Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
Wewe Maisha Yako Ndoto Zako - Family Care International
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
82

WEWE, MAISHA YAKO, NDOTO ZAKO

Gift, kutoka Ghana (umri wa miaka 14)

“Marafiki zangu wananipenda na kuniheshimu sana kwa sababu mimi ni

mwaminifu na ninawashauri kuhusu nini msichana anatakiwa kufanya.”

Unaweza kuwa na urafiki na watu wa jinsi moja au na watu wa jinsi tofauti.

Seif, kutoka tanzania (umri wa miaka 13)

“Ninao marafiki wa kike watatu. Tunakaa na kuongea au kusoma

pamoja. Rafiki wa kike ni kama rafiki wa kawaida tu.”

evans, kutoka Kenya (umri wa miaka 16)

“Mimi na rafiki yangu wa kike tunasaidiana kazi za shule na

kubadilishana mawazo kuhusu maisha na namna ya kujiheshimu mbele

za watu wazima.”

halima, kutoka Kenya (umri wa miaka 14)

“Kuwa na rafiki mvulana au msichana maana yake ni kusaidiana na

kufanya maamuzi pamoja. Vile vile kuzungumza kama kuna tatizo.”

Wavulana na wasichana wanaweza kuwa marafiki na wanaweza kuwa na urafiki bila ya

kujamiiana. Wavulana na wasichana wanaweza kuwa na mahusiano ya kimapenzi ambayo

hayahusishi ngono. Kwa hiyo tunapotumia maneno “rafiki wa kiume” na “rafiki wa kike”

haina maana ya kwamba mahusiano hayo ni ya kufanya ngono.

anthony, kutoka Kenya (umri wa miaka 15)

“Urafiki wetu sio wa kufanya ngono au kufanya kitu chochote

kitakachotufanya tujute baadaye. Urafiki wetu ni wa kusaidiana kama

marafiki na sio kitu kingine.”

Kwame, kutoka Ghana (umri wa miaka 17)

“Watu wanafikiri rafiki wa kike ni mtu ambaye unahusiana naye kingono

tu. Rafiki wa kike ni mtu ambaye unaweza kumwomba ushauri, mtu

ambaye unaweza kushirikiana naye kwenye matatizo.”

Urafiki mzuri na wa nguvu unapendeza sana. Unakufanya ufurahi.Unachangia katika kukua

kwa hisia kwa sababu unakufundisha jinsi ya kuwa karibu na mtu.

Urafiki mzuri vile vile unachangia katika kujiheshimu. Ukiwa na rafiki mzuri, unajisikia

vizuri. Inapendeza kuwa na mtu ambaye unaweza kumweleza siri zako. Vile vile inapendeza

kuwa na mtu anayejisikia vizuri kukueleza siri zake. Unaweza kushirikiana naye mawazo

bila wasiwasi wa kuchekwa. Unaweza kushirikiana naye siri na kujua kwamba hazitatoka

nje. Inapendeza kufahamu kwamba rafiki yako atakupenda na kukuheshimu hata kama

hukubaliani naye kuhusu jambo fulani.

Kupitia urafiki wa karibu, unaweza kujifunza jinsi ya kukubali au kukataa mambo tofauti.

Unajifunza pia jinsi ya kuwa na nguvu za kutosha kutetea maoni yako.

Kujiamini ni muhimu kwa maisha ya baadaye na kwa mahusiano na watu wengine. Ukweli ni

kwamba marafiki wanakusaidia kujenga stadi nyingi muhimu ambazo unazihitaji ili kufanikiwa

maishani. Stadi hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa:

SURA YA 8 | URAfIKI NA MApENZI

Kuwasiliana vizuri na kuwa muwazi kuhusu hisia zako na mawazo yako.

Kusikiliza na kujua hisia za mtu mwingine na maoni yake.

Kusaidia pale mtu anapokuwa na matatizo au anajisikia hovyo.

Kujadili (kwa mfano, wewe na rafiki yako hamjakubaliana kuhusu jambo fulani, utahitaji

kujadiliana na kuafikiana au kufikia mwafaka).

Kushirikiana, kufanya kazi pamoja na kuwajibika kwa pamoja

Kukubali na kuheshimu tofauti za maoni, imani na mazoea. (Kwa mfano, wewe na rafiki

yako mnaweza msiafiki kuhusu jambo fulani. Ni sawa tu.

Hasa urafiki unajengeka katika kipindi cha ujana balehe kwa sababu vijana wengi wanaona

aibu kuongea na wakubwa. Iwapo wazazi wako wanafikiri kutumia muda wako na marafiki

ni kupoteza muda, jaribu kuwaeleza namna marafiki zako walivyo muhimu kwako na kwa

nini. Unahitaji marafiki.

Urafiki mzuri na wa nguvu unachukua muda na bidii kuujenga. Hautokei usiku mmoja na

huwezi kupata marafiki wa kweli kila siku.

JINSI YA KUMTAMBUA MTU AMBAYE SI RAFIKI WA KWELI.

Inaweza ikatokea wakati mwingine mtu ambaye ulifikiri ni rafiki akageuka kuwa rafiki mbaya.

Kwa mfano rafiki anapotoa siri kwa watu wengine, au anaeneza uvumi wa hovyo kuhusu

wewe, huyu hafanyi vile ambavyo rafiki wa kweli anatakiwa kufanya. Rafiki wa namna hii

anaweza kukuumiza, lakini hayo ndiyo maisha. Jaribu kuzungumza naye na muombe aache

kufanya kitu chochote ambacho kina kukasirisha. Kama rafiki yako haachi kukufanyia

vibaya, kaa mbali naye. Kupoteza rafiki inasikitisha/inahuzunisha, lakini utapata rafiki

mwingine aliye bora zaidi.

ayoo, kutoka uganda (umri wa miaka 15)

“Niliwapoteza marafiki zangu wote kwa sababu

hawakuheshimu

maoni yangu. Sasa ninaye rafiki wa kweli mmoja tu, lakini

tunaheshimiana.”

Marafiki wanaweza kuwa chanzo cha shinikizo – Hasa shinikizo la kundi-rika ambalo ni

chanzo kikubwa cha wasiwasi kwa wazazi. Shinikizo la kundi-rika mara nyingi huwafanya

vijana wafanye makosa, kama kunywa pombe, au madawa ya kulevya. Shinikizo la kundi

rika linaweza kuwafanya vijana wajamiiane wakati kwa kweli hawapendi kufanya hivyo.

Florence, kutoka Ghana (umri wa miaka 16)

“Ninapata shinikizo kutoka kwa wasichana wengine

wanapojipamba na wanapotoka na kwenda kwa wavulana.

Ninajishauri mwenyewe nisionyeshe tabia mbaya au kufanya

mambo mabaya.”

83