Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
28

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Unaweza vilevile kuona vinundu vidogo vidogo kuzunguka duara hilo. Hivi vinundu ni tezi ambazo

ni za kawaida. Mwanamke anapokuwa na mtoto, tezi hizi zinatoa kiini kinachosaidia kulinda

chuchu wakati mtoto ananyonya.

Margaret kutoka tanzania (umri, miaka 18)

“Matiti yangu yalipoanza kukua, nilijisikia vizuri japo kuwa

wakati mwingine kulikuwa na maumivu kidogo”

Kadri chuchu na duara vinavyozidi kuwa vikubwa, matiti nayo yanakuwa makubwa na kujaa.

Mabadiliko haya yanavyoanza kutokea, matiti yanaanza kuuma. Unaweza kujisikia maumivu

ukiyabinya au ukiyagonga. Hii ni kawaida, na hakuna haja ya kuhofu. Matiti ni sehemu ya mwili

ambayo ni nyepesi kuhisi kitu. Iwapo kutatokea kiamshi cha namna tofauti, kama kuguswa au

hata ubaridi, chuchu zinakuwa ngumu na husimama.

Kwa wasichana wengine, matiti yao hukua taratibu na kwa wengine hukua haraka. Kwa wastani,

inachukua muda wa miaka 4 matiti kukua kabisa, lakini wasichana wengine matiti yao yanakua

kabisa kabla ya miaka 4, wakati wasichana wengine matiti yanaweza kuchukua hadi miaka 6

kukua kiukamilifu. Hivyo iwapo matiti yako yanachukua muda mrefu kukua tulia tu, yatakua.

Debora kutoka uganda, (umri, miaka 15)

“Matiti yangu yamekua hivi karibuni, lakini ninaogopa jinsi

yanavyoongezeka haraka. Sijali kuwa na matiti, ila ninatumaini

hayatakuwa makubwa sana. Mara ya kwanza nilikuwa

ninashangaa kwa nini yamechelewa kuota, lakini sasa ukubwa

wake unanitisha.”

Kuna matiti ya maumbo na ukubwa mbalimbali. Ukubwa na maumbile ya matiti yanatokana na

tabia vinasaba ulivyorithi toka kwa wazazi wako. Ukubwa pia unategemea tishu zenye mafuta

katika matiti. Hakuna unachoweza kufanya ili matiti yako yawe unavyotaka. Hakuna kiasi

chochote cha mazoezi kinachoweza

kuongeza ukubwa wa matiti yako.

Mazoezi yanajenga misuli lakini matiti

hayana misuli. Kumbuka tu kwamba

matiti yote, makubwa au madogo –

yana kazi kubwa moja - kunyonyesha

watoto.

Pia unatakiwa ujue kwamba, matiti

hayakui yote pamoja sawasawa. Titi

moja linaweza likawa kubwa kidogo

kuliko jingine. Ukweli ni kwamba

hakuna hata mmoja ambaye ana matiti

yanayolingana ukubwa na si rahisi

kuona tofauti hizi.Maumbile ya chuchu

vilevile yanatofautiana sana. Wanawake

wengine chuchu zao zimegeukia

ndani badala ya nje, wengine chuchu

zimezama ndani ya mduara n.k.

Kama matiti yako ni makubwa au madogo,

ni sahihi yalivyo kwako.

SURA YA 4 | WASICHANA

Matiti yana maana tofauti kutoka jamii moja hadi nyingine. Katika utamaduni mwingine

wanawake wanaweza kuacha matiti wazi, wakati katika tamaduni zingine wanashangaa na sio

heshima hata kidogo. Katika sehemu nyingi hata hivyo kuota matiti ni tukio kubwa katika maisha

ya msichana. Ni ishara ya msichana kukua. Wasichana wengi huyapenda matiti yao.

Prossy,kutoka uganda (umri,miaka 13)

“Ninayapenda matiti yangu. Nilikuwa nawahusudu dada zangu

walivyokuwa na matiti. Nilikuwa nachukua soksi na kuzikunja

halafu naweka ndani ya gauni nionekane kama nina matiti.”

barlay kutoka Kenya (umri, miaka 16)

“Nilikuwa ninawahusudu wasichana wanovaa nguo zinazobana

mwili. Nilifurahi nilipopata matiti, hivyo na mimi niliweza kuvaa

nguo zinazobana mwili.”

cathy kutoka uganda (umri, miaka 17)

“Matiti yangu yalikua nikiwa darasa la kwanza .Nilijiona kama

msichana mkubwa kuliko wote darasani. Ilichukuwa muda kukubaliana

na mabadiliko ya mwili wangu. Lakini nilikuwa napenda

nyonga yangu illivyo ya mduara. Marafiki zangu walisema nyonga

yangu inashawishi na hii ilinifanya nijivunie.”

Sherifan kutoka Ghana (umri, miaka 15)

“Nilifurahi sana kwa sababu nilianza kuonekana kama mama

yangu. Nilipokuwa sina matiti nilikuwa ninavaa sidiria ya mama

yangu na kuweka soksi ndani yake nionekane nina matiti kama

mama yangu.”

Baadhi ya wasichana wanajisikia vibaya matiti yao yanapoanza kukua.Pia hii ni kawaida.Hii ni

kwa sababu marafiki zao wa rika moja hawajaota matiti bado.

irene kutoka uganda (umri, miaka 16)

“Wakati matiti yangu yalipoanza kukua, nilikuwa ninavaa flana

zinazobana sana, flana za wadogo zangu. Nilitaka kujisawazisha

mwili nionekane kama sina matiti.”

angela kutoka Kenya (umri, miaka 17)

“Nilikuwa nina wasiwasi mno na nilikuwa ninavaa sweta wakati

wote matiti yangu yalipoanza kuonekana. Nilikuwa sijisikii vizuri

kwani nilikuwa ninasoma shule ya mchanganyiko na sikujua wavulana

wangesema nini.”

Wasichana wengine wanajipinda vibaya kwa kuinamisha vifua vyao kwa sababu ya

kufedheheshwa na kukua kwa matiti yao. Jambo hili linasikitisha kwa sababu kila mtu anatakiwa

kuupenda mwili wake, na kutojali watu wengine wanasema nini. Vyovyote vile matiti yako

yalivyo,kama ni makubwa au madogo yaliyochongoka au ya mviringo ni mazuri jinsi yalivyo.

29