Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
VVU na ukimwi

Ukimwi ni ugonjwa hatari ya ngono. Inasabibishwa na virusi viitwavyo

VVU. VVU inamaana ya ‘virusi vya ukimwi’ (VVU). Virusi hivi hudhuru

mwili polepole na baadaye mwili hushindwa kupambana na magonjwa

mengine. Mwishoni mtu anaweza kufa kwa ajili ya magonjwa

yanayosababbishwa na VVU.

Mtu akiambukizwa anaweza kuchukuwa muda mrefu bila kuelewa

kwamba VVU ipo kwenye mwili wake. VVU ipo kwenye shahawa,

majimaji ukeni, damu na maziwa ya mama aliyeambukizwa. Huwezi

kuelewa kuwa mtu ana VVU mwilini kwa kuangalia kwa macho tu. Njia

pekee ya kuelewa kuwa mtu ameshaambukizwa VVU ni kupima damu

kwenye kliniki au hospitalini.

Ukimwi inamaana kwamba ‘upungufu wa kinga mwilini’. Ukimwi ni

matokeo ya mwisho wa mwili kushindwa kukinga magonjwa. WaMaasai

hutumia jina ‘biitia’ kama ukimwi. Ni vizuri zaidi kutumia jina ukimwi

kwani bittia ni jina la zamani lakini ukimwi ni ugonjwa mpya (ukimwi

imegundukika 1981).

Kwa sababu watu wengi hawajui kwamba wameshaambukizwa, au wenzi

wao wameambukizwa, hawaendi kupima na hawajikingi wao wenyewe

wala kuwakinga wenzao. Ina maana kwamba mtu anaweza kuambukiza

watu wengi kabla dalili yake kuonekana.

Hakuna tiba wala chanjo ya VVU. Mtu aliye na VVU, virusi vitakaa

mwilini maishani. Siku hizi kuna madawa (ARVs) hospitalini yanayoweza

kupunguza makali ya VVU mwilini na kusaidia kuongeza muda kutoka

kuambukizwa VVU hadi kuwa na dalili ya kuumwa. Lakini madawa haya

hayatibu VVU moja kwa moja. Ni muhimu kukumbuka kuwa VVU ni

virusi hatari sana na inasabibisha matatizo makubwa.

7 KISWAHILI