08.06.2013 Views

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

12

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Pia, weka akilini haya: Watu wa umri wako mara nyingi wanajua taarifa nyingi za uongo kuliko za

ukweli hasa inapokuwa ni za kuelezea balehe na kujamiiana. Marafiki zako wanaweza kukueleza

mambo ambayo si ya kweli, hivyo unahitaji kufahamu wapi uende ili kupata ukweli. Kwa mfano,

unaweza kuambiwa kwamba, matiti au uume utakua iwapo utajamiiana. Au unaweza kutaniwa

kwamba matiti yako ni makubwa kwa sababu umekwishajamiiana. Hali kadhalika unaweza

kusikia kwamba chunusi ni dalili za kwamba unatakiwa ujamiiane. Lakini hakuna lolote katika

haya lenye ukweli. Yote ni uzushi/uwongo.

Uzushi kama huu unaweza kuleta hatari zaidi kwa sababu unaongeza hofu. Uzushi kama huu

unakufanya ufikirie kwamba unaweza kufanya mambo ili kubadilisha yale ambayo huwezi

kuyadhibiti.

VichOcheO (hOMOni)

Ni kitu gani hudhibiti mabadiliko ndani ya mwili wako? Ni kitu gani hufanya ukue haraka au

taratibu? Ni kitu gani hukufanya uongezeke?

Mwili wako wakati wote unatengeneza homoni, ambazo ni kemikali tarishi maalumu ambayo

huuambia mwili namna gani na lini ubadilike na kukua. Mfoko wa ukuaji wako husababishwa na

homoni za ukuaji ambazo zinatoka kwenye ubongo kwa wingi.

Pamoja na homoni za ukuaji, homoni za jinsi nazo huanza kutolewa wakati wa balehe. Kwa

wasichana homoni za jinsia zinatengenezwa ndani ya ovari na kwa wavulana zainatengenezwa

ndani ya korodani. Homoni za jinsi ndizo zinazosababisha tofauti katika maumbile ya mwanaume

na mwanamke. Wasichana wanapoingia kipindi cha balehe nyonga zao huongezeka. Kawaida

nyonga hukua haraka kuliko kifua . Nyonga ya msichana hupanuka na kujiviringa, na kiuno

huonekana kidogo na chembamba. Matiti vilevile huanza kukua.

Kwa wavulana, homoni za jinsia husababisha kifua kupanuka, mikono na miguu inakuwa minene

yenye misuli. Matiti ya wavulana hayabadiliki sana kama ya wasichana yanavyobadilika wakati

wa balehe, lakini hubadilika kidogo. Kwa wavulana wengine, matiti yao hukua kipindi cha balehe

lakini kawaida hupotea kadri muda unavyokwenda.

Homoni huathiri pia hisia zako. Vijana wengi hujisikia kuwa na hisia kali. Dakika moja tu anaweza

kuwa na furaha na msisimko, lakini dakika inayofuata akawa na huzuni karibia kulia. Anaweza

kujisikia vizuri siku moja na vibaya siku inayofuata. Mabadiliko haya katika hisia yanaitwa “hisia

za kuyumba”.

Kipindi cha balehe huwa kina ambatana na hisia kali

SURA YA 2 | MABADILIKO YA MWILI

Jambo hili huwatokea vijana wengi mara kwa mara. Wakati wa ujana balehe, utengenezaji wa

homoni huongezeka ghafla, kitendo ambacho huwafanya vijana wengi wawe na hisia kali za aina

mbalimbali.

Baadaye katika maisha utengenezaji wa homoni utapungua na utajisikia unao uwezo wa kudhibiti

hisia.

Weka akilini kwamba mabadiliko yote ya kimwili, kihisia na kiakili yanayotokea wakati wa balehe

yanasababishwa na homoni zinazotengenezwa na mwili wako. Hakuna unaloweza kufanya

kuharakisha au kuchelewesha utengenezaji wa homoni. Jaribu kukumbuka tu kwamba wewe ni wa

pekee na huna kasoro yoyote.

Via VYa uZaZi “SeheMu Za SiRi”

Pamoja na kuleta mabadiliko katika umbo la mvulana na msichana, homoni hufanya via vya

uzazi kukua. Via vya uzazi maana yake ni zile sehemu za siri za mwili wako ambazo mara nyingi

zinafunikwa na chupi/nguo za ndani.

Kabla hujawa kijana balehe, sehemu za siri zilikuwa kwa ajili ya kujisaidia tu (kukojoa). Wakati wa

ujana balehe hata hivyo, sehemu za siri zinakuwa kubwa. Kwa wasichana ngozi na tishu huwa laini

na yenye mafuta mafuta, kwa wavulana uume huanza kurefuka na kunenepa. Korodani vilevile

hukua na kuanza kutengeneza mbegu za kiume.

Kipindi cha balehe via vya uzazi huanza kutengeneza majimaji pia.

Wavulana huanza kutengeneza shahawa, majimaji yaliyo kama kamasi ambayo mbegu za kiume

huogelea. Shahawa hutoka nje ya uume wakati mvulana anapofikia mshindo. Wasichana vilevile

hutoa majimaji ya ukeni na damu ya hedhi. (soma sura ya 3 na ya 4 kwa maelezo zaidi kuhusu

wavulana na wasichana)

nYWele Za MWilini na MabaDiliKO Ya nGOZi

Ngozi yako na nywele za mwilini hubadilika vilevile katika kipindi cha balehe. Kwa vijana wengi

ngozi inakuwa na mafuta. Ngozi ya utotoni hupotea. Hii hupelekea chunusi kutoka, jambo ambalo

ni tatizo la kawaida kwa vijana wengi (soma sura ya 5 kwa maelezo zaidi kuhusu utunzaji mzuri

wa ngozi).

Dalili nyingine ya balehe ni nywele kuota sehemu mpya za mwili. Wavulana na wasichana wote

wanaweza kuota nywele kidogo miguuni na mikononi. Kwa kuongezea wavulana huota nywele

sehemu za siri, usoni kifuani na kwapani. Wasichana vilevile huota nywele sehemu za siri na

kwapani.

Nywele zinazoota sehemu za siri zinaitwa mavuzi, watu wengine wana mavuzi mengi na wengine

wanayo kidogo. Mavuzi husaidia kufanya eneo la via vya uzazi liwe safi, jambo ambalo ni zuri

sana kwani ngozi inayozunguka via vya uzazi ni laini/nyororo sana na ni rahisi kuumia.Mavuzi

husaidia kuzuia jasho na vitu vingine kutoka kwenye ngozi laini ya via vya uzazi.

13

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!