Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
140

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Je, unajua njia zipi za kuzuia mimba ambazo ni salama kwa vijana?

Njia zote hizi za kuzuia mimba ni salama kwa vijana:

Kondomu: Kondomu ni mpira laini ambao huwekwa kwenye uume

uliosimama kabla ya kujamiiana. Mwanaume anapotoa shahawa (“anafikia

mshindo”) zinanaswa nchani mwa kondomu. Majimaji toka kwa mwanaume

hayamwingii mwanamke na majimaji toka kwa mwanamke hayagusi uume

wa mwanaume. Kondomu zinatoa kinga nzuri dhidi ya magonjwa ya ngono, pamoja na VVU/ UKIMWI

na huzuia mimba. Bei ya kondomu ni ndogo na zinawasaidia wanaume wengine kuchelewa kutoa

shahawa mapema.

Vidonge: Vidonge vina kiasi kidogo sana cha homoni. Homoni hii huzuia uovishaji

kutoka kwenye makokwa ya mayai. Mwanamke aliyeingia kwenye hedhi

anapomeza kidonge lakini kidonge kinafanya hedhi ya mwanamke kuwa nyepesi

na maumivu kuwa mepesi. Pia matokeo ya kuzuia mimba kwa kutumia vidonge

ni mazuri sana, lakini lazima umeze kila siku. Ukikosa kumeza zaidi ya siku moja

unaweza kupata mimba kwa sababu rutuba inarudi pindi unapoacha kumeza

vidonge. Vidonge havizuii VVU au mangojwa mengine ya zinaa. Kwa hiyo, ni vizuri

iwapo unatumia kondomu, uwe na mwenzi mmoja tu na wote muwe mmepima na kuthibitisha hamna

magonjwa ya ngono/VVU.

Sindano: Sindano ina homoni ambazo zinazuia yai kurutubishwa. Huanza

kufanya kazi katika muda wa saa 24 na hutoa kinga dhidi ya mimba kwa

muda wa miezi mitatu. Kudunga sindano ni rahisi kwa sababu huhitaji

kukumbuka kumeza kidonge kila siku au kufanya chochote kabla ya

kujamiiana. Sindano pia inatunza siri, hakuna anayeweza kujua kwamba

unatumia mtindo huu kwa kuzuia mimba. Sindano zinafanya siku zako za

hedhi ziwe nyepesi na zenye maumivu kidogo ambapo zinaweza kuwasaidia

vijana wanaopata maumivu au hedhi nzito. Unapoacha kudunga sindano, huwi na rutuba tena mara

moja, kwa sababu homoni zinakaa mwilini kwa muda . Wanawake wengi wanakuwa na rutuba tena

ndani ya mwaka mmoja wanapoacha kutumia sindano, lakini wengine wanapata mimba mapema.

Sindano hazizuii magonjwa ya zinaa/VVU hivyo zinafaa tu kama unatumia kondomu au kama unaye

mwenzi mmoja na wote mmepima magonjwa ya ngono/VVU.

Vipandikizi: Vipandikizi ni vimrija vidogo vinavyowekwa ndani ya ngozi kwenye

mkono chini kidogo ya bega. Vimirija hivyo huwa vinatoa homoni inayozuia yai

kurutubishwa. Kama ilivyo kwa sindano huhitaji kukumbuka kumeza vidonge

au kufanya lolote kabla ya kujamiiana. Vipandikizi vinadumu miaka mitano.

Lakini vinaweza kuondolewa mapema. Ni kinga nzuri sana kuzuia mimba, lakini

haizuii magonjwa ya zinaa/VVU. Kwa hiyo unatakiwa kutumia kondomu au kuhakikisha kuwa wewe na

mwenzi wako hamna magonjwa ya ngono/VVU.

Dawa ya kuulia mbegu za kiume (vidonge mafuta au krimu na povu): Dawa

hizi zinaua mbegu za mwanaume kabla hazijaingia ndani ya mfuko wa kizazi,

lakini hazimuumizi mwanaume au mwanamke. Zipo aina mbalimbali za dawa

na zinaingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Dawa hizi zitumike na kondomu kwa

sababu zina kinga ndogo sana dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU. Zaidi ya hapo,

hazina kinga madhubuti kama ya vidonge au sindano katika kuzuia mimba.

Tofauti na vidonge na sindano, huhitaji kuzipata kutoka kwa mhudumu wa afya; unaweza kupata moja

kwa moja toka kwenye maduka ya dawa. Hii inaweza kuwa bahati kama una aibu kwenda kliniki, lakini

kumbuka kutumia kondomu.

Unapotumia vidonge vya dharura inakubidi umeze kiasi cha mchanganyiko wa vidonge vya kuzuia

mimba baada ya saa 12 katika kipindi cha saa 72 za kufanya ngono bila kinga. Kinga ya dharura ya

kuzuia mimba haifanyi kazi mimba inapokuwa imetungwa. Ndio maana ni muhimu kuipata haraka

baada ya ngono isiyo na kinga. Usijaribu kunywa dawa hizi bila ushauri wa mhudumu wa afya

mwenye ujuzi.

KinGa MaRa Mbili

SURA YA 11 | MIMBA NA UZUIAJI WA MIMBA

Je, unafahamu kuwa wanawake waliokeketwa wana mahitaji

Kuchomoa/kurusha: Kuchomoa au kurusha ni wakati mwanaume anatoa uume nje ya uke

kabla ya kukojoa shahawa. Njia hii sio salama kwa sababu wanaume wengi hawawezi kuutoa

uume kwa wakati unaotakiwa. Mara nyingi wanaume hawajui kwamba wanakaribia kukojoa

mpaka wanapokuwa wamekaribia sana. Pia, matone machache ya shahawa yanaweza kutoka

kabla ya kukojoa na matone machache haya yanatosha kusababisha mimba. Kuchomoa

hakuleti kinga dhidi ya VVU/UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa.

“Siku salama”: Wanawake wengine wanasubiri siku ambazo wanajua kwamba hawana rutuba.

Utaratibu huu unafaa kwa wanawake ambao hedhi zao ni za kawaida na wenzi wao wana

ushirikiano. Wasichana wa umri mdogo wengi hawana hedhi za kawaida hivyo si rahisi kujua

siku salama. Kama ilivyo kwa njia ya kuchomoa, siku salama hazileti kinga dhidi ya magonjwa

ya zinaa/VVU.

Kitanzi: Kitanzi kinatumbukizwa kwenye tumbo la uzazi na mhudumu wa afya. Ni rahisi

kukiingiza kwa mwanamke ambaye amewahi kuzaa, kwa hiyo haipendekezwi kwa vijana.

Kitanzi kinaweza kusababisha ugonjwa wa ngono ukue na kufikia hali ya kutisha. Kwa vile

vijana ni rahisi sana kuambukizwa magonjwa ya zinaa, wasitumie kitanzi. Kitanzi hakitoi kinga

dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Kufunga kizazi: Kukata au kufunga mirija ya kupitishia mbegu ya wanaume na wanawake ni

njia ya kudumu ya kuzuia mimba. Unafanyika upasuaji ambapo mirija ya kupitishia shahawa na

yai inazibwa. Njia hii inawahusu wanaume na wanawake ambao wanafikiri wamepata idadi ya

watoto inayowatosha. Njia hii haifai kwa vijana kwa sababu huwezi kupata watoto baada ya

upasuaji. Kufunga kizazi hakutoi kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Ugonjwa wa UKIMWI umebadilisha mawazo ya watu wengi kuhusu njia za kuzuia mimba.

Zamani watu walilenga katika kuangalia ni njia zipi zinaleta matokeo bora katika kuzuia mimba.

Hawakujali sana kama njia ya kuzuia mimba ilitoa kinga dhidi ya magonjwa ya zinaa/VVU.

Leo mambo ni tofauti. Kupata VVU ni maafa makubwa kuliko kupata mimba isiyotakiwa. Siku

hizi watu wanazungumzia kuhusu kinga mara mbili. Kinga mara mbili ni wakati unatumia njia

ambayo matokeo yake hupunguza hatari ya mambukizo ya magonjwa ya zinaa/VVU/UKIMWI, na

wakati huohuo, unatumia njia nyingine ambayo matokeo yake ni mazuri katika kukinga mimba

zisizotakiwa.

Angalia njia mbalimbali hapa chini uone jinsi zinavyotoa kinga dhidi ya mimba na magonjwa

mengine ya ngono pamoja na VVU.

141