au kiume anakulazimisha, epuka kutumia watu

wengine kama kisingizio. Usiseme, “mama yangu karibu atarudi nyumbani au tumbo

linaniuma au ninaogopa kupata mimba au nina kazi ya kusoma kwa hiyo sio muda mzuri

kwangu”. Unaweza ukamchanganya rafiki yako na visingizio hivi. Anaweza kudhani

unataka kwenda sehemu nyingine, au kwamba labda unataka kutumia kondomu.

Anaweza asitambue kwamba unachotaka kumwambia ni “siko tayari kufanya tendo hilo

kwa hiyo sitaki”. Kwa hiyo basi sema kile unachotaka.

• usisemewe na mtu mwingine. Iwapo hutaki kufanya jambo fulani, sema mwenyewe

na usiulize mtu mwingine kama ni sawa. Kwa mfano, kama mtu ana kushawishi unywe

pombe au madawa ya kulevya usiseme; “nisingependa, lakini kama unaona sawa …?

Badala yake sema “Hapana, ninashukuru.

67

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!