19.05.2013 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

Upande wa mambo haya mengine vile vile, ukiuliza swali lolote, unaambiwa yanatoka juu. Sasa, Bwana Commisioner, tunataka

mambo yawe yakitoka chini, kama vile tukichagua wale watu kuenda juu. Tuwe tukielewa ni kitu gani kinaendelea, mpaka

huko juu. Yaani tukiuliza swali, tujue tunauliza swali la aina gani. Hii ni kwa sababu tunaambiwa, ni kama mtoto. Sasa wakati

huu, wananchi wa kawaida ni kama watoto wale wamezaliwa, wale wachanga kabisa. Ni kuambiwa tunaambiwa. Yaani, sisi

hatusemi. Ni nikuambiwa tunaambiwa tu. Kwa hivyo sasa, kuanzia hii Katiba tunatengeneza sasa mwananchi wa kawaida

anapaswa kuwa akijua kila kitu kilicho, au kila kitu kinachoendelea. Hawa Wajumbe tuliwachagua kuenda Parliament,

wakatuongoze kwa mambo yale, kwa sababu ndio wako huko juu, watugawie kile kinatakikana. Ni ajabu sasa, kuona wale

tulipeleka Parliament, ndio wenye kila kitu. Mahindi, kahawa, mandizi haya tunalima huku, ni kama ndio wenyewe. Ukiwauliza

maswali wakija huku, wanasema Serikali imesema. Tukiendelea kuuliza maswali tunaambiwa Serikali ni sisi. Je Serikali ni sisi

na tuna taabika?

Kwa upande ule mwingine, nchi yetu ya Kenya iko na area kubwa sana, ile haifanyiwi kazi. Serikali yetu ya wakati huu inajua,

na inaona. Tunashangaa ni kwa nini, kama wanatembea kama tuseme President Wetu ameshawahi kwenda mahali pengi sana.

Mahali kule kulikuwa dry kama upande huu wa Isiolo huko, upande wa Garissa, ameshawahi kwenda huko. Huko sasa wakati

huu, wale watu wanalima, na wanalima na maji. Bahati yetu sisi tuna milima miwili hapa karibu sana na ina maji. Tuna Mount

Kenya hapa, tuna Nyambene hapa, mahali pengi sana. Pale maji yanaweza kufikiriwa, ikafikia wale watu wakaanza kulima.

Sasa msaada, ni huu msaada tunaona unapita na ma-lorry kuteremka chini, na kesho yake tunaona unapanda juu na lorry zile

zile? That means, wale wanapelekewa wanagonga kidole. Wanaweka kidole, kesho yake mahindi yanabebwa tena tunakuja

kuuziwa huku, na ni ya msaada. Sasa ningependelea hivi, maoni yangu, huo msaada, uwe ukijulikana kutoka mahali kule

unatoka huko store, ma-store yao huko Nairobi, iwe ikujulikana inakwenda Garissa, au Marsabit, na iwe announced katika

radio. Watu wa Marsabit wawe wanangojea malorry matano ya mahindi. Wajue itafika kama kweli, ama constitution yangu

ndiyo inasema hivyo. Kila kitu kikipatikana kwa msaada kiwe kina pelekwa mahali pale kinatakikana na wananchi wakule

wakiwa wanajua, kuna kitu kinakuja, na wangojee. Hii ni kwa sababu sasa, tunasikia tu msaada. Watu wanapatiwa msaada,

lakini hatuwezi kujua ni msaada wa aina gani.

Ni mshangao mkuu, kwa sababu wengi wetu kama hapa, wengi wetu wameelimika, ama, watoto wetu wameelimika kiasi

kikuu. Upande wa kazi, mtoto akiandika application, mara moja tu, barua ina-regret, hatuna kazi. Mimi ningependelea,

mbeleni hapo, mtoto akiwa amehitimu mtihani fulani, ilikuwa tu ni application kusomwa na kuonekana huyu mtoto amepita

kiwango fulani, na hii kazi kweli inapaswa ipatiwe mtoto huyu, Sio kuwachunguza kabila hii au kabla ile, hapana. Sio kusema

ati, tuje na hii, inaitwa back doors, hapana direct namna hivyo. Ikifanyikana hivyo, Serikali yetu itaendelea, na tutakuwa tukijua

Serikali ni gani, na tutakuwa tukisema ina tufanyia kazi. Asanteni sana.

Com. Lenaola: Mr. Kimakia, njoo ujiandikishe pale. Peter Kiambi, Erastus M’torukuma, utamfuata.

44

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!