Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Maambukizi ya VVU

VVU huishi kwenye mwili wa mtu aliyeambukizwa. Virusi huishi kwenye

majimaji yaliyoko kwenye:

1. Shahawa

2. Majimaji ukeni

3. Damu

4. Maziwa ya mama

Kwa hiyo shahawa, majimaji ukeni, damu na maziwa ya mama ni

hatari kuambukiza VVU.

Majimaji mengine mwilini kama mate, machozi, jasho na mkojo havina

virusi vingi vinavyoweza kuambukiza. Kwa hiyo mate, machozi, jasho na

mkojo siyo hatari kwa kuambukiza VVU.

Njia pekee ya kuambukiza VVU ni kutoka kwenye shahawa, majimaji

ukeni, damu au maziwa ya mama ameshaambukizwa na kuingia kwenye

damu ya mtu mwengine.

Njia zifuatazo zinaambukiza VVU:

1. Kujamiiana na mtu mwenye VVU bila kutumia kondom.

Kujamiiana bila kondom ni njia kuu ya kuambukizwa

VVU.

2. Kushirikiana sindano, wembe, visu vya kukata mwili, mswaki na

vyombo vingine vinavyoweza kuwa na damu yenye VVU.

3. Mwanamke anaweza kuambukiza mtoto wake akiwa tumboni,

wakati wa kujifungua au wakati wa kunyonyesha.

9 KISWAHILI