08.06.2013 Views

Ufunuo - kanisalakristo

Ufunuo - kanisalakristo

Ufunuo - kanisalakristo

SHOW MORE
SHOW LESS

Create successful ePaper yourself

Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.

kwakuwa Yesu anakuja. Kwakuwa Kristo anakuja tena kutuchukua nyumbani hivyo twahitaji kwenda

kwake 22:17-21. Ndio maana Roho, Bibi Arusi na Mungu wanasema “Njoo.”

Falsafa (Theory):

Kuna aina mbali mbali za tafsiri ya falsafa (theories) katika kitabu cha Ufunuo. Nyingi kati ya hizo hazina

msingi wowote. Lakini kadili tunavyojifunza kitabu hiki tunahitaji kuwa na mawazo pevu kwa kuangalia

ujumla katika maandiko. Kama kuna mtazamo tunaoweza kuuamini na mtazumo huo ni tofauti na

mafundisho mengine basi hatuwezi kuuacha hivihivi. Hatuwezi kuamini jambo ambalo ni tofauti na

maandiko mengine ya Biblia. Lakini tunachopaswa kukumbuka ni kwamba kitabu kiliandikwa kwa

Wakristo wa sehemu ya baadae katika karne ya kwanza. Na Imani tuliyonayo ni lazima iwe kwa faida yao.

Yaonekana kuwapo falsafa kuu nne kwenye hiki kitabu. Hata hivyo pengine zipo maelfu ya falsafa ndogo.

Moja yajionyesha kuwa ya baadae. Maana yake ni kwamba mambo yaliyoandikwa katika sura ya 4 -20.

Bado hayajatimia. Wanaanini kuwa yatatimizwa atakaporudi Yesu. Na Falsafa ya pili na ya kihistoria

kwamba mambo yamewekwa kwenye historia ambayo inachukua nafasi mpaka Yesu atarudi tena

yanafundishwa zaidi na Wakathoriki. falsafa ya tatu mtazamo wa utimilifu ikiwa na maana kwamba kila

kitu kilitimia wakati wa kipindi cha kuandika katika mtazamo ya misingi ya unabii wa kipindi cha mwisho

wa binadamu Falsafa (Theory) ya nne ni mtazamo wa kiroho ukimaanisha kuwa maono yote na unabii

haukuwa halisi sio kwamba unahusu jambo maalumu.

Hizi Falsafa (Theory) zote zimesomwa kwa miaka mingi na watu wameamua kuzifuata lakini watu pia

wamekuta matatizo mengi katika falsafa hizi. Hivyo njia rahisi ya kujifunza kitabu cha Ufunuo ni kujifunza

bila kuweka mambo yote katika falsafa tukiwa tunakumbuka kuwa katika kitabu hiki hakikuandikwa kwa

ajili yetu kiliandikwa ili kuwasaidia wazee wetu kuwapa imani kwa maswali yao mengi kuhusiana na jinsi

walivyoamini kwa muda mrefu.

Zipo pia falsafa (Theory) tofauti zenye misingi ya utawala wa miaka 1,000 tunayoisoma katika kitabu

hiki. Hizo Falsafa tuzisikiazo kila mara kwenye madhehebu kwanza ni ya umileniam ni falsafa

iliyogawanyika lakini pointi yake kuu ni kuwa Kristo alishindwa kuweka ufalme wake wakati wa kipindi

cha utawala wa Rumi na, atarudi kutawala kutoka kiti cha Daudi kwa miaka 1,000 kutoka Yerusalem. Pia

kuna kipindi baada ya mileniam wanaamini kuwa Yesu atarudi baada ya kuwa ametawala miaka 1,000 na

hapo kuna wamileniam wanaamini kuwa miaka 1,000 inaonyesha kipindi kisicho na mwisho.

Tarehe:

Kitabu kinazo tarehe kuu mbili ambazo zimependekezwa na watu siku hizi. Wengine wanadai kitabu

kimeandikwa wakati fulani kabla ya kuharibiwa kwa Yerusalem 67 -69 Bk. Na wengine wanaamini kitabu

kimeandikwa wakati wa utawala wa Douisian karibu 95-96 Bk.

Twaweza kuona katika kitabu hiki kuwa Wakristo katika Asia Ndogo walikuwa chini ya uangalizi mkubwa

- wakati wa utawala wa Kiroma kabla ya kuharibiwa Yerusalem Wakristo walikuwa hawana mateso yoyote

lakini Domitian aliyetawala toka 81-96 Bk. Aliwatawala Wakristo kwa ukali akiamini kuwa alikuwa

Mungu na anaongea kwa Mamlaka ya Mungu hivyo adha ikatokea Asia Ndogo mpaka mwisho wa utawala

wa Domintian.

Namba Za Biblia:

Moja - Umoja, upekee, peke yake angalia Efe. 4:3-5.

Mbili - Namba mbili inaonyesha nguvu na hatari kwa maisha ya kizamani. Wakati fulani Yesu

aliwatuma wanafunzi wake wawili wawili. Musa alituma wapelelezi wake wawili wawili. Nuhu

aliingiza wanyama wawili wawili. Katika Ufunuo 11 tunaona mashahidi wawili wanasimamia

mshahidi mwenye nguvu. Wanyama (Beasts) wawili wanaonekana kama adui mwenye nguvu.

Tuangalia Yoh. 15:26-27; Luka 10:1.

Tatu - Ni mfano wa Uungu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu) Mt. 3:13-17; 28:18-20.

4

Hooray! Your file is uploaded and ready to be published.

Saved successfully!

Ooh no, something went wrong!