Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Jinsi ya kumkinga mtoto akiwa tumboni na

wakati wa kujifungua

Mama mwenye VVU ana nafasi kati ya 15% hadi 25% ya kuambukiza

mtoto wake wakati akiwa na mimba au wakati wa kujifungua.

Njia bora ya mtoto kutopata maambukizi ya VVU ni mama kutoathirika.

Kama mama anajikinga vizuri na anaishi bila VVU hawezi kuambukiza

mtoto wake VVU.

Wanawake wengi hawafahamu kuwa wameshaambukizwa au

hawajaambukizwa VVU. Mwanamke asiyefahamu kuwa

ameshaambukizwa au hajaambukizwa VVU anaweza kumsaidia

kumkinga mtoto asiambukizwe wakati akiwa na mimba kwa kufuata

maagizo yafuatayo.

• Kutumia kondom kwa kila tendo la ngono wakati mtoto akiwa

tumboni.

• Akipata lishe bora wakati wa ujauzito na atajifungua mtoto

mwenye uzito.

Kama mama anafahamu ameshaambukizwa VVU anaweza kumsaidia

mtoto kwa kufuata maagizo ya juu na maagizo yafuatayo pia:

• Kutumia madawa (ARVs), zinazopatikana hospitalini tu, ya

kupunguza nguvu ya VVU mwilini.

• Kuhudhuria kliniki au hospitali na kujifungua hospitalini.

Mama akijifungua nyumbani, ni vyema mkunga kuvaa mpira mkononi

wakati wa kuzalisha, kwa sababu VVU inaweza kuingia mwilini mwake

kupitia jeraha mkononi.

45 KISWAHILI