Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
138

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Utoaji mimba usio salama ni hatari sana. Unaweza kupoteza maisha yako.

Kama wewe au yeyote unayefahamu anakabiliwa na mimba isiyotakiwa, tafuta msaada. Kuwa

mwaminifu kwa wazazi /walezi kuhusu hali hiyo. Kama wazazi wako hawakusaidii tembelea kituo

cha vijana na mwombe mshauri wa vijana ushauri kuhusu suala lako. Mwombe mshauri wa vijana

akuelekeze wapi unaweza kwenda kuzungumza na mhudumu wa afya anayejali na mpole.

Kama wewe au yeyote unayemjua alitoa mimba na hajisikii vizuri, nenda hospitali haraka. Kuvuja

damu, homa ya baridi, homa na/au kutoka majimaji yenye harufu ni dalili kwamba kuna mahali

pana matatizo makubwa. Afya yako na maisha yako yapo hatarini hivyo uchunguzi wa waganga

ni muhimu sana. Hata kama sheria ni kali kiasi gani, wahudumu wa afya wana miiko ya kitalaamu

ya kumsaidia yeyote atakayekuwa na matatizo. Usiache woga ukuzuie kupata matibabu na

hatimaye ukapoteza uhai.

Njia nzuri ya kujikinga mwenyewe dhidi ya matokeo ya kutoa mimba kwa njia isiyo salama ni

kukwepa kupata mimba isiyopangwa ama kuepuka ngono nzembe.

naMna Ya KuePuKa KuPata MiMba

Njia ya uhakika kabisa ya kutopata mimba ni kuacha kufanya ngono. Uzuiaji huu una uhakika wa

asilimia 100, na ni salama kihisia na kimwili. Kama hujamiiani, hakuna jinsi unavyoweza kupata

mimba au kumpa mimba msichana.

Ikiwa unajamiiana, hakikisha pia kuwa wewe na mwenzi wako mnatumia kondomu kujikinga dhidi

ya mimba na magonjwa ya ngono. Unatakiwa pia kuomba msaada kutoka kliniki ya uzazi wa

mpango. Unahitaji kuchukuwa hatua ili mwenzi wako asipate mtoto ambaye huwezi kumtunza

kwa wakati huu.

Kuna aina nyingi za dawa za kuzuia mimba ambazo ni salama kabisa kwa vijana (angalia

kisanduku ukurasa wa 140). Njia yoyote utakayotumia, hakikisha unaitumia inavyotakiwa. Kwa

mfano, kusahau kumeza kidonge kunaweza kusababisha upate mimba.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

je, ViDOnGe VYa KuZuia MiMba ni SalaMa?

Uvumi kama huu ni uwongo na si wa

kisayansi. Tangu miaka ya 1950, mamilioni

kwa mamilioni ya wanawake wametumia

dawa za vidonge za kuzuia mimba. Vidonge

vya kuzuia mimba vimefanyiwa uchunguzi

mkubwa katika historia ya dawa. Kwa

kuyafuatilia maisha ya maelfu ya wanawake

kwa miaka mingi waganga sasa wanajua

kwamba vidonge vya kuzuia mimba havileti

saratani. Uwezekano wa wanawake

wanaomeza vidonge kupata saratani ya

kokwa la mayai na uwezekano wa kupata

saratani kwenye ngozi laini ya kuta za

tumbo la uzazi ni mdogo kuliko wanawake

ambao hawajawahi kutumia vidonge hivyo.

Kuna uvumi mwingine kwamba kutumia vidonge vya kuzuia mimba wakati wa ujana balehe

kunaweza kuharibu kokwa la mayai na kusababisha isiwezekane kupata mimba baadaye. Huu pia

ni uzushi.Mwongozo wa kimataifa wa kutumia dawa za kuzuia mimba unasema vidonge ni vizuri

kwa wanawake ambao bado hawajapata watoto. Ukweli ni kwamba ,mara nyingine vinatumika

kuwasaidia vijana balehe kuwapunguzia maumivu makali wakati wa hedhi. Huhitaji kuwa na

mtoto kwanza ndipo uanze kumeza vidonge. Vidonge havitaharibu kokwa la mayai.

Wasichana na wanawake wengine wanapata kichefuchefu, matiti kuwa laini na kuongezeka

uzito wanapoanza kumeza vidonge. Matokeo haya huwa yanatoweka baada ya mwezi mmoja au

zaidi. Karibu wanawake wadogo na wanawake wa makamo wote wanaweza kumeza vidonge. Ni

wanawake wa makamo tu ambao wanaovuta sigara, walio wanene sana au wanashinikizo la damu

au magonjwa fulani kwenye mfumo wao wa damu wanashauriwa wasitumie njia ya homoni kuzuia

mimba (vidonge vya kuzuia mimba, sindano na vipandikizi). Unatakiwa kumwona mtoa huduma ili

akupime kama huna vidokezo vya mteja wa dawa za kuzuia mimba.

KuZuia MiMba KWa DhaRuRa

christine kutoka uganda (umri wa miaka 18)

“Nimesikia kwamba vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha

saratani au pia ulemavu kwa mtoto”.

Kuna njia moja zaidi ya kuzuia mimba ambayo hapana budi kuijua. Hii ni njia ya dharura ya kuzuia

mimba. Njia ambayo unaweza kuitumia kuzuia mimba haraka baada ya kufanya ngono isiyo

salama. Kwa mfano kama ulisahau kutumia kondomu au kama kondomu ilipasuka au ilitoka kwa

bahati mbaya (jambo ambalo ni nadra sana kama ikitumika vizuri).

Kinga ya dharura ya kuzuia mimba imeanza kupatikana sehemu nyingi siku hizi. Kama ukifanya

ngono bila kinga na una wasiwasi wa kupata mimba unaweza kwenda kwa muhudumu wa afya na

kumwomba kinga ya dharura ya kuzuia mimba. Ikiwa umebakwa omba kinga ya dharura ya kuzuia

mimba kutoka kwenye kliniki ya mpango wa uzazi au kituo cha vijana karibu na wewe katika

kipindi cha saa 72 (siku 3).

139