15.01.2013 Views

2 - мгимо

2 - мгимо

2 - мгимо

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

Wakazi wengi zaidi wa Mwanza ni Wasukuma, ingawa bado

kuna mchanganyiko mkubwa wa makabila mkoani humo, mathalani,

Wajita, Wakerewe, Wasumbwa na mengineyo.

ТЕКСТ №3

MJI WA ARUSHA

Mji wa Arusha umekuwa na maendeleo ya kusisimua katika

muda wa miaka michache iliyopita. Mji huu unazidi kuwa maarufu,

siyo katika Tanzania tu, bali katika Afrika ya Mashariki na Afrika

kwa jumla.

Kwa wanasiasa jina la Arusha lawakumbusha mahali

ilipotangazwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo siasa hiyo

ilikubaliwa na kupitishwa katika kikao cha Mkutano wa TANU

uliofanyika mwaka 1967. Katika Azimio la kuitangaza siasa hiyo

Watanzania wameamua kukomesha kila aina ya unyonyaji, ukabaila

na ubepari, na kusisitiza usawa wa binadamu. Azimio hilo limepewa

jina la Azimio la Arusha.

Licha ya Azimio hilo, mji huu ni maarufu kwa mambo

mengine ya kihistoria pia. Hapa ndipo palikuwa na makao makuu ya

Jumuiya ya nchi za Afrika ya Mashariki ambayo iliundwa zamani

kwa kuyashughulikia mambo mengi ya uchumi katika nchi za Tanzania,

Kenya na Uganda.

Kwa siku hizi katika mji wa Arusha unaweza kuona watalii

wengi mbalimbali wanaokwenda au kurudi kutoka kwenye mbuga

za wanyama huko Serengeti, Ngorongoro na Ziwa Manyara. Arusha

ndio mji mkubwa katika sehemu ya mbuga za wanyama za

kaskazini. Watu wengi huweza kupata mahitaji yao hapa mjini.

Kuna mahoteli makubwa na ya kisasa. Hoteli hizi pamoja na

mashirika ya utalii yaliyomo mjini (1) hushughulika kuwapa watalii

habari za mbuga zetu za wanyama. Mipango mingi ya kutalii katika

mbuga hizi za wanyama hufanyika hapa mjini Arusha. Utaweza

kuona magari mengi ya kutalii yakichukua wageni hawa.

Watalii wanaokuja nchini kwetu hununua vitu vingi kutoka

madukani, hivyo huongeza biashara ya taifa. Pia watalii hulipa

ushuru wa kuingia katika mbuga hizi za wanyama pamoja na ku-

25

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!