15.01.2013 Views

2 - мгимо

2 - мгимо

2 - мгимо

SHOW MORE
SHOW LESS

You also want an ePaper? Increase the reach of your titles

YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.

zilipunguzwa. Lakini wagonjwa walizidi sana kwenda hospitali kupata

matibabu. Ingawa hivyo yalikuwapo mafanikio mema fulani. Kazi

iliyokuwa ya maana sana ilikuwa ni kutiliwa mkazo kwa ubora wa

chakula kizuri kwa mwili na magonjwa yanayotokana na kutokula

chakula cha kutosha na cha kufaa.

Baada ya vita, Idara ya Utibabu ilifanya maendeleo mazuri ingawa

mambo mengine mabaya, kwa mfano kuwa na hospitali mbali

kwa Wazungu, yalikuwa bado yapo. Kazi za dawa hazikutosheleza

mahitaji ya watu kwa vile ambavyo watu wengi walikwenda hospitali

kutibiwa na kuacha miti shamba. Fedha iliyoongezwa haikutosha kununua

vifaa vya hospitali na pia haikutosha kupanua shule za kufundishia

waganga. Licha ya fedha, hawakuwapo (3) watu wa kutosha

wenye elimu iliyotakiwa ili wachukue mafunzo mbali mbali ya uganga.

Kazi za utibabu hazikuweza kuendelea pasipo Waafrika wenyewe kupewa

ujuzi na madaraka katika kila daraja la wauguzi. Manesi na

madaktari Waafrika wengi walitakiwa.

Katika mwaka 1951 halmashauri ya mafunzo ya waganga ilianzishwa.

Mafunzo ya miaka mitatu ya wasaidizi wa madaktari yaliendelea

Dar es Salaam wakiwa wanachukuliwa wanafunzi waliohitimu

darasa la kumi (4). Mafunzo ya miaka miwili kwa wasaidizi wa madaktari

katika hospitali za shamba, yaliendelea Mwanza. Kwa shule ya

Mwanza walichukuliwa wanafunzi waliohitimu darasa la nane.

Lakini kwa upande wa kuzuia magonjwa maendeleo hayakuwa

makubwa. Mahitaji ya kuwapo (3) kwa vituo vya kutolea dawa na

kuzuia magonjwa katika sehemu za shamba na pia kwa ajili ya kutolea

elimu ya mambo ya usafi na afya nzuri yalikuwa makubwa sana. Vituo

hivyo vingalikuwa vinatoa dawa (5) na kuwa na vyumba vidogo vya

kulaza wagonjwa, vyumba vya kuzalishia na sehemu za kuangalia afya

ya watoto wachanga, na pia vyumba vya kutolea mafunzo ya elimu ya

usafi na afya. Ilitazamiwa kuwa hatimaye vituo hivyo vingelikuwa

badala ya hospitali ndogo.

Katika mwaka 1960 hospitali kubwa ilifunguliwa mjini Dar es

Salaam, yaani hospitali iitwayo Muhimbili sasa. Palikuwa pia na hospitali

arobaini na nane nyingine za serikali, hospitali kwa matibabu

maalumu sita na hospitali ndogo ishirini.

204

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!