Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
172

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Ndoto yako ni nini? Ungependa uwe nani? Unajifikiriaje mwenyewe katika miaka mitano ijayo?

Katika miaka15? Utakuwa nani na utakuwa unafanya nini?

Sura hii inahusu kutimiza ndoto zako. Inahusu kuzifikiria ndoto zako na kutafakari ni kwa vipi

unaweza kuzifikia. Inahusu kufanya uamuzi mzuri wa busara na utakaokufikisha karibu na ndoto

zako. Aidha, inahusu namna ya kumudu vipingamizi vitakavyojitokeza katika maisha.

Si jambo rahisi kufanikisha ndoto. Inahitaji kufanya kazi kwa bidii na kuwa na dhamira/nia. Kwa

hiyo, jambo muhimu ni kujishughulisha na kufanya kazi kwa bidii. Fanya vitendo! Usikae chini na

kusubiri mambo yakutokee. Unatakiwa kuyajenga maisha yako ya baadaye.

KuZitaMbua nDOtO ZaKO.

Watu wengine wana ndoto nyingi sana na zinabadilika kila wakati. Kwa mfano mchukue Remijia

wa Tanzania:

Alipokuwa na miaka 6 alitaka kuwa ofisa wa polisi.

Alipokuwa na miaka 8 alitaka kuwa kapteni wa meli.

Alipokuwa na miaka 10 alitaka kuwa rubani wa ndege.

Alipokuwa na miaka 13 alitaka kuwa mwalimu.

Sasa ana miaka 19 anataka kuwa mhandisi.

Kwa nini ndoto hubadilikabadilika? Je, ni vibaya kuwa na ndoto nyingi

zilizo tofauti? Hapana! Ndoto ni nzuri, zinatia hamasa na zinakufanya

ufanye kazi kwa bidii. Zinakufanya uangalie maisha ya baadaye na

uwe na mipango thabiti.

Watu wengine wanaelekea kuwa na ndoto chache. Hawajui

wangependa wawe nani wakiwa wakubwa. Wanapata shida kujifikiria

watakuwa vipi miaka 5 ijayo.

Kama yanakugusa, usihofu. Hili ni jambo la kawaida! Haina maana

kuwa huna ndoto, bali ina maana kuwa bado hujafikiria ndoto zako ni

zipi. Lakini, unaweza kuanza sasa kuzitambua ndoto zako.

Ndoto za watu wengi zinaathiriwa na watu wanaowazunguka. Kwa

hiyo, kwanza angalia unazungukwa na nini. Fikiria kuhusu watu

walio ndani ya jamii. Ni nani unaowahusudu? Ni watu gani

unaowaheshimu? Mtu anaweza kuwa mwalimu

ambaye anajua majibu ya maswali yote

yanayoulizwa. Anaweza kuwa ni daktari

ambaye alijua kilichokuwa kinakufanya

uumwe miezi michache iliyopita.

Anaweza akawa mchungaji wa kanisa

lako. Wanaweza kuwa wazazi wako.

Pata muda wa kutafakari ndoto zako za baadaye

SURA YA 14 | KUTIMIZA NDOTO ZAKO

Pili, usiruhusu ndoto zako zikakwamishwa na mambo unayoyaona. Angalia hata nje ya jumuia

yako. Kuna mtu ambaye umemsoma kwenye gazeti au kitabuni ambaye alifanya jambo ambalo

linakushangaza? Pengine ni mwanasayansi ambaye anajifunza jinsi tembo wanavyowasiliana wao

kwa wao. Pengine ni muuguzi anayewahudumia wakimbizi katikati ya uwanja wa vita. Wapo watu

wengi wanaofanya mambo mengi mazuri yanayovutia na yenye manufaa na maisha yao. Watu

hawa wanaweza kuwa mfano mzuri wa kuigwa. Wanaweza kukuanzishia ndoto kuhusu maisha

yako ya baadaye.

Tatu, yaruhusu mawazo yako “yapae angani” usijiwekee mipaka ya vitu ambavyo unaweza

kufanya au ambavyo huwezi kuvifanya. Kwa mfano, usiiache ndoto kwa sababu ya mawazo

yaliyopitwa na wakati, kama mawazo kuhusu kazi wanazoweza kufanya wanaume pekee au

wanawake pekee. Mambo yanaenda yakibadilika. Wanawake siku hizi wanafanya kazi ambazo

mama zao hawakuwahi kufikiria kuzifanya. Sasa hivi wanawake wanaweza kuwa wahandisi,

marubani, madaktari, wanariadha, wanasayansi, maprofesa, wanaanga, Marais, waandishi wa

habari n.k. Kama ni mvulana au msichana, unaweza kuwa mtu unayetaka kuwa, ikiwa utadhamiria

na kufanya kazi kwa bidii.

MiPanGO Ya baaDaYe KuhuSu KaZi

Vijana balehe wachache wana vipaji vya ziada katika taaluma fulani, kama hisabati, muziki au

kuchora. Utafikiri kipaji kimewachagua. Wanakuwa wataalamu wazuri wa hisabati, wasanii,

walimu na viongozi wa kwaya au wasanifu majengo.

Watu wengine wanapendelea kitu kimoja tangu utoto wao, na mvuto huo mkubwa unarahisisha

sana wakati wa kutoa uamuzi kuhusu watakuwa nani. Unaweza kumsikia mzazi akisema “wakati

wote tulijua kwamba John atakuwa mganga wa mifugo. Alianza kuwahudumia wanyama wadogo

alipokuwa na umri wa miaka minne tu.

Watu kama hawa, maisha yao yanaonekana kuwa rahisi. Inaonekana kana kwamba njia yao ya

kazi imenyooka. Uamuzi wao unaonekana kuwa ni rahisi kwa sababu wanajua kabisa wanataka

kufanya nini, na wanacho kipaji katika eneo hilo maalumu.

Wengi hatuko hivyo. Wengi ni watu wa kawaida, wenye akili ambao tunaweza kufanya vizuri

katika mambo tofauti. Uwezekano wa kuwa nani au kufanya nini ni matokeo ya mchanganyiko wa

yale tunayoyapenda na tusiyoyapenda, uwezo wetu na utayari wa kufanya kazi kwa bidii na fursa

tunazopata.

Kufanikisha ndoto kwa watu wengi ni njia ndefu yenye kona nyingi. Wakati wote siyo moja kwa

moja na hatua sahihi za kuchukua haziko wazi. Zaidi ya hapo vikwazo visivyotegemewa vinaweza

kujitokeza njiani. Ni mambo ambayo yanatakiwa kushughulikiwa kwa makini sana.

Jitahidi kujitokeza kwenye kazi nyingi iwezekanavyo. Bila kufanya hivyo huwezi kufahamu nafasi

gani zipo duniani kwa ajili yako? Katika nchi nyingine, vijana balehe wanajitolea kufanya kazi

katika mashirika mbalimbali wakati wa likizo. Wakati mwingine wanapata malipo kidogo ya

kutosha usafiri kwenda na kutoka nyumbani. Lakini mara nyingi hawapati chochote. Wanajitolea

tu.

Usifikiri kwamba kwa vile jambo fulani siyo la shule na siyo la kazi ya kulipwa basi halina

thamani. Iwapo unaweza kupata kazi ya kujitolea, pengine unaweza kupata uzoefu mzuri na

wenye manufaa.

173