08.06.2013 Views

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

64

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Zungumza na watu wengine kuhusu hisia zako

Fanya mazoezi, na fanya mambo ambayo yanakufanya uwe na furaha na ujisikie vizuri.

Pamoja na haya, jaribu kutoka nje ya nyumba

yenu na pitisha muda na watu wengine. Jihusishe

na shughuli za kanisa/msikitini au kikundi cha

vijana. Kupitisha muda na watu wengine kunaweza

kukusaidia kuondoa fikra za mambo ambayo

yanakufanya uhuzunike sana. Kusaidia kazi

watu wengine kunaweza vilevile kuwa njia nzuri

ya kukufanya ujisikie vizuri. Kwa mfano; jaribu

kumsaidia mtoto anayejifunza kusoma, msaidie

rafiki au jirani yako kazi wanazozifanya. Inaonekana

kama upuuzi, lakini utashangaa namna ambavyo

kumsaidia mtu mwingine kazi kunavyoweza

kukufanya ujisikie vizuri zaidi pamoja na matatizo

uliyonayo.

unapojisikia hovyo, kusaidia watu wengine

kazi kunaweza kukufanya ujisikie vizuri zaidi.

Kama yote hayo hayakukusaidia kiasi cha kufikiria kujiua, tafadhali mtafute mtu wa kuzungumza

naye mara moja. Huyu anaweza akawa ndugu yako, mwalimu au mtaalamu wa ushauri nasaha.

Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengi ni washauri nasaha wazuri, na wanatoa msaada

na ushauri kwa watu wakati wote. Ufumbuzi wa matatizo yako unaweza kupatikana, kwa hiyo

usijaribu kuyatatua peke yako unapojisikia umenyong’onyea sana.

UNAJUA kwamba pombe inaongeza mfadhaiko?

Watu wengi hunywa pombe nyingi wanapokuwa na matatizo wakiamini kuwa inawasaidia

kusahau shida walizo nazo. Pombe hufanya ubongo uwe kama umepata ganzi na kufanya

matatizo kupungua papo hapo.

Kwa bahati mbaya, pombe haiwezi kutatua matatizo yako ya huzuni au kusononeka. Ukweli

ni kwamba pombe inaangukia katika kundi la madawa ya kupunguza uwezo wa ubongo

na sehemu zingine za mwili kufanya kazi vizuri. Pombe na dawa zingine za kupunguza

wasiwasi kwa hakika zinaongezea hali ya kusononeka. Kwa kuongezea, zinamsaidia mtu

akwepe kutatua matatizo yanayomfanya asononeke. Matokeo yake, pombe inaweza kuwa

ngao ya kutegemewa hasa matatizo yanapotokea. Watu wengine wanatawaliwa sana na

pombe kiasi cha kwamba hawawezi kuishi bila kunywa.

KUISHI VIZURI NA WATU

Kuishi na kuelewana na watu ni sehemu nyingine muhimu katika afya ya hisia. Mahusiano

mazuri na wazazi na marafiki zako yatakufanya wewe mwenyewe ujisikie vizuri kwa ujumla na

yatakusaidia kupambana na raha na shida za maisha. Kuelewana na watu wengine kunahitaji

stadi muhimu kama vile:-

SURA YA 6 | UTUNZAJI AfYA YA AKILI NA MOYO

Kujitambua: Kujitambua maana yake ni kuwa na uwezo wa kuelewa hisia zako ni zipi na kwa

nini ziko hivyo. Kujitambua maana yake ni kuwa unapojisikia ovyo ovyo unaachana na kufikiria

kile unachohisi – iwe huzuni, hasira, kukata tamaa, wasi wasi, n.k. Na baada ya kuachana

na unachohisi unaendelea na kufikiria ni kitu gani kinakufanya uwe hivyo. Kwa mfano je ni

wasiwasi juu ya masomo yako? Je unashuku urafiki ambao unaonekana kufifia? Je kuna

mtu amekufanya ujisikie vibaya?

Kujitambua ni muhimu kwa sababu kunakusaidia

uelewe tatizo na chanzo chake. Kwa

kutumia taarifa hii unaweza kuanza kutatua

tatizo. Kama una wasiwasi na kazi za shule,

unaweza kuzungumza na wazazi au mwalimu

wako na kuanza kupata msaada unaouhitaji

ili ujiamini tena. Kama una wasiwasi na rafiki

yako, unaweza kuchukua hatua ya kuzungumza

naye na kumueleza namna urafiki wenu

ulivyo wa muhimu, na kwa pamoja mnaweza

kuangalia namna ya kuufanya uwe urafiki wa

nguvu. Iwapo kuna mtu anakukosesha raha,

unaweza kuamua kukabiliana naye ili afahamu

kwamba unajisikia vibaya anapokutendea

vile, au kama hiyo haisaidii, unaweza kuamua

kukaa mbali na huyo mtu anayekufanya

ujisikie vibaya.

Kujitambua ni uwezo wa kugundua unachohisi na

kinachokufanya uhisi hivyo

Mwisho, kujitambua kunaweza kukusaidia kuujua udhaifu wako, - udhaifu unaotakiwa

kuufanyia kazi mwenyewe. Je, unazo tabia au mwelekeo fulani ambao ungependa kuubadilisha?

Kwa mfano: unaweza kugundua kwamba unapofanya vibaya mitihani yako ya shule

unakuwa na tabia ya kumlaumu mtu mwingine. “Mwalimu hanipendi” unajisemesha mwenyewe.

Au unafikiria “wanafunzi wengine walikuwa wanapiga kelele kwa hiyo nilishindwa

kufikiri.”

Ni rahisi sana kulaumu watu wengine, lakini ni tabia mbaya kwa sababu huwi mkweli na hujiwajibishi.

Labda ulipokuwa mtoto ilikuwa sawa kulaumu watu wengine hasa kwa vile yapo

mambo mengine ambayo watoto hawawezi kuyadhibiti. Lakini unapoingia utu uzima, unahitaji

kuwajibika kwa matendo yako. Kama kuna jambo ambalo haliendi kama unavyotaka ni

juu yako kujaribu kulibadilisha. Kujisikitikia na kujifanya kana kwamba wewe ni mwathirika

wa matendo ya watu wengine haitatatua jambo lolote.

Ushirikeli (uwezo wa kuelewa hisia za mtu mwingine): Uwezo wa kuelewa hisia za mtu

mwingine ni sawa na kujitambua ijapokuwa huu ni uwezo wa kuelewa kile ambacho mtu

mwingine anahisi na kwa nini anahisi hivyo. Kuwa na uwezo wa kuelewa hisia za mtu

mwingine maana yake ni kuwa na uwezo wa kufikiri na kujua pale penye tatizo la mtu

kama - rafiki, mzazi, ndugu, n.k. Unaweza kujua hofu zao,wasiwasi, woga na mahitaji yao, na

unaweza kuelewa wanavyojihisi. Kama ambavyo kujitambua kunavyosaidia ujue mahitaji

yako, ushirikeli unakuwezesha kujua hisia za mtu mwingine. Kwa mfano; kama rafiki yako

ana huzuni, kufahamu tatizo lake kunaweza kukusaidia ujue namna ya kumsaidia kulitatua.

65

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!