Create successful ePaper yourself
Turn your PDF publications into a flip-book with our unique Google optimized e-Paper software.
Ukweli kuhusu kondom

Baadhi ya watu wanahofu ya kutumia kondom, lakini baada ya kuelewa

VVU na magonjwa mengine ya ngono, hali hii ya hofu hubadilika. Na

hali hii ya kutumia kondom inawashiria kuwa unajali afya yako, familia

yako, rika yako na jamii yako kwa jumla.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa kutumia kondom ni hatari, au kuwa na

mianya inayo ruhusu VVU kepenya kwenye mwili, au hufikiri kuwa VVU

tayari imo ndani ya kondom kabla ya kutumia. Mambo haya yote siyo

ya ukweli kabisa. Watu huzumgumza mambo haya kwa sababu tu

hawaelewi ukweli kushusu kondom na wana hofu kutumia.

Inawezakana wewe mwenyewe una hofu ya kutumia kondom na

umeshakataa kutumia kondom mpaka sasa. Siku hizi kuna sababu kubwa

ya wewe kuanza kutumia kondom, kwani kondom tu ndiyo kinga ya

VVU.

Kondom hukukinga wewe na mwenzi wako kwa VVU na magonjwa

mengine ya ngono. Pia watu wengi wanasema kujamiiana na kondom ni

vyema kuliko kujamiiana bila kondom, kwa sababu inaleta matumaini

makubwa na kuondoa hofu kuhusu VVU na magonjwa mengine ya

ngono.

Kwa nini watu

wanalalamika kuhusu

KONDOM na mimi

silalamiki!

29 KISWAHILI