Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
166

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

naMna Ya KuShuGhuliKia ShiniKiZO la KutuMia DaWa

Kumudu shinikizo kutoka kwenye kundirika linalotaka utumie dawa kama wao ni vigumu sana.

Hapa kuna hadithi fupi ya kijana mmoja:-

Je, maelezo haya yanakukumbusha wewe pia hali ambayo imewahi kukutokea ukiwa na wenzako?

Hawa marafiki walikuwa wanahitaji sana Jeckton avute. Kwa nini walimshinikiza?

Watu wengi wanataka kuungwa mkono wanapofanya jambo wanalofikiri siyo sahihi. Wanafikiri

makosa yao yanakuwa madogo kama mtu mwingine anafanya nao. Marafiki zao wanapofanya

jambo la kijasiri pamoja nao, hawajisikii kuogopa sana kuhusu hatari iliyopo. Kama wako katika

kikundi wanajisikia kustarehe na kufurahia burudani wanazozipata kwenye dawa. Ndiyo maana

watakushinikiza sana wewe.

Hapa kuna vidokezo vya jinsi ya kushughulikia hali hiyo:

jeckton kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Nilipokuwa na miaka 13, nilikuwa naelekea nyumbani nikiwa na

baadhi ya marafiki zangu. Tulipita sehemu ambayo marafiki zangu

mara nyingine wanaenda kukutana na baadhi ya marafiki zao.

Tulipofika pale waliwakuta marafiki zao na wakapewa kifurushi

cha bangi. Bila kupita muda, msichana mmoja akaanza kuvuta

na akaniambia nivute pafu moja. Nilikataa, wakaanza kunicheka.

Waliniita majina mabaya na wakaniambia niache kuwaaibisha.

Waliniambia ilikuwa tamu sana na ingenifanya nijisikie vizuri. Kwa

sababu sikutaka waelewe kwamba nilikuwa naogopa, niliamua kuvuta

kidogo. Baada ya kuvuta kidogo, siwezi kusema yaliyotokea

baada ya hapo maana sikumbuki tena. Nilichanganyikiwa kwa

muda wa karibu siku tatu.”

Kumbuka kwamba huhitaji kumfanya rafiki ajisikie vizuri kwa kumuunga mkono kufanya

mambo ambayo siyo mazuri kwako.

Kama ni rafiki wa kweli, unaweza kumwambia rafiki yako kuwa mambo anayoyafanya ni ya

hatari.

Uwe mwazi kwa wenzio kwamba hutaki kutumia dawa au kitu. Waonyeshe rafiki zako

kwamba unazijua akili zako zilivyo na kwamba hata wakikusihi vipi hutabadilisha mawazo

yako.

Ondoka kama rafiki yako anazidi kukushinikiza au anaanza kukutukana ama kukucheka.

Usiendelee kujadili suala hilo zaidi. Subiri hadi atakapokuwa hatumii dawa ndiyo mwanze

kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Kofi kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Huwa nashinikizwa na marafiki zangu kutumia dawa za kulevya

ninapokuwa nao, lakini ninajizuia mwenyewe na kuwaeleza kwa

ujasiri kabisa kwamba nimeridhika bila ya kutumia dawa.”

Mara nyingine tatizo linaweza kuwa kubwa zaidi kuliko kukataa shinikizo toka kwa marafiki.

Unaweza kugundua kwamba rafiki yako analo tatizo kubwa la dawa au pombe, tatizo ambalo

unaona linamharibia maisha yake. Hili nalo ni gumu kulitatua. Haya ni mambo machache

unayoweza kufanya:

SURA YA 13 | MATUMIZI MABAYA YA DAWA

Zungumza na rafiki yako kuhusu matumizi ya dawa wakati hajanywa au hayuko katika hali ya

ulevi.

Usimlaumu au kumkosoa rafiki yako. Hii itazua mabishano baina yenu. Badala yake lenga

katika matatizo ya dawa na mwonyeshe rafiki yako kwamba unaogopa. Jaribu kumsaidia

rafiki yako aelewe kwamba ana matatizo.

Jaribu kumsaidia rafiki yako apate msaada na jaribu kumsaidia akwepe sehemu ambayo

atapata shinikizo la kutumia dawa au pombe.

Margaret kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Wengi wa marafiki zangu walikuwa wameshaharibiwa na dawa;

lakini baada ya kujua hatari na ukweli kuhusu dawa niliamua kuwasaidia

marafiki zangu. Wengi wamebadilika na mimi ninafurahi.”

Wakati mwingine watu wenye matatizo kutokana na dawa hawako tayari kukusikiliza wewe na

ushauri wako. Wanaweza kuzikataa juhudi zako za kusaidia na wanaweza kukukasirikia. Mnaweza

mkaishia kuwa na mabishano makali na rafiki zako, lakini angalau dhamira yako itakuwa wazi na

utakuwa umejitahidi kuwasaidia.

Wakati wote upo uwezekano wa urafiki kuvunjika kutokana na tabia yako ya kutokubaliana na

tabia zao.

hanifa kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Nilikuwa na rafiki ambaye nilimwamini sana kwa kipindi kirefu,

lakini sikujua mambo aliyokuwa anayafanya kwa kificho. Siku

moja nilimkuta na watu wenye sura za ajabu, macho yake yalikuwa

mekundu. Niligundua alikuwa ananuka bangi. Nilijaribu kuzungumza

naye mara kwa mara lakini hakunisikiliza. Hivyo nilimtaka

achague ama kuacha kutumia alichokuwa anatumia au kuacha

kuzungumza na mimi. Nilifikiri angefanya uamuzi sahihi lakini

nilikuwa nimekosea aliacha kuzungumza na mimi.”

Inaweza kuwa vigumu sana kumpoteza rafiki lakini angalau ulisimama kwenye kanuni zako,

ulijaribu kumsaidia rafiki na wewe binafsi hukujihusisha na hatari ya dawa. Mara chache, baada

ya muda, rafiki atabadilika.

hanifa kutoka tanzania (umri wa miaka 17)

“Baada ya miezi kadhaa, rafiki yangu aligundua madhara ya dawa

hizo kwa maisha yake, na akaniomba tuendelee kuwa marafiki

tena. Kwa sababu nilimwonea huruma nilikubali.”

167