Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Magonjwa ya ngono

Magonjwa ya ngono yanaweza kuambukizwa kwa jinsia zote kwa njia ya

kujamiiana.

Magonjwa ya ngono yanaweza kuwa na dalili mbaya, huzuinisha na

isiyoridhisha. Lakini tatizo kubwa kwa magonjwa haya ni kwamba mara

nyingi hayaonyeshi dalili kabisa. Kwa maana hii unaweza kuwa na

maambukizo bila kujua. Kwa hiyo unaweza kuambukizwa na

kuwaambukiza watu wengine, bila kufahamu.

Kama magonjwa ya ngono hayatatibiwa na madawa hospitalini yanaweza

kuleta matatizo makubwa ambayo yatasababisha magonjwa kama kansa,

ugonjwa wa moyo, kuumwa na macho, kuumwa na ubongo, kuumwa na

mifupa, kuumwa na viungo vya mwili, na kutoa mimba. Pia yanaweza

kuleta ugumba (kutopata watoto) na kuharibu kabisa kizazi cha

mwanaume au cha mwanamke.

Kama una ugonjwa ya ngono, au mwenzi wako anayo, ni muhimu kutibiwa

haraka kliniki au hospitalini. Na wale uliojamiiana nao labda

umeshawaambukiza na wasione dalili zozote. Na pia ni muhimu kuwaeleza

wale uliojamiiana nao kuwa umeathirika ili wapate matibabu haraka.

Kama wenzi wako hawakupata matibabu haraka wanaweza

kupata matatizo makubwa kiafya, wanaweza kuambukiza

watu wengine, na wanaweza kukuambukiza wewe tena.

5 KISWAHILI