19.05.2013 Views

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

constitution of kenya review commission (ckrc ... - ConstitutionNet

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Namwacha na watoto hao. Mama hana shamba, na watoto hawana elimu, kwa hivyo umaskini unaongezeka. Huyo bwana

aliyetunga huyo mwanamke mimba anafaa achukuliwe na ashtakiwe. Akishtakiwa, huyo mtoto naye anafaa asomeshwe na

Serikali, ikiwa huyo ameshtakiwa.

Kwa andikwa: – Mimi naonelea , iwe kama vile ilikuwa zamani, ili watu waandikwe, kwa sababu hawa watoto maskini

wanaosoma, hawawezi kuandikwa kazi, Kwa vile ukiitwa, unaitishwa pesa. Unaambiwa, ah, lete kitu kidogo, ili mtoto

andikwe. Sasa mimi nikiitishwa elfu hamsini, nitatoa wapi? Huyo mtoto hawezi kusoma. Serikali pia, haisemi uitishe mtu pesa.

Mtu kama huyo akipatikana anafaa afutwe kazi, na ashtakiwe kwa kuharibu kazi yake. Hayo ndiyo maoni yangu.

Com. Lenaola: Asante sana.

Wilson Marete: Mimi bado sija maliza . Hawa wanawake nao, wanaotaka ukubwa kwa mabwana, ai, kweli, wanataka

ukweli. Lakini zamani hata ukiangalia kwa maumbile hata kutoka kwa Mungu, kitabu cha Mungu hakikubali mwanamke awe

juu ya mwanamme. Watu ni wawili hata ukiangalia, iko Mungu, iko Yesu, na iko Malaika. Yesu hawezi kupanda juu ya

Mungu, na malaika hawezi kupanda juu ya Yesu. Kwa hivyo, watu wanafaa watumie mila yao. Kwa sababu, wale

wanaoharibu hivi ni kitu tunawekelewa sisi. Mwanamke yule aliyeshindwa na bwana yake, ni jina anaye ile ya kuolewa, lakini

alitupa bwana na akatupa watoto. Ndiyo anakwenda kujigamba kwenda Beijing, sijui wapi. Haija umiza bwana. Sasa

nikikasirika, si nitamwacha na watoto. Watoto hao, hawana shamba, mama hana shamba na hiyo shamba watatuma niuuze.

Wakati nitakapouza, mwanamke na mtoto wanaangamia, na umaskini unangia hapo, na wezi wanakuwa wengi. Kwa hivyo,

huyo mtu, anafaa achukuliwe na afanyiwe vile inavyowezakana, ili iwe adhabu kali kwake. Kuna mtu mwingine pia, anayeweza

kuenda kuuwa kijana kama huyu. Kumuua tu; akienda kotini, kesho unamuona hapa, na anakuambia, nilimuua na ulinipeleka

kotini, kwa hivyo hata wewe nitakuuwa.

Kitabu cha Mungu kinasema hivi, ukiuwa na panga, hata wewe utauwawa na panga ukiuwa na kamba, hata wewe unyongwe

na kamba. Kwa hii naye, maskini ananyakuliwa hata mali yake na mawakili. Mimi naweza kuwa sina mali, lakini tajiri

anayekujua, (akiona hii shamba yako) anasema, ah hii shamba si yako. Court injuction – naondolewe na shamba ni yangu. Sina

mtu wa kunisaidia. Sina pesa ya kufuata. Hapo inakuwa ni mahangaiko. Hiyo Serikali inafaa ichukue hatua, mtu kama ni

mwizi, awe kama huyo, mwingine anaiba mtu na panga. Ikiwa ni kunyongwa anyongwe kwa sababu hakuna mwizi wa panga

na wa kukunyanganya hivyo – mwizi ni mwizi.

Mashamba: – Kuna watu wanaambiwa kuwa Serikali inawapa mashamba; huko mashambani eka mbili, eka tatu, eka tano, au

eka kumi, lakini baadaye Serikali ililipa hayo mashamba, na baadaye, wanakuja kuitishwa pesa, ukaambiwa lete pesa ya

shamba ulilopewa. Sasa nilipewa nikiwa maskini, nitatoa pesa wapi bwana. Kwa hivyo, huyo mtu anafaa awachiwe shamba

kwa sababu alipewa free, afanye kazi yake free, kwa sababu huyo ni maskini ndiye aliyesaidiwa. Hii mashamba makubwa ya

wengine, tuseme wazungu wako na mashamba makubwa sana, jamaa anashikilia shamba kutoka hapa mpaka huko Tigania

8

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!