TPSEAL 2010 Financial Results. - Serena Hotels
TPSEAL 2010 Financial Results. - Serena Hotels
TPSEAL 2010 Financial Results. - Serena Hotels
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Notisi Kuhusu Mkutano Wa Pamoja Wa Mwaka

Notisi inatolewa hapa kwamba mkutano wa 39 wa pamoja wa mwaka

wa Kampuni utafanyika Mei 31, 2011 katika Ukumbi wa Mikutano

ya kimataifa wa Kenyatta International Confrence Centre kuanzia saa

tano asubuhi ili kuangazia maswala yafuatayo ya kibiashara:

SHUGHULI ZA KAWAIDA

1. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano wa thalathini na nane wa

pamoja wa mwaka uliofanyika Mei 24, 2010.

2. Kupokea, kuangazia na endapo itaonekana kuwa sawa, kupitisha

hesabu ya pesa kwa kipindi cha mwaka uliomalizika Desemba 31

2010 pamoja na ripoti kutoka kwa Wakurugenzi na Wakaguzi wa

pesa.

3. Kuidhinisha kutolewa kwa malipo ya mwisho ya mgawo wa faida

wa mwaka 2010 wa shilingi 1.25 kwa kila hisa ikitegema ushuru

ulioshikiliwa pale inapohitajika kwa wanachama ambao majina yao

yatakuwa kwenye sajili kufikia Mei 31, 2011. Malipo ya mgawo wa

faida yatatolewa kabla au kufikia Juni 20, 2011.

4. Kuchagua Wakurugenzi

(a) Bw. Ghislain de Valon aliteuliwa mwaka 2011 kujaza nafasi

iliyokuwa wazi. Anastaafu kwa mujibu wa kifungu nambari 109

cha sheria za kampuni na kwa kuwa hali inamruhusu, amejitokeza

tena kuchaguliwa.

(b) Bw. Kabir Hyderally anastaafu kwa zamu kwa mujibu wa vifungu

nambari 110, 111 na 112 vya sheria za Kampuni na kwa kuwa hali

inamruhusu, amejitokeza tena kuchaguliwa.

(c) Bw. Mahmood Manji anastaafu kwa zamu kwa mujibu wa

vifungu nambari 111 na 112 vya sheria za Kampuni na kwa hali

inamruhusu , amejitokeza tena kuchaguliwa.

(d) Bw. Kungu Gatabaki anastaafu kwa zamu kwa mujibu wa vifungu

nambari 110, 111 na 112 vya sheria za Kampuni na kwa kuwa hali

inamruhusu, amejitokeza tena kuchaguliwa.

5. Kuidhinisha malipo ya wakurugenzi ya mwaka 2010.

6. Kuteua PricewaterhouseCoopers kama wakaguzi wa pesa wa

kampuni kwa mujibu wa sehemu ya 159 (2) ya sheria za

makampuni (Cap 486). PricewaterhouseCoopers wameonyesha

nia yao ya kuendelea na jukumu hili.

7. Kuidhinisha malipo ya wakaguzi wa pesa kwa kipindi cha mwaka

2010 na kuwapa ruhusa wakurugenzi kuamua malipo ya wakaguzi

hao.

8. Kutekeleza shughuli nyingine ya kawaida ya kibiashara ya

mkutano mkuu wa pamoja wa mwaka.

SHUGHULI MAALUMU

9. Kurekebisha vifungu vya sheria

Kuzingatia na endapo itakubalika, kupitisha maazimio yafuatayo

ambayo yatapendekezwa kama maazimio ya kawaida:

(i) Kwamba vifungu vya sheria vya kampuni vibatilishwe na kuingiza

kifungu kifuatacho kama kifungu nambari 68.

‘’ Notisi yoyote au hati nyingine inaweza kutolewa na kampuni kwa

mwanachama au mkurugenzi yeyote wa kampuni aidha kwa mtu

binafsi au kutumia sanduku la barua ( kupitia barua pale ambapo

huduma hii inapatikana) au kupitia telegramu, teleksi, kipepesi au

barua pepe iliyotumwa kwa mwanachama au mkurugenzi kama

huyo kupitia anwani iliyosajiliwa kama inavyodhihirishwa kupitia

sajili ya wanachama au rekodi nyingine za kampuni iwe anwani

kama hiyo ni ya humu nchini au nje ya nchi ya Kenya au kupitia

teleksi, kipepesi, telegramu au barua pepe iliyotajwa au kwa kutumia

tangazo la magazeti mawili ya kila siku yanayosambazwa

kote nchini au kupitia tangazo kwa njia ya elektroniki. Katika hali

ambapo umiliki wa hisa utakuwa wa pamoja, notisi zozote kupitia

barua, telegramu, kipepesiau barua pepe, itatolewa kwa mmoja wa

wamiliki hao ambaye jina lake litakuwa la kwanza kwenye sajili

ya wanachama na notisi ikitolewa itachukuliwa kama inatosha

kwa wamiliki wote wa pamoja. Katika hali ya notisi ya mkutano ya

pamoja wa mwaka, notisi kama hii itatolewa kupitia:

(a) Kuchapishwa kwa notisi iliyo na muhtasari wa taarifa za matumizi

ya pesa na ripoti ya wakaguzi wa pesa kupitia magazeti mawili ya

kila siku yanayosambazwa kote nchini kwa siku mbili mfululizo au;

(b) Kutuma notisi moja kwa moja kwa kila mwanachama kupitia

mbinu za elektroniki (ikiwemo kipepesi na barua pepe) au kupitia

sanduku la posta huku notisi ikiwa na taarifa hizo za matumizi ya

pesa , hati nyingine na ripoti kama inavyohitajika kisheria.’’

(ii) Kifungu cha sheria nambari 156 kifutiliwe mbali kama kilivyo na

mahali pake kuwa kama ifuatavyo:

‘’ Mgawo wowote wa faida, riba au kiwango chochote cha pesa

kitakachotolewa kwa pesa taslimu kwa mmiliki wa hisa kilipwe

kupitia:

(a) Hundi au dhamana itakayotumwa kupitia sanduku la barua kwa

mmiliki kama huyu kwa anwani yake inayojulikana na katika hali

ambapo umiliki ni wa pamoja, itumwe kwa mmiliki ambaye jina

lake limesajiliwa mbele katika sajili ya wanachama kulingana na

hisa au

10 TPS EASTERN AFRICA LIMITED ANNUAL REPORT AND FINANCIAL STATEMENTS 2010