Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
Financial Statements 2011 - Investing In Africa
You also want an ePaper? Increase the reach of your titles
YUMPU automatically turns print PDFs into web optimized ePapers that Google loves.
TAARIFA YA MWENYEKITI

2011, mgao ambao uliokuwa haujaidhinishwa kikamilifu.

Wakurugenzi sasa wanapendekeza mgao wa mwisho wa mwaka

wa 2011 wa shilling 0.25 kwa kila hisa (Shilingi milioni 99) ili

kujumlisha mgao taslim wa mwaka huo wa shilingi milioni 198.

(2010 – Shilingi milioni 179)

Zaidi ya hayo, wakurugenzi wanapendekeza gawio la ziada

kwa mwenye hisa kwenye sehemu ya hisa moja (1) ya kawaida

kwa kila hisa kumi (10) za hisa za kawaida ambazo zimelipiwa

kabisa.

Ukijumlisha pamoja mgao taslim na gawio la ziada kwa mwenye

hisa ni shilingi milioni 396.

Ili kufikia mapendekezo haya, kamati ilichukua hatua za

kimsingi na umakinifu za nafasi ya mtaji wa shirika pamoja na

mipango na mikakati ya ukuaji iliyopo. Baada ya mazingatio ya

kina, iliafikiwa kuwa Kiwango imara cha Shirika la Benki la NIC

kiboreshwe zaidi na hivyo basi wakurugenzi wakapendekeza

idhini ya kuongeza mtaji wa shilingi bilioni 2 wa gawio la haki

kwa kila mwenye hisa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka.

Gawio la ziada na lile la haki kwa kila mwenye hisa hutegemea

kuidhinishwa na Mamlaka ya Mtaji wa Masoko.

MASHIRIKA-TANZU NA MAZINGIRA YA UANUAI WA

KIBIASHARA

Moja wapo ya nguzo ya mikakati ya Shirika inayonuiwa

kudumisha, uimarisha na kuthibiti ni kukuza biashara yenye

njia mbalimbali za mapato, vitengo vya kibiashara, aina za

wateja na kujipanua kwenye maeneo mbalimbali.

Lengo la jumla ni kuwajibika katika kupata mapato makuu

na yanayodumu katika kila eneo la kibiashara na nina furaha

kuripoti kuwa matawi ya biashara yalifanikiwa kupata faida

katika mwaka wa 2011, hivyo basi, kuchangia pakubwa katika

mafanikio ya Shirika hili.

Ubora uliopatikana kwenye utenda kazi wa benki ya NIC

Tanzania ni wa faida ukilinganishwa na kuwekeza kwetu kwa

mara ya kwanza katika mataifa ya nje. Katika mwaka wa 2011,

biashara zetu zilileta faida sawa na milioni 153 ikilinganishwa

na shilingi milioni 133 katika mwaka wa 2010. Twatarajia

utendakazi wa benki ya NIC Tanzania utakuwa bora zaidi jinsi

matawi ya mitandao ya kibiashara inavyozidi kupanuka na

kuanzisha bidhaa na huduma mpya. Utekelezaji wa mfumo

mpya halisi wa benki, T24, utawezesha kujumuishwa kwa

shughuli na huduma za kimaeneo katika kutambua uwezo wa

Shirika.

Mtaji wa uwekezaji kwenye Shirika la Benki ya NIC ulitia fora

zaidi huku ukipata faida ya karibu maradufu sawa na milioni 60

(2010-shs 32m). Biashara hizi sasa zaongoza katika ushauri wa

kifedha na zinazidi kujenga soko la hisa katika masoko ya hisa

na mtaji wa mikopo.

Kitengo cha Udalali wa Biashara cha NIC Securities uliendelea

katika soko la hisa lakini uliathirika sana na wanunuzi wa

hisa wa jumla katika soko la hisa la Nairobi (Nairobi securities

Exchange)na kupata faida ya shilingi milioni 11 kabla ya kutozwa

ushuru (2011-shs 20m) Kampuni tanzu hii sasa zaweza kupata

mapato bora pindi soko la hisa likifidia gharama zake.

Kampuni tanzu za maswala ya fedha, ikiwepo NIC Insurance

Agents, walipata faida ya kupigiwa mfano ya shilingi milioni 17

(2010- shs milioni 5)

Kwa jumla, kampuni-tanzu za shirika zilichangia asilimia 7%

(au shilingi milioni 244) ya mwaka katika kuongezeka kwa faida

ya Shirika kabla ya kutozwa ushuru.

Matokeo ya kuridhisha kutoka kwa kampuni-tanzu zetu,

hususan, benki ya NIC Tanzania, na muungano unaoendelea

wa Jumuiyya ya Afrika Mashariki ulichochea shirika

kutafuta nafasi zaidi katika upanuzi kwenye maeneo mapya

ya kuwekeza. Baada ya upembuzi yakinifu, kamati ilipitisha

kuanzisha kwa kampuni-tanzu ya benki ya biashara nchini

Uganda. Kampuni-Tanzu mpya ya benki ya NC Uganda

itawezesha shirika kupanuka kijiografia katika mataifa matatu

ya Muungano wa Afrika Mashariki. Kuanzishwa kwa kampunitanzu

hii kwa mtaji wa shilingi milioni 961 (shilingi bilioni 25

pesa za Uganda) kutategemea kuidhinishwa rasmi na wenye

hisa katika Mkutano wa Mkuu kila mwaka.

UTOAJI WA HUDUMA NA BIDHAA

Shirika limeamua kutoa huduma za kifedha zitazopatikana kwa

urahisi na zinazofaa kwenye upanuzi wa maeneo na hivyo basi

limeendelea kuboresha uwezo wake wa kiteknolojia.

Mfumo madhubuti wa utekelezaji wa shughuli za benki na

unaofahamika kama T24, na uliotoka kwa shirika la Temenos,

ndio sasa unaendelea kutekelezwa. Mfumo huu wa kifahari

utawezesha shirika hili kutoa huduma zinazofaa na za kimataifa

kwa wateja na uwe msingi wa bidhaa nyingine bora na mageuzi

yatakayozinduliwa. Mfumo huu pia unashughulikiwa kwenye

kampuni-tanzu na hii ni ishara kwamba bidhaa na huduma zote

za NIC zitapatikana katika maeneo yote.

Kwa sasa, mpango wa kupanua matawi unaendelea. Hata

hivyo mpango huu unaendelea kufaulu baada ya kupokelewa

vyema na wateja. Katika mwaka wa 2011 shirika lilifungua

matawi saba kwenye eneo hilo ili kutumia na kuwahi nafasi

muruwa za uwekezaji kwenye soko, na kadhalika kuhakikisha

kwamba wateja katika mji mkubwa na unaopanuka wa Nairobi

wanafuraahia na kufikia kwa urahisi huduma za shirika.Matawi

mapya yamefunguliwa katika maeneo ya Village Market,

Sameer Business Park, Galleria Mall, Karen Office Park na Taj

Mall (Embakasi). Pia tulifungua tawi katika mji wa Eldoret ili

kushugulikia eneo kubwa la Bonde la Ufa ambapo tawi la Nyali

lilihamishiwa sehemu inayofaa zaidi. Kwa faida na manufaa ya

wateja muda wa huduma za benki umeongezwa kwenye baadhi

ya matawi.

Kwenye eneo la Afrika Mashariki, shirika limefungua tawi

la pili huko jijini Dar es Saalam kwa lengo la kushughulikia

msongomano wa biashara karibu na mtaa wa Kariokor na

vituo vya biashara vya Ilala. Tawi la Ilala na matawi mengine

ya zamani katika miji ya Arusha na Mwanza kufikisha idadi ya

NIC Bank Limited • Annual Report & Financial Statements 2011 • 15