Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
TAARIFA YA MWENYEKITI

Inanifurahisha sana kuwasilisha kwenu Taarifa ya kila Mwaka

ya Benki ya NIC na Taarifa ya kifedha ya Mwaka uliomalizikia

tarehe 31 Disemba, 2011.

MAZINGIRA YA KIUCHUMI NA KIBIASHARA YA MWAKA WA

2011

Mategemeo makubwa ya Uchumi wa taifa la Kenya yaliathirika

pakubwa katika mwaka wa 2011 kutokana na changamoto

kubwa la kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, licha ya

changamoto hizo, uchumi ulitarajiwa kukua kwa asilimia 4.3

chini ya kiwango cha asilimia 5.6 iliyopatikana mwaka wa 2010,

hii ikiwa ni kulingana na mazingira ya kiuchumi yalivyokuwa.

Baada ya kuanza mwaka kwa hatua nzuri kutokana na kasi

na mwamko uliokuwepo mwaka wa 2010, uchumi wa Kenya

uliathirika kutokana na ghasia ama vurugu huko katika

Milki ya Nchi za Kiarabu na Afrika Kaskazini pamoja na jamii

kutoelewana na hali ya kisiasa ambayo ilisababisha kupanda

kwa bei ya mafuta. Na ni wakati huo huo ambapo tulikuwa

tumekabiliwa na janga la ukame lililosababisha uhaba wa

chakula na ongezeko la vyakula kuagizwa kutoka nchi za nje.

Kutokana na upungufu wa chakula nchini na ongezeko la bei ya

mafuta ambayo hayajasafishwa kwenye masoko ulimwenguni

yalisababisha mfumuko wa bei ambao uliongezeka kutoka

asilimia 5.4 kwenye mwezi Januari, 2011 hadi asilimia 19.7

kwenye mwezi wa Novemba, 2010. Kiwango cha wastani cha

mfumuko wa bei kwenye mwaka wa 2011 kilikuwa asilimia

14.0 kikilinganishwa na asilimia 4.1 kwenye mwaka wa 2010.

Ongezeko la matumizi ya kinyumbani na uwekezaji uliochangiwa

na ukuaji katika sekta za kibinafsi za mkopo pia ulichangia kwa

kiasi kikubwa katika mfumko wa bei.

Kutokana na ongezeko la bei ya mafuta ambayo hayajasafishwa,

matumizi ya hali ya juu ya kinyumbani, uwekezaji na ongezeko

la mahitaji ya chakula kutoka nchi za nje na vilevile mafuta ya

kuzalisha umeme yalisababisha kuanguka kwa thamani ya

shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu nyingine kuu za kimataifa.

Isitoshe, kuanguka kwa thamani ya shilingi kulisababishwa pia

na kuzorota kwa biashara ya nje ya nchi. Wakati huo ukame

uliathiri vibaya sana uzalishaji wa chai, kahawa na bidhaa za

kilimo cha bustani hali inayojumuisha kiwango kikubwa cha

mazao tunayo safirisha nje ya nchi. Kwa upande mwingine,

kuzorota kwa uchumi katika ukanda wa magharibi mwa Bara-

Yuropa ambalo ndilo miongoni mwa masoko yetu makuu,

yalipunguza mahitaji ya bidhaa zetu kutoka humu nchini. Kwa

upande mwingine, athari za madeni na misukosuko katika

baadhi ya mataifa ya Uarabuni, ilisababisha kudhoofika kwa

Dola ya Marekani na rasilimali zilizotazamiwa na wawekezaji

kuwa salama. Kutokana na mambo hayo yote kufikia Oktoba

2011, kiwango cha kubadilisha shilingi dhidi ya Dola ya

Marekani kilipungua hadi asilimia 25 kwa shilingi 107 kwa Dola

ya Marekani na ilifikia wakati shilingi ya Kenya ilitambuliwa

kuwa yenye thamani dhaifu zaidi ulimwenguni.

Ili kusimamisha kuzorota kwa thamani ya shilingi ya Kenya na

kuzuia mfumko wa bei, Benki Kuu ya Kenya (BKK) ilitekeleza

msururu wa hatua za sera za kifedha ambazo zilihusisha

kuongeza kwa haraka kwa Viwango vya Benki Kuu kutoka

asilimia 5.75 hadi asilimia 18 ili kuthibiti tatizo la kubanwa kwa

mzunguko wa fedha nchini na katika masoko ya uwekezaji.

Tatizo hilo sugu la mzunguko wa fedha lilisababisha kupanda

kwa ghafla kwa viwango vya riba. Viwango vya hazina ya fedha

kwa siku 91, siku 182 na siku 364 viliongezeka kwa wastani wa

kila mwezi wa asilimia 2.5, 2.7 na 3.7 katika mwezi wa Januari,

2011 hadi asilimia 18.3, 18.3 na 21.0 mwezi wa Disemba, 2011

mtawalia. Mwezi wa Januari, 2011 viwango vya mikopo katika

benki kwa benki vilisimamia katika kiwango cha wastani cha

asilimia1.2 na zikaazimia kumaliza mwaka zikiwa na kiwango

cha wastani cha asilimia 21.8.

Kufikia mwisho wa mwaka, Benki Kuu ya Kenya ilikuwa

imefaulu kurudisha hadhi ya shilingi yake na Dola ya Marekani

kupitia kwenye hazina ya fedha ulimwenguni. Huduma ya

Ziada ya Upatikanaji wa Mkopo pia iliboresha zaidi thamani ya

shilingi ya Kenya katika robo ya nne ya mwaka. Kiwango cha

ubadilishanaji wa fedha kufikia mwisho wa mwaka wa 2011

kilifikia kiwango cha wastani wa shilingi 85.1 dhidi ya Dola ya

Marekani.

Wakati ambapo hatua thabiti zilipochukuliwa na Benki Kuu ya

Kenya na kuleta mafanikio katika kuyatimiza malengo yake ya

kuboresha thamani ya shilingi ya Kenya, wakati huu, ni lazima

kuzingatia katika utawala wa viwango vya juu vya riba ambavyo

haviwezi kumudu ukuaji wa uchumi wa mda mrefu na hasara

iliyopo. Hali hii hususan itaathiri Sekta ya Benki ambapo baadhi

ya wateja na wenye kukopa watashindwa kutimiza malengo yao

na kuhudumia mikopo yao ipasavyo na kusababisha matukio

mengi ya kuwa na mikopo mingi isiyolipwa.

Swala la kimsingi zaidi, changamoto nyingi ambazo

zimesababisha mtafaruku huu wa malipo bado

haujashughulikiwa. Gharama ya juu ya kufanya biashara nchini

Kenya imefanya uzalishaji wa bidhaa za humu kutokuwa na

ushindani na kusababisha kuagizwa kwa bidhaa za wanunuzi

na zile zilizotengenezwa nje ya nchi kuletwa kutoka huko

ughaibuni. Kutokuwa na ufanisi katika sekta ya kilimo

imemaanisha kuwa hata baada ya mwaka wa mafanikio ya

kuwepo kwa mvua nyingi bado kuna uhaba wa chakula na

kusababisha umuhimu wa kuagiza chakula kutoka nchi za nje.

Nikiongezea ni kuwa Kenya kwa mda mrefu sasa imekuwa

ikitegemea sana utalii na kuuza bidhaa za msingi za kitamaduni

ambazo zina thamani ndogo, jambo ambalo linatufungia uwezo

wetu wa kupata kiwango cha juu cha pesa za kigeni. Ikiwa sera

na hatua thabiti hazitatekelezwa ili kuzithibiti changamoto hizo,

basi nchi hii itazidi kuathirika kiuchumi kutokana na matatizo

ya usawa wa malipo.

Matokeo ya soko la hisa yalikandamiza mafanikio kuanzia

mwanzo wa mwaka wa 2011 kutokana na “mabadiliko ya kanuni

za uwekezaji kwa wajasirili-amali” yaliyoonekana kwenye

masoko ya kifedha ulimwenguni ambayo yalisababishwa na

tatizo la viwango vya mikopo huko barani Yuropa na kuwepo kwa

wawekezaji wa kigeni katika masoko ya Afrika Kaskazini. Katika

sehemu ya pili ya mwaka, matokeo haya yasiyofaa yalipaliliwa

makaa na viwango vya juu vya riba ambavyo vilisababisha

wawekezaji kuhamisha hazina zao kwenye bidhaa bora za

uzalishaji. Ubora wa hisa ulianguka kila mahali na kusababisha

kupungua kwa asilimia 30 katika kiwango cha hisa cha Soko la

Ubadilishanaji wa Hisa la Nairobi (NSE-20) na kufikia kiwango

cha mwisho cha alama 3,123 mwaka huo wa 2011 kutoka kwa

NIC Bank Limited • Annual Report & Financial Statements 2011 • 13