our roots
Connect2015
Connect2015
Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Kuimarishwa na KUTUMIwa

kwa Kiswahili - Hatua Muhimu Ya

Kuhakikisha Umoja Katika Jumuiya

Ya Afrika Mashariki

Na Aron Mtunji

Kwa muda mrefu sasa, wana-Afrika

Mashariki wametamani kuwa na

Uhuru wa kufanya biashara pamoja,

kuzitembelea nchi jirani bila ya

kuwepo kwa vizuizi vyovyote na zaidi ya

hayo, kuona kuwa kuna amani kati ya nchi

husika. Zote hizi ni ndoto zinazoweka kuwa

kweli.

Ili kuwepo na mambo yote haya, kuna

mengi ambayo yamefanywa, yanayotendeka

sasa na yaliyo katika akili za washika dau

katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika

makala haya, nitazungumzia juhudi hizi na

kuwaeleza jinsi kuwepo kwa lugha moja

inayowaunganisha wana-Afrika Mashariki

kutaziwezesha kuwa kweli.

Kwanza kabisa, ili kufanya biashara,

kujihusisha katika siasa au kufanya lolote

lile, ni lazima kuwe na mawasiliano. Ili

yote haya yatendeke, tunahitaji lugha

tutakayoweza kuitumia na kuelewana, tuwe

Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda au katika

nchi yoyote ya Afrika Mashariki.

Moja kati ya juhudi za kufanya hivi

ni kuwepo kwa jumia iliyo na umoja.

Kuvunjika kwa jumuiya ya Afrika Mashariki

mwaka 1977 kulisababisha athari kubwa:

kukosekana kwa ajira, kutokuwa na

uaminifu kati ya nchi husika na kusitishwa

ka uhuru wa wananchi wa nchi hizi

kutembea ndani ya jumuiya. Pia, hakukuwa

na usawa wala uhuru wa kufanya huduma

za pamoja, jambo ambalo liliathiri

uchumi, uhusiano, siasa na zaidi ya hayo…

mawasiliano.

Baada ya kufufuliwa kwa jumuiya hii,

matunda ya kuwepo kwa umoja yalianza

kuonekana, jambo ambalo lilikuwa funzo

kwa nchi wanachama.

Pili, Jumuiya ya Afrika Mashariki

imehakikisha kuwa kuna ‘tume ya Kiswahili

ya Afrika Mashariki.’Lengo kuu la tume

hii ni kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili

imeimarika, kama njia moja ya kuhakikisha

kuwa kuna umoja na urahisi katika

mawasiliano yanayohusisha siasa, shughuli

za kifedha, shughuli za kijamii, za tamaduni,

teknolojia na masomo.

Mkataba uliotiwa sahihi mwaka 1999

uliimarisha uhusiano kati ya nchi husika.

Kipengee muhimu katika mkataba huu

(137) kiliitaja lugha ya Kiswahili kama lingua

franca ya nchi za Afrika Mashariki. Hivyo

basi, lilikuwa jambo muhimu kwa nchi hizi

kuunda baraza au chama ambacho lengo

lake lingekuwa kuhakikisha kuwa lugha ya

Kiswahili imetumiwa kuimarisha umoja,

kuhakikisha kuwa Kiswahili kimetumiwa

kama lugha ya jumuiya na kuhakikisha kuwa

lugha hii imetumiwa katika mawasiliano.

Kisha, mipango ya kuwasaidia walio na

matatizo ya kimawasiliano kwa lugha ya

Kiswahili, kubadilishana kwa waalimu na

wanafunzi wa Kiswahili baina ya shule za

nchi husika na kuzisaidia serikali za nchi hizi

katika juhudi za kuimarisha Kiswahili ni kati

ya ajenda walizokuwa nazo.

Lengo kuu lilikuwa kuwepo kwa vituo

vya utafiti vya Kiswahili katika nchi za Afrika

Mashariki, kuwepo kwa waalimu wa lugha

hii ambao wangeifunza katika vyuo vilivyo

katika nchi hizi na kuleta mabadiliko katika

MTAALA unaotumiwa katika shule za Afrika

mashariki, hasa zile za masomo ya juu kwa

kukifanya Kiswahili kuwa kati ya lugha rasmi

zinazotumiwa.

Kufikia sasa, Marais wan chi za Afrika

Mashariki wameunga mkono hatua hii.

Rais wa Kenya, Mheshimiwa Kenyatta

akiongea katika mkutano wa EALA (East

African Legislative Assembly) tarehe ishirini

na sita Novemba, mwaka alfu mbili kumi na

tatu alipongeza juhudi za Jumuiya ya Afrika

Mashariki kwa kukifanya Kiswahili kuwa

Lingua Franca. Aliongeza kuwa juhudi hizi

ni kati ya mambo muhimu yanayohitajika

iwapo tungependa kuiona Afrika Mashariki

ikiwa na umoja wa aina yoyote ile.

Katika mkutano kama huu uliofanyika

Bujumbura tarehe ishirini na tatu oktoba,

mwaka alfu mbili kumi na tatu, Mheshimiwa

Mike Sebalu alidokeza kuwa ingekuwa

vyema iwapo nchi za Afrika Mashariki

zingeweza kuwa na mpango wa kielimu

ambao ungewawezesha waalimu wa

Kiswahili kufanya kazi katika shule za nchi

hizi ili kuiimarisha lugha yenyewe, hasa

katika nchi yake. Alisema, “Madam speaker,

it would be a good idea to have teachers from

the United Republic of Tanzania crossing

to Uganda to teach.” na kuongeza kuwa

Kiswahili kimetiliwa mkazo katika katiba ya

Uganda, na ni jukumu lao kuhakikisha kuwa

ndoto yao imeonekana. Aliongeza, “We

hope soon, Kiswahili would be introduced in

schools in Uganda to bolster its popularity.”

Kufikia sasa kuna maendeleo

yanayoonyesha juhudi za jumuiya ya Afrika

Mashariki, kama vile kuwepo kwa mitandao

ya kiteknolojia inayotoa huduma kwa lugha

ya Kiswahili: (Microsoft Office 2010 pack.

Windows 7 Kiswahili local language pack)

Ni dhahiri kuwa ili ndoto ya kuwa na

jumuiya yenye nguvu iwe ya kweli, tunahitaji

lugha moja ya mawasiliano kati ya nchi

zetu. Bila shaka, tunakihitaji Kiswahili, na

si kukihitaji tu, bali kukienzi pia. Asilimia

kubwa ya Jamii za Afrika Mashariki ni za

ki-Bantu, hivyo basi haitakuwa vigumu

kwa jamii hizi kukijua Kiswahili kwani lugha

yenyewe ina asili ya ki-Bantu.

Ili jamii hizi ziweze kuienzi lugha hii,

itavibidi vyuo vya Elimu kutilia mkazo

utumizi wake katika Mtaala.

44 • DaystarConnect 2015