Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
TAARIFA YA MWENYEKITI

matawi manne nchini Tanzania na tuko mbioni kufungua tawi

jingine katika eneo la Kahama.

Kitengo cha shirika cha Utoaji wa Huduma za kielektroniki –

kikiwepo kile cha ‘NIC Mobile Banking na NIC Online Banking’,

vimeimarishwa na kuongezewa kiungo muhimu cha M-pesa,

ambacho kinaunganisha vitengo vyote viwili kwa mpigo. Shirika

hili sasa lina mifumo miwili madhubuti ya kielectroniki iliyo

na utendakazi wa shughuli za benki kwa kutumia rununu na

mtandao. Mifumo hii miwili inawapatia wateja wetu fursa

muafaka ya kupata huduma yoyote mahali popote.

Kulingana na wingi wa wateja na kijiografia, shirika hili

limefanya mkataba wa uwakala na benki ya Posta. Mkataba

huu ambao umeidhinishwa na Benki kuu ya Kenya na ambao

unawezesha benki ya NIC kutoa huduma kwa wateja wake

kupitia mitandao ya matawi 94 kote nchini kwa njia inayofaa

na isiyo na gharama ya juu.

Sababu kuu ya kutaka kuyashughulikia matatizo na maendeleo

ya katika Sekta ya Benki, yameendelea kuzalia mageuzi ya NIC

katika bidhaa na zabuni nyingine kwa wateja. Mafunzo ya Klabu ya

Mjasiriamali, pamoja na kuwatia shime wajasiriamali chipukizi,

imeendelea kuwa chanzo cha kupokea Elimu na maarifa

katika matarajio ya wateja – hali inayopelekea kuongezewa

kwa bidhaa zaidi kaatika kitengo cha Biashara ndogo ndogo

za benki (SME). Shirika limebadilisha na kurekebisha bidhaa

zilizoko na pia kuzindua kampeini zitakazohakikisha kwamba

wateja wetu wanaendelea kuzifahamu vyema bidhaa zetu zote

kadri zinavyokua.

WAFANYAKAZI

Shirika la benki ya NIC lina mpango mkubwa wa kuwavutia na

kukuza vipawa ili kuhakikisha kuwa lina wafanyikazi walio bora

zaidi kwa mahitaji ya kibiashara ya sasa na ya siku sijazo. Bidii

ya kazi kutoka kwa wafanyakazi zimeliwezesha shirika kupata

matokeo bora katika miaka iliyotangulia. Waajiriwa wake

hujenga uhusiano mwema na wateja, wanaotambua nafasi za

kibiashara – zikiwepo kubwa na ndogo – na wanaotoa Huduma

zinazowezesha NIC kukua na kuimarika kama shirika thabiti la

benki.

Kuna mfumo uliopendekezwa wa kusimamia na kuwapa

motisha wafanyakazi kama vile mpango wa kujiendeleza

kikazi na pia njia ya kutwaa majukumu katika nafasi mpya za

kazi , malipo bora , mafundisho na kujiendeleza vilevile kupata

maoni kuhusu utendakazi.

Kupitia bidii ya mchwa na uzingativu,wafanyikazi 596 wa shirika

la benki ya NIC kufikia tarehe 31 Desemba mwaka wa 2011,

walijitahidi mno ili kutoa huduma za kimataifa za kifedha

huku wakizingatia pia maadili ya ujumla ya kuwa wataalamu,

wabunifu, wenye moyo, wenye kufuata na wenye uadiliifu wa

hali ya juu.

USIMAMIZI BORA WA KIUSHIRIKA

Benki ya NIC ina imani kubwa katika usimamizi wa kiushirika.

Kamati Kuu imeandaa mfumo imara wa uongozi ili uwe kama

kigezo cha jumla cha majukumu ya usimamizi wa kibiashara

na maslahi mengine ya shirika. Ni katika mfumo huu ambapo

maelezo ya kina yanapatikana katika kitengo cha usimamizi

cha pamoja kwenye ripoti hii ili kuhakikisha kwamba malengo

ya kamati na yale ya usimamizi yameainishwa na majukumu

yao yote yanawalenga washika dau wote.

Mafanikio ya usimamizi wa shirika katika utawala wake unazidi

kutambulika na baadhi ya mashirika ya kigeni yanayojulikana

katika kutathmini kwa biashara zilizowajibika. Ninafuraha

kuwaeleza kwamba katika mwaka wa 2011 , shirika la benki ya

NIC lilishinda ,sasa kwa mwaka wa pili mfululizo, Tuzo la Jumla

la Mabingwa wa Utawala na Usimamizi Bora, lililodhaminiwa na

ICSPAK, Benki Kuu Ya Kenya, Halmashauri ya Manufaa Baada

ya Kustaafu na Halmashauri ya Kuthibiti Bima, na wengine

wengi. Benki ya NIC pia ilitangazwa kuwa mshindi katika kitengo

cha Viwango vya Ubora vya Kimataifa vya Utoaji wa Ripoti za

Kifedha (IFRS) pia waliibuka wa pili katika shindalo la Tuzo la

(FiRE), shindano ambalo liliandaliwa na Soko la Hisa la Nairobi

(NSE), Taasisi Ya Wahasibu ya Kenya (ICPAK) na Halmashauri

ya Masoko ya Mtaji (CMA).

JUKUMU LA KIJAMII

Kuwajibikia jamii huwa ni kiungo muhimu sana katika kanuni za

utendakazi za Benki ya NIC. Shirika linanuia kuwapa thamani

washika dau na wabia wake wote na kadhalika kuchangia

ipasavyo katika mazingira, kifedha na maslahi ya kijamii kwa

wateja, wafanyakazi wake, na wanajamii ambao ndio nguzo kuu

ya biashara ya Benki ya NIC.

Katika mwaka wa 2011, shirika liliendelea kusaidia kwenye

hatua za masomo, mazingira na michezo. Hali kadhalika,

lilijitwika jukumu la kuyashughulikia mahitaji mengine

yanayochipuka.

Katika sehemu ya Elimu, shirika hili liliingia ubia na asasi

muhimu ikiwepo ile ya Palm House Foundation na Edumed

Trust, mashirika yanayowasaidia watoto kifedha ili kuendelea

kimasomo. Hawa huwa ni watoto werevu na wenye vipawa lakini

hawana uwezo wa kifedha. NIC huchukua jukumu la kuwasaidia

wanajamii kupitia kwa mashirika hayo mawili. Kwa kuwasaidia

watoto hawa katika shule za upili na kuwapa ushauri, shirika

la benki ya NIC huwapa nafasi ya kuboresha maisha yao na ya

familia zao.

Kupitia ‘Junior Achievements Kenya’ ambayo ni sehemu ya

‘Junior Achievements Worldwide’, shirika lililosaidia vijana wa

Kikenya ili kuwawezesha kujiandaa kikazi kwa siku za usoni,

kuwapa maarifa na kuwafunza mbinu za ujasiri-amali kupitia

kwa miradi ama programu za JA.

Kadhalika, Shirika la Benki ya NIC huwapatia wanafunzi nafasi

za masomo ya kila mwaka ya huko nyanjani. Masomo haya ya

nyanjani huwawezesha mwanafunzi kuyazoea mazingira ya

kuajiriwa

Kuhusu mazingira katika mwaka wa 2011 ukiwa mwaka wa

tatu mfululizo, shirika lilihusika katika kampeini ya ‘’Tupande

Pamoja” shughuli ya kupanda miti kwenye msimu wa Krismasi.

Tupande paamoja ni kampeini iliyowashirikisha wafanyakazi wa

NIC na wale wa UNEP , vile vile shirika la Misitu nchini kwa

16 • NIC Bank Limited • Annual Report & Financial Statements 2011