Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
130

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Kumbuka kuwa mimba inaweza kutokea kama utafanya ngono isiyo salama mara moja tu.

Mimba inaweza kutokea kama mwanamume atakojoa shahawa zake karibu na uke hata kama

hamkujamiiana! Shahawa zikimwagwa nje ya mlango wa uke bado zinaweza kuogelea hadi

kwenye mlango wa mfuko wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi na kwenye mirija ya kupitisha yai.

Utadhani hakuna uwezekano, lakini inatokea.

Dalili Za MiMba

Dalili ya wazi kuwa mimba imetungwa ni kukosa kupata hedhi. Hii ni kwa sababu ukuta wa mfuko

wa kizazi hautoi damu mwanamke akiwa na mimba. Utando laini unabaki ndani ya mfuko wa

kizazi na unatengeneza kiota laini kwa ajili ya mtoto kukua. Kukosekana kwa hedhi haina maana

kuwa umepata mimba. Wasichana waliobalehe wanaweza kuwa na hedhi isiyo ya kawaida. Kwa

miaka mingi siku za hedhi kwa baadhi ya wasichana balehe, zinaweza kuchelewa au zikakosekana

mwezi mzima bila sababu yoyote.

Dalili nyingine za mimba:

Matiti kuwa laini

Kichefuchefu (hali ya kutaka kutapika) na kuwa na mate mdomoni.

Uchovu (kujisikia umechoka sana)

Kutaka kukojoa mara kwa mara

Kupendelea kula vitu fulani,wakati mwingine visivyo vya kawaida.

Wanawake wachache huwa hawaoni dalili zozote kati ya hizo hapo juu. Kwa mfano, wanawake

wengine hutoa damu kidogo sana wakati wa miezi mitatu ya mwanzo ya mimba zao na hivyo

wanaweza kufikiri hedhi imekuwa na damu kidogo kuliko kawaida.

Kama huna uhakika kuwa umepata au hujapata mimba, unaweza kufanya kipimo cha mimba.

Katika sehemu nyingine, unaweza kununua kipimo cha mimba kwenye maduka ya dawa. Vilevile,

unaweza kufanyiwa kipimo cha mimba kwenye kliniki. Mara nyingine kipimo kinafanywa kwa

kupima mkojo na unaweza kugundua viini fulani ambavyo vinatengenezwa na mwili wakati wa

mimba. Dakitari au nesi wa kituo cha afya anaweza vilevile akakufanyia uchunguzi wa mwili ili

kuona kama una mimba au la.

Mimba inachukuwa wiki 40 kabla ya mtoto kuzaliwa(toka mwanzo wa hedhi yako ya mwisho).

Hadi utakapokosa hedhi yako - kama siku 28 baada ya siku ya mwisho ya siku zako za hedhi

iliyopita - kibonge cha seli nyingi, yaani kiinitete kitakuwa kinakua katika mfuko wa kizazi kwa

karibu wiki nzima.

Kiinitete kinakua haraka sana. Wiki sita baada ya hedhi yako ya mwisho, ubongo na uti wa

mgongo vinakuwa vimeanza kutengenezwa na moyo unaanza kupiga. Katika wiki 9 kiinitete

kinaitwa fitasi. Katika wiki ya 12 fitasi inatambulika kama binadamu ila inakuwa na kichwa

kikubwa. Katika wiki 20 (miezi 5) mwanamke anaweza akajisikia fitasi inachezacheza au

kuzunguka ndani ya tumbo lake. Fitasi inaweza kugeuka au kusogea na inaweza pia ikashituka

kukiwa na kelele zenye sauti ya juu.

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Ukuaji na maendeleo ya mtoto ndani ya tumbo la uzazi

hataRi Za MiMba na uZaZi KWa WaSichana balehe

Mimba ni hatari kwa kila mwanamke lakini ni hatari zaidi kwa wasichana balehe. Tatizo kubwa

kwa wasichana chini ya miaka 20 ni nyonga. Mifupa inayozunguka mfereji wa kutolea mtoto

haujakua vizuri. Wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo wanapata taabu katika kuzaa

kwa sababu mlango wa uzazi kwenye mifupa ya nyonga ni midogo mno na mtoto hawezi kupita.

Tatizo hili linaitwa uzazi wa kukwama.

Kama mtoto hawezi kutoka nje inabidi mtoto atolewe kwa njia ya upasuaji. Vijijini, wanawake

wengi wenye matatizo kama haya huwa hawawezi kufika hospitali kwa muda unaotakiwa. Mtoto

anaweza kufia tumboni. Isitoshe mfuko wa kizazi unaweza kuchanika kwa sababu ya kipindi

kirefu cha uchungu na mwanamke anaweza kufa kwa kuvuja damu nyingi. Hii ni sababu mojawapo

inayowafanya wasichana balehe wengi wadogo kufa wakati wa kuzaa.

131