Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
48

utaFanYa nini na chunuSi

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Chunusi ni jambo la kawaida kwa vijana balehe. Kwa bahati mbaya , hakuna jinsi tunavyoweza

kuzikwepa kabisa; wala hakuna matibabu ya ajabu ya kutibu chunusi. Hata hivyo, yapo mambo

kadhaa ambayo unaweza kuyafanya ili kushughulikia chunusi.

Ni jambo muhimu sana kutunza ngozi yako, hususani kama unaishi sehemu zenye joto, vumbi

na unyevu unyevu. Unaweza kutumia sabuni ya kuogea na maji ya uvuguvugu kuosha taratibu

sehemu za mwili wako zenye mafuta – usoni, shingoni, mabegani, mgongoni na juu ya kifua.

Ukiosha sehemu hizi angalau mara moja kwa siku itasaidia kuondoa mafuta kwenye ngozi na

kusababisha vinyweleo kuwa safi na wazi.

Lakini usisugue sana ngozi yako au kutumia sabuni zenye nguvu na kali kwa sababu zinaweza

kusumbua ngozi yako na kusababisha chunusi zaidi. Kamwe usitumie sabuni za kufulia, sabuni

ya unga na dawa ya madoa, kwani zitaharibu ngozi yako. Jaribu kutoruhusu mafuta unayopaka

kichwani yasifike usoni kwa sababu mafuta haya yanaweza kuzuia vinyweleo vya ngozi yako.

Mwisho, kuwa mwangalifu na matumizi ya krimu za usoni na zile za kung’arisha ngozi. Ingawa

zimeandikwa kwamba ukizitumia ngozi yako itakuwa nyororo na nzuri, krimu zingine zinaharibu

ngozi kabisa. Kwa nyongeza, dawa nyingi za kulainisha ngozi zina vitu ambavyo si vizuri kwa afya

yako.

Ingawa wakati mwingine

unashawishika kuminya

chunusi,sio vizuri. Kama

utafanya hivyo, usaha

unaweza kutawanya

maambukizi kwenye

vinyweleo vingine, na

vilevile unaweza kupata

makovu ya kudumu.

Chunusi zinasumbua,

zinaweza kusababisha

maumivu na uchungu, na

zinaweza kuleta usumbufu

wakati mwingine. Lakini ni

sehemu ya ujana balehe.

Vijana wengi wanajihisi

Hata kama unafikiria kwamba chunusi zako ni mbaya, watu wengine

hawajaziona bado.

kuwa ni wao pekee wenye kusumbuliwa na matatizo ya ngozi, lakini hii ni kwa sababu hawajui

kwamba hata wenzao wa rika moja wanazo chunusi. Za kwako zinaonekana zaidi kwako

kuliko watu wengine wanavyoziona chunusi zako. Unaweza kudhani kilamtu anaziangalia, na

anaangalia ngozi yako mbaya tu na wala hakuangalii wewe. Lakini hii sio kweli. Watu wengine

wanayo mambo mengi ya kufikiria na kwa hakika wanachoangalia ni kujua wewe ni nani na wala

sio ngozi yako inaonekanaje. Kwa hiyo, usivunjike moyo na usiache chunusi chache zikunyime

raha! Hautakuwa nazo milele.

utunZaji Wa nYWele

Tunazo nywele mwili mzima, lakini zaidi kichwani, kwapani na maeneo yanayozunguka via vya

uzazi. Kutunza nywele zako ni sehemu nyingine ya kutunza usafi na kutunza vizuri mwili wako.

SURA YA 5 | MABADILIKO YA MSINGI KATIKA KUTUNZA MWILI

Nywele zilizopo kichwani mwako ni rahisi kuzitunza hususani kama utakuwa unazipunguza kila

mara. Hata kama unakata nywele kila mara na kuzisuka, unatakiwa kuziosha ili zisiwe na vumbi

na ziwe safi. Kama uko shuleni, jaribu kutochangia chanio kwa sababu unaweza kupata chawa,

maambukizi ya fangasi, na minyoo. Kama utachangia vitana, hakikisha unaviosha vizuri kwa maji

ya moto yenye sabuni kabla na baada ya kutumia.

Watu wengine wana matatizo ya mba, hali ambayo inasababishwa na ngozi ya nywele kuwa kavu

mno.Mba unasababishwa na chembechembe ndogo za ngozi mfu, na watu wengine wenye mba

nyingi wanatumia shampuu maalumu zenye dawa ili kuzuia mba.

Ni vema kuoga mara kwa mara ili kuziweka safi nywele zilizopo kwenye mwili wako, nywele

zilizopo kwenye kwapa, na nywele zilizopo kwenye maeneo ya via vya uzazi. Kama ulivyosoma

sura ya 2 nywele hizi zinasaidia kuondoa jasho na uchafu kwenye mwili wako. Hata hivyo, sehemu

nyingine za Afrika watu wananyoa nywele hizi kwa vile wanajisikia vizuri bila nywele hizo.

Kama mila na tamaduni zako zinapinga kuwa na mavuzi yakate kwa kutumia mkasi. Usiziondoe

zote kabisa kwa kutumia krimu ya kuondolea nywele au kwa kunyoa. Mafuta ya kunyolea nywele

yanasumbua na kuumiza ngozi laini katika sehemu za siri. Pia kunyoa mavuzi kuna madhara

yake. Kama unanyoa mavuzi, uwezekano wa kujikata ngozi ni mkubwa. Iwapo utajamiiana,

mikato hii ni milango ya kupitishia VVU. Hii ni hatari. Tatizo lingine la kunyoa mavuzi ni wakati

mavuzi yanaota tena. Nywele zinakuwa na incha kali kiasi cha kuweza kutoboa kondomu. Vilevile

maeneo yanayozunguka via vya uzazi yaliyonyolewa yanaweza kupata maambukizi kidogo

kwenye vinyweleo au sehemu ambazo mavuzi yanaota. Kunyoa mavuzi kiasi ni salama kidogo,

lakini kuwa mwangalifu usiondoe nywele zote.

liShe nZuRi

Margareth, kutoka tanzania (umri; miaka 18,)

“Nilipokuwa darasa la sita, nilianza kuota nywele sehemu za siri. Mama

yangu aliniambia kuwa, zikikua na kuwa ndefu ninatakiwa nizipunguze na

kuzisafisha vizuri, la sivyo nitanuka.”

lois kutoka tanzania (umri; miaka 13)

“Nimeona nywele kwenye kwapa, kwa vile sio muda mrefu nilipoziona

sijazikata bado”

Lishe nzuri ni muhimu kwa afya njema. Kula chakula chenye virutubisho ni muhimu katika maisha

yote lakini ni muhimu zaidi wakati wa utoto na wakati wa balehe kipindi ambacho mwili wako

unakua na unaongezeka kwa kasi sana.

Mwili wako unahitaji chakula kizuri ili ukue na upate nguvu kwa ajili ya kufanya vizuri shuleni,

kucheza michezo na kufanya kazi.

Wakati mwingine vijana wadogo hawali mlo wenye lishe na wanasahau kula kwa wakati maalum

uliopangwa. Wanaweza kuacha mlo kamili na badala yake wakakazania kula biskuti, chips,

chokoleti, vitu vitamu na soda. Hivi vyakula havina lishe, na mwili wako unahitaji zaidi ya hivi ili

uwe na afya.

49